Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

    Report Post
    Page 2 of 13 FirstFirst 123412 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 254
    1. #1
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 769
      Rep Power : 5117
      Likes Received
      584
      Likes Given
      111

      Default Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%



      Kauli aliyoitoa Dr Slaa wakati wa vuguvugu la kampeni za kisiasa kwamba mfuko wa sement utakuwa Tshs 5,000, badala ya Tshs16,500 kwa sasa kwa wakazi wa DSM na zaidi ya Tshs18,000 kwa wakazi wa nje ya mji huu, nimekuwa nikizitafakari kwa kina sana kwa muda mrefu. Kutokana na Uzoefu wangu wa masuala machache alonijalia mola, nilioona kama ni sentensi ya kisiasa zaidi ya kimatendo, lakini sasa nakiri ni sentenSi makini na ya kweli. Na si 5000 tu bali pia 2,500 au 3000 kwa mfuko wa 50kgs.

      Hivi majuzi, nilikuwa namsikiliza Waziri Viwanda na Biashara Dr. Kigoda akizungumzia masuala ya Kiuchumi kwenye kipindi cha TBC asubuhi. Kauli aliyotoa Abdala Kigoda ilinifanya kile kisifa cha kuitwa Dr nikiondoe haraka na natamani nikiingia ofisini kwake nimwite Mr Abdala. Mkongwe Huyu adui mkubwa wa mabango ya “sigara ni hatari kwa Afya yako” alisema , ‘AMESIKIA” wafanya biashara wa hapa wakimweleza kwamba bei ya mfuko wa sement inayouzwa hapa ni ghali sana kulinganisha na bei ya mfuko utaouagiza kutoka India.”

      Nikawaza kama mzee huyu, waziri wetu amesikia tu, ameshindwa kufanya tathimini kutumia ziada kidogo ya akili yake iliyompelekea kuitwa DR, kwamba kama hali iko hivyo kwa India km 4,600 tu kutoka TZ, sawa na kwenda kigoma na kurudi dsm mara mbili, ana mipango gani mbadala ya kuhakikisha na hapa kwetu unafuu wa neema unaonekana kwenye gharama ya mifuko ya cement, watu tukajenga?

      Sentensi yake hiyo ilinisukumia na kuamsha mawazo yale niliyokuwa nayo awali aliyoyasema Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Dr Wilbroad Slaa-2010, kwamba Bei ya sement ni ghali sana, Serikali yake itaipunguza hadi kufikia Tsh5,000. Na hapo ndipo nilipoona nifanye kauchunguzi kadogo sana ambako mdau wa jamvi unaweza kunikosoa lakini uwezo wa kuchunguz kwangu ndipo ulipofikia..

      Cha kwanza nikawapigia “madalali wa wagonjwa” (india kuna watu kazi yao ni udalali wa wagonjwa, wanatengeneza dili zao kwa kuwasaka wagonjwa kutoka kwenye nchi zao kama Africa na hata penginepo kupitia mashirika mengi kama LIONS CLUB na mengineyo na kuwa connect na daktari husika na kufanya protocal zote za maandalizi na ndivyo nao wanavyopata kula ..anyway that is not ma topic)..nikawauliza wanitajie bei ya mfuko wa sement kwenye soko la kawaida .. baada ya muda wakaniambia ni Rupia 230. Rupia moja ni sawa na Tsh28.

      Kwa hiyo mfuko mmoja wa Kg 50 wa sement kule India ni sawa na Tsh 6,440 (28 x 230). Kwa Kontena la 20ft lina uwezo wa kuchukua tani 35-40, lakini meli nyingi zina standard ya kujaza 40ft kwa tani 20 tu. Sasa tani 20 ni mifuko 400 a cement. Kwa bei ya meli zinazosafirisha 40ft kwa 20ton ni dolar 400 (sawa na tzs 632,000 (1,580 x 400).. tukiacha vikodi vidogo vidogo vya asilimia 2.

      so mzigo utafika TZ kwa gharama ya (400[20ton] x 6,440[mfuko] + 632,000[Usafiri] =3,208,000 so Mifuko 400 utaifikisha Tz kwa gharama ya Tshs 3,208,000 na Mifuko 400 utainunua Tz kwenye soko letu kwa gramama ya (400 x 16,500) = 6,600,000 tofauti ya zaidi ya (6,600,000 -3,208,000) = 3,392,000 .. he he he!

