Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

    Report Post
    Page 5 of 9 FirstFirst ... 34567 ... LastLast
    Results 81 to 100 of 170
    1. #1
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akionyesha begi lililobeba hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013, wakati akielekea kuingia katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi

      Jana nilijaribu kumsikiliza waziri wa fedha Dr. Mgimwa na swali lililokuwa likijirudia mara kwa mara kichwani mwangu ni hivi huyu Mheshimiwa ni mradi wa nani?

      Baada ya JK kudhalilishwa na mawaziri wake wawili wa fedha kwa maana ya utendaji duni wa Meghji na Mkullo ni dhahiri alitafuta ushauri wa nani anafaa kumsaidia kwenye wadhifa tajwa................ni nani ushauri wake JK aliuzingatia katika uteuzi tajwa?

      Wakati serikali ya JK ikikumbwa na kashfa ya CAG ya matumizi mabaya ya fedha ulikuwepo uvumi kuwa hata PM alikuwa anafikiria kujing'atua na kumwacha JK azame na merikebu yake ya TITANIC...................laki ni hakufanya hivyo ni kwa sababu zipi?

      Jingine ni kuwa wakati makabrasha ya wizara ya fedha ya bajeti yalipocheleweshwa alikuwa ni Pinda aliyemkingia kifua Dr. Mgimwa kuwa Dr. Mgimwa alikuwa na kibali cha Raisi ayapitie upya makadirio tajwa ili na yeye kwenye wadhifa wake mpya aweze kuweka michango yake.................baada ya kupitia bajeti husika sioni kama kuna jipya ukiondoa misamaha ya kodi kwa walalahoi wanaopata chini ya milioni tatu na hata hapo naona bado kuna uonevu umefanyika na nitafafanua baadaye..........

      Jingine, jipya ni kuamsha ari za usajili magari kwa majina binafsi na kuyalipia milioni 5 kila baada ya miaka 3...............hili ni kuiga marekani ambako utaratibu huu umeshamiri.................

      Mengineyo yote yaliyomo kwenye bajeti, hata Mkullo au Meghji wangelisoma hayohayo kwa hiyo sioni khoja ya Pinda ya ucheleweshwaji wa bajeti kama ina mashiko.......................

      Kwa hiyo, kama Pinda alilidanganya Bunge kwa minajili ya kumlinda Dr. Mgimwa alifanya hivyo kwa masilahi ya nani? Kwa maoni yangu binafsi, Pinda na wala siyo JK ndiye mhimili na mfadhili wa huyu waziri mpya wa fedha na Pinda anaona kavuna dume kwa sababu amekuwa akitafuta mianya ya hazina kusukuma kwa kasi maendeleo ya mkoa wa Rukwa hususani jimbo lake la uchaguzi........na Mkullo hakuwa akimsikiliza sana kwa sababu ana uhusiano wa moja kwa moja na JK uhusiano wa miaka mingi tangia akiwa NPF na JK akiwa kwenye baraza la Mwinyi........

      Bajeti hii ina sifa za kulinda masilahi ya viongozi na wala siyo ya walalahoi na maeneo haya ndiyo maangalizo 10 ambayo yananifanya nije na misimamo tajwa:-

      1) Viongozi wote serikalini wanakiri kuwa makali ya maisha yameongezeka lakini ufumbuzi wao ni kulinda walichonacho au hata kujiongezea bila ya kujua kwa kufanya hivyo walikuwa wanapunguza huduma za kijamii na hivyo kumwongezea makali mlalahoi. Mishahara ya viongozi na sheria ya pensheni ya viongozi vilitakiwa vifanyiwe marekebisho makubwa ili kuondoa ubaguzi ambao unafanywa na viongozi kwenye nyanja hiyo kinyume na sheria..................haya hayakufanyika na kamwe hayatafanyika katika kipindi cha JK akiwa madarakani kwa sababu yeye mwenyewe ni matunda ya mfumo mbovu wa upatikanaji wa viongozi kwa hiyo hawezi kuwa na hisia kali ya kurekebisha mapungufu yaliyopo na hata hisia tajwa angelikuwa nazo bado hana ujuzi wa kufanya hivyo....................kwa lugha nyingine JK ni matunda ya kunukuu staili ya utendaji mbovu ya wale aliyewarithi.

      2) Kumpunguzia makali mlipa kodi mwenye kipato cha chini ya milioni 3 ni unafiki wa kupindukia. Mtumishi wa serikalini mwenye kipato kama hicho hana
      capital costs kwenye mapato yake jambo ambalo anayejiajiri anazo. Tumchukulie mama ntilie mwenye kipato cha milioni 3 kwa mwaka utakuta gharama zake za kuendesha mradi ni asilimia 70 hadi 90 ya mapato tajwa sasa ukimtoza kodi katika kiwango hicho cha chini ni dhahiri unatoza mtaji na hivyo kumwongezea adha za kufukarika. Serikali iliyo makini ingeweka wazi apataye mapato chini ya Tshs 20 millioni kwa mwaka hapaswi kulipa kodi kwa sababu hicho kiwango ni cha kumwezesha kujiajiri na kumudu gharama za maisha...............hivyo pamoja na porojo za Dr. Mgimwa bado hana hisia kali za adha ya umasikini na vyanzo vyake hapa nchini..

      3) Kodi za magari chakavu kupandishiwa umri kutoka miaka 10 hadi zaidi ya miaka 8 ni panga linalokata pande mbili: sababu za kulinda mazingira ni lazima zilinganishwe na sababu za kukuza uchumi. Dr. Mgimwa alipaswa atofautishe aina ya vyombo husika.... magari ya anasa na vifaa vyovyote vile vya anasa ni sahihi kuvitoza kodi tajwa lakini vyombo vya uzalishaji kama vya barabara, ujenzi na viwandani vilipaswa kubaki umri uleule wa miaka 10 kutokana na mchango wake katika kuinua kipato cha nchi na kuwapatia ajira raia wake. Utashangaa kufahamu zaidi ya asilimia 90 ya mitambo ya barabara inayojenga barabara zetu in umri wa zaidi ya miaka 10. Sasa ukianza kutoza kodi ya asilimia 20 kwa yule anayeagiza mitambo hiyo ambayo bado kabisa ina khali nzuri sana huo ufukara unamletea nani kama siyo mlalahoi anayetegemea kujipatia kipato kutokana na vyanzo hivyo vya uzalishaji.

