Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 38 of 38
    1. #1
      mwananchi wa kawaida's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th February 2012
      Posts : 55
      Rep Power : 379
      Likes Received
      12
      Likes Given
      8

      Default Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

      Jamani watanzani wenzangu hivi hii bajeti ya matumizi 70% na uzalishaji 30% inatupeleka kwema kwel?

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      TaiJike's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2011
      Posts : 1,156
      Rep Power : 607
      Likes Received
      387
      Likes Given
      347

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Ama kweli hii ni nchi ya wendawazimu ina maana pombe inazalisha kuliko dhahabu, tanzanite, almasi, copper, uranium, nk.nk.nk.
      * Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi? * - Julius Kambarage Nyerere


    4. #22
      TaiJike's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th December 2011
      Posts : 1,156
      Rep Power : 607
      Likes Received
      387
      Likes Given
      347

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Quote By Ndahani
      Ukiona kila mwaka ni sigara, pombe na soda, jua hakuna sources nyingine za revenue. Badala ya kusaidia biashara ndogo ndogo na sekta isiyorasmi kukua, TRA na vijana wake wanakaba mpaka penalti. Misamaha siyo kwetu tunaoamua ku invest kwenye nchi yetu...ni kwa wale waliokuja kuvuna.
      Na sasa penati hiyo itakaba hata hizo soda, sigara, na pombe havitanunuliwa hakuna mjinga atakaye acha kununua mchele na dagaa akakimbilia anasa.
      * Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi? * - Julius Kambarage Nyerere


    5. #23
      Asnam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th January 2012
      Location : Yutong
      Posts : 2,622
      Rep Power : 11182
      Likes Received
      1639
      Likes Given
      1171

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      no wonder till 2015 ndo tutaona mwangaza kule Buzwagi ndege zinaruka kila uchwao na madini hayalipiwa kodi,kila sehemu yalipo madini kuna uwanja wa ndege ndani kodi utaipata wapi viongozi wanakatiwa fungu lao wanakaa pembeni.
      "Quality is always better than quantity. That's why the people I call true are few."

    6. #24
      seniorgeek's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th September 2008
      Location : Arusha
      Posts : 349
      Rep Power : 614
      Likes Received
      70
      Likes Given
      339

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Kumbe kila jioni ninapokuwa kaunta nachangia pato kubwa sana kwa hii nchi.
      No mercy

    7. #25
      Ngisibara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd January 2009
      Posts : 1,154
      Rep Power : 760
      Likes Received
      134
      Likes Given
      129

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Pakua Hapa
      SEMINA ELEKEZI, Mie ntakula mpaka kulee, wewe palee na nyie paleee, Mawaziri wangu angalieni msiingiliane mpaka tutakapokutana 2015


    8. Miaka 50

    9. #26
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,186
      Rep Power : 24275
      Likes Received
      4682
      Likes Given
      2300

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Serikali hii inawalazimisha watu kukaa counter kulipa kodi. Hivi tukigoma kunywa pombe nini kitatokea? kwani pombe ni dawa au chakula?
      Natamani watanzania wazire kunywa pombe na kuvuta sigara!

      Ee bwana Mungu tenda miujiza yako.
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    10. #27
      Lubaluka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th May 2009
      Posts : 468
      Rep Power : 603
      Likes Received
      20
      Likes Given
      19

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Shamba la bibi kama kawa!!!!!! Nimechoka sanaaaaaaa.......
      Always The Silence of Our Friends Hurts more than the Noise of Our Enemy.

    11. #28
      Babuu Rogger's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th November 2011
      Posts : 234
      Rep Power : 426
      Likes Received
      35
      Likes Given
      2

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Wasira anajua kuandaa budget dah! kumbe wazo la kilimo cha mchele lilikuwa lake na ndio maana akawahi kulitoa CHADEMA SQUARE.
      THERE AIN'T NO HIDING PLACE FROM THE FATHER OF CREATION.

    12. #29
      kichomiz's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2011
      Posts : 4,053
      Rep Power : 1232
      Likes Received
      652
      Likes Given
      80

      Default

      Quote By idawa
      idumu TBL kwa maendeleo ya tanzania.!
      Natamani kutukana ila nashindwa,
      kweli hii serikali legelege wanaacha mapato kwenye madini wanakomaa na vinywaji?huu ni upuuzi mwingine me nahamia kwenye ulanzi na kimpumu sasa.