      Mifuko 400, ukiinunua India na kuiuza TZ Tsh 10,000 tu kwa mfuko utapata Tshs (10,000 x 400)= 4,000,000 na kutengeneza faida chap ya (4,000,000-3,208,000)=792,000.

      Biashara ya haraka sana na mifuko itagombaniwa kama njugu na wewe unaifanya biashara yako yote ukiwa nyumbani nyuma ya laptop yako tu na simu ya mkononi basi.

      Nikaenda mbali kidogo na kujiuliza kwanini India cement ni bei rahisi. Nikagundua kwamba, kasheshe kubwa ya kutengenza sement iko kwenye maandalizi yake hasa hasa uzalishaji wa vijiwe vidoho vigumu sana vinavyoitwa Clinker. Mchakato wa Kutengeneza malighafi hii clinker ndio mgumu na ghali zaidi. Kwa utafiti mfupi nilioufanya nimegundua utengenezaji wa Clinker Kule India Ni Ghali sana Kulinganisha na hapa kwetu TZ. Nilibahatika kutembelea kiwanda cha Lafarge Mbeya Cement maarufu kwa kutengeneza Cement ya Mnyama (TEMBO CEMENT). --Simba ni Tanga na Twiga ni DSM.

      Mchakato wa Kutengeneza Clinker unaanzia kwenye machimbo ya miamba geu yenye vichambuzi (ingredients na Ore mbalimbali) miamba hii hutoka machimboni na kuingizwa kwenye ngome ya mapondo (Crushers) ambapo hupondwa na kuwa miamba midogo mithili ya kokoto na kuzukumizwa kwenye mkanda, na vile vile huchimbwa udongo wa mfinyanzi nao hukimbizwa kwenye mkanda wake mwingine kwa viwango vyao.

      Mikanda hii miwili huingizwa kwenye ngome kubwa ya mapondo na kusagwa kwa kuchanganywa kiasi cha kuwa vumbi, hapa ndipo kiasi kikubwa cha Vumbi huzalishwa, kutokana na shughuli pevu inayofanyika. Vumbi hili hudhibitiwa sana ila kiasi kidogo hutolewa nje na kuwa wingu zito sana la Vumbi hatari kwa mazingira. Vumbi hukusanywa kwenye Kiwiko kikubwa na kirefu sana nadhani ndio point ndefu kuliko zote kwenye kiwanda cha simenti, kinachoitwa Cyclone. Cyclone Hili hupokea vumbi hilo na kulisafirisha likahifadhiwe kweye maghala makubwa (Silos) Sasa Vumbi hili laini ndio malighafi ya kutengenezea hizo Clinker.

      Vumbi hili hukimbizwa kwenye kinu kikubwa (KILN). Na huko huchomwa kwenye jotoridi la takriban nyuzijoyo 1400. Udongo huyeyushwa na kuchangamana. Chanzo cha moto huwa ni makaa ya mawe ambayo hupondwa na kuwa vumbi kisha husukumwa kwa upepo wenye gandamizo kubwa na kuzalisha moto kama jehanam ya ajabu sana ndani ya jiko hilo. Moto ule (Carbon) na udongo huo ukijumlisha na mzunguko wa jiko lenyewe, manake linachoma huku linazunguka basi huzaa vijiwe vidogo vyeusi vinavyoitwa Clinker.

