JamiiSMS
  Show/Hide This

  Topic: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

  Report Post
  Page 1 of 8 123 ... LastLast
  Results 1 to 20 of 141
  1. dosama's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th December 2010
   Posts : 777
   Rep Power : 629
   Likes Received
   353
   Likes Given
   1

   Default Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Sasa deni la Tanzania limefika Trilioni 22 sasa tunaambiwa tunadaiwa sasa kwani ile misaada Jk anayopitisha bakuli ndo madeni haya au kuna kwingine wanakokopa? Kwa matumizi ya nani?

   Source: Star tv habari

   ============

   Jan 2014:

   Kila raia Tanzania anadaiwa 600,000/-. Deni la Taifa lafikia trillion 27.04

   Quote By Candid Scope View Post

   Kila Mtanzania bila kujali kama ni mtoto, mzee au mfanyakazi anadaiwa Sh. 600,000 miongoni mwa watu milioni 45 raia wote wa Tanzania.

   Hali hiyo inatokana na kuongezeka kwa deni la Taifa kufikia Dola za Marekani bilioni 17.10 (Sh. trilioni 27.04 hadi kufikia Desemba mwaka jana.

   Kwa mtumishi wa serikali anayelipwa kima cha chini cha Sh. 150,000 kwa mwezi atatakiwa kulipa deni kwa miezi minne mfululizo bila kubaki na chochote.

   Deni hilo ni bajeti ya serikali ya mwaka mmoja na nusu kwa mujibu wa bajeti ya mwaka 2013/14 ya Sh. trilioni 17.7.

   Kati fedha hizo, Dola bilioni 12.79 (Sh. trilioni 20.23) ni deni la nje na la ndani ni Sh. trilioni 6.81.

   Hayo yalibainishwa na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum, jijini Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari kuelezea utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo.

   Hata hivyo, alisema pamoja na kuongezeka kwa deni hilo, serikali itaendelea kukopa kwa sababu bado ina sifa za kukopa kwa kuwa kiwango cha deni ni asilimia 28 wakati ukomo wa kukopa ni asilimia 50.

   Aliongeza kuwa itakopa fedha kwa masharti nafuu ambazo zitaelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya miundombinu ambayo aliitaja kuwa ni barabara, reli, bandari, mkongo wa Taifa, bomba la gesi, viwanja vya ndege Zanzibar na Songwe.

   Waziri Mkuya alifafanua kuwa sababu za kuongezeka kwa deni ni mikopo iliyopokelewa na serikali ambayo muda wake wa kulipa haujafika kutoka vyanzo vya masharti nafuu na ya kibiashara na malimbikizo ya deni la nje kiasi cha dola za Marekani milioni 801.7 kwenye nchi zisizo wanachama wa jumuiya ya wahisani.

   Aliongeza kuwa serikali itajadiliana na nchi hizo kuhusu msamaha wa kufutiwa deni hilo.

   Alisema Serikali inatoa kipaumbele kwa miradi ya ubia kati ya serikali na sekta binafsi ili kuiwezesha kuchangia maendeleo ya uchumi na kuipunguzia serikali mzigo wa madeni.

   Alisema Septemba mwaka jana serikali kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa ilifanya thathmini kuangalia uhimilivu wa deni la taifa kwa kutumia vigezo vilivyowekwa na kutambuliwa kimataifa na kwamba ilionyesha deni ni himilivu kwa sababu viashiria vyote bado viko chini ya ukomo unaotakiwa.

   MATUMIZI YA EFD
   Akizungumzia matumizi ya mashine za kielektroniki EFD, alisema wataendelea kuyazitolea ufafanuzi na kuyasimamia vema kwa madhumuni ya kukusanya kodi kwa ufanisi zaidi ili kuongeza pato la taifa na kupunguza ukwepaji kodi.

   Alisema serikali itaendelea kutoa elimu kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa wafanyabiashara kwa kuwa huo ndiyo msimamo wa serikali. Alifafanua kuwa serikali iliwapa uhuru wafanyabiashara wanaolalamikia mashine hizo kuunda kamati na kwenda kutembelea nchi za China na Bulgaria zinapotengenezwa na kuangalia uhalisia wa bei, lakini walikataa.

