Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

    Report Post
    Page 14 of 62 FirstFirst ... 4121314151624 ... LastLast
    Results 261 to 280 of 1236
    1. #1
      Kiranja Mkuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th February 2010
      Posts : 2,084
      Rep Power : 886
      Likes Received
      284
      Likes Given
      34

      Default BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hawa Bakwata, wanaikomoa CCM au CUF?

      BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) limetangaza rasmi kutoshiriki sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika nchi nzima Agosti, hadi ombi lao la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa kitakapofanyiwa kazi.

      Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Amir Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Shehe Mussa Kundecha, alisema uamuzi huo umetokana na Serikali kushindwa kusikiliza upande wa Waislamu na kuamua kutokiingiza kipengele hicho.

      Alisema katika mkutano wa viongozi wa dini na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) uliofanyika Dodoma Juni 11, waliwasilisha ombi lao la kipengele cha dini kuingizwa kwenye dodoso za sensa ili kupata idadi kamili ya Watanzania kidini.

      “Kwa kweli mkutano ulikwenda vizuri, tulitoa sababu zetu za kutaka kipengele hicho kiwemo ili kuondoa utata wa sasa wa kila taasisi na dini kutoa takwimu zinazotofautiana na Kamishna wa Takwimu alipokea maombi yetu na kuahidi kuyawasilisha serikalini na kuyafanyia kazi,” alisema Shehe Kundecha.


      Alisema cha kushangaza wakati akifunga mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Uhusiano na Uratibu, Stephen Wasira alibainisha wazi kuwa kamwe Serikali haiwezi kukiingiza kipengele hicho kwenye dodoso za sensa, kwa kuwa kinavunja umoja, amani na utulivu wa Taifa.

      Aidha, alisema katika kutetea hoja hiyo, Serikali ilitoa mifano ya nchi za Nigeria na Kenya, ambazo zimefanya sensa na kuingiza kipengele hicho kwenye dodoso, lakini kutokana na kuibuka kwa vuguvugu la kidini katika nchi hizo, hadi leo matokeo ya sensa hizo hayajatangazwa.

      Shehe Kundecha alisema Baraza hilo limepokea hoja hizo na kuzisikiliza ingawa halikubaliani nazo kwa kuwa kwa Tanzania bado zipo taasisi na madhehebu ya dini yanayotoa takwimu za kidini yakionesha idadi ya Wakristo, Waislamu na Wapagani huku umoja na amani vikiendelea kuwapo.

      “Kama tatizo ni kuvurugika kwa amani, umoja na utulivu, mbona basi vyombo hivi visivyohusika na takwimu vinatoa takwimu hizi tena hadi kwenye mitandao na Serikali kuvifumbia macho, huku kukiwa hakuna umoja wala amani iliyovunjika? Kwa nini isifanyike sensa ya kidini na kupatikana takwimu halisi?” Alihoji.

      Alisema kutokana na kauli hiyo, inaonekana wazi kuwa Serikali haijasikiliza kilio cha Waislamu kutaka kipengele cha dini kiingizwe kwenye dodoso za sensa, ili zipatikane takwimu sahihi na rasmi za Watanzania kidini.

      “Hivyo basi tunasisitiza Waislamu hatutashiriki sensa mpaka mapendekezo yetu yatakapofanyiwa kazi, tunataka idadi halisi ya Waislamu, ili nasi tujue tunawasaidiaje kimaendeleo na kidini,” alisema.

      Ustaadh Sadiki Gogo, alisema mfano uliotumiwa na Serikali kukataa ombi la kuingizwa kwa kipengele cha dini kwenye dodoso la sensa hauna nguvu, kwa kuwa umeegemea upande mmoja na kusahau nchi kama Uganda, Uingereza, Australia na Canada, ambazo katika sensa zao wanatumia kipengele cha dini na hazina matatizo.


      Hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Shehe Ponda Issa Ponda, alisema atahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi.


      Alisema haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele hicho kwani uzoefu unaonesha kuwa baada ya Serikali kukiondoa, makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na Wapagani.

