Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 30
    1. #1
      Kiganyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th April 2012
      Posts : 1,162
      Rep Power : 983
      Likes Received
      708
      Likes Given
      400

      Default Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Bernard Membe
      Nimefafanua kuhusu uvumi uliotolewa na vyombo vya habari kuhusu kukutana kwangu na vijana wa CHADEMA waliofika nyumbani kwangu jimboni

      Bernard Membe

      Nimewaeleza kuwa upinzani si uadui na wapinzani si maadui zetu.

      Bernard Membe
      Sijawahi kuitabiria CHADEMA ushindi kwa kuwa sina kipaji hicho ambacho kinapatikana kwa Synovate, Mtoto wa Sheikh Yahya na TD Joshua

      Bernard Membe

      Upinzani upo kwa mujibu wa kanuni, sheria na Katiba hivyo hauwezi kuwa uadui. Wapinzani wako ndani ya vyama vyetu wenyewe

      Bernard Membe

      Nina imani uvumi huu haujaenezwa na CHADEMA bali watu nje ya CHADEMA wenye malengo ya kisiasa haswa kunifitinisha na wana CCM na CHADEMA

      Bernard Membe

      Kamwe watanzania tusikubali kulishwa kasumba ya kuwa Upinzani wa kisiasa ni uadui. Tusigawanywe kwa itikadi wala dini

      Bernard Membe
      Nawapenda watanzania wote bila kujali itikadi zao, dini zao, makabila yao na marika yao. Umoja wetu ndio nguvu yetu.

      MY TAKE; Nyoka ya MDIMU haiaminiki au Magazeti yalizusha hizo taarifa??

      Magamba wengine igeni toka kwa Membe kuwa na political tolerance!
      Quote By mlagha
      Bahati nzuri mimi nimeshiriki press Conference hii. Mhe. Membe alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Wizara ambayo yamekuwa yakiandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari isivyo.

      Masuala hayo ni pamoja na taarifa kuhusu uwasilishwaji wa Ripoti ya Tanzania kuhusu Mpango wa Nchi za Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

      Katika suala hili Mhe. Membe alitoa ufafanuzi kuwa, ni kweli Mhe. Rais hatoweza kuwasilisha ripoti ya tathmini ya Tanzania katika Mkutano ujao wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika mjini Addis Ababa mwezi Julai, 2012 kwa kuwa Timu ya Umoja wa Afrika chini ya APRM inayopitia ripoti hiyo ya Tanzania haijakamilisha kazi hiyo. Hivyo Tanzania itawasilisha ripoti yake Januari 2013baada ya timu hiyo kuipitia na si kwa sababu Tanzania inadaiwa Dola za Marekani laki nane (800,000) kama mchango wake kwa mpango huo.

      “APRM ni chombo kilichoanzishwa na Serikali za Afrika na kwa hapa Tanzania kinaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje, ni chombo cha hiari kwa nchi za Afrika kujitathmini zenyewe kiutawala bora, si kweli kuwa Rais atashindwa kuwasilisha Ripoti ya Tanzania AU kwa sababu hatujalipa deni, bali ni kwa sababu timu inayopitia ripoti hiyo ya Tanzania haijakamilisha kazi yake hivyo tunatarajia kuwasilisha ripoti yetu mwezi Januari 2013 wakati wa kikao kingine cha Wakuu wa nchi wa AU,” alisema Mhe. Membe.

      Kuhusu suala la fedha zilizotoweka Wizarani, Mhe. Membe alieleza kuwa hakuna fedha zilizopotea isipokuwa Wizara imewasimamisha kazi Watumishi watano waliofanya mchakato wa kuhamisha kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kutoka Hazina kuja Wizarani kwa ajili ya ziara za Mhe. Rais za Addis Ababa, Geneva,…na Arusha bila kibali cha Afisa Masuuli yaani Katibu Mkuu ambaye hakuwepo wakati mchakato huo unafanyika.

      Aliongeza kuwa, Watumishi hao wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguziunaofanywa na kamati iliyoundwa ili kujiridhisha kama taratibu za kifedha zilifuatwa au kukiukwa katika mchakato huo mzima.

