Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

    Report Post
    Page 7 of 11 FirstFirst ... 56789 ... LastLast
    Results 121 to 140 of 210
    1. #1
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1176
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Nimepata tabu kwa muda ili kujaribu kufikiri na kupata sababu na jibu la maana la waislamu kususia hesabu ya watu nchini yaani sensa. Bado sijaelewa idadi ya watu, ama hesabu ya watu inahusiana vipi na imani za kidini wakati wanaohesabiwa ni watanzania wenye dini mbali mbali walionea na kusambaa nchini kwetu.

      Je! Serikali ikichakachua idadi kamili ya watu wa dini fulani na kutoa idadi tofati kutakuwa na faida gani? Je! idadi ndogo ya waumini inasababisha kupungua imani ya watu kwa dini yao? Ukiwa na imani unaweza kuwa na dini yako peke yako, au ya watu sita tu na bado ikawa dini bila ya halaiki ya watu.

      Au lengo letu ni kushindana idadi na watu wa imani nyingine? Hiyo itakuwa na faida gani kwetu.

      Ikiwa ni hivyo, ushauri wangu ni huu.

      Tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu ya waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika. Maustadhi na mashekhe wetu mbona mengi mnayapigania na kufanikiwa? Je, sensa maalumu kwa ajili ya waislamu tu, itawashinda?

      Hakuna sababu ya kutaka kujua idadi yetu kwa kubebwa na sensa ya serikali wakati uwezo tunao watu wakihamasishwa. Huo ndio ushauri wangu, isije ikawa tunafanya mambo kinyume na demokrasia na matakwa ya jamii inayotuzunguuka.
      August, Kinyungu, Pasco and 16 others like this.
      NI FAHARI KUMFUKUZA SIMBA AKAKIMBIA, LAKINI NI HATARI KUFUATA NYAYO ZAKE

    2. FemaTV & Radio

    3. #121
      Las Mas Bobos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 537
      Likes Received
      302
      Likes Given
      84

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Kikwebo
      Ebwana enhe! kumbe saa nyingine Wassira ana point enhe! ambazo mkiingia madarakani 2015 zitakusaidieni..duuh! si mchezo. Labda nikusaidie kitu kimoja..

      ushauri wangu nyie CDM kubalini hiki kipengele ili mkiingia madarakani 2015 mruhusu MoU na Waislamu..kwa kuwa serikali isingekubali kuingia MoU ile ilihali hakuna umuhimu wakujua watu kwa dini zao.?

      Kipengele hiki for your information ni muhimu na serikali inatumia idadi ya wakristo kwa mlango wa nyuma kuwabeba. Hivi kama Wakrosto wangekuwa ni asilimia 2% unadhani wangekubali kuingia nao ile MoU!!! akili zao nikuwa wako wengi ndio maana wakawakubalia kuwapa mabilioni ya shilingi kila mwezi.
      MNACHOSHA, MNAKERA!

      MoU haikuandikwa kwa sababu ya wingi wala uchache wa Wakristo wala Wahindu, MoU iliandikwa kama mkakati wa uboreshaji wa huduma za kijamii zinazotolewa na Kanisa.

      Hivi lini akili itatumika badala ya hisia miongoni mwenu. Kama umeweza kuwa na kaelimu kidogo kiasi unaweza ku-browse web pages unashindwaje kufanya simple reasoning na ubakie kumsikiliza imamu ambaye hajafika hata kidato cha pili?

      Mimi ningewashauri kuwa hawa viongozi wenu wa dini muwasikilize katika yale ya dini lkn ya siasa na maisha mtumie akili zenu. Sina hakika na uelewa wa mtu ambaye hajaenda shule unavyoweza kuwaongoza watu wengine.

