Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 30 of 62 FirstFirst ... 20282930313240 ... LastLast
    Results 581 to 600 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 890
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.


    2. #581
      Kinyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2008
      Posts : 1,883
      Rep Power : 948
      Likes Received
      236
      Likes Given
      378

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Dawa ni kuigawa hii nchi baina ya Waislam na Wakristu halafu baada ya miaka miwili utakuja kuniambia ni watu wa dini ipi watakuwa wanazamia kwenye nchi ya dini tofauti na wao.
      Steve Dii likes this.
      Together in Poverty Apart in Riches

    3. #582
      KiongoziMchapakazi's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 14th June 2012
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 5
      Rep Power : 354
      Likes Received
      1
      Likes Given
      6

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Wengi mnapindisha pindisha! Lakini lengo kuu la kujua idadi yao ni kutaka kuibadili nchi iwe ya kiislamu, wakishajua idadi yao wataanzisha lingine la kutaka ipigwe kura ya kutaka nchi iwe ya kiislamu au la na hapo ndiyo katiba mpya inafuata. Mark my words!!
      Kwa nini leo iwe hivyo nawakati zamani hiko kipengele kilikuwepo na wala hawakuibadili nchi iwe ya Kiislamu na mbona nchi nyingi zenye maendeleo hiko kpengele kipo na hamsemi itakuwa unafiki eti kusema wakijua idadi yao watadai hiki na kile, Hakuna kitu chenye ushawishi kwa binadamu kama dini kwa hiyo Waislamu au Wakristo kudai kipengele cha dini katika sensa si suala la kutaka nchi iwe ya Kiislamu.
      Hilo dai si la waislamu peke yao na dini zingine pia ila watu wanataka eti wote wawe wanafiki kwa kulinyamazia alafu kumbe kuna njia yao ya kupata sensa za dini zao huo utakuwa unafiki
      Mbona hamkatazi viongozi wanapoapa wasitumie vitabu vyao vya dini badala yake watumie katiba ya nchi kama kweli wazalendo wa maendeleo na dini tunaiweka kando kwenye mambo ya kisiasa

    4. #583
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 406
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Invarbrass View Post
      Kuna faida gani kuweka dini kwenye sensa?
      Faida ziko nyingi,mojawapo ni kuiwezesha serikali kutenga pesa za kutekeleza memorandum of understanding kati ya serikali na kanisa

    5. #584
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,768
      Rep Power : 7665
      Likes Received
      4931
      Likes Given
      4509

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Naona watu mnabishana kitu ambacho kwanza hakina ubaya wowote. Sensa ni ya WATU sio nchi (na watu wake wana dini) hivyo unapotaka kuhesabu watu hakuna ubaya wowote kuweka vipengele hivi ikiwa leo hatutumikii tena siasa ya UJAMAA (Socialism). Hata Wachina na Warusi wao walikataza kabisa na kusema nchi yao haina dini na hata watu wake hawatakiwi kuwa na dini, haya yalikuwa ya miaka ile ya vita baridi. Hivi sasa Wakristu na Waislaam wapo na wanahesabiwa maana lengo la sensa ni kuwajua watu wake kwa makundi ya kijamii.

      Kupinga hoja ya Waislaam ni kuonyesha hofu na mashaka ktk matokeo na kama hakuna tunapinga kitu gani ama kutakuwa na ubaya gani kama kipengele hicho kikiwekwa?. Maana kila siku humu JF ubishi ni kuhusu asilimia ya Waislaam na Wakristu, basi bora sensa hii iondoe ubishi huu. Halafu pia sidhani kama sensa haina kipengele cha Jinsia, Kabila, uzawa na kadhalika (haina maana wanatengwa) kwani sensa hii itaweza tu kutufahamisha Tanzania ina wazawa wangapi na wageni wahamiaji wangapi na kwa vipengele vipi. Pasipo vipengele kama hivi utaweza vipi kumhesabu Mkenya au Mrwanda aliyehamia Tz. na vile vile wao wanaweza kusema kabila la nini mbona mnatutenga? Kesho inawezekana tukawa na duo citizenship tutaweza vipi kumtenga Mmalawi ambaye anadai Utazania?.

