Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

    Report Post
    Page 2 of 9 FirstFirst 1234 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 170
    1. #1
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?


      Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa akionyesha begi lililobeba hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2012/2013, wakati akielekea kuingia katika ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi


      Jana nilijaribu kumsikiliza waziri wa fedha Dr. Mgimwa na swali lililokuwa likijirudia mara kwa mara kichwani mwangu ni hivi huyu Mheshimiwa ni mradi wa nani?

      Baada ya JK kudhalilishwa na mawaziri wake wawili wa fedha kwa maana ya utendaji duni wa Meghji na Mkullo ni dhahiri alitafuta ushauri wa nani anafaa kumsaidia kwenye wadhifa tajwa................ni nani ushauri wake JK aliuzingatia katika uteuzi tajwa?

      Wakati serikali ya JK ikikumbwa na kashfa ya CAG ya matumizi mabaya ya fedha ulikuwepo uvumi kuwa hata PM alikuwa anafikiria kujing'atua na kumwacha JK azame na merikebu yake ya TITANIC...................laki ni hakufanya hivyo ni kwa sababu zipi?

      Jingine ni kuwa wakati makabrasha ya wizara ya fedha ya bajeti yalipocheleweshwa alikuwa ni Pinda aliyemkingia kifua Dr. Mgimwa kuwa Dr. Mgimwa alikuwa na kibali cha Raisi ayapitie upya makadirio tajwa ili na yeye kwenye wadhifa wake mpya aweze kuweka michango yake.................baada ya kupitia bajeti husika sioni kama kuna jipya ukiondoa misamaha ya kodi kwa walalahoi wanaopata chini ya milioni tatu na hata hapo naona bado kuna uonevu umefanyika na nitafafanua baadaye..........

      Jingine, jipya ni kuamsha ari za usajili magari kwa majina binafsi na kuyalipia milioni 5 kila baada ya miaka 3...............hili ni kuiga marekani ambako utaratibu huu umeshamiri.................

      Mengineyo yote yaliyomo kwenye bajeti, hata Mkullo au Meghji wangelisoma hayohayo kwa hiyo sioni khoja ya Pinda ya ucheleweshwaji wa bajeti kama ina mashiko.......................

      Kwa hiyo, kama Pinda alilidanganya Bunge kwa minajili ya kumlinda Dr. Mgimwa alifanya hivyo kwa masilahi ya nani? Kwa maoni yangu binafsi, Pinda na wala siyo JK ndiye mhimili na mfadhili wa huyu waziri mpya wa fedha na Pinda anaona kavuna dume kwa sababu amekuwa akitafuta mianya ya hazina kusukuma kwa kasi maendeleo ya mkoa wa Rukwa hususani jimbo lake la uchaguzi........na Mkullo hakuwa akimsikiliza sana kwa sababu ana uhusiano wa moja kwa moja na JK uhusiano wa miaka mingi tangia akiwa NPF na JK akiwa kwenye baraza la Mwinyi........

      Bajeti hii ina sifa za kulinda masilahi ya viongozi na wala siyo ya walalahoi na maeneo haya ndiyo maangalizo 10 ambayo yananifanya nije na misimamo tajwa:-

      1) Viongozi wote serikalini wanakiri kuwa makali ya maisha yameongezeka lakini ufumbuzi wao ni kulinda walichonacho au hata kujiongezea bila ya kujua kwa kufanya hivyo walikuwa wanapunguza huduma za kijamii na hivyo kumwongezea makali mlalahoi. Mishahara ya viongozi na sheria ya pensheni ya viongozi vilitakiwa vifanyiwe marekebisho makubwa ili kuondoa ubaguzi ambao unafanywa na viongozi kwenye nyanja hiyo kinyume na sheria..................haya hayakufanyika na kamwe hayatafanyika katika kipindi cha JK akiwa madarakani kwa sababu yeye mwenyewe ni matunda ya mfumo mbovu wa upatikanaji wa viongozi kwa hiyo hawezi kuwa na hisia kali ya kurekebisha mapungufu yaliyopo na hata hisia tajwa angelikuwa nazo bado hana ujuzi wa kufanya hivyo....................kwa lugha nyingine JK ni matunda ya kunukuu staili ya utendaji mbovu ya wale aliyewarithi.

