Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 23
    1. #1
      Omutwale's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2008
      Location : Kanyigo
      Posts : 1,138
      Rep Power : 811
      Likes Received
      578
      Likes Given
      496

      Default Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Bado najiuliza kwa nini “washika mipini” (Spika, Majaji, Mwanasheria Mkuu, Mawaziri, n.k) kwa maksudi wanachukua maamuzi ya kusiliba kaburi la ccm? Hakuna hata mmoja anajifunza kutokana na makosa yake ya awali au ya mtangulizi wake!

      Tuliona la Dr. Slaa na EPA Bungeni mwaka 2007, CDM wakashinda kesi Mahakama ya Wananchi na bado wanazidi kuvuna riba ya makosa yalitokana na udhaifu wa Bunge la wakati ule. Ikaja mwaka 2008 Zitto akafukuzwa Ubunge, wimbi la ushindi wa kuungwa mkono na wananchi likaendelea kusimama upande cha CDM. Bunge jipya 2011 tumewabeza CDM na Katiba, leo hii tunafakamia matapishi yetu tukiwa chooni kwa wapinzani. Juzi juzi tu Jaji wa Mahakama katika kesi ya Uchaguzi wa Arusha, kwa kufikiri amefanya kazi ya kusifiwa na chama, kaleta balaa uraiani kwa kumuacha Godbless Lema alande lande nchi nzima. Sasa badala ya watu wa Arusha wavue magamba, nchi nzima hata watoto wanavaa magwanda. Bado tu hatujajifunza wala kuwafunza au kuwaeleza watoa maamuzi kwamba; chonde chonde kujipendekeza kwenu kwa nia ya kukinusuru Chama Tawala, serikali na Taasisi zake (Bunge, Uraisi, Mahakama) havisaidii bali ndo vinamwaga petrol kwenye tanuru la kuni kavu za zinazoiteketeza serikali! Wananchi wa Tanzania ya leo, si wa Tanganyika ya Mwaka 1947! Wana maamuzi rohoni mwao tayari kwa kiama cha serikali yao hapo mwaka 2015.

      Ukiyatazama haya yote huwezi kuja na uamamuzi kama wa leo juu ya JJ Mnyika. Watoa maamuzi wa serikali yetu ya ccm lazima wajue kuwa hawa CDM wakati mwingine wanachezea sharubu za simba maksudi kwa sababu wanajua Simba mwenyewe ni wa plastiki. Na akibahatika kuwa na betri zenye chaji inayomwezesha kuunguruma basi ni furaha zaidi Maana watoto wa wana CDM wanafaidi muungurumo wake!

      Hivi kuna upya gani katika neno “UDHAIFU” lililosemwa na Mnyika leo Bungeni? Mbona watu wengi sana ikiwemo viongozi wa Dini na Vyama vya Siasa wamelisema na kulirudia neno hili na wakilihusisha na Taasisi ile ile (Rais Kikwete) bila kuchukuliwa hatua yoyote?

      Juzi Prof. Lipumba kasema wazi Rais JK ni dhaifu na kaenda mbali zaidi kumsifia Mkapa na utawala wake. Mh. Sitta akiwa Spika aliwahi kusema “kiutu uzima” kuwa “wewe rais umekuwa mpole mno” Hapa kwa wenye kung’amua Sitta alitumia uungwana tu kukwepa kutumia neno DHAIFU. Angeweza kusema “wewe rais umekuwa DHAIFU mno". Pia mwandishi Kondo Tutindaga – katika MwanaHalisi ya tarehe 01 June 2011 iliyobeba kichwa cha mada “Ni ubaya wa Lowassa au udhaifu wa JK?” alitumia neno “UDHAIFU” kama kisifa cha Rais JK si chini ya mara 15. Upya uko wapi mpaka huyo Spika anampa Mnyika kupiga penalti kwenye goli lisilo na golikipa?!

