Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: JamiiForums Premium Member Subscription

    Report Post
    Page 4 of 17 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 336
    1. #1
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 333
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      595
      Likes Given
      760

      Default JamiiForums Premium Member Subscription

      Ndugu wana JF

      Awali ya yote, niwashukuruni nyote!

      Tumeliongelea hili jambo kwenye andiko hii, Na sasa ni utekelezaji wake.

      Lengo kubwa la kuanzisha utaratibu huu ni kuiwezesha JamiiForums kujiendesha kwa ufanisi zaidi ndani na nje ya Tanzania.

      Tunayo mikakakati tuliyoianda ya jinsi gani tunafikiri JF inatakiwa iende, na tunaahidi kuwashirikisha kwanza "Premium Members" wetu kabla haijaanza kutekelezwa.

      Hizi alama maalumu zitadumu kwa mwaka moja.

      Baada ya mazungumzo marefu ya jinsi ya kupanga hii michango tulikubaliana hivi


      Annual Membership Subscriptions

      JF Bronze Member 20,000 - 99,000

      JF Gold Member 100,000 - 249,000

      JF Platinum Member 250,000 - 490,000

      JF Tanzanite Member 500,000 - Na zaidi...





      Utaratibu wa Malipo



      M-Pesa

      Tumefanikiwa kupata utaratibu mzuri sana wa kulipia kupitia M-Pesa. Utalipia Subscription Fee kama vile unavyonunua Luku au DSTV na kutuma kwenda kwenye number 888 888


      Jinsi ya Kutuma


      1. *150#

      2. Bonyeza 4 (Pay Bill)

      3. Bonyeza 1 (Enter Business Number)

      4. Weka 888888

      5. Enter Reference No. (tumia 1234)

      6. Enter Amount (Weka kiasi unachotaka kutuma)

      7. Weka password yako na kisha utume.

      Ukishatuma, tuma PM kuja kwangu Mike McKee ukituambia receipt no. uliyoweka na jina lako unalotaka liwekewe Premium Member au tuma email kwenda [email protected] ukituambia receipt number.


      CRDB Bank

      Account Name: Jamii Media Company Limited
      Account Number: 0150413278400
      Branch: CRDB Waterfront


      Ukishaweka pesa tuma SMS kwenda number hii 0755 642 929 kutuambia jina gani umetumia wakati unaweka hela, na nikiasi gani umeweka, na kutuambia jina unalotaka liwekewe alama maalumu (premium membership).

      Sisi tutaithibitisha kwa alama maalum (icon) na kukuwekea kwa hilo jina.

      Kwa wale watakaotumia malipo kwa njia ya mtandao (online transfer) ya CRDB, wanaweza wakatutumia receipt kwenda kwenye email ya [email protected]


      WesternUnion

      Name: Mike Mushi
      Address: P.O.BOX 4203 Dar es Salaam
      Phone: 0755 642 929
      Email: [email protected]


      PayPal

      Tuma kwenda kwenye email hii [email protected]



      Maswali na Majibu


      Alama maalumu kwa mtumiaji(Verified User) ni nani?

      Verified Users ni wale wanachama wa JF wanaotumia majina yao halisi. Sisi tuna hakikisha kujua kwamba yale majina ni yao kweli na kuwawekea alama maalumu inayoonesha kweli anayeandika kwa jina hili ni yeye halisi.

      Naweza kulipia kwa kidogokidogo?

      Malipo kidogokidogo yanaruhusiwa kwa wale Platinum na Tanzanite members na zinatakiwa kukamilishwa ndani ya miezi minne.

      Nataka kuchangia ila sitaki kuwekwa kwenye makundi

      Unaweza ukachangia kwa kutumia viwango hapo juu na usiwekwe kwenye hayo makundi ila ukawekewa “alama” ya premium member inayoonekana hapo juu.

      Kuna faida gani nikiwa Bronze Member na nikiwa Tanzanite Member?

      Lengo la hii program ni kuwezesha JF, hapa kinachofanywa ni uchangiaji na sisi tunachofanya ni kukutunuku “badge” kutoka na ulichochangia ili kutambua na kuthamini uchangiaji wako.

      Lengo letu ni mwakani tuweze kutoa packages nzuri kwa kila package. Na sisi pia inatupa mwangaza wa kutambua ni watu kiasi gani wapo, na wenye nia ya kuchangia na kununua hizo packages zitakapoanza.

      Kwa kipindi cha mwaka mzima kuna vitu vingi vitakuwa vinaanzishwa na vingi mtakuwa mnatuambia “premium members” mnataka nini.