      Kwa hiyo ndugu zangu tuyapokee malalamiko ya watu kwa fikra huru, sii kujifungia ktk sanduku la Udini hata ktk jambo dogo ambalo haliwezi kubadilisha maisha yako isipokuwa kuweka record ya usahihi wa watu wake ktk jamii zao. I wouldn't mind kuwepo vipengele vyote muhimu ktk utunzaji wa record za sensa ambayo kitaalam inatakiwa kuwa na majibu yote.
      Last edited by Mkandara; 15th June 2012 at 16:50.
      Steve Dii, Mdondoaji and mfumo like this.
      Exploration of reality

    6. #585
      KiongoziMchapakazi's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 14th June 2012
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 5
      Rep Power : 354
      Likes Received
      1
      Likes Given
      6

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Kinyungu View Post
      Dawa ni kuigawa hii nchi baina ya Waislam na Wakristu halafu baada ya miaka miwili utakuja kuniambia ni watu wa dini ipi watakuwa wanazamia kwenye nchi ya dini tofauti na wao.
      Itakuwa vizuri ukatuambia kitatokea nini ili tukumbuke maneno yako kwa kupindisha hoja ya wanaodai na si kusimamisha hoja


    7. #586
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 406
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Kinyungu View Post
      Dawa ni kuigawa hii nchi baina ya Waislam na Wakristu halafu baada ya miaka miwili utakuja kuniambia ni watu wa dini ipi watakuwa wanazamia kwenye nchi ya dini tofauti na wao.

      Waislamu wengi ni wajasirimali ndio maana pamoja na uchache wao katika ajira za uma bado wanapeta katika biashara.Lakini la kugawanya likitokea kitachofanya wengine wazamie kwingine ni rasilimali zitakazokuwepo

    8. #587
      KiongoziMchapakazi's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 14th June 2012
      Location : Dar Es Salaam
      Posts : 5
      Rep Power : 354
      Likes Received
      1
      Likes Given
      6

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By WA-UKENYENGE View Post
      Wengi mnapindisha pindisha! Lakini lengo kuu la kujua idadi yao ni kutaka kuibadili nchi iwe ya kiislamu, wakishajua idadi yao wataanzisha lingine la kutaka ipigwe kura ya kutaka nchi iwe ya kiislamu au la na hapo ndiyo katiba mpya inafuata. Mark my words!!
      Kwa nini leo iwe hivyo nawakati zamani hiko kipengele kilikuwepo na wala hawakuibadili nchi iwe ya Kiislamu na mbona nchi nyingi zenye maendeleo hiko kpengele kipo na hamsemi itakuwa unafiki eti kusema wakijua idadi yao watadai hiki na kile, Hakuna kitu chenye ushawishi kwa binadamu kama dini kwa hiyo Waislamu au Wakristo kudai kipengele cha dini katika sensa si suala la kutaka nchi iwe ya Kiislamu.
      Hilo dai si la waislamu peke yao na dini zingine pia ila watu wanataka eti wote wawe wanafiki kwa kulinyamazia alafu kumbe kuna njia yao ya kupata sensa za dini zao huo utakuwa unafiki
      Mbona hamkatazi viongozi wanapoapa wasitumie vitabu vyao vya dini badala yake watumie katiba ya nchi kama kweli wazalendo wa maendeleo na dini tunaiweka kando kwenye mambo ya kisiasa
      Mkandara likes this.

    9. #588
      Mzalendo JR's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th June 2012
      Posts : 911
      Rep Power : 537
      Likes Received
      277
      Likes Given
      213

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By ritz View Post
      Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.
      Uislamu kule haupo, ila hapa jinsi mlivyo waislamu ni vurugu tu halafu hamjali kama hamjiu kesho. Elimu ni kitu bora sana sema mnakichukulia poa.

