Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 38
    1. #1
      mwananchi wa kawaida's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th February 2012
      Posts : 55
      Rep Power : 378
      Likes Received
      12
      Likes Given
      8

      Default Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

      Jamani watanzani wenzangu hivi hii bajeti ya matumizi 70% na uzalishaji 30% inatupeleka kwema kwel?

    2. Miaka 50

    3. #2
      Endangered's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 22nd September 2011
      Location : Orbit
      Posts : 899
      Rep Power : 396
      Likes Received
      190
      Likes Given
      962

      Default Re: Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

      Nimeduwazwa pia, of all the money pesa za maendeleo ni only 30 percent.Tanzania ina mengi ya kushangaa, na machache ya kujivunia.
      "No matter how busy you may think you are, you must find time for reading, or surrender yourself to self-chosen ignorance" Confucius (551-479 BC)

    4. #3
      MKONGWE 12.com's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th May 2012
      Posts : 15
      Rep Power : 354
      Likes Received
      7
      Likes Given
      16

      Default Re: Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

      Mkuu unashangaa hii ya leo? zilizopita pia zilikuwa hivyo, mbali na misaada tunakwenda ki Mungu Mungu!!
      NAKAMO likes this.

    5. #4
      dosama's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th December 2010
      Posts : 736
      Rep Power : 573
      Likes Received
      296
      Likes Given
      1

      Default Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Mussa Juma, Dodoma
      SERIKALI jana ilitangaza Bajeti ya Sh15trilioni kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ambayo pamoja na mambo mengine, imelenga kudhibiti mfumuko wa bei kwa kutangaza kutoa vibali vya kuingiza chakula kutoka nje, huku ikiwabana matajiri kwa kuongeza kodi ya bidhaa zisizokuwa za lazima.

      Akisoma bajeti hiyo bungeni Dodoma jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alitangaza pia kwamba Serikali imepanua wigo wa Kodi ya Mishahara (Paye) na sasa itawagusa wafanyakazi wenye kipato cha kuanzia Sh170,000 badala ya Sh135,000 ya awali, huku ikirejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kutenga Sh7 bilioni kwa ajili ya kuchukua vijana 5,000.

      Dk Mgimwa katika Bajeti hiyo pia alitangaza ongezeko la kodi za bidhaa mbalimbali, ikiwamo, bia, soda, sigara, juisi zinazoingizwa kutoka nje huku ikifuta msamaha wa ushuru wa bidhaa kwa magari kwa wote waliokuwa wananufaika na msamaha huo.

      Alifafanua kwamba kodi ya vinywaji baridi imepanda kutoka Sh69 kwa lita hadi Sh83 na mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75, imeshuka kutoka Sh425 kwa lita hadi 145 kwa lita.

      Kodi ya mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, imepanda kutoka Sh1,345 kwa lita hadi 1,614 kwa lita.

      Alisema kodi ya vinywaji vikali imepanda kutoka Sh1,993 kwa lita hadi Sh2,392 kwa lita, bia inayotengenezwa nchini kwa nafaka na ambayo haijaoteshwa, kodi yake imepanda kutoka Sh248 kwa lita hadi Sh310 kwa lita. Bia nyingine zote kodi imepanda kutoka Sh420 hadi Sh525 kwa lita.

      Akizungumzia marekebisho ya ushuru kwenye bidhaa za sigara, Dk Mgimwa alisema zote zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kwa tumbaku inayozalishwa nchini, kiwango cha angalau asilimia 75, kodi imepanda kutoka Sh6,820 hadi Sh 8,210 kwa sigara 1,000.

      Alisema Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kwa tumbaku inayopatikana nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kodi imepanda kutoka Sh16,114 hadi Sh19,410 na sigara nyingine zenye sifa tofauti na makundi hayo, kodi imepanda kutoka Sh29,264 hadi Sh35,117 kwa sigara 1,000.

      Alisema tumbaku ambayo ipo tayari kutengenezwa sigara (cut filler) kodi yake imepanda kutoka Sh14,780 hadi Sh17,736 kwa bunda la sigara 1,000 wakati ushuru wa cigars unabaki kuwa asilimia 30.

      Gharama za simu juu
      Katika bajeti hiyo, Waziri Dk Mgimwa alisema muda wa maongezi (airtime) kwenye simu za mkononi umeongezeka kutoka asilimia 10 hadi 12.

      Alisema lengo la hatua hiyo ni kuoanisha ushuru wa bidhaa unaotozwa na huduma hiyo katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), kwa kipindi hiki ambacho nchi zipo katika Soko la Pamoja.
      Alisema hatua hizo za ongezeko la ushuru wa bidhaa kwa pamoja, zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh144,054.9 milioni.