    13. #30
      Njaare's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2010
      Posts : 572
      Rep Power : 661
      Likes Received
      92
      Likes Given
      168

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Quote By dosama
      Mussa Juma, Dodoma


      Concern

      Wakina Barick mbona hawaguswi ila TBL na Coca kina Azam, sigara kila mwaka kwanini serikali yetu tunaenda wapiiii????
      Imefika wakati wa wanywaji kususia kunywa ili kuishinikiza serikali kutumia vyanzo vingine vya mapato.

    14. #31
      Lusajo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Posts : 447
      Rep Power : 663
      Likes Received
      9
      Likes Given
      1

      Default

      hivi umewahi kuona mlevi kapunguza idadi ya pombe au sigara anazokunywa kwa sababu ya bei? mwalimu wangu aliniambia watakaopata shida ni kina mama na watoto ambao waume/baba zao wanakunywa maana watapunguza hata hela wanayoacha nyumbani ila sio idadi ya pombe na sigara wanazotumia kwa hiyo mwisho wa siku wanaopata shida ni kina mama kwa watoto kwa hizi kodi za pombe na sigara kuongezwa kila siku. hatuna jipya? nilijua Mgimwa angekuja na mpya.

    15. #32
      kanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th January 2011
      Posts : 737
      Rep Power : 571
      Likes Received
      292
      Likes Given
      410

      Default Re: Serikali iwe makini na jkt-bajeti mpya

      Kama hakutakuwa na nafasi za kazi na ajira na kujidanganya na hisia za kijinga kuwa kuwapa vijana uzalendo na utaifa ni kujenga taifa jipya la majambazi.Mie nauliza swali , hivi akina Mkulo,Karamagi,Chenge,Lowassa na majambazi na mafisadi makubwa na mapapa yaliyopo hivi sasa serikali hayakupitia JKT kwa wakati huo ambayo ilikuwa ni lazima baada ya kumaliza elimu ya sekondari kabla ya kujiunga na chuo kikuu au kuanza kazi ?.JKT itakuwa na maana kama itawapa vijana mbinu za ujasiriamali na uzalishaji pamoja na vifaa au vitendea kazi ,lakini naona ni gharama kubwa sana assume vijana wamepelekwa ruvu jkt na kujifunza ufugaji wa nguruwe na kuku je wote watapata mtaji wakuanzia au watatoka na kwenda vijiweni?.Utafiti na mfumo mzuri unahitajika sana wa kuendesha jkt ya kisasa zaidi tena iliyobora na siyo mitulinga na unyanyasaji wa kijinsia.
      vngenge likes this.

    16. #33
      mgt software's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,754
      Rep Power : 784
      Likes Received
      143
      Likes Given
      203

      Default Re: Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

      Pombe Oyeee, Madini Zii,leo natupa dhahabu zangu zote maana ni mapambo yasiyo na Tija, uenda pombe ni muhimu sana kwa taifa ili hata kwa mapato, kuna haja ya kufanya utafiti makini kuhusu pombe maana inategemewa sana,viwanda vyote vikifungwa, Chuo Kikuu kinafungwa, Barabara zinakuwa full madimbwi.
      "Mtoto wa Maskini Hachagui Malezi, Tanganyika siyo Masikini Masikini ni wewe Unayehonga Haki yako Kwa Mafisadi" Bamugileki

    17. #34
      Comi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 963
      Rep Power : 578
      Likes Received
      156
      Likes Given
      2

      Default Re: Duh!!Bajeti yenye matumizi zaidi ya uzalishaji

      Jamani sikusikiliza jana bunge, vipi kuhusu roadplane(vx) walizodai hazitatumika,wamesema wataziuza au ndiyo longolongo?

    18. #35
      kupelwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th August 2011
      Location : DAR-ES-SALAAM
      Posts : 456
      Rep Power : 483
      Likes Received
      120
      Likes Given
      31

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Quote By dosama
      Mussa Juma, Dodoma
      SERIKALI jana ilitangaza Bajeti ya Sh15trilioni kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ambayo pamoja na mambo mengine, imelenga kudhibiti mfumuko wa bei kwa kutangaza kutoa vibali vya kuingiza chakula kutoka nje, huku ikiwabana matajiri kwa kuongeza kodi ya bidhaa zisizokuwa za lazima.

      Akisoma bajeti hiyo bungeni Dodoma jana, Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alitangaza pia kwamba Serikali imepanua wigo wa Kodi ya Mishahara (Paye) na sasa itawagusa wafanyakazi wenye kipato cha kuanzia Sh170,000 badala ya Sh135,000 ya awali, huku ikirejesha mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kutenga Sh7 bilioni kwa ajili ya kuchukua vijana 5,000.