    10. #589
      Kinyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2008
      Posts : 1,883
      Rep Power : 948
      Likes Received
      236
      Likes Given
      378

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By KALAMAZOO1 View Post
      Waislamu wengi ni wajasirimali ndio maana pamoja na uchache wao katika ajira za uma bado wanapeta katika biashara.Lakini la kugawanya likitokea kitachofanya wengine wazamie kwingine ni rasilimali zitakazokuwepo
      Japan hakuna rasilimali yoyote ya maana lakini watu wengi wanatamani kwenda japan. Natamani Bakwata waje na hoja ya nchi igawanye wapewe nchi yao. Uone jinsi mtakavyo kuwa Somalia ya kusini mwa ikweta.
      Together in Poverty Apart in Riches

    11. #590
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 406
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mzalendo JR View Post
      Uislamu kule haupo, ila hapa jinsi mlivyo waislamu ni vurugu tu halafu hamjali kama hamjiu kesho. Elimu ni kitu bora sana sema mnakichukulia poa.
      Kumbe sasa unapinga nini wakati unajua kuwa waislamu hawana elimu inabidi serikali ijue idadi yao ili ipange mipango ya kuwaptia elimu

    12. #591
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 406
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Kinyungu View Post
      Japan hakuna rasilimali yoyote ya maana lakini watu wengi wanatamani kwenda japan. Natamani Bakwata waje na hoja ya nchi igawanye wapewe nchi yao. Uone jinsi mtakavyo kuwa Somalia ya kusini mwa ikweta.
      Aliyekwambia Japani hakuna rasilimali nani? umesoma Geography ipi? au ulikuwa jongolist darasani

    13. #592
      Invarbrass's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2011
      Location : PLANET EARTH
      Posts : 380
      Rep Power : 497
      Likes Received
      74
      Likes Given
      65

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By not so wise View Post
      Watanzania hawawezihesabiwa kwa kutumia Dini,Hattuwezi kuruhusu kuhesabiwa kama makundi tofauti malengo ya sensa hayahitaji kufahamu uwingi wa makundi hayo bali uwingi wa watanzania kwa ajili ya maendeleo. Tulitawaliwa zamani lakini sasa tuko huru na tufanye maamuzi kama taifa huru blila kushurutiwa na mtu au taifa au kundi lolote.
      Safi sana mkuuu. Wanao taka kujua idadi ya waumini basi wasiishie hapo watake pia kujua idadi ya mademu weupe, wafupi, idadi ya wabishi, idadi ya wacheza disco, nk maana nayo ni makundi.
      not so wise likes this.

    14. #593
      matawi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th March 2010
      Posts : 1,508
      Rep Power : 770
      Likes Received
      138
      Likes Given
      70

      Default

      Quote By Chesty View Post
      Hakuna ubishi kwamba katika level ya rohoni the whole world is under the authority of Jesus, waislam wako right kabisa. Kwani hamkumbuki Yesu alipofufuka alisema, 'Nimepewa mamlaka mbinguni na duniani". (Mathayo 28:18).

      Hicho ndicho kinachowasumbua wale wote wanaompinga (Anti-Christ). Na ndio maana kwa sasa kuna mpango unaitwa "NEW WORLD ORDER" ambao kusudi lake ni kuondoa mamlaka toka kwa Yesu kwenda kwa anayempinga akitumia wafuasi wake.(World Religion System and Government Leaders-Occults)

      Mamlaka ya Yesu ilitokana na DAMU aliyoimwaga (remember BLOOD is extremely powerful), ndio maana engineers wa NEW WORLD ORDER wanashed a lot of blood ili kufikia malengo hayo. Unfortunately no BLOOD can match the BLOOD of Jesus. Dose hii inatosha kwa sasa.
      Chesty kweli wewe mtata

    15. #594
      SNAKE HOUSE's Avatar
      Member Array
      Join Date : 4th October 2010
      Posts : 61
      Rep Power : 454
      Likes Received
      4
      Likes Given
      2

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mdondoaji View Post
      Mpuuzi we unafikiri unajadiliana na kihiyo hapa,

      For your information mimi ni senior economists nina PhD ya economics, Masters mbili ya sheria na uchumi na nimefanya kazi US na UK kama mshauri na hapa Tanzania na moja ya kazi nimefanya kusimamia suala la demographic usifikiri unajadiliana na mpuuzi kapeleke upuuzi wako kule mjinga wewe.

