Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

    Report Post
    Page 4 of 9 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 170
    1. #1
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,885
      Rep Power : 12960
      Likes Received
      4569
      Likes Given
      7574

      Default Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?


      Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akionyesha begi lililobeba hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013, wakati akielekea kuingia katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi


      Jana nilijaribu kumsikiliza waziri wa fedha Dr. Mgimwa na swali lililokuwa likijirudia mara kwa mara kichwani mwangu ni hivi huyu Mheshimiwa ni mradi wa nani?

      Baada ya JK kudhalilishwa na mawaziri wake wawili wa fedha kwa maana ya utendaji duni wa Meghji na Mkullo ni dhahiri alitafuta ushauri wa nani anafaa kumsaidia kwenye wadhifa tajwa................ni nani ushauri wake JK aliuzingatia katika uteuzi tajwa?

      Wakati serikali ya JK ikikumbwa na kashfa ya CAG ya matumizi mabaya ya fedha ulikuwepo uvumi kuwa hata PM alikuwa anafikiria kujing'atua na kumwacha JK azame na merikebu yake ya TITANIC...................laki ni hakufanya hivyo ni kwa sababu zipi?

      Jingine ni kuwa wakati makabrasha ya wizara ya fedha ya bajeti yalipocheleweshwa alikuwa ni Pinda aliyemkingia kifua Dr. Mgimwa kuwa Dr. Mgimwa alikuwa na kibali cha Raisi ayapitie upya makadirio tajwa ili na yeye kwenye wadhifa wake mpya aweze kuweka michango yake.................baada ya kupitia bajeti husika sioni kama kuna jipya ukiondoa misamaha ya kodi kwa walalahoi wanaopata chini ya milioni tatu na hata hapo naona bado kuna uonevu umefanyika na nitafafanua baadaye..........

      Jingine, jipya ni kuamsha ari za usajili magari kwa majina binafsi na kuyalipia milioni 5 kila baada ya miaka 3...............hili ni kuiga marekani ambako utaratibu huu umeshamiri.................

      Mengineyo yote yaliyomo kwenye bajeti, hata Mkullo au Meghji wangelisoma hayohayo kwa hiyo sioni khoja ya Pinda ya ucheleweshwaji wa bajeti kama ina mashiko.......................

      Kwa hiyo, kama Pinda alilidanganya Bunge kwa minajili ya kumlinda Dr. Mgimwa alifanya hivyo kwa masilahi ya nani? Kwa maoni yangu binafsi, Pinda na wala siyo JK ndiye mhimili na mfadhili wa huyu waziri mpya wa fedha na Pinda anaona kavuna dume kwa sababu amekuwa akitafuta mianya ya hazina kusukuma kwa kasi maendeleo ya mkoa wa Rukwa hususani jimbo lake la uchaguzi........na Mkullo hakuwa akimsikiliza sana kwa sababu ana uhusiano wa moja kwa moja na JK uhusiano wa miaka mingi tangia akiwa NPF na JK akiwa kwenye baraza la Mwinyi........

      Bajeti hii ina sifa za kulinda masilahi ya viongozi na wala siyo ya walalahoi na maeneo haya ndiyo maangalizo 10 ambayo yananifanya nije na misimamo tajwa:-

      1) Viongozi wote serikalini wanakiri kuwa makali ya maisha yameongezeka lakini ufumbuzi wao ni kulinda walichonacho au hata kujiongezea bila ya kujua kwa kufanya hivyo walikuwa wanapunguza huduma za kijamii na hivyo kumwongezea makali mlalahoi. Mishahara ya viongozi na sheria ya pensheni ya viongozi vilitakiwa vifanyiwe marekebisho makubwa ili kuondoa ubaguzi ambao unafanywa na viongozi kwenye nyanja hiyo kinyume na sheria..................haya hayakufanyika na kamwe hayatafanyika katika kipindi cha JK akiwa madarakani kwa sababu yeye mwenyewe ni matunda ya mfumo mbovu wa upatikanaji wa viongozi kwa hiyo hawezi kuwa na hisia kali ya kurekebisha mapungufu yaliyopo na hata hisia tajwa angelikuwa nazo bado hana ujuzi wa kufanya hivyo....................kwa lugha nyingine JK ni matunda ya kunukuu staili ya utendaji mbovu ya wale aliyewarithi.