      Mpaka hapa nimeanza kusoma motives behind the movements:
      1. Ikiwa Waislamu watakuwa wengi, basi Mahakama ya Kadhi itapata uhalali (Mawazo ya kijinga, issue ni misingi ya uanzishwaji na sio wingi)
      2. MoU iliingiwa na serikali kwa kuwa Wakristo walidhaniwa kuwa wengi (Mawazo ya kipuuzi kabisa, MoU haihusiani na wingi wa watu. Hata Aga Khan Foundation peke yake inaweza kuingia MoU ikiwa itaridhia uendeshwaji wa hospitali zake uwe chini ya serikali kama zilivyo designated hospitals)

      Kwa mawazo mafupi mafupi kama haya, mchango wa wengi wenu unakosekana sanasana mnakuwa mizigo. Hivi kwa nini hamjiulizi wenzenu waliosoma kwa nini hawaungi mkono mnapoanzisha mambo ya kipuuzi kama haya ya kususia Sensa? Makamu wa Rais na wake zake wa4 hana akili, akili anazo imamu wa msikiti wako ambaye ameishia darasa la 4?! Au Mwinyi na Kikwete sio waislamu, waislamu ni Ponda na imamu wako?

    4. #122
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,597
      Rep Power : 799
      Likes Received
      213
      Likes Given
      0

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By sweke34
      Ambayo muislam anaitumia kwenye shughuli za afya/elimu ya juu na shughuli nyingine za jamii bila kubaguliwa...aibu kubwa
      Huduma ambazo Muislamu amezichangia kupitia kodi yake?
      Haya tupeni basi nasisi Waislamu hayo mamilioni (MOU) miaka kwa miaka ili tufungue Shule na Mahospitali kwa ajili ya kuwahudumia wote bila ya kuwabagua!

    5. #123
      Las Mas Bobos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 537
      Likes Received
      302
      Likes Given
      84

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Sideeq
      Kwenye ajira na elimu ambapo Waislamu wanadai kubaguliwa pia hawataki kujua aidha Muislamu huyu ni msafi au si msafi!......una jina la Kiislamu basi inatosha kubaguliwa!
      Kubaguliwaje, manake mnaongea kimtaani mtaani tu. Angalia kwenye tume ya ajira wangapi mnaomba kazi. Hata sehemu mnazoshabikia kuwepo sio kazi oriented lkn mnataka mtu awafuate misikitini kuwaambia mtaje majina yenu awaandikie barua za kuwaombea kazi kwa kuwa nyinyi ni waislamu

      Uduni wa maisha ya mtu huanzia kwenye ubongo wake. Unashinda ukisoma magazet ya udaku, unategemea ajira zinatangazwa mule?

    6. #124
      Abdulhalim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th July 2007
      Location : Taipei 101
      Posts : 15,740
      Rep Power : 3770
      Likes Received
      1201
      Likes Given
      559

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Sideeq
      Kwenye ajira na elimu ambapo Waislamu wanadai kubaguliwa pia hawataki kujua aidha Muislamu huyu ni msafi au si msafi!......una jina la Kiislamu basi inatosha kubaguliwa!
      Jina la kisilamu linafananaje? au unamaanisha jinal la kiarabu?
      Moola's the motive

    7. #125
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1255
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Sideeq
      Huduma ambazo Muislamu amezichangia kupitia kodi yake?
      Haya tupeni basi nasisi Waislamu hayo mamilioni (MOU) miaka kwa miaka ili tufungue Shule na Mahospitali kwa ajili ya kuwahudumia wote bila ya kuwabagua!
      Jana nimeona ITV mama mmoja wa kiislam(na hijab yake) yupo kwenye kitanda cha wagonjwa baada ya kufanyiwa matibabu ya macho. Mradi huo upo nyakato/mwanza unaendeshwa na KKKT na wana mpango wa kuanza mradi kama huo Bagamoyo. Mtafute huyu mama aliyerekebishwa macho yake anaweza kukupa jibu zuri kuhusu kodi.
      Swali dogo...kama mnashindwa hata kujihesabu wenyewe ,haya mambo makubwa kweli mtayaweza?

    8. Miaka 50

    9. #126
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1176
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default

      Quote By Sideeq
      Lilikuwa jibu la swali ambalo ni mpya ya mwaka!
      JumaKidogo
      tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu Waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya Waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika.
      Sideeq
      Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
      Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
      - Atleast hao Ma-sheikh watakuwa wanalipwa kwa kazi walioifanya na muda wao waliopoteza kuliko Wakatoliki ambao wamejikalia tu na kupewa pesa ya bure na Serikali kupitia MOU, pesa ambayo inakusanywa katika kodi inayolipwa na Muislamu pia! aibu!
      Mkuu, ni aibu kufanya jambo linalohusu dini, kwa maslahi ya dini, halafu kutegemea posho kutoka serikalini. Hivi nchi hii ina misikiti mingapi? Badala ya kuanzisha migogoro ya kugombea sadaka kwa nini sadaka hiyo isifanye mambo mengine ya msingi kwa waislamu? Kama tatizo ni kodi zetu tunazotoa kumezwa na MOU. Ni afadhali basi tugome kulipa hiyo kodi kama inawezekana.

