Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

    Report Post
    Page 1 of 3 123 LastLast
    Results 1 to 20 of 55
    1. #1
      apolycaripto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th February 2011
      Posts : 576
      Rep Power : 531
      Likes Received
      136
      Likes Given
      0

      Default Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Na Mwandishi Maalumu

      NAIBU Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dk Asha-Rose Migiro amemaliza jukumu lake rasmi katika Umoja wa Mataifa (UN) jijini New York, Marekani.Kwa hatua hiyo, mashirika ya UN yanayohusika na masuala ya Idadi ya Watu (UNFPA), Ukimwi (Unaids) na Mpango wa Kupambana na Malaria (RBM) Jumanne yaliandaa tafrija ya kumshukuru na kumuaga.Tafrija hiyo ambayo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon, akifuatana na mkewe na wadau mbalimbali akiwamo Ofisa Mtendaji Mkuu wa UNDP, Helen Clark, mabalozi wanaowakilisha nchi zao UN, sekta binafsi na taasisi za kiraia, ilifanyika makao makuu ya UN.

      Akizungumza kwenye tafrija hiyo, Ban alielezea baadhi ya sababu zilizomsukuma kumteua Dk Migiro kuwa msaidizi wake wa karibu.“Nilimfahamu Migiro wakati huo sote tukiwa mawaziri wa mambo ya nje katika nchi zetu.“Uwezo wake na uelewa wake wa mambo ulinivutia sana, lakini nilivutiwa zaidi pale nilipofahamu kwamba alipata kuwa waziri wa masuala ya wanawake na watoto. Nikajiridhisha kwamba huyu ndiye atafaa kuwa msaidizi wangu wa karibu,” alisema Ban na kushangiliwa.Kama haitoshi, Ban alimwelezea Dk Migiro kama msaidizi wake wa karibu ambaye licha ya kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa, ni mtu asiye na makuu na hata siku moja hakujikweza.“Katika kipindi chote ambacho Migiro amekuwa msaidizi wangu wa karibu, amenisaidia katika mambo mengi, ni mtu mwadilifu sana, ni mtu aliye karibu sana na watu, aliyeamsha matumaini na kuwapa tabasamu waliokuwa katika mazingira magumu. Daima amekuwa mstari wa mbele kunisaidia na hakuna hata siku moja alipojikweza.Na kwa sababu hii, anastahili tafrija hii,” alisisitiza Ban. Aidha, Ban alimwelezea Migiro kama kiongozi ambaye daima alitoa kipaumbele cha aina yake katika masuala ya afya ya jamii, eneo alilotumia uwezo wake wote, maarifa yake yote kama Naibu Katibu Mkuu kupigania afya ya wanawake na watoto na watu wote walio katika mazingira magumu.

      Kwa upande wao, waandaaji wa tafrija hiyo na wakizungumza kwa nyakati tofauti wamemwelezea Naibu Katibu Mkuu, kama kiongozi ambaye mchango wake umesaidia kuhamasisha jumuiya ya kimataifa kuweka mkazo wa aina yake katika kushughulikia afya ya jamii. Michel Sidibe, Mkurugenzi Mtendaji wa UNAIDS alimwelezea Migiro kama dada yake ambaye sifa zake zinaanzia mbali.“Migiro ni dada yangu, ni dada ambaye ana sifa za kipekee, ni mwanamke wa kwanza aliyefaulu daraja la kwanza katika Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ni mwanamke wa kwanza kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Tanzania na mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UN,” alisema kauli iliyoamsha tena makofi kutoka kwa wageni waalikwa.

      Sidibe alimwelezea Migiro kama kiongozi aliyefanya kazi kwa karibu na shirika lake katika kuhakikisha maambukizi ya virusi vya Ukimwi yanapungua, ikiwa ni pamoja na kupatikana kwa tiba ya uhakika kwa waathirika.“Tuna kila sababu leo hii kumshukuru kwa namna alivyoshirikiana nasi, na ingawa unaondoka, lakini tambua kwamba mchango wako utaendelea kukumbukwa na kuenziwa,” alisisitiza Sidibe.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, Dk Babatunde Osotimehin alisema juhudi kubwa zilizooneshwa na Naibu Katibu Mkuu katika kushughulikia masuala ya afya ya jamii, zilipunguza kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo vya wanawake vitokanavyo na uzazi, hali kadhalika vya watoto wachanga wa chini ya umri wa miaka mitano.“Katika kipindi cha uongozi wako, umefanikisha kuhamasisha jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada na kutoa kupaumbele katika afya ya mama na mtoto, tunakushukuru sana kwa hili na Mungu aendelee kukubariki,” alisema Dk Osotimehin.

      Herve Verhoosel, Mwakilishi wa Mpango wa Kupunguza Malaria, alimwelezea Dk Migiro kwamba chini ya uongozi wa Ban, alijenga misingi bora ya ushirikiano na mwamko miongoni mwa wadau katika kuhakikisha unakuwapo uhusiano kati ya sekta za umma na binafsi katika kutimiza malengo ya afya ya jamii, ikiwa ni pamoja na kasi ya kupunguza malaria.