      4) Bajeti kama zile zilizoitangulia bajeti hii, imeshindwa kuainisha kwa kushirikiana na CAG mianya ya kuporomoka uwajibikaji katika matumizi ya serikali. Haitoshi kwa Dr. Mgimwa kudai usimamizi wa bajeti hii utakuwa tofauti na zile zilizotanguliwa bila ya kuonyesha kwa namna zipi. mfano serikali za mitaa inabidi zimilikishwe halmashauri kwa madiwani wawe na mamlaka ya kuajiri watumishi wa ngazi zote badala ya kutegemea serikali kuu kupandikiza mamluki wao ambao ni viwavi jeshi na madiwani kubakia ni wapiga tarumbeta za hamelini. Kwenye mashirika ya umma kuna uhaja wa kubadilisha mfumo mzima wa uteuzi wa bodi na bodi kuwa na mamlaka ya mwisho ya uteuzi wa watendaji wote wakiwemo CEOs kwenye taasisi zao badala ya Ikulu kuona ni kivuno cha kupanga safu za viwavi jeshi. Bodi za wakurugenzi zinapaswa zitokane na wadau wa sekta husika ambao watapatikana kwa kupigiwa kura na washiriki wa nyanja husika hivyo kuondoa mmomonyoko wa uwajibikaji. Wenyeviti wa Bodi kuchaguliwa moja kwa moja na wajumbe wa bodi badala ya Ikulu kuwabandikia mtu ambaye hushukuriwa kwa sababu za kumlinda kisiasa bila ya kujali kama ana mchango wowote wa taasisi ambayo amekabidhiwa kuisimamia....

      5) Kusahau nafasi ya michezo katika kuleta ajira na kukuza uchumi. Timu zote za daraja la juu (Premier league) la mpira wa miguu zilitakiwa zitengewe fungu la kuanzisha timu za watoto ili kuibua vipaji kama sehemu ya awali ya kuanzia. La ajabu viongozi wetu kila siku huimba soka huendelezwa na timu siyo timu ya taifa lakini ni wagumu kwenye mioyo yao kutoa fedha za shughuli hiyo nyeti katika kukuza vipaji vya michezo, kufufua uchumi na kuwapatia ajira vijana wetu. Kwa kuanzia kila timu iliyoko kwenye Premier league ingelitengewa shilingi milioni 200 kwa mwaka kwa kazi hiyo ya kukuza vipaji vya vijana na fedha hizo CAG lazima akague matumizi yake.
      Haya, huyu Dr. Mgimwa hawezi kuyafikiria kwa sababu ni kizazi kilichopitwa na wakati.

      6) (a) Upendeleo wa misamaha ya kodi zote kutofutwa kwa vigezo ambayo vinakinzana na katiba yetu ya kuondoa aina zote za ubaguzi. Katika hukumu ya KTM {Karibu Textiles Mills} mahakama zote za juu zilisema ni ukiukwaji wa katiba kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya makampuni tu tena yapo kwenye sekta moja khalafu wengine mkawabagua eti kwa sababu wana mikataba yao na wengineo hawana. Mbali ya ukweli kuwa ubaguzi tajwa unatibua nguvu ya soko lakini la kuzingatiwa ni kuwa katiba iko juu ya mikataba tajwa.
      Nilidhani kama Dr. Mgimwa is the real deal angeliifuta mikataba tajwa kwa kuongozwa na hukumu za KTM ya EAC na ya CAT (TZ COURT OF APPEAL) katika kutenda haki. Lakini kwa vile, Dr. Mgimwa hakuwekwa pale kwa dhamira safi ya kulisaidia taifa bali ni kujibu tu kiu ya aliyemweka ambaye ninaamini ni Peter Mizengo Pinda basi upeo wa kuyaona haya hana na hivyo hana sifa hata moja ya kuwa Waziri kwenye nyadhifa yoyote ile kwenye baraza la mawaziri achilia mbali Wizara ya fedha.

      b) Misamaha ya kodi kwenye mahoteli ya kitalii kanda ya kaskazini haijafutwa ambayo inaigharimu nchi zaidi ya dola 20-70 milioni kwa mwaka. Sasa Dr. Mgimwa alichelewesha bajeti hii kwa nini kama...........it is business as usual, na hata huyo Pinda aliyekuwa akimtetea hivi haoni hata haya?

      What a shame!

      7) Eneo ambalo humgusa mlalahoi moja kwa moja ni eneo la kodi. Kodi ya VAT ya asilimia 18 imesaidia sana katika kufifilisha soko la ajira. Hawa wakubwa wakisha kulamba hela yetu pale hazina hukimbilia kudai haya ni makusanyo ya serikali na kusahau hata siye ambao hatujaajiriwa serikalini nao ni sehemu hiyo hiyo ya serikali. Serikali yoyote ambayo haisikilizi kukua kwa gharama za maisha na uhaba wa vyanzo vya uzalishaji hiyo serikali siyo sikivu hata kama ikidai vinginevyo.

      a) Kwa kuanzia VAT ilipaswa kupunguzwa kutoka asilimia 18 hadi 15 ili kuhamasisha waajiri wakuze soko la ajira na kuongeza ushindani wa bidhaa zetu kwenye soko la dunia. Mapato ya serikali kuyaongeza siyo kuongeza viwango vya kodi tu bali kuwa na kiwango cha kodi ambacho kitahamasisha tija na uzalishaji. Hili tuendelee kulidai kwani ni haki yetu kukataa kuburutwa bila ya siye kutaka katika ufukara wa kujitakia.

