Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

    Report Post
    Page 1 of 13 12311 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 254
    1. #1
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 764
      Rep Power : 5115
      Likes Received
      579
      Likes Given
      111

      Default Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%



      Kauli aliyoitoa Dr Slaa wakati wa vuguvugu la kampeni za kisiasa kwamba mfuko wa sement utakuwa Tshs 5,000, badala ya Tshs16,500 kwa sasa kwa wakazi wa DSM na zaidi ya Tshs18,000 kwa wakazi wa nje ya mji huu, nimekuwa nikizitafakari kwa kina sana kwa muda mrefu. Kutokana na Uzoefu wangu wa masuala machache alonijalia mola, nilioona kama ni sentensi ya kisiasa zaidi ya kimatendo, lakini sasa nakiri ni sentenSi makini na ya kweli. Na si 5000 tu bali pia 2,500 au 3000 kwa mfuko wa 50kgs.

      Hivi majuzi, nilikuwa namsikiliza Waziri Viwanda na Biashara Dr. Kigoda akizungumzia masuala ya Kiuchumi kwenye kipindi cha TBC asubuhi. Kauli aliyotoa Abdala Kigoda ilinifanya kile kisifa cha kuitwa Dr nikiondoe haraka na natamani nikiingia ofisini kwake nimwite Mr Abdala. Mkongwe Huyu adui mkubwa wa mabango ya “sigara ni hatari kwa Afya yako” alisema , ‘AMESIKIA” wafanya biashara wa hapa wakimweleza kwamba bei ya mfuko wa sement inayouzwa hapa ni ghali sana kulinganisha na bei ya mfuko utaouagiza kutoka India.”

      Nikawaza kama mzee huyu, waziri wetu amesikia tu, ameshindwa kufanya tathimini kutumia ziada kidogo ya akili yake iliyompelekea kuitwa DR, kwamba kama hali iko hivyo kwa India km 4,600 tu kutoka TZ, sawa na kwenda kigoma na kurudi dsm mara mbili, ana mipango gani mbadala ya kuhakikisha na hapa kwetu unafuu wa neema unaonekana kwenye gharama ya mifuko ya cement, watu tukajenga?

      Sentensi yake hiyo ilinisukumia na kuamsha mawazo yale niliyokuwa nayo awali aliyoyasema Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Dr Wilbroad Slaa-2010, kwamba Bei ya sement ni ghali sana, Serikali yake itaipunguza hadi kufikia Tsh5,000. Na hapo ndipo nilipoona nifanye kauchunguzi kadogo sana ambako mdau wa jamvi unaweza kunikosoa lakini uwezo wa kuchunguz kwangu ndipo ulipofikia..

      Cha kwanza nikawapigia “madalali wa wagonjwa” (india kuna watu kazi yao ni udalali wa wagonjwa, wanatengeneza dili zao kwa kuwasaka wagonjwa kutoka kwenye nchi zao kama Africa na hata penginepo kupitia mashirika mengi kama LIONS CLUB na mengineyo na kuwa connect na daktari husika na kufanya protocal zote za maandalizi na ndivyo nao wanavyopata kula ..anyway that is not ma topic)..nikawauliza wanitajie bei ya mfuko wa sement kwenye soko la kawaida .. baada ya muda wakaniambia ni Rupia 230. Rupia moja ni sawa na Tsh28.

      Kwa hiyo mfuko mmoja wa Kg 50 wa sement kule India ni sawa na Tsh 6,440 (28 x 230). Kwa Kontena la 20ft lina uwezo wa kuchukua tani 35-40, lakini meli nyingi zina standard ya kujaza 40ft kwa tani 20 tu. Sasa tani 20 ni mifuko 400 a cement. Kwa bei ya meli zinazosafirisha 40ft kwa 20ton ni dolar 400 (sawa na tzs 632,000 (1,580 x 400).. tukiacha vikodi vidogo vidogo vya asilimia 2.

      so mzigo utafika TZ kwa gharama ya (400[20ton] x 6,440[mfuko] + 632,000[Usafiri] =3,208,000 so Mifuko 400 utaifikisha Tz kwa gharama ya Tshs 3,208,000 na Mifuko 400 utainunua Tz kwenye soko letu kwa gramama ya (400 x 16,500) = 6,600,000 tofauti ya zaidi ya (6,600,000 -3,208,000) = 3,392,000 .. he he he!

      Mifuko 400, ukiinunua India na kuiuza TZ Tsh 10,000 tu kwa mfuko utapata Tshs (10,000 x 400)= 4,000,000 na kutengeneza faida chap ya (4,000,000-3,208,000)=792,000.

      Biashara ya haraka sana na mifuko itagombaniwa kama njugu na wewe unaifanya biashara yako yote ukiwa nyumbani nyuma ya laptop yako tu na simu ya mkononi basi.