      “Tarehe 1 Machi, 2012 wakati mimi sipo Wizarani wala Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu kuna mchakato wa kuhamisha fedha kiasi cha shilingi bilioni 3.5 ulifanywa kutoka Hazina kuja Wizarani kwa ajili ya safari za Mhe. Rais za Geneva, Addis Ababa,…..na Arusha bila kibali cha Afisa Masuuli. Timu inayojumuisha watu kutoka TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Wizara na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali imeundwa ili kuchunguza suala hilo ili kujua kama taratibu za kifedha zilifuatwa au kukiukwa na uchunguzi ukikamilika tutaweka hadharani hakuna cha kuficha,” alisema Mhe. Membe.

      Vile vile, Mhe. Membe alipinga uvumi unaoenezwa kuwa amekitabiria ushindi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kwa kusema kuwa yeye si mtabiri na kwamba yeye ni mwanachama halisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa maneno na kwa matendo.

      Mhe. Membe aliongeza kuwa alichokifanya ni ukarimu kwa kuwakaribisha Vijana wa CHADEMA jimboni kwake Mtama mkoani Lindi na kushiriki nao chakula nyumbani kwake.

      “Ukarimu hauna udini, rangi wala itikadi, vijana wa CHADEMA walikuja nikawakaribisha kwa chakula nyumbani, na leo nataka niwape somo kidogo, upinzani sio uadui, nchi inayoona upinzani ni uadui haiko salama wala haitaendelea,”alisisitiza Mhe. Membe.
      Last edited by Kiganyi; 18th June 2012 at 13:51.
      Sheba and Profesa like this.

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      palalisote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th August 2010
      Location : WA HAPAHAPA
      Posts : 2,071
      Rep Power : 2041
      Likes Received
      938
      Likes Given
      3842

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      watakuja hapa kuweka video yake halafu atakataa kuwa nayo siyo yeye imefanyiwa photoshop tu
      Last edited by palalisote; 18th June 2012 at 14:29.

    4. #3
      Negotiator's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 9th August 2010
      Posts : 301
      Rep Power : 510
      Likes Received
      36
      Likes Given
      35

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      wenye video clip watuwekee hapa jamani. tuache kuandikia mate
      '

    5. #4
      Precise pangolin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 5,687
      Rep Power : 1913
      Likes Received
      1583
      Likes Given
      676

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Uwaziri utayeyuka sasa hivi

    6. #5
      matawi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th March 2010
      Posts : 1,449
      Rep Power : 754
      Likes Received
      123
      Likes Given
      67

      Default

      Quote By palalisote
      watakuja hapa kuweka video yake halafu atakaa kuwa nayo siyo yeye imefanyiwa photoshop tu
      Asante Membe mtu yeyote anaweza kutabiri maana utabiri na matokeo siyo lazima vilingane ila sasa utabiri wako umeutimiza kwa kusema aliyeeneza uvumi hatoki ndani ya chadema-asante baba

    7. Miaka 50

    8. #6
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,315
      Rep Power : 1200
      Likes Received
      1184
      Likes Given
      1560

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      kwani? hau vijana wa chadema walienda kwa membe kupigiwa ramli au vipi?
      saddam likes this.

    9. #7
      Sheba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 199
      Rep Power : 553
      Likes Received
      83
      Likes Given
      34

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Kumbe Membe anatweet! Safi sana.

      Ila msimamo na mtazamo wake huu nimeukubali. Wana ccm wangekuwa na mawazo ya aina hii nchi yetu ingekuwa mbali sana. Kwa mtaji huu zile nyimbo za Komba " wapinzani tuwachane chane tuwatupe" zimepitwa na wakati. Kwa mtazamo wangu CHADEMA wanafanya kazi nzuri ya siasa sidhani kama wanasubiria Membe awatabirie ndio waone.