      2) Kumpunguzia makali mlipa kodi mwenye kipato cha chini ya milioni 3 ni unafiki wa kupindukia. Mtumishi wa serikalini mwenye kipato kama hicho hana
      capital costs kwenye mapato yake jambo ambalo anayejiajiri anazo. Tumchukulie mama ntilie mwenye kipato cha milioni 3 kwa mwaka utakuta gharama zake za kuendesha mradi ni asilimia 70 hadi 90 ya mapato tajwa sasa ukimtoza kodi katika kiwango hicho cha chini ni dhahiri unatoza mtaji na hivyo kumwongezea adha za kufukarika. Serikali iliyo makini ingeweka wazi apataye mapato chini ya Tshs 20 millioni kwa mwaka hapaswi kulipa kodi kwa sababu hicho kiwango ni cha kumwezesha kujiajiri na kumudu gharama za maisha...............hivyo pamoja na porojo za Dr. Mgimwa bado hana hisia kali za adha ya umasikini na vyanzo vyake hapa nchini..

      3) Kodi za magari chakavu kupandishiwa umri kutoka miaka 10 hadi zaidi ya miaka 8 ni panga linalokata pande mbili: sababu za kulinda mazingira ni lazima zilinganishwe na sababu za kukuza uchumi. Dr. Mgimwa alipaswa atofautishe aina ya vyombo husika.... magari ya anasa na vifaa vyovyote vile vya anasa ni sahihi kuvitoza kodi tajwa lakini vyombo vya uzalishaji kama vya barabara, ujenzi na viwandani vilipaswa kubaki umri uleule wa miaka 10 kutokana na mchango wake katika kuinua kipato cha nchi na kuwapatia ajira raia wake. Utashangaa kufahamu zaidi ya asilimia 90 ya mitambo ya barabara inayojenga barabara zetu in umri wa zaidi ya miaka 10. Sasa ukianza kutoza kodi ya asilimia 20 kwa yule anayeagiza mitambo hiyo ambayo bado kabisa ina khali nzuri sana huo ufukara unamletea nani kama siyo mlalahoi anayetegemea kujipatia kipato kutokana na vyanzo hivyo vya uzalishaji.

      4) Bajeti kama zile zilizoitangulia bajeti hii, imeshindwa kuainisha kwa kushirikiana na CAG mianya ya kuporomoka uwajibikaji katika matumizi ya serikali. Haitoshi kwa Dr. Mgimwa kudai usimamizi wa bajeti hii utakuwa tofauti na zile zilizotanguliwa bila ya kuonyesha kwa namna zipi. mfano serikali za mitaa inabidi zimilikishwe halmashauri kwa madiwani wawe na mamlaka ya kuajiri watumishi wa ngazi zote badala ya kutegemea serikali kuu kupandikiza mamluki wao ambao ni viwavi jeshi na madiwani kubakia ni wapiga tarumbeta za hamelini. Kwenye mashirika ya umma kuna uhaja wa kubadilisha mfumo mzima wa uteuzi wa bodi na bodi kuwa na mamlaka ya mwisho ya uteuzi wa watendaji wote wakiwemo CEOs kwenye taasisi zao badala ya Ikulu kuona ni kivuno cha kupanga safu za viwavi jeshi. Bodi za wakurugenzi zinapaswa zitokane na wadau wa sekta husika ambao watapatikana kwa kupigiwa kura na washiriki wa nyanja husika hivyo kuondoa mmomonyoko wa uwajibikaji. Wenyeviti wa Bodi kuchaguliwa moja kwa moja na wajumbe wa bodi badala ya Ikulu kuwabandikia mtu ambaye hushukuriwa kwa sababu za kumlinda kisiasa bila ya kujali kama ana mchango wowote wa taasisi ambayo amekabidhiwa kuisimamia....

