Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 56 of 62 FirstFirst ... 465455565758 ... LastLast
    Results 1,101 to 1,120 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 886
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. FemaTV & Radio

    3. #1101
      Simiyu one's Avatar
      Member Array
      Join Date : 16th June 2012
      Posts : 27
      Rep Power : 354
      Likes Received
      4
      Likes Given
      1

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      waislam bana, hivi nani ana authority ya kutoa kauli ya waislam Tanzania kati ya Shekh Mkuu na Shekh Kundecha?

    4. #1102
      msasa's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th November 2008
      Posts : 81
      Rep Power : 550
      Likes Received
      1
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      hili swala liko wazi kabisa ni mvutano kati waislam na serikali japokuwa nimeona hapa kuna mvutano kati ya waislam na wasiokuwa waislam, sababu za waislam kupinga sensa hadi dodoso la dini liwekwe kwenye sensa wamezitaja, katika kuthibitisha hilo TBC waliomba radhi kwa waislam. sasa ifike mahala tuishie hapa tuwaache waislam na msimamo wao, na serikali ifanye hiyo SURVEY yake.

    5. #1103
      Seif al Islam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th November 2011
      Posts : 1,079
      Rep Power : 538
      Likes Received
      261
      Likes Given
      393

      Default Sheikh ponda na wenzio muheshimuni mufti simba

      nimesikitishwa sana na kitendo cha kiongozi wa jumuiya za kiislam ndugu yangu sheikh issa ponda kutangaza kuwa waislamu wasishiriki sensa kinyume na taarifa aliyoitoa mufti simba.mufti simba hata kama hautaki ndiye kiongozi mkuu wa waislamu hapa tanzania,kimsingi ndiye msemaji mkuu wa waislamu kama alivyo pengo kwa wakatoliki.kitendo cha kumpinga na kumdhalilisha mufti simba hadharani kinashusha hadhi ya mufti ,uislamu na waislamu wenyewe.hapa ndipo tunapoonekana watu tuliokosa maarifa na ujzi achilia mbali elimu.haiwezi kutokea padre yeyote akampinga pengo iweje sis waislamu tuanze kupingana na mufti wetu/huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na unapaswa kusitishwa mara moja.
      The Boss likes this.

    6. #1104
      Malaria Sugu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 2nd August 2009
      Posts : 1,783
      Rep Power : 0
      Likes Received
      246
      Likes Given
      18

      Default Re: Sheikh ponda na wenzio muheshimuni mufti simba

      Quote By seif al islam
      nimesikitishwa sana na kitendo cha kiongozi wa jumuiya za kiislam ndugu yangu sheikh issa ponda kutangaza kuwa waislamu wasishiriki sensa kinyume na taarifa aliyoitoa mufti simba.mufti simba hata kama hautaki ndiye kiongozi mkuu wa waislamu hapa tanzania,kimsingi ndiye msemaji mkuu wa waislamu kama alivyo pengo kwa wakatoliki.kitendo cha kumpinga na kumdhalilisha mufti simba hadharani kinashusha hadhi ya mufti ,uislamu na waislamu wenyewe.hapa ndipo tunapoonekana watu tuliokosa maarifa na ujzi achilia mbali elimu.haiwezi kutokea padre yeyote akampinga pengo iweje sis waislamu tuanze kupingana na mufti wetu/huu ni udhalilishaji wa hali ya juu na unapaswa kusitishwa mara moja.
      alieunda bakwata ashafariki. Mwalimu nyerere kwa nia ya kuundamiza uislam.

    7. #1105
      The Boss's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th August 2009
      Location : DARESALAAM
      Posts : 18,164
      Rep Power : 21615
      Likes Received
      13492
      Likes Given
      17791

      Default Re: Sheikh ponda na wenzio muheshimuni mufti simba

      ina maana hawajajifunza kutoka Muslim Brotherhood ??????????
      Watch your thoughts,They become words, Watch your words, They become deeds, Watch your deeds, They become habits, Watch your habits, They become character, Watch your character, It becomes your destiny!

    8. Miaka 50

    9. #1106
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,480
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4300
      Likes Given
      1248

      Default

      Quote By kanyi
      Huyu atakuwa hajasikia habari kuwa Pilau litakuwepo
      kweli kabisa!

      Umeni furahisha sana

      pata like yangu

    10. #1107
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,480
      Rep Power : 19785
      Likes Received
      4300
      Likes Given
      1248

      Default

      Quote By Malumbano
      harakati za waislam hazifanywi na bakwata. Waislam tunamuamini ponda
      ina maana wewe unampinga mufti?

      Kwahiyo we na ponda ni ndugu wa mawazo?

      Hata wanazuoni wakiislam hauwatambui?

      Basi wewe siku hiyo lala wenzio wana openda kuhesabiwa wahesabiwe.

    11. #1108
      Ponera's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd December 2011
      Posts : 178
      Rep Power : 412
      Likes Received
      16
      Likes Given
      107

      Default Re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Ikitokea kunawatu wakamsikiliza ponda hata kama wachache tayari atakuwa amefanikiwa kwani serikali na wakristo hawatajua idadi ya hoa wafuasi wa ponda, msimamo daima?

