Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 22 of 62 FirstFirst ... 12202122232432 ... LastLast
    Results 421 to 440 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 886
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. Miaka 50

    3. #421
      M-mbabe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th October 2009
      Location : here n' there
      Posts : 1,297
      Rep Power : 745
      Likes Received
      326
      Likes Given
      352

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Daudi mchambuzi
      Hebu wawekewe hicho kipengele tuone faida yake.
      Labda kuna maandalizi ya jambo flani so wanahitaji kujua idadi yao wajiandae vema.
      Wawekeeni yaishe.

      Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
      mkuu, hapo kwenye red... ndicho kinachofanya hekima ndogo tu iseme "hapana, kipengele cha dini kisiwepo".

      na uthibitisho wenyewe ni kauli kama hii hapa chini....

      7-MADAI YA PONDA NI YAPI?
      ponda anasema "enough is enough. tutumie sensa kama gia ili tujue idadi kisha yaje madai ya kuuliza mbona waislamu ni asilimia 35, 40 50 au 55 lakini kwenye ajira asilimia 9!!!!!!!?" NI BOMU AMBALO LIPO NA LITAPASUKA. NATABIRI KUWA kama kipengele cha dini hakitawekwa, waislamu watatafuta haki ya uwiano kiajira kwa njia ambazo zitavunja amani.
      Daudi Mchambuzi likes this.
      If you're not ready to die for it, put the word 'freedom' out of your vocabulary (Malcolm X)

    4. #422
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,668
      Rep Power : 975
      Likes Received
      580
      Likes Given
      10

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hata bajeti iliyotangazwa leo inawapendelea wakiristo!!!

    5. #423
      Angel Msoffe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2011
      Posts : 6,266
      Rep Power : 1825
      Likes Received
      1397
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      waislamu wanapenda malumbano yasiyo na tija.

    6. #424
      kekuwetu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Location : home
      Posts : 120
      Rep Power : 459
      Likes Received
      16
      Likes Given
      41

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      mbona hiyo ni rahisi kwa waislam, nadhani wanahitajika kufanya sensa yao wenyewe, wajipange, wafanye sensa yao kwa kuwahusika viongozi wa dini kwa kila mitaa.
      Kaa la Moto and MndemeF like this.

    7. #425
      mkurugenz's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 200
      Rep Power : 400
      Likes Received
      15
      Likes Given
      16

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      kwa nchi kujua idadi ya watu na dini zao si tatizo,baada ya kuanza kuhusisha udini na uongozi ndipo tatizo la kuto aminiana ktk dini linapokuja, ki ukweli ni nafikiri kiongozi wetu kashindwa kudhibiti dhana ya udini nchini na waislam kwa udahifu wa president na wakiamini ni wao peke yao hawaishiwi vituki vya udini,hatutuafika kwa mtindo huu bakwata waachw watu wa sensa wafanya kazi yao
      MndemeF likes this.

    8. FemaTV & Radio

    9. #426
      MndemeF's Avatar
      Member Array
      Join Date : 15th January 2011
      Posts : 32
      Rep Power : 429
      Likes Received
      2
      Likes Given
      3

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Mimi sielewi kwanini lazima tuhesabu watu kwa kufahamu dini zao. Kwani hilo la dini linahusina nini na lina tija gani katika sensa ya taifa?!

    10. #427
      proisra's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th June 2012
      Posts : 116
      Rep Power : 372
      Likes Received
      35
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Tumeshajua mikakati yenu, ajenda yenu ya siri ni kutafuta uhalali wa mahakama ya kadhi, kwani mtasema endapo sensa ya 2012 iliulizia dini za watanzania kwa gharama ya serikali, kwa nini mahakama ya kadhi isianzishwe na kugharamiwa na serikali..... Naamini wengi mtasoma maoni haya, lakini inahitajika akili ya form 2 au form one kuweza kubaini ujanja huu. Siyo muhimu sana kwenda vidato vya juu na universities kuwasoma hawa ndugu. Kwani wameshindwa kujihesabu wenyewe? Si kweli, kila kitu wanataka serikali iwafanyie: Chuo kikuu cha Morogoro, majengo walipewa bure na serikali, sasa wameshazoea. Kwa hiyo mnaagalia Quantity badala ya Quality. Zaeni mkaijaze nchi, bara na visiwani mkidhani faida.

