Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

    Report Post
    Page 1 of 2 12 LastLast
    Results 1 to 20 of 31
    1. #1
      Nikupateje's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd December 2009
      Posts : 856
      Rep Power : 966
      Likes Received
      545
      Likes Given
      604

      Default Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Ujue ukweli wa kiapo cha mbunge, waziri

      MWEZI uliopita ulizuka ubishi magazetini na kwenye vyombo mbalimbali vya mawasiliano ukihoji mantiki ya mbunge kuapa na kuanza uwaziri kabla hajaapa ubunge. Sina hakika kama ubishi ule sasa utahamia bungeni kujadili viapo vile.
      Naanza kufafanua ninavyoelewa kwa kueleza historia ya ubunge.

      Mfumo wa sasa wa Bunge uliundwa na kusimikwa na Simon De Montfort, tajiri aliyeitawala Uingereza kimabavu kwa muda.

      Kabla yake, wafalme wa nchi hiyo walizoea kuwaita kwa msimu matajiri wa kwenye jamii (Lords) ili kusikia taarifa na ushauri wao.

      De Montfort alipochukua madaraka, alibadili mtindo huo. Januari 20, 1265 aliwaita matajiri (Lords) lakini pia akaamua kila eneo lichague watakaokuja kuwawakilisha masikini (Commons).

      De Montfort alifanya hivyo ili apendwe kuepusha chuki dhidi ya kitendo chake cha kumuondoa madarakani mfalme halali yaani Henry III.

      Mfumo aliousimika De Montfort, japo ulirikebishwa kidogo, umedumu hadi leo. Ni mfumo wa Bunge kuwa na mikusanyiko miwili. Mkusanyiko wa kwanza umeendelea kujumuisha wanaoteuliwa na mfalme au malkia, ukijulikana kama “Upper House”.

      Mkusanyiko wa pili ni wa watu waliochaguliwa na wananchi. Mkusanyiko huu huitwa “Lower House”.
      “Lower House” inajulikana kwa majina kadhaa kama vile House of Commons (Uingereza), Bundestag (Ujerumani), House of Representatives (Marekani).

      Wakati “Upper House” ina majina yafuatayo: House of Lords (Uingereza), Bundesrat (Ujerumani) na Senate (Marekani).
      Mikusanyiko yote miwili kwa pamoja ndiyo huitwa Bunge (Parliament). Mtindo huu wa Bunge kuwa na mikusanyiko miwili huitwa “Bicameral”. Wakati mataifa yenye Bunge lenye mkusanyiko mmoja huitwa “Unicameral”.

      Je, sisi tuna mabunge mawili (Bicameral) au moja (Unicameral)? Ni rahisi kujibu kuwa tuna Bunge la mkusanyiko mmoja tu, yaani ule wa kina John Mnyika, Anne Makinda na wenzao (National Assembly).

      Lakini katiba haisemi hivyo. Katiba inasema kwamba yenyewe haikutungwa na Bunge kama hili, bali imetungwa bunge jingine tunaloliita “Bunge Maalumu,” au (Constituency Assembly).
      Hivyo, katiba imetaja mabunge mawili, yaani “Bunge Maalum” (Constituency Assembly) na Bunge la Jamhuri (National Assembly).

      Wanaosita kutamka kwamba tuna mabunge mawili (Bicameral), inabidi wasaidie kufafanua sababu zao kwani binafsi sioni ibara ya Katiba inayoonyesha kuwa lile “Bunge Maalumu” limefutwa.
      Haitofautiani na kudhani kwamba Tanzania haina Mahakama Maalumu ya Katiba kwa sababu hatujawahi kuiona ikifanya kazi, wakati imetajwa kwenye ibara ya 125 hadi 128 ya Katiba.

      Ni vizuri kueleza matukio yaliyotokea England Machi 2, 1629 na Januari 5, 1642 wakati wa utawala wa Mfalme Charles I wa England.

      Machi 2, 1629, Charles I alinuia kuvunja bunge kwa sababu alishachoshwa na ubishi wabunge kubishia matakwa yake hasa matumizi ya pesa. Mtumishi wa mfalme ambaye hadi sasa anaitwa “Black Rod” akatumwa kuwafikishia wabunge taarifa hiyo.

      Wabunge wa kikundi cha John Eliot walijua mtumishi sasa anakuja kuwaita ili bunge livunjwe. Wakajua Spika kwa woga wake akitoka kitini basi maamuzi yao yatakuwa batili yaani hakuna Bunge.