    12. #1109
      Ponera's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd December 2011
      Posts : 178
      Rep Power : 412
      Likes Received
      16
      Likes Given
      107

      Default Re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Bigirita
      Kama nyie wenyewe mnabaguana, hicho mnachopigania mtakipata kweli??!
      Quote By only83
      Hapo ndipo uwa nawashangaa waislamu..ni watu wa ajabu na kusikitikia sana. Tazama, baada ya kelele zao za muda kuwa wanagomea sensa kiongozi wao katepeta tena hoi. Ni kweli kuwa BAKWATA ni moja ya taasisi za CCM japo waislamu hawataki kusema wazi hilo na wanajua vyema. Hii ni dalili kuwa kuna waislamu wanaleta chokochoko binafsi wakati taasisi yao imekaa na kutoa tamko hilo. Huyo Ponda anawezaje kupingana na mawazo ya taasisi kubwa na yenye uwakilishi wa waislamu wote?

      Nimekuwa nikisema hapa mara nyingi uislamu ni dini nzuri ila kuna wahuni na wajinga wachache wanaifanya ionekane kama dini ya kigaidi na wapenda vurugu nk. Mufti kadhihirisha ukweli kuwa Radio Imaan na TV imaan ni majanga kwa taifa hili. Ni wachochezi na wavuruga amani.
      Hata nyie mnapingana na ndomaana kunamaaskofu wanakubali ushoga wengine wapinga, bakwata sio ya waislam wote, bakwata ni ya waislam ccm, we unakubali ndoa ya jinsia moja?

    13. #1110
      Ponera's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd December 2011
      Posts : 178
      Rep Power : 412
      Likes Received
      16
      Likes Given
      107

      Default Re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Bigirita
      Kama nyie wenyewe mnabaguana, hicho mnachopigania mtakipata kweli??!
      Quote By Lawkeys
      Nahisi kama uwezo wa watu kufikiri umepungua kwa kiasi kikubwa sana. Hivi kweli watu wenye akili timamu wanaweza wakaja na hoja za kipuuzi namna hii kupinga vitu vya msingi namna hii!

      Hawa jamaa nadhani wana kiu sana ya damu, sijui wanataka kuyanywesha yale yaliyofukuzwa mbinguni? Yaani kila kukicha wanatafuta sababu za kuvuruga amani! Washindwe katika Jina la YESU.
      Ushindwe wewe kafiri

    14. #1111
      Makala Jr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th August 2011
      Posts : 1,614
      Rep Power : 713
      Likes Received
      334
      Likes Given
      0

      Default

      [QUOTE=zomba;4143718]83/17 huijui?[/QU Siyo tu kama siijui bali pia sijawahi kuisikia labda ufafanue zaidi mkuu!

    15. #1112
      Makala Jr's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th August 2011
      Posts : 1,614
      Rep Power : 713
      Likes Received
      334
      Likes Given
      0

      Default

      [QUOTE=Ndechumia;4148104]akili ndogo inaongoza akili kubwa[/QU Akili ndogo ni ya nani na kubwa ni ya nani?

    16. #1113
      Sayfulhaq's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd April 2012
      Posts : 64
      Rep Power : 369
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Ticha
      Waislamu hawakutaka wao kuhesabiwa ila walikuwa wanaomba kipengere cha dini kiwepo kama zinavyowekwa katika fomu mbalimbali kama umewahikutana kujaza,mfano za utumishi zipo zenye kipengere hiki,za vyuo nk.

      Lakini jambo hili kwa sasa halipo tena kama jumuia ya waislam lilisha sawazishwa na tamko la kufuta kauli hiyo ilishatolewa na mamlaka husika.

      Kama bado lipo basi ni kwa matakwa ya mtu binafsi,ajitokeze hapa aeleze lengo lake ni nini.
      lengo lake kuu ni kutaka usawa ktk potential areas mbalimbali za kinchi ili kile kisemwacho AMANI ktk TZ yetu kiendelee kuwepo. Kisitumike kigezo kuwa eti uwepo wa wakristo wengi madarakani ni kwa sababu ya wingi wao, na uwepo wa waislamu wachache eti ni kwa sababu ya uchache wao. Kuliondosha hili bac zoezi la sensa lihusishe hicho kipengele cha dini ili justice na fairness iwe administered. Na co kutegemea takwimu za upogo zinazofanywa na mashirika mbalimbali.
      Kama una akili salama nadhani utakuwa umelifahamu lengo.

    17. #1114
      Sayfulhaq's Avatar
      Member Array
      Join Date : 22nd April 2012
      Posts : 64
      Rep Power : 369
      Likes Received
      9
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Gandagumu
      Hivi endapo mtagoma then zoezi likafanyika,mtafaidika nini? Naamini siyo wote,naomba wanaJF wenye data mwageni hapa-kwa nini waislamu wanataka wajue idadi yao tofauti na wapagani na Wakristo
      sababu wanataka usawa kwa watu wote ktk madaraka ya idara zote za serikali.