      5) Kusahau nafasi ya michezo katika kuleta ajira na kukuza uchumi. Timu zote za daraja la juu (Premier league) la mpira wa miguu zilitakiwa zitengewe fungu la kuanzisha timu za watoto ili kuibua vipaji kama sehemu ya awali ya kuanzia. La ajabu viongozi wetu kila siku huimba soka huendelezwa na timu siyo timu ya taifa lakini ni wagumu kwenye mioyo yao kutoa fedha za shughuli hiyo nyeti katika kukuza vipaji vya michezo, kufufua uchumi na kuwapatia ajira vijana wetu. Kwa kuanzia kila timu iliyoko kwenye Premier league ingelitengewa shilingi milioni 200 kwa mwaka kwa kazi hiyo ya kukuza vipaji vya vijana na fedha hizo CAG lazima akague matumizi yake.
      Haya, huyu Dr. Mgimwa hawezi kuyafikiria kwa sababu ni kizazi kilichopitwa na wakati.

      6) (a) Upendeleo wa misamaha ya kodi zote kutofutwa kwa vigezo ambayo vinakinzana na katiba yetu ya kuondoa aina zote za ubaguzi. Katika hukumu ya KTM {Karibu Textiles Mills} mahakama zote za juu zilisema ni ukiukwaji wa katiba kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya makampuni tu tena yapo kwenye sekta moja khalafu wengine mkawabagua eti kwa sababu wana mikataba yao na wengineo hawana. Mbali ya ukweli kuwa ubaguzi tajwa unatibua nguvu ya soko lakini la kuzingatiwa ni kuwa katiba iko juu ya mikataba tajwa.
      Nilidhani kama Dr. Mgimwa is the real deal angeliifuta mikataba tajwa kwa kuongozwa na hukumu za KTM ya EAC na ya CAT (TZ COURT OF APPEAL) katika kutenda haki. Lakini kwa vile, Dr. Mgimwa hakuwekwa pale kwa dhamira safi ya kulisaidia taifa bali ni kujibu tu kiu ya aliyemweka ambaye ninaamini ni Peter Mizengo Pinda basi upeo wa kuyaona haya hana na hivyo hana sifa hata moja ya kuwa Waziri kwenye nyadhifa yoyote ile kwenye baraza la mawaziri achilia mbali Wizara ya fedha.

      b) Misamaha ya kodi kwenye mahoteli ya kitalii kanda ya kaskazini haijafutwa ambayo inaigharimu nchi zaidi ya dola 20-70 milioni kwa mwaka. Sasa Dr. Mgimwa alichelewesha bajeti hii kwa nini kama...........it is business as usual, na hata huyo Pinda aliyekuwa akimtetea hivi haoni hata haya?


      What a shame!



      7) Eneo ambalo humgusa mlalahoi moja kwa moja ni eneo la kodi. Kodi ya VAT ya asilimia 18 imesaidia sana katika kufifilisha soko la ajira. Hawa wakubwa wakisha kulamba hela yetu pale hazina hukimbilia kudai haya ni makusanyo ya serikali na kusahau hata siye ambao hatujaajiriwa serikalini nao ni sehemu hiyo hiyo ya serikali. Serikali yoyote ambayo haisikilizi kukua kwa gharama za maisha na uhaba wa vyanzo vya uzalishaji hiyo serikali siyo sikivu hata kama ikidai vinginevyo.

      a) Kwa kuanzia VAT ilipaswa kupunguzwa kutoka asilimia 18 hadi 15 ili kuhamasisha waajiri wakuze soko la ajira na kuongeza ushindani wa bidhaa zetu kwenye soko la dunia. Mapato ya serikali kuyaongeza siyo kuongeza viwango vya kodi tu bali kuwa na kiwango cha kodi ambacho kitahamasisha tija na uzalishaji. Hili tuendelee kulidai kwani ni haki yetu kukataa kuburutwa bila ya siye kutaka katika ufukara wa kujitakia.