      Clinker hizo hupozwa kwenye ghala (hydrous)na baadae hukimbizwa kwenye mpipa mkubwa unaozunguka wenye magololi ya chuma na vikwazo ndani yake, huko clinker hugongwagongwa na kuwa vumbi laini sana ambalo huchanganywa na vumbi jingine linaloitwa gypsum (udongo unaochimbwa Tanga) na hapo kutoa vumbi ambalo likipata maji hukauka na kuwa jiwe linaloitwa CEMENT.

      Baada ya chochezi hilo nikapeleleza na utengenezji wa Clinker kule India, ambapo mawe hununuliwa, mfinyanzi hununuliwa na zaidi ya hayo wao huchoma kwa kutumia mafuta ambapo ni gharama sana sisi tunatumia makaa ya mawe ambayo kusini ni mengi tu..

      Ukiangalia mchakato huo HAPA KWETU, Miamba geu iko mingi na bure kabisa, Makaa ya Mawe Tunayo Kusini ya Kumwaga tu, Gypsum ni udongo unaopatikana Tanga mwingi sana na Bure tu. Sasa nani katuroga mpaka Cement isiwe na bei ya Tsh 2500 au 3000 tu????!!!????

      Nikagundua gharama Kubwa za Cement ni Unyonyaji tu, Viwanda vingi vinaendesha mataifa ya nje na si tanzania. Mfano waholanzi hawa Lafarge wanamlipa MZUNGU Technician tu mwenye certificate ya ufundi karibia Dola 8,500 sawa na (8500 x 2580) = Tshs 13,400,000/=kama mshahara wake mwezi, wakati Mhandisi Mtanzania mwenye Jiwe lake moja au mawili, aliyekokotoa shule ngumu ya FoE na term system that time, na kuvivuka vikwazo vyote vya kina Prop Chambega, Luhanga , Masuha Nk ambaye ndiye mkuu wa sekta mojawapo labda project manager, au Chief Electrical, mechanical, Civil nk kiasi cha Tsh 820,000 kwa mwezi. Usawa uko wapi?. Wakati huyu fundi wa kizungu maelekezo na miongozo ya kazi anaipata kwa Mtanzania huyu ambaye ni meneja wa kitengo husika. Hivi usawa uko .. kama Fundi tu anakula madolali yote hayo je Eng wa kizungu, je Chief of DPt je manager je CO wa kizungu anajichotea mangapi.. kama hiyo haitoshi je wanajilipia kwenye serikali yao kiasi gani kwa External security, BIMA, INSUARANCE nk (maana huduma hizi zote wanajitegmezea huko kwao) na kiasi gani wanarundika kwenye mabenki yao na kuimarisha uchumi wao?

      Fedha nyingi na Utajiri Mwingi wazawa hawafaidi, tunanyonywa na kukubali kunyonyeka. Kiwanda sio Inshu kubwa, Serikali ikiamua kujenga Kiwanda hiki ni kazi nyepesi na laini sana. Kama Hawa wazungu wanaleta makandamizi haya basi tuwaalike Wajerumani waliowajengea hawa waholanzi na wengineo viwanda waijengee serikali kupitia vichwa makini chini ya PSRC ikaendesha kiwanda hiki kwa ukombozi wa wananchi wake. INAWEZEKANA..

      Alamsik..!!


      NB: Kwa muda wako jisomee:

      Tanzania: Cement sh 5,000 yawezekana!

      &k
      Maisha BORA: Songea mfuko wa cement sh 20, 000 per bag!
      ...

      Quote By Ukana Shilungo
      you are real brialiant,uchambuzi safi kabisa,mbeya cement kiwanda cha songwe Injinia mwandamizi Maro ni alikuwa injinia mkuu toka kiwanda kinajengwa mpaka kinaanza uzalishaji,aliacha kazi kwa ajili ya mzungu asiyejua kazi kulipwa Milioni 13 ili hali yeye akipokea milioni 1.5,alipatwa na uchungu akaacha kazi.meneja mkuu Diyami alimshauri Mkapa kutobinafisisha kiwanda cha Songwe ila mkapa hakusikia,kwa hiyo bei ya saruji ingeweza kuwa nafuu tatizo ni ufisadi toka kwa hawa wageni tuliowapa viwanda kwa bei ya kutupa,lengo ni kupata super profit,so THE MISSION OF CAPITALIST WHEREVER THEY ARE IS EXPLOITATION by any means,hivyo saruji kuuzwa 5000 kama alivyosema Dr slaa ni kweli,kweli tupu.
      Last edited by Eng. Y. Bihagaze; 13th June 2012 at 21:03.
      Invisible, BAK, Small Boy and 59 others like this.

