Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 42 of 62 FirstFirst ... 32404142434452 ... LastLast
    Results 821 to 840 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 890
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. #821
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,686
      Rep Power : 821
      Likes Received
      237
      Likes Given
      1

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By MC babuu View Post
      Maswala ya udini hayana maana yeyote kwenye sensa ni ubinafsi wetu tu serkal inataka kujua idadi ya watu pekee kama tunaitaji kujua idadi yetu mufti mkuu awasiliane na masheh nchi nzima ili mtuhesabu ila sijui kama ina maana yoyte zaidi ya ubaguz
      Ubaguzi kivipi? hebu tufafanulie
      Quote By MC babuu
      mimi siwezi kugomea sensa sababu najua maana yake.mtafanya mpaka dini nyingine watucheke na kutuona wajinga tunajishusha hadhi wenyewe
      kama unaona kushiriki kwako katika sensa kutakusaidia ili watu wa dini nyingine wakuone wewe ni muerevu shiriki! lakini usisahau kuwa Quran inakwambia:
      Quran 2:120. "Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao. Sema: Hakika uwongofu wa Mwenyezi Mungu ndio uwongofu. Na kama ukifuata matamanio yao baada ya ujuzi ulio kwisha kujia, hutapata mlinzi wala msaidizi kwa Mwenyezi Mungu"
      Mod ninaongea na Muislamu mwenzangu hapa.

    3. #822
      Head teacher's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 489
      Likes Received
      124
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By Sideeq View Post
      Tafsiri ya neno ibada, hutafsiriwa kuwa ni kila kinachomridhisha Mwenyezi Mungu..........ukiielewa hii tafsiri basi aya utakazopewa zitakuwa ni nyingi tu Mkuu.
      Je, unakubaliana na mimi kuhusu hiyo tafsiri ili niendelee, au tusimame hapa kwenye tafsiri kwanza?
      Toa aya ya sensa
      Kigogo likes this.

    4. #823
      Mvaa Tai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th August 2009
      Location : Ngudu, Mwanza
      Posts : 3,640
      Rep Power : 1230
      Likes Received
      1553
      Likes Given
      1026

      Default Re: Bakwata,Je sensa ni ibada?

      Quote By sweke34 View Post
      Mimi siyo muislam lakini kwa kifupi wenyewe huwa wanasema Uislam ni Mfumo Kamili wa Maisha...kwa hiyo kila kitu kuanzia siasa,sensa nk vimo ndani yake...subiri wenyewe waje wakufafanulie vizuri...
      Ingekuwa vipi dunia isingekuwa na waislam, je kungekuwa na Alqaida na boko haramu, je tungeendelea kuwekeza mabilioni kwenye ulinzi wa amani? au ndiyo technologia ya siraha ingekuwa chini sana maana kusingekuwa na changamoto? je tungeendelea kuchekiwa tunapoingia ndani ya ndege? Najaribu tuu kutafakari.
      Haiwezekani Kabisa Twiga kupakiwa ndani ya ndege tayari kupelekwa nje ya nchi bila Polisi na Usalama wa Taifa kujua....

    5. #824
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 593
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Bakwata,Je sensa ni ibada?

      Quote By Safety last View Post
      "mungu" wa waislam hataki mchezo kabisa lazima kila kitu kiende kwa mfumo wa allah subhana wataala.Tutagomea sensa ,hesabuni hao wagalati.takbirr.
      Hujatulia, na huenda sio mtanzania wewe!

    6. #825
      Head teacher's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 489
      Likes Received
      124
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By Sideeq View Post
      Tafsiri ya neno ibada, hutafsiriwa kuwa ni kila kinachomridhisha Mwenyezi Mungu..........ukiielewa hii tafsiri basi aya utakazopewa zitakuwa ni nyingi tu Mkuu.
      Je, unakubaliana na mimi kuhusu hiyo tafsiri ili niendelee, au tusimame hapa kwenye tafsiri kwanza?
      Kwa hiyo kuhesabiwa haimpendezi Allah

    7. #826
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 593
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Bakwata,Je sensa ni ibada?

