Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

    Report Post
    Page 1 of 3 123 LastLast
    Results 1 to 20 of 45
    1. #1
      Kwetu Iringa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2011
      Posts : 339
      Rep Power : 465
      Likes Received
      54
      Likes Given
      595

      Default Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Wana JF, nimekuwa katika mawazo mazito sana toka Dr. Mwakyembe aanze kushughulikia sakata la ATCL. Hili jambo limejadiliwa sana hapa jamvini. Wengine wakisema Mwakyembe kakosea wakati wengine waki-support. Hoja yangu iko tofauti na hili. Siko upande wowote wa mjadala huu.

      Mara nyingi sana tumeshuhudia au kusikia Pinda akichelea kuchukua hatua juu viongozi waiopatikana na makosa kwa kisingizio kuwa anayepaswa kuwachukulia hatua za nidhamu ni Rais!!

      Sasa Mbona Dr. ameweza kuwachukulia hatua hawa vigogo wa ATCL? Pinda, ambaye ni boss wa Dr, anashindwaje kuwachukulia hatua vigogo wa aina hii?

      Je hii inathibitisha ile imani ya kuwa Pinda ni mwoga au dhaifu? Au hawa vigogo wa ATCL waliochukuliwa hatua za nidhamu na Dr ni tofauti na wale ambao Pinda anawaogopa?? Au Dr ni jasiri zaidi ya Pinda? Au ni nini?

      Nawasilisha!

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      Njowepo's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Location : Santiago
      Posts : 7,591
      Rep Power : 22053
      Likes Received
      992
      Likes Given
      769

      Default re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Kuna watu huzaliwa wana confidence na wengine huzaliwa hawana confidence!
      Haujawai kuta subordinate ana confidence kuliko bosi wake tena kwa kiwango ata cha kumpiga biti bosi tena akaufyata
      WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

    4. #3
      Kwetu Iringa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th July 2011
      Posts : 339
      Rep Power : 465
      Likes Received
      54
      Likes Given
      595

      Default re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Quote By Njowepo
      Kuna watu huzaliwa wana confidence na wengine huzaliwa hawana confidence!
      Haujawai kuta subordinate ana confidence kuliko bosi wake tena kwa kiwango ata cha kumpiga biti bosi tena akaufyata


      Nimewahi!!

    5. #4
      Asnam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th January 2012
      Location : Yutong
      Posts : 2,570
      Rep Power : 1011
      Likes Received
      1594
      Likes Given
      1131

      Default re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Quote By Kwetu Iringa
      [/COLOR]
      Nimewahi!!
      duuh ulivyoitikia kwa upole hadi nimecheka.
      Mupirocin likes this.
      "Quality is always better than quantity. That's why the people I call true are few."

    6. #5
      Asnam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th January 2012
      Location : Yutong
      Posts : 2,570
      Rep Power : 1011
      Likes Received
      1594
      Likes Given
      1131

      Default re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      nampongeza Dr kwa ujasiri wake mi nakasirika sana viongozi wanaosema 'ngoja fulani aje'utadhani wenyewe pale waliwekwa kuziba nafasi tu wanafanana na wanawake fulani ambao mtoto akikosea anamwambia ngoja baba'ko arudi anafikiri anatibu kumbe anaharibu,naomba hao viongozi wajifunze na wabadilike
      Kwetu Iringa likes this.
      "Quality is always better than quantity. That's why the people I call true are few."

    7. Miaka 50

    8. #6
      Comi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd October 2011
      Posts : 960
      Rep Power : 578
      Likes Received
      155
      Likes Given
      2

      Default re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Unashindwa kujua hata weledi wa kiongozi wako?ni mara ngapi umesikia mzee mapinda kuwa ni spring? Tabu yeye kawekwa kama pambo,wenzake wanajitolea maisha yao

    9. #7
      Kunta Kinte's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 18th May 2009
      Posts : 2,565
      Rep Power : 2534
      Likes Received
      595
      Likes Given
      762

      Default re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Pinda waziri mkuu dhaifu katika historia ya Tanzania
      Have patience with all things, but chiefly have patience with yourself.- Saint Francis de Sales

    10. #8
      MAKAWANI's Avatar
      Member Array
      Join Date : 3rd May 2012
      Posts : 95
      Rep Power : 374
      Likes Received
      27
      Likes Given
      21

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda??!!???