      Hivyo vitu watakaokuwa wa kwanza kujua na kuvitumia kabla havijaanza kuwa wazi ni hawa premium members wetu. Maana yake maoni, ushauri unaanza kutolewa na hawa kwanza.

      Kuchangia JF na kuwa premium member kunakupa nafasi wewe kuwa mmoja ya wanachama muhimu watakaoongoza mabadiliko na kuwa mmoja wa watakaoshuhudia mabadiliko hayo ya JF.

      Je Subscption fee yangu ya mwaka mzima inaanza lini?

      Subscription fee yako ya mwaka mzima inaanza pale utakapolipia. Kama utalipa July, itakwisha july mwaka kesho.

      Kwanini hakuna malipo ya TigoPesa na Airtel Money?

      Utaratibu kama tulioupata Mpesa ndio tulikuwa tunautaka kama huo TigoPesa, sasa TiGo wamesimamisha hiyo huduma mpaka mwezi wa nane. Hatuna tunachoweza kufanya ni kusubiri mpaka mwezi wa nane. Njia ya kawaida ya kuchukua line ya tigopesa na kuiweka hapa sio salama na wote tunafahamu hii, mtu anaweza kudurufu laini na akaenda kuchukua hiyo pesa.

      Airtel Money bado tupo kwenye mchakato wa kupata utaratibu mzuri, na itakapokamilika itawekwa hapa.

      Je, inamaana nisipolipia premium members sitoweza tena kuipata JF?

      Hapana, JF itaendelea kuwepo kama kawaida.

      Hamuoni kuweka hizi “levels” mtaleta matabaka ya waliokuwanacho na wasiokuwa nacho na wachangiaji watawaogopa Tanzanite au Platinum members?

      Kwanza lazima tuelewe kwamba “levels” zipo kama “incentive” ya kuwapa hao waliochangia na kiasi gani wamechangia pia kuvutia wengine wachangie. Hii ni kama harambee hivi. Na pia unaweza ukachangia na pia usitake kuwekewa hiyo “alama” ya premium member wala hizo “badge” za levels ukabaki kama kawaida.

      Na pia kama kweli utaogopa username ya mtu yenye “alama” ya tanzanite na utashindwa kuongea au kubishana kwenye mada kwasababu unaogopa labda anapesa, sasa hapo tatizo ni kwako wewe. Inakuwaje unaogopa username ya mtu na inakunyima wewe uhuru?

      Na kama kweli italeta matabaka na itaondolea watu uhuru wa kuongea, basi itakuwa haina faida na hatutasita kuitasitisha.

      Mwisho wa siku, kama wewe ni tanzanite member na hufuati sheria za JF, unapata BAN kama kawaida.


      .......

    2. Miaka 50

    3. #61
      Masanilo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2007
      Location : Swat valley, Keta Keta
      Posts : 19,127
      Rep Power : 5481
      Likes Received
      3530
      Likes Given
      1950

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By Mike McKee
      Mwisho wa siku, kama wewe ni tanzanite member na hufuati sheria za JF, unapata BAN kama kawaida.
      .......
      Haya wakuu nitawatafuta tumalizane.....ila hizi BAN mngetafutia namna mzifute.
      Mike McKee likes this.

      Kindness is the language which the deaf can hear and the blind can see - Mark Twain
      CCM is enemy of GOD

    4. #62
      Power G's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 20th April 2011
      Location : Msoga Kijijini
      Posts : 2,414
      Rep Power : 993
      Likes Received
      776
      Likes Given
      261

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Mike, mbona unakuwa bubu kuhusu offer ya Gold membership uliyotutangazia mwanzoni kwa mtu atakayelipia katika kipindi cha mwezi mmoja??? Mkuu, sitanyamaza mpaka unipe ufafanuzi wa hili. Samahani lakini kama utaona nakusumbua.
      Mike McKee likes this.
      TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE MENO KAMA AKINA EL, JK, EC na RA

    5. #63
      Mathias Byabato's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2010
      Posts : 581
      Rep Power : 547
      Likes Received
      161
      Likes Given
      90

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      wazo zuri sana

      byabato
      Mike McKee likes this.
      Kama Wewe ni Mwandishi kweli,unaamini ,una uhakika na uliandikalo basi Onesha Jina,Sura yako- Jeneral Ulimwengu

    6. #64
      Popompo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 309
      Rep Power : 494
      Likes Received
      36
      Likes Given
      34

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Naruhusiwa kulipia au ni hao premium members tuu?
      Mike McKee likes this.