    10. #127
      Edoedward1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Posts : 314
      Rep Power : 419
      Likes Received
      54
      Likes Given
      142

      Default

      Quote By Mtanzania makini
      Ni kweli kabisa physics, nimesoma hoja za wachangiaji wote naona wote wanaopinga hili jambo kama vile kuna maslahi flani wanayatetea. Vinginevyo sioni ugumu wa suala hili hata kidogo, na kwa ujumla hoja zao hazina uzito wala mantiki. Nitazieleza hoja chache tu kama ifuatavyo:

      1. Waislamu watafute idadi yao wenyewe: hoja hapa si kwamba waislamu wanataka idadi yao, bali wanataka idadi rasmi ya watanzania kwa dini zao. Wakijihesabu wao bado haitasaidia kujua makundi ya dini nyingine officially. Wengine wanadai kuwa dini si waislamu na wakristo tu kuna dini za asili na wapagani, tuambieni wapagani ni wangapi? dini asilia ni wangapi? Na hii ni takwimu ya kawaida tu kwa nchi na nchi nyingi duniani zina data hizi na zinapatikana kwenye sensa zao. (angalia country profiles za nchi katika websites za cia, undp, worldbank, n.k.). Hoja ni kuwa kipengele cha dini kikiwekwa itakuwa ndiyo official data ya Tanzania as of 2012. Sioni tatizo na nadhani wanaopinga na kujiona eti wamekwenda shule dunia itawacheka kwa kupinga jambo la kawaida mno.

      1. Waislamu wakijua wako wangapi so what? Kwani wamarekani, waingereza, wajerumani, wa Indonesia n.k. tunajua idadi ya dini zao mbali mbali so what? kusema hivyo si maanishi kwamba haina maana ina maana na partly maana hiyo ndiyo inayowafanya wanaopinga waendelee kupinga. Maana yake ni kubwa mno baadhi yake ni kutuwezesha kufanya country and regional comparisons of religious groups na preveiling social relations which affect their lives and the way they relate with others. Mf. unasema Northern Ireland majority ni Catholics, while England majority ni Anglican. Vile vile unasema nchi yenye waislamu wengi duniani ni Indonesia n.k. Kwa nchi takwimu za dini zina maana sana hata kwa serikali kwa mfan; katika mipango miji ni serikali inayotayarisha maeneo ya matumizi mbali mbali kama makazi, biashara, taasisi, viwanda, na maeneo ya ibada (misikiti, makanisa). Maeneo ya ibada hutengwa kwa kuangalia idadi ya waumini wa dini husika. Usipojua idadi yao unaweza ukaweka eneo kubwa na kuyanyima matumizi mengine yanayohitaji ardhi zaidi, au ukaweka eneo dogo ambalo halitoshelezi mahitaji ya waumini na hivyo kuleta msongamno ambao baadae huleta mizozo isiyokuwa ya lazima.

      3. Wakatoliki wanajua idadi yao: Kwani wakristu wote ni wakatoliki? mbona hamjasema Anglican, Lutheran, SDA, Assemblies of God nao wanajua idadi yao. Na hata hao wakatoliki mbona sijaona hata mmoja wenu amesema precisely wako milioni ngapi Tanzania, huko ndo kujua idadi yao. Na zaidi ya hayo wasio na dini nao wanaipataje idadi yao maana wao hawana kanisa la kuwafanya wahesabiane kwa matumizi yao ya kidini.

