Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 16 of 62 FirstFirst ... 6141516171826 ... LastLast
    Results 301 to 320 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 886
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. Study Abroad

    3. #301
      MAMMAMIA's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 25th February 2008
      Location : Near You
      Posts : 3,794
      Rep Power : 3256
      Likes Received
      1496
      Likes Given
      1206

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By ZionTZ
      duuuh mwaka huu lazma JK aombe likizo za kutosha daaah...huyu mzee wa watu hapumui?? likitoka hili linaibuka lile mbaya zaidi ni dini yake, so anakua kwenye tension ya hatari sana...pole JK pole sana duuh!!
      Kwa nini aombe likizo na ndege anayo? Yakimtinga anapanda ndege, huyoooooooo! Akirejeaa anatoa kauli "Huu ni upepo, utapita tu," anbadilisha nguo na kwenda safari nyengine.
      "JF - SAUTI YA WASIO NA SAUTI ............ na wapayukaji"

    4. #302
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 401
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By dotto
      Kwani Hospital ya Bugando, KCMC na zinginezo wanatibiwa Wakristo peke yao tu?? HAwa jamaa hata wawe na midigirii mingapi ni hakuna kabisa!
      Zote zilijengwa kwa kodi za wtz wote na bado zinaendeshwa kwa kodi za watz.kanisa halina ujiko hapo

    5. #303
      RubenM's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th April 2009
      Location : MBEYA
      Posts : 104
      Rep Power : 534
      Likes Received
      7
      Likes Given
      8

      Default

      Kalamazoo1 unakomoa jiweeee????
      Si serikali inajihudumiaaaa ikomeshe tu

    6. #304
      Azimio Jipya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Location : Universal Space Station
      Posts : 3,281
      Rep Power : 5414
      Likes Received
      1006
      Likes Given
      1731

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Kyaiyembe
      Uingereza ni nchi ya Anglikani
      Misiri ni nchi ya Kiislamu
      Israel ni nchi ya Kiyahudi

      Tanzania ni nchi ya imani gani?.
      Tanzania ina Imani ya UTU wa Mtu!

      Na utu wa kiisalam, kikristo, kiyahudi, kipagani etc ni huo huo ... UTU NI UTU period!!!! Hakuna kelele!!

      Utanzania ni Utu ikowapi shida!! Kama utu ukiwa na uisalam wake, ukristo wake, upagani wake ..that isnt our issue .. Issue kwetu ni Utu na Utu ni Utanzania.

      Mimi Ninamuamini MUNGU Ok !! Na Dini yangu Mimi ni UTU!!! Na utu ndio Uungu nadani yagu! Na uisalam, ukristo, upagani wote ni wadau wa Utu hawaupinga hata kidogo!!

      Naheshimu utu wangu na wa kila mtu na kuutetea na kuulinda hadi kiama!! How does that sound!!!!
      Steve Dii and Kyaiyembe like this.
      Never Get Angry; Never Make Threat; Reason With People;
      "Napenda the logic of the words because in some ways it says about individual-not to use emotions-when scrutinizing something, whether it involves you or not" ...-by AshaDiii @ Jamiiforums 26th July 2011.


    7. #305
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,690
      Rep Power : 902
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By Lu-ma-ga
      Idd Simba afikishwa mahakamani kwa kujipakulia fedha za mauzo ya UDA na kiungizwa ktkt account yake ya kifisadi
      .....asante sana mkuu ,umemaliza mkuu

    8. FemaTV & Radio

    9. #306
      Mdondoaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2009
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1483
      Likes Received
      807
      Likes Given
      341

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By MAMMAMIA
      Mimi sipingi suala la dini kuigizwa kwenye sensa kwa sababu ya kuhatarisha amani, kwani kama nilivyosema kwenye post nyengine ya udini, hata tusipoweka idadi ya wenye dini hii au ile tunajuana. Ninachopinga ni kuwa "SENSA NI KWA AJILI YA KUJUA IDADI YA WATU NA KUSAIDIA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO NA KUTOA HUDUMA ZA KIJAMII" kama vile shule, afya, maji, umeme, barabara, mipango miji na sio kujenga misikiti, makanisa, mahekalu, masinagogi n.k.

      Ama kweli "Ibilisi akikosa la kufanya hujipunga nzi kwa mkia wake". Kama BAKWATA, BAGOTI, BAKICHWA, BAMKWE au vyovyote watakavyojiita wanataka kujua idadi ya waumini wao kwa ksababu wanazozijua wao, wafanye sensa yao - kwishney - Tusijiumize vichwa kwa mambo ya kipuuzi kama haya.
      Rubish!!!