      2) Kumpunguzia makali mlipa kodi mwenye kipato cha chini ya milioni 3 ni unafiki wa kupindukia. Mtumishi wa serikalini mwenye kipato kama hicho hana
      capital costs kwenye mapato yake jambo ambalo anayejiajiri anazo. Tumchukulie mama ntilie mwenye kipato cha milioni 3 kwa mwaka utakuta gharama zake za kuendesha mradi ni asilimia 70 hadi 90 ya mapato tajwa sasa ukimtoza kodi katika kiwango hicho cha chini ni dhahiri unatoza mtaji na hivyo kumwongezea adha za kufukarika. Serikali iliyo makini ingeweka wazi apataye mapato chini ya Tshs 20 millioni kwa mwaka hapaswi kulipa kodi kwa sababu hicho kiwango ni cha kumwezesha kujiajiri na kumudu gharama za maisha...............hivyo pamoja na porojo za Dr. Mgimwa bado hana hisia kali za adha ya umasikini na vyanzo vyake hapa nchini..

      3) Kodi za magari chakavu kupandishiwa umri kutoka miaka 10 hadi zaidi ya miaka 8 ni panga linalokata pande mbili: sababu za kulinda mazingira ni lazima zilinganishwe na sababu za kukuza uchumi. Dr. Mgimwa alipaswa atofautishe aina ya vyombo husika.... magari ya anasa na vifaa vyovyote vile vya anasa ni sahihi kuvitoza kodi tajwa lakini vyombo vya uzalishaji kama vya barabara, ujenzi na viwandani vilipaswa kubaki umri uleule wa miaka 10 kutokana na mchango wake katika kuinua kipato cha nchi na kuwapatia ajira raia wake. Utashangaa kufahamu zaidi ya asilimia 90 ya mitambo ya barabara inayojenga barabara zetu in umri wa zaidi ya miaka 10. Sasa ukianza kutoza kodi ya asilimia 20 kwa yule anayeagiza mitambo hiyo ambayo bado kabisa ina khali nzuri sana huo ufukara unamletea nani kama siyo mlalahoi anayetegemea kujipatia kipato kutokana na vyanzo hivyo vya uzalishaji.

      4) Bajeti kama zile zilizoitangulia bajeti hii, imeshindwa kuainisha kwa kushirikiana na CAG mianya ya kuporomoka uwajibikaji katika matumizi ya serikali. Haitoshi kwa Dr. Mgimwa kudai usimamizi wa bajeti hii utakuwa tofauti na zile zilizotanguliwa bila ya kuonyesha kwa namna zipi. mfano serikali za mitaa inabidi zimilikishwe halmashauri kwa madiwani wawe na mamlaka ya kuajiri watumishi wa ngazi zote badala ya kutegemea serikali kuu kupandikiza mamluki wao ambao ni viwavi jeshi na madiwani kubakia ni wapiga tarumbeta za hamelini. Kwenye mashirika ya umma kuna uhaja wa kubadilisha mfumo mzima wa uteuzi wa bodi na bodi kuwa na mamlaka ya mwisho ya uteuzi wa watendaji wote wakiwemo CEOs kwenye taasisi zao badala ya Ikulu kuona ni kivuno cha kupanga safu za viwavi jeshi. Bodi za wakurugenzi zinapaswa zitokane na wadau wa sekta husika ambao watapatikana kwa kupigiwa kura na washiriki wa nyanja husika hivyo kuondoa mmomonyoko wa uwajibikaji. Wenyeviti wa Bodi kuchaguliwa moja kwa moja na wajumbe wa bodi badala ya Ikulu kuwabandikia mtu ambaye hushukuriwa kwa sababu za kumlinda kisiasa bila ya kujali kama ana mchango wowote wa taasisi ambayo amekabidhiwa kuisimamia....

      5) Kusahau nafasi ya michezo katika kuleta ajira na kukuza uchumi. Timu zote za daraja la juu (Premier league) la mpira wa miguu zilitakiwa zitengewe fungu la kuanzisha timu za watoto ili kuibua vipaji kama sehemu ya awali ya kuanzia. La ajabu viongozi wetu kila siku huimba soka huendelezwa na timu siyo timu ya taifa lakini ni wagumu kwenye mioyo yao kutoa fedha za shughuli hiyo nyeti katika kukuza vipaji vya michezo, kufufua uchumi na kuwapatia ajira vijana wetu. Kwa kuanzia kila timu iliyoko kwenye Premier league ingelitengewa shilingi milioni 200 kwa mwaka kwa kazi hiyo ya kukuza vipaji vya vijana na fedha hizo CAG lazima akague matumizi yake.
      Haya, huyu Dr. Mgimwa hawezi kuyafikiria kwa sababu ni kizazi kilichopitwa na wakati.