      4. Serikali kuwafanyia waislamu sensa: Kilichopo ni kwamba serikali inataka kufanya sensa ambao ni utaratibu wa kawaida wa nchi kujua idadi ya watu wake kila baada ya miaka kumi. Wanachoomba waislamu ni kuingizwa kipengele cha kujua dini ya mtu katika sensa ambayo inataka kufanyika. Jambo hili haliongezi wala kupunguza gharama ya serikali kufanya sensa. Ingekuwa serikali imekwisha fanya sensa, halafu waislamu wanaomba ifanyike tena hapo kidogo ungeweza kusema wanataka kufanyiwa, lakini si hivyo.

      5. Waislamu kutokusoma: Sioni mantiki ya kuingiza suala la kusoma katika hoja hii. Nadhani inataka kutumika kama kisingizio kukwepa au kupindisha hoja ya msingi. Siku zijazo nitaanzisha thread tujadili mnaposema waislamu hawakusoma maana yake hasa ni ipi, na hivi kweli sentesi hiyo ina nguvu leo kama ilivyokuwa mwaka 1961?

      6. Totofautishe usomi na kufundishwa: Kuna tofauti kati ya msomi (intellectual) na aliyefundishwa (trainee/trained person). Trained person hufanya na kuamua mambo kwa kufuata vile alivyo fundishwa, wakati intellectual hufanya na kuamua mambo kwa kufuata real and genuine facts hata kama zitapingana na dini, kabila, kundi, mkoa au kanda anayotoka, n.k. Nikitazama michango katika hoja hii naona wachangiaji wengi wanafanana zaidi na trained person kuliko intelectuals, ingawa wanawalaumu waislamu kuwa hawakusoma. Nadhani kusoma kwenye manufaa ni kuwa intellectuals na sio trainees.

      Mtanzania Makini
      binafsi sipingi umakini wako ila maswali mengi unayouliza nathan hukutegemea kujibiwa hapa labda uende kwnye ofis ya kadinali pengo na Malasusa

    11. #128
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,597
      Rep Power : 799
      Likes Received
      213
      Likes Given
      0

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By sweke34
      Jana nimeona ITV mama mmoja wa kiislam(na hijab yake) yupo kwenye kitanda cha wagonjwa baada ya kufanyiwa matibabu ya macho. Mradi huo upo nyakato/mwanza unaendeshwa na KKKT na wana mpango wa kuanza mradi kama huo Bagamoyo. Mtafute huyu mama aliyerekebishwa macho yake anaweza kukupa jibu zuri kuhusu kodi.
      Jaribio dhaifu hili! juzijuzi kulikuwa na taasisi ya Kiislamu iliyokuwa ikiwapa matibabu ya macho bure hata Wakristo kule Moshi na walikuwa na mpango wa kupanua huduma hizo Arusha!
      Watafute Wakristo waliopewa huduma za macho bure na taasisi ya Kiislamu ambayo haipewi hata senti moja kutoka katika hela zenu za kodi, wanaweza kukupa jibu zuri!
      Mmezoea kula mali za watu kwa batili nyinyi!

    12. #129
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Sisi wengine tunasubiri kwa hamu serikali ibadili msimamo na kutimiza matakwa ya Waislamu ili na sisi Wasukuma tulete madai yetu rasmi kuwa hatutashiriki sensa mpaka kipengele cha ukabila kiingizwe kwenye dodoso.

      Lengo ni kujua jee Wasukuma tuko wangapi?. Jee wangapi wako Kanda ya Ziwa na wangapi wamesambaa maeneo mengine ili sisi wa maeneo mengine tuanzishe diasphora yetu kuwasaidia wenzetu!.

      Hakuna ubishi kuwa kabila la Wasukuma ndilo kabila lenye idadi kubwa ya watu hivyo tukishaijua idadi yetu kamili tutafanya comparison na eneo tunalo miliki ili kupima kama ni halali jinsi tulivyo wengi kukalia eneo dogo la Kanda ya Ziwa huku wafugaji wetu wakitanga tanga na mifugo yao kutwa kucha wakifukuzwa kama kule Ihefu na juzi juzi Kisarawe?.

      Tukijua idadi tutahakikisha tunapatiwa coresponding land kutokana na idadi vinginevyo tutateka maeneo yote tupu yanayotuzunguka na kuyataifisha kama walivyofanya wana wa Israel kule Mashariki ya Kati.