      Mipango miji Mamamia pia inajumuisha mchanganuo wa mji ulivyo na watu na maendeleo. Hili suala si la kipuuzi bali la msingi ila linataka kugeuzwa kuwa la kipuuzi kwamaksudi. Hebu nikuulize hujaenda sehemu Tanzania ukaona misikiti imejaa au makanisa yamejaa bila ya sababu ya msingi? Kwanini zile nyumba za ibada zisiwe viwanja vya wazi kwa watoto kuchezea? Makaburi ya kinondoni, kisutu na kwengineko yamejaa hadi tunapumuliana (mtu anazikwa juu ya mtu mwengine) je huoni kuna umuhimu ya kuyapanua?

      Think vizuri badala ya kuwadharau Bakwata na Shura ya Maimamu. Nipeni sababu za msingi kisiwepo hicho kifungu?

    10. #307
      petrol's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 140
      Rep Power : 438
      Likes Received
      45
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By ruttashobolwa
      bora wewe umeliona hilo
      hivi vinatumika vigezo gani kumpata huyo mtu,yaani sheikh

      Swali hilo linanikumbusha wakati ambapo Askofu Kilaini alikataa kujibishana na 'askofu' Kakobe akijhoji vigezo vilivyotumika hadi akaukwa uaskofu. jamani, tuajache kuulizana maswali mazito kiasi hicho.

    11. #308
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 401
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By MAMMAMIA
      Mimi sipingi suala la dini kuigizwa kwenye sensa kwa sababu ya kuhatarisha amani, kwani kama nilivyosema kwenye post nyengine ya udini, hata tusipoweka idadi ya wenye dini hii au ile tunajuana. Ninachopinga ni kuwa "SENSA NI KWA AJILI YA KUJUA IDADI YA WATU NA KUSAIDIA KUANDAA MIRADI YA MAENDELEO NA KUTOA HUDUMA ZA KIJAMII" kama vile shule, afya, maji, umeme, barabara, mipango miji na sio kujenga misikiti, makanisa, mahekalu, masinagogi n.k.

      Ama kweli "Ibilisi akikosa la kufanya hujipunga nzi kwa mkia wake". Kama BAKWATA, BAGOTI, BAKICHWA, BAMKWE au vyovyote watakavyojiita wanataka kujua idadi ya waumini wao kwa ksababu wanazozijua wao, wafanye sensa yao - kwishney - Tusijiumize vichwa kwa mambo ya kipuuzi kama haya.
      Katika mipango miji serikali haitengi maeneo ya ibada? maziko tena kila dini sehemu yake? sasa kama haina data kwa nfano ni banianya wangapi katika mji husika ikakosa kuwatengea sehemu ya ibada huoni huo ni upungufu?

    12. #309
      Hebron Caleb's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 171
      Rep Power : 383
      Likes Received
      43
      Likes Given
      3

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Mbona hawataki kulalamikia mambo makubwa kama elimu katika mashule yanayomilikiwa na taasisi za kiislamu hapa nchini wanaangaika na vitu vidogo kama hivyo?? Mbona Wwakristo nao hawalalamiki kwamba ni kwanini sensa hiyo inafanyika siku ya Jumapili na ni siku maalumu iliyotengwa kwa ajili ya Ibada??

      Kwa HIYO NAIOMBA SERIKALI YETU TUKUFU IBADILISHE SIKU YA SENSA NA KUWA JUMATATU NA IWE NI SIKU KUU ILI KILA MTU AKAE HOME KWAKE AHESABIWE. Nawasilisha!!!!!!

    13. #310
      bushman's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st November 2010
      Posts : 1,431
      Rep Power : 719
      Likes Received
      307
      Likes Given
      84

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      yaaani hii nchi hataukiwachia hawa miaka 100 utaikuta vilevile zaidi ya kuirudisha nyuma kwa miaka 100 kimaendeleo,sasa mkisusia sensa mnamkomoa nani kila dhehebu lina takwimu zake toeni za kwenu mkianzia msikiti wa MTORO.

    14. #311
      MwalimuZawadi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st September 2007
      Posts : 623
      Rep Power : 723
      Likes Received
      50
      Likes Given
      3

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Serikali inataka kuhesabu raia wake kwa misingi na dhima yake. Ni kama mzazi anapotaka kuhesabu watoto wake. Ni sawa na mimi kuhesabu wapenzi wangu. Kila mtu mwenye shida ya kujua idadi ya vitu vyake, kuku, ng'ombe, magari, homa, malaria, wajukuu na vitukuu huwa anaiita serikali imfanyie sensa?
      Sent from my Nokia rinGo using JamiiForums

    15. #312
      RubenM's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 15th April 2009
      Location : MBEYA
      Posts : 104
      Rep Power : 534
      Likes Received
      7
      Likes Given
      8

      Default

      KCMC ilijengwa na kodi za MAAMUMA??? Asiyefanya kazi Mara nyingi hula ombaomba... So mnaomba ziwe zenu??? Mngesoma shule...

