Mimi hushangazwa sana na viongozi wetu wa Smz kusema kuwa Muungano ukivunjika Wazanzibar waloko Tanganyika waatapata tabu.
Viongozi wenye mawazo haya hawafai kabisa kuwa viongozi wa Serekali ya watu wa Zanzibar na nizaaifu kiuongozi.
Hivi kweli tukubali kuwatetea Wale waloko ugenini huku wandani ya nchi na nchi yao ikipotea kwa visingizio visivyo na Machiko? Maneno haya yamezoweleka na hata kufika hadi viongozi wa Tanganyika kuona ndio kisingizio cha kulinda Muungano na kutula kwa matonge.
Hivi kweli inaingia akilini kuza nchi yetu kwa kisingizio cha wenzetu waloko ugenini au viongozi kuekeza Tanganyika na kuwa na nyumba kule?
Mimi nahisi hichi sio kigezo sahihi cha kuto kulivua hili Jindamizi la Muungano kwa kisingizio cha kiongozi kaekeza miradi yake kule au Wazanzibar wenye kuishi kule, kwani chakujiuliza wenye kuishi Tanganyika ni Wazanzibar tu ndio wageni wa Muungano?.
Jee Muungano ukivunjika ni Wazanzibar tu ndio walengwa, kuna nchi nyingi ziliungana na bada ya kuona Muungano haukizi mahitajio yao na kuamua kuuvunja, mfano Senegali/Gambia, Syria/Egypt, Cheko/Slovakia, South Korea/North Korea etc.
Jee wachina, Wahindi, Walebanoni, Wasouthafrica, Wazambia na nchi jirani za Bara la Tanganyika Muungano ukivunjika hao vipi? Kwani kuna tatizo gani Wazanzibar kuishi Tanganyika na kufuataa sheria zote kama vile wageni wengine wachina na wengine walio Pakana na Tanganyika?.
Ikiwa viongozi wa Tanganyika wamekuwa wakitumia kigezo na ngao ya Kuvunjika kwa Muungano na Wazanzibar waloko Tanganyika, jee nyuma ya upande wa shilingi tukibiruza Watanganyika waloko Zanzibar vipi?
Nashindwa kuona viongozi wa Smz wakijizalilisha kwa kusema Wazanzibar walioko Tanganyika tu na kusahau Watanganyika waloko Zanzibar.
Tuangalie Faida na hasara za Wazanzibar walioko Tanganyika na Watanganyika waloko Zanzibar pindipo Muungano ukivunjika.
Wazanzibar walioko Tanganyika wengi wao ni wafanya biashara na wanaingiza pato kubwa katika Serekali ya Tanganyika kwa kulipa kodi.
Sasa tuangalie Watanganyika na biashara zao za Karanga, Dawa ya Panya na biashaza nyengi wazifanyazo Zanzibar zinaingiza pato gani katika Serekali ya Mapinduzi ya Zanzibar?.

Reply With Quote
Follow Us Here