Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 7 of 62 FirstFirst ... 5678917 ... LastLast
    Results 121 to 140 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 890
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. #121
      Mnyakatari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th October 2010
      Posts : 716
      Rep Power : 682
      Likes Received
      255
      Likes Given
      180

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Sidhani hata kama hiyo sensa ya 1957 ilikuwa sahihi katika kupata idadi ya watu na dini zao.Criteria ya jina wala haitoi dini ya mtu bila shaka yoyote.Majina ni tofauti na dini.Kwa mtazamo huu kama kweli kuna kundi la watu wanataka kujua idadi ya waumini wake basi sensa ta taifa haiwezi kutoa jibu sahihi hata kidogo.Kila dini inafahamu definition ya muumini wake hivyo ni yenyewe ndani ya mfumo wake wa kitaasisi inaweza kuja na majibu sahihi ya idadi ya watu wake.Kuilazimisha serikali kujumuisha kipengele cha dini kwenye sensa ni kuendeleza upotoshaji wa maana halisi za muislam au mkristo.Pengine inaweza kuwa sahihi kwa wapagani tu!Taasisi zenyewe ndizo zinazoweza kufanya sensa hii kwa usahihi kabisa na wala sio serikali isiyokuwa na dini.Ni wakati wa kuungana kwa pamoja kupiga vita viashiria vyovyote vya udini au ukabila badala ya kuvishabikia huku maendeleo yetu yakizidi kurudi nyuma.Kukumbatia vipengele vya udini kwenye taasisi za uma kama hospitali na polisi ni kuendeleza udini pia na serikali yapaswa kuachana na vipengele hivyo vya kipuuzi mara moja.Waislam kwa wakristo na wasio wa imani hizo tusikubali kutenganishwa kwa sababu ya imani zetu ili tusimame kwa pamoja kupigania maendeleo ya kweli ya taifa letu.

    3. #122
      Ibambasi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th July 2007
      Location : Iponyamakalai - Isungang'holo
      Posts : 752
      Rep Power : 764
      Likes Received
      128
      Likes Given
      823

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By sweke34 View Post
      Correction...ni dini moja tu inayoleta migogoro duniani...dini yenye kutoa matamko tunayojadili hapa...!
      Hakuna correction hapo, nyie wote wale wale tu, kazi kubishania miungu wa kigeni...kutawaliwa kifikra ni ukoloni wa kutisha na mbaya kabisa!

    4. #123
      Ibrah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd March 2007
      Location : TZ
      Posts : 2,883
      Rep Power : 1203
      Likes Received
      402
      Likes Given
      47

      Default

      Quote By ritz View Post
      Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.
      Pia kuna nchi nyingi ambazo hawahesabu watu wao kidini na hakuna shida yoyote? Kwa fikra zako, ukichukua faida na hasara za udini kwenye sensa upande gani una faida zaidi kitaifa?

    5. #124
      LOMAYANN's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th March 2012
      Posts : 218
      Rep Power : 410
      Likes Received
      35
      Likes Given
      78

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By WA-UKENYENGE View Post
      Wengi mnapindisha pindisha! Lakini lengo kuu la kujua idadi yao ni kutaka kuibadili nchi iwe ya kiislamu, wakishajua idadi yao wataanzisha lingine la kutaka ipigwe kura ya kutaka nchi iwe ya kiislamu au la na hapo ndiyo katiba mpya inafuata. Mark my words!!
      hapo umena mkuu hawa jamaa hawanazo kabisa yaani wao hii amani imewachosha kabisa sijui hawa watu vip hivi kama wanataka kujua idadi yao c wahesabu tu waumini wao kwanza hapa mi naona wanaonyesha udhaifu mkubwa kiutawala .......... wewe unataka m/kiti wa kijiji akupe idadi ya watoto wako badala wewe uwahesabu wewe mwenyew ........... hapa naona wanataka kuwa kama somalia ............... mali kaskazini au Nigeria na kwingineko

    6. #125
      Newvision's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th November 2010
      Posts : 443
      Rep Power : 525
      Likes Received
      27
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Kuna ajenda ya siri nyuma ya pazia la DINI lakini nadhani tunahitaji kufikiria na kujiuliza je kwa kusema huyu ni Mwislamu huyu ni Mkristo ndiyo nchi itajengeka au ndiyo maendeleo yatakuja? Kutakuwa na haja zaidi kufikiria kuiweka nchi kuwa Jamhuri ya Kiislamu etc maana ndiyo tunayoyaona Nigeria na sehemu za Kenya (Cost republic), swala la kadhi etc etc.

