Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 62 of 62 FirstFirst ... 52606162
    Results 1,221 to 1,236 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 890
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.


    2. #1221
      mkataba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 147
      Rep Power : 379
      Likes Received
      35
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Bajabiri View Post
      suala la sensa lenyewe kwa ujumla wake halina tija sembuse kuweka kipengele cha dini
      Hata faida ya sensa sijaiona wala na mimi sitoshiriki, ikiwa itafanywa kama hamna kipengele cha dini sitoshiriki.

      Hakuna maendeleo yyte hapa Tz ni uhuni na ufisadi.

    3. #1222
      mkataba's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th July 2012
      Posts : 147
      Rep Power : 379
      Likes Received
      35
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By RGforever View Post
      Nadhani habari huwa zinakupita pembeni.... Imekatazwa Mtu yeyote awe mwanasiasa au Viongozi wa Dini kukataza Watu kushiriki Sensa na ikibainika Watachukuliwa sheria ya kutenda kosa la Jinai..-MKURUGENZI WA SENSA
      Kwanza wawakamate UAMSHO huko Zanzibar maana wametoa mpaka machapisho yanayowataka Wazanzibari waislam wasishiriki sensa na yamebandikwa kwenye nyumba nyingi sehemu tofauti huko Zenji.

    4. #1223
      kipili.pili's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th July 2012
      Posts : 34
      Rep Power : 355
      Likes Received
      5
      Likes Given
      2

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By David webb View Post
      Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

      Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

      Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
      ingekuwa hivyo mbona lipumba angeshinda.kwasababu cuf =islam.

    5. #1224
      hassan hamad's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th June 2012
      Posts : 28
      Rep Power : 358
      Likes Received
      5
      Likes Given
      1

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Ndugu zangu Waislamu, tunataka kuhesabiwa lakini je tuko tayari kupokea majibu? Je tukikuta wakristu ndo wengi, tuko tayari kuwaruhusu watangaze Jamhuru ya kikristo?
      Siasa kali ya udini haijawahi kujenga nchi kokote duniani. "somalia waliuana na uislamu wao" na "Rwanda waliuana na ukristo wao". Na isitoshe, mwislam wa leo ndo mkristo wa kesho na mkristo wa leo ndo mwislamu wa kesho.
      Kama kweli BAKWATA wameamua waislamu tusishiriki katika sensa waetupoteza, wakumbuke wanamuharibia mwislamu mwenzetu utwala wake.

    6. #1225
      Asa79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th July 2012
      Posts : 591
      Rep Power : 466
      Likes Received
      162
      Likes Given
      10

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Waiuslamu wanatak tz iige kila kinachofanyika na nchi fulani..................sio kuiga kila kitu hata ambacho hakina faida kwa watz wote sisi ni taifa huru ni lazima tuwe na uamuzi na mambo tunayoona yanafaa kwa mustakabali wa amani na umoja wetu.........
      Mbona kila mtu anajua kuwa wakristo ni 60% waislamu ni 23% na the rest ni mchanganyko?


    7. #1226
      Asa79's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th July 2012
      Posts : 591
      Rep Power : 466
      Likes Received
      162
      Likes Given
      10

      Default

      Quote By opaque View Post
      ushauri wangu kwa waisilamu:

      - shiriki sensa
      - ukiulizwa maswali ukaona jamaa amemaliza bila kukuuliza dini yako, mwambie mimi ni muisilamu

      waislamu zingatieni ushauri huu muhimu kuliko kuumiza vichwa posipo sababu..........hivi uislamu unafundisha kulalamika tu kila wkt na hakuna mambo mengine ya kuzungumzia?

    8. #1227
      Chiya Chibi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th July 2011
      Location : Penye Oxygen
      Posts : 441
      Rep Power : 491
      Likes Received
      102
      Likes Given
      12

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Kwan kuna faida gan mkishajua kuwa mpo wengi au mpo wachache kuliko wengine..? Asilimia kubwa ya Wanzanzibar ni waislam, Je idad hiyo imewasaidia nin waislam wa Zanzibar.? Je hizo data zilizotolewa kwenye taasis mbalimbal nchin zikionyesha uchache wa Waislam, zimewaathir vp waislam na zimewanufaisha vp wakristo.? Je yup mtamsikiliza, Kat ya mashekh wa Bakwata (wanaogomea) na Shekh mkuu (aliyekubali).? Je Bakwata wana data (Idad) gan ya waislam wao na wamewasaidia vp waislam hao.?
      Last edited by Chiya Chibi; 23rd July 2012 at 09:55.

    9. #1228
      Ileje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th December 2011
      Posts : 1,120
      Rep Power : 603
      Likes Received
      436
      Likes Given
      120

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Waislamu bana wanadeka!
      • Hatushiriki sensa!
      • Tunataka OIC!
      • Baraza la mitihani livunjwe!
      • Idadi ya ma-DC wa kiislamu waongezwe!
      • Idadi ya ma-REO wa kiislamu waongezwe!
      • Waalimu wakuu waislamu waongezwe!
      • Tunataka Khadhi!
      • Khadhi aliyeteuliwa na Mufti hajasoma sharia wala hawezi kuunda idara!
      • Mufti ni wa BAKWATA na siyo wa waislamu!
      • nk!

      Lini mtaacha kulalama na kujikita katika maendeleo e.g. kujenga mashule na vyuo, kujenga hospitali nk
      Never give up your right!

    10. #1229
      abousalah2's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th June 2012
      Posts : 76
      Rep Power : 367
      Likes Received
      6
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA haitoshiriki zoezi la Sensa mwaka huu......!!

