Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

    Report Post
    Page 6 of 9 FirstFirst ... 45678 ... LastLast
    Results 101 to 120 of 171
    1. #1
      Jackbauer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : CTU
      Posts : 4,873
      Rep Power : 1690
      Likes Received
      1348
      Likes Given
      277

      Default Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      baada ya kushuhudia migomo ya madaktari kwa awamu mbili na baadaye kufuatiwa na majadiliano yalioyoisha hivi karibuni sasa kuna kila dalili ya kutokea kwa mgomo mwingine mara itakapofika tarehe 23 juni 2012.
      migomo miwili ya kwanza ilipuuzwa hivihivi lakini mwishowe tuliona viongozi wakuu wa nchi wakirudi nyuma na kuomba huruma ya mazungumnzo.
      je iwapo mgomo wa tarehe tajwa utatokea ni nani alaumiwe kwa kushindwa kutatua mgogoro huu uliodumu kwa kipindi cha nusu mwaka sasa??


      haya ni ya morogoro

      TAARIFA KWA UMMA
      Katika kikao cha madaktari na wahudumu wa afya Ifakara kilichofanyika tarehe 16.June 2012, Kwa pamoja kilikataa taarifa iliyotolewa na serikali kuhusu madai ya Madaktari na Wahudumu wa Afya. Kikao kilitoa maazimio yafuatayo
      1. Tunasikitishwa na msimamo wa serikali kutokuonyesha lengo la kutatua madai ya madaktari na wahudumu wa afya.
      2. Tunatangaza mgogoro rasmi dhidi ya serikali kuhusiana na madai yetu kudharauliwa na kutofanyiwa kazi.
      3. Tutaungana na madaktari na wahudumu wengine wa afya Tanzania katika mgomo utakaoanza tarehe 23 Juni 2012. Kama Serikali haitafanyia kazi madai yetu
      4. Tunaukumbusha umma kuwa serikali ilikuwa na muda wa kutosha kufanyia kazi na kutatua madai ya madaktari na wahudumu wa afya

      haya ni ya BUGANDO


      TAMKO:
      Kutokana na kikao cha tarehe 15/06/2012 hapa Bugando na kanda ya Ziwa kwa ujumla tunatamka kwamba:-
      1. Hatukubaliani na namna serikali ilivyo- na inavyoshughulikia suala la madaktari na wahudumu wengine wa afya hapa nchini.

      2. Ni vema serikali itoe tamko lenye tija juu ya mgogoro unaondelea kati yake na wafanyakazi wa sekta ya afya nchini

      3. Tutaungana na madakrai wote pamoja na wahudumu wengine wa afya katika mgomo utakaonza tarehe 23/06/2012 ikiwa hatua madhubuti na zenye tija hazitachukuliwa

      Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika


      na haya ni ya Dodoma karibu kabisa na mjengoni
      TAMKO LA MADAKTARI NA WAHUDUMU WA AFYA DODOMA
      Baada ya kupata muda wa kupitia na kuchambua kwa kina ufafanuzi wa serikali kuhusu madai ya madaktari. Madaktari na wahudumu wa afya Dodoma tunapenda kutoa tamko kama ifuatavyo

      1. Tunaunga mkono maamuzi ya kikao cha madaktari na wahudumu wa afya cha tarehe 9/06/2012 kwa kuukataa ufafanuzi wa madai ya msingi kwani hauna nia ya dhati wa kuleta suluhisho la kudumu katika sekta ya afya. Hivyo tupo katika mgogoro na serikali na tutaungana na wenzetu katika mgomo utakaoanza tarehe 23/06/2012.

      2. Tunaitaka serikali iache mara moja jitahada zake za kutugawa wahudumu wa sekta ya afya kwani kwa kufanya hivyo kutadhorotesha ufanisi wa utoaji wa huduma za afya katika hospitali mbalimbali nchini. Hivyo tunaitaka serikali ianze mara moja kuwalipa wahudumu wote wa afya posho mpya za kuitwa kazini.

      3. Tunawaomba wahudumu wa afya wote na popote walipo kuendelea kuwa pamoja katika kutetea huduma bora na maslahi mazuri katika sekta ya afya.