      Hapa chini ni baadhi ya waandishi wachache tu miongoni mwa Watanzania lukuki waliosema hadharani UDHAIFU wa Rais Kikwete

      Kondo Tutindaga
      ………..Hali ya nchi kwa sasa ni tete kisiasa, kiuchumi na hata kijamii. Wale wanaojipendekeza kwa Rais Kikwete ni wepesi kumshauri kuwa anayesababisha haya ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na wengine wanamwambia sababu ni mapacha watatu. Hakuna anayemwambia rais kuwa udhaifu wake ndicho chanzo cha utete wa taifa…………
      Quote By Pasco
      Nimemkumbuka Nyerere, angekuwepo, tusingefika hapa!. Tukiwaambia JK is a weak president, watu hawataki kukubali!. Hao masheikh wa kukundi cha Uamsho, wanakuwa tolerated under pretex ya religious tolerance hivyo kutenda vitendo vya jinai ya uhaini kwa muda mrefu na kuachwa hivi hivi wakiangaluwa!. Lakini wafuasi wao walipofanya jinai ya violence, ndipo wakakamatwa!. Kwa huu udhaifu wa JK, sasa sio tena CCM itamfia mikononi
      Kondo Tutindaga
      ….. Lakini upo upande wa pili unaowakilishwa na udhaifu wa Kikwete kama Rais na mwenyekiti wa chama chetu. Rais na mwenyekiti mwenye udhaifu wa kiuongozi husababisha makundi ya watu wanaojipendekeza kwake au kujituma kufanya mambo ambayo yeye angefanya……..

      …….Kwamba, udhaifu wa Kikwete ambao wakati mwingine unaitwa “uungwana wake” kwa vile unatendwa na mkuu wa nchi, ndio unaosababisha makada wachinjane, wauane, wakamiane, wasingiziane, na hatimaye waangamizane kisiasa……..

      ………Udhaifu wa Kikwete umelifikisha taifa mahali pagumu sana. Ili kurekebisha hali hii, gharama kubwa kisiasa na kiuchumi itatumika. Rais kwa hofu na aibu ya kusemwa sana na watu, anaweza kuzinduka na kuchukua hatua kwa jazba na hasira na kufanya makosa yanayoweza kuligharimu taifa kwa muda mrefu……….
      Saed Kubenea
      MwanaHalisi 30 November 2011
      Kikwete, Lowassa hapatoshi


      Baadhi ya wachambuzi wa mambo wanasema kauli ya Lowassa ambayo ilitolewa mbele ya viongozi wake wakuu, akiwamo rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ililenga kuonyesha udhaifu wa Kikwete ndani ya CCM kwa kuasisi falsafa ya kujivua gamba na kuikimbiza moja kwa moja kwenye CC na NEC, kinyume cha taratibu na kanuni za chama chake.
      Last edited by Omutwale; 19th June 2012 at 15:30.
      Chakaza, Kigogo, Sikonge and 16 others like this.
      Kijana, litumikie Taifa lako kwa moyo wako woote, akili zako zoote na nguvu zako zoote.

    2. Miaka 50

    3. #2
      palalisote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th August 2010
      Location : WA HAPAHAPA
      Posts : 2,047
      Rep Power : 2035
      Likes Received
      925
      Likes Given
      3819

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      "siku za mwisho watu huikimbia kweli na kufuata manabii wa uwongo"
      Omutwale likes this.

    4. #3
      Power G's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 20th April 2011
      Location : Msoga Kijijini
      Posts : 2,405
      Rep Power : 991
      Likes Received
      773
      Likes Given
      259

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Mkuu, Kikwete si kiongozi DHAIFU tu bali pia ni GOIGOI, kwa sababu hana uwezo au ni muoga wa kuchukua maamuzi kwa wakati. Wala huhitaji kusumbuka kutafuta references kwa ajili ya kuthibitisha hilo, maana hata mke wake na watoto wake wanalitambua hilo.
      Kigogo and Omutwale like this.
      TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE MENO KAMA AKINA EL, JK, EC na RA

    5. #4
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,152
      Rep Power : 24267
      Likes Received
      4662
      Likes Given
      2294

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Na tunaomba waendelee kuzishika hizo mipini ili waendelee kuwaudhi watanzania.
      Nimeona wabunge wengi baadhi wa ccm kila waliposimama waliiponda hotuba ya Zitto, kana kwamba ina kasoro, eti chadema wanawadanganya watanzania.
      wamesahau kuwa bajeti ya upinzani haitaishia bungeni, itaenda kusomwa kwa wananchi ili wajue kuwa ccm ni wasanii, rais ni mdaifu, CCM ni wapuuzi nk.
      Mbunge anapewa dk. 10 kuchangia, badala ya kuijadili bajeti kwa maslahi ya wananchi anabaki kuiponda chadema mpaka dk.10 zinaisha.
      Mungu aendelee kuwafumba macho mpaka kieleweke!
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    6. #5
      MANI's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 22nd February 2010
      Location : CHINI YA MBUYU
      Posts : 1,904
      Rep Power : 950
      Likes Received
      564
      Likes Given
      627