      Dk Mgimwa katika Bajeti hiyo pia alitangaza ongezeko la kodi za bidhaa mbalimbali, ikiwamo, bia, soda, sigara, juisi zinazoingizwa kutoka nje huku ikifuta msamaha wa ushuru wa bidhaa kwa magari kwa wote waliokuwa wananufaika na msamaha huo.

      Alifafanua kwamba kodi ya vinywaji baridi imepanda kutoka Sh69 kwa lita hadi Sh83 na mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nchini kwa kiwango kinachozidi asilimia 75, imeshuka kutoka Sh425 kwa lita hadi 145 kwa lita.

      Kodi ya mvinyo unaotengenezwa kwa zabibu inayozalishwa nje ya nchi kwa kiwango kinachozidi asilimia 25, imepanda kutoka Sh1,345 kwa lita hadi 1,614 kwa lita.

      Alisema kodi ya vinywaji vikali imepanda kutoka Sh1,993 kwa lita hadi Sh2,392 kwa lita, bia inayotengenezwa nchini kwa nafaka na ambayo haijaoteshwa, kodi yake imepanda kutoka Sh248 kwa lita hadi Sh310 kwa lita. Bia nyingine zote kodi imepanda kutoka Sh420 hadi Sh525 kwa lita.

      Akizungumzia marekebisho ya ushuru kwenye bidhaa za sigara, Dk Mgimwa alisema zote zisizo na kichungi na zinazotengenezwa kwa tumbaku inayozalishwa nchini, kiwango cha angalau asilimia 75, kodi imepanda kutoka Sh6,820 hadi Sh 8,210 kwa sigara 1,000.

      Alisema Sigara zenye kichungi na zinazotengenezwa kwa tumbaku inayopatikana nchini kwa kiwango cha angalau asilimia 75, kodi imepanda kutoka Sh16,114 hadi Sh19,410 na sigara nyingine zenye sifa tofauti na makundi hayo, kodi imepanda kutoka Sh29,264 hadi Sh35,117 kwa sigara 1,000.

      Alisema tumbaku ambayo ipo tayari kutengenezwa sigara (cut filler) kodi yake imepanda kutoka Sh14,780 hadi Sh17,736 kwa bunda la sigara 1,000 wakati ushuru wa cigars unabaki kuwa asilimia 30.

      Gharama za simu juu
      Katika bajeti hiyo, Waziri Dk Mgimwa alisema muda wa maongezi (airtime) kwenye simu za mkononi umeongezeka kutoka asilimia 10 hadi 12.

      Alisema lengo la hatua hiyo ni kuoanisha ushuru wa bidhaa unaotozwa na huduma hiyo katika nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC), kwa kipindi hiki ambacho nchi zipo katika Soko la Pamoja.
      Alisema hatua hizo za ongezeko la ushuru wa bidhaa kwa pamoja, zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha Sh144,054.9 milioni.

      Misamaha ya kodi ya magari

      Waziri huyo alipendekeza kufanyika marekebisho kwenye sheria husika za kodi ya matangazo ya Serikali yanayotoa msamaha wa kodi kwenye magari kwa walengwa mbalimbali ili kuweka ukomo wa umri wa miaka minane kwa magari hayo badala ya miaka 10.

      Alisema magari yenye umri wa zaidi ya miaka minane yatatozwa ushuru wa bidhaa wa asilimia 20. Lengo la hatua hiyo ni kupunguza wimbi la uingizaji magari chakavu na kulinda mazingira.
      Alitangaza pia marekebisho katika ushuru wa forodha, ikiwemo kufuta msamaha wa ushuru wa forodha katika vitu mbalimbali vikiwemo magari yenye ujazo wa CC 3000 huku pia ushuru wa forodha ukifutwa katika bidhaa nyingine nyingi muhimu.

      Alisema katika kuhamasisha na kuchochea ukuaji wa sekta ya ufugaji wa nyuki, vifaa vinavyotumika katika ufugaji na kurina asali vimepewa msamaha wa ushuru wa forodha vinavyoingizwa kutoka nje ya nchi na wafugaji wa nyuki.

      Alisema msamaha wa ushuru wa forodha kwenye migahawa ya majeshi ya ulinzi utaendelea kutolewa kwa kipindi cha mwaka mmoja.
      Alisema kumefanyika marekebisho katika Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ya mwaka 2004 ili kutoa msamaha wa ushuru wa forodha kwa wazalishaji wa vyakula vinavyotengenezwa mahsusi kwa lishe ya watoto wenye utapiamlo na watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi.