      Pamoja na kauli ya Wasira, Mkurugenzi Mkuu wa NBS, Dk Albina Chuwa, alikataa ombi la mashehe la kujumuisha kipengele cha dini katika dodoso za maswali wakati wa sensa. Alisisitiza mbele ya viongozi wa dini mbalimbali wakiwemo mashehe kuwa maswali yanayohusu kabila na dini hayatajumuishwa kwenye dodoso kwani Serikali haipangi mipango ya maendeleo ya wananchi kwa kufuata itikadi za kidini au ukabila.

      CHANZO: HabariLeo
      takashi and Lokissa like this.

    2. Miaka 50

    3. #261
      Manyanza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th November 2010
      Location : Look Behind You......
      Posts : 4,419
      Rep Power : 25469
      Likes Received
      1143
      Likes Given
      909

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By KALAMAZOO1
      OIC sio upuuzi mzee.Fungua website ya IDB uone Waganda wanavyonufaika na OIC tena bila kujali dini zao.Mahakama ya Kadhi ingekuwa ni upuuzi Kenya wasingeiweka kwenye katiba ya mpya pia na South Afrika,wakati SA inasifiwa na kuwa na katiba nzuri ya kuigwa sio tu Afrika bali duniani
      sijasema OIC ni upuuzi we mtetea islamu, ili nimesema malalamiko yenu ni ya kipuuzi na hakuna sababu mnazotoa za msingi...... mahakama ya kadhi serikali iwe inawalipia gharama za uendeshaji we huoni huu ni upuuzi? ndio maana baba mwanaAsha akawatolea nje live bila chenga
      Insanity is doing the same thing over and over again and expecting different results.

    4. #262
      Ibambasi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th July 2007
      Location : Iponyamakalai - Isungang'holo
      Posts : 724
      Rep Power : 754
      Likes Received
      118
      Likes Given
      762

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By sweke34
      Mungu wa kigeni or Mungu wa kienyeji , matatizo yatatoka wapi kama kila mtu atajali imani yake tu? Huyo Mungu wako wa kienyeji si ndiyo ameishia kuua albino,wazee vikongwe na mifugo kwa kutambika? Huko kutawaliwa kwako kifikra umekuona kwenye dini tu? mbona karibu kila kitu ni cha kikoloni? Mkuu kama umeamua kuabudu mbuyu, joka kubwa, kwenda kanisani, kwenda msikitini nk ni choice yako, cha muhimu hapa ni kutoanza kuingilia imani za watu wengine na kuleta chokochoko kama hizi tunazoziona...!
      Red: Na nyie pia si mmeishia kuua waumini wenzenu (e.g. Kibwetere) kwa ajili ya huyo wa kwenu?

      Blue: Hicho ndicho cha muhimu, tatizo nyie na wenzenu wa Mungu Allah ndio mnaoleta hizo chokochoko, sasa mnataka kubishania waumini wa mungu yupi ndio wengi!

    5. #263
      Lu-ma-ga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2010
      Posts : 1,823
      Rep Power : 808
      Likes Received
      518
      Likes Given
      8

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Ibrah
      Hivi kukataa kuhesabiwa si kosa la jinai? Kwa serikali makini ingekuwa imeshatoa tamko kuhadharisha hata kabla ya wanaharakati kuanza porojo zao.
      Serikali haiwezi kupoteza muda kubembeleza wapiga filimbi wa HAMELINI

    6. #264
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,712
      Rep Power : 907
      Likes Received
      433
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By ntamaholo
      kwa nini kufanya mambo kwa kuiga? Kila siku copying tu? Tunaishi kufuatana na tamaduni zetu wenyewe. Yaani maslahi yenu nyie mnataka yafanyike kwa fedha za watanzania wote? Uze,be mwingine hata shetani hauvumiliii
      ....nashangaaa

    7. #265
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,138
      Rep Power : 604
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Nono
      Hapa namnukuu Shekhe Ponda


      Sasa mie nilichozusha ni kipi?
      Kama ni kuhusu ajira sawa lakini akzanie kipengele cha Elimu
      Ili kujua wasomi wa imani zote wasio na ajira na uwiano wa jumla wa idadi yao katika taifa!.