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Omutwale Kuna vitabu vya hadithi wakati tukiwa lower school std i -iv kulikuwa na mfalme mmoja ambaye alitaka ashonewe suti ya kipekee isio na mfano kwa yoyote, kitu ambacho kiliwashinda mafundi wakamwacha mtupu na kumwambia suti yako tayari mwilini. Mfalme alizunguka mitaani akiwa mtupu ili kuonyesha suti yake mpya, na kwa woga wa raia hakuna aliethubutu kumwambia kuwa uko mtupu mpaka mtoto mdogo alipopiga kelele mbona mfalme hakuvaa nguo? Sasa basi nafikiri alichofanya Mnyika ni kumkumbusha mfalme kuwa hajavaa nguo na si zaidi ya hivyo maana kama mabvyo umeweka baadhi ya nukuu hapo juu watu wanajipendekeza hawawezi kumweleza kuwa udhaifu .
      " TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA"

    7. Study Abroad

    8. #6
      Alfred Daud Pigangoma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th March 2009
      Location : TABORA, TANZANIA
      Posts : 636
      Rep Power : 643
      Likes Received
      256
      Likes Given
      209

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Imewapasa wafanye hivyo kama walivyoagizwa na mkuu wa kaya kuwatoa nje wale wote watakao onekana kupinga na ole wao waingize neno ambalo litaweza kubadilishwa na jamii ikaamini kuwa ni tusi...

      Sishangai kwani ndugu na jamaa wa marehemu wamekwishawasiri (CUF, TLP, UMD na sasa Mbatia wamemleta ili awe mshika chetezo kwa tiketi ya NCCR) kama ni kaburi tayari limekwisha chimbwa.... MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI ALIPOJICHAGULIA, AMMMMEEEEEENNNN!!!!!!!
      “The person who says it cannot be done should not interrupt the person doingit.” Chinese proverb

    9. #7
      Omutwale's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2008
      Location : Kanyigo
      Posts : 1,138
      Rep Power : 811
      Likes Received
      578
      Likes Given
      496

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Quote By MANI
      Omutwale Kuna vitabu vya hadithi wakati tukiwa lower school std i -iv kulikuwa na mfalme mmoja ambaye alitaka ashonewe suti ya kipekee isio na mfano kwa yoyote, kitu ambacho kiliwashinda mafundi wakamwacha mtupu na kumwambia suti yako tayari mwilini. Mfalme alizunguka mitaani akiwa mtupu ili kuonyesha suti yake mpya, na kwa woga wa raia hakuna aliethubutu kumwambia kuwa uko mtupu mpaka mtoto mdogo alipopiga kelele mbona mfalme hakuvaa nguo? Sasa basi nafikiri alichofanya Mnyika ni kumkumbusha mfalme kuwa hajavaa nguo na si zaidi ya hivyo maana kama mabvyo umeweka baadhi ya nukuu hapo juu watu wanajipendekeza hawawezi kumweleza kuwa udhaifu .
      MANI

      Umenikumbusha enzi za Zama za "Uwazi na Ukweli" Jenerali Ulimwengu aliamua kumweleza Che Nkapa kuwa "Mfalme uko uchi" adhabu yake akaambiwa "wewe si raia"

      Ndiyo...tunahitaji watu wa kumueleza Mfalme jinsi sura yake ilivyo, maumbile yake na muonekano wake kwa watu wake. Inaniuma sana kila nikiongea na East Africana "wananisifia" eti Watanzania tuna Rais Handsome! Aibu iliyoje badala ya tusifiwe kwa kutumia vema utajiri wa rasilimali tulio jaaliwa kukuza uchumi, tunapakwa lipsticks na cosmetics kwa sababu ya udhaifu wa Wakuu wetu.
      Last edited by Omutwale; 20th June 2012 at 00:21.

    10. #8
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,650
      Rep Power : 715
      Likes Received
      289
      Likes Given
      36

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Wajifunze Kenya ambako katiba yao inawataka waombe upya kazi zao kwenye tume huru, na wote waliojihusisha na matumizi mabaya ya madaraka na wizi mwingine, Tufike mahala tuwe waadilifu kwa manufaa ya nchi yetu
      Omutwale likes this.

    11. #9
      Kigogo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2007
      Location : Calabash
      Posts : 8,146
      Rep Power : 2084
      Likes Received
      1219
      Likes Given
      313

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      hivi dhaifu ni = na kutokuwa na akili?
      ______________________________ _
      Niko tayari kufa huku nimesimama kuliko kuishi huku nimepiga magoti....