      Alisema kuwa katika Bajeti hiyo, pia wametoa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye malighafi zinazotumika katika kutengeneza vifaa vya kufanyia uchunguzi wa magonjwa (medical diognastic kits) kwa kuwa vifaa hivyo hutozwa asilimia sifuri vinapoagizwa kutoka nje ya nchi.

      Katika marekebisho hayo, utatolewa msamaha kwenye mitambo (machinery) na vipuri vyake vinavyotumika kwenye uchimbaji wa madini lakini hautahusisha vipuri vya magari vitakavyoagizwa na makampuni yanayojihusisha na uchimbaji wa madini.

      Katika bajeti hiyo, pia umetolewa msamaha wa ushuru wa forodha kwenye vyuma vinavyowekwa kwenye kingo za barabara na lengo lake ni kutoa unafuu katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

      Alisema ushuru wa forodha umepunguzwa kwa ving’amuzi kutoka asilimia 25 hadi asilimia sifuri ili kuwezesha mabadiliko katika teknolojia ya analogia na kwenda katika teknologia ya digitali.

      Alisema katika Bajeti hiyo, pia ushuru wa ngano umeondolewa kuwa asilimia 0 badala ya asilimia 35
      Alisema Serikali pia imesamehe VAT katika mashine za kutolea stakabadhi (electronic fiscal devices), ili kupunguza bei yake na kuwezesha wafanyabiashara wengi kuwa nazo, kuhamasisha matumizi yake na hivyo, kuongeza mapato ya Serikali.

      Katika eneo hilo, Serikali imeondoa VAT kwa vifaa mbalimbali vya kuhifadhia, kusafirisha na kusambaza gesi asilia ili kuongeza matumizi ya nishati hiyo katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kwenye magari, majumbani na viwandani.

      Kodi kwa wafanyabiashara
      Wafanyabiashara ambao mapato yao hayazidi Sh3,000,000 hawatalipa kodi kuanzia Julai Mosi, mwaka huu. Dk Mgimwa alisema mpango huo umefanywa kulinda mapato ya Serikali.

      Kabla ya msamaha huo, wafanyabiashara hao ambao mapato yao hayazidi Sh3,000,000 walikuwa wanalipa Sh35,000.

      Marekebisho mengine ya kodi ya mapato ni kuwa wenye mapato kati ya Sh3 milioni –Sh7.5 milioni watalipa Sh100,000 badala ya Sh95,000.

      Malengo ya Bajeti
      Waziri Mgimwa alisema Bajeti hiyo imejielekeza katika Kukuza Pato la Taifa kwa asilimia 6.8 mwaka 2012 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.4 mwaka 2011.

      Malengo mengine ni kuimarisha miundombinu ya uchumi, ikijumuisha umeme, barabara, reli na bandari, kuongeza upatikanaji wa huduma za kifedha na kuongezeka kwa mapato ya ndani yatakayofikia uwiano na Pato la Taifa wa asilimia 18 kwa mwaka 2012/13 kulinganisha na mwelekeo wa asilimia 16.9 mwaka 2011/12.

      Dk Mgimwa alitaja malengo mengine kuwa ni pamoja na kuendelea kudhibiti mfumuko wa bei ili urudi kwenye viwango vya tarakimu moja na kuwa na kiwango tengemavu cha ubadilishaji wa fedha kitakachotokana na mwenendo wa soko la fedha.

      Malengo mengine ni kukuza mikopo kwa sekta binafsi kwa kiwango cha asilimia 20 ya Pato la Taifa ifikapo mwishoni mwa Juni 2013, sambamba na jitihada za kudhibiti mfumuko wa bei, kuboresha mazingira ya wafanyabiashara wadogo na wa kati, kulinda na kuendeleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta za huduma za jamii, kuimarisha utawala bora na uwajibikaji na kujenga uwezo wa nchi kukabiliana na misukosuko ya kiuchumi na kifedha pamoja na kushiriki kwa ufanisi katika ushirikiano kikanda na kimataifa.

      Matumizi ya Maendeleo
      Kuhusu matumizi ya maendeleo, Waziri Mgimwa alisema itazingatia vipaumbele vya miundombinu ya umeme - mkazo ukiwa upatikanaji wake kwa kuongeza uzalishaji, usafirishaji na usambazaji na jumla Sh498.9 bilioni zimetengwa.

      Serikali pia itatekeleza mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam kwa mkopo kutoka Benki ya Exim ya China wenye thamani ya Dola za Marekani 1.2 milioni utakaosimamiwa na TPDC.
      Kuhusu usafirishaji na uchukuzi, alisema mkazo katika sekta hiyo utakuwa ni kuimarisha reli ya kati ikijumuisha ukarabati wa injini na mabehewa ya treni.

