Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 46 of 62 FirstFirst ... 36444546474856 ... LastLast
    Results 901 to 920 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 887
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #901
      majebere's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 2,210
      Rep Power : 0
      Likes Received
      322
      Likes Given
      111

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Malumbano
      harakati za waislam hazifanywi na bakwata. Waislam tunamuamini ponda
      Mnamuamini kama nani vile? Watu wana muamini mungu halafu wewe unamuamini ponda

    4. #902
      MwanaFalsafa1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Posts : 5,451
      Rep Power : 9880
      Likes Received
      615
      Likes Given
      448

      Default

      Mbona wote huyo sheikh Ponda na Mufti wana wasemea Waislamu. Kama kweli ni msimamo wa Waislamu wa Tanzania (na si taasisi tu) ni wapi walifanya survey yoyote ya kujua waislamu wanataka nini? Hamuwezi amui kitu kama taasisi halafu mdai ni msimamo wa waislamu. Je kama waislamu walio wengi wana pingana nao? Fanyeni utafiti wa nini Waislamu wanacho taka kisha toeni matokeo ya uchunguzi huo na mseme Waislamu asilimia fulani wana msimamo fulani. Otherwise waache kusingizia ni msimamo wa Waislamu wote na waseme ni ni msimamo wa taasisi zao binafsi.
      Peasant likes this.

    5. #903
      Robato's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th June 2012
      Posts : 31
      Rep Power : 357
      Likes Received
      10
      Likes Given
      18

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Malumbano
      kINACHOFURAHISHA ZAIDI HARAKATI ZA WAISLAM HAZIFANYWI NA MMUFTI WALA BAKWATA. UDINI WATZ WALIOIBUA SIO BAKWATA. SENSA NOOOOOOO. WATAFANYA WAKIRISTO NA WAPAGANI
      Mtalia weee, mtagalalaaaa, mtarusharusha miguuu mpaka visigino vichubuke! lakini SENSA tutawahesabu tu!

    6. #904
      Kinyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2008
      Posts : 1,883
      Rep Power : 944
      Likes Received
      236
      Likes Given
      378

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Waungwana naombeni mniambie Sheikh Ponda ni mwenyeji mkoa gani hapa TANZANIA
      FJM likes this.
      Together in Poverty Apart in Riches

    7. #905
      Malaria Sugu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 2nd August 2009
      Posts : 1,783
      Rep Power : 0
      Likes Received
      246
      Likes Given
      18

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By majebere
      Yeye kama hataki kuhesabiwa basi asifungue mlango siku ya sensa. Hawa ndio wale mashehe njaa.
      nYIE SEMENI CHADEMA HADI MUMIIZE KICHWA. WAKIRISTO SI MJIHESABU TU KWA KUSHIRIKIANA NA SEREKALI?

    8. Miaka 50

    9. #906
      majebere's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 2,210
      Rep Power : 0
      Likes Received
      322
      Likes Given
      111

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By MwanaFalsafa1
      Mbona wote huyo sheikh Ponda na Mufti wana wasemea Waislamu. Kama kweli ni msimamo wa Waislamu wa Tanzania (na si taasisi tu) ni wapi walifanya survey yoyote ya kujua waislamu wanataka nini? Hamuwezi amui kitu kama taasisi halafu mdai ni msimamo wa waislamu. Je kama waislamu walio wengi wana pingana nao? Fanyeni utafiti wa nini Waislamu wanacho taka kisha toeni matokeo ya uchunguzi huo na mseme Waislamu asilimia fulani wana msimamo fulani. Otherwise waache kusingizia ni msimamo wa Waislamu wote na waseme ni ni msimamo wa taasisi zao binafsi.
      hawa wanatafuta misaada ya mwezi wa ramadhani, ndio karibu wakati wake.

    10. #907
      Bigirita's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th February 2007
      Location : Under a mango tree
      Posts : 11,269
      Rep Power : 3044
      Likes Received
      3057
      Likes Given
      4144

      Default

      Quote By Malumbano
      kINACHOFURAHISHA ZAIDI HARAKATI ZA WAISLAM HAZIFANYWI NA MMUFTI WALA BAKWATA. UDINI WATZ WALIOIBUA SIO BAKWATA. SENSA NOOOOOOO. WATAFANYA WAKIRISTO NA WAPAGANI
      Kama nyie wenyewe mnabaguana, hicho mnachopigania mtakipata kweli??!
      Peasant likes this.

    11. #908
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1255
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default

      Quote By Malumbano
      harakati za waislam hazifanywi na bakwata. Waislam tunamuamini ponda
      bila umoja nakuhakikishia 100% hamuwezi ku achieve kitu chochote zaidi ya kitengeneza migogoro yenu mingine...poleni sana...!

    12. #909
      kelvito's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th May 2012
      Posts : 388
      Rep Power : 522
      Likes Received
      97
      Likes Given
      74

      Default

      Quote By ruttashobolwa
      Sasa huyu ni gaidi anatakiwa akamatwe.

      Serikali naomba imuangalie huyu mtu ni tishio kwa usalama wa nchi.
      Mkuu si unajua udhaifu wa jk hawezi kufanya hvyo!