      b) VAT ya EWURA na REA, kwenye umeme ni ya kuondoa tena kinatakiwa kiwe kitendo cha haraka sana. Hivi huo umeme wa vijijini hata ukipelekwa ni nani kule atakayeweza kuumudu gharama zake kama hata wakaazi wengi wa mijini naona wamerudishwa kwenye vibatali tu? Kiujumla wakaazi wa mijini wana uwezo wa kumudu gharama za maisha zaidi ya wale wa vijijini na kama mfupa umemshinda mzee fisi je nani atauweza?

      c) Kila Halmashauri ilipaswa kutengewa 7% ya VAT kwenda moja kwa moja kwenye shughuli zao badala ya kutegemea hisani ya serikali kuu au udanganyifu wa mfuko wa jimbo ambao nao ni kituko kwani siyo shirikishi hata chembe. Serikali kuu ingelibaki na 8% ya makusanyo ya VAT kwa minajili ya kusawazisha maeneo ambayo yana mapato madogo na hivyo kuleta maendeleo yenye uwiano mzuri. Mfumo wa mgawanyo uliopo unaipa serikali kuu hususani DSM upendeleo wa kila kitu na hivyo kuacha mikoa ya pembezoni kuwa nyuma sana kimaendeleo. Huu ndiyo mtazamo mpya wa kulikwamua taifa kutoka hapa lilipo hadi kwenda kwenye maendeleo kwa kila mtanzania..................... ...azma ambayo ianaelekea ni tamu wakati wa kuomba kura lakini ni chungu katika kuitekeleza..............

      Hivi huyu Dr. Mgimwa anaelewa nchi hii inatoka wapi, iko wapi na yaelekea wapi? Kama siyo mbabaishaji tu?


      8) Kukwepa kufuta road tolls za magari makubwa. Kila mahali alipokuwa akihalalisha kupanda kwa kodi, Dr. Mgimwa alikuwa anajificha kwenye kichaka cha EAC na sheria zake. Bajeti ya jana ya Kenya wamefuta vizuizi vyote vya barabarani vikiwemo vya tozo za magari makubwa, usafirishaji wa vyakula n.k .......................sasa hayo maigizo ya EAC mbona hayakufika kwenye kufuta road tolls ambazo zinatajirisha watu wachache badala ya kulitajirisha taifa?????????????..........Ku husu uzito wa magari ni udhibiti wa idadi ya matairi ya nyuma la gari au load axles unatosha kabisa kuhakikisha magari yetu hayazidi tani stahiki. Kenya wao lori lenye axles 3 tu ndizo zinaruhusiwa kwenye barabara zao. Sasa ukiisha kulisimamia hilo huu uchafu wa road tolls ambazo zinaongeza mrundikano wa bidhaa na kuchelewesha huduma kwa jamii huku zikimwongezea mlaji gharama zisizorejesheka ni wa nini kama siyo kulinda ajira na ufisadi wa watoto wa vigogo ambao ndiyo wamerundikwa kwenye vituo vya matozo tajwa?

      9) Ukuaji wa deni la taifa Dr. Mgimwa aliuchukulia kimzahamzaha tu na hakuna maelezo ya kutosha kuelezea ni kwa sababu zipi taifa limebebeshwa mzigo wa deni la trilioni 5 tu wakati Mkapa anamkabidhi Jk nchi na khalafu deni hilo lipande khadi trilioni 8 mwaka 2009 na leo lifikie trilioni 22 (Kwa fedha za kitanzania)? Tathmini ya nani alikopa na kwa idhini ya nani inabidi ijulikane sasa na hata CAG sijui yuko wapi kutathmini hilo na badala yake anatumia muda mwingi kuwabana halmashauri ambao mapato yao ni kiduchu. Dr. Mgimwa kama angelikuwa makini angelianzisha sheria ya kuhakikisha bunge ndilo lenye mamlaka ya kupitisha mikopo yote ya serikalini. Hatukumchagua Raisi aende Ikulu kufanya atakavyo bila ya kuwajibika kwa yeyote. Haya madeni yatalipwa na wajukuu zetu na vilembwekazi hata hatujui hizo fedha zilifanya nini na aliyekuwa aziidhinisha alifanya hivyo kwa mashinikizo ya akina nani...........

