Wadau,
Hasa kwa wale waliopata nafasi ya kufuatilia bunge la leo.
Ninayo masikitiko makubwa sana, kwa utoto unaoonyeshwa na baadhi ya wabunge wetu, tuliowaamini na kuwakabidhi nafasi ya kutuwakilisha bungeni. Kwa hakika bunge la bajeti ni miongoni mwa mabunge muhimu sana, sio tu kwa jina lake hapana, pia ni kwa kuwa ndio linakusanya mustakabari wa taifa kwa mwaka mzima ujao
Kwa waliosikiliza bunge la leo, watakubaliana na mimi kwamba wapo wapinzani makini na wenye lengo la kusaidia taifa hili na wapiga kura wao, na wapo waliolewa sifa/utoto kama Mnyika. nitatoa mifano michache toka kwa hoja zilizotolewa leo.
na waheshimiwa.
Mifano wa mpinzani mwenye nia njema
Ndugu Augustine Mrema (TLP):
Wadau, kwa wale waliomsikiliza mrema, alikataa kuiunga hoja bajeti ya serikali, kutokana na udhaifu aliouonyesha. Mweshimiwa mrema alisema kuna matatizo makubwa sana katika utekelezwaji ya yale yaliyokubalika katika bajeti iliyopita kutokana na WIZI na UFISADI wa baadhi ya watendaji katika halmashauri katika jimbo lake, Mrema akaendelea kusema kwa kutolea mfano, kuna pesa ambazo zilitoka hazina na zikaishia kutafunwa na hata ile kazi iliyokusudiwa haikufanyika, pia mrema amesema, katika mafungu yaliyotengewa halmashauri yake, si pesa zote zilifika nyingi hazikufika kwa wakati hadi mwaka wa bajeti ilipoisha.
Lakini pia mrema alizungumzia kuhusu mgogoro wa ardhi ambao umeshapatiwa ufumbuzi na mahakama kuu lakini bado serikali inasita kuchukua hatua, na akaongeza kusema kwa nini kuna double standard? wakati mahakama kuu ikitoa bmaamuzi katika baadhi ya mambo serikali na vyombo husika husimamia amri mara moja na sio kule jimboni mwake?
Kutokana na haya aliyoyorodhesha Mh. Mrema, alisema HATOUNGA mkono hoja hadi ahakikishiwe utekelezaji wa wa kile kilichokuwemo ndani ya bajeti na hao watendaji wa halmashauri kuchukuliwa hatua, pia alimuomba waziri mkuu atoe tamko juu ya hilo.
Wakuu, ukiangalia alichofanya mrema ni kuikataa bajeti kwa hoja na ndio ilivyotakiwa, sasa tuangalie kichekesho cha leo
Mnyika (Chadema)
Huyu ndie alikuwa kituko cha mwaka katika bajeti yetu, takriban dakika 4-7 alizotumia kati ya dakika 10 alizopewa hakuongelea kabisa mahitaji ya wana ubungo, la ajabu alimuattack Kikwete personal, hata alipoambia afute kauli hakufanya hivyo.
Wadau huu ni "UTOTO" wa hali ya juu, na ni dharau kubwa kwa wana ubungo, huenda hili linatokana na uwezo mdogo wa waheshimiwa katika kuichambua bajeti, au SIFA zilizowalevya hawa wabunge wetu. Binafsi nimechukizwa sana na mbunge huyu, ambaye wanaubungo walitegemea ahoji kwa niaba yao matatizo mbali mbali yanayowakumba.
Mwisho, kama ushauri: Wabunge wa upinzani msilewe sifa,wananchi wa majimbno yenu wanaumia. Kama hamna uwezo wa kuchambua bajeti ombeni msaada kwa wanaojua. "Mwaka mwingine, wana ubungo wameupoteza kwa kuchagua WANAHARAKATI"
By:
Tume ya katiba
Follow Us Here