      6) (a) Upendeleo wa misamaha ya kodi zote kutofutwa kwa vigezo ambayo vinakinzana na katiba yetu ya kuondoa aina zote za ubaguzi. Katika hukumu ya KTM {Karibu Textiles Mills} mahakama zote za juu zilisema ni ukiukwaji wa katiba kutoa misamaha ya kodi kwa baadhi ya makampuni tu tena yapo kwenye sekta moja khalafu wengine mkawabagua eti kwa sababu wana mikataba yao na wengineo hawana. Mbali ya ukweli kuwa ubaguzi tajwa unatibua nguvu ya soko lakini la kuzingatiwa ni kuwa katiba iko juu ya mikataba tajwa.
      Nilidhani kama Dr. Mgimwa is the real deal angeliifuta mikataba tajwa kwa kuongozwa na hukumu za KTM ya EAC na ya CAT (TZ COURT OF APPEAL) katika kutenda haki. Lakini kwa vile, Dr. Mgimwa hakuwekwa pale kwa dhamira safi ya kulisaidia taifa bali ni kujibu tu kiu ya aliyemweka ambaye ninaamini ni Peter Mizengo Pinda basi upeo wa kuyaona haya hana na hivyo hana sifa hata moja ya kuwa Waziri kwenye nyadhifa yoyote ile kwenye baraza la mawaziri achilia mbali Wizara ya fedha.

      b) Misamaha ya kodi kwenye mahoteli ya kitalii kanda ya kaskazini haijafutwa ambayo inaigharimu nchi zaidi ya dola 20-70 milioni kwa mwaka. Sasa Dr. Mgimwa alichelewesha bajeti hii kwa nini kama...........it is business as usual, na hata huyo Pinda aliyekuwa akimtetea hivi haoni hata haya?


      What a shame!



      7) Eneo ambalo humgusa mlalahoi moja kwa moja ni eneo la kodi. Kodi ya VAT ya asilimia 18 imesaidia sana katika kufifilisha soko la ajira. Hawa wakubwa wakisha kulamba hela yetu pale hazina hukimbilia kudai haya ni makusanyo ya serikali na kusahau hata siye ambao hatujaajiriwa serikalini nao ni sehemu hiyo hiyo ya serikali. Serikali yoyote ambayo haisikilizi kukua kwa gharama za maisha na uhaba wa vyanzo vya uzalishaji hiyo serikali siyo sikivu hata kama ikidai vinginevyo.

      a) Kwa kuanzia VAT ilipaswa kupunguzwa kutoka asilimia 18 hadi 15 ili kuhamasisha waajiri wakuze soko la ajira na kuongeza ushindani wa bidhaa zetu kwenye soko la dunia. Mapato ya serikali kuyaongeza siyo kuongeza viwango vya kodi tu bali kuwa na kiwango cha kodi ambacho kitahamasisha tija na uzalishaji. Hili tuendelee kulidai kwani ni haki yetu kukataa kuburutwa bila ya siye kutaka katika ufukara wa kujitakia.

      b) VAT ya EWURA na REA, kwenye umeme ni ya kuondoa tena kinatakiwa kiwe kitendo cha haraka sana. Hivi huo umeme wa vijijini hata ukipelekwa ni nani kule atakayeweza kuumudu gharama zake kama hata wakaazi wengi wa mijini naona wamerudishwa kwenye vibatali tu? Kiujumla wakaazi wa mijini wana uwezo wa kumudu gharama za maisha zaidi ya wale wa vijijini na kama mfupa umemshinda mzee fisi je nani atauweza?

      c) Kila Halmashauri ilipaswa kutengewa 7% ya VAT kwenda moja kwa moja kwenye shughuli zao badala ya kutegemea hisani ya serikali kuu au udanganyifu wa mfuko wa jimbo ambao nao ni kituko kwani siyo shirikishi hata chembe. Serikali kuu ingelibaki na 8% ya makusanyo ya VAT kwa minajili ya kusawazisha maeneo ambayo yana mapato madogo na hivyo kuleta maendeleo yenye uwiano mzuri. Mfumo wa mgawanyo uliopo unaipa serikali kuu hususani DSM upendeleo wa kila kitu na hivyo kuacha mikoa ya pembezoni kuwa nyuma sana kimaendeleo. Huu ndiyo mtazamo mpya wa kulikwamua taifa kutoka hapa lilipo hadi kwenda kwenye maendeleo kwa kila mtanzania..................... ...azma ambayo ianaelekea ni tamu wakati wa kuomba kura lakini ni chungu katika kuitekeleza..............

      Hivi huyu Dr. Mgimwa anaelewa nchi hii inatoka wapi, iko wapi na yaelekea wapi? Kama siyo mbabaishaji tu?