      Quote By Matola View Post
      Hii Habari siwezi kuiamini haina ukweli wowote, Bakwata ni tawi la CCM sasa ni kitu ambacho hakiwezekani kupingana na Serikali yao wanayoitumikia, kama kuna kauli ya namna hii imetolewa basi itakuwa ni ya yule muhuni anayeitwa Shekh Ponda ambaye yuko kwenye jumuiya nyingine ambayo haina tofauti na UAMSHO.
      TAFAKARI KABLA YA KUNENA! SHEIKH kundecha ni mtu muadilfu mno uadilfu ambao hata huyo pengo, mukiwa na wngine wengi waliopotea katika njia ya M/MUNGU hawaufikii uadilifu wake, hivi huyu kundecha amekumbana na moja ya mambo yafuatayo! amewahi kubaka? amewahi kudhulumu? amewahi kuuza madawa ya kulevya? amewahi kulawiti? acheni upungufu wa fikra ni nani uamsho? punguzeni kula nguruwe musiwe wapungufu wa akili kiasi hicho! UAMSHO ni taasisi ya karaia iliyopo kisheria na sasa tunakubalika za wazanzibar zaid ya 90%, UAMSHO imewatibu wa zanzibar wangapi? FUATILIA TAKWIMU! Tumesomesha wangapi? na tumehudumia wangapi? Nataka mufahamu kuwa tuna uhusiano mzuri wa balozi wa america, israel na uk! fuatilia uchaguzi wa zanzibar 2010 jee uamsho walikuwa nafasi gani? acheni pumba na musijidanganye tunajua mengi juu ya mkakati wenu mchafu juu yetu. fuatilia semina ya baraza la wawakilishi 21- 22 july 2012 . Sensa haina umuhimu kwetu! sisi kam UAMSHO tunawapongeza bakwata katka hili
      takashi likes this.

    11. #1230
      Mtz.mzalendo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd July 2012
      Posts : 295
      Rep Power : 407
      Likes Received
      39
      Likes Given
      3

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Selikali isipokuwa makini sensa haitafanikiwa hivyo mimi nashauri kigezo cha dini kiingizwe kama hakitakuwa madhara kwa nchi,kwani itakuwa hasara kwa taifa kwa kupoteza pesa za watz bila sababu.

    12. #1231
      Ennie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2011
      Location : DAR ES SALAAAM
      Posts : 1,599
      Rep Power : 822
      Likes Received
      501
      Likes Given
      539

      Default

      Quote By kipili.pili View Post
      ingekuwa hivyo mbona lipumba angeshinda.kwasababu cuf =islam.
      Too low. Yaani mpaka leo unamchagua mtu kwa kuangalia dini yake!

    13. #1232
      Ennie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th January 2011
      Location : DAR ES SALAAAM
      Posts : 1,599
      Rep Power : 822
      Likes Received
      501
      Likes Given
      539

      Default

      Quote By Asa79 View Post
      Waiuslamu wanatak tz iige
      kila kinachofanyika na nchi fulani..................sio kuiga kila kitu
      hata ambacho hakina faida kwa watz wote sisi ni taifa huru ni lazima
      tuwe na uamuzi na mambo tunayoona yanafaa kwa mustakabali wa amani na
      umoja wetu.........
      Mbona kila mtu anajua kuwa wakristo ni 60% waislamu ni 23% na the rest
      ni mchanganyko?
      Hizi takwimu zenu za kuokoteza bila kutaja source ni sensa ya mwaka gani ndio zinaleta yote haya.

    14. #1233
      Hayajamani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd July 2012
      Location : Utopia
      Posts : 625
      Rep Power : 476
      Likes Received
      174
      Likes Given
      404

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Kweli tofauti ipo! Hii ni shida, maswala ya dini ni ubaguzi usio na maana. Sisi wote ni Watanzania haijalishi tumechukua itikadi gani ya kigeni. Haya madini makubwa yote ni maitikadi ya wageni waliotuletea hivyo tusijifanye tunajua sana. Kitu cha Mwarabu na Mzungu kipi genuine? Kazi kwenu
      MPIGA ZEZE likes this.

    15. #1234
      ralphjn's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 1st June 2012
      Posts : 126
      Rep Power : 380
      Likes Received
      13
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By ntamaholo View Post
      hivi hamwezi kuhesabiana ninyi kwa ninyi? mbona kila kanisa linajua lina waumini wangapi active na inactive, ninyi mmeshindwa nini?
      Hawa wenzetu huwa wanapenda kufanyiwa kila kitu,Mahakama ya kadhi serikali iwaanzishie,Bakwata inahudumiwa na serikali 100%,chuo kikuu wamepewa na serikali kimewashinda.what do u expect?

    16. #1235
      Billie's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 13th August 2011
      Posts : 1,795
      Rep Power : 817
      Likes Received
      462
      Likes Given
      186

      Default

      Quote By Opaque View Post
      Ushauri wangu kwa waisilamu:

      - Shiriki sensa
      - Ukiulizwa maswali ukaona jamaa amemaliza bila kukuuliza dini yako, mwambie mimi ni muisilamu
      Teh teh teh nimecheka sana nimependa ulivyosolve tatizo kirahisi mno.

    17. #1236
      PAMOKONUNDA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd July 2012
      Posts : 32
      Rep Power : 357
      Likes Received
      4
      Likes Given
      7

      Default Re: Sheikh ponda na wenzio muheshimuni mufti simba

      Quote By Malumbano View Post
      alieunda bakwata ashafariki. Mwalimu nyerere kwa nia ya kuundamiza uislam.
      waambie hao mzee.....safi sana

    Page 62 of 62 FirstFirst ... 52606162

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...