Ndugu wana JF
Awali ya yote, niwashukuruni nyote!
Tumeliongelea hili jambo kwenye andiko hii, Na sasa ni utekelezaji wake.
Lengo kubwa la kuanzisha utaratibu huu ni kuiwezesha JamiiForums kujiendesha kwa ufanisi zaidi ndani na nje ya Tanzania.
Tunayo mikakakati tuliyoianda ya jinsi gani tunafikiri JF inatakiwa iende, na tunaahidi kuwashirikisha kwanza "Premium Members" wetu kabla haijaanza kutekelezwa.
Hizi alama maalumu zitadumu kwa mwaka moja.
Baada ya mazungumzo marefu ya jinsi ya kupanga hii michango tulikubaliana hivi
Annual Membership Subscriptions
JF Bronze Member 20,000 - 99,000
JF Gold Member 100,000 - 249,000
JF Platinum Member 250,000 - 490,000
JF Tanzanite Member 500,000 - Na zaidi...
Utaratibu wa Malipo
M-Pesa
Tumefanikiwa kupata utaratibu mzuri sana wa kulipia kupitia M-Pesa. Utalipia Subscription Fee kama vile unavyonunua Luku au DSTV na kutuma kwenda kwenye number 888 888
Jinsi ya Kutuma
1. *150#
2. Bonyeza 4 (Pay Bill)
3. Bonyeza 1 (Enter Business Number)
4. Weka 888888
5. Enter Reference No. (tumia 1234)
6. Enter Amount (Weka kiasi unachotaka kutuma)
7. Weka password yako na kisha utume.
Ukishatuma, tuma PM kuja kwangu Mike McKee ukituambia receipt no. uliyoweka na jina lako unalotaka liwekewe Premium Member au tuma email kwenda [email protected] ukituambia receipt number.
CRDB Bank
Account Name: Jamii Media Company Limited
Account Number: 0150413278400
Branch: CRDB Waterfront
Ukishaweka pesa tuma SMS kwenda number hii 0755 642 929 kutuambia jina gani umetumia wakati unaweka hela, na nikiasi gani umeweka, na kutuambia jina unalotaka liwekewe alama maalumu (premium membership).
Sisi tutaithibitisha kwa alama maalum (icon) na kukuwekea kwa hilo jina.
Kwa wale watakaotumia malipo kwa njia ya mtandao (online transfer) ya CRDB, wanaweza wakatutumia receipt kwenda kwenye email ya [email protected]
WesternUnion
Name: Mike Mushi
Address: P.O.BOX 4203 Dar es Salaam
Phone: 0755 642 929
Email: [email protected]
PayPal
Tuma kwenda kwenye email hii [email protected]
Maswali na Majibu
Alama maalumu kwa mtumiaji(Verified User) ni nani?
Verified Users ni wale wanachama wa JF wanaotumia majina yao halisi. Sisi tuna hakikisha kujua kwamba yale majina ni yao kweli na kuwawekea alama maalumu inayoonesha kweli anayeandika kwa jina hili ni yeye halisi.
Naweza kulipia kwa kidogokidogo?
Malipo kidogokidogo yanaruhusiwa kwa wale Platinum na Tanzanite members na zinatakiwa kukamilishwa ndani ya miezi minne.
Nataka kuchangia ila sitaki kuwekwa kwenye makundi
Unaweza ukachangia kwa kutumia viwango hapo juu na usiwekwe kwenye hayo makundi ila ukawekewa “alama” ya premium member inayoonekana hapo juu.
Kuna faida gani nikiwa Bronze Member na nikiwa Tanzanite Member?
Lengo la hii program ni kuwezesha JF, hapa kinachofanywa ni uchangiaji na sisi tunachofanya ni kukutunuku “badge” kutoka na ulichochangia ili kutambua na kuthamini uchangiaji wako.
Lengo letu ni mwakani tuweze kutoa packages nzuri kwa kila package. Na sisi pia inatupa mwangaza wa kutambua ni watu kiasi gani wapo, na wenye nia ya kuchangia na kununua hizo packages zitakapoanza.
Kwa kipindi cha mwaka mzima kuna vitu vingi vitakuwa vinaanzishwa na vingi mtakuwa mnatuambia “premium members” mnataka nini.
Hivyo vitu watakaokuwa wa kwanza kujua na kuvitumia kabla havijaanza kuwa wazi ni hawa premium members wetu. Maana yake maoni, ushauri unaanza kutolewa na hawa kwanza.
Kuchangia JF na kuwa premium member kunakupa nafasi wewe kuwa mmoja ya wanachama muhimu watakaoongoza mabadiliko na kuwa mmoja wa watakaoshuhudia mabadiliko hayo ya JF.
Je Subscption fee yangu ya mwaka mzima inaanza lini?
Subscription fee yako ya mwaka mzima inaanza pale utakapolipia. Kama utalipa July, itakwisha july mwaka kesho.
Kwanini hakuna malipo ya TigoPesa na Airtel Money?
Utaratibu kama tulioupata Mpesa ndio tulikuwa tunautaka kama huo TigoPesa, sasa TiGo wamesimamisha hiyo huduma mpaka mwezi wa nane. Hatuna tunachoweza kufanya ni kusubiri mpaka mwezi wa nane. Njia ya kawaida ya kuchukua line ya tigopesa na kuiweka hapa sio salama na wote tunafahamu hii, mtu anaweza kudurufu laini na akaenda kuchukua hiyo pesa.
Airtel Money bado tupo kwenye mchakato wa kupata utaratibu mzuri, na itakapokamilika itawekwa hapa.
Je, inamaana nisipolipia premium members sitoweza tena kuipata JF?
Hapana, JF itaendelea kuwepo kama kawaida.
Hamuoni kuweka hizi “levels” mtaleta matabaka ya waliokuwanacho na wasiokuwa nacho na wachangiaji watawaogopa Tanzanite au Platinum members?
Kwanza lazima tuelewe kwamba “levels” zipo kama “incentive” ya kuwapa hao waliochangia na kiasi gani wamechangia pia kuvutia wengine wachangie. Hii ni kama harambee hivi. Na pia unaweza ukachangia na pia usitake kuwekewa hiyo “alama” ya premium member wala hizo “badge” za levels ukabaki kama kawaida.
Na pia kama kweli utaogopa username ya mtu yenye “alama” ya tanzanite na utashindwa kuongea au kubishana kwenye mada kwasababu unaogopa labda anapesa, sasa hapo tatizo ni kwako wewe. Inakuwaje unaogopa username ya mtu na inakunyima wewe uhuru?
Na kama kweli italeta matabaka na itaondolea watu uhuru wa kuongea, basi itakuwa haina faida na hatutasita kuitasitisha.
Mwisho wa siku, kama wewe ni tanzanite member na hufuati sheria za JF, unapata BAN kama kawaida.
.......


Reply With Quote






Follow Us Here