      8) Kukwepa kufuta road tolls za magari makubwa. Kila mahali alipokuwa akihalalisha kupanda kwa kodi, Dr. Mgimwa alikuwa anajificha kwenye kichaka cha EAC na sheria zake. Bajeti ya jana ya Kenya wamefuta vizuizi vyote vya barabarani vikiwemo vya tozo za magari makubwa, usafirishaji wa vyakula n.k .......................sasa hayo maigizo ya EAC mbona hayakufika kwenye kufuta road tolls ambazo zinatajirisha watu wachache badala ya kulitajirisha taifa?????????????..........Ku husu uzito wa magari ni udhibiti wa idadi ya matairi ya nyuma la gari au load axles unatosha kabisa kuhakikisha magari yetu hayazidi tani stahiki. Kenya wao lori lenye axles 3 tu ndizo zinaruhusiwa kwenye barabara zao. Sasa ukiisha kulisimamia hilo huu uchafu wa road tolls ambazo zinaongeza mrundikano wa bidhaa na kuchelewesha huduma kwa jamii huku zikimwongezea mlaji gharama zisizorejesheka ni wa nini kama siyo kulinda ajira na ufisadi wa watoto wa vigogo ambao ndiyo wamerundikwa kwenye vituo vya matozo tajwa?

      9) Ukuaji wa deni la taifa Dr. Mgimwa aliuchukulia kimzahamzaha tu na hakuna maelezo ya kutosha kuelezea ni kwa sababu zipi taifa limebebeshwa mzigo wa deni la trilioni 5 tu wakati Mkapa anamkabidhi Jk nchi na khalafu deni hilo lipande khadi trilioni 8 mwaka 2009 na leo lifikie trilioni 22 (Kwa fedha za kitanzania)? Tathmini ya nani alikopa na kwa idhini ya nani inabidi ijulikane sasa na hata CAG sijui yuko wapi kutathmini hilo na badala yake anatumia muda mwingi kuwabana halmashauri ambao mapato yao ni kiduchu. Dr. Mgimwa kama angelikuwa makini angelianzisha sheria ya kuhakikisha bunge ndilo lenye mamlaka ya kupitisha mikopo yote ya serikalini. Hatukumchagua Raisi aende Ikulu kufanya atakavyo bila ya kuwajibika kwa yeyote. Haya madeni yatalipwa na wajukuu zetu na vilembwekazi hata hatujui hizo fedha zilifanya nini na aliyekuwa aziidhinisha alifanya hivyo kwa mashinikizo ya akina nani...........

      10) BOT imekuwa haitazamwi juu ya vyanzo vyake vya mapato na matumizi na imekuwa kinara wa ufisadi ambao hata CAG huwa anaufumbia macho. Wakati umefika mapato na matumizi ya BOT yakawekwa wazi na ile sheria ya kulizuia bunge kudhibiti BOT ikafutwa na kurejesha BOT mikononi mwa udhibiti wa Bunge......................

      Kwa haraka haraka, Dr. Mgimwa ni bomu na tusitishike na kauli zake za kujiamini..mara nyingi matapeli ndivyo walivyo.............na nimpa D minus kwenye maandalizi ya bajeti inayomjali mnyonge....................... ........have your say too.

      Last edited by Rutashubanyuma; 17th June 2012 at 12:21. Reason: spelling, additional points
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    2. Miaka 50

    3. #21
      thatha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2011
      Posts : 5,034
      Rep Power : 0
      Likes Received
      227
      Likes Given
      1

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Nimeipenda bajeti kwa kurudisha JKT kisheria,vijana sasa tutapata nafasi ya kutoka

    4. #22
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      In fact, nowhere where I see this government has any plans to the poor of this country rather to make life more difficult. Taxes we pay is very much still has been just words. No politician now is concentrate on this. very heartening.
      Rogi I agree entirely with your views.............so long as our politicians across the political divide fill their bellies we do not matter.......................i t is time we remind them we do matter...........
      Rogie likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    5. #23
      Mtambuzi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 29th October 2008
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 6,094
      Rep Power : 27014
      Likes Received
      8231
      Likes Given
      17325

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Mie bora nakula kaugali kangu na kujishibia, sitaki presha za bajeti hii ambayo hata sijaelewa itanisaidia vipi
      Freedom is coming tomorrow (2015)

    6. #24
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Nimeipenda bajeti kwa kurudisha JKT kisheria,vijana sasa tutapata nafasi ya kutoka
      @ kutoka uende wapi......kijijini?
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    7. #25
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Mie bora nakula kaugali kangu na kujishibia, sitaki presha za bajeti hii ambayo hata sijaelewa itanisaidia vipi
      Freedom is coming tomorrow (2015)
      @ni mpaka siku vibaka watakapokutembelea na kukukatakata bila huruma kwa kukudai hata huo ugali ulipaswa uwagawie ndipo utakapojua kuwa ubinafsi wako na uvivu wako siyo suluhisho ila ni adha nyingine umejisogezea.........
      NARE likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    8. RukaaJuu Final

