Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 32 of 62 FirstFirst ... 22303132333442 ... LastLast
    Results 621 to 640 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 890
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.


    2. #621
      Olaigwanani lang's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th April 2012
      Posts : 360
      Rep Power : 826
      Likes Received
      56
      Likes Given
      386

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Nasubiri nione kikwete,bilal,makamba,kigoda,z ungu,zitto, kama nao watakataa kuhesabiwa...kweli nasubiri kwa hamu....!
      mzozaji likes this.

    3. #622
      JacksonMichael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd March 2012
      Posts : 331
      Rep Power : 431
      Likes Received
      61
      Likes Given
      37

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Huenda ni umbumbumbu wangu, naomba mwenye utaalamu anieleze kwa nini DINI si halali kuwepo katika sensa tanzania?

    4. #623
      Chikwakara's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th April 2012
      Posts : 100
      Rep Power : 384
      Likes Received
      19
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      elimu ndogo ni sumu. sisi waislam twende shule kwanza ndo tutajitambua vizuri. viongozi wetu uwa wanakurupuka tu kwa sababu ya shule ndogo ukilinganisha na wakristu

    5. #624
      betty marandu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th April 2011
      Posts : 139
      Rep Power : 443
      Likes Received
      15
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By Tume ya katiba View Post
      Hilo jicho lako la tofauti lina makengeza dada betty!
      Jicho langu zima kabisa Katiba,halina chongo wala kengeza.Swali langu ni kuwa kama kweli hawana ajenda ya siri na sababu ya kuweka kipengele cha dini ni ili kutoa huduma za kidini waanze Zanzibar maana kule hakuhitaji sensa kujua Waislam ni wengi.Au watumie ushauri wa kuhesabiana misikitini kama wakristo wanavyofanya kupata idadi yao.

    6. #625
      Bosi Michembe's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th June 2011
      Location : Sengerema
      Posts : 213
      Rep Power : 446
      Likes Received
      52
      Likes Given
      33

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mtambuzi View Post
      Hivi katika nchi hii, dini zinazotambulika kisheria ni uislamu na ukristo? kwa nini dini nyingine hazizungmziwi hapa,mfano dini za kimila sijasikia zikizungumziwa kabisa.

      Niliwahi kwenda Polisi, katika kuandikisha malezo yangu nikaulizwa dini yangu, nikajibu kuwa sina dini, mimi ni mpagani, lakini yule askari alilazimisha kwamba lazima nina dini, baada ya kubishana sana akaniuliza dini ya wazazi wangu nikamwambia nao hawana dini, yule askari akasema haiwezekani na mwishowe akanipachika dini ambayo si yangu...
      Pole mkuu sio peke aisee. Mi nilipoteza kitambulisho changu pamoja na cha benki nikiwa chuoni Ud nikafuata taratibu zote ilipofika polisi ilikuwa ishu asikwambie mtu ilipofika kipengele cha dini nilisema sina, nikalazimishwa kujaza kutokana na mwelekeo wa jina langu la kuendea shule nikagoma, wakamwita mkuu wa kituo nae bila kufikiri akaanza kunichimba mkwara eti wewe utaenda motoni kijana ebu jaza hapo hizo takwimu zinahitajika, nikamwambia kwani hamuhitaji takwimu za wapagani aisee ikageuka sinema ya bure wakaanza kuitana na kunikejeli. Niligoma aisee na fomu zao za loss report nikawachia kaunta nikasema na watu wa Smartcard nilamba ID nyingine..


    7. #626
      Tume ya Katiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Chumbuni-Zanzibar
      Posts : 2,838
      Rep Power : 0
      Likes Received
      565
      Likes Given
      295

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By betty marandu View Post
      Jicho langu zima kabisa Katiba,halina chongo wala kengeza.Swali langu ni kuwa kama kweli hawana ajenda ya siri na sababu ya kuweka kipengele cha dini ni ili kutoa huduma za kidini waanze Zanzibar maana kule hakuhitaji sensa kujua Waislam ni wengi.Au watumie ushauri wa kuhesabiana misikitini kama wakristo wanavyofanya kupata idadi yao.
      Unafikili ni sababu ipi ilipelekea chombo cha habari cha taifa kutoa takwimu za watu kwa dini zao? eti dada yangu hebu nijibu? pia mbona mataifa mengi yana hiki kipengele cha dini na hakuna issue? pia dada betty nini hasa wasiwasi wako kitaalamu kabisa ukiacha hizo hisia?