    7. #126
      MIGNON's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd November 2009
      Posts : 584
      Rep Power : 664
      Likes Received
      176
      Likes Given
      136

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By OSOKONI View Post
      Kwani hata waislamu wangekuwa 99% ina implication gani kwa maendeleo ya taifa? Itasaidia kujenga shule zaidi, hospitali, maji safi, barabara umeme, n.k?

      Mbona watanzania mnaacha kufuatilia na kushuguligikia mambo ya maana mnakeshea ujinga? Sasa hivi tulitakiwa tunaumiza kwa miaka 50 ya uhuru wetu mbona hali inazidi kuwa duni? Kwa rasilimali tulizo nazo madini, ardhi, watu, maji, bahari, milima mbuga za wanyama, amani, maziwa, mito hali nzuri ya hewa mbona umaskini unatumaliza! Mnakalia kutokwa mishipa ya shingo kutaka kujua waislamu na wakristu wepi wengi!! Au mnataka kutangaza taifa la kiislamu muwafukuze wakristu?

      Mtanzania amka, umaskini, magonjwa, ujinga havichagui dini hata mnekuwa waislamu peke yenu isingewasaidia!!
      Mimi ni Muislamu lakini nashangazwa na wabahatishaji wa maisha ambao wanatumia elimu yao ya dini kuvuruga watu.
      waislamu wapo nyuma katika elimu zote mbili za dunia na akhera na ni jukumu walioelimika kuwasaidia wenzao.
      Tumekuwa ni watu wa kutoa vitisho na ultimutum nyingi na tumeshindwa kutumia busara katika mikakati yetu.
      Ningetegemea wanaharakati hao watujie na maombi ya kuanzisha chuo kiukuu ambayo yamekataliwa,maombi ya kuanzisha hospitali itakayoendeshwa katika msingi ya dini na wakataliwa.
      Tunachokishuhudia ni shule za Kiislamu kutokufanya vizuri mwaka hadi mwaka.
      Tunachokishuhudia ni wale wanaojiita waislamu kuwa vinara katika mambo yanayokwenda kinyume na Uislamu (angalia wana muziki,wacheza shoo,wanaondaa mashindan ya u miss nk)
      Hatuna mkakati tumekuwa kama yatima,ni kulalamika tu.
      Tumekosa Ucha MUngu wa kweli (katoe milioni kweny msikiti kama hazitachakachuliwa na hao hao ambao wanazijua aya.
      Waislamu tuamke,tuangalie adui yetu hasa ni nanai na tupange namna za kumkabili.
      Kwangu mimi adu mkubwa ni ukosefu wa Elimu zote mbili na hili tulipe kipaumbele tutayaona mabadiliko hata bila kutishia.
      Serikali isikubali kuyumbishwa,sheria ifuatwe na watu wahesabiwe tuweze kupanga maendeleo bila kujali itikadi ya dini.
      OSOKONI likes this.

    8. #127
      twatwatwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th September 2011
      Posts : 885
      Rep Power : 569
      Likes Received
      102
      Likes Given
      3

      Default Re: tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya Agosti 2012

      Kwani kuna tatizo gani ?

    9. #128
      Mwanamayu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2010
      Location : Manzese
      Posts : 3,049
      Rep Power : 1072
      Likes Received
      240
      Likes Given
      112

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Jasusi View Post
      Sensa ya mwaka 1957 haikuonyesha idadi ya Waislamu kuwa 65%. Pia kuna sensa iliyofuata 1967 pia ina takwim inayoonyesha idadi ya Waislamu na Wakristo. Kwa hiyo si sahihi unaposema kuwa baada ya 1957 sensa zote zilizofuata zilifuta kipengele kinachoonyesha dini za watu.
      Leteni hizo sensa nasi tuone kama mnasema ukweli!

    10. #129
      Mbimbinho's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st August 2009
      Posts : 1,850
      Rep Power : 873
      Likes Received
      476
      Likes Given
      213

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mtambuzi View Post
      Ndio maana mimi niliamua kuwa MPAGANI..........
      Mkuu mbona huwa nakuona kwa Mzee wa Upako?

      Quote By Ibambasi View Post
      Na huwezi kuamini wapagani ndio wanaishi maisha ambayo vitabu vya hao wenye dini vinataka...wao wenye dini wamebaki kueneza chuki dhidi Yao na kuuana. Ni nadra kusikia wapagani wameuleta vurugu za kidini, kila siku tunasikia waislamu na wakristo katika fujo.
      Connect dots mkuu.
      Mbwa ukimjua jina wala hakupi shida....