      MUNGU IBARIKI TANZANIA.

      updates;mahakama kuu divisheni ya kazi imetoa zuio la mgomo huu.
      madaktari washikilia msimamo wao na baadhi yao kusema
      "BASI NASISI HIYO TAARIFA YA SERIKALI TUNAICHAMBUA KWA KINA ,TUNAIFANYIA MPANGO MKAKAKATI KABAMBE,TUNAISHUGHURIKIA,TUTAI FANYIA UPEMBUZI YAKINIFU MBALI NA HAYA MGOMO UKO PALEPALE''

      SIKU YA KWANZA
      hospitali kadhaa zimeingia kwenye mgomo ikiwa ni pamoja na Bugando,Muhimbili,Mbeya na Amana.
      bado ni vigumu ku-assess makali ya mgomo hasa ukizingatia leo haikuwa 'siku ya kazi' tusubiri siku ya jumatatu ambayo ni siku inayohudhuriwa na wagonjwa wengi.

      SIKU YA TATU

      Mbeya,Bugando,Muhimbili,Dodoma ,amana,KCMC,mwananyamala,TMK,i fakara, wako kwenye mgomo.
      kuna tetesi kuwa Ocean road wako mbioni kujiunga.
      Vyombo vya habari mbalimbali vyaanza kuripoti madhara ya mgomo huu.baadhi ya waandishi wakataliwa kuingia hospitali ili kuhabarisha wananchi juu ya mgomo.
      Channel ten yafanya mjadala na madaktari.madaktari wajieleza vizuri kwa nini wamefikia hatua hii.kesho tutegemee mgomo kuwa mkali zaidi.

      SIKU YA NNE
      Mgomo bado unaendelea katika sehemu tajwa hapo juu.pia kuna taarifa kuwa hospitali ya hydom imeingia rasmi kwenye mgomo.
      waziri wa afya amekwepa kufanya mahojiano ya 'live kupitia star TV' ili kujibu madai ya madaktari.katika kipindi hicho kulikuwepo wawakilishi wa madaktari na wajumbe wa kamati ya bunge huduma za jamii.Mwinyi aliomba udhuru kwa kusema kuna mambo muhimu uanayashughulikia.
      huko bugando mkurugenzi wa hospitali anaelekea kurudia kosa lililofanywa na mkurugenzi mwenzake wa Muhimbili kwa kutishia kuwarudisha intern doctors wizarani.tukumbuke kosa hili ni moja ya chanzo cha mgomo huu unaoendelea mpaka leo.

      SIKU YA TANO
      Kiongozi wa jumuiya ya madaktari Dr Ulimboka steven atekwa na kupigwa hadi kupoteza fahamu.
      Madaktari waapa kuongeza mgomo.
      Mh pinda kutoa tamko la serikali kesho.

      SIKU YA SITA

      Afya ya dr ulimboka yaanza kuimarika,asema bado maumivu ni makali!
      Pinda akataa kutoa tamko.
      mgomo unaendelea huku kukiwa na ripoti ya madaktari bingwa wa MNH wamejiunga katika mgomo

      SIKU YA SABA
      Hali ya ulimboka si nzuri sana
      madaktari bingwa wa MNH,MOI,MUHAS,ORCI, Wametoa tamko rasmi la kujiunga kwenye mgomo.
      nawasilisha...
      Last edited by Jackbauer; 29th June 2012 at 20:18.

    2. FemaTV & Radio

    3. RMA
      #101
      RMA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2010
      Posts : 410
      Rep Power : 519
      Likes Received
      87
      Likes Given
      0

      Default Re: Madaktari waamua kuanza kugoma baada ya siku mbili serikali kwenda Mahakamani

      Tupo hapa tulipo kwa sababu ya UDHAIFU wa Rais Kikwete, Bunge legelege na upuuzi wa CCM! - J J Mnyika - Mbunge - Ubungo.

    4. Uda
      #102
      Uda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2010
      Posts : 431
      Rep Power : 1817
      Likes Received
      197
      Likes Given
      14

      Default

      Quote By dosama
      Ni taarifa toka kwa Waziri wa Afya Hissein Mwinyi:

      Mambo watakayo watekelezea ni

      Kadi ya Green Card

      Posho toka 10,000- 15,000

      Uchunguzi wa maiti toka 50,000 - 100,000

      Ila habari za mshahara serikali imekiri kushindwa haiwezi kuwalipa 3,500,000
      aliyesema kuwa posho ya uchunguzi wa maiti ni sh 50000 ni nani?

