Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Sheikh Ponda yuko sahihi

    Report Post
    Page 2 of 16 FirstFirst 123412 ... LastLast
    Results 21 to 40 of 313
    1. #1
      mwongozo's Avatar
      Member Array
      Join Date : 26th October 2011
      Posts : 45
      Rep Power : 392
      Likes Received
      9
      Likes Given
      21

      Default Sheikh Ponda yuko sahihi

      Juzi Sheikh Ponda Issa ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu alitanabahisha kuwa iwapo serikali haitoweka kipengele cha dini katika fomu za sensa ya mwaka, jumuiya yao itahamasisha Waislamu wasishiriki katika zoezi la sensa.Alisema kuwa nchi hii siyo ya Kikristo lakini INATAWALIWA NA MFUMO KRISTO.

      Alisema kutokana na mazoea, Waislamu wanabaguliwa katika mgawanyo wa keki ya taifa khasa upande wa ajira. ofisi na idara za serikali zinaongozwa na Wakristo kwa asilimia kubwa kulinganishwa na waislamu. alitoa mfano wa TRA, NECTA, Wizara ya Eimu, Wizara ya Ujenzi, Afya, Mahakama nk........... kwa mujibu wa Sheikh Ponda, wastani wa ajira ni karibu Wakristo 77% na Waisalmu siyo zaidi ya asilimia 20%. Licha ya hoja inayojengwa kuwa Waislamu hawajasoma lakini akasema waliosoma wapo.

      Akatanabahisha kuwa kwa maslahi na umoja wa kitaifa, kupuuza watu ambao ni sehemu ya jamii ktk keki ya taifa ni jambo hatari sana! Kwa kuwa wtu wanadai waislamu ni chini ya 20% katika nchi hii, akapendekeza sensa ya mwaka huu kiwekwe kipengele cha dini ili idadi ya watanzania kidini ijulikane. Kwa mujibu wa Sheihk Ponda, anaamini kuwa waislamu ni takriban 64% ya rais wa Tanzania.

      "SIYO SAHIHI WATU WENYE IDADI HII KUPUUZWA KATIKA UWIANO WA AJIRA SERIKALINI", alisema Sheikh Ponda.Alitoa mifano wa nchi karibia zote za Ulaya, Marekani, asia pamoja na Afrika, kipengele cha dili kipo kwenye fomu za sensa zao. "Ukisoma country profile au fact file uingiapo katika nchi mbalimbali, utakuta wameandika wastani wa idada ya raia kidini" alisisitiza Ponda. "Mbona mnajifanya kama hamtembei au hamjui kinacho endelea ulimwengunu jamani!" alilalama Ponda.

      HOJA YANGU Ndugu znaguni Watanzania, tufike sehemu tuache ukweli udhihiri. kama Waislamu wanalalamika kuwa wanabaguliwa katika ajira labda kutokana na uchache wao, kwa nini suala la dini lisiwekwe wazi? au utakua udini? au uchochezi? au uvunjifu wa amani? Kama ni hivyo, mbona karibu 98% ya sensa zote duniani zina kipengele cha dini!? je huko wameuana kutoakana na kipengele hicho? TUBADILIKE!!!

      Naomba kuwasilisha!
      takashi, Ally Kombo, NIMO and 2 others like this.

    2. RukaaJuu Final

    3. #21
      Lyimo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th March 2006
      Posts : 1,800
      Rep Power : 1527
      Likes Received
      796
      Likes Given
      451