      Quote By Head teacher View Post
      Swali hili lijibiwe na wanaoifahamu Qurani si maamuma,Kwani tunahitaji surat na aya za Kurani tukufu.Maana Mufti amewataadhalisha wafuasi wa dini kukiona cha moto kwa Allah kwa wale watakaokubali kuhesabiwa bila kuulizwa Kama ni wafuasi wa dini ya Islam. Inawezekana wameamriwa na mola wao kugomea sensa za makafiri na mapagani.Tupe aya
      Mimi siifahamu Qurani na wala sio muislam lakini nakujibu vilevile --Kwa ujumla hawa watu ni wakorofi wa kupitiliza, ingawa sio waislam wote ambao wana-support hilo, ni wachache tu ambao wana mtazamo finyu wanakataa sensa. Imagine, hata sheikh mkuu wa DSM anawapinga kwa nguvu zote hao watu ambao wanakataa sensa. Ni kuwa na akili duni tu.

    8. #827
      Head teacher's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 489
      Likes Received
      124
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By Mvaa Tai View Post
      Ingekuwa vipi dunia isingekuwa na waislam, je kungekuwa na Alqaida na boko haramu, je tungeendelea kuwekeza mabilioni kwenye ulinzi wa amani? au ndiyo technologia ya siraha ingekuwa chini sana maana kusingekuwa na changamoto? je tungeendelea kuchekiwa tunapoingia ndani ya ndege? Najaribu tuu kutafakari.
      Upo nje ya mada

    9. #828
      Head teacher's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 489
      Likes Received
      124
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By webondo View Post
      Mimi siifahamu Qurani na wala sio muislam lakini nakujibu vilevile --Kwa ujumla hawa watu ni wakorofi wa kupitiliza, ingawa sio waislam wote ambao wana-support hilo, ni wachache tu ambao wana mtazamo finyu wanakataa sensa. Imagine, hata sheikh mkuu wa DSM anawapinga kwa nguvu zote hao watu ambao wanakataa sensa. Ni kuwa na akili duni tu.
      Upo nje ya mada

    10. #829
      Head teacher's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 489
      Likes Received
      124
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By Safety last View Post
      "mungu" wa waislam hataki mchezo kabisa lazima kila kitu kiende kwa mfumo wa allah subhana wataala.Tutagomea sensa ,hesabuni hao wagalati.takbirr.
      Toa aya

    11. #830
      IGWE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2011
      Location : Blue Plaza Building-Arusha
      Posts : 5,314
      Rep Power : 3307
      Likes Received
      1335
      Likes Given
      1240

      Default

      Quote By Head teacher View Post
      Upo nje ya mada
      Yeah..tufike mahali tuwe wastaarabu kwa iman za wenzetu,.pia mleta mada hata pata jibu sahihi kwa udandiaji huu...swali limeelekezwa kwa wajuvi wa quaran...tusiojua bora tuwe waangalizi mkuu

    12. #831
      MAKUNDA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th April 2012
      Posts : 76
      Rep Power : 378
      Likes Received
      27
      Likes Given
      1

      Smile Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Tume ya katiba View Post
      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      Nafikia mahala nashindwa kuamini kuwa kauli hizi zinatoka BAKWATA maana siwezi kuamini kuwa ndani ya BAKWATA wote ni Bongo lala kiasi hiki. Pia sitaki kuamini kuwa haya ni mawazo ya Waislam wote kwa kwani sitaki kujiamimisha kuwa waislam wote ni bongo lala kiasi hiki. Kuna watu kama Prof. LIPUMBA mwanauchumi wa kuaminika hivi naye nimweke katika kundi la watu wasiojua maana ya Sensa kiasi cha kugoma kushiriki au tuseme naye hatashiriki! la hasha. Ewe unayejifanya ndiye mtoa sauti ya Waislam unataka kusema waislam wote wanakuunga Mkono? la hasha siyo wote ni BONGOLALA Kama wewe.
      Hivi nyie mashehe na hao mnaotaka kuwagomesha wenzenu kisa eti mnataka kupitia SENSA mjue idadi ya waislam mnashindwa kufanya hata Hesabu za kujumlisha na Kutoa. Uislam siyo jina bali ni mfumo mzima wa maisha pamoja na Ibada. Kama ndivyo basi chukueni idadi ya waumini wenu misikitini alafu jumulisha kwa kijiji, Kata,Tarafa, Kiwilaya,Kimkoa na Kitaifa baada ya kupata idadi yenu subiri baada ya matokeo ya SENSA toa mjue asilimia ya Waislam ni ngapi.
      Sensa manufaa yake yako kiuchumi zaidi mnavyodhani kuwa nikwa mtaji wa kujiimalisha Kisiasa msidhani hiyo inatija hachana na hiyo kabisa

    13. #832
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,045
      Rep Power : 14670
      Likes Received
      2954
      Likes Given
      2093

      Default Re: Bakwata,Je sensa ni ibada?

