Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 29 of 62 FirstFirst ... 19272829303139 ... LastLast
    Results 561 to 580 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 887
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. Miaka 50

    3. #561
      Ibrah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd March 2007
      Location : TZ
      Posts : 2,883
      Rep Power : 1199
      Likes Received
      402
      Likes Given
      46

      Default

      Quote By KALAMAZOO1
      Mi natokea bara tena kijijini ndani kabisa.We huoni tatizo hapo kuwa eti serikali badala ya kujenga na kuimarisha hospitali zake inaimarisha za kanisa tena kwa kodi ya wtz wote?
      Unatokea bara, mkoa na wilaya gani Mkuu? Nijibu tafadhali.

    4. #562
      Ibrah's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd March 2007
      Location : TZ
      Posts : 2,883
      Rep Power : 1199
      Likes Received
      402
      Likes Given
      46

      Default

      Quote By KALAMAZOO1
      Kwa kweli hilo silijui lazima nikiri.Nimeishi na wakriustu kwa muda wote sijawhi kuona wanachinja.hebu nipe somo mnachinja vip vile?
      Maana ya kuchinja hujui? Au mpaka mnyama aelekezwe kaskazini mashariki ndio anakuwa kachinjwa?

    5. #563
      not so wise's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 14th June 2012
      Posts : 7
      Rep Power : 351
      Likes Received
      2
      Likes Given
      2

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Watanzania hawawezihesabiwa kwa kutumia Dini,Hattuwezi kuruhusu kuhesabiwa kama makundi tofauti malengo ya sensa hayahitaji kufahamu uwingi wa makundi hayo bali uwingi wa watanzania kwa ajili ya maendeleo. Tulitawaliwa zamani lakini sasa tuko huru na tufanye maamuzi kama taifa huru blila kushurutiwa na mtu au taifa au kundi lolote.

    6. #564
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Ibrah
      Unatokea bara, mkoa na wilaya gani Mkuu? Nijibu tafadhali.
      Hata nikikutajia haitasidia kwa vile huwezi kuthibitisha.Kwa mfano nikikwambia natokea Ukerewe utathibitishaje?

    7. #565
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By not so wise
      Watanzania hawawezihesabiwa kwa kutumia Dini,Hattuwezi kuruhusu kuhesabiwa kama makundi tofauti malengo ya sensa hayahitaji kufahamu uwingi wa makundi hayo bali uwingi wa watanzania kwa ajili ya maendeleo. Tulitawaliwa zamani lakini sasa tuko huru na tufanye maamuzi kama taifa huru blila kushurutiwa na mtu au taifa au kundi lolote.
      Unalazimisha au unatoa maoni? sijakupata uzuri

    8. #566
      Sideeq's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th December 2009
      Posts : 1,603
      Rep Power : 801
      Likes Received
      213
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By not so wise
      Watanzania hawawezihesabiwa kwa kutumia Dini,Hattuwezi kuruhusu kuhesabiwa kama makundi tofautimalengo ya sensa hayahitaji kufahamu uwingi wa makundi hayo bali uwingi wa watanzania kwa ajili ya maendeleo.
      Tulitawaliwa zamani lakini sasa tuko huru na tufanye maamuzi kama taifa huru blila kushurutiwa na mtu au taifa au kundi lolote.
      Tatizo lenu jingine! mmejisahau kabisa kuwa Waislamu nao ni Watanzania!........Hii nchi bora igawanywe kimajimbo tu (ya Kiislamu na Kikristo) ili kuukata huu mzizi wa fitna.
      KALAMAZOO1 likes this.

    9. #567
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Kwa waliosoma Marketing wanajua kitu kinachoitwa PEST analysis.Hapa pia utakuta kuwa kujua idadi ya watu kidini inasaidia katika kufanya Marketing.Ukienda katika maktaba ya Uingereza (British Library) mjini London utakuta data za kila nchi ili ziwasaidie katika uwekezaji(Country risk),hapa utakutana na idadi ya nchi na idadi ya waumini wa dini mabalimbali.Pia data za idadi ya watu kidini zinasadia kama mtu anatka kufanya NICH marketing

    10. #568
      Kingo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th May 2009
      Posts : 372
      Rep Power : 585
      Likes Received
      54
      Likes Given
      108

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Baada ya kujua idadi ni kuangalia mgawanyo wa ajira na wingi wa watu kidini, halafu mgogoro unaanza bila kungalia vigezo na uwezo wa utendaji kazi. Dini tu ndo itaangaliwa katika ajira, then elimu, nk

    11. #569
      barakaisbaraka's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 14th April 2012
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      2

      Default Re: BAKWATA haitoshiriki zoezi la Sensa mwaka huu......!!