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Quote By mwongozo
      juzi Sheikh Ponda Issa ambaye ni katibu wa Jumuiya ya Kutetea Haki za Waislamu alitanabahisha kuwa iwapo serikali haitoweka kipengele cha dini katika fomu za sensa ya mwaka, jumuiya yao itahamasisha Waislamu wasishiriki katika zoezi la sensa.Alisema kuwa nchi hii siyo ya Kikristo lakini INATAWALIWA NA MFUMO KRISTO. alisema kutokana na mazoea, Waislamu wanabaguliwa katika mgawanyo wa keki ya taifa khasa upande wa ajira. ofisi na idara za serikali zinaongozwa na Wakristo kwa asilimia kubwa kulinganishwa na waislamu. alitoa mfano wa TRA, NECTA, Wizara ya Eimu, Wizara ya Ujenzi, Afya, Mahakama nk........... kwa mujibu wa Sheikh Ponda, wastani wa ajira ni karibu Wakristo 77% na Waisalmu siyo zaidi ya asilimia 20%. Licha ya hoja inayojengwa kuwa Waislamu hawajasoma lakini akasema waliosoma wapo. akatanabahisha kuwa kwa maslahi na umoja wa kitaifa, kupuuza watu ambao ni sehemu ya jamii ktk keki ya taifa ni jambo hatari sana! kwa kuwa wtu wanadai waislamu ni chini ya 20% katika nchi hii, akapendekeza sensa ya mwaka huu kiwekwe kipengele cha dini ili idadi ya watanzania kidini ijulikane. Kwa mujibu wa Sheihk Ponda, anaamini kuwa waislamu ni takriban 64% ya rais wa Tanzania. "SIYO SAHIHI WATU WENYE IDADI HII KUPUUZWA KATIKA UWIANO WA AJIRA SERIKALINI", alisema Sheikh Ponda.Alitoa mifano wa nchi karibia zote za Ulaya, Marekani, asia pamoja na Afrika, kipengele cha dili kipo kwenye fomu za sensa zao. "Ukisoma country profile au fact file uingiapo katika nchi mbalimbali, utakuta wameandika wastani wa idada ya raia kidini" alisisitiza Ponda. "Mbona mnajifanya kama hamtembei au hamjui kinacho endelea ulimwengunu jamani!" alilalama Ponda.HOJA YANGUNdugu znaguni Watanzania, tufike sehemu tuache ukweli udhihiri. kama Waislamu wanalalamika kuwa wanabaguliwa katika ajira labda kutokana na uchache wao, kwa nini suala la dini lisiwekwe wazi? au utakua udini? au uchochezi? au uvunjifu wa amani? kama ni hivyo, mbona karibu 98% ya sensa zote duniani zina kipengele cha dini!? je huko wameuana kutoakana na kipengele hicho? TUBADILIKE!!!!!!!!naomba kuwasilisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!! !!!!!!!!!!
      Naona hii habari yako umechanganya habari. Unataka kutuaminisha kuwa, kuhusu keki ya Taifa huwa inagawiwa kufuata dini? Pia unataka kutuaminisha kuwa Dini ndiyo interview ya kupata kazi? Badala ya kung'ang'ania kazi za upendeleo maalumu, ningeshauri watanzania tujikite kwenye elimu kisawasawa kwanza na kipigania mazingira ya elimu.
      Bigirita likes this.
      "Wisdom is not a product of schooling, but of the lifelong attempt to acquire it"

    4. #22
      Lokissa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Location : Goba
      Posts : 4,092
      Rep Power : 5807
      Likes Received
      1026
      Likes Given
      2876

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      tatizo la waislamu nadiriki kuwaita wengi ni vilaza
      kutwa kulalamika. niwaulize mkuu wa nchi ni nani, makamu wake, jaji mkuu???wakristo hao?
      wanataka wapewe mgawanyo sawa wa madaraka nani aliwaambia nchi hii ina dini? wanataka kutupeleka wapi?
      wao wanakaa vijiweni na kunywa kahawa na walikataa kusoma shule za wakristo eti ni makafiri sasa wanataka wapewe vyeo bila kusoma? wamuulize JK alisoma shule ya watu gani? angesoma madrasa na kuishia kunywa gahawa leo angekuwa rais?
      suala la ukabila na udini Nyerere alilikataa siku nyingi sana


      pili wakubali kwa Tanzania asilimaia 62 ni wakristo, 35 ni waislamu na 3% ni watu wa dini zingine. kwa hivo tukiamua leo wakristo hata kupiga kura bado tunaweza kuwapita kwa mengi na pia idadi kubwa ya wasomi ni wakristo, nakumbuka nikiwa chuo kati ya wanafunzi 240 darasani 40 tu ndi walikuwa waislamu. acheni kelele pelekeni wanenus shule.
      sijaona mantini ya wao kulalamika,
      katika kazi hatuajiriwi kwa kigezo cha udini wala ukabila bali ni elimu na ujuzi wako.
      You may know me but you have no Idea who I am !