      b) VAT ya EWURA na REA, kwenye umeme ni ya kuondoa tena kinatakiwa kiwe kitendo cha haraka sana. Hivi huo umeme wa vijijini hata ukipelekwa ni nani kule atakayeweza kuumudu gharama zake kama hata wakaazi wengi wa mijini naona wamerudishwa kwenye vibatali tu? Kiujumla wakaazi wa mijini wana uwezo wa kumudu gharama za maisha zaidi ya wale wa vijijini na kama mfupa umemshinda mzee fisi je nani atauweza?

      c) Kila Halmashauri ilipaswa kutengewa 7% ya VAT kwenda moja kwa moja kwenye shughuli zao badala ya kutegemea hisani ya serikali kuu au udanganyifu wa mfuko wa jimbo ambao nao ni kituko kwani siyo shirikishi hata chembe. Serikali kuu ingelibaki na 8% ya makusanyo ya VAT kwa minajili ya kusawazisha maeneo ambayo yana mapato madogo na hivyo kuleta maendeleo yenye uwiano mzuri. Mfumo wa mgawanyo uliopo unaipa serikali kuu hususani DSM upendeleo wa kila kitu na hivyo kuacha mikoa ya pembezoni kuwa nyuma sana kimaendeleo. Huu ndiyo mtazamo mpya wa kulikwamua taifa kutoka hapa lilipo hadi kwenda kwenye maendeleo kwa kila mtanzania..................... ...azma ambayo ianaelekea ni tamu wakati wa kuomba kura lakini ni chungu katika kuitekeleza..............

      Hivi huyu Dr. Mgimwa anaelewa nchi hii inatoka wapi, iko wapi na yaelekea wapi? Kama siyo mbabaishaji tu?

      8) Kukwepa kufuta road tolls za magari makubwa. Kila mahali alipokuwa akihalalisha kupanda kwa kodi, Dr. Mgimwa alikuwa anajificha kwenye kichaka cha EAC na sheria zake. Bajeti ya jana ya Kenya wamefuta vizuizi vyote vya barabarani vikiwemo vya tozo za magari makubwa, usafirishaji wa vyakula n.k .......................sasa hayo maigizo ya EAC mbona hayakufika kwenye kufuta road tolls ambazo zinatajirisha watu wachache badala ya kulitajirisha taifa?????????????..........Ku husu uzito wa magari ni udhibiti wa idadi ya matairi ya nyuma la gari au load axles unatosha kabisa kuhakikisha magari yetu hayazidi tani stahiki. Kenya wao lori lenye axles 3 tu ndizo zinaruhusiwa kwenye barabara zao. Sasa ukiisha kulisimamia hilo huu uchafu wa road tolls ambazo zinaongeza mrundikano wa bidhaa na kuchelewesha huduma kwa jamii huku zikimwongezea mlaji gharama zisizorejesheka ni wa nini kama siyo kulinda ajira na ufisadi wa watoto wa vigogo ambao ndiyo wamerundikwa kwenye vituo vya matozo tajwa?

      9) Ukuaji wa deni la taifa Dr. Mgimwa aliuchukulia kimzahamzaha tu na hakuna maelezo ya kutosha kuelezea ni kwa sababu zipi taifa limebebeshwa mzigo wa deni la trilioni 5 tu wakati Mkapa anamkabidhi Jk nchi na khalafu deni hilo lipande khadi trilioni 8 mwaka 2009 na leo lifikie trilioni 22 (Kwa fedha za kitanzania)? Tathmini ya nani alikopa na kwa idhini ya nani inabidi ijulikane sasa na hata CAG sijui yuko wapi kutathmini hilo na badala yake anatumia muda mwingi kuwabana halmashauri ambao mapato yao ni kiduchu. Dr. Mgimwa kama angelikuwa makini angelianzisha sheria ya kuhakikisha bunge ndilo lenye mamlaka ya kupitisha mikopo yote ya serikalini. Hatukumchagua Raisi aende Ikulu kufanya atakavyo bila ya kuwajibika kwa yeyote. Haya madeni yatalipwa na wajukuu zetu na vilembwekazi hata hatujui hizo fedha zilifanya nini na aliyekuwa aziidhinisha alifanya hivyo kwa mashinikizo ya akina nani...........

      10) BOT imekuwa haitazamwi juu ya vyanzo vyake vya mapato na matumizi na imekuwa kinara wa ufisadi ambao hata CAG huwa anaufumbia macho. Wakati umefika mapato na matumizi ya BOT yakawekwa wazi na ile sheria ya kulizuia bunge kudhibiti BOT ikafutwa na kurejesha BOT mikononi mwa udhibiti wa Bunge......................

      Kwa haraka haraka, Dr. Mgimwa ni bomu na tusitishike na kauli zake za kujiamini..mara nyingi matapeli ndivyo walivyo.............na nimpa D minus kwenye maandalizi ya bajeti inayomjali mnyonge....................... ........have your say too.

      Last edited by Rutashubanyuma; 17th June 2012 at 12:21. Reason: spelling, additional points
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    2. FemaTV & Radio

    3. #81
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Tatizo ni kubebana tu
      Comi na hizi mbeleko ni lazima sasa zichanike tu zimechoka..............
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    4. #82
      MAMMAMIA's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Near You
      Posts : 3,794
      Rep Power : 3257
      Likes Received
      1496
      Likes Given
      1206

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Maundumula
      Nakubaliana na wewe juu ya kupunguza Kodi, ila mimi nafikiri kwa kipindi tulichonacho hiki cha ukosefu wa ajira wangetoa punguzo maalum la kodi kwa yale makampuni ya size ya kati ambayo kazi zake labour intensive na wanaoajiri watu kuanzia 3000 na kuendelea ili waje wawekeze hapa pengine ingesaidia vijana.
      Mkuu, mimi mambo ya sayansi ya uchumi siyajui, lakini kwa hisisa tu, kampuni yenye kuajiri kuanzia watu 3000 nahisi ni kampuni kubwa sana. Nakubaliana nawe hilo, lakini pia iko haja ya kufikiria hivi vimradi vidogo vidogo vya wazawa. Ikiwa huko kijijini aliko amweza kuajiri watu 20-50, basi huyo alipaswa kupunguziwa kama si kuondoshewa kodi, tukitilia maanani kuwa wale wanaokosa kazi vijijini huishia kukimbilia mijini.