      Eneo la Usukumani ndiko kwenye migodi ya madini ya dhahabu na almasi, tukishajua Idadi ya Wasukuma tunapiga jumla ya pato la madini na kuoanisha na asilimia inayowafaidia wenye madini halisi ili kuandaa sheria mpya ya mrahaba wa kubaki Usukumani ni asilimia 20% ya gross asiyetaka na aache na kufungasha tutawekeza wenyewe kwa kuuza ngombe na kusomesha vijana wetu Ulaya waje na mitaji tuchimbe wenyewe, tuuze wenyewe na kujifaidia wenyewe!.

      Tukisha jua idadi tunaangalia jee ni Wasukuma % ngapi kwenye kila sekta mfano kama itakutukana Wasukuma ni 30% ya Watanzania then lazima tuwe na 30% proportions kwenye kila mahali kuanzia Uwaziri, bungeni, BOT, TRA, Majeshini etc etc hadi vyuo vikuu haiwezekani vikabila vidogo vidogo vikajazana sehemu nono za nchi hii huku kabila kubwa wakitangatanga kutafuta malisho ya ng'ombe wao tena fisi wakitengewa maeneo ya malisho (hifadhi) Ili wazungu waje wawatazame wao wapate pesa huku ng'ombe wetu wakikosa maeneo ya malisho!.

      Tukisha jua idadi yetu, tutaitumia idadi hiyo kama fimbo ya kushinikiza kutendewa haki ikiwemo sisi ndio determinant nani anakuwa rais wa nchi hii!. Tutajiorganize kuhakikisha tunaleta mabadiliko ya kweli, haiwezekani katika miaka 50 ya uhuru wetu tumekuwa tukipelekwa pelekwa tuu na kunyamaza sasa tufike mahali tuseme basi!, na ikibidi tujitangazie uhuru wa maeneo yetu kama Biafra kwa sababu tuna kila kitu!, ika tutakuwa sehemu ya Tanganyika chini ya federation!.

      Ndugu zetu Waislamu simameni imara kudai haki zenu!. Kumbe nyinyi ndio mko wengi zaidi ya asilimia 50%!, ulipaswa kupata nafasi za asilimia 50 kwenye kila kitu hadi teuzi mbalimbali!, lakini nyinyi mmekuwa mkipatiwa asilimia mia 10% na hizo haki zenu 40% zimekuwa zikishikwa na dini nyingine!, msikubali kabisa simameni kidete hata ikibidi kutangaza jihad tangazeni!.

      Na serikali ikiwakatalia kata kata, kutekeleza madai yenu, nawashauri dawa sio kususia hiyo sense bali kuwaonyesha serikali uwezo wenu kwa kuisomea Albadir hiyo sensa isifanyike kabisa!.

      I'm not jocking!.

      Pasco.
      Las Mas Bobos likes this.

    13. #130
      Edoedward1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2012
      Posts : 314
      Rep Power : 419
      Likes Received
      54
      Likes Given
      142

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Mim huwa nashindwa kuelewa ni kweli hawa viongozi wetu waislam huwa wanashindwa logic ndogo tu kwamb kwanin in 1960's waislam walikuwa about 70% ya watanzania lakini leo hii tupo 35%,ki0ngoz wangu mmoja akah0ji eti waislam walienda wapi? Ikiwa hatujawah kuwa na vita ya ndan?..Lol
      Akashindwa kutambua ukweli kwamba wenzetu wakristo huwa wanafanya jitihada za maksudi katika mikutano yao ya kiroho,makanisani na hata one to one c0nversati0n kuwabadili/kuwa0koa wana wapotev kila uchao ILA sisi waislam mikutano yetu ni kupiga kelele zisizokuwa na malengo

    14. #131
      Las Mas Bobos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 537
      Likes Received
      302
      Likes Given
      84

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Sideeq
      Huduma ambazo Muislamu amezichangia kupitia kodi yake?
      Haya tupeni basi nasisi Waislamu hayo mamilioni (MOU) miaka kwa miaka ili tufungue Shule na Mahospitali kwa ajili ya kuwahudumia wote bila ya kuwabagua!
      MoU haikutolewa kujengea Hospitali. Hizi Hospitali kama ukitumia akili yako vizuri (kama unayo) utagundua nyingi zilianza wakati au mara baada ya ukoloni. Hizi fedha ni za matumizi ya uendeshaji na usimamizi ambao unasimamiwa na serikali. Haya maisha yenu ya kuzaliwa Buguruni, kukulia Buguruni na kuzikwa Mburahati yanawafanya mdumae kifikra. Itembee Tanzania ndio utajua kuwa kuna maeneo hayana Zahanati zaidi ya ile iliyojengwa na mkoloni mwaka 1897.