    5. #23
      Mtanzania1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2010
      Location : Kalenga, Liringa
      Posts : 980
      Rep Power : 622
      Likes Received
      124
      Likes Given
      94

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Quote By sweke34
      Halafu wakokotoe kwenye idadi itakayopatikana ya watanzania wote ili wajue waislam ni roughly asilimia ngapi ya population ya tzii
      katika imani ya kiislam imebainisha wazi kuwa tofauti ya muislam na yule asiyekuwa muislam ni kuswali mara tano kwa siku......kwa hiyo kama wewe huswali basi wewe ujue siyo muislam....sasa kama tuna imani ya kweli ya dini sijui kama hii sensa itasaidia vipi kwa waislam wao binafsi nadhani sensa nzuri ya waislam wa kweli ifanyike misikitini japo nadhani haitakuwa sahihi kwani siyo lazima sana kuswali misikitini
      Ndahani likes this.
      Ukifanya jambo la werevu utaitwa mwerevu, ukifanya jambo la kijinga basi utaitwa mjinga pia

    6. #24
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,672
      Rep Power : 977
      Likes Received
      584
      Likes Given
      10

      Default

      Hizo takwimu zitakataliwa,watadai mfumo Kristo umezichakachua! Maana wamekua wanajidanganya kwamba wao ni wengi,bila kutumia akili tu ya kawaida kwamba ktk mikoa 10 yenye wakazi wengi Tanzania,takribani yote inakaliwa na Wakristo. Kwamba mikoa kama Pwani,Lindi na Mtwara ni kati ya mikoa yenye idadi ndogo ya watu ktk Tanzania!
      Quote By sweke34
      Halafu wakokotoe kwenye idadi itakayopatikana ya watanzania wote ili wajue waislam ni roughly asilimia ngapi ya population ya tzii

    7. #25
      MAMA POROJO's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd November 2007
      Posts : 4,858
      Rep Power : 1844
      Likes Received
      593
      Likes Given
      413

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Kauli ya Ponda inazungumzika kwa maslahi yetu zote bila kujali tunakubaliana naye au hatukubaliani naye si jambo la kututengenisha bali kujenga hoja kushawishi umuhimu na ubaya wa kuwa na kipengere cha dini katika sensa.
      mwongozo likes this.

    8. Miaka 50

    9. #26
      Ndahani's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 3rd June 2008
      Location : Somewhere
      Posts : 9,647
      Rep Power : 4016
      Likes Received
      2940
      Likes Given
      5063

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Quote By Mtanzania1
      katika imani ya kiislam imebainisha wazi kuwa tofauti ya muislam na yule asiyekuwa muislam ni kuswali mara tano kwa siku......kwa hiyo kama wewe huswali basi wewe ujue siyo muislam....sasa kama tuna imani ya kweli ya dini sijui kama hii sensa itasaidia vipi kwa waislam wao binafsi nadhani sensa nzuri ya waislam wa kweli ifanyike misikitini japo nadhani haitakuwa sahihi kwani siyo lazima sana kuswali misikitini
      Na wanaoua wenzao bila sababu yoyote nao inakuwaje? Siamini kama hao nao wanatimiza masharti ya dini. Maana kama kigezo ni hicho kimoja tu, watu watajipa uhalali wa kufanya hata mambo haramu na kuamini watafika kwa Mwenyezi Mungu....tafadhali nieleweshe mkuu
      We are all inventors, each sailing out on a voyage of discovery, guided each by a private chart, of which there is no duplicate. The world is all gates, all opportunities.
      Ralph Waldo Emerson

    10. #27
      NYARUGANDO's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 5th February 2012
      Posts : 4
      Rep Power : 0
      Likes Received
      0
      Likes Given
      0

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      hawa wenzetu huwa nakuwa na wasiwasi nao juu ya uwezo wao wa kufikiri

    11. #28
      Katufu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th May 2012
      Posts : 187
      Rep Power : 392
      Likes Received
      77
      Likes Given
      7

      Default

      Quote By mfumo
      ahsante mwongozo kwa taarifa hii.
      Nakufagilia sheikh ponda, hayo uliyosema ni kweli tupu. Nafurahi pia kusikia mkutano wa jana wa sensa dodoma waislamu wote pamoja na bakwata wamekubaliana kususia sensa ya mwaka august 2012 kama kipendele cha dini hakitakuwepo kwenye fomu ya sensa. Cha kushangaza zaidi maaskofu wao wanataka kipengele hicho kisiwepo ati kitahatarisha amani. Amani itaharibika vipi ikiwa tutajua idadi ya waislamu wangapi na wakristo wangapi? Maaskofu walishindwa kujibu swali hili!!!!!! What is behind the scene maaskofu??? Kuna jambo gani limejificha hapa mpaka hamtaki tujue idadi yetu kutokana na dini zetu?!!
      Acheni ulimbukeni ndugu, ikiwa mnataka kujua mko wangapi ili kudai uwiano katika ajira je na makabila, kwa mfano Wasukuma nao wadai hivyo? Wahaya na wachaga nao wadai uwiano wa kikabila? Ni mtu mbumbumbu asiyeweza kuona hatari mbele na kushabikia ujinga wa namna hii