      Kwa ukosefu huo huo wa ajira, katika nchi niliyo na uzoefu nayo (iliyoendelea), serikali imetangaza msamaha/punguzo la kodi la viwango mbali mbali kwa biashara ndogo na za kati ambazo zinaajiri kuanzia watu 30 tu.

      Quote By Mungi
      why do we wait until 2015? something must be done to rescue the majority!
      Na mimi huwa ninajisemea na kujiuliza hilo hilo. Tunateseka leo, tunabebeshwa mizigo leo, tusubiri 2015 tunasubiri nini? Maajabu kutoka mbinguni? Ni kiongozi gani mahiri anayeweza kwa kipindi kifupi kile kilicharibiwa muda wa miaka 50 mfululizo?

      Quote By mizambwa
      Ndugu Rutashubanyuma, hongera kwa tathmini kubwa uliyoifanya.

      Ukweli Waziri huyu mpya katiak Wizara anapaswa afuatilie jinsi pesa zilivyokopwa na hadi kufikia kiasi kikubwa hivi. Asifanye kazi ya kulindana kama wenzie waliomtrangulia, yasije yakamkuta yaliyowakuta wenzie kwani Watanzania wameamka siyo wale wa mwaka 1961.

      Bila shaka hili deni ni pesa ambazo wajanja wamekula yaani zimeingia mifukoni mwao na siyo katika maslahi ya Taifa.

      Waziri ameshindwa kueleza jinsi deni hili litakavyolipwa na mikakati yake katika kuepusha deni lisiongezeke.

      MIZAMBWA
      NABII MTARAJIWA!!!
      Kwa nchi kama Tanzania yenye Rasilimali nyingi na utajiri mkubwa iweje kuwe na deni kubwa kuliko Bajeti ya Serikali.
      Waziri wa sasa [wa CCM] ni zao la mfumo mbovu wa kulindana. Tusitarajie waziri aliyewekwa kwa fadhili kutafuna mkono unaomlisha. Hii kazi ya kupekua na kufichua maovu ifanywe na vyama vya upinzani, kwa niaba hii, kamati ya fedha ya bunge. Iingie katika kila kabrasha, kila dawati, kila chini ya zulia palipofichwa uoza na kuyaweka hadharani madudu yaliyo/yanayofanyika, sio kwa kutegemea kuwashikisha adabu wahusika mbele ya sheria bali mbele ya wananchi wakati muafaka ukifika.
      mizambwa likes this.
      "JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"

    5. #83
      mtotowamjini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Location : None of Your Business
      Posts : 4,532
      Rep Power : 1263
      Likes Received
      1109
      Likes Given
      28

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      longolongo nyingi hamna kitu
      Every saint has a past, every sinner has a future' ...Oscar Wilde

      One man's good fortune is another man's misfortune

    6. #84
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Hii migongano ya hoja hapa mwisho wake ni nini? Ningewaelewa kama baada ya yote mngekuja na maazimio ambayo yangeweza kupelekwa bungeni kwa kutumia wawakilishi wetu au na PACs kama ilivyo marekani
      @ acha kulaumu ushauri wa bure wa kuiboresha hii bajeti umetolewa hebu rudia kuzisoma hoja zilizooredheshwa hapo chini kwa ushahidi zaidi............
      1) Viongozi wote serikalini wanakiri kuwa makali ya maisha yameongezeka lakini ufumbuzi wao ni kulinda walichonacho au hata kujiongezea bila ya kujua kwa kufanya hivyo walikuwa wanapunguza huduma za kijamii na hivyo kumwongezea makali mlalahoi. Mishahara ya viongozi na sheria ya pensheni ya viongozi vilitakiwa vifanyiwe marekebisho makubwa ili kuondoa ubaguzi ambao unafanywa na viongozi kwenye nyanja hiyo kinyume na sheria..................haya hayakufanyika na kamwe hayatafanyika katika kipindi cha JK akiwa madarakani kwa sababu yeye mwenyewe ni matunda ya mfumo mbovu wa upatikanaji wa viongozi kwa hiyo hawezi kuwa na hisia kali ya kurekebisha mapungufu yaliyopo na hata hisia tajwa angelikuwa nazo bado hana ujuzi wa kufanya hivyo....................kwa lugha nyingine JK ni matunda ya kunukuu staili ya utendaji mbovu ya wale aliyewarithi.

      2) Kumpunguzia makali mlipa kodi mwenye kipato cha chini ya milioni 3 ni unafiki wa kupindukia. Mtumishi wa serikalini mwenye kipato kama hicho hana
      capital costs kwenye mapato yake jambo ambalo anayejiajiri anazo. Tumchukulie mama ntilie mwenye kipato cha milioni 3 kwa mwaka utakuta gharama zake za kuendesha mradi ni asilimia 70 hadi 90 ya mapato tajwa sasa ukimtoza kodi katika kiwango hicho cha chini ni dhahiri unatoza mtaji na hivyo kumwongezea adha za kufukarika. Serikali iliyo makini ingeweka wazi apataye mapato chini ya Tshs 20 millioni kwa mwaka hapaswi kulipa kodi kwa sababu hicho kiwango ni cha kumwezesha kujiajiri na kumudu gharama za maisha...............hivyo pamoja na porojo za Dr. Mgimwa bado hana hisia kali za adha ya umasikini na vyanzo vyake hapa nchini..