    7. #65
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 333
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      595
      Likes Given
      760

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By Tume ya katiba
      Umesomeka mkuu!

      La msingi, michango hii itumiwe kwa maendeleo mazima ya JF Only. ikiwa pamoja na kuuboresha zaidi mtandao, sometimes frame za page zinashake.

      Tupo pamoja mkuu, ina maana Precise pangolin, kachangia kilo hadi kilo 2 na nusu? du ngoja nijikongoje japo nitafute ka BURONZE ka kuuzia sura
      Tume ya katiba

      Ni kweli JF inahitaji marekebisho mengi, ila sio siri marekebisho pia yanahitaji rasimimali watu na fedha na kwa hali ya sasa hivi, hata uendeshaji wa kila siku tunatoa mifukoni mwetu. Tukiwezeshwa tunaweza tukafanikisha maboresho zaidi

      Quote By Anheuser
      "Hivyo vitu watakaokuwa wa kwanza" hivyo vitu vitu gani?

      Kwa nini ununue kitu cha laki tano na hujui unapata nini?

      Kwenye public media nyingine kukiwa na michango ya lazima kama hii basi angalau mtu unapewa ka T-Shirt au kikombe chenye nembo ya JF ukanywee kahawa na utangazie jamvi. Nyinyi JF mmeshindwa hata kuchapisha T-Shirt za buku kumi kumi? Halafu mnaomba laki tano? Hebu kuweni na fund raising creativity for a change.

      Idea yako ni nzuri ya kutoa T-Shirt au kikombe. Tutaifanyia kazi. Mkuu huu ni uchangiaji ili kuiwezesha JF.

      Quote By Precise pangolin
      Mkuu ni muhimu kuchangia siyo tung'ang'anie kufanya michango ya kwenye harusi tu
      Ni Kweli siyo tunganganie kufanya michango ya kwenye harusi.

      Quote By mfereji maringo
      Nikitaka kuanZa kutumia jina langu halisi kwa kubadili lile lisilo halisi ambalo nimekua nikilitumia humu mnaweza kunisaidi?
      Yes, Linawezekana kabisa.

      Quote By Papizo
      Kwa hiyo mkuu Mac kama mtu ana miaka 5 humu ndani na hajatoa mchango wake ila anachangia post kama kawaida na ana uzoefu wa JF then hawezi kuusishwa kuombwa msaada au mawazo yoyote ila ataombwa msaada yule aliyeingia leo na kulipia amount fulani au sijaelewa??nadhani ni vizuri pia mkawafikiria na wale member wa mda mrefu zaidi kuliko kuwaweka pembeni ambapo wanaijuwa vizuri JF kuliko aliyeingia jana au leo.

      Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
      Mkuu, wapo members wa JF ambao sio premium members na tuna consult nao katika maswala mengi. Hapa ni uchangiaji na njia ya sisi kuwafanya wachangiaji wajue nini tunafanya ni kuwashirikisha katika maswala mapya na pia sisi kusikia kutoka kwao wanataka nini. Hii haimanishi kwamba wewe huwezi kutupa sisi ushauri au kutupa maoni yako.

      Quote By Papizo
      Member wengi waliongia siku chache au miezi kadhaa naona ndio wanaingia na majina yao ila mkongwe wa JF huwezi sikia anasema anataka kutumia jina lake, me still siwezi shawishika kutumia jina langu hapa hili la Papizo linanitosha sana na nitamwaga nondoz humu kama kawaida.

      Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
      Mkuu, hakuna anayekulazimisha kutumia jina lako halisi na wala sio lazima kutumia jina lako.

      Quote By georgeallen
      je mapato na matumizi ya michango yetu itawekwa wazi? Hii itatusaidia kujua kweli michango yetu ni muhimu na inatumika kwa kazi iliyokusudiwa.
      Ndio hii itawekwa wazi mkuu.

      Quote By Mzito K
      Mkuu kama una akaunti imekula BAN na sio premium mwana jf akichangia kwa akaunti hiyo itakuwa imekula kwake?
      Kama umepigwa ban, utasubiri mpaka ban yako iishe ndio utaendelea kutumia jina lako.


      Quote By Mtoto Wa Mbale
      Suala la 'UsIri' kwa wale wasiotumia majina yao halisi kutokana na sababu mbalimbali mtalilinda vipi? Tunajua kuwa ukitumia malipo kwa njia ulizotaja hapo, M-pesa na Bank, lazima jina kamili litaonekana.