      Shida niionayo hapa ni ufinyu wa elimu. Pili, ni ile hali ya 'inferiority complex', kujihisi kwa nini.... kwa nini wale.... kwa nini sisi..... Serikali najua itakachofanya. Wachache wenu wataitwa ikulu kisirisiri, watapewa mshiko, halafu utaona vyombo vya habari vikitoka na habari ktk front pages "BAKWATA wakubaliana na sensa 2012". Hii siyo siri wala mizaha, imetokea kwani CCM hao hao wamepandikiza udini hapa Tanzania hasa baada ya JK kuingia madarakani kwa ile ilani ya 2005. Sasa wanahaha, hawajui waende wapi. Na bado CCM inawatumia mashekhe ktk chaguzi ili watoe matamko ya udini na kuchonganisha watanzania (KUMBUKENI Tamko la Mashekhe wa Igunga ktk uchaguzi mdogo).

      CCM waliotesha hii michongoma ktk akili za hawa jamaa, ni kazi yao pia kuifyeka au kuipogolea. Bye

    11. #428
      S.Liondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2011
      Posts : 338
      Rep Power : 476
      Likes Received
      55
      Likes Given
      6

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Waislamu wanataka kupima nguvu ya waliyonayo kupitia wingi. Wakishabaini kuwa wao ni wengi, basi kila siku serikali itashinikizwa kuingiza mambo yanayowahusu wao katika Serikali na sheria ya nchi. Hawa jamaa wana mashinikizo Mengi dhidi ya Serikali na dini nyingine. Mfano: Uanachama wa Tz katika OIC na Mahakama ya Kadhi, Wakiisha kuyapata hayo, mengine watakayoongeza ni: Ijumaa kuwa siku ya mapumziko, Kila mtanzania kutopika wala kula kipindi cha mfungo wa Ramadhani, hii ni pamoja na hoteli zote kufungwa kipindi hicho, Wanawake wote kuvaa kininja hata kama wewe si Mwislamu, kutumika kwa sharia Tanzania nzima, kuifanya tanzania kuwa nchi ya kiislamu, na mwishowe, kuanzu kuchoma makanisa yote kama ilivyo kule Zanzibar.

    12. #429
      Edward Teller's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st October 2010
      Location : Area 51
      Posts : 3,431
      Rep Power : 1120
      Likes Received
      570
      Likes Given
      612

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By David webb
      Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%. Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo. Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
      hio ni mwaka 1957,hujajua coverage ya hio sensa ilikuwa vipi,na wapi hawakuweza kufika. sensa ya 1967 ilionyesha kipengele cha dini,na wakristo walikuwa wengi,1977 the same,ndipo wakazuia hicho kipengele
      Quote By Jasusi
      Sensa ya mwaka 1957 haikuonyesha idadi ya Waislamu kuwa 65%. Pia kuna sensa iliyofuata 1967 pia ina takwim inayoonyesha idadi ya Waislamu na Wakristo. Kwa hiyo si sahihi unaposema kuwa baada ya 1957 sensa zote zilizofuata zilifuta kipengele kinachoonyesha dini za watu.
      kuna watoto wa miaka ya 90's wanadakia mambo hawajui taarifa kama hizi
      Quote By Baija Bolobi
      Tukimaliza kuhesabu Waislam, watasema tuhesabu na wasiosali swala tano, wasiofunga mwezi Mtukufu, wasiovaa hijab, wenye wake wawili, n.k. Hii ni kwa sababu ikiwa mtu unang'ang'ania kipengele cha dini katika sensa, ina maana unataka kufanya mipango fulani iendane na jinsi watu walivyo waaminifu katika dini yao. Jamani hawa wananifanya nijione siko Tanzania! Hoja wa dini fulani kuwa inataja idadi ya waumini wake ni ya kitoto kwa sababu kuna baadhi ya madhehebu yana utaratibu wake wa kufanya sensa ya waumini wake.
      ukiangalia sana ukishakuwa mtu wa dini flan,basi unakuwa ni tatizo kwenye kila kitu-waislmu si wapo wengi huko uarabuni-sioni cha muhim wanachofanya. mimi ninataka serikali ifanye utaratibu ijulikane nani wapo weng then tuone hali itakuwaje,maana kama watapewa majibu tofauti lazima watabwatuka tu, Kwa wakristo ni simple sana ku-round off idadi yao,maana kuna system ya kuwa na kadi na mambo mengine,so unaweza kupata data za active adherents-kwa hio ni simple sana kuwa na ufaham wa idadi kamili-sasa hawa wasiojua kitu wanakuwa wanapiga blah blah tu, naomba wakubaliwe wapewe idadi then tuone watafanyaje- BTW,naomba mnisaidie-swala la sensa ni swala la muungano?
      “Talk slowly but think quickly”