      10) BOT imekuwa haitazamwi juu ya vyanzo vyake vya mapato na matumizi na imekuwa kinara wa ufisadi ambao hata CAG huwa anaufumbia macho. Wakati umefika mapato na matumizi ya BOT yakawekwa wazi na ile sheria ya kulizuia bunge kudhibiti BOT ikafutwa na kurejesha BOT mikononi mwa udhibiti wa Bunge......................

      Kwa haraka haraka, Dr. Mgimwa ni bomu na tusitishike na kauli zake za kujiamini..mara nyingi matapeli ndivyo walivyo.............na nimpa D minus kwenye maandalizi ya bajeti inayomjali mnyonge....................... ........have your say too.

      Last edited by Rutashubanyuma; 17th June 2012 at 12:21. Reason: spelling, additional points
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."


    2. #61
      Jimbi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th August 2010
      Location : ILALA
      Posts : 738
      Rep Power : 596
      Likes Received
      131
      Likes Given
      547

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      bajet uchwara tu hii
      Rutashubanyuma likes this.
      KIKUPACHO UTAMU.... NA UCHUNGU KITAKUPA!!

    3. #62
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,161
      Rep Power : 613
      Likes Received
      350
      Likes Given
      307

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Rutashubanyuma View Post
      Kyaiyembe ubora wa kiongozi siyo kufanya kazi zote mwenyewe bali kujenga miundo mbinu ya kimfumo ambayo itawashirikisha wenzie kusukuma gurudumu la maendeleo yetu.........na hivyo hata kama hayupo hiyo mifumo itaendelea kufanya kazi............
      Nakubaliana na wewe katika hili. Lakini mfumo upo usimamizi ndio mbovu tu
      Haiwezekani upeleke fedha halimashauri bila kuzifuatilia zilivyotumika!.
      Nilichelea kulaumu mwanzoni lakini sasa nafikiri ni mda mhafaka.
      Kwanini unamtwisaha Pinda mzigo usio wake? mara zote umemsikia akilalamika kuwa hana mamlaka juu ya mawaziri.
      Sasa wewe umejuaje kuwa alishinikiza uteuzi?.
      Binafsi nahisi alisema hivyo bungeni ili kuepusha kushushwa hadhi yake kama siku zote!.
      Rutashubanyuma likes this.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    4. #63
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,822
      Rep Power : 1939
      Likes Received
      1226
      Likes Given
      1189

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Mimi nafikiri mnahitaji kuwa na Subra.

      mnatakiwa ili kuwe na bajeti lazima kuangalia hali halisi ya nchi kisha kuweka mipango ndipo mnaandika bajeti yenu. Huwezi kuangalia mambo ya mbele pasi na kujua yale yaliyopo na yaliyopita lakin bado yapo.

      Kuna mengi ngoja niipitie kisha nitarudi kuijadili kwani kunahitaji utulivu kidogo katika kuichambua.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    5. #64
      Mwanaweja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 3,520
      Rep Power : 1128
      Likes Received
      480
      Likes Given
      1065

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      serikali na viongozi wake wote akili zilisha fika kikomo cha kuweza kiufikiria kwa hiyo ni ngumu sana kuwalekebisha ila kikubwa ni kuitoa hii system ilitujaribu nyingine tena
      Rutashubanyuma likes this.

    6. #65
      Ronn M's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2012
      Location : Moshi~Arusha
      Posts : 1,283
      Rep Power : 615
      Likes Received
      660
      Likes Given
      403

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      it as if the whole country no one thinks! We have chosen fools to lead us. We ve to bear the costs
      Rutashubanyuma likes this.


