Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

    Report Post
    Page 4 of 5 FirstFirst ... 2345 LastLast
    Results 61 to 80 of 84
    1. #1
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,602
      Rep Power : 15259
      Likes Received
      3727
      Likes Given
      2862

      Default Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Masha: Vijana wengi hawaipendi CCM

      ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, amesema vijana wengi nchini hawataki CCM kwa sababu hawaoni kilichofanyika tangu kilipoanzishwa.

      Masha alisema wananchi wanahitaji kuona mabadiliko na kwamba, hali hiyo inatokana na kutosoma vizuri historia ya Tanzania. Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV, alisema hatua ya kutopenda chama hicho imetokana na vijana kutosoma historia.

      “Vijana wengi hawaipendi CCM, wengi wanataka mabadiliko… siyo kosa lao, hawakufundishwa. Kuna wakati nilikuwa Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza nazungumza, kijana mmoja akasimama akasema nyie, wazee ndiyo wanarudisha nyuma nchi. Nikaangalia nyuma nikajiuliza huyo mzee yuko wapi... Nikagundua kumbe na mimi ambaye nilikuwa najiona kijana kniko kwenye kundi la wazee” alisema Masha.

      Masha ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Fortunatus Masha, alisema vijana wengi wanapenda mabadiliko ya haraka jambo ambalo hawalioni ndani ya CCM na kuongeza kuwa, hali hiyo inasababishwa na kutokuwapo kwa mkakati wa kuwafundisha historia ya mafanikio ya Serikali na viongozi wake.

      “Leo hii ukienda Nairobi ukitaka kitabu kuhusu maisha ya Raila Odinga utaipata, ukitaka historia ya (Daniel) Moi .. Kenyatta utaipata. Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili ajue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna,” alisema Masha na kuongeza:

      “Sasa kama mtoto ambaye anataka kujua nchi yake, anakosa hata pa kuipata, nchi yake ikoje, marais waliotawala, tumefikaje hapa? Lazima waseme tumekuwa maskini kwa sababu ya chama ambacho kiko madarakani.”

      Kuhusu kushindwa kwake ubunge mwaka 2010, Masha alisema amekubali kushindwa na anaendelea na kazi zake nyingine.

      “Ukiingia kwenye uchaguzi ni sawa tu na kuingia kwenye mpira, kuna kushinda na kushindwa, kikubwa ukishashindwa kubali matokeo endelea na maisha. Tatizo watu wengi na hasa wanasiasa wenzangu hawana kazi nyingine za kufanya,” alisema Masha.

      Alipinga madai kuwa kipindi chake cha ubunge na uwaziri hakufanya lolote katika jimbo lake, badala yake alitoa mifano ya kazi alizofanya na kwamba, wanaoeneza hayo ni watu wenye fitina.

      “Sidhani kama ni kweli, unajua kwenye siasa kuna fitina imani yangu ni kwamba kazi yangu nilifanya na kazi yangu ya uwaziri niliifanya. Of course (bila shaka) kutokana na mfumo tulionao, mwenzako lazima akumalize ili akushinde,” alisema Masha na kuongeza:

      “Leo hii tunapoongelea Nyamagana kuna chuo cha polisi kimejengwa, kuna Sekondari ya Mkolani imejengwa nje ya bajeti ya Serikali… ni kutoka kwa wafadhili na marafiki, there’s a lot of works (kuna kazi nyingi).”

      Alisema alikuwa akisomesha watoto 236 kwa mshahara wake wa ubunge na kwamba, tangu alipoingia bungeni mshahara wake ulikuwa ukipelekwa jimboni kusaidia wasiokuwa na uwezo.

      “Leo hii ndiyo watu wanakumbuka, ndiyo nasema leo hii hata mke wangu na watoto wangu nao wafurahi kidogo kile ninachokipata, nipeleke kwenye maendeleo ya familia,” alisema.

      Hata hivyo, Masha alisema kazi za siasa zinahitaji uvumilivu hivyo alijitahidi kuvumilia changamoto hizo kipindi chote cha uongozi wake.
      Ndahani and Ben Mugashe like this.