      Muheza (Teule) Designated Hospital ipo Tanga ambapo kama una akili angalau kidogo utakubaliana na mimi Waislamu si wachache. Ukienda pale na mimba yako ya 8 (kama ilivyo kwa watu wanaopenda kuzaa bila kuajli uwezo wa kutunza familia) unalipia KADI kwa gharama sawa na ambavyo ungelipa AMANA, UTAMUONA DAKTARI kwa gharama sawa na MWANANYAMALA na utapata dawa kwa gharama sawa na TEMEKE.

      Stakabadhi zinazotolewa pale ni za serikali na haya maneno yenu mnayoongelea TANDALE wenzenu wa kule Muheza hawatawaelewa kwani hawajawahi kubaguliwa. Tatizo la uvivu wa kufikiri linawafanya mtumike kushinikiza ujinga wa watu wengine kwa manufaa yao.

      Tembea, acha kumsikiliza mtu ambaye hajasoma na wala hajaenda huko kufanya utafiti.

      ANGALIZO: Upo uwezekano mama mmoja na mimba yake ya 13 alienda kwenye Zahanati ya Kanisa iliyopo huku mjini na mia 5 yake akidhani na pale huduma ni ya serikali. Ndugu zetu msiopenda kuelewa, RUZUKU ya serikali inatolewa kwa hospitali kadhaa zilizoteuliwa na kuidhinishwa na serikali yenyewe. Zinaendeshwa pia kwa usimamizi wa serikali na ndio maana utaona hata mishahara inalipwa na serikali na mtumishi anaweza kufukuzwa kazi na serikali kwa kuwa ndie muajiri. Hizi mnazoziona zina viyoyozi ni michango yetu na zinaendeshwa na Parokia au Jimbo husika. Sasa asitoke mtu mapuvu kuwa kauziwa dawa 2000 badala ya 700 mkadhani kila cha Kanisa ni cha serikali. Kama unayo fedha ya matibabu nenda, lkn kama una mia 3 yako nenda kwenye zile zinazosimamiwa na serikali, huko ndio kuna MoU. Pale Kibangu Parish Hospital huduma ni private si sawa na KCMC, hakuna MoU pale. Manake kuna msikiti jirani pale unaongoza kwa kucritisize kila kinachofanywa na kanisa wakati wao hata choo chao ni cha makuti sababu ya akili za namna hii
      Talklicious likes this.

    15. #132
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,597
      Rep Power : 799
      Likes Received
      213
      Likes Given
      0

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Jumakidogo
      Mkuu, ni aibu kufanya jambo linalohusu dini, kwa maslahi ya dini, halafu kutegemea posho kutoka serikalini.
      Waislamu hawajataka kufanyika sensa kwa ajili ya dini ili wapate posho!.....umeitoa wapi hii?
      Aibu ni pale Wakatoliki wanapochota mabilioni ya walipa kodi kwa maslahi yao binafsi!

    16. #133
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1176
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default

      Quote By Sideeq
      Huduma ambazo Muislamu amezichangia kupitia kodi yake?
      Haya tupeni basi nasisi Waislamu hayo mamilioni (MOU) miaka kwa miaka ili tufungue Shule na Mahospitali kwa ajili ya kuwahudumia wote bila ya kuwabagua!
      Mimi ni mwislamu, japo sijasoma madrasa lakini nataka mwislamu ajikomboe kutokana na hali halisi ya mazingira tulipo. Maisha ya sasa siyo ya kutafuta ukombozi kwa kufuata hadithi zilizoandikwa na manabii wa kale.