    7. #66
      mizambwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2008
      Posts : 1,445
      Rep Power : 980
      Likes Received
      373
      Likes Given
      1822

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Rutashubanyuma View Post

      Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akionyesha begi lililobeba hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013, wakati akielekea kuingia katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi


      Mengineyo yote yaliyomo kwenye bajeti, hata Mkullo au Meghji wangelisoma hayohayo kwa hiyo sioni khoja ya Pinda ya ucheleweshwaji wa bajeti kama ina mashiko.......................

      Kwa hiyo, kama Pinda alilidanganya Bunge kwa minajili ya kumlinda Dr. Mgimwa alifanya hivyo kwa masilahi ya nani?
      4) Bajeti kama zile zilizoitangulia bajeti hii, imeshindwa kuainisha kwa kushirikiana na CAG mianya ya kuporomoka uwajibikaji katika matumizi ya serikali.
      9) Ukuaji wa deni la taifa Dr. Mgimwa aliuchukulia kimzahamzaha tu na hakuna maelezo ya kutosha kuelezea ni kwa sababu zipi taifa limebebeshwa mzigo wa deni la trilioni 5 tu wakati Mkapa anamkabidhi Jk nchi na khalafu deni hilo lipande khadi trilioni 8 mwaka 2009 na leo lifikie trilioni 22 (Kwa fedha za kitanzania)? Tathmini ya nani alikopa na kwa idhini ya nani inabidi ijulikane sasa na hata CAG sijui yuko wapi kutathmini hilo na badala yake anatumia muda mwingi kuwabana halmashauri ambao mapato yao ni kiduchu. Dr. Mgimwa kama angelikuwa makini angelianzisha sheria ya kuhakikisha bunge ndilo lenye mamlaka ya kupitisha mikopo yote ya serikalini. Hatukumchagua Raisi aende Ikulu kufanya atakavyo bila ya kuwajibika kwa yeyote. Haya madeni yatalipwa na wajukuu zetu na vilembwekazi hata hatujui hizo fedha zilifanya nini na aliyekuwa aziidhinisha alifanya hivyo kwa mashinikizo ya akina nani........
      Ndugu Rutashubanyuma, hongera kwa tathmini kubwa uliyoifanya.

      Ukweli Waziri huyu mpya katiak Wizara anapaswa afuatilie jinsi pesa zilivyokopwa na hadi kufikia kiasi kikubwa hivi. Asifanye kazi ya kulindana kama wenzie waliomtrangulia, yasije yakamkuta yaliyowakuta wenzie kwani Watanzania wameamka siyo wale wa mwaka 1961.

      Bila shaka hili deni ni pesa ambazo wajanja wamekula yaani zimeingia mifukoni mwao na siyo katika maslahi ya Taifa.

      Waziri ameshindwa kueleza jinsi deni hili litakavyolipwa na mikakati yake katika kuepusha deni lisiongezeke.



      MIZAMBWA
      NABII MTARAJIWA!!!
      Kwa nchi kama Tanzania yenye Rasilimali nyingi na utajiri mkubwa iweje kuwe na deni kubwa kuliko Bajeti ya Serikali.
      Rutashubanyuma likes this.
      SASA NIMEAMINI KUWA TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA!!!!, TUANDAE KABURI LA KUIZIKA MWAKA 2015

    8. #67
      georgeallen's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd June 2011
      Location : Seattle, WA, USA
      Posts : 2,136
      Rep Power : 0
      Likes Received
      539
      Likes Given
      277

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Hii migongano ya hoja hapa mwisho wake ni nini? Ningewaelewa kama baada ya yote mngekuja na maazimio ambayo yangeweza kupelekwa bungeni kwa kutumia wawakilishi wetu au na PACs kama ilivyo marekani
      Rutashubanyuma likes this.