    2. FemaTV & Radio

    3. #61
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,692
      Rep Power : 903
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By Candid Scope

      Thanks Jasusi, elimu ni pana na wala tuizungumzayo hatumaanishi ya vitabuni tu na wewe unafahamu fika juu ya niongeleacho. Mfano makamanda wa Chadema wanavyozunguka nchi nzima kutoa somo la uraia kwa wananchi na jinsi wananchi wanavyowaelewa na kuitikia kiasi cha kubadili kabisa wimbi la mtazamo wa kisiasa za mageuzi nchini mwetu. Hii ni moja wapo ya elimu ambayo wananchi wameikosa na CCM imefanya kila jitihada kuwanyima kwa ajili ya wachache wabaki kuwa katika nafasi wanazotaka bila kunyoshewa vidole na wananchi.

      Serikali haijawa na mfumo wa kuwafunda watu namna ya kutoa elimu ya kujitegemea kama enzi za awamu ya kwanza ambapo vijijini kulikuwa na msukumo wa kujitegemea na watu baada ya kuhitimu shule walikuwa na mwelekeo wa uzalishaji vijijini. Leo elimu hiyo imekosekana, vijana toka vijijini baada ya kuhitimu shule wanakimbilia mijini. Ukiona vijana walivyojaa mijini huwezi kuamini wanakula nini na wanaajiriwa wapi na ndio maana wako waitikiaji wazuri sana kwenye mihadhara kwa kuwa hawana cha kufanya. Nenda vijiji wamebaki vijana wachache wana ambao nao wengi wanatafuta nafasi ya kwenda mijini na vijiji vimebaki makazi ya wazee tu.

      Amini nisemayo kwani nimefanya utafiti na kushuhudia hali ilivyo vijijni na mijini. Shule za kata zimesaidia kuwashika walio mashuleni kubaki huko, na wakishahitimu wanatimkia mijini, ni dalili ya kukosa somo la elimu ya kujitegemea ambalo nio muhimu kwa mazingira ya kujiajiri vijijini ingawa nako kuna changamoto nyingi zinazotokana na kukosekana kwa miundo mbinu mbalimbali na kukosekana kwa utility.
      ..asante,kwa mwerevu atakuwa amekuelewa vema.na hapa ndo kuna shida!

    4. #62
      Kaseisi's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th March 2012
      Posts : 88
      Rep Power : 380
      Likes Received
      24
      Likes Given
      15

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Mshahara wangu umesomesha watoto ??? Ni lazima uwe Mbunge kufanya hili? Hivi kazi ya Ubunge ni ipi? This is too cheap, kwani kwa biashara zako tu ungeweza kusomesha watoto wengi zaidi ya hao Mr. Masha, well kubali kuwa ulishindwa kuzikonga nyoyo za wakazi wa Mwanza, next time if there will be next time kuwa karibu na wananchi waliokuchagua

    5. #63
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,692
      Rep Power : 903
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By TIMING
      kilikua cheo cha maana kwasbabu ya siasa za chama kimoja

      u-DC ni sawa na u-CD tu kisiasa.... hasa kutokana na matendo ya baadhi ya ma DC kudhani kazi yao ni kusimamia interest za chama badala ya interest za wilaya
      ...kwanza hiki cheo kifutwe,hakina maadili yyte,matumizi mabaya ya rasilimali za taifa!...

    6. #64
      Sangarara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th September 2011
      Posts : 3,291
      Rep Power : 1195
      Likes Received
      1178
      Likes Given
      1551

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By Janjaweed
      hapana, umemiss his point

      anazungumia knowledge... wakiwa na knowledge watafanya better decisions
      Umemiss point tena
      Masha yuko very clear, anazungumzia Historia ya Viongozi wetu hata sio Jamii yetu. VIONGOZI WETU, Kwamba tukijua Historical Background ya Ben Mkapa tutaipenda CCM. Kama Historia hii ni Knowledge inayoweza kunisaidia kurudi na mkate nyumbani jioni basi uko sawa.

    7. #65
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,154
      Rep Power : 24267
      Likes Received
      4668
      Likes Given
      2294

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By POMPO
      Mkuu, avatar yako ile tuliizoea sana irudishe kamanda, mpaka nimejiuliza huyu ni Mungi yupi but siyo issue kanyaga twende,
      Mkuu avatar ni ya yule yule we sema hapo nimepo kwenye suti kwa mapunziko, mapambano yakianza natinga tena!
      POMPO likes this.
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    8. Study Abroad

    9. #66
      POMPO's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 12th March 2011
      Posts : 2,955
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1090
      Likes Given
      625

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Huyu Masha anavuta shuka kumekucha leo ndio analifaham hilo?