    9. #26
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Mkuu usikate tamaa kwa hilo, katika 100 utakaowapigia kelele utavuna angalau samaki wakuridhisha, wengine ndo hivyo tena.
      @ uko sahihi..........Kongosho anatakiwa kutokata tamaa matunda ya mapambano siyo siku moja tu................
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    10. #27
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      ... Mbowe, Lipumba, Mbatia walia Send to a friend
      Thursday, 14 June 2012 21:59
      0digg

      Baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini na wageni waalikwa, wakipitia kitabu cha hotuba ya bajeti ya Serikali katika mwaka ujao wa fedha, wakati Waziri wa Fedha na Uchumi Dk William Mgimwa alipokuwa akiwasilisha bajeti hiyo jana mjini Dodoma. Picha na Edwin Mjwahuzi

      Neville Meena na Mussa Juma, Dodoma
      WENYEVITI wa vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi na CUF wameiponda Bajeti ya Serikali ya mwaka wa fedha 2012/2013 iliyowasilishwa bungeni jana na Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa wakisema imeongeza mzigo kwa walipa kodi kutokana na gharama kubwa za uendeshaji wa Serikali.Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kuwasilishwa kwa bajeti hiyo jana, wenyeviti hao walisema hakuna matumaini kwa Watanzania kupitia Bajeti hiyo kwani fedha nyingi zimerundikwa kuwanufaisha wachache huku umma ukiambulia patupu.
      Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema: “Hakuna mkataba wa makusudi wa kupunguza matumizi ya Serikali, ahadi yake ya kupunguza matumizi kwa kupunguza posho zisizo na tija na matumizi mengine haikutekelezwa.”
      Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema ameshangazwa na kutokuwapo kwa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma na badala yake fedha nyingi kurundikwa katika matumizi ya kawaida ya Serikali.
      “Mfumo wa kodi kama mlivyosikia ni mbaya kabisa, hakuna kinachoashiria kwamba mkulima wa kawaida atapunguziwa mzigo na badala yake wanaendelea kuwanufaisha wafanyabiashara wa vyakula kwa kuwaruhusu kuagiza vyakula nje bila kodi, hiki naweza kusema ni kichekesho,” alisema Mbowe na kuongeza:
      “Hakuna ubunifu kwenye kupanua wigo wa kodi, tungeweza kusikia katika construction (sekta ya ujenzi) ambayo inakua haraka na inachukua asilimia 18 ya Pato la Taifa kwamba tungetoza kodi huko, lakini badala yake ni yaleyale ya siku zote, kodi kwenye sigara, vinywaji na bia.”
      Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema matatizo makubwa katika bajeti hiyo ni kutengwa kwa fedha kidogo za maendeleo na kwamba kinachoshangaza ni Serikali kushindwa hata kugharimia matumizi ya kawaida.
      “Utawala unagharimiwa kwa Sh10 trilioni hali uwezo wa kukusanya mapato ya ndani ni Sh8 trilioni, hii inamaanisha kwamba Serikali yetu pia inatumia fedha za wahisani kugharimia matumizi ya kawaida,” alisema Profesa Lipumba ambaye pia ni mtaalamu wa uchumi.
      Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alisema Serikali lazima ijifunze kubadilika kwani kilichotangazwa jana kwenye Bajeti yake ni marudio ya miaka yote.
      “Huwezi kuchukua fedha zote ukaurundikia utawala halafu ukawaacha wananchi bila kitu, hicho ndicho tulichokiona leo, Sh10 trilioni ni kwa ajili ya mishahara na watumishi na matumizi ya kawaida, maendeleo ambako ndiko wananchi waliko kumeachwa tena kutegemea fedha za wafadhili,” alisema Mbatia.
      Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu alisema, Bajeti hiyo haitatekelezeka... “Mwaka jana wamekuja na Bajeti kama hii ya kutegemea fedha za wafadhili, zaidi ya asilimia 40 ya fedha zilizotengwa hazikupatikana na leo wanakuja na bajeti ya aina ileile,” alisema Lissu.
      Mbunge wa Ngorongoro (CCM) Saning’o Ole Telele, alisema Bajeti hiyo ni pigo kubwa kwa wafugaji kwani wameshindwa kutengewa fedha kwa ajili ya kuboresha ufugaji hasa wale ambao wanahamahama.
      Hoja hiyo ya Telele, iliungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Rose Kamili ambaye alisema Bajeti ya mwaka huu, badala ya kuongeza fedha kusaidia wafugaji hasa wa asili ambao wanatangatanga, imeendelea kupunguza fedha za wizara hiyo.
      Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka alisema Bajeti hiyo kama zilivyo nyingine, imeendelea kujikita katika kuongeza kodi katika bidhaa zilezile kila mwaka.
      Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Ester Bulaya alisema Bajeti hiyo ni nzuri akipongeza mkakati wa ukarabati mkubwa wa Reli ya Kati.
      Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Cecilia Paresso alisema, Bajeti ya mwaka 2012/13 kama alivyoisikiliza imeendelea kukosa ubunifu wa vyanzo vipya vya mapato na hivyo kuongeza makusanyo ya ndani.