      Naomba ufafanuzi tafadhali.
      Mtoto Wa Mbale Mkuu njia ni nyingi sana ukitaka usiri na watu wasijue jina lako halisi. Mfano, unaweza kumtuma mtu aka deposit pesa CRDB huyo mtu wakati ana depost wala halazimishwi kutumia jina lake halisi, na wewe ukisha deposit unatuma email kutueleza umefanya hivo. Sasa hapo sisi tutakujuaje?

      Pia vibanda vya MPESA vipo vingi, unaweza ukatuma kupitia hivo vibanda na wewe ukaja huku ukatutumia hata email au Private Message kwamba malipo yenye receipt number fulani ni yangu.

      Quote By Biohazard
      Tupo Pamoja
      Cheers


      Quote By Sizinga
      OK etlist m-mezingatia mawazo yetu Watanzania!! Hasa reduction ya viwango hivi vipya!!
      Yes. Tumezingatia mawazo ya Watanzania.

    8. RukaaJuu Final

    9. #66
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 333
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      595
      Likes Given
      760

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By LoyalTzCitizen
      Ina maana baada ya mwaka kuisha na status nayo itapotea kama member hayuko tayari ku renew status yake? Mfano alikuwa Senior expert then akawa premier, anaweza tena kurudi kuwa senior expert kama hajarenew hiyo status?
      LoyalTzCitizen Hii Program kwa sasa lengo lake ni uchangiaji na uwezeshaji wa JF. Na hiyo icon utakayopewa itadumu kwa mwaka moja. Mwaka kesho mwezi kama huu tutareview kama tutaendelea au la na je tukiendelea itakuwaje. Tunachofikiria kwa sasa ni kwamba, wale wote watakao changia mwaka huu na kushindwa kufanya hivo mwaka kesho basi watapewa icon iliyoandikwa "Proudly JF Member"


      Cheers

      Quote By ruttashobolwa
      Tunashukuru kwa taarifa mkuu
      Shukran Sana

      Quote By Bondpost
      Nimelitafakari hili jambo hata mimi. Nadhani hapo ndipo watu watakuwa traced kiurahisi sana. Mie kwaukweli sina uhakika kama nitajaribu kufanya hivyo mambo mengi tumeyaongea humu jamvini na watu watakuwa waoga kuleta mada au kuchangia. Mpesa, crdb, lazima zitadisplay anaetuma!

      Na ukipiga simu kwao hata namba itaonekana, napata kigugumizi sana kwa hii forum sasa! Fanyeni marketing ya kutafuta matangazo. Kama jf imekuwa na members wengi ni moja ya sababu ya mtu kutangaza biashara zake humu! Sijui marketing officer hajaangalia hilo suala? Pia unapoanza kuweka matabaka madharau yatakuwa zaidi.

      Nimeona sana hapa jamvini waweza kutoa mchango wa mawazo mtu anaibuka kusema sijui junior member, kwani kuwa junior member inamaana hata umri, upeo wa kufikiri, elimu na pesa ni junior pia? Nadhani instead ya kuongeza viewers ili mpate matangazo mengi zaidi inaweza kuwa vice versa.
      Bondpost

      Mkuu ni kweli JF ndio website inayotembelewa na watu wengi zaidi na ndio yenye traffic kubwa Tanzania nzima na hii haina ubishi. Sio kwamba Marketing officer wetu hawafanyi kazi, hapana. Ni kwamba wanaotaka kutangazwa wanakuja na sheria kali.

      Mfano wanataka kutangaza, ila nyie members msiongele kampuni yao wala kuongelea managers au CEO wa hizo kampuni, sasa unataka kuona kitu cha aina hiyo JF?

      Na pia makampuni hayaoni umuhimu wa kutangaza online. Hawana hata website, email wanatumia za Yahoo.

      Wengine wanataka kutangaza ila bei wanayokupa ni ndogo mno kwahiyo ni heri usichukue kabisa.

      Mwisho wa siku matangazo yanasaidia kidogo ila kwa sasa hayawezi kugharamia gharama za uendeshaji na pia ukuaji wa JF


      Quote By muwaha
      Nimekupata Mkuu...ngoja nianze kukusanya fedha ili niipate 'platinum badge'
      Cheers Mkuu

      Quote By mysteryman
      nikitumia jina langu halisi na at the same time nina lets say platinum.......je nitawekewa nembo zote???
      Utachagua moja unalitaka liwekewe platinum.

      Quote By Shark
      Kuna mtu alishawahi kupost thread hapa Jf,
      Alivyotoka nje akakana Katu katu kua hakua yeye na leo mmemuwekea "verified user", maana yake nini sasa??
      Ukiona yupo verified maana yake anayeandikwa ndio mwenyewe.