    8. #627
      Tume ya Katiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Chumbuni-Zanzibar
      Posts : 2,838
      Rep Power : 0
      Likes Received
      565
      Likes Given
      295

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Bosi Michembe View Post
      Pole mkuu sio peke aisee. Mi nilipoteza kitambulisho changu pamoja na cha benki nikiwa chuoni Ud nikafuata taratibu zote ilipofika polisi ilikuwa ishu asikwambie mtu ilipofika kipengele cha dini nilisema sina, nikalazimishwa kujaza kutokana na mwelekeo wa jina langu la kuendea shule nikagoma, wakamwita mkuu wa kituo nae bila kufikiri akaanza kunichimba mkwara eti wewe utaenda motoni kijana ebu jaza hapo hizo takwimu zinahitajika, nikamwambia kwani hamuhitaji takwimu za wapagani aisee ikageuka sinema ya bure wakaanza kuitana na kunikejeli. Niligoma aisee na fomu zao za loss report nikawachia kaunta nikasema na watu wa Smartcard nilamba ID nyingine..
      Sasa mkuu kama ni wajibu polisi hadi ukapoteza haki yako ya kisheria, iweje isiwe halali kabisa katika sensa tujue moja?

    9. #628
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,718
      Rep Power : 989
      Likes Received
      598
      Likes Given
      10

      Default

      Hii ni hoja chovu kupindukia kutoka kwa Premium Member wa JF!
      Quote By ritz View Post
      Serikali ina wajibu wa kuwahesabu raia wake kwenye sensa tunatakiwa tujue kuna Watanzania wangapi Wakirsto, Waislam, Jewish, Hindu, Buddhist, na wasiokuwa na dini, ndio maana ya sensa.

    10. #629
      betty marandu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 4th April 2011
      Posts : 139
      Rep Power : 443
      Likes Received
      15
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By Tume ya katiba View Post
      Unafikili ni sababu ipi ilipelekea chombo cha habari cha taifa kutoa takwimu za watu kwa dini zao? eti dada yangu hebu nijibu? pia mbona mataifa mengi yana hiki kipengele cha dini na hakuna issue? pia dada betty nini hasa wasiwasi wako kitaalamu kabisa ukiacha hizo hisia?
      Katiba hujajibu swali langu.Unajua case ya mataifa mengine na letu haiwezi kufanana.Hebu fikiria nchi kama Uingereza ambako haikuwa na madhara,kule watu wamestaarabika zaidi yetu(wengi wamesoma ukilinganisha na sisi).Halafu idadi ya watu kwa dini zao haijakaribiana na sisi.sisi kwa haraka haraka tunakaribiana wakristo na waislam.sasa hiyo sensa ikiweka kipengele cha dini unafikiri itakuwaje kwa wenye misimamo kama ya wanauamsho?Mimi naona kwa hali inavyooneka tz mfano mzuri hapa jf kipengele cha dini kisiwepo.

    11. #630
      Tume ya Katiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Chumbuni-Zanzibar
      Posts : 2,838
      Rep Power : 0
      Likes Received
      565
      Likes Given
      295

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By betty marandu View Post
      Katiba hujajibu swali langu.Unajua case ya mataifa mengine na letu haiwezi kufanana.Hebu fikiria nchi kama Uingereza ambako haikuwa na madhara,kule watu wamestaarabika zaidi yetu(wengi wamesoma ukilinganisha na sisi).Halafu idadi ya watu kwa dini zao haijakaribiana na sisi.sisi kwa haraka haraka tunakaribiana wakristo na waislam.sasa hiyo sensa ikiweka kipengele cha dini unafikiri itakuwaje kwa wenye misimamo kama ya wanauamsho?Mimi naona kwa hali inavyooneka tz mfano mzuri hapa jf kipengele cha dini kisiwepo.
      Dada yangu JF haiwezi kuwa sample size sahihi hata kigodo kugeneralize kwa waTZ, labda haupo TZ mwenzangu, lakini huku mtaani hata hiyo JF haijulikani, sikuambii wenye access ya hiyo internet.

      Mfumo wa UDINI upo sana kwenye maofisi hasa ya serikali na kwa wasomi tu, huenda mifumo yetu ya ajira ina matatizo na ndio sababu ya yote haya. Lakini kwenye mitaani hakuna hii tensio kubwa, watu wanaishi vyema na wameshazoea "umasikini" walionao. Kuhusu swali lako, ninashindwa kulijibu kwa kuwa limejengeka kihisia zaidi kuwa kuna agenda ya siri jambo ambalo si sahihi na ninahisi ni mtazamo wako binafsi. Mwisho ingawa sensa ni ya Tanzania nzima, lakini kwa upande wa znz hakuna ulazima wa kihivyo, ila huku mainland watu wanachakachua sana hizi takwimu na ndio maana bora ifanyike ijulikane rasmi.