      Wadau wengine
      Rais Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema fedha zilizotengwa kwenye Wizara ya Elimu ni ndogo kiasi cha kutoweza kukidhi mahitaji ya walimu na kueleza kuwa hiyo itaendeleza migogoro.
      “Kwa kweli ni kiasi kidogo sana, tena imetuvunja nguvu, kwa sababu tulitegemea wafanyakazi tutapewa kipaumbele kwenye Bajeti, lakini kilichotokea ni tofauti kabisa,” alisema Mukoba.
      Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba alisema Bajeti ya mwaka huu imeendelea kuwa yenye manufaa kwa viongozi wa Serikali na kuwaumiza wananchi wa hali ya chini.
      Alisema haiwezekani Bajeti ya mwaka 2006/7 ikawa zaidi ya Sh4 trilioni halafu ya mwaka 2012/13 ikafika Sh15.2 trilioni na bado ikawa ina manufaa kwa wananchi.
      Mkurugenzi Mkuu wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellein Kijo-Bisimba alisema Bajeti imeegemea upande mmoja wa Serikali badala ya kuwa upande wa wananchi.
      Dk Bisimba alisema haiwezekani kodi ya huduma ya simu ikapandishwa na kulingana na nchi za Afrika Mashariki bila kujali kwamba itawaumiza watumiaji wa hali ya chini.
      Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari za Wanawake (Tamwa), Ananilea Nkya alisema Bajeti haina kipaumbele kwa huduma za kijamii na imejikita kwenye masuala ya anasa.
      Mchumi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Haji Semboja alisema Bajeti ya mwaka huu haina tofauti na zilizowahi kutolewa.
      Alisema kutokana na ukweli kuwa Bajeti ya mwaka jana haikuwa na ufanisi, ilitegemewa mwaka huu kusikia maelezo ya kina yakifafanua sababu za kutofanya vizuri kwa Bajeti ya mwaka jana, jambo ambalo halikufanyika.
      Alisema hata ongezeko la trilioni mbili kwa Bajeti ya 2012/13 ikilinganishwa na iliyopita, siyo jambo geni kwani limekuwa likifanyika mara kadhaa lakini ufanisi wake hauonekani.
      Nyongeza na Habari hii imeandikwa na Patricia Kimelemeta, Ibrahim Yamola, Dar; Salim Mohammed, Tanga; Joseph Lyimo, Manyara na Peter Saramba, Arusha.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    11. #28
      Kituko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th January 2009
      Posts : 3,712
      Rep Power : 1287
      Likes Received
      495
      Likes Given
      174

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Kilichonisikitisha, hii bajeti imeegemea kwa watu wa miji mikubwa tu, ni bajeti ya watu wa mijini, wala haikumfikiria mtu wa kijijini kabisa,
      Unapozungumzia gari kuwa na jina la mmiliki hilo sijuhi lina faida gani kwa mtu wa kijijini, hata kama ni jambo linaloliletea mapato serikali basi lisingekuwa kwenye bajeti kuu,

      Unaposema magari yanayozidi umri wa miaka kumi ushuru uwe 20%, hiyo ni kumuua mtu wa chini kabisa, usafiri wote wa mijini na vijijini unategemea magari ya mitumba yenye huo umri, MAlori almost yote yanayoangaika kubeba mizigo na watu Vijijini yana kuja Tanzania yakiwa na umri wa Zaidi ya miaka kumi, ingekuwa inamaana kama ingesemwa magari ya starehe tu ndio yaingie kwenye hiyo kodi, lakini magari yanayohusika na public yabaki ama kupunguzwa kodi yake

    12. #29
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Huku sipapendi maana watu wanapiga makelele afu kura hawapigi, Wizi mtupu
      Tunapandishana mori afu wanakimbia vitani, ya nini wanitoe na kitaulo ndani?

      PAYE inanifanya hata biya sinywi tena
      Kongosho kumbuka hata Nyerere hakufanikiwa siku moja alichezeshwa kwata na baadaye alifanikiwa..silaha yake ilikuwa ni aluta continue........mapambano bado yanaendelea
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    13. #30
      Ndinani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2010
      Posts : 2,950
      Rep Power : 1532
      Likes Received
      745
      Likes Given
      237