      Misamaha ya kodi ya magari

      Waziri huyo alipendekeza kufanyika marekebisho kwenye sheria husika za kodi ya matangazo ya Serikali yanayotoa msamaha wa kodi kwenye magari kwa walengwa mbalimbali ili kuweka ukomo wa umri wa miaka minane kwa magari hayo badala ya miaka 10.

      Alisema magari yenye umri wa zaidi ya miaka minane yatatozwa ushuru wa bidhaa wa asilimia 20. Lengo la hatua hiyo ni kupunguza wimbi la uingizaji magari chakavu na kulinda mazingira.
      Alitangaza pia marekebisho katika ushuru wa forodha, ikiwemo kufuta msamaha wa ushuru wa forodha katika vitu mbalimbali vikiwemo magari yenye ujazo wa CC 3000 huku pia ushuru wa forodha ukifutwa katika bidhaa nyingine nyingi muhimu.

      Alisema katika kuhamasisha na kuchochea ukuaji wa sekta ya ufugaji wa nyuki, vifaa vinavyotumika katika ufugaji na kurina asali vimepewa msamaha wa ushuru wa forodha vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi na wafugaji wa nyuki.

      Alisema msamaha wa ushuru wa forodha kwenye migahawa ya majeshi ya ulinzi utaendelea kutolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
      Alisema kumefanyika marekebisho katika Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ya mwaka 2004 ili kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwa wazalishaji wa vyakula vinavyotengenezwa mahsusi kwa lishe ya watoto wenye utapiamlo na watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

      Alisema kuwa katika Bajeti hiyo, pia wametoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi zinazotumika katika kutengeneza vifaa vya kufanyia uchunguzi wa magonjwa (medical diognastic kits) kwa kuwa vifaa hivyo hutozwa asilimia sifuri vinapoagizwa kutoka nje ya nchi.

      Katika marekebisho hayo, utatolewa msamaha kwenye mitambo (machinery) na vipuri vyake vinavyotumika kwenye uchimbaji wa madini lakini hautahusisha vipuri vya magari vitakavyoagizwa na makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini.

      Katika bajeti hiyo, pia umetolewa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyuma vinavyowekwa kwenye kingo za barabara na lengo lake ni kutoa unafuu katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

      Alisema ushuru wa forodha umepunguzwa kwa ving’amuzi kutoka asilimia 25 hadi asilimia sifuri ili kuwezesha mabadiliko katika teknolojia ya analogia na kwenda katika teknologia ya digitali.

      Alisema katika Bajeti hiyo, pia ushuru wa ngano umeondolewa kuwa asilimia 0 badala ya asilimia 35
      Alisema Serikali pia imesamehe VAT katika mashine za kutolea stakabadhi (electronic fiscal devices), ili kupunguza bei yake na kuwezesha wafanyabiashara wengi kuwa nazo, kuhamasisha matumizi yake na hivyo, kuongeza mapato ya Serikali.

      Katika eneo hilo, Serikali imeondoa VAT kwa vifaa mbalimbali vya kuhifadhia, kusafirisha na kusambaza gesi asilia ili kuongeza matumizi ya nishati hiyo katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kwenye magari, majumbani na viwandani.

      Kodi kwa wafanyabiashara
      Wafanyabiashara ambao mapato yao hayazidi Sh3,000,000 hawatalipa kodi kuanzia Julai Mosi, mwaka huu. Dk Mgimwa alisema mpango huo umefanywa kulinda mapato ya Serikali.

      Kabla ya msamaha huo, wafanyabiashara hao ambao mapato yao hayazidi Sh3,000,000 walikuwa wanalipa Sh35,000.

      Marekebisho mengine ya kodi ya mapato ni kuwa wenye mapato kati ya Sh3 milioni –Sh7.5 milioni watalipa Sh100,000 badala ya Sh95,000.

      Malengo ya Bajeti
      Waziri Mgimwa alisema Bajeti hiyo imejielekeza katika Kukuza Pato la Taifa kwa asilimia 6.8 mwaka 2012 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.4 mwaka 2011.

      Malengo mengine ni kuimarisha miundombinu ya uchumi, ikijumuisha umeme, barabara, reli na bandari, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongezeka kwa mapato ya ndani yatakayofikia uwiano na Pato la Taifa wa asilimia 18 kwa mwaka 2012/13 kulinganisha na mwelekeo wa asilimia 16.9 mwaka 2011/12.

      Dk Mgimwa alitaja malengo mengine kuwa ni pamoja na kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei ili urudi kwenye viwango vya tarakimu moja na kuwa na kiwango tengemavu cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha.

      Malengo mengine ni kukuza mikopo kwa sekta binafsi kwa kiwango cha asilimia 20 ya Pato la Taifa ifikapo mwishoni mwa Juni 2013, sambamba na jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei, kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo na wa kati, kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta za huduma za jamii, kuimarisha utawala bora na uwajibikaji na kujenga uwezo wa nchi kukabiliana na misukosuko ya kiuchumi na kifedha pamoja na kushiriki kwa ufanisi katika ushirikiano kikanda na kimataifa.