      Quote By Lyimo
      Ninaimani jukwaa letu litazidi kuimarika na kuwa chombo muhimu katika mabadiliko chanya, kuelimishana na kukosoana kwa mantiki.
      Ni kweli Juukwa Letu litaimarika

      Quote By Ronal Reagan
      Kazi nzuri, taarifa safi inajitosheleza twende kazi. Mi mwaka wangu wa bajeti ni September so let's meet there
      Quote By WFM
      Umetusaidia mkuu..! Binafsi ckujua wajibu wangu kwa JF kwa sababu tunaingia humu kwa kuiba muda wa kazi, hvo sazingine sio rahisi kujua mambo mengi. Naomba uiweke kwny sticky ili na wengine wapate hii knowledge.

      Eng. Willy
      Mkuu Tutaweka njia ambayo kila member atalazimishwa kusoma hii thread kabla hajasoma kitu kingine chochote. Tutaiweka na sticky pia

      Quote By Yo Yo View Post
      umeeleweka arifu.......

      hivi pesa zatumwa kweli twaona...lakini ni vema kama mngekuwa mnatuambia pia mapato na matumizi ya hiyo michango.....
      mfano..mmetumia kiasi gani kulipia server au fedha kiasi gani mmetumia kulipia gharama za watumishi na kiundeshaji..nikiwa zimechanguliwa kihasibu....nasema haya najua litakalotokea later....na ni jambo jema kwa mtu kujua fedha yake inatumika vipi?
      Hii taarifa itapatikana. Sasa hivi tunataka fedha ya gharama za uendeshaji na pia fedha kwaajili ya kuanda mikakati mipya ya ukuaji wa JF.

      Quote By Chamoto
      mzurimie kuendesha hii forum siyo mchezo tukianza na ukarabati (maintenence) inahitaji mtu wa kuangalia kila wakati kama kuna tatizo. Na hapa siongelei moderators bali mtaalamu anayeangalia ulizi wa data na attacks kutoka sehemu mbalimbali mtandaoni.

      Pia nafikiri umeone jinsi JF inavyobadilika mara kwa mara, ujue kuna mtu/watu hawalali kuiboresha hii huduma.

      Software (Vbulletin) inayoendesha hii forum siyo bure na ni lazma ilipiwe kila mwaka. Pili, lazima ile kwenye servers (dedicated) ambazo gharama zake si chini ya shilingi milioni moja ($800) kwa mwezi ili iweze kutoa huduma maridadi.

      Tatu, data zote hizi (mabandiko, picha n.k) lazima zihifziwe mahala fulani kama akiba (backup) endapo tatizo litatokea, hayo yote yanahitaji pesa na hapa sijaongelea malipo ya wafanyakazi, domain name n.k.

      Kwahiyo dada yangu usifikiri kuwa watu wanataka kula vichwa bali hizi ni gharama halisi kabisa za uendeshaji.

      Hizo forums unazozisema ambazo ni bure sijui ni zipi kwasababu ninavyojua mimi lazima kuwe na njia ya kuingiza mapato, iwe kwa subsription, matangazo au njia nyingine. Binfsi sijui menejimenti ya JF ikoje lakini nauhakika kama wangeweza endesha JF kwa matangazo tuu wasingeweka subscription.

      JF wamewahi kuweka matangazo ya google adsense mara kadhaa na kuyatoa na hii nafikiri ni kutokana na matangazo hayo kutokidhi gharama za uendeshaji. Matangazo ya google hayalengi watumiaji wa JF kwahiyo wengi wetu hatu-click hizo ads (Kumbuka unapo-click matangazo ya google JF inalipwa).

      Pia wengi wetu tunapokuja JF tunataka kuganda hapa hapa tukisoma mabandiko mbalimbali, hatutaki ku-click ads ambazo zitatutoa JF na kutupeleka sehemu nyingine.

      Elewa kwamba makampuni makubwa ya kitanzania ambayo yanajitangaza kwenye blog kama za michuzi, MO n.k hayataki kuweka matangazo yao hapa kwasababu zao za kimaslahi kwahiyo JF imekuwa mkiwa aliyekosa mtu wa kumfadhili.

      Eniwei niliona nitoe maelezo yasiyo na upendeleo wala maslahi yoyote kama member wakawaida tu isijeonekana jamaa wa JF wanataka kula vichwa kumbe gharama za uendeshaj ni kubwa.
      Chamoto

      Safi Safi Safi sana Mkuu kwa kuwaelewesha watu. Ulichosema ni 1000% ukweli kabisa.