    11. #130
      ntamaholo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2011
      Location : Mwilavya
      Posts : 4,119
      Rep Power : 1391
      Likes Received
      919
      Likes Given
      412

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      kuna ofisa mmoja wa serikali kanishangaza sana, yeye ni muislam halafu amesoma. nilimjulisha waislam wanataka kugomea sensa amesapoti, nikamwulza kwa nini, aksema serikali inakataa kuingiza kipengle hicho. nikamwuliza, kwani hamwezi kuhesabiana misikitini? mbona wakristo wanajua waumini wao, tena walio active na wasio active? yeye akajibu, kuna waislam wengi hawaingii msikitini, ila walishasomewa sijui kaitaje!!!! yaani kukubali kuwa mwisilam.

      kwa kuwa ni kiongozi wangu, nimemchunia tu lakini nimemwona naye sio mtu makini, kwani mwisho wa siku kaelezea hadi baraza la mitihani, kuwa ni kwa sababu hakuna wailam. nikampa mchanganuo wa waliopo baraza, iliwahi kutolewa, mwisho wa siku amesema, tnagu baraza kuundwa, limeongozwa na wakristo tu, kwa hiyo hoja siyo waislamu wangapi baraza, bali nani kiongozi baraza.
      UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

    12. #131
      WA-UKENYENGE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : Inside a Smart Grid
      Posts : 2,491
      Rep Power : 5057
      Likes Received
      806
      Likes Given
      1903

      Default Re: tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya Agosti 2012

      Quote By SALMA2015 View Post
      Hivi huyu Rais wetu wa sasa aliyebakiza miaka yake miwili Na nusu aondoke Na Chama lake ana MSHAURI kweli BABU HUYU..!! Akifanya mchezo muda wake uliobaki utamletea huzuni ya milele..

      Nilisikia kwamba washauri wake wote walimkimbia Kwa sababu alikuwa anawatosa..Kabaki Wassira.. Sasa huyu aliyewahi kukiasi Chama toka lini akawa mshauri mzuri.. Ushauri wake utakuwa umautimauti tu, kwanini serikali isikae Na viongozi hawa wa Dini Na kuwauliza Chanzo cha vurugu zao badala ya kuwaona wapuuzi wanaostahili kumwagiwa Maji ya uchungu Na virungu.. Hata Kama kweli ni wapuuzi Lakini bado ni raia halali Wa JMT.. Wanastahili kusikilizwa Na kuelekezwa wanachodhani ni Hoja Na mtagundua ni nani Yuko nyuma ya mapazia Haya ya chokochoko.

      Sasa serikali iko kimya, inaachia raia wahukumiane.. Na hukumu ya raia ni ubaguzi Na Chuki vitazuka.. Kwanini serikali hii sio SIKIVUU..

      Mrisho.. Muda wako uliobaki ni kidogo.. Usipobadili mwelekeo nakwambia Utaona 2 years Kama gunia la Miaka Elfu ..
      Wakati mwingine chama tawala ndiyo kete kiliyobaki nayo!! Naimani waislamu wengi hii kitu haiwanyimi usingizi ila BAKWATA.
      "The usual conclusion is that you can't put a price on a human life. But you can if you must".

    13. #132
      Mwanamayu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th May 2010
      Location : Manzese
      Posts : 3,049
      Rep Power : 1072
      Likes Received
      240
      Likes Given
      112

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Tume ya katiba View Post
      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      Hapo kwenye red: hivi hizo takwimu zinazotolewa na hizo taasisi nyingine ni kwamba zina walakini au vipi? Halafu kwa nini wasilipe kampuni lolote likawahesabu hawa jamaa na kujua idadi yao halafu wakafanya kahesabu kepesi kakuchua ile idadi ya jumla itakayotolewa na serikali na kutoa idadi yao iliyopatikana na hiyo kampuni binafsi halafu watajua idadi ya wasio waislamu!

      Hivi wanataka idadi ya waumini wa dini tofauti ili iweje?

      Waislamu waige mfumo wa taarifa wa RC wala haitakuwa mmesilimu!!

    14. #133
      ntamaholo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2011
      Location : Mwilavya
      Posts : 4,119
      Rep Power : 1391
      Likes Received
      919
      Likes Given
      412

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mbimbinho View Post
      Mkuu mbona huwa nakuona kwa Mzee wa Upako?