      Hivyo, wabunge wakagawana majukumu. Wengine wakaenda kuubamiza mlango mbele ya yule mtumishi ili asiingie, na wengine wakakimbia hadi kwa Spika wakamshika kwa nguvu asiinuke kitini.

      Mlango ukiwa umefungwa na Spika akiwa amebanwa pale kitini wenzao wakatumia mwanya huo kupitisha maazimio matatu waliyoyataka, kisha wakamwachia Spika wakatawanyika.

      Januari 5, 1642 hali ikuwa ni tofauti, kwani Charles I hakutaka kuishia kumtuma mtumishi, bali pia aliamua sasa aingie kwa nguvu bungeni kuwakamata wabunge watano ambao ni vinara wa ubishi hasa John Pym.

      Mtumishi wake alipofika mlangoni wabunge wakaubamiza lakini askari wa mfalme wakagonga na kuingia kwa nguvu. Charles I hakufanikiwa kuwakamata John Pym na wenzake kwani walishatoroka.

      Kitendo cha Charles I kuvamia bungeni na kuvunja uhuru wa Bunge kilisababisha Waingereza wapigane vita vya wenyewe kwa wenyewe yaani askari wa Bunge na wa Mfalme.

      Lakini kiliifanya hiyo Januari 5, 1642 iwe ndiyo siku ya mwisho kwa mfalme au malkia wa Uingereza kukanyaga kwenye mkusanyiko wa House of Commons. Hotuba za uzinduzi wa Bunge za malkia au mfalme huzitoa akiwa House of Lords.

      Kitendo cha kuubamiza mlango hurudiwa hadi leo kila mara wabunge wanapoitwa kumsikiliza Mfalme au Malkia kule House of Lords. Waweza kukishuhudia kikifanywa mbele ya malkia Elizabeth II mwaka 2008 kwenye tovuti hii (www.youtube.com/watch?v=h1bJ8nY2pcc).

      Kwanini kitendo cha kuubamiza mlango mbele ya mtumishi wa mfalme kinaadhimishwa kwa miaka 383 sasa.
      Maana yake ni kwamba Bunge liko juu ya kila mtu hata kwa mkuu wa nchi yaani Mfalme au Malkia.

      Hivyo, ni kazi ya Mkuu wa nchi kuwabembeleza wabunge kufungua mlango tena mara tatu ndipo awaombe kwa heshima na taadhima kuja kujiunga na wenzao kumsikiliza.

      Hapa nchini, yapo mengi yanayohitajika ili mkusanyiko uwe ni kikao halali cha bunge. Ibara ya 146(2) ya Kanuni za Bunge inamtaka Spika avae joho lenye bendera ya Taifa akiwa kwenye shughuli za Bunge.

      “Siwa” ni lile rungu linalobebwa na askari anayeongoza msafara wa Spika kuingia Bungeni. Hii “Siwa” ni ishara ya mamlaka ya Bunge.

      “Siwa” isipokuwepo, basi mamlaka ya Bunge yanakosekana kwenye mkusanyiko uliokuwapo. Vikao vya kamati za Bunge hufanywa bila “Siwa”. Hivyo Kamati hizo si shughuli ya Bunge.

      Nimerudia maneno “Shughuli za Bunge” hivyo nalazimika kuyafafanua. Ibara ya 89(2) ya Katiba inasema “Shughuli za Bunge” ni zile za ndani ya Bunge tu, na wala si za kamati, si za kamati ndogo wala si zile za Ofisi ya Bunge.

      Maneno haya “Shughuli za Bunge” yanajirudia tena kwenye Ibara ya 68 inayomtaka mbunge kuapa kabla ya kuanza kushiriki “Shughuli za Bunge”.

      Kwa mamlaka ya ibara ya 46A ya Katiba, Bunge lina uwezo wa kumshitaki Rais aliyeko madarakani. Utaratibu wa kumshtaki Rais unamtaka Spika kuunda Kamati Maalumu ya Uchunguzi wa Mashtaka dhidi ya Rais (Ib. 46A(4)). Mwenyekiti wa Kamati hii ni Jaji Mkuu wa Tanzania, na mjumbe mmoja ni Jaji Mkuu wa Zanzibar.

      Kitendo cha Kamati ya Bunge kuongozwa na Jaji Mkuu, ni mfano mzuri kuonyesha kwamba Kamati si “Shughuli ya Bunge” na inaweza kuhudhuriwa na hata kuongozwa na asiye mbunge.

