Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 20 of 62 FirstFirst ... 10181920212230 ... LastLast
    Results 381 to 400 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 886
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. Miaka 50

    3. #381
      Mgombezi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd March 2009
      Posts : 628
      Rep Power : 643
      Likes Received
      130
      Likes Given
      139

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Tume ya katiba
      Nabii mtarajiwa mizambwa, haukuoteshwa kuwa kuna siku itafikia waislam wataamka na kudai haki zao zinazonyonywa na watanzania wenzao?
      Huu ni mtazamo mbaya sana, inonekana mbegu ii imepandwa kwa miaka mingi na sasa immeanza kuzaa matunda.
      Ebenezer

    4. #382
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1255
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Dinya
      Harooo Ntamahoro! Eti "These people are narrow minded", Kweli, are they or are you? You clever people, educated, civilized but drankards, fornicators, corrupt people. The country is under your leadership bro, you clever people. You know sometimes I remember the story of a psychitrist who wanted to find out who, among his patients is cured. He drew an image of a door on the wall using a piece of chalk and commanded the patients " Go out all of you". They began to struggle to open the door but one clever!educated guy like you just stood aside wondering about those opening the imaginery door!!! When asked why he isn't going out? He replied "I am just watching them, they are opening the door while I have the keys!!! The doctor said "I thought you are cured but now I know you are the C-r-a-Z-i-e-S-T".T-he t-he t-hee he he eheeeeee! ndo ninyi wagala. Think you are clever but you are just like that clever guy. We aren't narrow minded buddy, we are oppressed people, exploited people, ensalved people in the slavery of ignorance. You know what, was it not Martin Luther King who said "It is not the evil-doors who are to blame but those who keep quit about the evils". Just opne up your mind, how can a country develop when half of its population is systematically marginalized since colonial time? Do you read history books of rationally minded people or you are aaah busy with safari moja huanzisha nyingine? acheni bwana, mnaimaliz anji hii kwa udini wenu. You always think about Muslims with negativities no positivities because you are selfish, greedy, materialistic, febble-minded aaahh! Inatosha wka leo.
      (inferiority complex + self-negativity) = part and parcel ya waislam Tanzania... ohh tunadhulumiwa ooh tunafelishwa oooh tunanyimwa ajira serikalini...wewe ukikutana na mtu anayelalama kila siku anaonewa wakati wenzake kwenye mazingira hayohayo wanajitahidi na kufanikiwa utamwitaje? Kama mtu mwenyewe anajiona inferior wewe utamuonaje? acheni hizo mambo mengine ni ya kujitakia wenyewe halafu mnalalamika...

    5. #383
      debito's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Posts : 151
      Rep Power : 417
      Likes Received
      27
      Likes Given
      9

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      hakyanani sijui tunakwenda wapi sensa ni kwa maendeleo ya wananchi na c kwa maendeleo ya dini au dhehebu watu c waelewa

    6. #384
      Inanambo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2011
      Posts : 614
      Rep Power : 522
      Likes Received
      97
      Likes Given
      20

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Nashindwa kuwaelewa Waislamu. Kama shida ni kujua IDADI yenu kwa nini msihesabu huko msikitini mnapoSWALI kila sku mkajuana msikiti huu una wanaume, wanawake, watoto kiasi gani mkamjulisha takwimu hizo msikiti hadi msikiti mjue Idadi yenu Tanzania mzima? Nyie mmejijengaje kama hamjui hata Idadi yenu? Mnataka serikali iwafanyie sensa hakika mnaboa na matakwa yenu ya kulazimisha kila kitu mfanyiwe. Nina imani Wakristo madhehbu yote wanajua idadi yao kwa sababu wao hujisajili kila mwaka kwa ajili ya kupatiwa huduma za kiroho na kimwili. Hawalazimishi serikali hata siku moja kutoa idadi yao kwa sababu sensa haina lengo la kutoa huduma za jamii kwa mtazamo wa dini. huduma za Jamii hutolewa kwa kila mtanzania hata awe Banyani.

    7. MTK
      #385
      MTK's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th April 2012
      Posts : 928
      Rep Power : 4494
      Likes Received
      300
      Likes Given
      329

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Tume ya katiba
      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.

      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.

      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.

      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      Waislamu nao! hivi mpaka leo hajui umuhimu wa sensa ya watu kwa taifa, hawa watu akili zao vipi jamani???????!!!!!!!!!!.
      kwa hili serikali isimame kidete; wote watakaobainika kuchochoea baadhi ya waislamu kugomea sensa ya taifa wakamatwe na kushitakiwa kwa kuhujumu uchumi wa taifa.

    8. FemaTV & Radio

    9. #386
      Jumakidogo's Avatar
      R I P Array
      Join Date : 16th July 2009
      Location : DOM & DAR
      Posts : 1,868
      Rep Power : 1176
      Likes Received
      390
      Likes Given
      42

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Mi nadhani kipengele cha kutambua idadi ya walevi nchini na kiwepo kwani wao ndio wanachangia kodi kubwa sana katika pato la taifa. Kwa nchi walevi ni watu muhimu kuliko hata dini, lazima idadi yao ijulikane!
      Buswelu and angedizzle like this.