      Mtizamo wangu ni tofauti kidogo! Isingekuwa busara kwa Waziri Mkuu kuingilia kati jambo kama lile wakati kuna Baraza la Mawaziri lanalokaa na kila mmoja kuwajibika. Pili ikumbukwe Lowasa ukiherehere wake wa kuingilia kila kitu ulimponza na hatimae ikamlazimu kujiuzulu. So Pinda amekuwa ni mtu wa kuzingatia sana utawala wa kisheria, kwa mfano hili la ATCL lilikuwa chini ya bodi ambayo ikishindwa anafuatia Waziri husika. Na kama Pinda hajapokea malalamiko yoyote toka kwa Waziri husika au taarifa yoyote yenye utata juu ya aliyetimuliwa hawezi kukurupuka kama alivyofanya Mwakyembe kwa kuamini taarifa za mdomoni (eti nasikia baadhi yenu mkawapigia simu kuwa hela imetoka) na kutengua uteuzi wake. So nadhani sometimes hawa mawaziri pamoja na uzuri wao pia wana mapungufu ambayo huwa ni vigumu kuyaona kwa mtu wa kawaida.

    11. #9
      POMPO's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 12th March 2011
      Posts : 2,955
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1090
      Likes Given
      625

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Kwetu Iringa,
      Pinda hajawahi kufanya maamuzi yoyote yale toka awe PM, zaidi ya Kulia na kuahidi ahid tu, na amekuwa PM wa kwanza TZ kutaka kung`olewa na Bunge. yupo buze na Sumry bus service,

    12. #10
      MKALIKENYA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 703
      Rep Power : 499
      Likes Received
      281
      Likes Given
      403

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Acheni kuwafananisha ZIDANE(MWAKYEMBE) na LUNYAMILA(PINDA).
      Njowepo likes this.

    13. #11
      mtotowamjini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Location : None of Your Business
      Posts : 4,531
      Rep Power : 1262
      Likes Received
      1109
      Likes Given
      28

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      sasa imagine Mwakyembe angekua ni waziri mkuu ingekuaje?? mbona viongozi wengi wangetafutana???
      Mpalisya Imbogo likes this.
      Every saint has a past, every sinner has a future' ...Oscar Wilde

      One man's good fortune is another man's misfortune


    14. #12
      mlaizer's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st January 2011
      Posts : 225
      Rep Power : 465
      Likes Received
      39
      Likes Given
      90

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Bosi Chizi ATCL ampinga Mwakyembe
      Aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi ambaye hivi karibuni alitenguliwa katika cheo hicho na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe wiki jana, amefikisha ramsi malalamiko yake kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

      Uchunguzi wa gazeti la Habari Leo umebaini kuwa Chizi amewasilisha malalamiko yake kwa Waziri Mkuu akipinga tuhuma zilizoelekezwa kwake na Waziri, Mwakyembe akidai si za kweli na kwamba zimelenga kumshushia hadhi kwa jamii.

      Pamoja na barua hiyo, Chizi amewasilisha lundo la vielelezo vikifafanua tuhuma mbalimbali zilizotolewa na Dkt. Mwakyembe dhidi yake, ili kuthibitisha kutokubaliana na tuhuma hizo kwake. Kaimu Mkurugenzi huyo wa zamani wa ATCL alipotafutwa jana ili kuzungumzia suala hilo alikiri suala hilo kuwasilishwa ofisi ya Waziri Mkuu, ingawa hakuwa tayari kulizungumzia zaidi kwa madai kuwa liko kwenye mamlaka za juu sasa.

      Tuhuma ya sare za milioni 80/-

      Maelezo ya Chizi kwa Pinda, yanafafanua kwamba ATCL ilinunua loti 30 za vifaa mbalimbali vya wafanyakazi zikiwamo sare zilizotajwa na Dk Mwakyembe kwa thamani ya dola za Marekani 18, 920 na si dola za Marekani 50,000 kama alivyodai Waziri Mwakyembe, hatua ambayo ilifanya ATCL kuokoa zaidi ya Sh milioni 44 kama ingenunua sare hizo nchini kulingana na bei ya ununuzi iliyowasilishwa ATCL.