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Serikali haiko makini kujua challenges inazokabiliana nazo na jinsi ya kuzipa umuhimu wake na kuzikabili vilivyo. Challenges ambazo serikali inatakiwa kuzipa kipaumbele sio kwa maneno tu na kuzitengea fedha bali kuhakikisha kuwa fedha zinazotengewa zinafanya kazi tarajiwa!! Changamoto za kuzifanyia kazi haraka kabla bya madhara kuikumba nchi ni mfumuko wa bei[ Inflation] na ajira kwa vijana inayokua by leaps and bounds. Reli ya kati ni lazima itengenezwe na kuwe na injini na mabehewa ya kutosha ili mizigo ya aina yote vikiwemo vyakula na mafuta yapelekwe kwa reli upcountry badala ya malori hivyo kupunguza gharama za uzalishaji viwandani na mashambani na pia kupunguza gharama za road maintenance na ajali za magari barabarani. Kuanzisha commuter train services toka ubungo maziwa mpaka stesheni hakuwezi kupunguza gharama za uzalishaji viwandani na mashambani. Serikali haina budi kupunguza matumizi yake hasa kuhsu magari ya serikali; na fungu litakalopatikana kutumika kuwasaidia vijana wanaotoka vyuoni na wanafeasible ideas za kuanzisha start-up companies za kujiajiri. Vijana wengi wana good ideas lakini hawana start up capital. Serikali lazima itenge mfuko wa kuweza kuwasaidia hawa vijana ili waweze kukidhi matakwa yao ama sivyo machafuko yatatokea nchini!!
      Rutashubanyuma likes this.

    14. #31
      Crashwise's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Location : Safarini
      Posts : 13,127
      Rep Power : 14289
      Likes Received
      4015
      Likes Given
      3273

      Default

      Quote By Kongosho
      Mmmmmh, jukwaa la presha.
      rudi zako MMU huku ni maumivu mwanzo mwisho
      Rutashubanyuma likes this.

    15. #32
      Rogie's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 22nd November 2010
      Location : Darul Islamia
      Posts : 1,917
      Rep Power : 1146
      Likes Received
      485
      Likes Given
      334

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Quote By Rutashubanyuma
      Rogi I agree entirely with your views.............so long as our politicians across the political divide fill their bellies we do not matter.......................i t is time we remind them we do matter...........

      Rutashubanyuma. Its the time now we decide to make changes that shall redeem the theft of these politicians ..we have to decide for our own future..this is our country...
      Rutashubanyuma likes this.
      "You have your people,and I have mine"
      [email protected]

    16. #33
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,140
      Rep Power : 606
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Tatizo lako Ruta unaweka matumaini kwa marehemu! hatakusaidia kitu.
      Rutashubanyuma likes this.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    17. #34
      Mbalamwezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th September 2007
      Posts : 701
      Rep Power : 739
      Likes Received
      71
      Likes Given
      134

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Ruta,
      Unaweza kuwa na point kidogo kwenye hoja zako. Lakini ni vema ukajizuia kwa kuweka nguvu nyingi kumsema waziri kama mtu binafsi, kama vile anatengeneza bajeti hii chumbani kwake na mkewe.

      Utatusaidia sana watu kama mimi kama utakuwa unakosoa na kuweka wazo mbadala. Mambo mengine umeweka sana emotions zako bila kutafuta ukweli halisi.

      Mfano, unapoweka magari yanayozidi miaka nane pamoja na mitambo ya barabara, uko sahihi? Hata trekta tu linatifautiana sana na gari na hivyo kodi ni tofauti.

      Weka arguments, na siyo kuuliza waziri ni mradi wa nani. Ni waziri gani wa fedha alikufurahisha wewe na kwa bajeti ipi?
      Nasolwa and Rutashubanyuma like this.

    18. #35
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Serikali haiko makini kujua challenges inazokabiliana nazo na jinsi ya kuzipa umuhimu wake na kuzikabili vilivyo. Challenges ambazo serikali inatakiwa kuzipa kipaumbele sio kwa maneno tu na kuzitengea fedha bali kuhakikisha kuwa fedha zinazotengewa zinafanya kazi tarajiwa!! Changamoto za kuzifanyia kazi haraka kabla bya madhara kuikumba nchi ni mfumuko wa bei[ Inflation] na ajira kwa vijana inayokua by leaps and bounds. Reli ya kati ni lazima itengenezwe na kuwe na injini na mabehewa ya kutosha ili mizigo ya aina yote vikiwemo vyakula na mafuta yapelekwe kwa reli upcountry badala ya malori hivyo kupunguza gharama za uzalishaji viwandani na mashambani na pia kupunguza gharama za road maintenance na ajali za magari barabarani. Kuanzisha commuter train services toka ubungo maziwa mpaka stesheni hakuwezi kupunguza gharama za uzalishaji viwandani na mashambani. Serikali haina budi kupunguza matumizi yake hasa kuhsu magari ya serikali; na fungu litakalopatikana kutumika kuwasaidia vijana wanaotoka vyuoni na wanafeasible ideas za kuanzisha start-up companies za kujiajiri. Vijana wengi wana good ideas lakini hawana start up capital. Serikali lazima itenge mfuko wa kuweza kuwasaidia hawa vijana ili waweze kukidhi matakwa yao ama sivyo machafuko yatatokea nchini!!
      Nd

