Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

    Report Post
    Page 5 of 5 FirstFirst ... 345
    Results 81 to 84 of 84
    1. #1
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,617
      Rep Power : 15263
      Likes Received
      3732
      Likes Given
      2868

      Default Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Masha: Vijana wengi hawaipendi CCM


      ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, amesema vijana wengi nchini hawataki CCM kwa sababu hawaoni kilichofanyika tangu kilipoanzishwa.

      Masha alisema wananchi wanahitaji kuona mabadiliko na kwamba, hali hiyo inatokana na kutosoma vizuri historia ya Tanzania. Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV, alisema hatua ya kutopenda chama hicho imetokana na vijana kutosoma historia.

      “Vijana wengi hawaipendi CCM, wengi wanataka mabadiliko… siyo kosa lao, hawakufundishwa. Kuna wakati nilikuwa Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza nazungumza, kijana mmoja akasimama akasema nyie, wazee ndiyo wanarudisha nyuma nchi. Nikaangalia nyuma nikajiuliza huyo mzee yuko wapi... Nikagundua kumbe na mimi ambaye nilikuwa najiona kijana kniko kwenye kundi la wazee” alisema Masha.

      Masha ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Fortunatus Masha, alisema vijana wengi wanapenda mabadiliko ya haraka jambo ambalo hawalioni ndani ya CCM na kuongeza kuwa, hali hiyo inasababishwa na kutokuwapo kwa mkakati wa kuwafundisha historia ya mafanikio ya Serikali na viongozi wake.

      “Leo hii ukienda Nairobi ukitaka kitabu kuhusu maisha ya Raila Odinga utaipata, ukitaka historia ya (Daniel) Moi .. Kenyatta utaipata. Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili ajue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna,” alisema Masha na kuongeza:

      “Sasa kama mtoto ambaye anataka kujua nchi yake, anakosa hata pa kuipata, nchi yake ikoje, marais waliotawala, tumefikaje hapa? Lazima waseme tumekuwa maskini kwa sababu ya chama ambacho kiko madarakani.”

      Kuhusu kushindwa kwake ubunge mwaka 2010, Masha alisema amekubali kushindwa na anaendelea na kazi zake nyingine.

      “Ukiingia kwenye uchaguzi ni sawa tu na kuingia kwenye mpira, kuna kushinda na kushindwa, kikubwa ukishashindwa kubali matokeo endelea na maisha. Tatizo watu wengi na hasa wanasiasa wenzangu hawana kazi nyingine za kufanya,” alisema Masha.

      Alipinga madai kuwa kipindi chake cha ubunge na uwaziri hakufanya lolote katika jimbo lake, badala yake alitoa mifano ya kazi alizofanya na kwamba, wanaoeneza hayo ni watu wenye fitina.

      “Sidhani kama ni kweli, unajua kwenye siasa kuna fitina imani yangu ni kwamba kazi yangu nilifanya na kazi yangu ya uwaziri niliifanya. Of course (bila shaka) kutokana na mfumo tulionao, mwenzako lazima akumalize ili akushinde,” alisema Masha na kuongeza:

      “Leo hii tunapoongelea Nyamagana kuna chuo cha polisi kimejengwa, kuna Sekondari ya Mkolani imejengwa nje ya bajeti ya Serikali… ni kutoka kwa wafadhili na marafiki, there’s a lot of works (kuna kazi nyingi).”

      Alisema alikuwa akisomesha watoto 236 kwa mshahara wake wa ubunge na kwamba, tangu alipoingia bungeni mshahara wake ulikuwa ukipelekwa jimboni kusaidia wasiokuwa na uwezo.

      “Leo hii ndiyo watu wanakumbuka, ndiyo nasema leo hii hata mke wangu na watoto wangu nao wafurahi kidogo kile ninachokipata, nipeleke kwenye maendeleo ya familia,” alisema.

      Hata hivyo, Masha alisema kazi za siasa zinahitaji uvumilivu hivyo alijitahidi kuvumilia changamoto hizo kipindi chote cha uongozi wake.
      Ndahani and Ben Mugashe like this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #81
      mkurugenz's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 200
      Rep Power : 400
      Likes Received
      15
      Likes Given
      16

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      ni kweli bila kujua historia ya kitu na ukweli wake si rahisi kukipenda na kukithamini

    4. #82
      Biohazard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,368
      Rep Power : 991
      Likes Received
      309
      Likes Given
      210

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By PlanckScale
      Kwanza kwa aliyekuwa waziri kusema anaelimisha wanae nje bila hofu niishara kwamba hajali maslahi ya wananchi.
      Out of touch.
      CCM sio TANU
      Ama kweli sie maskini 2na kazi kubwa sana. Halafu anadai hakuna vitabu vya historia. Kama serikali haiwapi vipaumbele waandishi hapa bongo unategemea nani ataandika kitabu cha Nyerere, Kawawa,Mkwawa na wengine. kwanza ukiandika makala ambayo ni non-fiction yenye ukweli mtupu unamwagiwa tindikali. Sasa hizo vitabu ukisema fulani kauwawa si khali yako itakua mbaya sana?

    5. #83
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Hivi kuna tatizo gani kuanza kuandika upya historia ya matukio na wahusika wa matukio mbali mbali ndani ya Tanzania? Kila kitu kinapindihswa pindishwa. Why? I am very much interested kujua kwa undani participation yetu kwenye vita vya ukombozi kusini mwa Africa na michango ya wahusika mbali mbali
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    6. #84
      Chakaza's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2007
      Location : everywhere
      Posts : 3,563
      Rep Power : 1478
      Likes Received
      893
      Likes Given
      530

      Default

      Quote By Jasusi
      Candid Scope,
      Unataka kuniambia kuwa tungekuwa na elimu bora kuliko tuliyo nayo hivi sasa vijana wetu wangeshabikia CCM? I think there is more to it than simply blaming it on education. CCM imewapoteza vijana kwa sababu kimegeuka kuwa chama cha kulaghai. Angalia ahadi alizozitoa Kikwete katika uchaguzi wa 2010. Hivi kweli unaamini Kigoma itageuzwa kuwa Dubai wakati wa utawala wa Kikwete, ambao amebakiwa na miaka mitatu tu?
      Masha anapaswa kushukuru kuwa kutokana na Elimu kuwa chini chuki kwa CCM ni ndogo maana kama vijana kama wangepatiwa elimu iliyobora zaidi na kuelewa tumetoka wapi na kwanini tuko hapa basi chuki ingekuwa kubwa zaidi.Na sio ajabu wangeiondoa CCM kwa style ya Tunisia
      Jasusi likes this.

    7. Miaka 50
    Page 5 of 5 FirstFirst ... 345

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...