      Connect dots mkuu.
      kwani kwa mzee wa upako ni wakristo? si utambulisho wao ni miliki ya mzee wa upako?
      UTUMISHI WA HAKI, NI SULUHISHO LA MAOVU YOTE

    15. #134
      Ileje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th December 2011
      Posts : 1,120
      Rep Power : 603
      Likes Received
      436
      Likes Given
      120

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Katika hali ngumu ya maisha kama sasa wengi wangependa kupata ajira angalau waweze kujikimu! Hivyo wenzetu wanaomba uwakilishi katika sensa ili angalau waambulie posho! Kwi! kwi! kwi! kwi! ...........
      Never give up your right!

    16. #135
      Mr.Professional's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th October 2010
      Location : Dar
      Posts : 1,514
      Rep Power : 744
      Likes Received
      211
      Likes Given
      95

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      nchi hii inasafari ndefu sana ya kimaendeleo kama jambo la kujua idadi ya raia wakazi wa nchi kwa maendeleo ya nchi nalo linawekewa misingi ya udini. Kwani taifa likiwa lina waamini wa dini fulani wengi kuliko wengine itasaidia nini kwa ustawi wa taifa changa kama hili?

      Ingekuwa kuna upendeleo wa huduma kutokana na imani yako ya kidini basi hata mie ningeliwaunga mkono lakini tukienda mahospitalini au mashuleni au hata sokoni basi huduma tunapata sawia hawa haijalishi misingi yetu ya udini sasa hizi vurugu za udini kwenye taifa lisilo fungamana na imani yoyote zinatoka wapi kama sio kujaribu kuvuruga amani ya nchi?
      for further assistance please press "CTRL + W"

    17. #136
      Jibaba Bonge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th May 2008
      Posts : 1,006
      Rep Power : 769
      Likes Received
      145
      Likes Given
      61

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Tangu lini Bakwata walishiriki sensa? Nijuavyo sensa inahusisha mtu mmoja mmoja katika / na familia yake. Sensa haihusiani na taasisi yoyote iwe ya kidini ama la. Sensa inahusu wananchi mmoja mmoja.

      Serikali ina nia ya kujua idadi ya wananchi kwa ajili ya mipango yake. kama kuna taasisi, Bakwata, CCT, PCT, au shirikisho la mpira wanataka kujua idadi ya wadau wake inaweza kugharamia costs na kufanya sensa yake ni ruksa! Bakwata wanaweza kufanya sensa ya waislamu kwa utaratibu wao, say kwa kutumia misikiti, hivyo hivyo CCT au PCT wanaweza kutumia makanisa yao wakapata idadi ya waumini wao.

    18. #137
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya Agosti 2012

      Quote By Mbako View Post
      habari kwa wanajamii wote.leo kwa mshituko nimesoma tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya 2012. wanataka watu tuhesabiwe kwa idadi ya dini zetu.
      swali kwenu BAKWATA mnataka kujua mko wangapi ili iweje? mbona hamwishi vituko ?
      Ili malumbano ya nani wengi yaishe na tunataka ile 83/17 ikome.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    19. #138
      Ciril's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th January 2011
      Posts : 2,015
      Rep Power : 893
      Likes Received
      252
      Likes Given
      19

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Zimebaki siku chache maneno ya baba wa taifa yatimie.Hivi Leo hii Kama watu wazima tumeanza kuuzungumzia au kutaka kuuingiza udini kwenye mambo ya kitaifa.Haya tukimaliza kuingiza kipengele hichi cha udini au kesho tutazua lingine.

      Watanzania tumegeuka kuwa majuha kwa kujadili mambo yasiokuwa na tija,badala ya kujadili hali hii ngumu ya maisha inayotukabili kila uchwao!!!!Hii ni aibu yetu,na hili litakuwa janga letu siku za usoni.Sababu za ndugu zangu waislam kugomea sensa ni kutaka kipengele hichi cha dini(Yao)kiwepo,sasa mkishajua idadi ndio ili iweje!!?Nnawasihi sana ndugu zangu waislam huko tunapoelekea siko.Msikubali kupelekwa na misimamo ya viongozi wachache,ni lazima mpime jambo sio kulikubali mapema na kulichekelea.Sitaki kuamini Kama ni kweli waislam wote wanakubaliana moja kwa moja na misimamo au matamko ya viongozi wao ndio maana kuna wakati huwa zinazuka fujo misikitini.