      Ndinani tatizo ni kuwa siyo bajeti shirikishi na ndiyo maana tunaiita ni bajeti ya viongozi pekee yao.,.......................wa nafikiri wakishiba nasi tumeshiba..................... tatizo wakiachia ushuzi siye hatuna cha kuachia matumbo yetu ni njaa kali sana.............
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    19. #36
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Ruta,
      Unaweza kuwa na point kidogo kwenye hoja zako. Lakini ni vema ukajizuia kwa kuweka nguvu nyingi kumsema waziri kama mtu binafsi, kama vile anatengeneza bajeti hii chumbani kwake na mkewe.

      Utatusaidia sana watu kama mimi kama utakuwa unakosoa na kuweka wazo mbadala. Mambo mengine umeweka sana emotions zako bila kutafuta ukweli halisi.

      Mfano, unapoweka magari yanayozidi miaka nane pamoja na mitambo ya barabara, uko sahihi? Hata trekta tu linatifautiana sana na gari na hivyo kodi ni tofauti.

      Weka arguments, na siyo kuuliza waziri ni mradi wa nani. Ni waziri gani wa fedha alikufurahisha wewe na kwa bajeti ipi?
      Mbalamwezi acha kusoma kwa kurukaruka...................m izengo pinda ndiye mlengwa na hii mada baada ya kudai ya kuwa bajeti imechelewa kwa matakwa ya Waziri ambaye ni mpya na anahitaji muda kuifumua kuona kama itagusa vipa umbele vyake......................... .............hilo pekee linatosha kuchunguza kama hayo yametekelezwa..............hoj a zangu binafsi nimuhimu kama raia kujaribu kubainisha chanzo cha huyu mbambaishaji kinaanzia wapi na nani mnufaikaji kama mlaji katelekezwa?
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    20. #37
      sanga malua's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Posts : 226
      Rep Power : 420
      Likes Received
      46
      Likes Given
      54

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Nadhani mleta hoia huna hoja.kusema dr hana jipya siyo kweli kwani anataka kutumia ulimbukeni wa watanzania kuiingizia nchi fedha kupitia hizo namba za magari.halafu ulitaka nafasi hiyo awe nani ndio uridhike? bajeti yenye mwelekeo wa kutaka watu wawajibike zaidi na yenye wigo mpana wa kodi ni nzuri ingawa tumezoea kuwa kuanzia sasa elimu bure halafu usipate bure,afya bure hala ukienda dawa hupati!KODI ZAIDI MAENDELEO ZAIDI

    21. #38
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Tatizo lako Ruta unaweka matumaini kwa marehemu! hatakusaidia kitu.
      Kyaiyembe tatizo siyo ni chama gani kipo madarakani bali ni matatizo ya kimfumo ya upatikanaji wa viongozi bora...............tuzame kubadili mfumo mzima wa uendeshaji wa nchi na hawa wababaishaji watakuwa ni historia......
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    22. #39
      TIQO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2011
      Posts : 4,591
      Rep Power : 6851
      Likes Received
      1037
      Likes Given
      131

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Ngoja tuone
      Mwisho wa Ubaya Aibu.

    23. #40
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,733
      Rep Power : 12925
      Likes Received
      4432
      Likes Given
      7462

      Default Re: Ni nani alishinikiza uteuzi wa Dr. William Mgimwa kuwa waziri wa fedha?

      Nadhani mleta hoia huna hoja.kusema dr hana jipya siyo kweli kwani anataka kutumia ulimbukeni wa watanzania kuiingizia nchi fedha kupitia hizo namba za magari.halafu ulitaka nafasi hiyo awe nani ndio uridhike? bajeti yenye mwelekeo wa kutaka watu wawajibike zaidi na yenye wigo mpana wa kodi ni nzuri ingawa tumezoea kuwa kuanzia sasa elimu bure halafu usipate bure,afya bure hala ukienda dawa hupati!KODI ZAIDI MAENDELEO ZAIDI
      @ hata kama huyu umeamua kumtetea unajua bajeti ni trilioni 15 na matarajio yake kwa mwaka huu hizo namba zitaingiza shilingi milioni 50 ambaye ni chini ya silimia 0 katika uwiano wa bajeti...................na hata kulipia mshahara wake kwa mwaka hayo mapato hayatoshi kwa hiyo ni ubabaishaji kumrundikia misifa hapo bali anafaa kuumbuliwa tu.........
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    Page 2 of 9 FirstFirst 1234 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...