      3) Kodi za magari chakavu kupandishiwa umri kutoka miaka 10 hadi zaidi ya miaka 8 ni panga linalokata pande mbili: sababu za kulinda mazingira ni lazima zilinganishwe na sababu za kukuza uchumi. Dr. Mgimwa alipaswa atofautishe aina ya vyombo husika.... magari ya anasa na vifaa vyovyote vile vya anasa ni sahihi kuvitoza kodi tajwa lakini vyombo vya uzalishaji kama vya barabara, ujenzi na viwandani vilipaswa kubaki umri uleule wa miaka 10 kutokana na mchango wake katika kuinua kipato cha nchi na kuwapatia ajira raia wake. Utashangaa kufahamu zaidi ya asilimia 90 ya mitambo ya barabara inayojenga barabara zetu in umri wa zaidi ya miaka 10. Sasa ukianza kutoza kodi ya asilimia 20 kwa yule anayeagiza mitambo hiyo ambayo bado kabisa ina khali nzuri sana huo ufukara unamletea nani kama siyo mlalahoi anayetegemea kujipatia kipato kutokana na vyanzo hivyo vya uzalishaji.

      4) Bajeti kama zile zilizoitangulia bajeti hii, imeshindwa kuainisha kwa kushirikiana na CAG mianya ya kuporomoka uwajibikaji katika matumizi ya serikali. Haitoshi kwa Dr. Mgimwa kudai usimamizi wa bajeti hii utakuwa tofauti na zile zilizotanguliwa bila ya kuonyesha kwa namna zipi. mfano serikali za mitaa inabidi zimilikishwe halmashauri kwa madiwani wawe na mamlaka ya kuajiri watumishi wa ngazi zote badala ya kutegemea serikali kuu kupandikiza mamluki wao ambao ni viwavi jeshi na madiwani kubakia ni wapiga tarumbeta za hamelini. Kwenye mashirika ya umma kuna uhaja wa kubadilisha mfumo mzima wa uteuzi wa bodi na bodi kuwa na mamlaka ya mwisho ya uteuzi wa watendaji wote wakiwemo CEOs kwenye taasisi zao badala ya Ikulu kuona ni kivuno cha kupanga safu za viwavi jeshi. Bodi za wakurugenzi zinapaswa zitokane na wadau wa sekta husika ambao watapatikana kwa kupigiwa kura na washiriki wa nyanja husika hivyo kuondoa mmomonyoko wa uwajibikaji. Wenyeviti wa Bodi kuchaguliwa moja kwa moja na wajumbe wa bodi badala ya Ikulu kuwabandikia mtu ambaye hushukuriwa kwa sababu za kumlinda kisiasa bila ya kujali kama ana mchango wowote wa taasisi ambayo amekabidhiwa kuisimamia....

      5) Kusahau nafasi ya michezo katika kuleta ajira na kukuza uchumi. Timu zote za daraja la juu (Premier league) la mpira wa miguu zilitakiwa zitengewe fungu la kuanzisha timu za watoto ili kuibua vipaji kama sehemu ya awali ya kuanzia. La ajabu viongozi wetu kila siku huimba soka huendelezwa na timu siyo timu ya taifa lakini ni wagumu kwenye mioyo yao kutoa fedha za shughuli hiyo nyeti katika kukuza vipaji vya michezo, kufufua uchumi na kuwapatia ajira vijana wetu. Kwa kuanzia kila timu iliyoko kwenye Premier league ingelitengewa shilingi milioni 200 kwa mwaka kwa kazi hiyo ya kukuza vipaji vya vijana na fedha hizo CAG lazima akague matumizi yake.
      Haya, huyu Dr. Mgimwa hawezi kuyafikiria kwa sababu ni kizazi kilichopitwa na wakati.

      6) (a) Upendeleo wa misamaha ya kodi zote kutofutwa kwa vigezo ambayo vinakinzana na katiba yetu ya kuondoa aina zote za ubaguzi. Katika hukumu ya KTM {Karibu Textiles Mills} mahakama zote za juu zilisema ni ukiukwaji wa katiba kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya makampuni tu tena yapo kwenye sekta moja khalafu wengine mkawabagua eti kwa sababu wana mikataba yao na wengineo hawana. Mbali ya ukweli kuwa ubaguzi tajwa unatibua nguvu ya soko lakini la kuzingatiwa ni kuwa katiba iko juu ya mikataba tajwa.
      Nilidhani kama Dr. Mgimwa is the real deal angeliifuta mikataba tajwa kwa kuongozwa na hukumu za KTM ya EAC na ya CAT (TZ COURT OF APPEAL) katika kutenda haki. Lakini kwa vile, Dr. Mgimwa hakuwekwa pale kwa dhamira safi ya kulisaidia taifa bali ni kujibu tu kiu ya aliyemweka ambaye ninaamini ni Peter Mizengo Pinda basi upeo wa kuyaona haya hana na hivyo hana sifa hata moja ya kuwa Waziri kwenye nyadhifa yoyote ile kwenye baraza la mawaziri achilia mbali Wizara ya fedha.

      b) Misamaha ya kodi kwenye mahoteli ya kitalii kanda ya kaskazini haijafutwa ambayo inaigharimu nchi zaidi ya dola 20-70 milioni kwa mwaka. Sasa Dr. Mgimwa alichelewesha bajeti hii kwa nini kama...........it is business as usual, na hata huyo Pinda aliyekuwa akimtetea hivi haoni hata haya?

      What a shame!

