Nimepata taarifa za kiuchunguzi kwamba Mbunge wa Nzega Hamisi Kigwangallah amepigwa stop na chama chake wilayani Nzega kutokufanya maandamano yake akiambatana na wananchi na viongozi mbalimbali yaliyopangwa kufanyika kule Nzega tarehe 16/06/12.
Nimewasiliana na mbunge huyo kwenye facebook muda si mrefu na amesema kuwa ataendelea na maandamano kama yalivyopangwa kwa kuwa mpaka sasa polisi hawajamzuia kisheria na kwa kuwa ni ya amani hakuna haja ya chama chake kuwa na mashaka kwa kuwa anafanya kazi waliyomtuma kufanya ya kuwawakilisha wananchi na kudai maslahi yao.
Mbunge huyo anasema chama hakina sababu ya kumzuia na wala hakina uwezo huo maana kitakuwa kinamuingilia katika utekelezaji wa majukumu yake na hakuna kanuni hata moja ya kimaadili anayovunja kufanya kazi hiyo bega kwa bega na wananchi na viongozi wenzake. anaendelea kusema kwamba katibu wa CCM wilayani pale amekurupuka kuandika barua ile (ambayo nimeiamabatanisha hapa) maana haina nguvu yoyote ile kisheria na wala kikatiba ya CCM.
Anawaalika wananchi, viongozi na wapenda haki pote nchini kwenda Nzega kuhudhuria maandamano yale. Asema mpaka sasa wabunge wafuatao waahidi kuwepo na kuhutubia mkutano huo unaotarajiwa kuwa mkubwa wa aina yake; mhe. Seleman Zeddy (CCM, Bukene), mhe. Kangi Alphaxard Lugola (CCM, Mwibara), mhe. James Lembeli (CCM, Kahama), mhe. Nyambari Nyangwine (Tarime) na anaendelea kualika wengine.
Chikaka.

Reply With Quote





Follow Us Here