   Kuhusu ukuaji wa uchumi, Mkuya alisema umekua kwa kiwango kikubwa na unaendelea kuimarika kwa wastani na kwamba pato la taifa lilikuwa kwa asilimia saba kwa kipindi cha miezi tisa ya mwanzo wa mwaka 2013.

   MFUMUKO WA BEI

   Kwa upande wa mfumuko wa bei, alisema umeendelea kushuka hadi asilimia 5.6 Desemba mwaka jana kulinganisha na asilimia 19.8 mwaka 2012. Alisema kupungua kwake kulitokana na sera thabiti za fedha na kibajeti pamoja na kuimarika kwa uzalishaji na usambazaji wa chakula.

   Alisema matumizi ya fedha za kigeni katika mzunguko wa uchumi Mtanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yoyote nchini kwa fedha hizo isipokuwa sehemu za utalii na ada za shule za kimataifa.

   Alisisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia vyema suala hilo ikiwamo kuwachukulia hatua wanaokiuka utaratibu huo.

   SARAFU MOJA EAC
   Akizungumzia matumizi ya sarafu moja kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mkuya alisema wanaendelea na mchakato na watalipeleka bungeni kwa majadiliano zaidi kabla ya maamuzi.

   Akizungumzia Bunge la Bajeti, alisema licha ya kufanyika kwa Bunge la Katiba, wanatarajiwa kuwa bajeti itawasilishwa, kupitishwa na kuanza kutumika Julai Mosi, mwaka huu, lakini alisema kama kutakuwapo na viashiria, serikali itatoa taarifa.

   Alipoulizwa kuhusu baadhi ya wanasiasa wanaohoji uwezo na uzoefu wake wa kusimamia wizara hiyo, alijibu kwa kifupi kuwa hataki maswali hayo kwani ni historia na kwamba Rais Jakaya Kikwete amekwisha kumteua na anaendelea kuchapa kazi.

   Kuhusu madai ya baadhi ya watumishi wa serikali na watoa huduma serikalini, alisema tatizo liko katika halmashauri kwa kuwa fedha zinatumwa na kuwa kinachofanyika ni uzembe. Hata hivyo, Mkuya aliahidi kwamba serikali itafuatilia.
   Dotworld and Askari wa miguu like this.


  2. PrN-kazi's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 5th February 2011
   Posts : 2,643
   Rep Power : 5493
   Likes Received
   365
   Likes Given
   5

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Aiseee! Nchi inauzwa hivihivi!!!!!!!!!

  3. nachid's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th April 2011
   Location : IRINGA
   Posts : 689
   Rep Power : 595
   Likes Received
   94
   Likes Given
   9

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Watu wa mahisabati hebu tuambieni hiyo tirion ina sifuri ngapi? tuongeze mastress

  4. Precise Pangolin's Avatar
   JF Gold Member Array
   Join Date : 4th January 2012
   Posts : 7,854
   Rep Power : 339833
   Likes Received
   1768
   Likes Given
   723

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Tumuombe shimbo atupunguzie Hilo deni
   eddo likes this.

  5. Mkiliman's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 8th June 2011
   Posts : 736
   Rep Power : 602
   Likes Received
   150
   Likes Given
   22

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Hii noma....sijui mie nadaiwaga mahera mangapi hapo, nilisikiaga last time ilikuwaga kama laki 3 na ujinga fulani hivi..aaa?
   eddo likes this.

  6. JF SMS Swahili

  7. Uwezo Tunao's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th November 2010
   Posts : 6,955
   Rep Power : 2354
   Likes Received
   1166
   Likes Given
   1517

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   ... ni kichefuchefu kwa mtindo huu wa kuendesha uchumi wa nchi yetu; maneno kibao midomoni na majukwaani na kazi sifuri kwa sehemu kubwa ya viongozi 'wetu' wanaojipa vyeo vy kila aina kwa njia ya UCHAKACHUAJI.

   Hakika hadi hapo, kuna hatari kubwa ya kudharaulika mno huko ktika jumuia ya kimataifa na Tanzania kupoteza uhuru wake wa 'kutetea chochote' kwa kuwa ni MDENI KWA KILA NCHI NA TAASISI kaadhaa za huko kwa wenzetu.

   Lakini, enyi MAFISADI msiokua na huruma hata chembe na taifa, je tumefikaje hapa???