    2. Miaka 50

    3. #21
      STIDE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st September 2011
      Posts : 805
      Rep Power : 556
      Likes Received
      270
      Likes Given
      0

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Vichwa kama wewe mnaipa hadhi JF na kunifanya niendelee kuwa member, hakika ongera sana japo inatia hasira!!

      Wale waliobeza kuhusu kauli hii ya Dr. Slaa naomba mrudi tena mpingane na hoja hii!!
      Eng. Y. Bihagaze likes this.

    4. #22
      Don The Great's Avatar
      Member Array
      Join Date : 25th March 2011
      Posts : 15
      Rep Power : 417
      Likes Received
      8
      Likes Given
      5

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Big Up kwa kutufungua macho,analysis nzuri sana.Nhi yetu sisi ndio imekuwa ya chuma ulete.Kila kitu kina mwisho wake hapa duniani.Tutaendelea kusali na kuomwomba mwenyezi MUNGU atupe faraja ya ukombozi wa hii taifa.

    5. #23
      joeprince's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th October 2010
      Posts : 76
      Rep Power : 450
      Likes Received
      10
      Likes Given
      14

      Default re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      SALMA2015,

      Soma hapa chini:

      Cement firms to face action for not cutting prices


      TNN Dec 25, 2011

      DHARAMSHALA: Facing stiff opposition from the Congress on the issue of high cement price in the state in comparison to neighboring states and seeing the proceedings of the recently concluded assembly session being disrupted on the issue, state government on Saturday warned cement companies of facing stern action on failing to reduce prices.

      Industries minister Kishan Kapoor said all three companies having their plants in the state were instructed to either cut cement prices or the facilities being provided to them by the state government would be withdrawn. Kapoor said that the government would not tolerate exploitation of people of the state. "Cement companies have been asked to reduce prices immediately by at least Rs 30 per bag or the government would withdraw facilities given to them," he said.

      He added that if they fail to act immediately, facilities like subsidy on electricity and transportation of cement would be withdrawn. The minister said that according to the Central Tariff Commission, production cost of cement bag weighing 50 kg comes to only Rs 136 and if current price index was added even then production cost in Himachal does not exceed Rs 150.

      "If we calculate the production cost by adding all the components like Value Added Tax (VAT), freight charges, and dealers' margin even on the higher side, the price comes out to be around Rs 225 at most of the places in Himachal," Kapoor said.

      He said despite the low production cost, companies were selling cement at much higher prices ranging between Rs 305 to Rs 335 and that was sheer exploitation of people who sacrificed their land and environment for setting up these cement plants. "As there are only three cement companies operating in the state, they were trying to create monopoly by increasing cement prices time and again, which is not tolerable," he added.





      Mid-market rates: 2012-06-13 13:43 UTC



      1.00 USD = 55.5707 INR
      US Dollar
      Indian Rupee
      1 USD = 55.5707 INR
      1 INR = 0.0179951 USD

      FANYA UTAFITI NDUGU YANGU USISIKILIZE UONGO WA WANASIASA UCHWARA WASIOJUA TOTAUTI YA Cm NA M HILO LINAWEZEKANA KABISA USIDANGANYIKE KINACHOTAKIWA NI KUHAMISHA TECHNOLOGY SIYO KULETA CEMENT MALIGHAFI YA CEMENT IKO BURE HAPA NCHINI

    6. #24
      GOMA's Avatar
      Member Array
      Join Date : 5th December 2007
      Posts : 13
      Rep Power : 588
      Likes Received
      1
      Likes Given
      14

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      This is well researched, congrats! kwa kiwango chako umejitahidi sana, . I'm wondering, some comment that this thread is too long, wamezoea kuambiwa maneno marahisi marahisi, by the way ndio wanaishi maisha magumu sana kiasi kwamba hawawezi kuhoji, kutathmini wala kutafiti japo kidogo.