      Sasa tujadili aina mbili za viapo yaani Kiapo cha Uaminifu na Kiapo cha Ofisi. Viongozi wakuu wa mihimili ile mitatu Bunge, Serikali na Mahakama huapa viapo vyote viwili wanapokabidhiwa zao. Inaelekea kwamba kile kinachoitwa Kiapo cha ofisi katiba haikitamki kama Kiapo cha ofisi. Badala yake yapo maneno mengi yasemayo (Kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake).

      Wingi wa maneno haya umewachanganya hata wataalam hadi kusema labda hicho ’Kiapo kingine’ ndicho kile mawaziri wanachotakiwa kuapa siku wanayoingia Bungeni. Kwa kudhani hivyo hisia zilionekana zikihoji kwamba inawezekana ilikuwa ni makosa kuwaapisha wabunge kuwa mawaziri kabla ya hicho kiapo kingine.

      Je, mtu anakuwa mbunge siku anapotangazwa au siku anapoapa? Mbunge akishatangazwa tayari ni mbunge, maana hakuna wa kutugeuza tusimpende.

      Lakini, sheria yaani katiba inamfanya kuapa kwake bungeni kumpatie uhalali wa kushiriki “Shughuli za Bunge”.
      Je, kwani lazima mbunge aende bungeni Dodoma? Mbona anaweza kubaki jimboni akawa anachimba visima au akanunua magari ya zahanati au akajenga shule kwa wanajimbo wake?

      Tumeona kwamba shughuli inayofanyika bila lile rungu la Spika, si “Shughuli ya Bunge”. Kitendo cha mbunge kununua gari la zahanati au kusomesha yatima ni uhisani kama uhisani wowote. Si “Shughuli ya Bunge” kikatiba wala kihistoria duniani.

      Mbunge akiendelea na huo uhisani wake, tena hata akadiriki kuigharimikia bajeti ya nchi nzima lakini asikanyage bungeni kwa mikutano mitatu mfululizo, basi atapoteza ubunge wake kwa uzembe yaani utoro kama walivyodai Zitto alipoanza kutosaini fomu za mahudurio bungeni.

      Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Spika, Mbunge wote hawa wanaapa kiapo cha uaminifu kwa sababu wanautumikia umma kwa nyadhifa walizokabidhiwa.

      Kwa nini mtu akiteuliwa kuwa Waziri anaapa tena kiapo cha uaminifu pale Ikulu wakati alishaapa bungeni?
      Bungeni, mbunge anautumikia umma kwenye mhimili mmoja (Legislature). Wizarani, waziri anautumikia umma kwenye mhimili mwingine (Executive). Kule Mahakamani Jaji Mkuu anautumikia umma kwenye mhimili wa tatu (Judiciary).

      Hivyo, mawaziri wale walioteuliwa hivi karibuni ubunge na uwaziri ndani ya saa 24 waliapa kiapo cha uaminifu, ili wautumikiea umma kwenye mhimili wa utendaji, yaani ule uwaziri wake.

      Hivyo, tuwatarajie kuanzia keshokutwa waape kiapo cha uaminifu, lakini sasa kwenye mhimili wa uwakilishi.
      Kwa nini mbunge haapi mara mbili pale bungeni kama Spika? Wala si kama Spika tu. Viongozi wakuu wengi wa ile mihimili mitatu huapa viapo hivi viwili.

      Kwa nini sasa mbunge haapi kiapo cha ofisi? Kwani hana ofisi? Katiba imetaja majukumu ya viongozi watano : Rais (Ibara. 33-37), Makamu wa Rais (Ibara. 47-48), Waziri Mkuu (Ibara. 52), Waziri (Ibara. 58), Jaji Mkuu (Ibara. 119)}.
      Katika ibara zote hizo 40, hakuna hata moja inayotaja majukumu au madaraka ya Mbunge. Badala yake, ibara ya 63 na 64 imetaja na kufafanua majukumu ya mkusanyiko mzima unaoitwa Bunge.

      Kumbe, kila kinachotamkwa au kuulizwa au kuamriwa mle bungeni, kikipita bila kipingamizi basi katiba inatufundisha tutamke kwamba (“...Bunge limesema hivi...”) au (“...Bunge limeazimia hivi...”). Katiba inatufundisha hivyo hata kama mzungumzaji mkuu alikuwa ni mmoja tu kati ya wabunge wote zaidi ya 350.

      Kwa maelezo haya mle bungeni panatakiwa uangalifu wa hali ya juu, kwani yanayojadiliwa, yanayoulizwa, yanayoamriwa pale ni ya bunge zima. Kama ni mafanikio yanakuwa ya Bunge zima. Kama ni lawama litupiwe Bunge zima.