      Sorry the reply "very sensible....." Was meant for ha ha ha "ii you find yourself in a hole the first thing to do is stop digging"

    12. #570
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Kingo
      Baada ya kujua idadi ni kuangalia mgawanyo wa ajira na wingi wa watu kidini, halafu mgogoro unaanza bila kungalia vigezo na uwezo wa utendaji kazi. Dini tu ndo itaangaliwa katika ajira, then elimu, nk
      Sio hivo mkuu,elimu ni muhimu na wapo wasomi wazuri wa dini zote japo sio kwa kiwango sawa.Kuna kazi za kitaalamu kwa mfano udaktari huwezi kuangalia dini kwani hata hivo madaktri waliopo hawatoshi,lakini kazi za kiutawala kama ukuu wa wilaya,uwaziri nk hizi wapo wasomi wa kumwaga kabisa

    13. #571
      Mr. Zero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2007
      Posts : 4,076
      Rep Power : 1436
      Likes Received
      481
      Likes Given
      72

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By ritz
      Kwani kuna tatizo gani kuweka dini kwenye sensa, mbona nchi nyingi duniani wameweka sehemu ya dini, kama Uingereza, Misri, Israel, na hakuna tatizo lolote.
      Kwani waislam wanataka nini kwenye sensa ya dini??? Kama wanawaumini si wawahesabu huko misikitini kama wanavyofanya wakristo. Kwa nini wanang'ang'ania serikali iwafanyie kazi............... Kama kuna waislamu hawaendi msikitini na hawajajiandikisha hao syo waislamu. Kwa hiyo wawaambie mashehe wote wawakilishe idadi ya wafuasi wao na watajua kuna waislamu wangapi TZ. Otherwise, wasituletee mambo ya Uingereza, Misri na Israeli wakati wanajua hapa ni TZ.

      Mbona tuaposema ktunataka katiba huru huwa hamtoi hiyo mifano ya Uingereza, Canada n.k.
      "The Only Necessary for the Triumph of Evil is for Good Men to do Nothing" Edmund Burke (1729 - 97)

    14. #572
      OSOKONI's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th October 2011
      Posts : 3,639
      Rep Power : 1111
      Likes Received
      1001
      Likes Given
      758

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By nngu007
      yeah Waislamu walikuwa wengi, Msisahau pia Wapagani au Wanaoamini Dini za kienyeji walikuwa wengi sana...
      Waislamu wengi ni wepi? ni wale wanaoitwa juma,bakari, seif, ali, mohamed au ni wale wanaoishi kwa kufuata amri za mungu na mafundisho ya mitume wake??ni wapi mnaruhusiwa kuchoma nyumba za ibada za dini nyingine? ni wapi mnaruhusiwa kuiba mali? Uislamu si jina tu hapa ni kuyaishi yanayofundishwa na uislamu!!
      Narrow minded people discuss people,common minded people discuss events great minded people discuss ideas!!!

    15. #573
      Kima Mchanga's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 3rd October 2011
      Location : Dynamic
      Posts : 4,517
      Rep Power : 11229
      Likes Received
      611
      Likes Given
      446

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Haya sasa!
      Watanzania tumefikia hatua mbaya,kujibagua kidini.Lengo kuu la ndugu zangu waislamu kutaka kipengele cha dini ni
      ili wajue wao na wakristo ipi ni dini kubwa tanzania.Kama dhumuni ni hilo,haiingii akilini kodi za watanzania wengine kutumika katika hili;kwani kimsingi sensa lengo lake kuu ni kuwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi wote,bila kujali itikadi zao za kidini!
      Do what you feel in your heart to be right-for yot will be criticized anyway.You will be damned if you do,and damned if you don't

    16. #574
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mr. Zero
      Kwani waislam wanataka nini kwenye sensa ya dini??? Kama wanawaumini si wawahesabu huko misikitini kama wanavyofanya wakristo. Kwa nini wanang'ang'ania serikali iwafanyie kazi............... Kama kuna waislamu hawaendi msikitini na hawajajiandikisha hao syo waislamu. Kwa hiyo wawaambie mashehe wote wawakilishe idadi ya wafuasi wao na watajua kuna waislamu wangapi TZ. Otherwise, wasituletee mambo ya Uingereza, Misri na Israeli wakati wanajua hapa ni TZ.