      Akishukuru waandaaji wa tafrija hiyo, Dk Migiro alimshukuru Ban kwa kumwamini kuwa msaidizi wake wa karibu kwa miaka mitano na nusu. Alisema ingawa alijituma kutekeleza majukumu yake kwa ukamilifu, alifanya hivyo kwa kuwa Ban alimwamini kwamba anaweza. Na kwamba daima ataendelea kuienzi heshima hiyo.Alitumia fursa hiyo kumwelezea Ban kama kiongozi ambaye yuko mstari wa mbele kuhakikisha kila mtoto angalau analala kwenye chandarua na wajawazito hawapotezi maisha kutokana na uzazi.Migiro alishukuru kwa moyo wa dhati wasaidizi wake wa karibu aliofanya nao kazi akiwa Naibu Katibu Mkuu na kwamba bila wao asingefika alipo, alishukuru pia wadau wakiwamo mabalozi kwa ushirikiano wa hali na mali waliompa muda wote wa uongozi wake.
      Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiwa na Dkt Asha-Rose Migiro katika hafla ya kumuaga rasmi iliyofanyika leo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa baada ya kumaliza muda wake kama Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

      Dkt Asha-Rose Migiro akiongea katika hafla hiyo ya kumuaga rasmi

      Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akiongea katika hafla hiyo

      Dkt Asha-Rose Migiro baada ya kupokea zawadi ya maua katika hafla hiyo ya kumuaga rasmi
      Last edited by apolycaripto; 14th June 2012 at 12:48.

    2. Miaka 50

    3. #2
      MANGUNGO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2011
      Posts : 1,146
      Rep Power : 620
      Likes Received
      251
      Likes Given
      14

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Hale penshen sasa asilete uroho wa madaraka tanzania maana magamba hawaridhiki hasa hawa sampuli za batrida,

    4. #3
      Mwakalinga Y. R's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 22nd October 2008
      Location : UVUNGUNI
      Posts : 2,169
      Rep Power : 973
      Likes Received
      924
      Likes Given
      2281

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Umoja wa mataifa ulimpenda sana ila Watanzania wanampenda zaidi arudi nyumbani
      " You're still my enemy tonight. But even enemies can show respect. " -Priam




    5. #4
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,170
      Rep Power : 24272
      Likes Received
      4677
      Likes Given
      2296

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Quote By MANGUNGO
      Hale penshen sasa asilete uroho wa madaraka tanzania maana magamba hawaridhiki hasa hawa sampuli za batrida,
      Jk atamteua kuwa mbunge
      Mwakalinga Y. R likes this.
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    6. #5
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,606
      Rep Power : 15261
      Likes Received
      3731
      Likes Given
      2866

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Quote By Mwakalinga
      Umoja wa mataifa ulimpenda sana ila Watanzania wanampenda zaidi arudi nyumbani
      Je, ameacha jina zuri la Tanzania kuhusu wajibikaji au ameacha tu jila historia kwamba Tanzania ilikuwa na Naibu katibu mkuu umoja wa mataifa?

    7. RukaaJuu Final

    8. #6
      Ndinani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2010
      Posts : 2,949
      Rep Power : 1531
      Likes Received
      745
      Likes Given
      237

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Quote By Mungi
      Jk atamteua kuwa mbunge
      Lazima iwe hivyo kwani mkweree hamna koo anazoziona hapa nchini isipokuwa zawakina Asha Rose na Mwanaidi Sinare!! Ndio maana hata dada zao wanakomba teuzi kubwa kubwa za mkweree!! Hongereni wakina mama.

    9. #7
      Mchwechwele's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th January 2011
      Posts : 1,139
      Rep Power : 651
      Likes Received
      325
      Likes Given
      82

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Akirudi vp ataanza kujipanga kwa ajiri ya urais au atapewa uwaziri?
      Maskini hana Mpambe

    10. #8
      mkomatembo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th December 2011
      Location : Bweleo
      Posts : 1,019
      Rep Power : 637
      Likes Received
      228
      Likes Given
      1269

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Kuna mama mmoja juzi juzi ametoka UN amewepwa wizara ya mazingira, sasa huyu nae si vibaya akapewa wizara ,

    11. #9
      mamajack's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 1,153
      Rep Power : 583
      Likes Received
      275
      Likes Given
      71

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Quote By mkomatembo
      Kuna mama mmoja juzi juzi ametoka UN amewepwa wizara ya mazingira, sasa huyu nae si vibaya akapewa wizara ,
      yule mama anamipango mingi utekelezaji zero kabisaaaaaaaaa,nadhani hata huyu sina niwalewale.magamba hawana product ya kujivunia.