      Tuhuma ya ukodishaji wa ndege

      Anapinga pia kuhusishwa na ukodishaji wa ndege aina ya Airbus ambayo Waziri Mwakyembe alisema haikuwa na sababu ya kukodishwa, akisema ndege hiyo ilikodishwa mwaka 2007 na kufanya kazi hadi mwaka 2008, wakati yeye aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Agosti 2011. Dk Mwakyembe akizungumzia mkataba huo tata wa Airbus, alisema umeifanya nchi kudaiwa Sh bilioni 69 na kusisitiza kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali haikuwa tayari kufumbia macho mambo mengine ya ovyo yanayoendelea katika shirika hilo.

      “Kuhusu ukodishaji wa ndege aina ya Boeing 737 – 500 kutoka Kampuni ya Aerovisto, utaratibu wa kawaida wa ukodishaji wa ndege kwa njia ya wetlease ulifanyika, taratibu zote kama zinavyotakiwa kisheria zilifuatwa.

      “Ilikuwa ni suala la kushitua sana kwangu pale nilipopata maelekezo kutoka kwa Katibu Mkuu (Wizara ya Uchukuzi, Omar Chambo) kwamba taratibu hazikufuatwa, na hivyo ndege tuliyoikodi haikutakiwa kuruka kinyume na barua ya Waziri Mwakyembe mwenyewe ya Mei 12, akieleza kuridhishwa na hatua tulizochukua katika ukodishaji ndege na kuturuhusu kuendelea na mchakato,” ilisema barua hiyo.

      “Suala la kupeleka mkataba wa ACMI kwa AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) ambao si utaratibu wa kawaida, lilikuja wakati mchakato wa kuleta ndege uko katika hatua za juu kabisa. Hata hivyo, maagizo yalizingatiwa; mkataba ulikwenda kwa AG hata baada ya Waziri kutoa maoni yake kuwa ni mzuri. Waziri alitoa kauli kama hiyo pia kwenye kikao cha Kamati ya Bunge ya Miundombinu kilipokaa Ofisi Ndogo za Bunge hivi karibuni,” ilisema barua hiyo.

      Tuhuma za fedha na akaunti

      Barua hiyo kwa Waziri Mkuu ikifafanua kuhusu suala la sare za ATCL ilisema lilishafanyiwa uchunguzi baada ya Chambo kuunda Tume kuchunguza ubadhirifu huo ikiongozwa na DAP wa Sekretarieti ya Utumishi wa Umma Shekiondo Magesa na Tume kubaini hakukuwa na ubadhirifu wowote na kumpongeza Chizi kwa kuokoa fedha za Kampuni.

      “Madai ya Waziri Mwakyembe kuhusu fedha za bima ni kwamba kampuni ya Alexander Forbes ilitoa taarifa, kuwa fedha za bima zingetumwa kwenye akaunti yetu wiki ya nne ya Mei 2012.

      Menejimenti ya ATCL ilikaa na kutafakari agizo la Wizara kutaka fedha hizo zipelekwe CHC (Kampuni Hodhi ya Mashirika ya Umma).

      “Tulisubiri kupata akaunti ya CHC ili tutoe maagizo hayo. Hata hivyo, akaunti hiyo tulichelewa kuipata, ndipo tulipokwenda benki kutaka kupata njia mbadala ya kuhakikisha usalama wa fedha zetu. Mei 28 dola za Marekani milioni 3 zililipwa kwenye akaunti yetu ya Stanbic na Menejimenti ya ATCL ikaagiza benki ihamishe fedha hizo ili zishikiliwe kama dhamana ya ATCL kupata mtaji wa kujiendesha.

      “Maagizo ya kuhamishwa pesa hiyo ili zihifadhiwe na benki yalitolewa kwa benki siku hiyo hiyo Mei 28. Asubuhi ya Mei 29 wakati mchakato wa kuzihifadhi haujakamilika, tulitaarifiwa kuwa dola milioni moja zimezuiwa na amri ya mahakama kutoka Kampuni ya Ultimate Security yenye thamani ya dola 993,000.

      “Hapo hapo tulielekeza wanasheria wetu wazuie utekelezaji wa amri hiyo na jambo hilo lilifanyika na pesa hiyo ipo kwenye akaunti salama hadi leo, hakuna aliyelipwa kama alivyosema Waziri Mwakyembe. Shauri hilo litatolewa uamuzi Juni 18,” ilisema barua hiyo.