      Nikaenda mbali kidogo na kujiuliza kwanini India cement ni bei rahisi. Nikagundua kwamba, kasheshe kubwa ya kutengenza sement iko kwenye maandalizi yake hasa hasa uzalishaji wa vijiwe vidoho vigumu sana vinavyoitwa Clinker. Mchakato wa Kutengeneza malighafi hii clinker ndio mgumu na ghali zaidi. Kwa utafiti mfupi nilioufanya nimegundua utengenezaji wa Clinker Kule India Ni Ghali sana Kulinganisha na hapa kwetu TZ. Nilibahatika kutembelea kiwanda cha Lafarge Mbeya Cement maarufu kwa kutengeneza Cement ya Mnyama (TEMBO CEMENT). --Simba ni Tanga na Twiga ni DSM.

      Mchakato wa Kutengeneza Clinker unaanzia kwenye machimbo ya miamba geu yenye vichambuzi (ingredients na Ore mbalimbali) miamba hii hutoka machimboni na kuingizwa kwenye ngome ya mapondo (Crushers) ambapo hupondwa na kuwa miamba midogo mithili ya kokoto na kuzukumizwa kwenye mkanda, na vile vile huchimbwa udongo wa mfinyanzi nao hukimbizwa kwenye mkanda wake mwingine kwa viwango vyao.

      Mikanda hii miwili huingizwa kwenye ngome kubwa ya mapondo na kusagwa kwa kuchanganywa kiasi cha kuwa vumbi, hapa ndipo kiasi kikubwa cha Vumbi huzalishwa, kutokana na shughuli pevu inayofanyika. Vumbi hili hudhibitiwa sana ila kiasi kidogo hutolewa nje na kuwa wingu zito sana la Vumbi hatari kwa mazingira. Vumbi hukusanywa kwenye Kiwiko kikubwa na kirefu sana nadhani ndio point ndefu kuliko zote kwenye kiwanda cha simenti, kinachoitwa Cyclone. Cyclone Hili hupokea vumbi hilo na kulisafirisha likahifadhiwe kweye maghala makubwa (Silos) Sasa Vumbi hili laini ndio malighafi ya kutengenezea hizo Clinker.

      Vumbi hili hukimbizwa kwenye kinu kikubwa (KILN). Na huko huchomwa kwenye jotoridi la takriban nyuzijoyo 1400. Udongo huyeyushwa na kuchangamana. Chanzo cha moto huwa ni makaa ya mawe ambayo hupondwa na kuwa vumbi kisha husukumwa kwa upepo wenye gandamizo kubwa na kuzalisha moto kama jehanam ya ajabu sana ndani ya jiko hilo. Moto ule (Carbon) na udongo huo ukijumlisha na mzunguko wa jiko lenyewe, manake linachoma huku linazunguka basi huzaa vijiwe vidogo vyeusi vinavyoitwa Clinker.

      Clinker hizo hupozwa kwenye ghala (hydrous)na baadae hukimbizwa kwenye mpipa mkubwa unaozunguka wenye magololi ya chuma na vikwazo ndani yake, huko clinker hugongwagongwa na kuwa vumbi laini sana ambalo huchanganywa na vumbi jingine linaloitwa gypsum (udongo unaochimbwa Tanga) na hapo kutoa vumbi ambalo likipata maji hukauka na kuwa jiwe linaloitwa CEMENT.

      Baada ya chochezi hilo nikapeleleza na utengenezji wa Clinker kule India, ambapo mawe hununuliwa, mfinyanzi hununuliwa na zaidi ya hayo wao huchoma kwa kutumia mafuta ambapo ni gharama sana sisi tunatumia makaa ya mawe ambayo kusini ni mengi tu..

      Ukiangalia mchakato huo HAPA KWETU, Miamba geu iko mingi na bure kabisa, Makaa ya Mawe Tunayo Kusini ya Kumwaga tu, Gypsum ni udongo unaopatikana Tanga mwingi sana na Bure tu. Sasa nani katuroga mpaka Cement isiwe na bei ya Tsh 2500 au 3000 tu????!!!????