    5. Uda
      #103
      Uda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2010
      Posts : 431
      Rep Power : 1817
      Likes Received
      197
      Likes Given
      14

      Default

      Quote By dosama
      Ndo lengo lao eti ufanane na wajumuiya ya Afrika Mashariki
      ni bora madaktari wakaacha kazi wakagombee ubunge.

    6. #104
      gango2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st August 2011
      Location : From Moshi
      Posts : 682
      Rep Power : 526
      Likes Received
      197
      Likes Given
      166

      Default Re: Madaktari waamua kuanza kugoma baada ya siku mbili serikali kwenda Mahakamani

      madaktari nao wameanza kuwa wanasiasa eeeh! gomeni tumechoka na kelele zenu mnatutiiisha!!!! tutaenda kwa waganga wa jadi sasa, kitu kidogo mnataka kugoma duuu!
      "Kama tunalipa wabunge sitting allowances, basi tulipe walimu standing allowance!"- Dr.Slaa

    7. RMA
      #105
      RMA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2010
      Posts : 410
      Rep Power : 519
      Likes Received
      87
      Likes Given
      0

      Default Re: Madaktari waamua kuanza kugoma baada ya siku mbili serikali kwenda Mahakamani

      Wagome tu sisi makamanda wa kesho tupo nyuma yao!!!

    8. Miaka 50

    9. #106
      sembuli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2012
      Posts : 599
      Rep Power : 487
      Likes Received
      243
      Likes Given
      167

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      naunga mkono hoja 500% gomeni tena hata referal za nje ya nchi kutibiwa waheshimiwa hakuna kutoa.mh mnyika sasa nakuelewa kwa nini ulisema vile mjengoni.

    10. #107
      Mrimi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th July 2011
      Posts : 1,225
      Rep Power : 735
      Likes Received
      327
      Likes Given
      314

      Default Re: Madaktari waamua kuanza kugoma baada ya siku mbili serikali kwenda Mahakamani

      Ninakerwa na hizi post za mgomo wa madaktari kuwekwa ktk hili jukwaa la siasa. Kwani mmeambiwa issue hii inahusiana na siasa?

    11. #108
      meningitis's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2010
      Location : sewahaji
      Posts : 2,918
      Rep Power : 3206
      Likes Received
      1014
      Likes Given
      149

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      COMFIRMED: dr rose mrina wa kilimanjaro atangaza kuunga mkono mgomo wa madaktari.
      Source:ITV
      Laurence likes this.

    12. #109
      meningitis's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2010
      Location : sewahaji
      Posts : 2,918
      Rep Power : 3206
      Likes Received
      1014
      Likes Given
      149

      Default

      Quote By Andy1
      Mwinyi kabariki mgomo wa madr, kupeleka swala tume ya usuluhishi ili hatua za sheria zifuatwe ikiwamo mahakama ya kazi
      mwinyi acha kuhadaa umma!
      My take:huduma za afya zitasitishwa mpaka mahakama ya kazi itoe uamuzi.madaktari wote watakuwa wanahudhuria kesi mahakamani.

    13. #110
      Laurence's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2011
      Location : ULIMWENGUNI
      Posts : 2,042
      Rep Power : 1394
      Likes Received
      175
      Likes Given
      41

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      Nipo Kigoma kwa sasa ngoja nifuatilie nione nao wanasemaje juu ya kujiunga na wenzao

    14. #111
      Laurence's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2011
      Location : ULIMWENGUNI
      Posts : 2,042
      Rep Power : 1394
      Likes Received
      175
      Likes Given
      41

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      NI kweli hapa KIGOMA ulianza tokea asubuhi,haya keyjei kazi unayo mzee maana hamuwezi badilisha chochote kwa sasa hapa nchini

    15. #112
      Kabembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2009
      Location : ITETE-Kandwesi
      Posts : 876
      Rep Power : 702
      Likes Received
      170
      Likes Given
      169

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      Hakuna atakaye walaumu mkigoma,viongozi wa nchi hii ni viburi na waliojaa ubinafsi na dharau na ndio maana hawaoni haya kujiongezee posho za mattako na mishahara kwa kazi ya kupiga domo,kugonga meza na kulala.