      7) Eneo ambalo humgusa mlalahoi moja kwa moja ni eneo la kodi. Kodi ya VAT ya asilimia 18 imesaidia sana katika kufifilisha soko la ajira. Hawa wakubwa wakisha kulamba hela yetu pale hazina hukimbilia kudai haya ni makusanyo ya serikali na kusahau hata siye ambao hatujaajiriwa serikalini nao ni sehemu hiyo hiyo ya serikali. Serikali yoyote ambayo haisikilizi kukua kwa gharama za maisha na uhaba wa vyanzo vya uzalishaji hiyo serikali siyo sikivu hata kama ikidai vinginevyo.

      a) Kwa kuanzia VAT ilipaswa kupunguzwa kutoka asilimia 18 hadi 15 ili kuhamasisha waajiri wakuze soko la ajira na kuongeza ushindani wa bidhaa zetu kwenye soko la dunia. Mapato ya serikali kuyaongeza siyo kuongeza viwango vya kodi tu bali kuwa na kiwango cha kodi ambacho kitahamasisha tija na uzalishaji. Hili tuendelee kulidai kwani ni haki yetu kukataa kuburutwa bila ya siye kutaka katika ufukara wa kujitakia.

      b) VAT ya EWURA na REA, kwenye umeme ni ya kuondoa tena kinatakiwa kiwe kitendo cha haraka sana. Hivi huo umeme wa vijijini hata ukipelekwa ni nani kule atakayeweza kuumudu gharama zake kama hata wakaazi wengi wa mijini naona wamerudishwa kwenye vibatali tu? Kiujumla wakaazi wa mijini wana uwezo wa kumudu gharama za maisha zaidi ya wale wa vijijini na kama mfupa umemshinda mzee fisi je nani atauweza?

      Hivi huyu Dr. Mgimwa anaelewa nchi hii inatoka wapi, iko wapi na yaelekea wapi? Kama siyo mbabaishaji tu?

      8) Kukwepa kufuta road tolls za magari makubwa. Kila mahali alipokuwa akihalalisha kupanda kwa kodi, Dr. Mgimwa alikuwa anajificha kwenye kichaka cha EAC na sheria zake. Bajeti ya jana ya Kenya wamefuta vizuizi vyote vya barabarani vikiwemo vya tozo za magari makubwa, usafirishaji wa vyakula n.k .......................sasa hayo maigizo ya EAC mbona hayakufika kwenye kufuta road tolls ambazo zinatajirisha watu wachache badala ya kulitajirisha taifa?????????????..........Ku husu uzito wa magari ni udhibiti wa idadi ya matairi ya nyuma la gari au load axles unatosha kabisa kuhakikisha magari yetu hayazidi tani stahiki. Kenya wao lori lenye axles 3 tu ndizo zinaruhusiwa kwenye barabara zao. Sasa ukiisha kulisimamia hilo huu uchafu wa road tolls ambazo zinaongeza mrundikano wa bidhaa na kuchelewesha huduma kwa jamii huku zikimwongezea mlaji gharama zisizorejesheka ni wa nini kama siyo kulinda ajira na ufisadi wa watoto wa vigogo ambao ndiyo wamerundikwa kwenye vituo vya matozo tajwa?

      9) Ukuaji wa deni la taifa Dr. Mgimwa aliuchukulia kimzahamzaha tu na hakuna maelezo ya kutosha kuelezea ni kwa sababu zipi taifa limebebeshwa mzigo wa deni la trilioni 5 tu wakati Mkapa anamkabidhi Jk nchi na khalafu deni hilo lipande khadi trilioni 8 mwaka 2009 na leo lifikie trilioni 22 (Kwa fedha za kitanzania)? Tathmini ya nani alikopa na kwa idhini ya nani inabidi ijulikane sasa na hata CAG sijui yuko wapi kutathmini hilo na badala yake anatumia muda mwingi kuwabana halmashauri ambao mapato yao ni kiduchu. Dr. Mgimwa kama angelikuwa makini angelianzisha sheria ya kuhakikisha bunge ndilo lenye mamlaka ya kupitisha mikopo yote ya serikalini. Hatukumchagua Raisi aende Ikulu kufanya atakavyo bila ya kuwajibika kwa yeyote. Haya madeni yatalipwa na wajukuu zetu na vilembwekazi hata hatujui hizo fedha zilifanya nini na aliyekuwa aziidhinisha alifanya hivyo kwa mashinikizo ya akina nani...........

      10) BOT imekuwa haitazamwi juu ya vyanzo vyake vya mapato na matumizi na imekuwa kinara wa ufisadi ambao hata CAG huwa anaufumbia macho. Wakati umefika mapato na matumizi ya BOT yakawekwa wazi na ile sheria ya kulizuia bunge kudhibiti BOT ikafutwa na kurejesha BOT mikononi mwa udhibiti wa Bunge......................

      Kwa haraka haraka, Dr. Mgimwa ni bomu na tusitishike na kauli zake za kujiamini..mara nyingi matapeli ndivyo walivyo.............na nimpa D minus kwenye maandalizi ya bajeti inayomjali mnyonge....................... ........have your say too.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    7. #85
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Rutashubanyuma
      Ndahani hapo umelonga.................tatiz o siyo mtu bali ni mfumo na mtu anatajwa ili kuthibitisha kuwa huu mfumo unawalakini wa kutupatia viongozi
      Rutashubanyuma, kwa sababu hizo basi, hata iweje, hapa tulipo kubadilisha status quo kunahitaji mtu mwenye maarifa kweli kweli. Tell me one, I would guess what you have in mind,lol! Maarifa yetu sasa hivi ni sifuri...tunaongozwa na nyota na miongozo ya waganga na wapiga ramli.
      Rutashubanyuma likes this.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    8. Miaka 50

    9. #86
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Kimsingi nakubaliana na wewe, tatizo lililopo hapa ni serikali kuongozwa na watu wenye akili za mgando. Hakuna jipya katika hii bajeti. Imekosa kapisa ubunifu zaidi ya kuweka bold kwenye font na kuongeza font size.
      Bajeti inaposomwa inakosa msisimko kuisikiliza maana utakuta yale yale yalionzishwa na Mkapa ndo yanawekewa bold. Pombe, sigallah, na vinavyofanana navyo.
      Tunachoweza Tanzania siyo kubuni vyanzo vipya vya mapato, bali kubuni vyanzo vipya vya misamaha ya kodi.