    10. #67
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,602
      Rep Power : 15259
      Likes Received
      3727
      Likes Given
      2862

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By Biohazard
      Sasa hizo shule za kata mliwajengea kina nani kama nyie watoto wenu wanasoma nje?
      Mwenye nafasi ya kwenda kulima shamba ng'ambo ya pili hana kosa kwa vile nafasi inamruhusu, kwani ninayelalamika labda uwezo wa kufikia sina, laiti ningekuwa nao huenda ningeenda mbali ya hapo.

    11. #68
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,602
      Rep Power : 15259
      Likes Received
      3727
      Likes Given
      2862

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By nngu007
      Na aliucheza bahati mbaya Mpinzani wake alikuwa Makini Ukamshinda; Wakumbuka alijitangaza yeye na Ngeleja wamepita bila kupingwa? Anasubiri kuapishwa tu na Rais? Alimsingizia Mpinzani wake Vidudu Vya Ajabu; Leo hii anaongea haongelei hayo baada ya zaidi ya Nusu Mwaka anapanga Interview akiwa anajua ana Jambo Jipya kila Mtu atafurahia na Masikini kama Sisi tutalipenda, anajitokeza anatunusisha alivyofanya Mazuri... Woote tunalala chini na kumpigia Makofi...
      Wakati wa kutafuta kuingia mjengoni ye yote aatatumia kila upenyo unaowezekana kumpitisha kwa urahisi, lakini hilo si la kuzuia kutoa ya moyoni ambayo yana manufaa kwa nchi na mageuzi kwa nchi yetu.

    12. #69
      Manumbu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2009
      Location : Close to U
      Posts : 1,127
      Rep Power : 723
      Likes Received
      259
      Likes Given
      760

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      sikubaliani na analysis ya kuwa vijana wakielimishwa/wakielimika wataona mazuri ya CCM na kukikubali. In fact ni kinyume chake. kwa yeyote mwenye knowledge na asiye beneficiary wa moja kwa moja wa CCM, hawezi katu kukishabikia CCM. kwa sababu ndogo tu. Kwa mwenye knowledge ataona madudu makubwa yafanywayo na CCM na hatokubali.

      lakini kwa upande mwingine pia, tumeona jinsi CCM inavyo manipulate watu wenye elimu ndogo na uelewa mdogo hususan vijijini na hasa maeneo ya kusini mwa nchi. na kwa kutumia huo uelewa wao mdogo wamekuwa wakijipatia kura zao kwa wingi. so hii hypothesis ya Masha sio sahihi
      "Falling Down does not mean being Buried" - Manumbu on 1st June 2011

    13. #70
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,156
      Rep Power : 3545
      Likes Received
      3037
      Likes Given
      460

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By Candid Scope
      Wakati wa kutafuta kuingia mjengoni ye yote aatatumia kila upenyo unaowezekana kumpitisha kwa urahisi, lakini hilo si la kuzuia kutoa ya moyoni ambayo yana manufaa kwa nchi na mageuzi kwa nchi yetu.
      LOL... Angalia familia inayomzunguka ameisaidiaje? Au Amesaidia hao wanafunzi kujitangaza? Hizo ndio siasa za Sasa
      Nimesomesha hawa, Nimejenga hiki, Anaweza kufanya hivyo, kama ana Nyumba South Africa...

      Angalia Amesaidia Ndugu Wangapi halafu uje uniambia kweli huyu ni mtu swafi, ni hivyo alivyo pleasing public for his own advantages, angalia sasa alivyopata hawa Mashabiki wa ajabu

      Mnadhani alipokuwa waziri nani angefika ofisini kwake? mlisha wahi kuuliza watu waliomjua jinsi walivyonyanyasika?

    14. #71
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,602
      Rep Power : 15259
      Likes Received
      3727
      Likes Given
      2862

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By nngu007
      LOL... Angalia familia inayomzunguka ameisaidiaje? Au Amesaidia hao wanafunzi kujitangaza? Hizo ndio siasa za Sasa
      Nimesomesha hawa, Nimejenga hiki, Anaweza kufanya hivyo, kama ana Nyumba South Africa...