    12. #10
      Rwechu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 17th March 2009
      Posts : 76
      Rep Power : 533
      Likes Received
      12
      Likes Given
      0

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Angalia mh alivyotolewa chini ulinzi wa masajenti wa bunge
      Attached Thumbnails    

    13. #11
      wagaba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 598
      Rep Power : 478
      Likes Received
      123
      Likes Given
      92

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Omutwale, well said mkuu. upinzani unapelekwa makida makida na chama tawala. Lakini huu ushabiki wa kinyambaf una mwisho wake.
      Haya magamba yamekaa vikao mapema ili kutetea hiyo budget bila ya kuangalia masilahi ya Taifa. Matokeo yake akina Komba (mnyama anaepiga mnazi) anakurupuka na kuunga mkono bajeti 100% huku akisema jimbo lake ni masikini sana asaidiwe!!
      unaunga mkono mavi!!! Wako brain washed kama members wa Mirembe!
      B....shit!
      Mnyika apige mawe kama kawa, after all, yupo ktk kibanda cha makuti, hakuna vioo!
      Omutwale likes this.
      "Tanzania ni ya watanzania, na watanzania wenyewe ndo sisi"

    14. #12
      andrews's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th March 2012
      Posts : 1,683
      Rep Power : 0
      Likes Received
      142
      Likes Given
      76

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      manabii wa uongo nape lusinde komba mwigulu na mpuuzi kama wewe

    15. #13
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,707
      Rep Power : 1309
      Likes Received
      712
      Likes Given
      146

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Omutwale well said sir Maspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano,Wabunge wa CCM na Mawaziri hawajitambui jinsi wanavyoipaisha CDM
      Omutwale likes this.

    16. #14
      swrc's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th June 2012
      Posts : 442
      Rep Power : 548
      Likes Received
      35
      Likes Given
      18

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Power


      Today 15:16
      #3 JF Premium Member Array


      Join Date : 20th April 2011
      Location : Msoga Kijijini
      Posts : 1,898
      Rep Power : 740
      Likes Received537
      Likes Given37


      Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Mkuu, Kikwete si kiongozi DHAIFU tu bali pia ni GOIGOI, kwa sababu hana uwezo au ni muoga wa kuchukua maamuzi kwa wakati. Wala huhitaji kusumbuka kutafuta references kwa ajili ya kuthibitisha hilo, maana hata mke wake na watoto wake wanalitambua hilo. (HATA MKE WAKE NA WATOTO?)

    17. #15
      meeku's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Location : Kirimatunda
      Posts : 267
      Rep Power : 422
      Likes Received
      51
      Likes Given
      3

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Jamani JK siyo dhaifu tu, bali ni janga la Taifa

    18. #16
      Mwanaweja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 3,447
      Rep Power : 1108
      Likes Received
      457
      Likes Given
      923

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      najiuliza ni aibu sana kushindwa kutoa tofasiri maalumu ya ya neno "dhaifu" ina maana ni tusi naomba wataalamu wa lugha tusaidiane

    19. #17
      zumbemkuu's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : street dweller
      Posts : 5,317
      Rep Power : 1998
      Likes Received
      2114
      Likes Given
      7786

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Taasisi ya urais ni dhaifu na ccm ni wapuuzi including mwenyekiti wao,
      "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema

    20. #18
      Kaitampunu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2011
      Location : Kwenye Corner
      Posts : 653
      Rep Power : 508
      Likes Received
      137
      Likes Given
      195

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Quote By meeku
      Jamani JK siyo dhaifu tu, bali ni janga la Taifa
      JK ni dhaifuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu uuuuuuuuuuu

    21. #19
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,650
      Rep Power : 715
      Likes Received
      289
      Likes Given
      36

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      Watu wengi ni Dhaifu na viongozi wengi ni dhaifu But Sija wahi kumwona rais wa nchi DHAIFU kama Kikwete, Amefanya Nafasi ya urais itamaniwe na hata mazezeta wanaona wanaweza kuliko yeye. haku faa hata kuwa balozi wa nyumba 10

    22. #20
      asigwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Location : TANDHANIYA
      Posts : 4,388
      Rep Power : 1264
      Likes Received
      1207
      Likes Given
      1253

      Default Re: Washika Mipini Mnawaisha Mazishi ya CCM!

      KIPOFU HAWEZI KUMUONGOZA KIPOFU MWENZIE MWISHO WA SIKU WOTE WATATUMBUKIA SHIMONI...
      bubge limeamua kuizika ciciem makusudi kabisaaaaaaaaaaaa

    23. FemaTV & Radio
    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...