      Serikali ya Tanzania inahitaji watanzania (wananchi/watu)ktk kuendeleza uchumi Wa nchi hii,vivyo hivyo Serikali inaziheshimu dini/imani zote za wananchi wake lakini kamwe haihitaji dini yeyote ktk ktk kutekeleza mipango yake.Kamwe watanzania tusijinasibishe ktk taifa hili kwa dini ya mtu/kabila la mtu/rangi(asili) ya mtu na mengine ya kufanana na hayo sababu yanaondoa umoja wetu na mshikamano tulionao.

      Mungu ibariki Tanzania

    20. #139
      simplemind's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2009
      Posts : 2,954
      Rep Power : 1180
      Likes Received
      531
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Ninaweza View Post
      Baada ya kujua idadi ya wana imani fulan!, nini kitafata?
      kukata keki ya taifa kulingana idadi ya waumini katika kila dini.

    21. #140
      Mdondoaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2009
      Posts : 4,731
      Rep Power : 1490
      Likes Received
      808
      Likes Given
      343

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By dotto View Post
      Wewe ni shia au suni maana hao si wamoja pia katika mipango yao kama ilivyo kwa wakristo pia ambapo kuna waanglikani, wakatoliki n.k. Inayofanya sensa ni serikali sasa wanadini wanataka takwimu za nini. Tatizo la Waislamu ni utawala uliogawanyika ambapo kupata idadi hao kwa sensa yao wenyewe ni kikwazo. Mfano. Utakuta shehe wa Tabora anaitwa kuja kufungisha ndoa hapa Lindi lakini shehe wa hapa Lindi hajui na hana taarifa yoyote. so, kumbukumbu ya msikiti wa hapa Jirani hawana records. Ni kukosa busara kwa Bakwata kutokuwa na mipango yake ya kujijua yenyewe na watu wake bali kutegemea vya bure toka serikalini. Yawezekana serikali ikawakubalia but matokeo yakaja kuwa wakristo wako wengi na hapo waislamu watakuja na hoja ingine ya kuwa takwimu zimechakachuliwa na hivyo NBS iundwe upya ili na dini zishiriki. Waislamu ni tatizo kubwa mno!!!
      Wewe shida yako nini? Mbona nyie mna TAG, Catholics, Lutheran and etc hamsemi? Hakuna kinachogawanyika huu ni upumbavu kwasababu suala la dini ya mtu lina umuhimu katika mipango miji ya nchi. Mfano Uingereza hamuwezi tu kujenga msikiti au kanisa hadi upewe kibali na halmashauri ya jiji. Sasa unadhani kwanini wamesisitiza halmashauri ndio zitoe vibali? Tatizo lenu mnasumbuliwa na UDINI TU!!!! Suala la dini lina umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu . Dini itatusaidi kujua yafuatayo nawaelekezi nchi vihiyo wa udini:-
      a. Tufahamu katika kila eneo ni nyumba za ibada ngapi zijengwe (misikiti, makanisa au masinagogi) na vile vile maeneo ya kuzikana yatengwe kiasi gani yaani makaburi. Hivyo basi dini itatusaidia katika mipango miji nchini mwetu.

      b. Tufahamu sababu za kurudi nyuma kimaendeleo (mfano waislamu) je imesababishwa na wao wenyewe? taasisi au mfumo mbovu uliopo?

      c. Tufahamu mfumo wa nchi kiutendaji unakuwaje tukijumuisha na imani za watu kama sehemu ya maisha yao mfano ni likizo ngapi ziwepo katika nchi kama sikukuu za mapumziko. Uingereza mfano au Marekani hawana kitu kinaitwa public holiday for Eid but wana public holiday for Christmas, New Year, St. Patricks etc. Saudi Arabia, UAE, na Oman hawana sikukuu za Christmas and New Year. Ni kwasababu ya sensa wameona hakuna umuhimu wa kupumzika siku hizo. Sasa taarifa hizo hakuna mahali zinatoka zaidi ya katika sensa ILIYOANDALIWA NA SERIKALI YA MLIPA KODI!!!!

      d. Kufahamu pia usambazi wa vyakula nchini. Mfano waislamu wana mwezi mtukufu wa ramadhani na huwa wanatumia vyakula vya aina fulani nchini. Vile vile wakristo wana Kwaresma huwa pengine wanatumia vyakula vya aina fulani. Hatuwezi kufahamu hilo bila ya kuwepo takwimu sahihi.

      Hembu nipeni nyie sababu za msingi kisiwepo kipengele cha dini zaidi ya fear zilizogubikwa na imani za ubaguzi wa kidini???

    Page 7 of 62 FirstFirst ... 5678917 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...