      Nakubaliana na wewe kabisa kuwa bei ya cement inaweza kupungua, hata kama haitafika Tshs 5,000 lakini inaweza kuuzwa chini ya elfu 10,000 za kitanzania. Cement ya Pakstan na most of imported cements gharama zake za kuingiza nchini pamoja na ushuru hazizidi elfu saba kwa mfuko wa kilo 50. Tuamue, tubadilishe hali zetu na wenzetu wavivu wengi waliokata tamaa na kuchoka kufikiria hata kidogo

    7. #25
      figganigga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2010
      Location : dar es salaam
      Posts : 8,226
      Rep Power : 12018
      Likes Received
      2670
      Likes Given
      1584

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Mkuu wewe ni great thinker. Asante kwa utafiti wako. Naomba wahusika waufanyie kazi kwa maendeleo ya watanzania. mia


    8. #26
      Mazingira's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st May 2009
      Posts : 1,430
      Rep Power : 794
      Likes Received
      115
      Likes Given
      393

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Quote By Comi
      Kaka hongera umenena na kuichambua vizuri
      Quote By Sting007
      Thanx Man umetuelewesha zaidi, tupo tunajipanga.
      Wakuu nafikiri avatar na jina la mtoa mada ni la kike. So huyu ni mdada nafikiri.

      Back to the topic: Kwa kweli inatia hasira kuona kuwa viongozi wetu hawako makini na hawa majangili wa kizungu, kiarabu, kihindi n.k. Jamaa wanakuja kutunyonya tu kila sekta. Madini wanachukua, gesi wanatupimia kwenye kibaba, umeme wanatuhujumu, wanyama wetu wanachukua wazimawazima, bandarini nako wako, kwenye mabenki wanatuibia, shirika letu la ndege wameua, reli wameihujumu, kwenye makampuni ya simu wanatubia, yaani inatia hasira.
      Last edited by Mazingira; 13th June 2012 at 18:19.
      Invisible and Yo Yo like this.
      Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda (Mithali 3:27)

    9. #27
      Godwinnko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2012
      Location : Moshi
      Posts : 485
      Rep Power : 670
      Likes Received
      111
      Likes Given
      64

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      najenga 2016..over..!

    10. #28
      kekuwetu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th October 2010
      Location : home
      Posts : 120
      Rep Power : 459
      Likes Received
      16
      Likes Given
      41

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Quote By Negotiator
      Asante Salma uchambuzi makini. ndo maana najiuliza nani katuloga?
      chichiam ndio mchawi wetu
      asigwa likes this.

    11. #29
      POMPO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th March 2011
      Posts : 3,036
      Rep Power : 1192
      Likes Received
      1123
      Likes Given
      649

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      maisha bora kwa kila mtanzania vipi?
      "Tumefika hapa kutokana na UDHAIFU wa Rais Jakaya Kikwete.." J.J. Mnyika, Bungeni,June,2012.

    12. #30
      Nyangomboli's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th November 2010
      Location : Mwisenge
      Posts : 887
      Rep Power : 608
      Likes Received
      121
      Likes Given
      4

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Ambulance please!

    13. #31
      Biohazard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,368
      Rep Power : 991
      Likes Received
      309
      Likes Given
      210

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Well said

    14. #32
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      SALMA2015

      Container la futi 40 kutoka India mpaka hapa ni Dollar 400? nipe hiyo kampuni inayosafirisha kwa bei hii, kila kontena mimi ntakupa wewe commission ya dollar 100. Niko tayari, sasa hivi hata container 200 kuzi reserve meli nzima.