      Mbona tuaposema ktunataka katiba huru huwa hamtoi hiyo mifano ya Uingereza, Canada n.k.
      Mzee karibu kwenye mada naona wewe ndo kwanza unajiunga.pitia thread za nyma utapata majibu

    17. #575
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By mtu wenu
      Haya sasa!
      Watanzania tumefikia hatua mbaya,kujibagua kidini.Lengo kuu la ndugu zangu waislamu kutaka kipengele cha dini ni
      ili wajue wao na wakristo ipi ni dini kubwa tanzania.Kama dhumuni ni hilo,haiingii akilini kodi za watanzania wengine kutumika katika hili;kwani kimsingi sensa lengo lake kuu ni kuwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo ya wananchi wote,bila kujali itikadi zao za kidini!
      Nawe karibu kwenye mada,ulikuwa umelala nini?

    18. #576
      chitage's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd March 2008
      Posts : 28
      Rep Power : 578
      Likes Received
      36
      Likes Given
      1

      Default Re: tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya Agosti 2012

      Kwa mpango huu Tanzania inaelekea kutokuwa salama teena.Tutaikumbuka kwa uchungu ileee tanzania yenye amani na watu wanaopendana.....ila naamini katika jambo moja,haitofika siku wanadaamu wote wakaamini imani moja bila kutofautiana....hivyo kila mmoja azoee tu kuishi na mwenzake na kuvumiliana katika tofauti zetu..Dunia ni moja na tanzania ni moja.

    19. #577
      Mr. Zero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2007
      Posts : 4,076
      Rep Power : 1436
      Likes Received
      481
      Likes Given
      72

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Kingo
      Baada ya kujua idadi ni kuangalia mgawanyo wa ajira na wingi wa watu kidini, halafu mgogoro unaanza bila kungalia vigezo na uwezo wa utendaji kazi. Dini tu ndo itaangaliwa katika ajira, then elimu, nk
      Rais Muislam, Makamu muislam, Rais wa ZNZ, Makamu wa kwanza na wapili wa Zanzibar ni waislamu. Nafikiri kama hicho kipengere ni muhimu kwa waislamu sidhani kama kunalinaloshindikana. Tatizo hawa wenzetu wamezoea tabia ya kujilizaliza tu!!
      "The Only Necessary for the Triumph of Evil is for Good Men to do Nothing" Edmund Burke (1729 - 97)

    20. #578
      Invarbrass's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2011
      Location : PLANET EARTH
      Posts : 380
      Rep Power : 494
      Likes Received
      74
      Likes Given
      65

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Kuna faida gani kuweka dini kwenye sensa?

    21. #579
      Invarbrass's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th February 2011
      Location : PLANET EARTH
      Posts : 380
      Rep Power : 494
      Likes Received
      74
      Likes Given
      65

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Lu-ma-ga
      Serikali haiwezi kupoteza muda kubembeleza wapiga filimbi wa HAMELINI
      E bwana umenikumbusha huyo jamaa mpiga filimbi

    22. #580
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya Agosti 2012

      Quote By chitage
      Kwa mpango huu Tanzania inaelekea kutokuwa salama teena.Tutaikumbuka kwa uchungu ileee tanzania yenye amani na watu wanaopendana.....ila naamini katika jambo moja,haitofika siku wanadaamu wote wakaamini imani moja bila kutofautiana....hivyo kila mmoja azoee tu kuishi na mwenzake na kuvumiliana katika tofauti zetu..Dunia ni moja na tanzania ni moja.
      Mkuu una busara kweli. Waislamu wana demand serikali iweke kipengele cha dini kwenye sensa lakini wakristu wanapinga.Si waiachie serikali? wao kinachowauma nini? ni ukosefu wa uvumilivu

    Page 29 of 62 FirstFirst ... 19272829303139 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...