      What a shame.
      MESTOD tumewasaidia kufikiri lakini usishangae mawazo yetu watayatupilia mbali na baadaye huwa wa kwanza kujigamba ya kuwa wao ni viongozi wasikivu sana sasa huwa ninajiuliza usikivu wao uko wapi kama kero zetu hawzifanyii kazi?
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    10. #87
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Rutashubanyuma, kwa sababu hizo basi, hata iweje, hapa tulipo kubadilisha status quo kunahitaji mtu mwenye maarifa kweli kweli. Tell me one, I would guess what you have in mind,lol! Maarifa yetu sasa hivi ni sifuri...tunaongozwa na nyota na miongozo ya waganga na wapiga ramli.
      @kikubwa ni ufahamu na kadri wengi watakavyo yafahamu mapungufu ya mfumo tulionao basi msukumo wa kuubadili utaongezeka na kila mmoja atadai ya kuwa ashirikishwe na hapo ndipo mwanzo wa kusonga mbele utakapoanza.

      Sioni kama jitihada ya mtu mmoja mmoja yaeza kushindana na huu mfumo ambao tulirithi kutoka kwa mwingereza wa kuiangalia Ikulu kama ndiyo baba na mama wakati ukweli haina mchango mkubwa katika maisha yetu ya kila siku zaidi ya kutuongezea karaha tupu.......
      Ndahani likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    11. #88
      mamajack's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 1,153
      Rep Power : 583
      Likes Received
      275
      Likes Given
      71

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      kiukweli sikutaka kujifariji kupata budget yenye matumaini maana nilihisi kuwa wtanzania wanaenda kubebeshwa mizigo mizito kuliko.na ndo yaliyotokea,maskini watanzania haya maisha mpaka lini? najipa tumaini kwamba,njinsi tunavyo umia ndivyo ukombozi unakaribia.
      iko siku,Mungu atafanya njia.

    12. #89
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,646
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Rutashubanyuma
      Ndahani kikubwa ni ufahamu na kadri wengi watakavyo yafahamu mapungufu ya mfumo tulionao basi msukumo wa kuubadili utaongezeka na kila mmoja atadai ya kuwa ashirikishwe na hapo ndipo mwanzo wa kusonga mbele utakapoanza.

      Sioni kama jitihada ya mtu mmoja mmoja yaeza kushindana na huu mfumo ambao tulirithi kutoka kwa mwingereza wa kuiangalia Ikulu kama ndiyo baba na mama wakati ukweli haina mchango mkubwa katika maisha yetu ya kila siku zaidi ya kutuongezea karaha tupu.......
      Njaa ndio itatufanya tuamke...bado tumeshiba shiba. Mpaka kiporo cha juzi bado hakijakwisha maana hakuna wakula.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    13. #90
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      tatizo lingine TANZANIA NI USHIRIKINA...ukiwa mchapakazi na mweli ...siku zako ni chache hapa Duniani..nimeshaona kwa wengi..na ndo kisa kimenitoa kwenye ajira ya serikali na kujiajiri...wewe jifanye ni mchapa kazi , ukaanza kupata viji safari vya hapa na pale na marupu rupu..utaona jinsi watu wanavyokutazama kwa macho makali...watu wafanyi kazi lakini chuki na wivu vimewatawala..bora kujiajiri kuliko kufa kwenye ajira za serikali...huku nako kwenye kujiajiri taabu tupu..ukianza kufanikiwa mara ooo jamaa anauza unga...mara oo free masons...ina maana ni Tanzania pekee mbapo mafanikio huja kwa kuuza unga na ufreemasons pekee.. naipenda sana nchi yangu...lakini tabia za wakazi wake ni za ajabu sana....Mungu ibariki Tanzania...labda vizazi vijavyo na si hiki wataishi kwa amani na kuifaidi hii nchi bila ushirikina , majungu na wivu...
      @ ushirikina na saratani kubwa hapa nchini. Wivu a fitina ni matunda ya ushirikina na nchi hii kamwe hatuwezi kusonga mbele kama hatuachi ushirikina.............angalia maeneo mengi ambayo yanasifika kwa ushirikina hakuna maendeleo..................... .ukileta maendeleo wewe utapigwa vita ile mbaya.................washirik ina hujivunia umasikini na hiyo ndiyo silaha ya kuitawala jamii
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    14. #91
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,741
      Rep Power : 1317
      Likes Received
      720
      Likes Given
      146

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Rutashubanyuma Nimependa ulivyoona mzigo wa huyu mwenyekiti wa CCM ambaye ndie Raisi wa nchi hii , si ulisema huyu mtu ambaye hana uwezo wa kusafisha nyumba yake anawezeje kutuachia au kutuchagulia Raisi atakaye faa,Ruta nakuuliza kwenye thread yako huko nyuma uliona huyu mtu anatufaa,Raisi Kikwete kazi imemshina na tusitegemee muujiza kwamba kutakuwa na mapinduzi ya kiuchumi nchi hii,wageni watatajirishwa mara elfu kumi wazawa watadhulumiwa hata ile senti ya mwisho.ahsante sana kwa kutunyambulishia mapungufu mengi ambayo yamekuwa somo zuri kwetu
      Rutashubanyuma likes this.