      Utimilifu wa kazi yao unaonekana dhahiri kwenye mapokeo ya watu. Nadhani Membe yuko sahihi, sdhani kama CHADEMA ndio wenye kueneza uvumi huu, watakuwa ni wanasiasa ndani ya CCM wenye siasa za maji taka.
      TMwamafupa likes this.
      Argue Dont Shout,shouting will make it worse.......if you are forced to be really nasty, don't shout;use ridicule instead. Ridicule is argument; and it requires knowledge!-Mwl.Nyerere 1969

    10. #8
      Sheba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 199
      Rep Power : 553
      Likes Received
      83
      Likes Given
      34

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Quote By Negotiator
      wenye video clip watuwekee hapa jamani. tuache kuandikia mate
      Video ingekuwep siamini kama tungepata hata fursa ya kuiulizia ingeshawekwa long time.
      Argue Dont Shout,shouting will make it worse.......if you are forced to be really nasty, don't shout;use ridicule instead. Ridicule is argument; and it requires knowledge!-Mwl.Nyerere 1969

    11. #9
      Mgelukila's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th May 2012
      Posts : 224
      Rep Power : 396
      Likes Received
      42
      Likes Given
      2

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Mh Membe anaonyesha ni mkomavu ktk siasa, anajiamini, anasimama ktk kweli na kweli inamweka huru, bila kujua dini yake ana hofu ya Mungu anajua mbele ya safari kuna kuulizwa juu ya matendo ya hapa duniani.
      Sheba likes this.

    12. #10
      Negotiator's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 9th August 2010
      Posts : 301
      Rep Power : 510
      Likes Received
      36
      Likes Given
      35

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Quote By Sheba
      Video ingekuwep siamini kama tungepata hata fursa ya kuiulizia ingeshawekwa long time.
      nasikia tu kua alioneshwa live ITV akitamka maneno hayo.
      '

    13. #11
      Tumaini Makene's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2012
      Posts : 1,062
      Rep Power : 8907
      Likes Received
      2231
      Likes Given
      768

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Hivi anachokanusha hapa Membe ni kitu gani. Vyombo vya Habari vinavyoaminika viliandika na kutangaza maneno ya Membe. Wazi kabisa. Hawakuongeza wala kupunguza. Wangefanya hivyo wangekuwa wanakiuka misingi muhimu ya tasnia muhimu ya uandishi wa habari. Angekuwa na haki ya kuwashtaki (ofcourse MCT).

      Kwa mtu yeyote makini hapa kaongeza tu stori nyingine, AMEPINGANA NA PROPAGANDA ZA HOVYO, CHEAP ZA CHAMA CHAKE CCM na wana CCM wenzake. Stori juu ya stori. Asante Membe. Tusubiri kesho watakuandikaje au leo jioni kwenye Tvs zetu.

      Ofcoz with the coming back of Andrew Chenge on board and the like wakiendelea kujipatia nguvu katika Kamati za Bunge na sasa wakielekea kuliteka bunge, baada ya kuwa wameishaiteka ikulu, wakaiteka CCM na wameiweka mfukoni serikali ya CCM, watu kama Membe hawana namna sasa hivi isipokuwa kujionesha kuwa wako upande wa wanamabadiliko!

      Mtu kama Membe na wenzake ni wa kuazimwa milango yote ya fahamu, kwa tahadhari kubwa hata wanachosema (kwa kuchelewa sana) ni ukweli.

      "Nothing in the world is more dangerous than sincere ignorance and conscientious stupidity." Martin Luther King

    14. #12
      TandaleOne's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th September 2010
      Location : SF Kiosk Tandale Sokoni
      Posts : 1,144
      Rep Power : 670
      Likes Received
      170
      Likes Given
      61

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Mhe. Membe ni mtu muelewa na mwenye msimamo makini..,anajitambua lakini pia anawatambua wanasiasa wenzake ndani ya Nchi hii. Yuko sahihi akisema kuwa upinzani si uadui. Haina maana kwa watanzania kuwagawa kwa misingi yeyote hata ikiwa ina manufaa ya kisiasa ndani yake.,kwani ubaguzi wa aina yeyote hauna mwisho mwema.
      Hatred is gained as much by good works as by evil.
      Niccolo Machiavelli

    15. #13
      SAGANKA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th June 2012
      Posts : 272
      Rep Power : 241
      Likes Received
      187
      Likes Given
      32

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Maneno ya membe yana uoga ndani yake. Awe ametabiri au la,kulikuwa na ulazima gani wa kujibu,Kama anajua vyama vya siasa vipo kwa mujibu wa sheria,nini ubaya wa kukitabiria ushindi chama mojawapo. Na kwanini ameamua kukanusha leo,pengine hilo nalo angetuambia,kwamba alikuwa anatafakari nini hadi leo.