    18. #1115
      Mohamed Said's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd November 2008
      Posts : 4,538
      Rep Power : 1757
      Likes Received
      2390
      Likes Given
      166

      Default Re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      [QU=majebere;4122398]Sasa mkishajua kuna waislamu wengi itawasaidia nini?[/QUOTE]

      Kaka umeuuliza swali kuwa tukishajua sie wengi itatusaidia kitu gani.
      Labda ningekuuliza kipi kinachowatisha kama idadi ya Waislam itajulikana?

      M

    19. #1116
      Physics's Avatar
      Member Array
      Join Date : 14th June 2012
      Posts : 20
      Rep Power : 353
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By mnazareti
      Connection ya dini na sensa siipati. Huu ni udini uliokithiri
      kwasababu ww ni mnazareti.

    20. #1117
      Cheida's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 3rd July 2012
      Posts : 5
      Rep Power : 348
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Kwa hili la sensa waislamu mtachemka

      Tatizo halipo kwenye waumini wa kiislamu kukataa kuhesbiwa katika sensa ya taifa bali ni tatizo lililojitokeza hivi karibun kuna mtu na ofic yake ikiwa na kalenda lenye kuonesha tatthmini ya idadi ya watanzania kwa ujumla..Eti 70%ya watanzania ni waumini wa dini ya kikristo na 30% ni waislamu hivyo kutokana na idadi hiyo waumini wa kiislamu tumeweza kupinga juu ya hilo mpaka kiingizwe cha udini na kubainisha wepi wengi na si kukaa kwa watu fulani wakatoa tu tathmini, na hiyo pia bodi ya sensa iwe na usawa kwa waumini katika ngazi zote na ngazi zote,,Hapo tutashiriki kikamilifu

    21. #1118
      BabieWana's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 136
      Rep Power : 461
      Likes Received
      17
      Likes Given
      0

      Default Waislam wakataa kuhesabiwa sensa bila kipengele cha dini

      waislam wamekataa kuhesabiwa kwenye kongamano lilofanyika jumapili jijini Arusha
      wakitoa msimamo wao wamesema hawaoni umuhimu wa kuhesabiwa bila kipengele cha DINI kwani kilikuwepo kikaondolewa bila maelezo sasa waislam wanataka kipngele hicho kirudi tupate takwimu sahihi ambazo zitatumika na wadua wa maendeleo na jamii mbalimbali, kinnachoshangaza ni kwamba watahesabu nyumba za ibada bila kuwahesabu wanaosali humo. idadi ya misikiti na makanisa yanini wakati wanaosali humo hawahesabiwi.

      waislam waweke bango la "Hatuhesabiwi" kwenye milango yao


      mwongozo wa sensa wa UN unaelekeza kipengele cha dini na dhehebu kiwepo angalia website yake un.org
      Careboy wamuntere likes this.

    22. #1119
      Las Mas Bobos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th June 2012
      Posts : 940
      Rep Power : 537
      Likes Received
      302
      Likes Given
      84

      Default Re: Waislam wakataa kuhesabiwa sensa bila kipengele cha dini

      Quote By BabieWana
      waislam wamekataa kuhesabiwa kwenye kongamano lilofanyika jumapili jijini Arusha
      wakitoa msimamo wao wamesema hawaoni umuhimu wa kuhesabiwa bila kipengele cha DINI kwani kilikuwepo kikaondolewa bila maelezo sasa waislam wanataka kipngele hicho kirudi tupate takwimu sahihi ambazo zitatumika na wadua wa maendeleo na jamii mbalimbali, kinnachoshangaza ni kwamba watahesabu nyumba za ibada bila kuwahesabu wanaosali humo. idadi ya misikiti na makanisa yanini wakati wanaosali humo hawahesabiwi.

      waislam waweke bango la "Hatuhesabiwi" kwenye milango yao


      mwongozo wa sensa wa UN unaelekeza kipengele cha dini na dhehebu kiwepo angalia website yake un.org
      Nenda wewe ukaweke bango nyumbani kwa yule muislamu wa magogoni na yeye asihesabiwe.

      Sura mbaya kama UN
      By the time a man comes to realize that his father was right, he usually has a son who think he is wrong.

    23. #1120
      yaya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th June 2011
      Posts : 676
      Rep Power : 535
      Likes Received
      210
      Likes Given
      67

      Default Re: Waislam wakataa kuhesabiwa sensa bila kipengele cha dini

      waislam waweke bango la "Hatuhesabiwi" kwenye milango yao
      mwongozo wa sensa wa UN unaelekeza kipengele cha dini na dhehebu kiwepo angalia website yake un.org[/QUOTE]

      Mkuu, ahsante kwa taarifa. Umenisaidia sana. Awali nilikuwa sijui kwamba kumbe sensa ni kwa mujibu wa maelekezo ya UN. Na kwa sababu hiyo ni lazima kufuata format ya madodoso ya UN yanayotaka kujua kuna misikiti na makanisa mangapi na pia idadi ya waumuni na madhehebu yao!!!???

    Page 56 of 62 FirstFirst ... 465455565758 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...