Uvumi ulioenea kuwa Mbunge wa Korogwe Vijijini Steven Ngonyani a.k.a. Prof. Maji Marefu (C.C.M) amefariki dunia
Sio wa kweli baada ya yeye mwenyewe kutembelea baadhi ya mitaa kuuthibitishia uma kuwa bado anahema.
Habari zinasema kuwa, uvumi huo uliwashtua wengi na kutokana na simu pamoja na watu wengi kufika nyumbani kwake ilimpasa mbunge huyo kutembea na Lap top yake ili kwa kadri alivyoweza-awaonyeshe watu kile kilichofanyika akiwa nchini India kwa matibabu.
Hata hivyo, shuhuda mmoja anasema kuwa hali ya mbunge huyo bado haiko sawa na ndio maana hayupo kwenye kikao kinachoendelea sasa DODOMA.
source: Wadau kutoka eneo la tukio. Korogwe

Reply With Quote






Follow Us Here