    9. #68
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,779
      Rep Power : 19847
      Likes Received
      4407
      Likes Given
      1715

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Ili ni bomu lingine la pinda
      Rutashubanyuma likes this.

    10. #69
      Ndakilawe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2011
      Location : Kumasi
      Posts : 481
      Rep Power : 498
      Likes Received
      53
      Likes Given
      64

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      huyu waziri ni sifuri kweli! ila smlaumu kwa vile kazi yake ni kosoma tu pale mjengoni, ila wanaopanga ni hao hao wenzake wa magambani, Mh. Chenge, eti kampa big up kwa ushauri mzuri alioutoa katika kuandaa bajeti! mmh, kweli shetani akizeeka anazaa mashetani wengi zaidi... Jamaa kilaza sana, kuna wakati alikuwa anasoma hoja, then akiona amechemka, anaaanza kuitetea hapo hapo..aibu hii... Tujifunge mkanda jamani, CCM itatumaliza, natama yale yaliyotokea Misri, Tunisia na hapa yatokee, 2015 mbali sana, sisi tusiokuwa na ajira maalumu tutafia njiani..
      Rutashubanyuma likes this.

    11. #70
      Ulimakafu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2011
      Location : Itabanya Balasi
      Posts : 11,258
      Rep Power : 2669
      Likes Received
      722
      Likes Given
      1637

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Ndahani View Post
      Why dont we wait until 2015? Is there anything new now? Au ndio mambo ya kuweka zabibu mpya kwenye kiriba cha kale....
      Ni sahihi kabisa uyasemayo.

    12. #71
      Comi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 1,031
      Rep Power : 596
      Likes Received
      164
      Likes Given
      2

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Tatizo ni kubebana tu
      Rutashubanyuma likes this.

    13. #72
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,968
      Rep Power : 3411
      Likes Received
      1340
      Likes Given
      494

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      hii nchi ya ajabu kweli mapato ya serikalì ni trioni 8 matumizi trioni 10 ... Maendeleo trioni 5 tena kwa hisani ya watu wa ulaya.!
      muonamambo and Rutashubanyuma like this.

    14. #73
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,660
      Rep Power : 4023
      Likes Received
      2943
      Likes Given
      5072

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      System ilivyokaa ilikuwa inawasukuma watu wengi sana kuamua kujiunga na siasa kwa kupitia CCM. CCM ikabeba kila Tom, Dick and Harry...viongozi wa kweli walio wengi walipigwa kumbo wakaangushwa. Wenye fedha ndio hao leo wanapigana front kama mawaziri na viongozi wa umma. Tutegemee nini? Pengine Dr. Mgimwa ni mzuri...lakini a drop in a ocean itasaida nini? Bila kuwa na mfumo mzuri wa kupata viongozi, nchi hii tusitegemee muujiza. Watu wasichojua ni kuwa we are sailing in the same boat...tukizama tutazama sooote kwa ujumla wetu
      Rutashubanyuma likes this.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    15. #74
      Ulimakafu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th March 2011
      Location : Itabanya Balasi
      Posts : 11,258
      Rep Power : 2669
      Likes Received
      722
      Likes Given
      1637

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Queen Esther View Post
      Naomba kukuuliza mheshimiwa yafuatayo: i. Kwani Mh. Waziri kaandaa hiyo bajeti peke yake? ii. Wataalamu wa wizara ya Fedha, BOT, Mashirika ya Fedha nk hawakuhusika?iii. Je ana muda gani hapo HAZINA hata tumtoe makosa kupitia bajeti aliyokuta imeandaliwa?. iv. Mwisho usisahau ni mara ya kwanza yeye kusimama Bungeni na kupewa jukumu kubwa kama hili. It is obvious anaweza kuwa ametetereka ktk kuongea na kuwasilisha mada. Hilo lisitufanye tuendelee kumuona hafai.v. Watanzania wenzangu safari ya ukombozi wa Mtanzania bado ni ndefu hivyo nasisitiza tumpe muda anaweza kuwa Daudi aliyemuua Goliati. Tupunguze negativity kubwa tuliyonayo inayosababisha upofu hata yaliyo mazuri hatuyaoni wala hatutayaona tukiendelea hivi. Tumuombee yeye na viongozi wengine watuongoze vizuri na kwa uadilifu, pia na tuiombee Tanzania yetu, nani ajuae Daudi amepatikana?Queen Esther
      No mate BIG NO!!!!.Kwa serikali hii NOOOOOO....
      Rutashubanyuma likes this.