    12. #29
      Kakubilo Kasota's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 14th March 2012
      Posts : 166
      Rep Power : 396
      Likes Received
      53
      Likes Given
      21

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Ninacho kiona kwa huyu Sheikh na wengine wenye mtazamo kama wake ni kutaka kila kitu cha dini yake kifanywe na serikali, mfano, wanasema Mahakama ya Kaadhi ni sehemu ya ibada yao lakini igharamikiwe na serikali, hivi inaingia akilini serikali igharamie ibada ya dini? mara uongozi uwe wa kuachiana, wa dini hi kipindi hiki na kipindi kingine dini nyingine, sasa hapa kuna mtego wanataka kuutega, issue hapa wanataka kujua Waislam wako wangapi? mi sidhani kama ni hii ni kazi ya serikali, hi ni kazi ya masheikh kama yeye, conduct your own Censor ili mjue mko wangapi? Ninahakika kama Kadinari Pengo anataka kujua kuna wakatoriki wangapi hapa nchini, ni yeye kuwasiliana na maaskofu wake ambao nao watashuka kwa mapadre then atajua tu wako wangapi, hali kadhalika Anglican, Lutheran Walokole kwa madheebu yao the same, hivi nyie waislam mnashindwa nini kufjua idadi yenu hadi serikali iwafanyie?

      Kigezo kwamba dini zingine zinafanyaje nadhani si issue, kuna serikali humu duniani zina sheria ya kuruhusu mashoga, je na siye tu copy toka kwao? kuna nchi waislam hawaruhusiwi kuvaa Hijabu, tukopi na hiyo pia? Hebu tuwe realistic na masuala common na muhimu kwa nchi yetu, umasikini ni mkubwa sana Tanzania ambao kimsingi haungalii dini ya mtu, tuwekeze nguvu zetu huko, mlitaka rais mwislam, naye mmempata then mnakuja na story nyingine, ninahakika mkikubaliwa hili na la Kaadhi, kesho mtasema kuhiji Makka ni ibada, serikali iwagharamikie.
      Jasusi, sosoliso and sweke34 like this.

    13. #30
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,625
      Rep Power : 2894
      Likes Received
      3845
      Likes Given
      12250

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Si kweli kwamba Marekani kwenye sensa wanahesabu ufuasi wa dini. Hicho kifungu kinachotaja dini ya mtu sijawahi kukiona.
      Bigirita, sweke34 and Power G like this.

    14. #31
      EDOMU's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 1st April 2012
      Posts : 9
      Rep Power : 361
      Likes Received
      0
      Likes Given
      6

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      hivi ktk ajira mliona mtu akiulizwa jina,au elimu na uwezo wake ndio vigezo!!
      kama dini fulani ina wasomi wachache kwenye soko wekezeni zaidi ktk elim=suluhisho la mda mrefu
      tatizo la watz tunapenda vitu vya haraka haraka na pia fanyeni sensa zenn misikitini,mahekaluni, matambikoni na makanisani
      napinga hoja za udini na ukabili ktk sensa

    15. #32
      Katufu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 8th May 2012
      Posts : 187
      Rep Power : 392
      Likes Received
      77
      Likes Given
      7

      Default

      Quote By Barubaru
      Kuna kitu kimejificha hapo.

      Mbona mkiwa mnatoa maelezo Polisi mnaandika sio tu kabila mpaka dini mnabainisha. Kwenye vitabu vya wageni hotelini na nyumba za kulala wageni mbona kunakipengele cha dini na kabila. Kwanini msikiweke hata kwenye sensa zenu.

      Nafikiri kiuchumi wanazuia kuona ni misada au misamaha ya kodi kiasi gani wanayopata dini moja dhidi ya zingine na kunufaika kwa namna gani kiuchumi dhidi ya wengine.