      Angalia Amesaidia Ndugu Wangapi halafu uje uniambia kweli huyu ni mtu swafi, ni hivyo alivyo pleasing public for his own advantages, angalia sasa alivyopata hawa Mashabiki wa ajabu

      Mnadhani alipokuwa waziri nani angefika ofisini kwake? mlisha wahi kuuliza watu waliomjua jinsi walivyonyanyasika?
      Naona tumetoka nje ya uringo kwani mada haikulewa kumjadili Masha, ila kauli yake ndiyo tunayoijadili. Kauli na uchambuzi wa Masha una maana gani kwa umma. Kuhusu kukosekana kwa elimu kwa vijana ambao awali elimu ilikuwa inafundishwa hasa vijijini kujitetemea, leo kwa nini vijana karibu wote wanakimbilia mijini badala ya kufanya uzalishaji vijijini? Kuna tatizo la uelimishaji umma hapa. Elimu ni pana si kusoma vitabu tu.

      Masha ni sawa na mchezaji wa basketi, mambo yakimzidi uwanjani huenda kupumzika kwenye benchi na kutafakari yaliyojilia hadi kuzidiwa kete. Kutafakari huko ni muhimu na ndio maana tunamwona ameamua kuchukua mkondo wake ambao anaona unamlindia heshima yake kuliko hizi nafasi za utwa na utwana na kuvuana nguo mbele ya wakwe.

      Masha kajadili jambo zuri ambalo nimependezwa nalo. Wengi tatizo letu kujadili jambo tunamtazama nani kasema hayo badala ya kufikiria maudhui ya mada yana maana gani kwetu. Binadamu si kama jiwe. Tujifunze static na dynamic. Kwa vyo vyote binadamu hubadilika na mazingira yanayomzunguka ni darasa kubwa la maisha kwa wanofungua akili tofauti na jiwe ambalo lipo kama lilivyo miaka nenda rudi.

    15. #72
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,602
      Rep Power : 15259
      Likes Received
      3727
      Likes Given
      2862

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By Manumbu
      sikubaliani na analysis ya kuwa vijana wakielimishwa/wakielimika wataona mazuri ya CCM na kukikubali. In fact ni kinyume chake. kwa yeyote mwenye knowledge na asiye beneficiary wa moja kwa moja wa CCM, hawezi katu kukishabikia CCM. kwa sababu ndogo tu. Kwa mwenye knowledge ataona madudu makubwa yafanywayo na CCM na hatokubali.

      lakini kwa upande mwingine pia, tumeona jinsi CCM inavyo manipulate watu wenye elimu ndogo na uelewa mdogo hususan vijijini na hasa maeneo ya kusini mwa nchi. na kwa kutumia huo uelewa wao mdogo wamekuwa wakijipatia kura zao kwa wingi. so hii hypothesis ya Masha sio sahihi
      Kuelimika kwa vijana hakuna maana ya kuyaelewa ya Chama fulani, ila elimu ya maisha. Vijana wanachofuata Chadema si kupata ya Chadema ila kupata kiu ya elimu kwa ajili ya maisha yao.

    16. #73
      +255's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st January 2012
      Posts : 1,079
      Rep Power : 588
      Likes Received
      205
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Ezan
      Ningalipata chanzo cha hii habari ningalichangia japo kidogo
      Kulikuwa na umuhimu gani ku quote post yote ka hauna la kuchangia? Mnatusumbua tunaotumia simu.

    17. #74
      mangikule's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 907
      Rep Power : 530
      Likes Received
      174
      Likes Given
      235

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By Candid Scope
      Masha: Vijana wengi hawaipendi CCM

      ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani na Mbunge wa Nyamagana, Lawrence Masha, amesema vijana wengi nchini hawataki CCM kwa sababu hawaoni kilichofanyika tangu kilipoanzishwa.

      Masha alisema wananchi wanahitaji kuona mabadiliko na kwamba, hali hiyo inatokana na kutosoma vizuri historia ya Tanzania. Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV, alisema hatua ya kutopenda chama hicho imetokana na vijana kutosoma historia.

      “Vijana wengi hawaipendi CCM, wengi wanataka mabadiliko… siyo kosa lao, hawakufundishwa. Kuna wakati nilikuwa Chuo Kikuu cha St Augustine Mwanza nazungumza, kijana mmoja akasimama akasema nyie, wazee ndiyo wanarudisha nyuma nchi. Nikaangalia nyuma nikajiuliza huyo mzee yuko wapi... Nikagundua kumbe na mimi ambaye nilikuwa najiona kijana kniko kwenye kundi la wazee” alisema Masha.