    8. FemaTV & Radio

    9. #266
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,657
      Rep Power : 717
      Likes Received
      291
      Likes Given
      36

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Hivi Dini inaingiaje kwenye sensa? Kwanini Bakwata hawatumii akili? Hivi hawaoni Madhara ya Dini kuingizwa kwenye sensa? Je na kila kabila wakitaka wajue idadi yao kwa malengo sawa na ya Bakwata nini matokeo yake? Ni kweli tatizo la waislamu ni idadi? Na je Idadi yao itakidhi mahitaji yao? kawnini Bakwata isijikite kwenye mambo ya msingi, kama kujenga Shule, vyuo zahanati na Hospitali?

    10. #267
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1843
      Likes Received
      592
      Likes Given
      413

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Napata kigugumizi kuchangia

    11. #268
      Lu-ma-ga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2010
      Posts : 1,823
      Rep Power : 808
      Likes Received
      518
      Likes Given
      8

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Baba Mwanaasha tunamkubali sana hasa anapokutana na issue za kizushi kama hizi, huwaga analala usingizi wa pono kana kwamba hajasikia kwani nduguze awajua walivyo vilaza, yeye anakula matunda ya wakatoliki mnaowachukia nyinyi

    12. #269
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By christine ibrahim
      ...mkuu,hakuna dini ambayo inasema ufisadi c haram!kumbuka hata hao walioko madarakani waliapa kwa kutumia vitabu hivyohivyo vya dini,waislam kwa wkristu,lkn at the end ndo wametufikisha hapa...pili,unataka kuniambia mafisadi wote kwny huu mfumo uliooza ni wakristo?..tatu,so kupitia hiyo hesabu yenu mnayotaka kujua mpo wangapi, itasaidiaje hapa kwny kupiga vita ufisadi?tukisema mnataka iwe nchi ya kiislam mnakataa,ss hii hoja yako inajieleza hapa!
      HUU SI NI MFUMO KRISTU? Wakisha fanya ufisadi wanaambiwa na viongozi wao wapeleke sadaka ili pesa zao zitakaswe.Ubaguzi katika ajira ni matokeo ya ufisadi,hujuma katika elimu ni matokeo ya ufisadi,should I say more?

    13. #270
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,712
      Rep Power : 907
      Likes Received
      433
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By dazu
      Ushauri: Serikali ikikataa kuingiza kipengele hicho, Bakwata iandae sensa ya kuhesabu Waislamu tu, tujue idadi ya misikiti inayohitajika.
      ...sio ikikataa,imeshakataa,na wasira ndo katoa tamko!ss kazi kwao

    14. #271
      Mwanaweja's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th February 2011
      Posts : 3,464
      Rep Power : 1112
      Likes Received
      458
      Likes Given
      938

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      hii imani wanamwamini nani?kama mungu mbona wana vijimambo vya ajabu sana hawa jamaa? badirikeni msiwe kama bendera kufuata upepo, dini ni mapokeo na wala isifike sehemu mkwa watumwa wa dini

    15. #272
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,712
      Rep Power : 907
      Likes Received
      433
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By KALAMAZOO1
      HUU SI NI MFUMO KRISTU? Wakisha fanya ufisadi wanaambiwa na viongozi wao wapeleke sadaka ili pesa zao zitakaswe.Ubaguzi katika ajira ni matokeo ya ufisadi,hujuma katika elimu ni matokeo ya ufisadi,should I say more?
      jibu swali langu?mafisadi wote ni wakristo?...na hao wanaoenda makanisani ni kina nani wataje?...