      Kuna mengi sana . Lakin msingi mkuu ni mipango ya nchi yenu kuweka usawa wa kitabaka na kijamii kwa kupata taarifa sahihi ndani ya sensa.
      Nadhani huko ulikotaja wanataka taarifa hizo ili kumtambua mtu iwapo tatizo lolote litatokea ili iwe rahisi kufahamu mgeni au mhalifu huyu ni nani hasa. Lakini katika mipango ya taifa hilo la dini na kabila halina mashiko hata kidogo

    16. #33
      NgomaNgumu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 20th November 2010
      Posts : 192
      Rep Power : 473
      Likes Received
      21
      Likes Given
      0

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Quote By Ndahani
      Barubaru,
      Kwani namba ya waamini wa dini yako, hata kama ni kubwa ina faida gani kwa uwepo na ustawi wa Taifa hili? Kama namba ni tija, waafrika tulivyo, tunaweza kuanzisha mashindano ya kuzaana bila utaratibu, bila kujua kwamba anayeongoza dunia ya leo sio kwamba ana namba kubwa, la hasha!!! Ana elimu, uwezo na ujuzi mkubwa.
      Ndio maana waisrael kwa idadi ni wadogo lakini pale walipo waliwahi kupigana na mataifa karibu yote yaliowazunguka kwa wakati mmoja na kuwashinda. It was not by chance....it was by design and intelligence to come with victory. So hoja hapa kwetu sisi wengine ni kuhakikisha generations zetu zina aim higher kwa kutafuta mambo ya msingi yatakayotusukuma huko. Sio haya mambo ya kujua nani ni dini gani! So what?
      Idadi ya watu ni muhimu ktk taifa lolote ujitaka kujua faida yake angalia China na inavyokuja juu kiuchumi. Resources zilizopo Tanzania zinaweza kutosha Africa nzima kama zikitumiwa vizuri na kukawa na ktk ugavi muhimu ni kujipanga tu. Kuhusu dini ni muhimu kujulikana kwa sababu karibi million

    17. #34
      Jasusi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th May 2006
      Posts : 10,625
      Rep Power : 2894
      Likes Received
      3845
      Likes Given
      12250

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Quote By Kakubilo Kasota
      Ninacho kiona kwa huyu Sheikh na wengine wenye mtazamo kama wake ni kutaka kila kitu cha dini yake kifanywe na serikali, mfano, wanasema Mahakama ya Kaadhi ni sehemu ya ibada yao lakini igharamikiwe na serikali, hivi inaingia akilini serikali igharamie ibada ya dini? mara uongozi uwe wa kuachiana, wa dini hi kipindi hiki na kipindi kingine dini nyingine, sasa hapa kuna mtego wanataka kuutega, issue hapa wanataka kujua Waislam wako wangapi? mi sidhani kama ni hii ni kazi ya serikali, hi ni kazi ya masheikh kama yeye, conduct your own Censor ili mjue mko wangapi? Ninahakika kama Kadinari Pengo anataka kujua kuna wakatoriki wangapi hapa nchini, ni yeye kuwasiliana na maaskofu wake ambao nao watashuka kwa mapadre then atajua tu wako wangapi, hali kadhalika Anglican, Lutheran Walokole kwa madheebu yao the same, hivi nyie waislam mnashindwa nini kufjua idadi yenu hadi serikali iwafanyie?

      Kigezo kwamba dini zingine zinafanyaje nadhani si issue, kuna serikali humu duniani zina sheria ya kuruhusu mashoga, je na siye tu copy toka kwao? kuna nchi waislam hawaruhusiwi kuvaa Hijabu, tukopi na hiyo pia? Hebu tuwe realistic na masuala common na muhimu kwa nchi yetu, umasikini ni mkubwa sana Tanzania ambao kimsingi haungalii dini ya mtu, tuwekeze nguvu zetu huko, mlitaka rais mwislam, naye mmempata then mnakuja na story nyingine, ninahakika mkikubaliwa hili na la Kaadhi, kesho mtasema kuhiji Makka ni ibada, serikali iwagharamikie.
      Sensa ya mwaka 1967 ilionyesha kuna wakristo wangapi, waislamu wangapi, na wapagani wangapi. Tunaweza kuanzia hapo. Mambo ya kuhesabu watu kwa dini zao hayana tija katika serikali ambayo haina dini.
      NtakuwaSikuchukui likes this.