    12. #631
      last man standing's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Location : Dar es salaam
      Posts : 54
      Rep Power : 374
      Likes Received
      7
      Likes Given
      30

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Naona fitna zinaanza taratiiiibu, baada ya kuutangazia ulimwengu uwepo wa mafuta, gesi na uranium, fitna za mmarekani zinaanza kujidhihirisha, si bure kuna mkono wa mtu hapa, kesho hujui watademand nin hawa jamaa. ili mgeni atawale lazima wenyeji wagombane na wasiwe na maelewana. mmarekani mshenzi sana.

    13. #632
      mzozaji's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th July 2010
      Posts : 248
      Rep Power : 501
      Likes Received
      8
      Likes Given
      2

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Mimi sioni sababu ya serikali kufanya sensa kwa wakati huu ambapo wanatoa vitambulisho vya Taifa. Idadi ya watu itajulikana tuu kwenye vitambulisho vya Taifa. Hao jamaa Kama wanna guts wasusie na vitambulisho vya Taifa basi maana navyo sijui Kama vina dini.

    14. #633
      mzozaji's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 28th July 2010
      Posts : 248
      Rep Power : 501
      Likes Received
      8
      Likes Given
      2

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Kuna watu wanashangaza sana kuhoji eti data za hao waliojitangazia percentage za kidini wameonyesha wao wamepungua percent sasa wameenda wapi? Hivi inakuwaje mtu anashindwa kutofautisha kupungua percent na kupungua idadi? Kupungua percent inawezekana hata kama idadi yao imeongezeka toka wakati ule walipohesabu kwani inawezekana wengine wameongezeka zaidi yao, au wanakufa kwa rate kubwa zaidi nk. Kama kuwabana wakawabane hao waliotoa hizo data na sio serikali inayotaka kujua idadi tuu.

    15. #634
      Twasila's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th May 2011
      Posts : 442
      Rep Power : 498
      Likes Received
      61
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By JacksonMichael View Post
      Huenda ni umbumbumbu wangu, naomba mwenye utaalamu anieleze kwa nini DINI si halali kuwepo katika sensa tanzania?
      Siyo kila kilicho halali lazima kiwepo kwenye dodoso.

    16. #635
      AMARIDONG's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th June 2010
      Posts : 2,489
      Rep Power : 953
      Likes Received
      53
      Likes Given
      47

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Tangaaaa kunani paleeeee؛mbona maisha yamibadilika؛‎ tangaaa

    17. RMA is offline
      RMA
      #636
      RMA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th October 2010
      Posts : 410
      Rep Power : 523
      Likes Received
      87
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Ninaweza View Post
      Baada ya kujua idadi ya wana imani fulan!, nini kitafata?
      Uchomaji wa makanisa!

    18. #637
      Hakikwanza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th December 2010
      Posts : 1,172
      Rep Power : 2670
      Likes Received
      161
      Likes Given
      19

      Default

      Quote By RMA View Post
      Uchomaji wa makanisa!
      Kazi tunayo tunacho omba Mungu wa kweli atunusuru, Mungu gani anafundisha ukatili? Mungu gani haambiliki? Mungu gani anahukumu pasipo kufuata haki? MTU ANACHOMA KANISA LA MWENZIE NA HAPO ANAFIKIRIA PEPO? kazi kwelikweli?

    19. #638
      Mshuza2's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 1,309
      Rep Power : 691
      Likes Received
      201
      Likes Given
      17

      Default

      Quote By Chikwakara View Post
      elimu ndogo ni sumu. sisi waislam twende shule kwanza ndo tutajitambua vizuri. viongozi wetu uwa wanakurupuka tu kwa sababu ya shule ndogo ukilinganisha na wakristu
      wewe ndio mwenye elimu ndogo, na ndio maana unachelea kusema hayo! Sikulaumu,tayari umeshaathirika na propaganda za hawa jamaa,ukweli hauko hivyo ndugu yangu,hizo ni dhana na mbinu za hawa ndugu zetu kutuathiri kisaikolojia! Nawaheshimu sana hawa wenzetu kwani wengine tumeshaoleana! Kifupi ni kwamba tunaishi kwa kutegemeana!
      Hujiulizi kwanini sensa za nyuma kipengele hiki kilikuwepo? Haya mambo yaache kama yalivyo! Bora uwe muoga kwenye kundi la mashujaa! Haki na batili havitangamani! Nitarudi..

    20. #639
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1259
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      By Mkandara

      Naona watu mnabishana kitu ambacho kwanza hakina ubaya wowote. Sensa ni ya WATU sio nchi (na watu wake wana dini) hivyo unapotaka kuhesabu watu hakuna ubaya wowote kuweka vipengele hivi ikiwa leo hatutumikii tena siasa ya UJAMAA (Socialism). Hata Wachina na Warusi wao walikataza kabisa na kusema nchi yao haina dini na hata watu wake hawatakiwi kuwa na dini, haya yalikuwa ya miaka ile ya vita baridi. Hivi sasa Wakristu na Waislaam wapo na wanahesabiwa maana lengo la sensa ni kuwajua watu wake kwa makundi ya kijamii.