      Unajitia aibu...unaongelea 'Gender' au 'Sex'? Hivyo ni vitu viwili tofauti, nadhani unataka kuongelea Sex lakini unaconfuse na Gender...Gender is a very wide subject with lots of evidence-generating research done and other going on..kuna watu wana PhDs za mambo ya gender! Gender sio 'Mwanamme' na 'Mwanamke' tu, it goes far beyond that my brother!


      Kuhusu gender nilikuuliza hilo swali hujalielewa ni kwamba gender is subjective na kuna weakness nyingi katika gender kwani wapo wanawake, wanaume na wanaopenda kujiona wanawake au wanaume etc. But kinachofanyika ni assumption kuwa kuna jinsia mbili tu nazo ni mwanaume na mwanamke hivyo a SIMILAR ASSUMPTION INAWEZA KUTUMIKA KATIKA RELIGION KWA KUASSUME ZIPO DINI KUU NNE AU TANO NAZO NI UKRISTO, UISLAMU, DINI NYENGINEZO NA WAPAGANI. KUNA SHIDA GANI?

      Hapo kwenye purple ni uthibitisho kuwa huna idea yeyote kuhusu research. Primarily kabla hujafanya research, ni lazima u-define clearly your variables of interest, kwamba utakaposema kwenye reseach yako fulani ni dini fulani...basi ina maana ana vigezo (criteria) moja, mbili, tatu etc. ili kuondoa bias. Na kwa kumuuliza mtu 'wewe dini gani' (kama unavyosuggest) naye ajibu 'muIslam' au 'mKristo' bila kuzingatia vigezo vya dini ya kiIslamu kuita mtu muIslam au vigezo vya dini ya kiKristo kuita mtu mKristo..then hujawa na evidence kuwa kuna waIslam au waKristo wangapi sehemu husika!


      MPUUZI KABISA WEWE! Kwani variable ya religion ina ambiguity gani? Kuna variable isiyokuwa na assumption? Wewe kama upo WHO ndio maana hamna maana kabisa kwasababu kwa jinsi health system ilivyokuwa mbovu no wonder eti variable has to be defined clearly on what basis??? Hebu tuondolee ridiculous thinking zako any variable is subject to have clear definition which is subject to certain assumption. Kumuuliza mtu wewe ni dini gani unampa uhuru wa kupata majibu ya a. huyu muislamu, b. mkristo, c. dini nyenginezo d. hana dini ambiguity iko wapi? Na rudia post yangu ya nyuma nilikuambia kuwa any primary data has to be verified hivyo TAASISI ZA KIDINI ZITAKUJA KUVERIFY WANACHOKISEMA WATU KWANI KILA TAASISI INAWAFAHAMU WAUMINI WAO NDIO MAANA KUNAKUWA REGISTER KATIKA MISIKITI NA MAKANISANI. AU UNATAKA KUTUAMBIA WATU HAWAOI NA KUOLEWA? KAMA HAKUNA TAARIFA HIZO MAKAZINI NA KWENGINEKO KUNAZO HIZO TAARIFA.

      Lete utumbo wako mwengine nimekuambia fani ya utafiti nimebobea na najisifu kwani nina journals articles za kutosha kimataifa na sio Tanzania. Kadanganye wengine na sio mimi?
      Kihiyo !............................. The word sounds really marvelous !!!!

      Inawezekana una vyeti graded bla bla bla........Labda you attended some bloody courses and got awarded accordingly.......... Lakini from your hojas, I can obsverve immaturity ,kutoelimika vyema,inferiority complex....... Plus intense bitterness !!!!!!!!

      What is wrong with you fella ???????? What does that fella cold Tanzania,benefit from you ?


      I will doubt your level .........(or better for you) Investigate whether,you are mentally fit !!!!!!!!!!