      Wala ukombozi wa kweli wa waislamu hauwezi kuja kwa kudai kila kitu tufanyiwe na serikali. Kama wenzetu walitengeneza MOU. Tuwaache na MOU yao, tutafute mbinu nyingine ya kujikomboa. Kwanza tutengeneze mtandao wa fedha wa waislamu kwa njia ya kuchangishana wenyewe kwa wenyewe. Tatizo letu ni ubinafsi, kuna waislamu wangapi wenye uwezo wa kuchangia ili kutunisha mfuko? Tuwe na mtandao wa fedha ambao utatuwezesha kujenga mashule na mambo mengine.

      Hakuna serikali katika nchi kama hiyo itakayofanya kazi kwa niaba ama amri ama matakwa ya dini fulani. Tuamke, tupambane kwa mbinu mpya ili kufikia malengo.
      introvert likes this.

    17. #134
      ntamaholo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2011
      Location : Mwilavya
      Posts : 4,116
      Rep Power : 1387
      Likes Received
      918
      Likes Given
      412

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By eltontz
      Itakubalika kwa sababu haina matumizi yoyote kwa serikali zaidi ya umo makanisani na misikitini mwenu.
      matokeo ya sensa hayatakubalika, hayatakubalika kwa kuwa waislamu hawatamaliza kulalamika. utasikia wanasema wengi walikuwa na madodoso ni wakristo na mkurugenzi ni mkristo
      UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

    18. #135
      Talklicious's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 50
      Rep Power : 370
      Likes Received
      6
      Likes Given
      12

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Sideeq
      Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
      Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
      Sioni point/sababu ya serikali kugharamia kwa vyovyote vile hiyo sensa kwa sababu ni kwa manufaa ya dini yenyewe. Tusitake kuingiza serikali kwenye gharama nyingi kwa maana kwa kufanya hivyo hata kikundi kingine cha dini kinaweza kikademand the same thing na hapo si budget itaishia kwenye kuhesabu idadi ya waumini wa dini fulani fulani.
      Fikiria waislam wapewe hela ya kufanya sensa halafu itokee wakristo nao wahitaji patatosha kweli, unajua kuna jumla ya dhehebu ngapi hapa Tz?!

    19. #136
      Las Mas Bobos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 537
      Likes Received
      302
      Likes Given
      84

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Pasco
      Sisi wengine tunasubiri kwa hamu serikali ibadili msimamo na kutimiza matakwa ya Waislamu ili na sisi Wasukuma tulete madai yetu rasmi kuwa hatutashiriki sensa mpaka kipengele cha ukabila kiingizwe kwenye dodoso.

      Lengo ni kujua jee Wasukuma tuko wangapi?. Jee wangapi wako Kanda ya Ziwa na wangapi wamesambaa maeneo mengine ili sisi wa maeneo mengine tuanzishe diasphora yetu kuwasaidia wenzetu!.

      Na serikali ikiwakatalia kata kata, kutekeleza madai yenu, nawashauri dawa sio kususia hiyo sense bali kuwaonyesha serikali uwezo wenu kwa kuisomea Albadir hiyo sensa isifanyike kabisa!.

      I'm not jocking!.

      Pasco.
      Well said mkuu, kadude kangu ka kugongea like kamefichika wallah ilikuwa halali yako. Hivi kuna nini?

      Watu wanapigania maendeleo hawa wengine wetu wanapigania mambo ambayo sijui ni kwa faida ya nani. Vipaumbele vyao kwenye katiba mpya ni kuruhusiwa kufuga madevu jeshini, polisi kuvaa hijab na mambo kama hayo, ina maana kuhusu uchumi, uhamiaji, biashara, madini n.k wao hawana michango? Au hayo mengine wajibu kina nani?

      This is very very tatizo and disapointingi

    20. #137
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,597
      Rep Power : 799
      Likes Received
      213
      Likes Given
      0

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Jumakidogo
      Kama wenzetu walitengeneza MOU. Tuwaache na MOU yao, tutafute mbinu nyingine ya kujikomboa.
      Kwa hiyo sisi tulipie kodi ili wapewe wao wazidi kutubamiza, halafu turidhike nalo hilo!
      The dayz of Slavery has gone dude!
      Mtanzania makini likes this.