    10. #387
      tusichoke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2011
      Posts : 657
      Rep Power : 543
      Likes Received
      77
      Likes Given
      8

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Tatizo ni pale ambapo ombi likikubaliwa na matokeo yakitangazwa iwapo itanyesha waislam ni wachache itakuja hoja ya kwamba sensa imechakachuliwa ,mara waliochukuwa takwimu ni watu wa dini fulani etc

    11. #388
      NG'OMBE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th March 2011
      Posts : 290
      Rep Power : 437
      Likes Received
      60
      Likes Given
      125

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      kwa hiyo hata rais na makamu wa rais hawatahusika na zoezi hili? au ni waislamu wa wapi ambao hawatashiriki?. Hivi kujua idadi ya waumini wa kislamu hadi sensa ya Taifa? Hamuwezi kupitisha daftari katika misikiti yenu mkajua idadi yenu au mna jambo nyuma ya pasia.

    12. #389
      Msemaovyo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2010
      Posts : 391
      Rep Power : 511
      Likes Received
      82
      Likes Given
      59

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Mwalimu wangu mmoja aliwahi kutufundisha kuwa religion is an Opium of Mind yaani na bangi kwenye mawazo ya mtu.Hii dini haiwasadii waumini wake kutoka kwenye matatizo waliyonayo but inawafundisha kulalamikia vitu visivyowezekana.Nina jamaa yangu ni HR sehemu flani ametangaza kazi 10 kapokea application zinazoqualify 100 na kati ya 17 tu ndo waislamu sasa hapa akichukua mathalani wakristo 10 na waislamu wawili mtajiteteaje?kwamba dini imekuwa kigezo?wacheni kelele nendeni shule mkaelimike mkomboe mapoyoyo wenzenu kama Ponda na Kundecha.
      sweke34 likes this.

    13. #390
      GEMBESON's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th April 2012
      Location : Tanganyika
      Posts : 209
      Rep Power : 399
      Likes Received
      25
      Likes Given
      41

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Ninaweza
      Baada ya kujua idadi ya wana imani fulan!, nini kitafata?
      Baada ya hapo, ikibainika sisi wa dini fulani tuko wengi kwa zaidi ya 65%, tutailazimisha serekali yetu sikivu ianzishe mahakama ya kadhi.
      Ninaweza likes this.

    14. #391
      Mr Emmy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2012
      Posts : 631
      Rep Power : 594
      Likes Received
      74
      Likes Given
      16

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Ushauri kwa Bakwata na Waislam wote

      Mkitaka kujua idadi ya Waislam Tanzania ni Rahisi Sana, Kila Shekhe na Maustadhi katika mitaa wanayoishi wahesabu Wanawake/ Watu wa Jinsia ya Kike wanaovaa Hijabu na Wanaumme/ Jinsia ya Kiume wanaovaa suruali fupi na waliofuga Ndeve/ Mzuzu na kufunga vilemba kichwani. Kwakufanya hivyo mtapata idadi iliyosahihi ya Waislam Tanzania na kuondoa dukuduku linalowakabili
      .
      Uhuru wa kweli wa Taifa utaletwa na Mapinduzi ya kweli ya Fikra ndani ya Wanachama na wapenzi wa CCM!@

    15. #392
      Mr Emmy's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2012
      Posts : 631
      Rep Power : 594
      Likes Received
      74
      Likes Given
      16

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      <SPAN style="COLOR: #b22222"><STRONG>Ushauri kwa Bakwata na Waislam wote<BR><BR>Mkitaka kujua idadi ya Waislam Tanzania ni Rahisi Sana,&nbsp;Kila&nbsp;Shekhe na Maustadhi katika mitaa wanayoishi wahesabu Wanawake/ Watu wa Jinsia ya Kike wanaovaa Hijabu na Wanaumme/ Jinsia ya Kiume wanaovaa suruali fupi na waliofuga&nbsp;Ndeve/ Mzuzu na kufunga vilemba&nbsp;kichwani. Kwakufanya hivyo mtapata idadi iliyosahihi ya Waislam Tanzania na kuondoa dukuduku linalowakabili</STRONG></SPAN>.&nbsp;
      Uhuru wa kweli wa Taifa utaletwa na Mapinduzi ya kweli ya Fikra ndani ya Wanachama na wapenzi wa CCM!@

    16. #393
      iron2012's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 16th February 2012
      Location : Dar es Salaam-Tanzania
      Posts : 309
      Rep Power : 427
      Likes Received
      58
      Likes Given
      53

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      tumia nguvu na juhudi katika kuswali na si kutegemea serikali ikutafutie idadi yenu mfano kanisa katoliki ina utaratibu wake wa kufanya sensa kwa waamini wake na hivyo inakuwa na uelewa wa idadi yao bila kutegemea serikali, kwa nn nyie mtake serikali ndiyo iwahesabie uvivu wa kufikiri my take.

    17. #394
      mzaire's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 10th April 2012
      Posts : 200
      Rep Power : 399
      Likes Received
      40
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Mpangamji
      Hivi nyie huwa mnatumia ubongo wa masaburi kufanya maamuzi!