      Wasomi wengine uchwara .......... wanatusumbua kwelikweli .

    16. #595
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,854
      Rep Power : 1343
      Likes Received
      758
      Likes Given
      153

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Sioni shida mimi naungana na wanao sema kipengele cha dini kiwepo tena na dhehebu pia waweke tujuwe mujahidina wangapi alshaabab wangapi walokole wangapi

    17. #596
      matawi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th March 2010
      Posts : 1,508
      Rep Power : 770
      Likes Received
      138
      Likes Given
      70

      Default

      Quote By andate View Post
      Kama BAKWATA wameweza kuwashawishi Waislam wasusie sensa ya taifa kwa sababu walizozitaja, ina maana kuwa BAKWATA wana uwezo wa kuwaamuru Waislam wote kujiorodhesha kwenye Misikiti walio karibu nayo ili wapate idadi yao. Inasikitisha kuona viongozi wa kidini waliokubalika na waumini wanakuwa wavivu kufikiri.
      kuna wale waislamu wala kiti moto itakuwa ngumu sana kuwapata maana masjidi huwa hawatokei

    18. #597
      crome20's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2010
      Posts : 261
      Rep Power : 528
      Likes Received
      60
      Likes Given
      30

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By ritz View Post
      Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.
      Si utuambie faida yake nini, hili ndilo la msingi Acha copy and paste wewe, kila nchi na mazingira yake. Du MNA KAZI NYIE, hili nalo la kugomea sensa? Yaani kiongozi mkubwa wa dini anashinikizwa kushabikia ujinga huu maskini. Hao wanaotoa takwimu zisizo sahihi wanaathiri vipi mipango yenu?
      "I may be wearing a smile but it could be very deceptive. I'm firm on issues. J.K

    19. #598
      Kinyungu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2008
      Posts : 1,883
      Rep Power : 948
      Likes Received
      236
      Likes Given
      378

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By KALAMAZOO1 View Post
      Aliyekwambia Japani hakuna rasilimali nani? umesoma Geography ipi? au ulikuwa jongolist darasani
      Kilaza kweli wewe sasa Japan wana rasilimali gani kulinganisha na Tanzania? Au jografia za shule za kata zinakuzingua!
      Together in Poverty Apart in Riches

    20. #599
      amulikekamwela's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 20th May 2012
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA haitoshiriki zoezi la Sensa mwaka huu......!!

      Dah

      Hii mpya.....................

    21. #600
      Mussa Mussa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th January 2012
      Posts : 106
      Rep Power : 397
      Likes Received
      23
      Likes Given
      1

      Post Re: tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya Agosti 2012

      Ndugu zangu nasikitika sana na hili tamko la waislam ambolo kwa mtu anayeshrikisha ubongo atalipuuza tena hata bila kujiuliza maswali mengi. Ivi kwan waislamu wanamatatizo gani? Mbona kila siku tunasikiliza matatizo yao tu? Mara mahakama ya kadhi, mara hawataki sensa na mengineyo mengi. Ivi wanajiona wao ndio wao sana katika nchi hii.

      Tumechoka kuwasikiliza na maada zenu ambazo hazililikishi ubongo. Ninaomba mfikiri zaidi namna ya kupata maendeleo katika maisha yenu siyo mambo ya kijinga mnayotushilikisha tusiohusika.

      Serikali inafanya sensa sensa kwa malengo maalumu siyo kushindana uwingi wa wafuasi wa dini yeyote. Kwani kukiwa na waislamu asilimia 100 shule ngapi zitaongezeka au kkukiwa na wakristu 2% zahanati ngapi zitaongezeka. Acheni upuuzi wa kijinga. Waislamu wenye akili naamini watalipuuza hili na watashiriki sensa.

      Ninaomba selikali wasikubali hatakidogo kuendeshwa na hao waislamu kwa kuwa wakiwaendekeza na wakristo watakuja na madai yao na hatutafika. Muislamu ukiambiwa jambo changanya na zako. Kwa heri na hayo ni mawazo yangu.

    Page 30 of 62 FirstFirst ... 20282930313240 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...