      Gharama zinaongezeka kila siku mfano sasa hivi tuna posts 8,000 kwa siku, maana yake ni kwamba tunahitaji moderators wengi wanaolipwa wanaofanya kazi ya moderation JF kama kazi yao na hii yote inahitaji fedha ambayo hatuna.

      Pia JF inakuwa inabidi tuanze ku explore revenue sources zingine sasa kufanya hivi pia inahitaji fedha.

      Kuhusu Matangazo nimeongelea hapo juu kwamba hayasaidi kabisa uendeshaji tunahitaji hii michango ili tuendele kukua. Tumekuwa tukiendesha JF kutoka fedha zetu mfukoni ila sasa gharama zinakuwa kubwa kwasababu watu wanaongezeka

      Nathani mnakumbuka mwezi uliopita tulipata down time kubwa. Hiyo ni kwasababu ya kuweka miundombinu mingine mipya kwaajili ya ku accomodate watu wengi zaidi.
      Quotestyle="display:none;visibility:hidden;" data-cfsrc="template/JamiV1/default/misc/progress.gif" alt="" /> Reply With Quote

    10. #67
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 333
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      595
      Likes Given
      760

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By Mkirua
      Umesomeka mkuu kinachofuata utekelezaji....
      Yaaap. Sasa ni utekelezaji.

      Quote By kibakwe
      asante mkuu nimekupata
      Shukraan

      Quote By Delegate
      Mike vipi sisi tunaoishi nje ya nchi,anyway nilifikiria jinsi ya kutuma hela naona kama ni ngumu kidogo,au tuwekee hapa itakuwaje
      Mkuu unaweza kutumia paypal au western union au kuomba ndugu, jamaa au rafiki akakutumia huku tanzania kwa Mpesa au CRDB. Njia zote nimeziweka hapo juu

      Quote By Delegate
      Mike kama umetembelea facebook na baadhi ya forum kubwa online,je kuna kitu mmjifunza pale??manake mimi ni member wa facebook lakini sijawahi kupata ujumbe kwamba nilipie huduma,facebook wanafanyeje kazi zao mpaka kuweza kuwa na member mil100???je kuna ulazima wa kujifunza kitu pale?
      Mkuu naomba unipe link ya baadhi ya forums kubwa duniani unazozijua wewe zenye watu wengi wanaojiendesha kwa faida naamini tukifanya uchunguzi kwao tutaweza kujifunza mengi

      Pia huwezi kufananisha Facebook na JF. Huwezi kufananisha investment wanazofanya makampuni ya nje na jinsi hapa kwetu inavyokuwa. Facebook pia wanamatangazo na ndio the only revenue kwa wao kutengeneza pesa. Sisi kampauni hayawezi kutangaza kwetu yanaogopa.

      Wewe unaweza kuona kwamba unatumia facebook bure ila kina Facebook wenywe walipewa Millions of dollard na Venture Capitalist au Angel Investment miaka ya mwanzo kwaajili ya investment wakiamini kwamba facebook itakuja kutengeneza pesa siku moja.

      Hapa kwetu hata makampuni yanaogopa kutangaza JF na kama wakitangaza JF wanataka makampuni yao yasisemwe au baadhi ya watu wanataka wasiandikwe sasa je ni kitu unachokitaka wewe?

      Je unataka kusikia mafisadi wamenunua hisa JF alafu iendeshwe bure kabisa huku ukiwa hauna uhuru wa kuongea?

      Kwa Tanzania tunaweza tukafanikisha kuiendesha JF bure kabisa kama wewe Delegate utaichangia JF sisi tuna explore njia Revenue Channels nyingi tukifanikiwa, maana yake hakutakuwa tena na uchangiaji. Anayeweza kuifanyikisha JF na ikawa bure, ni wewe.



      Quote By PPM
      Kwa watu ambao hawataki ID zao zifahamike tutalipaje?
      Unaweza kumtuma mtu bank akaweka deposit. Unaweza kwenda kwenye vibanda vya Mpesa ukatuma then ukatutumia email pamoja na receipt number ya malipo. Sisi hatutaki kujua wewe ni nani.

      Quote By WildCard
      Akaunti ya Max pale NBC inaweza kuendelea kutumika?
      Nitakutumia maelezo mkuu.

      Quote By Power
      Mike, mbona unakuwa bubu kuhusu offer ya Gold membership uliyotutangazia mwanzoni kwa mtu atakayelipia katika kipindi cha mwezi mmoja??? Mkuu, sitanyamaza mpaka unipe ufafanuzi wa hili. Samahani lakini kama utaona nakusumbua.
      Hii nimekujibu Mkuu


      Quote By Popompo
      Naruhusiwa kulipia au ni hao premium members tuu?
      Kila mtu anaruhusiwa kulipia.