      Quote By Head teacher View Post
      Toa aya ya sensa
      Qur'an 83: 1-3

      1. Ole wao hao wapunjao!
      2. Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
      3. Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    14. #833
      Blayi wa Mpwapwa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th January 2012
      Posts : 111
      Rep Power : 397
      Likes Received
      44
      Likes Given
      0

      Default Re: Bakwata,Je sensa ni ibada?

      Tuangalie Somalia, wote ni waislam tena kabila moja tu ila koo ziko nyingi, narudia tena dini ni moja tu waislamu lakini sasa je! Somalia kuna nini cha kuigwa?

    15. #834
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,686
      Rep Power : 821
      Likes Received
      237
      Likes Given
      1

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By MAKUNDA View Post
      Uislam siyo jina bali ni mfumo mzima wa maisha pamoja na Ibada. Kama ndivyo basi chukueni idadi ya waumini wenu misikitini alafu jumulisha kwa kijiji, Kata,Tarafa, Kiwilaya,Kimkoa na Kitaifa baada ya kupata idadi yenu subiri baada ya matokeo ya SENSA toa mjue asilimia ya Waislam ni ngapi.
      Utaeleweka tu kama hiyo sensa itakayofanywa na Waislamu itatambulika rasmi Kitaifa (serikali).

    16. #835
      Head teacher's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 489
      Likes Received
      124
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By zomba View Post
      Qur'an 83: 1-3

      1. Ole wao hao wapunjao!
      2. Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe.
      3. Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza.
      Hapo Allah amezuia sensa?

    17. #836
      Head teacher's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 489
      Likes Received
      124
      Likes Given
      6

      Default

      Quote By Blayi wa Mpwapwa View Post
      Tuangalie Somalia, wote ni waislam tena kabila moja tu ila koo ziko nyingi, narudia tena dini ni moja tu waislamu lakini sasa je! Somalia kuna nini cha kuigwa?
      Hoja ni sensa ni ibada?

    18. #837
      Ipycalypse's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2011
      Location : Mjini hapa
      Posts : 1,191
      Rep Power : 646
      Likes Received
      249
      Likes Given
      148

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By David webb View Post
      Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

      Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

      Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
      Ushahida tafadhari
      Life is like video footage Hard to edit directors,that never understood it

    19. #838
      mikatabafeki's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th December 2010
      Posts : 4,873
      Rep Power : 1407
      Likes Received
      778
      Likes Given
      1463

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      naingia mashaka kuona sensa inageuzwa kuwa ibada

    20. #839
      Bornvilla's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th February 2011
      Posts : 637
      Rep Power : 549
      Likes Received
      141
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Blayi wa Mpwapwa View Post
      Tuangalie Somalia, wote ni waislam tena kabila moja tu ila koo ziko nyingi, narudia tena dini ni moja tu waislamu lakini sasa je! Somalia kuna nini cha kuigwa?
      Wewe umezoea kulishwa uchafu na vyombo vyenu mfumokristo vilivyoenea ulimwenguni. Kama kweli wewe nimjuzi wa mambo nipe chanzo cha Al-shabaab na Al-qaida. Tatizo lenu huwa mnameza tu pasipokuangalia mnalishwa nini. Maranyingi mnalishwa konokono badala ya samaki,mfano mzuri ni habari ya sensa na suala la Uamsho Zanzibar,mmelishwa makonokono yakutosha na hata ikafika wakati mkabaini lakini mkaendelea kutamani konokono badala ya samaki. Mjinga huelimika,lakini mpumbavu hata ugonge na nyundo bado haelewi!

    21. #840
      Chatumkali's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th September 2011
      Location : DOM
      Posts : 1,384
      Rep Power : 978
      Likes Received
      184
      Likes Given
      166

      Default Re: Bakwata,Je sensa ni ibada?

      Tulikuwa tumeanza kuzisahau hizi thread naona mmeanza kuzileta tena!

    Page 42 of 62 FirstFirst ... 32404142434452 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...