      Na kwanini aseme yeye si mpiga ramli wakati tayari amekwisha tuambia kuwa aliyesema maneno hayo si CCM wala CHADEMA,ni nani basi kama si ramli.

      Kaka yangu Membe, elewa kuwa wananchi ndio walinzi wa kweli wa mpenda haki,mwalimu Nyerere alikuwa akikisema sana chama cha mapinduzi, lakini haikuwahi kuonekana kama ana hatari ya kufanyiwa jambo baya na chama chake kwani siku zote alilindwa na wananchi. Wewe unaogopa chama kusimamia ukweli.

      Mbona hujatuambia jitihada zako za ku-establish mahakama ya kadhi ziliishia wapi,hizo ndo baadhi ya ajenda muhimu za kutuelezea wa-tz na sio whether uliitabiria CDM ushindi au la!

    16. #14
      asigwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Location : TANDHANIYA
      Posts : 4,389
      Rep Power : 1265
      Likes Received
      1208
      Likes Given
      1253

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Kwa mtu mwenye akili hata hizi kauli ukizichunguza bado unaona zina mwelekeo chanya kuelekea CHADEMA...ameng'ata na kupuliza hapa hamna kupinga wala kuunga mkono
      CHEZEA POLITICIANS WEWE........

    17. #15
      mlagha's Avatar
      Member Array
      Join Date : 12th March 2011
      Posts : 52
      Rep Power : 425
      Likes Received
      8
      Likes Given
      2

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Bahati nzuri mimi nimeshiriki press Conference hii. Mhe. Membe alitumia fursa hiyo kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu Wizara ambayo yamekuwa yakiandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari isivyo.

      Masuala hayo ni pamoja na taarifa kuhusu uwasilishwaji wa Ripoti ya Tanzania kuhusu Mpango wa Nchi za Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

      Katika suala hili Mhe. Membe alitoa ufafanuzi kuwa, ni kweli Mhe. Rais hatoweza kuwasilisha ripoti ya tathmini ya Tanzania katika Mkutano ujao wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) unaotarajiwa kufanyika mjini Addis Ababa mwezi Julai, 2012 kwa kuwa Timu ya Umoja wa Afrika chini ya APRM inayopitia ripoti hiyo ya Tanzania haijakamilisha kazi hiyo. Hivyo Tanzania itawasilisha ripoti yake Januari 2013baada ya timu hiyo kuipitia na si kwa sababu Tanzania inadaiwa Dola za Marekani laki nane (800,000) kama mchango wake kwa mpango huo.

      “APRM ni chombo kilichoanzishwa na Serikali za Afrika na kwa hapa Tanzania kinaratibiwa na Wizara ya Mambo ya Nje, ni chombo cha hiari kwa nchi za Afrika kujitathmini zenyewe kiutawala bora, si kweli kuwa Rais atashindwa kuwasilisha Ripoti ya Tanzania AU kwa sababu hatujalipa deni, bali ni kwa sababu timu inayopitia ripoti hiyo ya Tanzania haijakamilisha kazi yake hivyo tunatarajia kuwasilisha ripoti yetu mwezi Januari 2013 wakati wa kikao kingine cha Wakuu wa nchi wa AU,” alisema Mhe. Membe.

      Kuhusu suala la fedha zilizotoweka Wizarani, Mhe. Membe alieleza kuwa hakuna fedha zilizopotea isipokuwa Wizara imewasimamisha kazi Watumishi watano waliofanya mchakato wa kuhamisha kiasi cha shilingi bilioni 3.5 kutoka Hazina kuja Wizarani kwa ajili ya ziara za Mhe. Rais za Addis Ababa, Geneva,…na Arusha bila kibali cha Afisa Masuuli yaani Katibu Mkuu ambaye hakuwepo wakati mchakato huo unafanyika.