      Nikagundua gharama Kubwa za Cement ni Unyonyaji tu, Viwanda vingi vinaendesha mataifa ya nje na si tanzania. Mfano waholanzi hawa Lafarge wanamlipa MZUNGU Technician tu mwenye certificate ya ufundi karibia Dola 8,500 sawa na (8500 x 2580) = Tshs 13,400,000/=kama mshahara wake mwezi, wakati Mhandisi Mtanzania mwenye Jiwe lake moja au mawili, aliyekokotoa shule ngumu ya FoE na term system that time, na kuvivuka vikwazo vyote vya kina Prop Chambega, Luhanga , Masuha Nk ambaye ndiye mkuu wa sekta mojawapo labda project manager, au Chief Electrical, mechanical, Civil nk kiasi cha Tsh 820,000 kwa mwezi. Usawa uko wapi?. Wakati huyu fundi wa kizungu maelekezo na miongozo ya kazi anaipata kwa Mtanzania huyu ambaye ni meneja wa kitengo husika. Hivi usawa uko .. kama Fundi tu anakula madolali yote hayo je Eng wa kizungu, je Chief of DPt je manager je CO wa kizungu anajichotea mangapi.. kama hiyo haitoshi je wanajilipia kwenye serikali yao kiasi gani kwa External security, BIMA, INSUARANCE nk (maana huduma hizi zote wanajitegmezea huko kwao) na kiasi gani wanarundika kwenye mabenki yao na kuimarisha uchumi wao?

      Fedha nyingi na Utajiri Mwingi wazawa hawafaidi, tunanyonywa na kukubali kunyonyeka. Kiwanda sio Inshu kubwa, Serikali ikiamua kujenga Kiwanda hiki ni kazi nyepesi na laini sana. Kama Hawa wazungu wanaleta makandamizi haya basi tuwaalike Wajerumani waliowajengea hawa waholanzi na wengineo viwanda waijengee serikali kupitia vichwa makini chini ya PSRC ikaendesha kiwanda hiki kwa ukombozi wa wananchi wake. INAWEZEKANA..

      Alamsik..!!


      NB: Kwa muda wako jisomee:

      Tanzania: Cement sh 5,000 yawezekana!

      &k
      Maisha BORA: Songea mfuko wa cement sh 20, 000 per bag!
      ...

      Quote By Ukana Shilungo
      you are real brialiant,uchambuzi safi kabisa,mbeya cement kiwanda cha songwe Injinia mwandamizi Maro ni alikuwa injinia mkuu toka kiwanda kinajengwa mpaka kinaanza uzalishaji,aliacha kazi kwa ajili ya mzungu asiyejua kazi kulipwa Milioni 13 ili hali yeye akipokea milioni 1.5,alipatwa na uchungu akaacha kazi.meneja mkuu Diyami alimshauri Mkapa kutobinafisisha kiwanda cha Songwe ila mkapa hakusikia,kwa hiyo bei ya saruji ingeweza kuwa nafuu tatizo ni ufisadi toka kwa hawa wageni tuliowapa viwanda kwa bei ya kutupa,lengo ni kupata super profit,so THE MISSION OF CAPITALIST WHEREVER THEY ARE IS EXPLOITATION by any means,hivyo saruji kuuzwa 5000 kama alivyosema Dr slaa ni kweli,kweli tupu.
      Attached Thumbnails  
      Last edited by Eng. Y. Bihagaze; 13th June 2012 at 21:03.
      Invisible, BAK, Small Boy and 59 others like this.

    2. Study Abroad

    3. #2
      Mukalunyoisa's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th March 2012
      Posts : 139
      Rep Power : 389
      Likes Received
      19
      Likes Given
      2

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      inawezekana kabisa kuuzwa kwa bei kama huamini angalia wenzetu Rwanda hakuna nyumba za udongo kule
      snochet, Adharusi and monaco like this.

    4. #3
      NICE LAMECK's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 206
      Rep Power : 400
      Likes Received
      26
      Likes Given
      37

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      sasa ni nini ambacho unaona kinashindikana wewe Magamba,wakati hapo ni kupunguza gharama za uzalishaji cement kama vile umeme na ushuru wa bidhaa hiyo.
      snochet and monaco like this.

    5. #4
      maswitule's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th November 2010
      Posts : 406
      Rep Power : 514
      Likes Received
      116
      Likes Given
      44

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Umechambua vizuri wa Tz tunajitakia umasikini kwa kutompigia kura mtu anayejali maisha yetu. Baadaye tutamlaumu nani?
      Hakuna wa kumlaumu wacha tuteseke dhambi hii inatumaliza wenyewe
      Mavukilo and monaco like this.

    6. #5
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,291
      Rep Power : 1195
      Likes Received
      1178
      Likes Given
      1551

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      wewe naona unataka kunitoa machozi tu, mpaka sasa pesa yangu nyingi sana imelala kwenye kiwanja nilichonunua nikitegemea kuanza ujenzi baada ya uchaguzi. I wish ningeizungusha pesa yangu saa hizi ningekuwa safi sana.

    7. Miaka 50

    8. #6
      Negotiator's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 9th August 2010
      Posts : 301
      Rep Power : 509
      Likes Received
      36
      Likes Given
      33

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Asante Salma uchambuzi makini. ndo maana najiuliza nani katuloga?
      Invisible likes this.
      '

    9. #7
      jmura's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th April 2010
      Posts : 53
      Rep Power : 470
      Likes Received
      8
      Likes Given
      4

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      mkuu wewe ni great thinker! umesema freshi sana!BIG UP!
      Invisible likes this.