      “Kwa upande wa barabara, miradi inayopewa kipaumbele ni pamoja na barabara zenye kufungua fursa za kiuchumi. Katika usafiri wa anga na majini, miradi itakayotekelezwa ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege na uendelezaji wa gati ya Ziwa Tanganyika. Jumla ya Sh 1,382.9 bilioni zimetengwa katika eneo hili,” alisema.

      Kuhusu maji safi na salama, alisema lengo ni - kuongeza upatikanaji wake mijini na vijijini na kwamba kiasi cha Sh568.8 bilioni kimetengwa.

      Kwa upande wa kilimo, uvuvi na ufugaji alisema katika sekta hizo, Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi itawekeza katika kilimo cha mpunga na miwa katika mabonde makuu ya Wami, Ruvu, Kilombero na Malagarasi pamoja na kuongeza tija na thamani, kubadilisha mfumo wa kilimo na kukuza kilimo cha misitu.

      Kuhusu kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula pamoja na kuhakikisha uhakika wa chakula, Serikali itaimarisha utekelezaji wa dhana ya Kilimo Kwanza kwa kuhakikisha nguzo zake zote zinaendelea kuzingatiwa.

      Alisema mikoa inatakiwa kuendelea kutenga ardhi na vijiji kutakiwa kupima na kurasimisha ardhi kwa ajili ya wawekezaji wa ndani na wa nje na kwamba kiasi cha Sh192.2 bilioni kimetengwa katika eneo hilo.

      Ikizungumzia maendeleo ya viwanda, alisema Serikali inakusudia kuendeleza viwanda vinavyotumia malighafi zinazopatikana nchini; viwanda vinavyoongeza thamani ya madini; viwanda vikubwa vya saruji na viwanda vya eletroniki na Tehama pamoja na kuboresha mazingira ya biashara na kutenga maeneo maalumu ya uwekezaji mijini na vijijini na kukuza ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.


      Concern

      Wakina Barick mbona hawaguswi ila TBL na Coca kina Azam, sigara kila mwaka kwanini serikali yetu tunaenda wapiiii????
      kuna siku moja bungeni zito alotoa tamko kuwa amepata waraka mabo serikali ya tanzania na barick wamesainiana kuwa serikali iwalinde masilahi yao kwa nguvu zote , bila kujali.spika wakati ule mzee sita akajibaraguza na kumpotea zito.kwasasa nathibitisha kuwa barick lazima walindwe kwa nguvu zote.hakuna sekta inachongia mapoto mengi kwenye gdp kama madini lkn pesa yake kiuhalisia haionekani kimsingi sababu wazalishaji ni migodi mikubwa ambayo inalindwa kwa nguvu zote, kwann watozwe kodi kubwa?

    19. #36
      ha ha ha's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th December 2011
      Location : Hapahapa
      Posts : 456
      Rep Power : 466
      Likes Received
      45
      Likes Given
      71

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Tumethubutu, tumeweza, tunasonga mbele.
      "If you find yourself in ahole, the first thing to do is stop digging"



    20. #37
      MANI's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 22nd February 2010
      Location : CHINI YA MBUYU
      Posts : 1,921
      Rep Power : 955
      Likes Received
      573
      Likes Given
      636

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Quote By Ndahani
      Ukiona kila mwaka ni sigara, pombe na soda, jua hakuna sources nyingine za revenue. Badala ya kusaidia biashara ndogo ndogo na sekta isiyorasmi kukua, TRA na vijana wake wanakaba mpaka penalti. Misamaha siyo kwetu tunaoamua ku invest kwenye nchi yetu...ni kwa wale waliokuja kuvuna.
      Ndahani Hivi kwa nini serekali yetu haitujali? Maana ukiondoa misamaha kwa investors kutika nje unawainua watu wako lakini hapa kwetu ni vice versa !
      Ndahani likes this.
      " TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA"

    21. #38
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Hii hapa bajeti ya kutegemea Pombe na misaada na kuwaacha wachimba madini

      Quote By MANI
      Ndahani Hivi kwa nini serekali yetu haitujali? Maana ukiondoa misamaha kwa investors kutika nje unawainua watu wako lakini hapa kwetu ni vice versa !
      MANI, Hatuna american english accent....labda ndio inawafanya watu kutingisha vichwa na kukubaliana na kila kitu kinachowekwa mbele yao
      MANI likes this.
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...