  8. Tume ya Katiba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Location : Chumbuni-Zanzibar
   Posts : 3,435
   Rep Power : 0
   Likes Received
   729
   Likes Given
   378

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Hakuna nchi isiyodaiwa hapa duniani! so sio issue kuubwa kihivyo! Hata wanaotupa misaada wana madeni makubwa sana!

  9. Viol's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 15th December 2009
   Location : Shamna
   Posts : 10,305
   Rep Power : 21852005
   Likes Received
   329
   Likes Given
   116

   Default

   Quote By nachid View Post
   Watu wa mahisabati hebu tuambieni hiyo tirion ina sifuri ngapi? tuongeze mastress
   22,000,000,000,000
   Dotworld likes this.

  10. Kibanga Ampiga Mkoloni's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 10th August 2007
   Location : Here! here!
   Posts : 8,921
   Rep Power : 0
   Likes Received
   2697
   Likes Given
   1900

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Hujuhi wewe hakuna hela ya Bure huwa napitisha bakuli la MIKOPO.
   For the Holy Quran says in Sura 42, verse 41: 'All those who fight when oppressed incur no guilt, but Allah shall punish the oppressor, Come the day.

  11. FJM's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 11th April 2011
   Posts : 7,826
   Rep Power : 1354141
   Likes Received
   5833
   Likes Given
   4706

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Quote By Tume ya katiba View Post
   Hakuna nchi isiyodaiwa hapa duniani! so sio issue kuubwa kihivyo! Hata wanaotupa misaada wana madeni makubwa sana!

   Wenzetu wanakopa kujenga madaraja, barabara sisi tunakopa kulipa mishahara na mafuta ya mashangingi!

  12. Jackbauer's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 28th October 2010
   Location : CTU
   Posts : 5,229
   Rep Power : 31755
   Likes Received
   1475
   Likes Given
   306

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   nijuavyo mimi nina deni la mahari tu,sh. Laki tatu hilo jingine ni la jakaya and co.
   Msinipakazie bure!

  13. Makala Jr's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 25th August 2011
   Posts : 3,324
   Rep Power : 14450
   Likes Received
   991
   Likes Given
   0

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Saizi nimetoka kutoa salamu za rambirambi mjini shinyanga.Duuuh Kumbe ndo maana naona gari hilifiki haraka kumbe tumeuzwa.R.I.P BOB MAKANI mwambie Nyerere kwamba kile alichokiacha kimeuzwa,la zaidi kila mtanzania anadaiwa na nchi za magharibi.It is a bad news but namwomba Mungu tufike salama SAUT.

  14. Honolulu's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 20th January 2012
   Posts : 3,341
   Rep Power : 0
   Likes Received
   451
   Likes Given
   0

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Watanzania hamna sababu ya kulalamika! Mambo mengine mnayataka wenyewe!! Ndiyo malupulupu ya kuweka ushabiki wa Yanga na Simba katika siasa bila kuangalia uhalisia wa mambo. Kwa kuwa kura mlipiga wenyewe, basi vumilieni!! Hadi 2015 mtakuwa mmepata akili!!

  15. jnuswe's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 2nd November 2010
   Posts : 1,084
   Rep Power : 1876
   Likes Received
   442
   Likes Given
   49

   Post re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Quote By Tume ya katiba View Post
   Hakuna nchi isiyodaiwa hapa duniani! so sio issue kuubwa kihivyo! Hata wanaotupa misaada wana madeni makubwa sana!
   Nikuweke kundi gani la watu, chagua wewe, kuna kundi la wajinga, wapumbavu na mbumbumbu, hata hivyo utakuwa umpependelewa kuwekwa kwenye makundi hayo , upeo wako ni sifuri
   UKI likes this.

  16. BONGOLALA's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 14th September 2009
   Posts : 8,223
   Rep Power : 2189
   Likes Received
   2136
   Likes Given
   425

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Gaddafi anaondoka madarakani,LIBYA ilikua haina deni wana mafuta tuu,hakuna hata mmea!SISI JEEEEEE?

  17. Tume ya Katiba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Location : Chumbuni-Zanzibar
   Posts : 3,435
   Rep Power : 0
   Likes Received
   729
   Likes Given
   378

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Quote By FJM View Post
   Wenzetu wanakopa kujenga madaraja, barabara sisi tunakopa kulipa mishahara na mafuta ya mashangingi!
   Mkuu JFM hii ni propaganda na serikali ya chama cha mapinduzi kupitia aliyekuwa waziri wake wa fedha mustafa mkulo alikanusha, na kubainisha makusanyo ya kodi ikilinganishwa na matumizi ikiwemo mishahara. Kwa hiyo sio kweli hata kidogo kuwa misaada inatumiwa kwa mishahara.