    15. #92
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Nakubaliana na wewe katika hili. Lakini mfumo upo usimamizi ndio mbovu tu
      Haiwezekani upeleke fedha halimashauri bila kuzifuatilia zilivyotumika!.
      Nilichelea kulaumu mwanzoni lakini sasa nafikiri ni mda mhafaka.
      Kwanini unamtwisaha Pinda mzigo usio wake? mara zote umemsikia akilalamika kuwa hana mamlaka juu ya mawaziri.
      Sasa wewe umejuaje kuwa alishinikiza uteuzi?.
      Binafsi nahisi alisema hivyo bungeni ili kuepusha kushushwa hadhi yake kama siku zote!.
      Kyaiyembe labda wewe humfahamu Pinda jinsi ninavyomfahamu..hapendi lawama na yupo tayari kutauta visingizio anapoona kazi imemshinda...................m athalani atasemaje hana madaraka wakati katiba imempa madaraka ya kulithibiti baraza la mawziri kwenye nyanja tatu...moja kulisimamia/ supervise, pili, kuliratibu/co-ordinate na tatu kuliongoza au control....................hiz i ni constitutional powers......kama kazi imemshinda ni vyema akabwaga manyanga na siyo kutafuta visingizio....................

      hili la kumbebesha mzigo siye mimi ila ni hizo hizo taarifa za kiinetelejensia ndizo zinamtia hatiani kwenye huu mradi ni wa kwake akisaidiana na makinda...........anne
      Kyaiyembe likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    16. #93
      Hofstede's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2007
      Posts : 3,604
      Rep Power : 21341
      Likes Received
      981
      Likes Given
      988

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Nilichoki-note jana kwenye hotuba ya Mgimwa ni kuwa, alikuwa akisoma kitu ambacho amepewa tu asome. Hakujiandaa ipasavyo ku-present budget effectly, there was alot of noise (hapa naamina noise in communication siyo kupiga kelele kwa wabunge, bali ni kushindwa kufikisha ujumbe effectively). Nilishangaa pale anaoposema 'utekelezaji huu unaanza mara moja'- baada ya miguno ya wabunge then akarudia kutafuta sehemu kujiridhisha na kujisahihisha kuwa unaanza trh 1/7/2012.

      Kwanza ningependa kufahamu udaktari wake ni nini hasa?, wanyama?, binadamu? au philosophy?, kama ni philosophy basi atakuwa amewashusha madaktari wengi sana kwa poor presentation. Hapa naongelea presentation siongelei substance.
      Last edited by Hofstede; 15th June 2012 at 16:16.
      Rutashubanyuma likes this.

    17. #94
      BIG Banned's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2012
      Location : Banned
      Posts : 263
      Rep Power : 407
      Likes Received
      63
      Likes Given
      77

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Jamani huyu jamaa mimi kwa kumuangalia tu simpendi!!, sidhani kama ana jipya huyu!!, walewale tu!!. anachekelea kwamba ni zamu yake kuiba.
      Rutashubanyuma likes this.
      Vua GAMBA Vaa GWANDA

    18. #95
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,138
      Rep Power : 604
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Kwa Bajeti hii Wa-Tz wanaofurahia ni wale wanaopokea posho na wanaowategemea tu.
      Rutashubanyuma likes this.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    19. #96
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,138
      Rep Power : 604
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Rutashubanyuma
      Kyaiyembe labda wewe humfahamu Pinda jinsi ninavyomfahamu..hapendi lawama na yupo tayari kutauta visingizio anapoona kazi imemshinda...................m athalani atasemaje hana madaraka wakati katiba imempa madaraka ya kulithibiti baraza la mawziri kwenye nyanja tatu...moja kulisimamia/ supervise, pili, kuliratibu/co-ordinate na tatu kuliongoza au control....................hiz i ni constitutional powers......kama kazi imemshinda ni vyema akabwaga manyanga na siyo kutafuta visingizio....................

      hili la kumbebesha mzigo siye mimi ila ni hizo hizo taarifa za kiinetelejensia ndizo zinamtia hatiani kwenye huu mradi ni wa kwake akisaidiana na makinda...........anne
      Kazi kumshinda hilo liko wazi sana na kuhusu katiba mkuu ni formality tu katiba haifanyikazi
      Rutashubanyuma likes this.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    20. #97
      Ogah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Posts : 5,668
      Rep Power : 21814
      Likes Received
      735
      Likes Given
      3189

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Simply lets put this way.........Huyu Mgimwa na timu yake ni "Vilaza"...........mishe mishe zao za serikalini zinawafanya kumsahau kabisa Mtanzania wa kawaida (average) na pia mkulima.........damn!

    21. #98
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Simply lets put this way.........Huyu Mgimwa na timu yake ni "Vilaza"...........mishe mishe zao za serikalini zinawafanya kumsahau kabisa Mtanzania wa kawaida (average) na pia mkulima.........damn!
      Ogah wakiisha shiba wao wanafikiria sote tumeshiba wakati siye njaa inatuuma sana........mlo mmoja kwa siku wakati wao milo yao ni kila lisaa..............
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    22. #99
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Kazi kumshinda hilo liko wazi sana na kuhusu katiba mkuu ni formality tu katiba haifanyikazi
      Kyaiyembe kama una kiongozi hawezi kusimamia misingi ya katiba huyo hatufai kabisa sasa atakuwa na ujasiri gani wa kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo nsdogo kama hizo kubwa yuko kaputi kuzisimamia?
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    23. #100
      muonamambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd September 2010
      Posts : 553
      Rep Power : 552
      Likes Received
      164
      Likes Given
      935

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Wakuu Mimi huwa sioni umuhimu wa Tz kusoma bajeti na Kikao cha bunge la bajeti kwa Sababu zifuatazo...
      1. Vikao vyote havichambui bajeti iliyopita Kuona mapungufu na wapi wajipange zaidi...

      2. Maeneo yenye kodi za kutosha Kama Madini, viwanda na telecom industries hayaguswi na Mkazo siku zote huko kwenye bbidhaa za walalahoi Kama sigara, bia na soda.
      3. Bunge linakuwa ni rubber stamp na Hakuna mabadiliko yoyote zaidi ya watu kupiga kelele kisha wanaunga mkono hoja 100%
      ki ujumla bunge la bajeti ni kupoteza hela za mlalahoi....
      Ogah and Rutashubanyuma like this.

    Page 5 of 9 FirstFirst ... 34567 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...