    18. #35
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Naunga mkono hoja na Waislaam wote tususe sensa, kwani itakuwa nini? Amma waweke hicho kipengele halafu wakachezee kompyuta kama walivyofanya mitihani wa Waislaam amma sensa tuisusie.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    19. #36
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,672
      Rep Power : 977
      Likes Received
      584
      Likes Given
      10

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Akina Ponda wapo hata ktk nchi za Kiislamu,wengi wao wanaozea jela kwasababu ya kupandikiza chuki na mifarakano ktk jamii!

    20. #37
      Mtanzania1's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2010
      Location : Kalenga, Liringa
      Posts : 980
      Rep Power : 622
      Likes Received
      124
      Likes Given
      94

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Quote By Ndahani
      Na wanaoua wenzao bila sababu yoyote nao inakuwaje? Siamini kama hao nao wanatimiza masharti ya dini. Maana kama kigezo ni hicho kimoja tu, watu watajipa uhalali wa kufanya hata mambo haramu na kuamini watafika kwa Mwenyezi Mungu....tafadhali nieleweshe mkuu
      Mkuu nadhani hii inafanana na hapa.... http://www.jamiiforums.com/kenyan-po...ml#post4035837
      Ukifanya jambo la werevu utaitwa mwerevu, ukifanya jambo la kijinga basi utaitwa mjinga pia

    21. #38
      TWIZAMALLYA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st October 2011
      Location : NG'WAMAGUNGULI
      Posts : 392
      Rep Power : 464
      Likes Received
      69
      Likes Given
      155

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Quote By Mtanzania1
      Nadhani hii ni busara kwani muanisho huu wa kipengele cha dini ni muhimu hasa kukiwa na mipango inayohusu dini.. kama kujua tunahitaji kutenga ardhi kiasi gani kwa ajili ya misikiti/makanisa... au makaburi
      It doesn't make any sense

      No man can stand on top because he is put there.
      H.H. Vreeland



    22. #39
      mangikule's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 930
      Rep Power : 536
      Likes Received
      176
      Likes Given
      239

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Quote By mfumo
      ahsante mwongozo kwa taarifa hii.
      Nakufagilia sheikh ponda, hayo uliyosema ni kweli tupu. Nafurahi pia kusikia mkutano wa jana wa sensa dodoma waislamu wote pamoja na bakwata wamekubaliana kususia sensa ya mwaka august 2012 kama kipendele cha dini hakitakuwepo kwenye fomu ya sensa. Cha kushangaza zaidi maaskofu wao wanataka kipengele hicho kisiwepo ati kitahatarisha amani. Amani itaharibika vipi ikiwa tutajua idadi ya waislamu wangapi na wakristo wangapi? Maaskofu walishindwa kujibu swali hili!!!!!! What is behind the scene maaskofu??? Kuna jambo gani limejificha hapa mpaka hamtaki tujue idadi yetu kutokana na dini zetu?!!
      Na maaskofu walikuwepo kwenye mkutano wa waislamu? wakaulizwa juu kipengele hiki wakakataa wakasema KITAHATARISHA amani!! Kuna kazi!!

    23. FJM
      #40
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,179
      Rep Power : 2569
      Likes Received
      5331
      Likes Given
      4587

      Default Re: Sheikh Ponda yuko sahihi

      Baada ya mauaji ya kimbari Rwanda walijua hatari ya 'ukabila' kwenye mustakabali wa taifa. Wameondoa kipengele cha ukabila kwenye mambo mengi sana. Tanzania tunaweza tusiwe na tatiza la ukabila lakini 'udini' unaanza kutunyemelea na sasa watu kama Sheikh Ponda 'wanatumiwa' kupanda mbegu ya udini.

      Kwa maoni yangu mtu yoyote anayetaka kujua waaumini wa dini fulani wako wangapi basi afanye hayo na waumini husika. Serikali ya Tanzania ijishughulishe na watanzania (walio na dini na hata wale wasio na dini). Sheikh Ponda awafuate hao wafadhili wake wampe hela ya kuzunguka kila msikiti ili apate idadi ya waislam, au azunguke kila kanisa, temple na kupata idadi wa waumini. Lakini sio kutuelea hoja ambazo hazijaenda shule.

    Page 2 of 16 FirstFirst 123412 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...