    13. #430
      Nanren's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th May 2009
      Posts : 1,047
      Rep Power : 720
      Likes Received
      363
      Likes Given
      561

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mdondoaji
      Wewe shida yako nini? Mbona nyie mna TAG, Catholics, Lutheran and etc hamsemi? Hakuna kinachogawanyika huu ni upumbavu kwasababu suala la dini ya mtu lina umuhimu katika mipango miji ya nchi. Mfano Uingereza hamuwezi tu kujenga msikiti au kanisa hadi upewe kibali na halmashauri ya jiji. Sasa unadhani kwanini wamesisitiza halmashauri ndio zitoe vibali? Tatizo lenu mnasumbuliwa na UDINI TU!!!! Suala la dini lina umuhimu mkubwa sana katika maendeleo ya nchi yetu . Dini itatusaidi kujua yafuatayo nawaelekezi nchi vihiyo wa udini:-
      a. Tufahamu katika kila eneo ni nyumba za ibada ngapi zijengwe (misikiti, makanisa au masinagogi) na vile vile maeneo ya kuzikana yatengwe kiasi gani yaani makaburi. Hivyo basi dini itatusaidia katika mipango miji nchini mwetu.

      b. Tufahamu sababu za kurudi nyuma kimaendeleo (mfano waislamu) je imesababishwa na wao wenyewe? taasisi au mfumo mbovu uliopo?

      c. Tufahamu mfumo wa nchi kiutendaji unakuwaje tukijumuisha na imani za watu kama sehemu ya maisha yao mfano ni likizo ngapi ziwepo katika nchi kama sikukuu za mapumziko. Uingereza mfano au Marekani hawana kitu kinaitwa public holiday for Eid but wana public holiday for Christmas, New Year, St. Patricks etc. Saudi Arabia, UAE, na Oman hawana sikukuu za Christmas and New Year. Ni kwasababu ya sensa wameona hakuna umuhimu wa kupumzika siku hizo. Sasa taarifa hizo hakuna mahali zinatoka zaidi ya katika sensa ILIYOANDALIWA NA SERIKALI YA MLIPA KODI!!!!

      d. Kufahamu pia usambazi wa vyakula nchini. Mfano waislamu wana mwezi mtukufu wa ramadhani na huwa wanatumia vyakula vya aina fulani nchini. Vile vile wakristo wana Kwaresma huwa pengine wanatumia vyakula vya aina fulani. Hatuwezi kufahamu hilo bila ya kuwepo takwimu sahihi.

      Hembu nipeni nyie sababu za msingi kisiwepo kipengele cha dini zaidi ya fear zilizogubikwa na imani za ubaguzi wa kidini???
      Mdondoaji, I didn't expect this from you. It is too low. I'm disappointed.
      Kama ni hivyo tu-include na ukabila. Maana kuna makabila yapo nyuma (mfano Hadzabes), ili pia tufahamu wako nyuma kwa sababu gani. Na pia iwe rahisi kuwasambazia vyakula ndugu zetu wakati wa various festivals, mfano, tuwasambazie senene wahaya, na nyama ya fungo tuwasambazie wamakonde...

      Serikali isiyo na dini wala kabila, inapanga mikakati ya kumuendeleza raia bila kujali dini yake au kabila lake. That information (dini na kabila) is not important kwenye development plans and projections. C'mon, you know that...
      Mdondoaji likes this.

    14. #431
      proisra's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th June 2012
      Posts : 116
      Rep Power : 372
      Likes Received
      35
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mtemakuni
      Most of time we see and judge the smoke bt who set the fire anaachwa aside..!! Hv ni kwanini tunapenda sana kuchokonoa mambo ya udini..!! Do we real know the consequences of it..? Hao mapadri walifanya lini hiyo sensa na kupublish hizo figures..? Na hata kama walifanya kwanini wasibaki nazo makanisani na kwanini walifanya na kwanini sasa hv hawataki kipengele cha dini kiwekwe ili kuconfirm walichokua wanakitafuta..? Me nadhani serikali ikae tena na viongozi wa dini zote mpaka freemansons walizungumze kwa kina hili na kama ni provocative waban kabisa swala la madhehebu kuhesabu waumini na hao waliopublish sensa zao zifutwe na kupigwa marufuku..!!
      Jamani tusiwashe moto tusioweza kuuzima...!! Wengine tutakua tunawaangalia tu kwenye tv mkiuana pamoja na hao viongozi wenu wanafiki ..!!
      ARE WE CONCERNED WITH THE QUALTITY OR QUALITYY? Makanisa kuhesabu waumini wao, kosa liko wapi? Je uhuru wa Tanzania unaishia mitaa ipi? Kwani umuhimu wa takwimu ni upi, zaidi kwamba husaidia kujua jinsi utakavyoendeleza watu wako au raslimali zako. Sioni shida, ingawa siyo mkatoliki, kama waliwahi kuhesabu waumini wao, it is fine. Kwani waliomba serikali kugharamia? Sasa Waislamu wameshindwa nini kuitisha majina yao, au takwimu kama hizi hazina faida kwao? Acheni maneno, hizi ni harufu za MAHAKAMA YA KADHI NA O.I.C.