      Kama mnataka kujua mko wangapi fanyeni sensa yenu, kila shehe kwenye msikiti wake ahesabu waumini wake muwajumulishe. Kwa madai yenu ya kuhesabiwa kwenye sensa, Mnataka serikali itambue mko wangapi itusaidie nini, mnataka kujua wapi mnaweza kujitoa mhanga mkaua wakristu wengi zaidi na wapi msijitoe mhanga.

      Fanyeni sensa yenu wenyewe na serikali itaendelea na taratibu zake.
      Ok, sawa tutafanya ya kwetu na nyinyi wakristu na serikali fanyeni ya kwenu.

    18. #395
      Chesty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2009
      Posts : 1,044
      Rep Power : 703
      Likes Received
      155
      Likes Given
      20

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By ntamaholo
      kwani kwa mzee wa upako ni wakristo? si utambulisho wao ni miliki ya mzee wa upako?
      Itabidi sasa tusaidiane ukristo maana yake nini maana Illuminati wamedanganya watu wengi na sasa imetosha, mkristo ni mfuasi wa Yesu Kristo,sio DINI.

      Wafuasi wa Yesu walipatikana kwa wao kuamua kumfuata Yesu na wakiwa na akili zao timamu, kama akina Peter, Paul, n.k. Hawakuzaliwa wakristo kama ilivyo kwetu leo. Something is wrong with what we refer today as Christianity.

    19. #396
      Chesty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2009
      Posts : 1,044
      Rep Power : 703
      Likes Received
      155
      Likes Given
      20

      Default Re: tamko la BAKWATA kuhusiana na sensa ya Agosti 2012

      Quote By zomba
      Ili malumbano ya nani wengi yaishe na tunataka ile 83/17 ikome.
      Halafu malumbano yakishaisha what next...

    20. #397
      Kakalende's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2006
      Posts : 2,911
      Rep Power : 1228
      Likes Received
      381
      Likes Given
      371

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hivi tangia lini Bakwata wakawasemea waisilamu wa Tanzania? Hawa mashekhe wasubiri kutangaza mwazi na sikukuu ya Idd haya mengine wanajaribu kutikisa kiberiti kuona kama kuna njiti!
      Volunteers are not paid -- not because they are worthless, but because they're priceless!

    21. #398
      Hodarism's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 89
      Rep Power : 377
      Likes Received
      13
      Likes Given
      3

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Waislamu hii ni kazi nyepesi tu sensa ikishamalizika iteni waislamu wote misikitini halafu wajumlishe halafu mtoe idadi ya serikali iliyopatikana. Hapo mtajijua idadi yenu. msitupelekepeleke kama mnaishi peke yenu nchini. na nchi mnazozitolea mifano nendeni huko nanyi mkahesabiwe. wote wanaoongelea udini hawana cha kufanya zaidi ya kuwa makaburu tuliowakataa.

    22. #399
      Hodarism's Avatar
      Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 89
      Rep Power : 377
      Likes Received
      13
      Likes Given
      3

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      wajumlishe (Misikitini) na watoe idadi itakayopatikana kutoka serikalinivery simple

    23. #400
      Kahinda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th February 2009
      Posts : 410
      Rep Power : 606
      Likes Received
      33
      Likes Given
      23

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By ntamaholo
      hivi hamwezi kuhesabiana ninyi kwa ninyi? mbona kila kanisa linajua lina waumini wangapi active na inactive, ninyi mmeshindwa nini?
      Sioni tatizo hapa la kujua idadi ya makundi mbalmbali ya jamii, kama hakuna ajenda ya siri. Kama wakristo wana taratibu za kujua idadi ya waumini wao na amini hata waislamu pia wanao uaratibu kama huo na takwimu kama hizo zinapata nguvu zaidi zikitolewa na serikali maana hilo linakuwa (tamko rasmi).

      Binafsi ningeonelea vyema vikundi vyote viwe vya dini ,jinsia, umri viwe vinaeleweka. Hii inatuondolea utata nimekuwa nikiona takwimu za waislamu na wakristo kwenye taarifa za CIA waislamu %kadha wakristo% na hata wapagani % kadha na wakati mwingine taarifa zao zinapingana, sasa watu wakukosoa hizi taarifa ni sisi kwenye sensa yetu.

      Hivyo basi hakuna tatizo la kujua idadi yetu na hata idadi yetu ki makundi. Kwa ndugu zangu wakristo idadi ya waislamu kwanza hivi karibuni itapungua kwani Zanzibar na Pemba wakijiondoa kwenye Muungano namba kubwa
      ya waislamu wa Tanganyika itakuwa imepungua na Bakwata watakuwa wamepata jibu.Hivyo hakuna haja ya kulihofia hili.

      Jambo la msingi ni kuhakikisha serikali haijiingizi kwenye maswala ya dini, haijalishi rais ni dini gani endapo atakumbatia udini huyo hatufai na wala hatuna sababu ya kumruhusu atuongoze kwa kipindi cha miaka 5.

    Page 20 of 62 FirstFirst ... 10181920212230 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...