      Aliongeza kuwa, Watumishi hao wamesimamishwa kazi ili kupisha uchunguziunaofanywa na kamati iliyoundwa ili kujiridhisha kama taratibu za kifedha zilifuatwa au kukiukwa katika mchakato huo mzima.

      “Tarehe 1 Machi, 2012 wakati mimi sipo Wizarani wala Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu na Mhasibu Mkuu kuna mchakato wa kuhamisha fedha kiasi cha shilingi bilioni 3.5 ulifanywa kutoka Hazina kuja Wizarani kwa ajili ya safari za Mhe. Rais za Geneva, Addis Ababa,…..na Arusha bila kibali cha Afisa Masuuli. Timu inayojumuisha watu kutoka TAKUKURU, Usalama wa Taifa, Wizara na Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali imeundwa ili kuchunguza suala hilo ili kujua kama taratibu za kifedha zilifuatwa au kukiukwa na uchunguzi ukikamilika tutaweka hadharani hakuna cha kuficha,” alisema Mhe. Membe.

      Vile vile, Mhe. Membe alipinga uvumi unaoenezwa kuwa amekitabiria ushindi Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015 kwa kusema kuwa yeye si mtabiri na kwamba yeye ni mwanachama halisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa maneno na kwa matendo.

      Mhe. Membe aliongeza kuwa alichokifanya ni ukarimu kwa kuwakaribisha Vijana wa CHADEMA jimboni kwake Mtama mkoani Lindi na kushiriki nao chakula nyumbani kwake.

      “Ukarimu hauna udini, rangi wala itikadi, vijana wa CHADEMA walikuja nikawakaribisha kwa chakula nyumbani, na leo nataka niwape somo kidogo, upinzani sio uadui, nchi inayoona upinzani ni uadui haiko salama wala haitaendelea,”alisisitiza Mhe. Membe.
      Invisible and Profesa like this.

    18. #16
      Comi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 962
      Rep Power : 578
      Likes Received
      156
      Likes Given
      2

      Default Membe akana kukitabiria chadema ushindi mwaka 2015

      Waziri wa mambo ya nje benard membe akana kusema kwamba alikitabiria chama cha chadema pamoja ni vyama vingine kushinda katika chaguzi za mwaka 2015

      chanzo :star tv

    19. #17
      Tumaini Makene's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th January 2012
      Posts : 1,062
      Rep Power : 8907
      Likes Received
      2231
      Likes Given
      768

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      He still adds no value. Ameendelea ku-cement tu yaliyoandikwa. Ok bado APRM hapa tunaipitia, je vipi kuhusu kuwa tunadaiwa Dola Laki 8...?
      "Nothing in the world is more dangerous than sincere ignorance and conscientious stupidity." Martin Luther King

    20. #18
      Bubona's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st August 2011
      Posts : 280
      Rep Power : 447
      Likes Received
      53
      Likes Given
      11

      Default Re: Membe akana kukitabiria chadema ushindi mwaka 2015

      Akane asikane huo ndio ukweli. Hata hivyo kachelewa sana kukanusha! Ni sawa na mtu kuzuia message aliyomaliza kuituma kwenye simu yake, haiwezekani. Message was delivered!!!

    21. #19
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,657
      Rep Power : 717
      Likes Received
      291
      Likes Given
      36

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      Ushindi wa CDM uko wazi hauhitaji mtabiri kuutabiria, hata kama membe asingekua ametabiri CDM ndo washindi
      Kilasara and Tumaini Makene like this.

    22. #20
      Endeleaaa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Posts : 556
      Rep Power : 705
      Likes Received
      125
      Likes Given
      43

      Default Re: Membe akanusha kuitabiria CHADEMA ushindi 2015!!

      AMESEMA MTU ATAKAELETA USHAHIDI WA UTABIRI HUO BASI YEYE ATAKUWA TAYARI KUWAJIBIKA. mwenye ushahidi wa kauli kuwa CHADEMA itachukua nchi 2015 aweke tuone uwajibikaji wa mkuu Membe.
      1. HARNESS THE POWER OF CHANGE, 2. FACE REALITY!, 3. MANAGING LESS IS MANAGING BETTER
      4. CREATE A VISION AND THEN GET OUT OF THE WAY

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...