
By
Kiranga
Very mechanical thinking.
Wewe inaonekana unakariri a la "rote learning". Nani kakwambia hayo? Nani anaweza kuipinga signature style yangu ya "toe to toe"? Mimi naweza kukwambia anayejibu kwa mpigo anaweza kuruka kitu au kukwepa, anayeenda kipengeie kwa kipengele anahakikisha na cover kila kitu. Ndicho ninachofanya hapa.
Sema tu huna umakini wala fortitude ya kujibu kipengele kwa kipengele, na hivyo nina ku frustrate kiasi cha kusema "sizitaki mbichi hizi".
Halafu kuhusu kwenda "back to school" wajanja wote wanajua hilo ndilo jambo la muhimu. Mie kila siku naenda back to school, tena nimeihamishia school nyumbani hapa juzi kaja profesa mmoja hapa anasema "you have a small college's library in here, I carried books to read but I will not need them because you have so many wonderful books". Kwa hiyo mie back to school kila siku, si kitu cha kuniambia. Kama wewe huendi back to school on the regular imekula kwako kwani elimu haina mwisho.
Hapa una force king. Hata hao watu wa fasihi wanatofautiana, wengine wanasema mashairi lazima yawe na vina na mizani, wengine wanasema si lazima. Sasa wewe sheria zako za wapi hizo zinazosema siwezi kutumia signature style yangu ya toe to toe kama Chama na Mogella?
Ama u mgumu wa kuelewa au mbishi kama mshipa, nimekuambia swali si kwamba Masha ana haki ya kupata tenda. tena unakosea unaposema kupata tenda ni haki ya kiraia kwa sababu anaweza kuja mwekezaji wa nje ambaye si raia akapata tenda vile vile.
Talk about going back to school. It seems you also need to go back to school kujua "haki za kiraia" ni nini.
Nimeongea kuhusu umuhimu wa culture ya biashara hapo juu. Sipingi culture ya biashara. Ninachofanya hapa ni kupalilia culture ya biashara yenye standards za juu zaidi.
Wewe unayekandia "njia za mkato" hujatuonyesha kwamba kwa Masha hii si njia ya mkato. Hujatuonyesha kwamba kulikuwa na open tender. Hujatuonyesha kwamba Masha hakutumia influence yake kupata biashara kinyume cha taratibu. Unaposema kwamba hutaki njia za mkato wakati unayemtetea, kwa culture ya biashara ya Tanzania, anaweza kuwa amepata biashara kwa njia ya mkato, nashindwa kukuchukulia seriously.
Basically ulichosema hapa ni kwamba huna jibu.Hujui kitu. Kama hujui kitu kaa kimya, waache wanaojua wajibu.
Hakuna aliyekutaka kufanya utafiti. Utafiti unaujua hata mwanzo wake wewe? Hii forum ina watu wengi, wa kila rika, kutoka kila kona ya nchi wenye access na info tofauti.
Last time I checked, kuuliza swali si kosa. Mie sijatoa hata statement hapa kusema Masha kapata biashara kinyume na tenda. Nimeuliza swali. Huna jibu kaa kimya. Una jibu lilete. Unataka libeneke, lilete. Wewe naona katika makundi haya unaangukia kwenye libeneke, maana huna jibu halafu unataka kuleta longolongo nyingi.
Sihitaji kufanya lolote kati ya hayo kuwaonyesha cheerleaders wanaomshangilia Masha kwamba ni mfano kuwa hatuwezi kupiga makofi wakati hatujui deal limefikwaje.
Hata ukiwekewa sinia la utafiti unaonukia chini ya pua zako huwezi kuujua wewe.
Ni tabia ya waliokosa hoja wakibanwa kukimbilia kutaja chuki. Mie nina chuki na nani wakati nakula bata zangu viwanja? Huyo Masha atanizuia nini mambo yangu mpaka niwe na chuki naye?
Hapa ndipo unajionyesha kabisa kwamba bingwa wa tangential wandering, nani kasema Masha maisha yamemshinda?
Unaposema "wengine tunafikiri" umejiweka wewe na wenzako, wewe na nani mnafikiri hivyo?
Stick to one thing already, mara wengine tunafikiri, mara la hasha. Which is which?
Kutembea si hoja, Hata Wiliam MAlecela katembea na probably kaka viwanja kuliko most of us since yeye mkubwa halafu kakanyaga viwanja na meli enzi hizo, lakini angalia uozo unaomtoka hata wadogo zangu wa Mkuranga ambao meli sanasana wanapanda kwenda Mafia, na ndege ndio sahau, wamemzidi kipimo kwa fikra. Kwa hiyo kutembea si tija kama akili haijatulia.
Wewe unamjua Masha personally?
Kama hilo ndilo unaona la kujifunza basi una mengi saaana ya kujifunza, na pengine ndio maana huwezi kuelewa this "Securities and Exchange Commission" level of scrutiny I am bringing down here.
We have a long way to go kama hawa ndio vijana wenyewe wanaotegemewa kuleta mabadiliko nchini. Hata kimawazo tu hawajachamgamka bado.
Follow Us Here