      Matumizi ya Maendeleo
      Kuhusu matumizi ya maendeleo, Waziri Mgimwa alisema itazingatia vipaumbele vya miundombinu ya umeme - mkazo ukiwa upatikanaji wake kwa kuongeza uzalishaji, usafirishaji na usambazaji na jumla Sh498.9 bilioni zimetengwa.

      Serikali pia itatekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa mkopo kutoka Benki ya Exim ya China wenye thamani ya Dola za Marekani 1.2 milioni utakaosimamiwa na TPDC.
      Kuhusu usafirishaji na uchukuzi, alisema mkazo katika sekta hiyo utakuwa ni kuimarisha reli ya kati ikijumuisha ukarabati wa injini na mabehewa ya treni.

      “Kwa upande wa barabara, miradi inayopewa kipaumbele ni pamoja na barabara zenye kufungua fursa za kiuchumi. Katika usafiri wa anga na majini, miradi itakayotekelezwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege na uendelezaji wa gati ya Ziwa Tanganyika. Jumla ya Sh 1,382.9 bilioni zimetengwa katika eneo hili,” alisema.

      Kuhusu maji safi na salama, alisema lengo ni - kuongeza upatikanaji wake mijini na vijijini na kwamba kiasi cha Sh568.8 bilioni kimetengwa.

      Kwa upande wa kilimo, uvuvi na ufugaji alisema katika sekta hizo, Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi itawekeza katika kilimo cha mpunga na miwa katika mabonde makuu ya Wami, Ruvu, Kilombero na Malagarasi pamoja na kuongeza tija na thamani, kubadilisha mfumo wa kilimo na kukuza kilimo cha misitu.

      Kuhusu kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula pamoja na kuhakikisha uhakika wa chakula, Serikali itaimarisha utekelezaji wa dhana ya Kilimo Kwanza kwa kuhakikisha nguzo zake zote zinaendelea kuzingatiwa.

      Alisema mikoa inatakiwa kuendelea kutenga ardhi na vijiji kutakiwa kupima na kurasimisha ardhi kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na wa nje na kwamba kiasi cha Sh192.2 bilioni kimetengwa katika eneo hilo.

      Ikizungumzia maendeleo ya viwanda, alisema Serikali inakusudia kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini; viwanda vinavyoongeza thamani ya madini; viwanda vikubwa vya saruji na viwanda vya eletroniki na Tehama pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji mijini na vijijini na kukuza ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.


      Concern

      Wakina Barick mbona hawaguswi ila TBL na Coca kina Azam, sigara kila mwaka kwanini serikali yetu tunaenda wapiiii????
      Ndahani and kupelwa like this.

    6. #5
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,690
      Rep Power : 902
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default Re: Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

      agrrrrrr,015 ifike tu wasepe hawa!ngoja nisubiri bajeti ya upinzani itanipa moyo!

    7. Study Abroad

    8. #6
      mikonomiwili's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th January 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 446
      Likes Received
      27
      Likes Given
      199

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Wale wanao sema pombe nishetani waone serikali inavyo itegeme pombe na kama hakuna pombe serikali haina mapato.

      hi inamaana kama watu wana ipenda serikali yao na kama wanataka ipate mapato mengi basi kila mwananchi anywe angalau bia mbili kilasiku

      huo ndo uelewa wa serikali tulio nayo wala sishangai
      seniorgeek likes this.

    9. MKL
      #7
      MKL's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd March 2012
      Posts : 96
      Rep Power : 541
      Likes Received
      62
      Likes Given
      6

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Wanmaojiita walokole, Uamsho na woote wanaoamini kuwa matumizi ya pombe ni haramu oneni serikali yetu invyowatumikia kupitia mapato ya Kilaji... sasa mwombeni mungu sana wote tuwe walokole muone serikali hii itavyo miminika ardhini kama maji ya mto.
      seniorgeek likes this.

    10. #8
      Maundumula's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Posts : 4,896
      Rep Power : 3090
      Likes Received
      1324
      Likes Given
      5608

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Pombe inalipa kuliko dhahabu

      Kama wewe mtumishi wa umma inabidi uwe na heshima sana na viwanda vya pombe hehehe
      Ndahani likes this.

    11. #9
      MPAMBANAJI.COM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2011
      Location : IN THE PLANNET
      Posts : 381
      Rep Power : 492
      Likes Received
      117
      Likes Given
      105

      Post Serikali iwe makini na jkt-bajeti mpya

      Naipongeza Seikali kwa hatua yake yakuendeleza JKT kwa lengo kusudiwa.Ila lazima kuwa makini na mafunzo kwa kuhakikisha ya kuwa kazi zitapatikana baada ya mafunzo.Ongezeko la ukosefu wa ajira kwa watakopata mafunzo hayo linaweza kuleta chaors katika jamii.i.e the JKT output must be stimulated by increase in new employment opportunities for friendly sustainable effects, out of that the trained outputs may have some characters to destruct peace and order with Tanzania motiveated by military technics. New employment opportunities must therefore be available to absorve the trained ones.