    12. #10
      MANGUNGO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2011
      Posts : 1,146
      Rep Power : 620
      Likes Received
      251
      Likes Given
      14

      Default

      Quote By Mungi
      Jk atamteua kuwa mbunge
      kama wapemba vile!!kazi kwelikweli

    13. #11
      mkizungo's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Posts : 249
      Rep Power : 408
      Likes Received
      47
      Likes Given
      298

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      karibu nyumban,karibu dada asha,rose sahaban mtengeti migiro,,,kazi umeifanya na heshima umeijenga,,,,,,come back home with comfidence,,,,mungu aliyekufikisha huko usimuache,,,,watumikie wa tz,,tuna tatizo la uongozi,,,tumekosa mtu anayeheshimiwa na jamii katika watawala wetu,,,nasema watawala kwakua hatuna kiongozi,,,tumekosa dira na mwelekeo kama taifa,,,,,,,tunaongozwa na matukio,,chama chako kinahenyeshwa kwata na umma unaohitaji mabadiliko,,,chenyewe kinasaka wachawi badala ya kuleta mabadiliko,,,,,,kinasubiri kilazimishwe,,,,,njoo upesi ,,,njoo usikawie,,,,njoo na mbadala njoo tofauti,,,njoo uwaone wa tz masikini wasio na matumaini tena,,kila siku heri ya jana,,,,,ukifika jipange,,,usake urais ili 2015,,ushindan ndan ya chama chako uwe mgumu,,na uchaguzi uwe mgumu ,kuupata urais kuwe kugumu,,huenda wapiga kura wakaheshimiwa,,,,,njoo,,ulete changamoto,,,haiwezekani wenzetu wanafuta umasikin ,,na kuboresha maisha cc tungali tunakoroma usingizi,,,,udiniiii,,udiniiii ,,uamshoooo,,muunganoooo,,nyam bafu kabisa,,huku nchi ikiporwa kila uchao na huduma za jamii zikiporomoka,,,,nan anajali,,,,,hapa nalia,,nalia kwakua najiuliza nani ametuloga,,,,ajira hamna,,maadili kwisha,,hata ule umoja wetu kama taifa unasambaratishwa na hoja za udini na ukanda,wallonacho na wasionacho,,,, mungu atusaidie,

    14. #12
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Kifaa hicho kinarudi, magwanda ya khaki kaeni chonjo.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    15. #13
      Lu-ma-ga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2010
      Posts : 1,831
      Rep Power : 810
      Likes Received
      519
      Likes Given
      8

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Anarudi na kukuta chama chake kinanuka kinyesi cha Nyani watanganyika wamekihama.

    16. #14
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,480
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4300
      Likes Given
      1248

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Atakuwa mbunge.

    17. #15
      Mwakalinga Y. R's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 22nd October 2008
      Location : UVUNGUNI
      Posts : 2,169
      Rep Power : 973
      Likes Received
      924
      Likes Given
      2281

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Quote By Candid Scope
      Je, ameacha jina zuri la Tanzania kuhusu wajibikaji au ameacha tu jila historia kwamba Tanzania ilikuwa na Naibu katibu mkuu umoja wa mataifa?
      candid Zama hizi historia hamtambii mtu ambaye hakuwa na mchango chanya kwa taifa/jamii yake.Yeye kuwa makamu katibu mkuu wa UN amechangia nini kwenye maendeleo na ustawi wa wanajuia wa UN, tz ikiwemo?.Achalia mbali na utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku ,Je amefanya nini ambacho wenzake hawakufanya chenye manufaa kwa jumuiya ya kimataifa? .
      " You're still my enemy tonight. But even enemies can show respect. " -Priam




    18. #16
      Chimunguru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd May 2009
      Posts : 7,795
      Rep Power : 2149
      Likes Received
      1222
      Likes Given
      545

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Hiko alikotoka kachemsha, asipewe chochote apishe na wengine wajaribu, sio kila siku watu hao hao, hizo ndo fikra potofu za CCM mnaziendeleza

    19. FJM
      #17
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,174
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5326
      Likes Given
      4587

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Quote By zomba
      Kifaa hicho kinarudi, magwanda ya khaki kaeni chonjo.
      zomba, huyu mama amefanya nini cha maana wakati akiwa UN?

    20. #18
      umumura's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 57
      Rep Power : 371
      Likes Received
      11
      Likes Given
      5

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      hana lolote, ndo welewale, itakuwa na maana akafundishe watoto udom

    21. #19
      Adrian Stepp's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st July 2011
      Posts : 1,573
      Rep Power : 713
      Likes Received
      438
      Likes Given
      2560

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      Ban Ki moon nomaa...kamtimua..halaf kila nikimuangali huyu mama inaonekana anapenda sana misifa..we mtazame gustures
      Watu wakimya wamejaliwa busara, ufahamu na midomo inayonuka!

    22. #20
      andishile's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2012
      Posts : 604
      Rep Power : 480
      Likes Received
      149
      Likes Given
      304

      Default Re: Dr. Asha Rose Migiro aagwa rasmi Umoja wa Mataifa (UN)

      karibu nyumbani!

    Page 1 of 3 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...