      Kupinga hoja ya Waislaam ni kuonyesha hofu na mashaka ktk matokeo na kama hakuna tunapinga kitu gani ama kutakuwa na ubaya gani kama kipengele hicho kikiwekwa?. Maana kila siku humu JF ubishi ni kuhusu asilimia ya Waislaam na Wakristu, basi bora sensa hii iondoe ubishi huu. Halafu pia sidhani kama sensa haina kipengele cha Jinsia, Kabila, uzawa na kadhalika (haina maana wanatengwa) kwani sensa hii itaweza tu kutufahamisha Tanzania ina wazawa wangapi na wageni wahamiaji wangapi na kwa vipengele vipi. Pasipo vipengele kama hivi utaweza vipi kumhesabu Mkenya au Mrwanda aliyehamia Tz. na vile vile wao wanaweza kusema kabila la nini mbona mnatutenga? Kesho inawezekana tukawa na duo citizenship tutaweza vipi kumtenga Mmalawi ambaye anadai Utazania?.

      Kwa hiyo ndugu zangu tuyapokee malalamiko ya watu kwa fikra huru, sii kujifungia ktk sanduku la Udini hata ktk jambo dogo ambalo haliwezi kubadilisha maisha yako isipokuwa kuweka record ya usahihi wa watu wake ktk jamii zao. I wouldn't mind kuwepo vipengele vyote muhimu ktk utunzaji wa record za sensa ambayo kitaalam inatakiwa kuwa na majibu yote.
      Shehe wenu kasema hivi


      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.
      Waislam mmelogwa? Kupanga maendeleo yenu mnahitaji kuhesabiwa na serikali? Yaani mkuu Mkandara kwenye karne hii ya 21 Waislam Tanzania hawajui idadi yao mpaka wasubiri serikali iwahesabu ndiyo wapange maendeleo yao?
      Naomba unijibu kutoka moyoni...hivi Muislam ni nani? ni mtu tu muislam kwa jina lakini hata msikiti haujui ulivyo au ni mtu anayefuata ibada ya kiislam na kutimiza matakwa yake?
      Mkuu wangu sisi wakatoliki(Sijui madhehebu mengine) huwa tunafanya hivi:
      Tunazo jumuiya ndogondogo kwenye kila Parokia/Kigango
      Kwenye kila jumuiya tuna orodha kamili ya wakatoliki na familia zao
      Maendeleo:
      Kuna vikundi kama:-
      Utoto Mtakatifu-Watoto
      Umoja wa Vijana Wakatoliki-vijana
      Umoja wa wanawake wakatoliki -wanawake
      Umoja wa wanaume wakakatoliki - wanaume

      Maendeleo ya vikundi vyote hivyo yanapangwa kwa ushirikiano mkubwa wa ngazi ya chini kabisa(jumuiya ndogondogo)
      mpaka ngazi za juu kabisa katika jimbo na Taifa.
      Shughuli zote za maendeleo zinakwenda kama zilivyopangwa kwa sababu data zote zipo makao makuu.

      Nyinyi ndiyo mnasubiri serikali iwahesabu ndiyo mpange jinsi ya kuwasaidia wenzenu...kweli?
      Mimi nadhani wenye hofu ni hawa mashehe(siyo waislam wote) kwa sababu wanaficha lengo lao la ukweli la kutaka kuwekwa kigezo cha dini kwenye sensa. Na hapa inaonekana lengo siyo kupanga maendeleo/kusaidia waislam maana hiyo ingewezekana kirahisi sana kufanyika misikitini.
      Last edited by sweke34; 16th June 2012 at 09:05.

    21. #640
      Kingmairo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Location : In the Palace
      Posts : 875
      Rep Power : 538
      Likes Received
      268
      Likes Given
      87

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Mi najiuliza ni kwanini kila chokochoko inaanzishwa na waislamu? Tena ikiwa inahusisha kutendewa jambo na serikali. Mara mnadai mahakama ya kadhi kwa kugharamiwa na serikali, sasa hivi mnataka sensa ya udini. Hii ni kujidharau wenyewe na uwezo wenu. Katika mazingira ya sasa hivi ambapo kuna mgawanyiko wa wazi kidini katika masuala mengi serikali imeamua vyema kwa maslahi ya taifa. Mkae mkijua taifa ni kubwa kuliko dini yenu na mshiriki au msishiriki sensa itafanyika.

    Page 32 of 62 FirstFirst ... 22303132333442 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...