      Nawatakia heri wabunge wapya watakaoapa siku yoyote kuanzia keshokutwa. Pia nalitakia heri Bunge zima katika mjadala mzima wa bajeti.

      *********************

      Source: Tanzania Daima
      Date: June 10, 2010 (Sunday)
      Website: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=36836
      zomba, MpendaTz and KOMBESANA like this.
      .."ni heri Dr. Willibrod Slaa ashinde na aingie Ikulu, kuliko Tundu Lissu kushinda ubunge na kuingia Bungeni"......Jakaya Mrisho Kikwete, Oct. 2010.

    2. RukaaJuu Final

    3. Paw
      #2
      Paw's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 1,549
      Rep Power : 2844
      Likes Received
      620
      Likes Given
      2129

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapat tena leo.

      Nimesoma kwa kusaka elimu mpya hapo.
      Nachelea kukuamini maana unataka tuamini kwamba shughuli za Bunge ni zile ulizofafanua wewe na si zilizoainishwa kwenye mkusanyiko wa Ibara za Katiba.

      Ni kweli Ibara za 63 pamoja na ile ya 64 zimeainisha madaraka ya Bunge ambayo ndiyo kwa tafsiri sahihi yanatengeneza shughuli zote za Bunge.

      Inaposemwa Kuisimamia na kuishauri serikali Ibara 64 (2), (3) ni wazi kwamba Bunge limetumia Ibara ya 89 (1), (2) (ambayo umejitahidi kuipotosha) kutunga sheria (kanuni za kudumu) namna ya kutekeleza hayo madaraka. Labda Katiba niliyosoma mimi imechapwa kwa makosa ya kisarufi... Nanukuu Ibara ya 89
      89. Kanuni za Kudumu za Bunge Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 14

      (1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.

      (2) Kanuni za Kudumu zilizotungwa kwa mujibu wa ibara hii zaweza kuweka utaratibu wa kusimamia utekelezaji wa shughuli za Sekretarieti ya Bunge na pia utekelezaji wa shughuli za Bunge ndani ya Bunge na zile za kamati na kamati ndogo za Bunge.
      , Hivyo katika kutekeleza madaraka yake Bunge limeweka kanuni za kudumu zinazoweka maelekezo jinsi ya ushiriki na mipaka ya Wabunge kutekeleza Ibara za 63 na 64.

      Hivyo ni wazi kwamba Uwaziri ni kazi inayohusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge ambapo kikatiba Waziri ni LAZIMA atokane na WABUNGE. na mbunge yeyote anahuishwa kwa KIAPO kabla ya kushiriki shughuli za Bunge. hili tunaliona kwenye Ibara ya 68 ya Katiba kama ninavyonukuu hapa
      68. Kiapo cha Wabunge Sheria Na. 15 ya 1984 ib. 13

      Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa.
      Hapo kwenyer bold ni exception (nafuu) yake. Hivyo shughuli pekee ya mbunge mteule anayoruhusiwa kuifanya ni kumchagua Spika pekee ambaye baadaye wabunge watakuja kuapa kwake. Naamini wadau wanafahamu nini maana na aina ya wabunge wa Bunge letu la jamhuri ambapo hakuna mahala popote kwenye katiba, Sheria hata kanuni panapoelekeza kwamba aina fulani ya wabunge wataanza mjukumu yao ya kibunge MARA MOJA! bila ya kuapa kwanza.

      Ni wazi kwenye suala la Mawaziri kuapishwa na kuanza kushiriki shughuli za Bunge ni ukiukwaji wa Katiba.


      Nimewajibika kuliweka sawa hili kwa mtazamo wangu na uelewa wangu kwa kuwa katika maongozi au utawala aina yeyote ni budi kuwa makini na uangalifu wa hali ya juu kutekeleza makubaliano ya pamoja (Katiba, Sheria na kanuni) kwa manufaa ya walio wengi....
      MpendaTz and KOMBESANA like this.
      (BADILIKA, bofya hapa ===> ####)

    4. #3
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 769
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapat tena leo.

      Quote By Paw
      Nimesoma kwa kusaka elimu mpya hapo.
      Nachelea kukuamini maana unataka tuamini kwamba shughuli za Bunge ni zile ulizofafanua wewe na si zilizoainishwa kwenye mkusanyiko wa Ibara za Katiba.