    13. #910
      Malaria Sugu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 2nd August 2009
      Posts : 1,783
      Rep Power : 0
      Likes Received
      246
      Likes Given
      18

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By kinyungu
      waungwana naombeni mniambie sheikh ponda ni mwenyeji mkoa gani hapa tanzania
      kijiji cha vaertican kiliopo dar

    14. #911
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 12,014
      Rep Power : 24158
      Likes Received
      4736
      Likes Given
      2652

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Kinyungu
      Waungwana naombeni mniambie Sheikh Ponda ni mwenyeji mkoa gani hapa TANZANIA
      Mkoa wa BURUNDI

      Soki Ozali Mwasi Yaka, Soki Ozali Mobali Koya Te

    15. #912
      Power G's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 20th April 2011
      Location : Msoga Kijijini
      Posts : 2,413
      Rep Power : 993
      Likes Received
      776
      Likes Given
      261

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      "Uislam ni dini siyo imani", mwisho wa mapambano tutaona ni nani mwislam wa kweli Ponda au Mufti.
      TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE MENO KAMA AKINA EL, JK, EC na RA

    16. #913
      majebere's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 2,210
      Rep Power : 0
      Likes Received
      322
      Likes Given
      111

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Malumbano
      nYIE SEMENI CHADEMA HADI MUMIIZE KICHWA. WAKIRISTO SI MJIHESABU TU KWA KUSHIRIKIANA NA SEREKALI?
      sasa na wewe Chadema imehusika vipi hapa?

    17. #914
      Nivea's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st May 2012
      Posts : 5,691
      Rep Power : 16249
      Likes Received
      3145
      Likes Given
      4061

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Safari_ni_Safari
      Hivi wajumbe wa tume ya sensa huyu Ponda anadhani wanapatikananje na wanafanya kazi zipi?
      jamani wapelekeni watoto wenu shule unaona watu wanavyozeeka vibaya huku ?tatizo ni elimu ndogo yeye anafikiri wajumbe wa sensa wanapatikana kama unavyochagua nyanya sokoni hii safi hii mbaya du!la hasha sensa its all about keeping recods watu wa recods management au hawajui maana halisi ya sensa ref:Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kupata na kurekodi habari kuhusu watu na makazi yao.
      jamani ni kweanini hawa watu wanapend a kulazimisha mambo jamani mfano:zimetolewa nafasi hizo watu wakaaply vigezo vimezingatiwa waislam hawakumeet reqremt je tuwachukue watu watakao tuharibia sababu yakuogopa minung'uno yao?MWAMBIENI HIVI HII NI DUNIA NYINGINE SIO ILE ALIYOZALIWA YEYE KUMEKUCHA ,AMUULIZE NYERERE KWANINI ALIACHIA MADARAKA ,ALIONA DUNIA ALIYOIZOEA NA WATU ALIOZOEA KUWAONGOPEA SIO TENA NI KIZAZI KIPYA .SO ASITULETEE HAPA !AKHA
      Safari_ni_Safari likes this.
      Kosea njia utaelekezwa,lakini usikosee mtu wakuoa /kuolewa naye,vinginevyo majuto yatakuwa sehemu ya maisha yako.tuliza kichwa unapochagua mwenzi wa maisha.

    18. #915
      Malaria Sugu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 2nd August 2009
      Posts : 1,783
      Rep Power : 0
      Likes Received
      246
      Likes Given
      18

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By kelvito
      mkuu si unajua udhaifu wa jk hawezi kufanya hvyo!
      naskia jana mumemtuma mbowe kuwakilisha bungeni. Hotuba yake imejaa udini

    19. ck1
      #916
      ck1's Avatar
      Member Array
      Join Date : 19th December 2011
      Posts : 19
      Rep Power : 378
      Likes Received
      5
      Likes Given
      0

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Kuna dini nyingi hapa duniani lakini ki ukweli waislam wananiboa
      19don likes this.

    20. #917
      Malaria Sugu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 2nd August 2009
      Posts : 1,783
      Rep Power : 0
      Likes Received
      246
      Likes Given
      18

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By nivea
      jamani wapelekeni watoto wenu shule unaona watu wanavyozeeka vibaya huku ?tatizo ni elimu ndogo yeye anafikiri wajumbe wa sensa wanapatikana kama unavyochagua nyanya sokoni hii safi hii mbaya du!la hasha sensa its all about keeping recods watu wa recods management au hawajui maana halisi ya sensa ref:Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kupata na kurekodi habari kuhusu watu na makazi yao.
      nDIO HOJA ZENU ZA KILA. MNAOGOPA MKIJUA WAISLAM WAPO WENGI HALAFU NYINYI NDIO MLIOSHIKA NCHI YENYE UFISADI WA KUTISHA. HAMNA JENGINE MNALOOGOPA.

    21. #918
      majebere's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 2,210
      Rep Power : 0
      Likes Received
      322
      Likes Given
      111

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Bigirita
      Kama nyie wenyewe mnabaguana, hicho mnachopigania mtakipata kweli??!
      ponda na mufti si wagawane tu hiyo misaada kuliko kugombania.

    22. #919
      Malaria Sugu's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 2nd August 2009
      Posts : 1,783
      Rep Power : 0
      Likes Received
      246
      Likes Given
      18

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By ck1
      kina dini nyingi hapa duniani lakini ki ukweli waislam wananiboa
      hahaha. Hata thienry henry aliwahi kusema hayo. Sasa tunae

    23. #920
      majebere's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 2,210
      Rep Power : 0
      Likes Received
      322
      Likes Given
      111

      Default re: Sheikh Ponda apinga kauli ya Mufti; Asisitiza waislamu kutoshiriki sensa

      Quote By Malumbano
      nDIO HOJA ZENU ZA KILA. MNAOGOPA MKIJUA WAISLAM WAPO WENGI HALAFU NYINYI NDIO MLIOSHIKA NCHI YENYE UFISADI WA KUTISHA. HAMNA JENGINE MNALOOGOPA.
      Sasa mkishajua kuna waislamu wengi itawasaidia nini?

    Page 46 of 62 FirstFirst ... 36444546474856 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...