Re: Ushauri wa bure kwa BAKWATA na waislamu wenzangu wote kuhusu kususia SENSA

By
Free World
Juma Salaam,
Kwanza sina shaka juu ya uislamun wako kama wengine humu JF, wanaojifanya waislamu kumbe ni makafiri wazuri.
Kimsingi hata mimi binafsi siathiriki na sensa na matokeo yake.
lakini unapaswa kuangalia mbali zaidi ya hoja zako hapo juu. Wakristo wanataka Waislamu wafikiri kama wewe ulivyofanya, kwa hiyo itawahakikishia
dhulma bila bughdha
- Madai ya msingi ya Waislamu ni kuwa Wakristo kwa kuwa ndio wengi serikalini na kwenye ufanyaji maamuzi wanatumia mwanya wa kutokuwa na takwimu sahihi kuhalalisha wao kuwa wengi kila mahali.
- kama idadi ya watu wa dini fulani sio issue, kwa nini izungumzwe ile ya makadirio?
- Kama kuna haja ya kuwa na makadirio (estimates) kwanini kusiwe na real data?
- Pia kuna confusion inayotokana na records za nyuma, mwanzo waislamu walikuwa majority TZ, leo kwa nini wawe 35%?
Mwisho KWA NINI TUNAOGOPA KUPIMWA? wakati tunasisitiza watu wakapimwe ukimwi! Hapa tunaogopa ukweli?
Ndugu yangu, sensa, wala idadi ya watu si suluhu ya matatizo ya waislamu. Wala sensa si mkombozi wa waislamu. Hata kama tungekuwa wengi ambao tunawazidi wakristo mara sita au kumi. Kama hatuna elimu na wasomi wa kutosha katika dini yetu bado tutalalamika.
Cha msingi ni kuamka sasa na kuanza kutafuta tatizo lilianzia wapi, chanzo kilikuwa nini mpaka tumeathirika kwa kiasi kikubwa na kutokuwa na elimu dunia.
Nadhani historia iko wazi tangu zamani watoto wa kislamu hawakushiriki kwa karibu sana elimu dunia. Yatupasa tubadilike sasa, elimu ya ahera kwa dunia ya sasa haimsaidii sana mtu. Tuangalie namna ya kubadili mfumo wa elimu yetu waislamu. Hiyo itatusaidia kwenda sambamba na dunia ya sasa bila kulalamika,
NI FAHARI KUMFUKUZA SIMBA AKAKIMBIA, LAKINI NI HATARI KUFUATA NYAYO ZAKE
Follow Us Here