    16. #313
      Mdondoaji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th March 2009
      Posts : 4,722
      Rep Power : 1483
      Likes Received
      807
      Likes Given
      341

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Ngongo
      Thread imejaa wachangiaji na watazamaji bila shaka watazamaji wengi ni TISS.

      There are currently 304 users browsing this thread. (96 members and 208 guests)
      Fearmongering as usual so what wakiwepo TISS??? Kwanini usiseme bila shaka wengi ni jamaa wa National Bureau of Statistics? Maana tunawapa somo la bure badala ya kulipa mabilioni kuleta mzungu kuja kuwafundisha kuhusu Sensa!!!!

    17. #314
      Lu-ma-ga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2010
      Posts : 1,820
      Rep Power : 807
      Likes Received
      517
      Likes Given
      8

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Naona uamsho wamewadanganya mmesikiliza cd yao mkaona ndiyo nitoke vipi yenu.Hilo halitakubalika na wala halitatokea ndiyo maana mnaongea nyinyi kina Pengo, Malasusa na wengine wamekaa kimya wanajua na threat at all.Mchana mtaongea usiku mtalala

    18. #315
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 401
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By RubenM
      Kalamazoo1 unakomoa jiweeee????
      Si serikali inajihudumiaaaa ikomeshe tu
      sasa kama serikali ni jiwe mbona inataka kutuhesabu? si iache tu? Sensa ina umuhimu lakini sio kwa nchi kama yetu ya wachakacuaji na mafisadi

    19. #316
      Wingu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2011
      Posts : 3,961
      Rep Power : 1215
      Likes Received
      247
      Likes Given
      41

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Kujua idadi ya dini ni muhimu sana nchi zilizoendelea zinatakwimu halisi ya dini zilivyo katka nchi zao ije kuwa Tanzania.Kwa wanaopinga kuna kitu wanaficha

    20. #317
      dotto's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2010
      Posts : 1,395
      Rep Power : 717
      Likes Received
      156
      Likes Given
      16

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By KALAMAZOO1
      Zote zilijengwa kwa kodi za wtz wote na bado zinaendeshwa kwa kodi za watz.kanisa halina ujiko hapo
      Majengo ya KCMC na Bugando ni mali biinafsi ya dini zao na sio unavyoandika. Mmelala usingizi wa Allah!

      Truly, god loves those who fight

      - Fight and slay the pagans wherever you find them,
      and seize them, beleaguer them, and lie in wait for
      them in every stratagem.

      - Chop off their hands and chop off their fingertips

      - When you meet the unbelievers, chop off their
      heads

      - Fight and slay those who don't convert wherever
      you find them

      - Believers, take neither Jew nor Christians for your
      friends

      - Those who follow Muhammad are ruthless to
      unbelievers

      - Those who reject Islam are "the vilest of creatures"
      and thus deserve no mercy

      - Fight them until Islam reigns supreme (throughout
      the world)

    21. KHZ
      #318
      KHZ's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 2
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      kwa ajili ya mipango endelevu,hicho ni kipengele cha msingi sana.
      BIG UP!

    22. #319
      Mponella's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd December 2011
      Posts : 22
      Rep Power : 381
      Likes Received
      2
      Likes Given
      27

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Kuna kila dalili kuwa tunakoelekea ni kubaya chokochoko zimeanza yangu macho!..

    23. #320
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,690
      Rep Power : 902
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By KALAMAZOO1
      Aslimia 91 ya watumishi wa uma ni wakristu,kati ya hawa asilimia 90 ni mafisadi.mbona hiyo ya ufisadi na kutakaswa pesa makanisani sio siri? wengine ninao hapa ofisini ndio walionipa habari hizo
      ...ok,kwahiyo unakubali kuwa wote ni mafisadi,waislam kwa wakristu!bt tatizo lako ni idadi,kuwa wengi wa hao mafisadi ni wakrito!what if wangekuwa sawa kwa idadi,msingelalamika?na huko kujua hiyo idadi yenu ndo itasaidia kuondoa ufisadi?

    24. Miaka 50
    Page 16 of 62 FirstFirst ... 6141516171826 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...