    16. #75
      Mr Rocky's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2007
      Location : Hungumalwa
      Posts : 9,706
      Rep Power : 68642
      Likes Received
      7080
      Likes Given
      5587

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      jukwaa la ban ni bora kukaa mbali maana huchelewi kutukana hapa
      Rutashubanyuma likes this.
      When you are in Love you can't fall asleep because reality is better than your dreams

    17. #76
      Ikwanja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th July 2011
      Posts : 566
      Rep Power : 515
      Likes Received
      106
      Likes Given
      48

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Kuona kwamba bajeti hiihaina kitu hebu angalia ulinganifi na nchi zingine jirani kuhusu highlight za bajet zaoHighlights2012_Tanzania.pdf
      Rutashubanyuma likes this.

    18. #77
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,885
      Rep Power : 12960
      Likes Received
      4569
      Likes Given
      7574

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      No mate BIG NO!!!!.Kwa serikali hii NOOOOOO....
      Ulimakafu mweleze huyu @ atuelewe mambo yanap[oharibika waziri ndiye mwajibikaji nambali wani na hapa Dr. Mgimwa hawezi kunusurika lawama zetru za kucheza na maisha yetu zote zinaangukia kwake tu.................
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    19. #78
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,885
      Rep Power : 12960
      Likes Received
      4569
      Likes Given
      7574

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Kuona kwamba bajeti hiihaina kitu hebu angalia ulinganifi na nchi zingine jirani kuhusu highlight za bajet zaoHighlights2012_Tanzania.pdf
      Ikwanja wqenzetu wako serious siyo blahblah kama siye
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    20. #79
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,885
      Rep Power : 12960
      Likes Received
      4569
      Likes Given
      7574

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      System ilivyokaa ilikuwa inawasukuma watu wengi sana kuamua kujiunga na siasa kwa kupitia CCM. CCM ikabeba kila Tom, Dick and Harry...viongozi wa kweli walio wengi walipigwa kumbo wakaangushwa. Wenye fedha ndio hao leo wanapigana front kama mawaziri na viongozi wa umma. Tutegemee nini? Pengine Dr. Mgimwa ni mzuri...lakini a drop in a ocean itasaida nini? Bila kuwa na mfumo mzuri wa kupata viongozi, nchi hii tusitegemee muujiza. Watu wasichojua ni kuwa we are sailing in the same boat...tukizama tutazama sooote kwa ujumla wetu
      Ndahani hapo umelonga.................tatiz o siyo mtu bali ni mfumo na mtu anatajwa ili kuthibitisha kuwa huu mfumo unawalakini wa kutupatia viongozi
      Ndahani likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    21. #80
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,885
      Rep Power : 12960
      Likes Received
      4569
      Likes Given
      7574

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      hii nchi ya ajabu kweli mapato ya serikalì ni trioni 8 matumizi trioni 10 ... Maendeleo trioni 5 tena kwa hisani ya watu wa ulaya.!
      idawa ni ajabu sana baada ya siku chache utasikia serikali haina hela lakini kila mwaka hujigamba na bajeti nene na makusanyo yetu yanategemea wafadhili kwa karibu asilimia 70 kwa maendeleo na karibu asilimia 30 ya bajeti ya matumizi ya kawaida nayo ina fadhiliwa na wahisani. Tatizo ni kuwa mambo muhimu huwa hayafanyiki na yale ambayo siyo muhimu hufanyika............
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    Page 4 of 9 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...