   Hizi ni propaganda za kina zitto.

  18. Marire's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st May 2012
   Posts : 5,533
   Rep Power : 2264577
   Likes Received
   1413
   Likes Given
   0

   Default

   Quote By Tume ya katiba View Post
   Hakuna nchi isiyodaiwa hapa duniani! so sio issue kuubwa kihivyo! Hata wanaotupa misaada wana madeni makubwa sana!
   mkuu tume,
   sisi ni masikini na tunadaiwa,hizo nchi unazosai kuwa zinatusaidia na zinadaiwa ungetaja japo mbili alafu uzifananishe na tz. Pesa wamekula hao ccm na usitafute kuwatetea hapa!

  19. Marire's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 1st May 2012
   Posts : 5,533
   Rep Power : 2264577
   Likes Received
   1413
   Likes Given
   0

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Alafu mnasema uchumi unakuwa,unakuwa kwa ritz babake na mkulo

  20. Ulukolokwitanga's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 18th September 2010
   Location : ndzengelendete
   Posts : 4,289
   Rep Power : 13714
   Likes Received
   2433
   Likes Given
   529

   Default

   Hii sasa ni hatari tunaelekea kuwa kama Ugiriki. Hivi wanakopa wanafanyia nini hizo fedha maana barabara full vumbi, watoto wanakaa chini shuleni, hospitali hazina dawa!! Kweli CCM ni janga la kidunia, 2015 ifike haraka watuachie nchi yetu

   Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

  21. Tume ya Katiba's Avatar
   JF Senior Expert Member Array
   Join Date : 6th April 2012
   Location : Chumbuni-Zanzibar
   Posts : 3,435
   Rep Power : 0
   Likes Received
   729
   Likes Given
   378

   Default re: Deni la Taifa lafikia zaidi ya Trilioni 20: Nini hatma ya nchi kiuchumi?

   Quote By jnuswe View Post
   Nikuweke kundi gani la watu, chagua wewe, kuna kundi la wajinga, wapumbavu na mbumbumbu, hata hivyo utakuwa umpependelewa kuwekwa kwenye makundi hayo , upeo wako ni sifuri
   Asante kwa maoni yako mazuri, ila nina wasiwasi sana na upeo wako kuhusu madeni ya taifa. Karibu nchi zote hapa duniani zina madeni, tena tanzania ni afadhari. Angalia nchi kama ugiriki, spain na nyenginezo wana mizigo ya madeni.

   Only issue, ni je hiyo misaada(mikopo) inatumikaje? Mwenye uwezo wa kujenga hoja hapa ni yule atakayetuletea mchanganuo wa hiyo misaada tunayopata TZ tunaipeleka katika shughuli gani in comparison to other countries. sio UTULETEE FIGURE tu hapa. huu ni upuuzi.

  22. JF SMS Swahili

  Page 1 of 8 123 ... LastLast

  Similar Topics

  1. Deni la Taifa sasa lakimbilia kuwa Trilioni 25
   By Return Of Undertaker in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 70
   Last Post: 1st February 2014, 11:37
  2. Replies: 74
   Last Post: 31st January 2014, 14:58
  3. Replies: 150
   Last Post: 23rd February 2013, 01:01
  4. Tanzania: Deni la taifa lafikia Sh. Trilioni 20!
   By EMT in forum Jukwaa la Siasa
   Replies: 108
   Last Post: 4th January 2013, 09:20
  5. Replies: 18
   Last Post: 18th April 2012, 22:48

  Posting Permissions

  • You may not post new threads
  • You may not post replies
  • You may not post attachments
  • You may not edit your posts
  •  

  Who are WE?

  JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

  You are always welcome! Read more...

  Where are we?

  We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

  For anything related to this site please Contact us.

  Contact us now...

  DISCLAIMER

  JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

  Read more...

  Forum Rules

  JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

  You MUST read them and comply accordingly. Read more...

  Privacy Policy

  We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

  Read our Privacy Policy. Proceed here...