      Kulingana na vielelezo vilivyowasilishwa Ofisi ya Waziri Mkuu, gazeti la Habari Leo limebaini kuwa wakati Wizara ya Uchukuzi ikiwasilisha barua ya maagizo ya fedha hizo za bima kuwekwa kwenye akaunti ya CHC, malipo hayo ya bima yalikuwa yamelipwa kupitia akaunti ya Stanbic na kampuni ya Alexander Forbes asubuhi siku hiyo.

      Gazeti la Habari Leo lilipowasiliana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo jana, alithibitisha kupokewa kwa malalamiko hayo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo wa ATCL na kusema ofisi yake ilikuwa bado inayafanyia kazi ili kufahamu mwenendo mzima wa suala hilo kabla ya kulizungumzia.



      Source: Chizi awasilisha barua kwa Waziri Mkuu kupinga 'tuhuma' za Dkt. Mwakyembe dhidi yake - wavuti

    15. #13
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14620
      Likes Received
      2841
      Likes Given
      1961

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Umekosa cha kuandika?
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    16. #14
      brazilian's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th February 2012
      Posts : 609
      Rep Power : 1358
      Likes Received
      101
      Likes Given
      5

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Quote By Kwetu Iringa
      Wana JF, nimekuwa katika mawazo mazito sana toka Dr. Mwakyembe aanze kushughulikia sakata la ATCL. Hili jambo limejadiliwa sana hapa jamvini. Wengine wakisema Mwakyembe kakosea wakati wengine waki-support. Hoja yangu iko tofauti na hili. Siko upande wowote wa mjadala huu.


      Pi
      Mara nyingi sana tumeshuhudia au kusikia Pinda akichelea kuchukua hatua juu viongozi waiopatikana na makosa kwa kisingizio kuwa anayepaswa kuwachukulia hatua za nidhamu ni Rais!!

      Sasa Mbona Dr. ameweza kuwachukulia hatua hawa vigogo wa ATCL? Pinda, ambaye ni boss wa Dr, anashindwaje kuwachukulia hatua vigogo wa aina hii?

      Je hii inathibitisha ile imani ya kuwa Pinda ni mwoga au dhaifu? Au hawa vigogo wa ATCL waliochukuliwa hatua za nidhamu na Dr ni tofauti na wale ambao Pinda anawaogopa?? Au Dr ni jasiri zaidi ya Pinda? Au ni nini?

      Nawasilisha!
      Pnda amkanza lini kuwa na madaraka. Yupo yupo tu kwenye cabinet

    17. #15
      Njowepo's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 26th February 2008
      Location : Santiago
      Posts : 7,591
      Rep Power : 22053
      Likes Received
      992
      Likes Given
      769

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Chizi utalalamika sana ila suala la wewe kurudi pale halipo!
      Maana nimjuavyo Mwakyembe anaweza ata Kujiuzulu kwa ilo suala!
      Kama hauna ukweli kwenye izo tuhuma si usubiri kamati ya uchunguzi waje na report yao!
      WB Tanzania lead economist Jacques Morisset said the GDP doubled in 10 years, but it has failed to produce any significant decline in poverty levels.

    18. #16
      OPTIMUS TZ's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th January 2012
      Posts : 390
      Rep Power : 446
      Likes Received
      60
      Likes Given
      1

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      wazazi kumlinganisha pinda na mwkb ni sawa na kulinganisha mshumaa na genereta

    19. #17
      data's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2011
      Posts : 2,094
      Rep Power : 853
      Likes Received
      363
      Likes Given
      315

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      hata mimi sijui ni nini?

    20. #18
      TUMY's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2009
      Posts : 706
      Rep Power : 654
      Likes Received
      90
      Likes Given
      200

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Wakati mwingine inategemea unamwajibisha nani.Pinda si dhaifu ila ni waziri mkuu aliyenyimwa mamlaka.

    21. #19
      massai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd May 2011
      Posts : 625
      Rep Power : 532
      Likes Received
      109
      Likes Given
      2

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Pinda hajui wajibu wake,kazi kulialia tu,hovyo kabisa,mlokole mnafiki huyo.

    22. #20
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 589
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default Re: Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

      Simply ni kuwa Mh. Pinda hana confidence, ingawa ni mwadilifu na ni mtu ambaye yuko honest, kuhusu Dr. Mwakyembe ni kuwa yeye ni jasiri wala sio mwoga.

    Page 1 of 3 123 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...