      Wacha kudanganya umma.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    15. #33
      Remote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th May 2011
      Posts : 4,281
      Rep Power : 1364
      Likes Received
      954
      Likes Given
      182

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      your a great thinker, hivi ndio vitu vya kupost sio kutwa mada za kina sheikh issa ponda.

    16. #34
      asigwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Location : TANDHANIYA
      Posts : 4,389
      Rep Power : 1265
      Likes Received
      1210
      Likes Given
      1253

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      docta ni mtu makini sana..inawezakana kuuza kwa bei hii kwani tatizo wakubwa wengi wana mikono yao katika bidhaa nyingi zinazoingia sokoni

    17. #35
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Quote By zomba
      SALMA2015

      Container la futi 40 kutoka India mpaka hapa ni Dollar 400? nipe hiyo kampuni inayosafirisha kwa bei hii, kila kontena mimi ntakupa wewe commission ya dollar 100. Niko tayari, sasa hivi hata container 200 kuzi reserve meli nzima.

      Wacha kudanganya umma.
      una matatizo sana......
      I'm Naturaly Evasive..

    18. #36
      mashami's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th May 2012
      Posts : 168
      Rep Power : 388
      Likes Received
      23
      Likes Given
      1

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Nakumbuka kuna siku DR. SLAA katika kampeni 2010 alisema msiponichagua mtajuta ndio haya sasa yanatokea na ndio tulipofikishwa naandika kwa uchungu na hasira kwa sababu tunazidi kuwaneemesha wenye nyumba na kodi za pango huku wakitupandishia bei wanavyotaka vile wanajua hatuwezi wafanya lolote.

      MUNGU nipe ujasiri kwa wale vilaza watakao kuja kupotosha hapa kwenye hii thread iliyotugusa wengi bora kupigwa BAN kuliko kukubali comment za kipuuzi zitakazo wekwa hapa namshukuru mdau hapo juu na mimi ntaungana nae KUJENGA 2016

    19. #37
      Henge's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2009
      Posts : 5,440
      Rep Power : 1675
      Likes Received
      918
      Likes Given
      1673

      Default

      Asante mkuu hata kama umeniongezea hasila!

    20. #38
      Edson's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2009
      Posts : 7,308
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1799
      Likes Given
      433

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      salma nipe vipimo vyako ili nimwambie linda Express akushonee gwanda!! uchambuzi umetulia sana...
      I'm Naturaly Evasive..

    21. #39
      Kakubilo Kasota's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th March 2012
      Posts : 166
      Rep Power : 396
      Likes Received
      53
      Likes Given
      21

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Kama ni hiv, basi sisi tumelogwa na aliyetuloga aliisha kufa siku nyingi na kaburi lake lilisha futika! Haaa, wakati ninasoma hii article yako imenifanya nijiulize hiv, Hivi Viongozi wetu hasa JK kwenye hizo safari zake huwa anajifunza nini? Sishawishiki hata kidogo kudhani kwamba eti hawa waheshimiwa hawajui haya, sinasikia wana nyumba huko Nje? kwani Cement huwa wananunuaje?

      Hivi viongozi wetu mbona wanatuchukia kiasi hiki? maana'ke mi naona ni kama wanatukomoa tu, Daa!

    22. #40
      S.Liondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th April 2011
      Posts : 344
      Rep Power : 478
      Likes Received
      55
      Likes Given
      6

      Default Re: Dr. Slaa: Mfuko wa cement utakuwa Tshs 5,000.. Ni KWELI 100%

      Kwa hii taarifa yako mkuu, basi uduni wa maisha tulionao watanzania ni wa kujitakia wenyewe, tena kwa kuukumbatia kwa mapenzi makubwa kiasi cha kushindwa kuihukumu CCM kupitia sanduku la kura. Hakuna maendeleo ya maana hapa Tanzania mpaka kuwe na mabadiliko ya maana katika serikali inayotawala.

    Page 2 of 13 FirstFirst 123412 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...