    15. #432
      Mag3's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 31st May 2008
      Posts : 3,533
      Rep Power : 1803
      Likes Received
      2450
      Likes Given
      2493

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hakika inashangaza;

      1. Chama tawala Tanzania ni CCM na mwenyekiti wake ni Muislaam,
      2. Tanzania tunao Raisi wawili na wote ni Waislaam.
      3. Anayeunda serikali na kuiongoza ni Muislaam
      4. Anayewateua watendaji wakuu pamoja na Waziri Mkuu ni Muislaam.
      5. Tanzania tunao Makamu wa Raisi watatu na wote ni Waislaam.
      6. Jemadari Mkuu wa majeshi Tanzania ni Muislaam.
      7. Mkuu wa polisi Tanzania ni Muislaam.
      8. Mkuu wa Usalama wa Taifa ni Muislaam.
      9. Mkuu wa Mahakama Tanzania ni Muislaam.
      10. Ardhi yote ya Tanzania ni mali ya serikali inayoongozwa na Muislaam.

      Katika hali kama hii, mfumo Kristo unawezekanaje? Je, hali ingekuwaje kama mambo yangekuwa tofauti? Kama pamoja na huu ukweli bado mfumo Kristo umeweza kushamiri, basi sidhani kugomea sensa kutafanikisha lolote...ni mawazo yangu tu!
      The true sign of intelligence is not knowledge but imagination.
      Education is what remains after one has forgotten what one has learned in School
      -Albert Einstein.

    16. #433
      malema 1989's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2012
      Posts : 806
      Rep Power : 741
      Likes Received
      147
      Likes Given
      117

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      kumbe ndio maana wanahimizana kuoa wake wengi na kuzaa bila mpango hata kama hawawezi kulea familia kubwa, mmejidhihirisha hadharani sasa . Mipango yenu kwishne labda huko huko misikitini kwenu!

    17. #434
      Macos's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th May 2008
      Posts : 777
      Rep Power : 718
      Likes Received
      167
      Likes Given
      13

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Tume ya katiba
      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      BAKWATA sio wanao husika na taarifa jio wewe sijui umeipta wapi.Sheikh Kundecha SIO KIONGOZI WALA MSEMAJI WA BAKWATA YEYE NI KIONGOZI WA BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KISLAM ..BAKWATA HAIHUSIANI NA HAWA..
      KAREKEBISHE TAARIFA YAKO

    18. #435
      malema 1989's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2012
      Posts : 806
      Rep Power : 741
      Likes Received
      147
      Likes Given
      117

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      bila kusahau wanungunikaji wakubwa na wachoma makanisa pia ni waislamu.

    19. #436
      Unstoppable's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th January 2011
      Posts : 938
      Rep Power : 611
      Likes Received
      330
      Likes Given
      2041

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mpangamji
      Hizo data zinapewa nguvu kwa sababu ipi, kama wanaona wakristu wametangaza cooked data na wao watangaze roasted data. tatizo liko wapi hapo. Hii nchi si ya kidini, mnataka tujue mko wangapi kiserikali ili tufanyeje?
      Ha ha ha! Take five my friend! Kwakweli sipendi mashindano yasiyo na kichwa wala mguu. However, labda serikali ilipowakatalia ingewapa suggestions kufanya sensa through taasisi zao. By the way, kuna watu wanabadilisha dini ili kuolewa na ndoa ikienda mrama wanarudia dini zao, kuna wenye vitambulisho vya dini mbili (yes dini mbili) i.e. ana badilisha identification e.g. passport depending na nchi anayokwenda, watu/taasisi anayofanya nayo biashara, shule anayosoma etc. Kuna waliozaliwa na wazazi wa dini tofauti na hawajitambui wao ni dini gani hasa ; sasa Hawa sijui watajaza dini gani. Je ikiwekwa dodoso ya dini kwenye form za sensa kuna option yakutojaza dodoso hiyo?