      Masha ambaye ni mtoto wa mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Fortunatus Masha, alisema vijana wengi wanapenda mabadiliko ya haraka jambo ambalo hawalioni ndani ya CCM na kuongeza kuwa, hali hiyo inasababishwa na kutokuwapo kwa mkakati wa kuwafundisha historia ya mafanikio ya Serikali na viongozi wake.

      “Leo hii ukienda Nairobi ukitaka kitabu kuhusu maisha ya Raila Odinga utaipata, ukitaka historia ya (Daniel) Moi .. Kenyatta utaipata. Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili ajue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna,” alisema Masha na kuongeza:

      “Sasa kama mtoto ambaye anataka kujua nchi yake, anakosa hata pa kuipata, nchi yake ikoje, marais waliotawala, tumefikaje hapa? Lazima waseme tumekuwa maskini kwa sababu ya chama ambacho kiko madarakani.”

      Kuhusu kushindwa kwake ubunge mwaka 2010, Masha alisema amekubali kushindwa na anaendelea na kazi zake nyingine.

      “Ukiingia kwenye uchaguzi ni sawa tu na kuingia kwenye mpira, kuna kushinda na kushindwa, kikubwa ukishashindwa kubali matokeo endelea na maisha. Tatizo watu wengi na hasa wanasiasa wenzangu hawana kazi nyingine za kufanya,” alisema Masha.

      Alipinga madai kuwa kipindi chake cha ubunge na uwaziri hakufanya lolote katika jimbo lake, badala yake alitoa mifano ya kazi alizofanya na kwamba, wanaoeneza hayo ni watu wenye fitina.

      “Sidhani kama ni kweli, unajua kwenye siasa kuna fitina imani yangu ni kwamba kazi yangu nilifanya na kazi yangu ya uwaziri niliifanya. Of course (bila shaka) kutokana na mfumo tulionao, mwenzako lazima akumalize ili akushinde,” alisema Masha na kuongeza:

      “Leo hii tunapoongelea Nyamagana kuna chuo cha polisi kimejengwa, kuna Sekondari ya Mkolani imejengwa nje ya bajeti ya Serikali… ni kutoka kwa wafadhili na marafiki, there’s a lot of works (kuna kazi nyingi).”

      Alisema alikuwa akisomesha watoto 236 kwa mshahara wake wa ubunge na kwamba, tangu alipoingia bungeni mshahara wake ulikuwa ukipelekwa jimboni kusaidia wasiokuwa na uwezo.

      “Leo hii ndiyo watu wanakumbuka, ndiyo nasema leo hii hata mke wangu na watoto wangu nao wafurahi kidogo kile ninachokipata, nipeleke kwenye maendeleo ya familia,” alisema.

      Hata hivyo, Masha alisema kazi za siasa zinahitaji uvumilivu hivyo alijitahidi kuvumilia changamoto hizo kipindi chote cha uongozi wake.
      Kumbe njaa ikiuma unazinduka usingizini. Shibe ilimlevya wakati ule akashindwa kufanyia kazi anayoyasema.
      Candid Scope likes this.

    18. #75
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,156
      Rep Power : 3545
      Likes Received
      3037
      Likes Given
      460

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By Candid Scope
      Naona tumetoka nje ya uringo kwani mada haikulewa kumjadili Masha, ila kauli yake ndiyo tunayoijadili. Kauli na uchambuzi wa Masha una maana gani kwa umma. Kuhusu kukosekana kwa elimu kwa vijana ambao awali elimu ilikuwa inafundishwa hasa vijijini kujitetemea, leo kwa nini vijana karibu wote wanakimbilia mijini badala ya kufanya uzalishaji vijijini? Kuna tatizo la uelimishaji umma hapa. Elimu ni pana si kusoma vitabu tu.

      Masha ni sawa na mchezaji wa basketi, mambo yakimzidi uwanjani huenda kupumzika kwenye benchi na kutafakari yaliyojilia hadi kuzidiwa kete. Kutafakari huko ni muhimu na ndio maana tunamwona ameamua kuchukua mkondo wake ambao anaona unamlindia heshima yake kuliko hizi nafasi za utwa na utwana na kuvuana nguo mbele ya wakwe.