    16. #273
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,712
      Rep Power : 907
      Likes Received
      433
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By KALAMAZOO1
      HUU SI NI MFUMO KRISTU? Wakisha fanya ufisadi wanaambiwa na viongozi wao wapeleke sadaka ili pesa zao zitakaswe.Ubaguzi katika ajira ni matokeo ya ufisadi,hujuma katika elimu ni matokeo ya ufisadi,should I say more?
      jibu swali langu?mafisadi wote ni wakristo?...na hao wanaoenda makanisani ni kina nani wataje?...kwahiyo mnataka kuleta mfumo islam?

    17. #274
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,712
      Rep Power : 907
      Likes Received
      433
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By Lu-ma-ga
      Serikali haiwezi kupoteza muda kubembeleza wapiga filimbi wa HAMELINI
      ....kabisa mkuu

    18. #275
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Manyanza
      sijasema OIC ni upuuzi we mtetea islamu, ili nimesema malalamiko yenu ni ya kipuuzi na hakuna sababu mnazotoa za msingi...... mahakama ya kadhi serikali iwe inawalipia gharama za uendeshaji we huoni huu ni upuuzi? ndio maana baba mwanaAsha akawatolea nje live bila chenga
      Mbona unajichanganya? inaelekea una elimu ya kukariri au hujasoma.Changia kwa mantiki acha kubwabwaja

    19. #276
      Lu-ma-ga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2010
      Posts : 1,823
      Rep Power : 808
      Likes Received
      518
      Likes Given
      8

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By christine ibrahim
      jibu swali langu?mafisadi wote ni wakristo?...na hao wanaoenda makanisani ni kina nani wataje?...
      Idd Simba afikishwa mahakamani kwa kujipakulia fedha za mauzo ya UDA na kiungizwa ktkt account yake ya kifisadi

    20. #277
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By christine ibrahim
      jibu swali langu?mafisadi wote ni wakristo?...na hao wanaoenda makanisani ni kina nani wataje?...
      Aslimia 91 ya watumishi wa uma ni wakristu,kati ya hawa asilimia 90 ni mafisadi.mbona hiyo ya ufisadi na kutakaswa pesa makanisani sio siri? wengine ninao hapa ofisini ndio walionipa habari hizo

    21. #278
      David webb's Avatar
      Member Array
      Join Date : 20th November 2011
      Posts : 56
      Rep Power : 390
      Likes Received
      22
      Likes Given
      16

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      kigoma iko pwani?tabora je, zanzibar haihusiki kwenye sensa ya 1957 kwa kuwa hatukuungana nao mwaka huo.na wao walikuwa na sensa yao.

    22. #279
      KALAMAZOO1's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 23rd November 2011
      Posts : 119
      Rep Power : 402
      Likes Received
      6
      Likes Given
      4

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Quote By Lu-ma-ga
      Idd Simba afikishwa mahakamani kwa kujipakulia fedha za mauzo ya UDA na kiungizwa ktkt account yake ya kifisadi
      Hivi Idd Simba ni mtumishi wa uma?

    23. #280
      Kyaiyembe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st December 2011
      Location : Kisukuru
      Posts : 1,138
      Rep Power : 604
      Likes Received
      345
      Likes Given
      303

      Default Re: BAKWATA yatangaza rasmi waislam kugomea sensa!

      Jamani tuwe wakweli mimi nimeajiriwa na BOSI wangu ni mwislamu mzuri sana.

      Katika Kampuni yake waajiriwa wa kudumu tulikuwa tisa, mmoja akaacha mwenyewe na mwingine akafukuzwa.

      Tukabakia saba na wote saba ni ama wakristo au wapagani. Mwislamu alikuwa mmoja ndiye aliyeacha kazi. Sasa sikujua aliona labda bosi wetu naye anatumia mfumo Kristo.

      Sababu za kuajiri hivi ni kutokana sifa za wafanyakazi anaohitaji na sana sana ni elimu zaidi!.
      "Ikulu ni mahala PATAKATIFU,
      mimi sikuchaguliwa kuja kupageuza kuwa pango la wala RUSHWA."
      By J.K. NYERERE.

    Page 14 of 62 FirstFirst ... 4121314151624 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...