    16. #113
      sahini's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th April 2012
      Posts : 22
      Rep Power : 360
      Likes Received
      3
      Likes Given
      10

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      Ninawaunga mkono kabisa na niko nao mwanzo mwisho kwa wameshindwa kuwawekea mazingira mazuri ya kazi.Twende mbele

    17. #114
      meningitis's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th November 2010
      Location : sewahaji
      Posts : 2,918
      Rep Power : 3206
      Likes Received
      1014
      Likes Given
      149

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      wabunge wameongezewa posho kufikia milioni kumi kwa mwezi.madaktari wanaotaka milioni 3.5 wameambiwa haiwezekani.

    18. #115
      jingalao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th October 2011
      Location : kikonga
      Posts : 728
      Rep Power : 529
      Likes Received
      127
      Likes Given
      27

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      idadi y amadaktari nchini ni ngapi?


      KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

    19. #116
      Ndekirhepva's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2012
      Location : Lubumbash
      Posts : 304
      Rep Power : 413
      Likes Received
      27
      Likes Given
      77

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      Quote By Uda
      no politics!
      serikali yako ya ccm ndio inafanya mambo mengine hata kama yallikua sio ya kupeleka mbali yafike huko,

    20. #117
      Nyamizi's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 19th February 2009
      Posts : 351
      Rep Power : 592
      Likes Received
      115
      Likes Given
      646

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      Tuko pamoja Madaktari,gomeni mpaka mtekelezewe hoja zenu,serikali isiwafanye kuwa kama mtoto mdogo unampa ahadi ya kumletea zawadi ya gari akiwa anakulilia ukitaka kutoka nyumbani, ukirudi huna hilo gari ulilomwahidi na kisha sahau kama ulimuahidi.

    21. #118
      sahini's Avatar
      Member Array
      Join Date : 28th April 2012
      Posts : 22
      Rep Power : 360
      Likes Received
      3
      Likes Given
      10

      Default Mgomo wa madaktari wa sasa unatisha!!!!

      Viongozi wanapokosa utashi wa dhati,haya ndio majibu yake.Mgomo wa madaktari umeandaliwa na wamejipanga kwa kutoa taarifa karibia kwa kila jamii.Tuwaelewe,niko nao kwa mikono na miguu yote.

    22. #119
      marejesho's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 6th January 2011
      Location : MULA
      Posts : 3,364
      Rep Power : 13046
      Likes Received
      1553
      Likes Given
      1137

      Default Re: Mgomo wa madaktari wa sasa unatisha!!!!

      Endelea kutupa updates mkuu!

    23. #120
      satellite's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th November 2010
      Location : HOMELAND SECURITY
      Posts : 546
      Rep Power : 540
      Likes Received
      94
      Likes Given
      60

      Default Re: Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

      Quote By Jackbauer
      baada ya kushuhudia migomo ya madaktari kwa awamu mbili na baadaye kufuatiwa na majadiliano yalioyoisha hivi karibuni sasa kuna kila dalili ya kutokea kwa mgomo mwingine mara itakapofika tarehe 23 juni 2012.
      migomo miwili ya kwanza ilipuuzwa hivihivi lakini mwishowe tuliona viongozi wakuu wa nchi wakirudi nyuma na kuomba huruma ya mazungumnzo.
      je iwapo mgomo wa tarehe tajwa utatokea ni nani alaumiwe kwa kushindwa kutatua mgogoro huu uliodumu kwa kipindi cha nusu mwaka sasa??


      haya ni ya morogoro


      haya ni ya BUGANDO





      na haya ni ya Dodoma karibu kabisa na mjengoni


      updates;Taarifa zilizonifikia ni kuwa madaktari wa KCMC wametoa tamko la kujiunga kwenye mgomo huu kupitia televisheni ya ITV.



      nawasilisha...

      SEASON 3 hii nahisi itakua balaa,ngoja nisubiri ianzwe kurushwa

    Page 6 of 9 FirstFirst ... 45678 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...