      Masha kajadili jambo zuri ambalo nimependezwa nalo. Wengi tatizo letu kujadili jambo tunamtazama nani kasema hayo badala ya kufikiria maudhui ya mada yana maana gani kwetu. Binadamu si kama jiwe. Tujifunze static na dynamic. Kwa vyo vyote binadamu hubadilika na mazingira yanayomzunguka ni darasa kubwa la maisha kwa wanofungua akili tofauti na jiwe ambalo lipo kama lilivyo miaka nenda rudi.

      He was not on the same game with you from the start; Nadhani alikuwa na best opportunities than most of us from way back, na wengi wao kama yeye wana NGO's kusaidia Nchi zao; Sio kugombea Ubunge na Madini ili kuendeleza ulaji.

      Sasa hivi angekuwa anafanya kwa Wananchi kwa Yeye na Baba yake walivyopata Nje na Hapa Nchini Wote Wamekuwa Wabunge Mmojwa wa East Africa na Mwingine wa Tanzania hapo ingekuwa bora; Kama kweli unaipenda nchi yako

      Vijana sio hawaipendi CCM; Mimi ni wa Mwanza watu wengi walikuwa na Imani na Lau, lakini ukienda huko kila mtu ana Jambo la kukueleza kuhusu alivyotenda; kabla ya kusifia fanya Uchunguzi wako be fair; Usione Mtu kwenye TV na Maneno Mazuri ukanunuliwa. Hapo hatutaweza kuwa na Viongozi bora hata kidogo kila siku tutachagua Mafisadi.

    19. #76
      Mvaa Tai's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th August 2009
      Location : Ngudu, Mwanza
      Posts : 3,394
      Rep Power : 1175
      Likes Received
      1388
      Likes Given
      905

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By +255
      Kulikuwa na umuhimu gani ku quote post yote ka hauna la kuchangia? Mnatusumbua tunaotumia simu.
      Sorry sikujua kwamba una simu ya hivyo
      Mnang'oa meno ya Tembo ili mukayauze, mnang'oa meno na Kucha za Watanzania wasio na hatia ili iweje?

    20. #77
      Biohazard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2011
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,365
      Rep Power : 991
      Likes Received
      308
      Likes Given
      210

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By Candid Scope
      Mwenye nafasi ya kwenda kulima shamba ng'ambo ya pili hana kosa kwa vile nafasi inamruhusu, kwani ninayelalamika labda uwezo wa kufikia sina, laiti ningekuwa nao huenda ningeenda mbali ya hapo.
      Nimekusoma barabara
      Candid Scope likes this.

    21. #78
      Noboka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th November 2011
      Posts : 493
      Rep Power : 2248
      Likes Received
      153
      Likes Given
      23

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Alichoongea Masha kina mashiko, suala la kwamba alikuwa waziri au mbunge si la msingi sana, binafsi naamini wengi walio CCM kama viongozi kuna wakati akili zao kama wanaziacha mahali wanabaki kama misukule tu, wakitoka ndiyo akili zao zinarudi wanaanza kuuona ukweli. Hongera Masha endelea na maisha yako ya ujasiriamali na siasa ikibidi achana nayo lakini usihame CCM.
      Ni mtizamo wako tu!
      Candid Scope likes this.

    22. #79
      PlanckScale's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2008
      Location : Bongo
      Posts : 404
      Rep Power : 1027
      Likes Received
      34
      Likes Given
      89

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Quote By Biohazard

      Mimi kijana wangu ana miaka 17 anasoma South Africa (Afrika Kusini) alikuja hapa anaomba kitabu ili nijue Tanzania imetoka wapi,..Hakuna,” alisema Masha na kuongeza:

      Sasa hizo shule za kata mliwajengea kina nani kama nyie watoto wenu wanasoma nje?

      Kwanza kwa aliyekuwa waziri kusema anaelimisha wanae nje bila hofu niishara kwamba hajali maslahi ya wananchi.
      Out of touch.
      CCM sio TANU
      "It is better to die for an idea that will live, than to live for an idea that will die." Steve Biko

    23. #80
      Bubona's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st August 2011
      Posts : 278
      Rep Power : 445
      Likes Received
      53
      Likes Given
      11

      Default Re: Masha athibitisha Vijana wengi hawaipendi CCM

      Vijana hawahitaji kufundishwa historia ya mafanikio, wanahitaji kuona mafanikio!!

    24. Miaka 50
    Page 4 of 5 FirstFirst ... 2345 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...