      Quote By Mathias Byabato
      wazo zuri sana

      byabato

      Cheers!!!

    11. #68
      sir.JAPHET's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2012
      Posts : 609
      Rep Power : 475
      Likes Received
      90
      Likes Given
      45

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      ahsante kwa taarifa
      Mike McKee likes this.

    12. #69
      Popompo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 309
      Rep Power : 494
      Likes Received
      36
      Likes Given
      34

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      ni sawa nitachangia .wazo ni zuri sana, nawaombea afya njema!
      Mike McKee likes this.

    13. #70
      Las Mas Bobos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 973
      Rep Power : 544
      Likes Received
      310
      Likes Given
      92

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Aaah! This time next year = Las Mas Bobos, JF Tanzanite Member

      What a shame Tanzanite zenyewe zimeshachimbuliwa na kuhamishiwa India, Mbuguni kumebaki mishimo tu. Babu Nyerere alisema kama hatujapata akili bado tuziache kwanza haziozi lkn kina dhaifu hawataki kumsikia
      Mike McKee likes this.
      By the time a man comes to realize that his father was right, he usually has a son who think he is wrong.

    14. #71
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,661
      Rep Power : 718
      Likes Received
      291
      Likes Given
      36

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Niwashukuru kwanza kwa kazi nzuri sana mi nitachangia muda si mrefu toka sasa. Ombi langu kwenu nataka ni jue gharama za kuweka tangazo langu la biashara, nipeni kwa mwezi, miezi sita, mwaka, nimekuwa nikiulizia hili sipati majibu, Mnaweza kunitumia utaratibu kwa email yangu [email protected]
      Last edited by Bob G; 20th June 2012 at 16:53. Reason: nilisahau kuweka email yangu
      Mike McKee likes this.

    15. #72
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,661
      Rep Power : 718
      Likes Received
      291
      Likes Given
      36

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Nilikua naanza kutuma kwa M Pesa but network inasumbua kutuma, mimi nataka kutoa tangazo hapa JF naomba nijulishwe gharama zake kwa wiki,mwezi miezi 6 na mwaka, na nifanyeje ili kupata huduma hii, E-mail [email protected]. plz nijulisheni
      Quote By Mike McKee
      mzurimie

      Kuchangia uendeshaji wa JF. Hiyo kupata jina au kuwekewa icon ni kama sisi kusema asante ila zaidi ya hapo inakuingiza kwenye "inner circle" ya watu tutakao consult nao katika maswala mbali mbali ya mabadiliko tutakayoanza kufanya hapa JF.

      Naomba pia nisaidie link ya hizo Forums za Africa zenye members karibu na million naamini tutaweza kujifunza mengi kutoka kwao katika uendeshaji wa Forums.

      Matangazo yalikuwa yanalipa gharama za servers miaka miwili iliyopita ila sio sasa hivi na ongezeko kubwa la watu wanaotumia JF. Inatulazimu sisi kutumia pesa zetu wenywe kuendesha JF.

      Sasa mkuu utakapoweza kuchangia maana yake unatuwezesha sisi maana yake tunakuwa katika wakati mzuri sasa wakuanza kuongelea maboresho unayotaka kuyaona JF na sisi ndipo tunaweza kurekebisha.

      Kuna changamoto kwenye swala zima la Mods ila hichi sio sababu ya mods kupendelea yeyote yule. Tuna jukwaa la malalamiko kama umehisi umeonewa au hujatendewa wema sehemu yeyote ni wajibu wako wewe kwenda kule na kureport hilo tatizo na sisi tutalifanyia kazi.
      Mike McKee likes this.

    16. #73
      Mike McKee's Avatar
      JF Founder Array
      Join Date : 10th February 2006
      Posts : 333
      Rep Power : 100000
      Likes Received
      595
      Likes Given
      760

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By Popompo
      ni sawa nitachangia .wazo ni zuri sana, nawaombea afya njema!
      Shukran sana..

      Quote By Bob G
      Niwashukuru kwanza kwa kazi nzuri sana mi nitachangia muda si mrefu toka sasa. Ombi langu kwenu nataka ni jue gharama za kuweka tangazo langu la biashara, nipeni kwa mwezi, miezi sita, mwaka, nimekuwa nikiulizia hili sipati majibu, Mnaweza kunitumia utaratibu kwa email yangu [email protected]
      Mkuu, nitakutumia email in few hours!!