    20. #437
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,695
      Rep Power : 904
      Likes Received
      432
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By proisra
      Tumeshajua mikakati yenu, ajenda yenu ya siri ni kutafuta uhalali wa mahakama ya kadhi, kwani mtasema endapo sensa ya 2012 iliulizia dini za watanzania kwa gharama ya serikali, kwa nini mahakama ya kadhi isianzishwe na kugharamiwa na serikali..... Naamini wengi mtasoma maoni haya, lakini inahitajika akili ya form 2 au form one kuweza kubaini ujanja huu. Siyo muhimu sana kwenda vidato vya juu na universities kuwasoma hawa ndugu. Kwani wameshindwa kujihesabu wenyewe? Si kweli, kila kitu wanataka serikali iwafanyie: Chuo kikuu cha Morogoro, majengo walipewa bure na serikali, sasa wameshazoea. Kwa hiyo mnaagalia Quantity badala ya Quality. Zaeni mkaijaze nchi, bara na visiwani mkidhani faida.

      Shida niionayo hapa ni ufinyu wa elimu. Pili, ni ile hali ya 'inferiority complex', kujihisi kwa nini.... kwa nini wale.... kwa nini sisi..... Serikali najua itakachofanya. Wachache wenu wataitwa ikulu kisirisiri, watapewa mshiko, halafu utaona vyombo vya habari vikitoka na habari ktk front pages "BAKWATA wakubaliana na sensa 2012". Hii siyo siri wala mizaha, imetokea kwani CCM hao hao wamepandikiza udini hapa Tanzania hasa baada ya JK kuingia madarakani kwa ile ilani ya 2005. Sasa wanahaha, hawajui waende wapi. Na bado CCM inawatumia mashekhe ktk chaguzi ili watoe matamko ya udini na kuchonganisha watanzania (KUMBUKENI Tamko la Mashekhe wa Igunga ktk uchaguzi mdogo).

      CCM waliotesha hii michongoma ktk akili za hawa jamaa, ni kazi yao pia kuifyeka au kuipogolea. Bye
      ...get LIKE!natumia cm

    21. #438
      Mzee wa fund's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Posts : 493
      Rep Power : 533
      Likes Received
      78
      Likes Given
      2

      Default

      Quote By David webb
      Sensa ya mwaka 1957 ya kikoloni kipengele cha kuonesha dini kilikuwepo na ndio kinachoonesha takwimu waislamu wangapi na wakristo wangapi, na ukiangalia mwaka huo 1957 waislamu walikuwa ni 65%.

      Baada ya hapo sensa zote zilizofuata kipengele cha dini kilifutwa; ajabu leo hii watu wanasema wakristo wapo wengi kuliko waislamu kwa takwimu zipi ikiwa kipengele cha kuorodhesha watu dini zao hakipo.

      Pili ni kwanini wanaogopa kuhesabu watu kwa kutumia kigezo cha dini? Wengi watasema wanaogopa udini, hii hoja ni dhaifu maana nchi nyingi duniani sensa zinahebabiwa kwa mtindo wakujua idadi ya watu na dini zao ni asilimia ngapi katika nchi hizo.
      Haya bwana.napita tuu.nitarudi.

    22. #439
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,695
      Rep Power : 904
      Likes Received
      432
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By Macos
      BAKWATA sio wanao husika na taarifa jio wewe sijui umeipta wapi.Sheikh Kundecha SIO KIONGOZI WALA MSEMAJI WA BAKWATA YEYE NI KIONGOZI WA BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KISLAM ..BAKWATA HAIHUSIANI NA HAWA..
      KAREKEBISHE TAARIFA YAKO
      ...kumbe sio bakwata?mbona hamueleweki nyie?kajipangeni,ndo mje na hoja

    23. #440
      Waridi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th March 2008
      Posts : 854
      Rep Power : 739
      Likes Received
      88
      Likes Given
      84

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Serikali inahesabu raia wa nchi 'Sensa itaambatana na ugawaji wa vitambulisho vya uraia; hujahesabiwa na kitambulisho chako hakitengenezwi, na kwa hiyo wewe sio raia, na kwa hiyo...' Bora taasisi husika za kidini zingeomba uwezesho wa serikali katika kuhesabu waumini wao.

    Page 22 of 62 FirstFirst ... 12202122232432 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...