      Hili ni wazo langu kutokana na bajeti ya Jana.
      Am not sure if all Leaders knows everything and therefore am a Leader of Myself.

    12. #10
      Komeo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2011
      Location : Mlangoni
      Posts : 904
      Rep Power : 587
      Likes Received
      338
      Likes Given
      106

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Inakera sana tunaposhupalia vitu vidogo vidogo wanavyotumia walalahoi, na kuviacha holela vitu vikubwa kama madini ambako ndiko kwenye fedha nyingi. Hatujifunzi kutoka Botswana, Sauzi, na Ghana ambako madini ndiyo yenye mchango wa msingi wa uchumi, vingine wanajazia tu.
      LIWALO NA LIWE - PINDA.

    13. #11
      charminglady's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 16th April 2012
      Posts : 8,817
      Rep Power : 17522
      Likes Received
      4859
      Likes Given
      5183

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      poor country!

      “You can get a thousand "no's" from people, and only one "yes" from God.”

    14. #12
      idawa's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,516
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1205
      Likes Given
      454

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      idumu TBL kwa maendeleo ya tanzania.!

    15. #13
      dav22's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 585
      Rep Power : 482
      Likes Received
      41
      Likes Given
      25

      Default Re: Serikali iwe makini na jkt-bajeti mpya

      kweli kabisa aisee

    16. #14
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,435
      Rep Power : 19775
      Likes Received
      4279
      Likes Given
      906

      Default Re: Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

      Huu ni uwendawazimu

    17. #15
      Samkyjr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st March 2011
      Posts : 319
      Rep Power : 476
      Likes Received
      40
      Likes Given
      20

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Mimi nilitaka kuona kiasi fulani cha fedha kimetengwa rasmi kiwekezwe kufufua mashamba ya mpunga kama kapunga rice au kufungua mashamba makubwa ya mahindi kwenye mapori makubwa iringa au mbeya ili kutengeneza ajira kuliko kutoa vibali kwa wafanyabiashara kama kawaida yao kuingiza vyakula vibovu. Kwa mfano wangetenga fedha kwa ajiri ya kujenga mfereji wa maji toka ziwa Nyasa ambao ungesaidia wakula katika umwagiliaji ili wasitegemee mvua.

    18. #16
      Prisoner 46664's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th December 2010
      Posts : 1,119
      Rep Power : 650
      Likes Received
      593
      Likes Given
      1562

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Kilimo kimetendewa 192 billion ikilinganishwa na 760 billion kwenye bajeti ya 2011/12-halafu tunasema tunapambana na mfumuko wa bei wakati chanzo chake kikubwa ni kupanda kwa bei ya vyakula...je tumefikiria vizuri??

    19. #17
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By mikonomiwili
      Wale wanao sema pombe nishetani waone serikali inavyo itegeme pombe na kama hakuna pombe serikali haina mapato.

      hi inamaana kama watu wana ipenda serikali yao na kama wanataka ipate mapato mengi basi kila mwananchi anywe angalau bia mbili kilasiku

      huo ndo uelewa wa serikali tulio nayo wala sishangai
      astaghfilulah

    20. #18
      Bajabiri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st December 2010
      Posts : 9,741
      Rep Power : 2884
      Likes Received
      1115
      Likes Given
      52

      Default

      Quote By Prisoner 46664
      Kilimo kimetendewa 192 billion ikilinganishwa na 760 billion kwenye bajeti ya 2011/12-halafu tunasema tunapambana na mfumuko wa bei wakati chanzo chake kikubwa ni kupanda kwa bei ya vyakula...je tumefikiria vizuri??
      ulihusika kuitengeneza???

    21. #19
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,645
      Rep Power : 4015
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Quote By Maundumula
      Pombe inalipa kuliko dhahabu

      Kama wewe mtumishi wa umma inabidi uwe na heshima sana na viwanda vya pombe hehehe
      Haaahaaaa...This is one of those countries.....pombe ni muhimu kuliko natural resources! sijapata ona.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    22. #20
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,645
      Rep Power : 4015
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Ukiona kila mwaka ni sigara, pombe na soda, jua hakuna sources nyingine za revenue. Badala ya kusaidia biashara ndogo ndogo na sekta isiyorasmi kukua, TRA na vijana wake wanakaba mpaka penalti. Misamaha siyo kwetu tunaoamua ku invest kwenye nchi yetu...ni kwa wale waliokuja kuvuna.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    23. FemaTV & Radio
    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...