    10. #8
      Comi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 960
      Rep Power : 578
      Likes Received
      154
      Likes Given
      2

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Kaka hongera umenena na kuichambua vizuri

    11. #9
      mtotowamjini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Location : None of Your Business
      Posts : 4,531
      Rep Power : 1262
      Likes Received
      1109
      Likes Given
      28

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      umechambua vizuri sema sasa mada kama hizi ndio zinanifanya nizidi kupata hasira na hii serikali yetu bora usiwe unaziweka hapa tutakuja kuuana bure
      saddam and Mavukilo like this.
      Every saint has a past, every sinner has a future' ...Oscar Wilde

      One man's good fortune is another man's misfortune


    12. #10
      idawa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2012
      Posts : 4,520
      Rep Power : 3318
      Likes Received
      1205
      Likes Given
      454

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      umechambua vizuri. Inatia hasira sana kuona viongozi wanashindwa kufikiri kwa ajili ya wananchi zaidi wanafikiria matumbo yao tu.!
      Mazingira likes this.

    13. #11
      Sting007's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 27th July 2011
      Posts : 215
      Rep Power : 438
      Likes Received
      22
      Likes Given
      0

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Thanx Man umetuelewesha zaidi, tupo tunajipanga.

    14. #12
      luhaga's Avatar
      Member Array
      Join Date : 18th January 2012
      Posts : 13
      Rep Power : 372
      Likes Received
      0
      Likes Given
      8

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      sure,i agree!

    15. #13
      wikolo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th October 2010
      Posts : 449
      Rep Power : 524
      Likes Received
      129
      Likes Given
      59

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Nimeukubali uchambuzi wako mkuu SALMA2015 na hasa shule ya uzalishaji wa sementi. Si kwamba watawala hawayajui haya bali ni kama wanafanya makusudi tu kwa sababu zao binafsi. Achana na tumbo ndugu yangu!

    16. #14
      POMPO's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 12th March 2011
      Posts : 2,955
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1090
      Likes Given
      625

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      I agree
      MwanzoMwisho likes this.

    17. #15
      Kiganyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th April 2012
      Posts : 1,162
      Rep Power : 982
      Likes Received
      708
      Likes Given
      400

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Aisee nimeipenda sana hii makala, haichoshi kusoma!

      Unafaa sana kuwa Mwandishi Baby lol!!

      Kwa kweli Dr Slaa alikuwa na point kubwa sana katika hili ila magamba walivyo wavivu kufikiri huwa wanageuza hii hoja kama comedy! shauri wako tunaomba viongozi makini wapite hapa na wausome!
      monaco likes this.

    18. #16
      Landala's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th December 2010
      Posts : 562
      Rep Power : 538
      Likes Received
      122
      Likes Given
      25

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pempeni,DR SLAA aliwaambia mkabisha sasa ukweli umejidhihirisha kuwa mfuko wa saruji unaweza kushuka hadi sh 5000.Nakumbuka wakati wa uchaguzi TBC wakitumiwa na CCM walisema haiwezekani kumbe uongo mtupu hakuna lisilowezekana.

    19. #17
      mwenyenguvu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 85
      Rep Power : 376
      Likes Received
      25
      Likes Given
      28

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      umenitia hasira sana,yaan viongozi wa nchi yetu kwani nabni aliyeloga?,walianza vema chini ya mwalimu,mwalimu alipoondoka 1985 taratibu yule mwovu akaanza kupanda magugu,hakika nimepatwa na hasira sana,Mungu akubariki mleta mada hii
      monaco likes this.

    20. #18
      Marire's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 2,207
      Rep Power : 954
      Likes Received
      597
      Likes Given
      0

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Mimi nimependa ulivyochambua na ulivyotafiti ,ila nakuapia kwa jina la Mungu kwa sirikali hii ya magamba huo mpango hautafanikiwa.

    21. #19
      Mapi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2011
      Posts : 571
      Rep Power : 0
      Likes Received
      142
      Likes Given
      141

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      laana na ziwatembelee wale wote wanaoshndwa kung'amua utamu ulioko kwenye uchambuzi huu. Vidole vinawakereketa kukatsha tamaa wengne sababu ya uvivu wao wa kuchambua mambo na kuyaelewa... SALMA2015 nimekuelewa mkuu. Naomba kama kuna mwandsh wa habar apewe ruhusa ya kuuchapisha uchambuzi wako lakini atumie JF kama ndie mwandsh na sio ajiweke yeye tafadhali
      monaco likes this.

    22. #20
      Noboka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2011
      Posts : 493
      Rep Power : 2248
      Likes Received
      153
      Likes Given
      23

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Hongera sana kwa uchambuzi uliokwenda shule!

    23. FemaTV & Radio
    Page 1 of 13 12311 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...