    21. #138
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,597
      Rep Power : 799
      Likes Received
      213
      Likes Given
      0

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Quote By Talklicious
      Sioni point/sababu ya serikali kugharamia kwa vyovyote vile hiyo sensa kwa sababu ni kwa manufaa ya dini yenyewe. Tusitake kuingiza serikali kwenye gharama nyingi kwa maana kwa kufanya hivyo hata kikundi kingine cha dini kinaweza kikademand the same thing na hapo si budget itaishia kwenye kuhesabu idadi ya waumini wa dini fulani fulani.
      Fikiria waislam wapewe hela ya kufanya sensa halafu itokee wakristo nao wahitaji patatosha kweli, unajua kuna jumla ya dhehebu ngapi hapa Tz?!
      JumaKidogo
      tuiache sensa ya serikali ifanye kazi yake, tukubali kuhesabiwa. Baada ya hapo tufanye sensa yetu Waislamu tu. Nina hakika kila mtaa haukosi kuwa na shekhe ambaye anaweza kupita na kujua idadi ya Waislamu walio katika mtaa wake, ndani ya kipindi kifupi tunaweza kupata majibu kwa kupitia sensa yetu ya uhakika.
      Sideeq
      Sawa! lakini itambulike officially na Serikali.
      Na kama serikali inaweza kugharimia ufanyaji wa sensa , vilevile hawa Masheikh watakaofanya hii kazi wagharimiwe na Serikali.
      - Atleast hao Ma-sheikh watakuwa wanalipwa kwa kazi walioifanya na muda wao waliopoteza kuliko Wakatoliki ambao wamejikalia tu na kupewa pesa ya bure na Serikali kupitia MOU, pesa ambayo inakusanywa katika kodi inayolipwa na Muislamu pia! aibu!

    22. #139
      Las Mas Bobos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 537
      Likes Received
      302
      Likes Given
      84

      Default Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

      Jumakidogo

      Mkuu kuchanga ni spirit. Msikiti wa Ubungo darajani kwa miaka na miaka umekuwa kama mahame, kama kibanda tu cha biashara fulani kama soko ulhali nje pale siku ya Ijumaa utaona magari mawili matatu yakipaki na watu wenye kanzu zenye vidani na kani wakitoka na kuingia, lkn hamna aliyewahi kuona ule msikiti ni mchafu na umepitwa na wakati.

      Kwa hivi tunavyoonge, umevunjwa na unajengwa upya. Sasa hapo kama si mwarabu mmoja kajitolea basi usingejengwa kwani kuchanga ni mwiko kwenu. Labda kuchangia maulid. Nyinyi wenye upeo na uelewa wa maisha ya karne ya leo, msikae kimya, tumikeni kama chachu kwa jamii zenu. Mikutano ya kujadili jinsi wakristo wasivyotahiriwa ife badala yake iamke mihadhara ya kuhubiri maendeleo.

      Kuna msikiti kule kibangu unasifika kwa mihadhara ya kashfa lkn una choo kama kibanda cha kuku na wenyewe hauna hata sakafu, pembeni yake ni kanisa lenye shule ya chekechea na hospitali kubwa ya ghorofa. Wakati wa harambee za kuchangisha fedha za ujenzi wa hospitali ilikuwa kawaida kusikia spika za msikiti zikitangaza kejeli kuwa 'Vatican imegoma kutoa hela sasa wanachanga wenyewe', hicho ndio pekee wanachoweza kufanya (umbea na kejeli).

      Wote tunafahamu mwarabu aliyeleta dini hakuwa na kitu kichwani, lkn sisi wenyewe si tunaakili, basi ni wajibu wetu kufanya yaliyo ya manufaa na kusonga mbele.

    23. #140
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1176
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default

      Quote By Sideeq
      Waislamu hawajataka kufanyika sensa kwa ajili ya dini ili wapate posho!.....umeitoa wapi hii?
      Aibu ni pale Wakatoliki wanapochota mabilioni ya walipa kodi kwa maslahi yao binafsi!
      Shekhe! Wewe ndiye uliisema hiyo. Mi nimeitoa kwenye post yako ya kuwa, waislamu wakianzisha sensa yao basi serikali iingie gharama kwa kuwalipa posho mashekhe, hiyo ni yako kaka. Umeanza kuikataa!

    Page 7 of 11 FirstFirst ... 56789 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...