    17. #74
      Oxlade-Chamberlain's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th May 2009
      Location : dodoma
      Posts : 7,616
      Rep Power : 4422
      Likes Received
      789
      Likes Given
      750

      Default

      Quote By Mike McKee
      Shukran sana..



      Mkuu, nitakutumia email in few hours!!
      Mkuu, nimekumbuka kitu baada kuona hio post ya Bob G.

      Jaribu kutafuta mpango ambao utawezesha watu wanao weka biashara zao ndogo ndogo kama laptop, magari wawe wanatoa japo kamchango kidogo wa kuweka tangazo.

      Kwa vile inaweza kuwa ngumu kuwachaji watu bila kuuza na ni ngumu kujua kama mtu kauza , unaweza kufikiria njia nzuri zaidi hili watu wenye matangazo ya biashara nndogo ndogo waweze kutoa mchango.

      Njia moja nimefikiria ni kwamba mtu lazima awe na status ya premium member na zingine zinazoonesha kwamba kashawai kutoa mchango wowote hili kuweza kuweka tangazo la biashara yake ndogo ndogo.
      Najua kuna members wengine wamechangia lakini hawa status hizo, nina huakika mtakua mnawajua na kuweza kuruhusu matangazo yao.

      Baaadae pia mnaweza kuwa na jukwaa lime list items zinazo uzwa namembers humu hili watu wawe wanaenda huko moja kwa moja na kuona vitu ( kama ebay) na kikiuzwa kinatolewa.

      Ni wazo tu mkuu hili kuwezesha JF kujiendeleza zaidi.
      Mike McKee likes this.

    18. #75
      Remmy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th June 2009
      Location : home
      Posts : 4,348
      Rep Power : 7769
      Likes Received
      1546
      Likes Given
      1799

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Tumekusoma, duuuuuuuuuu.....
      Mike McKee likes this.

    19. UKI
      #76
      UKI's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Location : Mali
      Posts : 682
      Rep Power : 486
      Likes Received
      149
      Likes Given
      176

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Quote By delegate
      mike vipi sisi tunaoishi nje ya nchi,anyway nilifikiria jinsi ya kutuma hela naona kama ni ngumu kidogo,au tuwekee hapa itakuwaje
      kwa wale wanaoshi nje mkuu kuna option ya online payment visa, master card etc ni rahisi sana, tumefsnya hivyo na sasa mdundo tu
      Mike McKee likes this.

    20. #77
      Zogwale's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 10th July 2008
      Posts : 6,004
      Rep Power : 6482
      Likes Received
      1207
      Likes Given
      509

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Asante sana Mkuu Mike kwa kazi nzuri and taking into consideration our opinion,
      Sasa naona mambo yako vizuri zaidi. Ni action tu zinatakiwa sasa ili JF isonge mbele.
      Mike McKee likes this.
      "Kama unaingia Ikulu kwa njia ya rushwa, je ni biashara gani iko huko ya kuwezesha kulipa fadhila ya rushwa hiyo???"

    21. UKI
      #78
      UKI's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 12th June 2012
      Location : Mali
      Posts : 682
      Rep Power : 486
      Likes Received
      149
      Likes Given
      176

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Ila mkuu kweli kuna mtu kauliza swali hapo kuwa kwa walipaji kutumia mtandao kugundulika ni rahisi sana na vile vile navyojua bongo kitu privacy watu kutunza ni ngumu sana je mmejiandaaje na changamoto hizi kaka? Maana unaweza kumsema rais wako kwa kitendo kibaya cha ukweli aichokifanya ila afunike aibu anaweza kutumia mamlaka yake kukutafuta mpka uchochoroni kukupata na hapo ni kwa kuanzia kwenye hayo malipo. Please naomba hili nifahamishwe bro. Na nyie mko tayari kusimamia kwenye usiri??
      Mike McKee likes this.

    22. #79
      Adharusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd January 2012
      Location : Mtwara
      Posts : 518
      Rep Power : 473
      Likes Received
      69
      Likes Given
      298

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      Nitajitahidi niwepo katika Msafara
      Vox populi,Vox dei
      Mike McKee likes this.

    23. #80
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,350
      Rep Power : 12596
      Likes Received
      5869
      Likes Given
      781

      Default Re: JamiiForums Premium Member Subscription

      JF Daima Paw
      Mike McKee and Zion Daughter like this.
      "Kuna kontena la futi 40 lilobeba karatasi za kupigia kura limekamatwa Tunduma" Dk W. Slaa

    Page 4 of 17 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...