      Ni kweli Ibara za 63 pamoja na ile ya 64 zimeainisha madaraka ya Bunge ambayo ndiyo kwa tafsiri sahihi yanatengeneza shughuli zote za Bunge.

      Inaposemwa Kuisimamia na kuishauri serikali Ibara 64 (2), (3) ni wazi kwamba Bunge limetumia Ibara ya 89 (1), (2) (ambayo umejitahidi kuipotosha) kutunga sheria (kanuni za kudumu) namna ya kutekeleza hayo madaraka. Labda Katiba niliyosoma mimi imechapwa kwa makosa ya kisarufi... Nanukuu Ibara ya 89 , Hivyo katika kutekeleza madaraka yake Bunge limeweka kanuni za kudumu zinazoweka maelekezo jinsi ya ushiriki na mipaka ya Wabunge kutekeleza Ibara za 63 na 64.

      Hivyo ni wazi kwamba Uwaziri ni kazi inayohusu utekelezaji wa maazimio ya Bunge ambapo kikatiba Waziri ni LAZIMA atokane na WABUNGE. na mbunge yeyote anahuishwa kwa KIAPO kabla ya kushiriki shughuli za Bunge. hili tunaliona kwenye Ibara ya 68 ya Katiba kama ninavyonukuu hapa

      Hapo kwenyer bold ni exception (nafuu) yake. Hivyo shughuli pekee ya mbunge mteule anayoruhusiwa kuifanya ni kumchagua Spika pekee ambaye baadaye wabunge watakuja kuapa kwake. Naamini wadau wanafahamu nini maana na aina ya wabunge wa Bunge letu la jamhuri ambapo hakuna mahala popote kwenye katiba, Sheria hata kanuni panapoelekeza kwamba aina fulani ya wabunge wataanza mjukumu yao ya kibunge MARA MOJA! bila ya kuapa kwanza.

      Ni wazi kwenye suala la Mawaziri kuapishwa na kuanza kushiriki shughuli za Bunge ni ukiukwaji wa Katiba.


      Nimewajibika kuliweka sawa hili kwa mtazamo wangu na uelewa wangu kwa kuwa katika maongozi au utawala aina yeyote ni budi kuwa makini na uangalifu wa hali ya juu kutekeleza makubaliano ya pamoja (Katiba, Sheria na kanuni) kwa manufaa ya walio wengi....
      Kama wewe umesoma na wengine tumesoma. Ungekuwa mtetezi wa ukweli usingeficha facts kadhaa. Hukuongelea kabisa kuhusu Jaji Mkuu na Jaji wa Zanzibar kuongoza kamati ya Bunge kwa maana ya kwamba wao si wabunge na hivyo Kamati si kazi ya Bunge.

      Kazi ya Bunge ni ile ambayo mace ipo mbele ya kila mmoja. Mace ni fimbo ambayo mwandishi kaieleza kwamba inaitwa "Siwa".

      Soma vizuri katiba na changia kila hoja iliyoletwa usiache zingine ili ku-tune maana yako.
      MpendaTz, Kieleweke and Kisanduku like this.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    5. #4
      Kisanduku's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th July 2009
      Posts : 65
      Rep Power : 516
      Likes Received
      9
      Likes Given
      10

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Huhitaji kuapa kufanya shughuli yoyote kama kwenda ofisini kwa Spika. Huhitaji kuapa ili kushiriki Kamati ya Bunge.

      Unahitaji kuapa kusimama mbele ya "mace" maana hiyo ndiyo shughuli pekee ya Bunge na inafanyikia Bungeni tu huku Spika akiwa na joho lake.

      Kama "mace" haipo basi hiyo si shughuli ya Bunge na haina mamlaka ya Kibunge. Ndiyo maana hata uchaguzi wa kumchagua Spika huitwa kamati ya uchaguzi wa SPika.

      Kamati ni kamati haiwi bunge ata siku moja. Tumeona Kamati zikifanyia kazi zake hata nje ya nchi. Tumeona kamati ya Lowasa ikienda hadi Japan. TUliona Kamati ya RICHMOND ikisafiri hadi Marekani.

      Kazi ya Kamati ni kurahisisha mjadala itakapoleta taarifa pale Bungeni wakati "mace" ikiwepo.

      NIlipoacha hoi ni kutambua kwamba kumbe kuna kamati za Bunge zinaweza kuongozwa na hata wasio wabunge. Jaji Mkuu kuongoza Kamati ya Bunge inatosha kumaliza ubishi huu.

      Kumbuka Jaji Mkuu ni mtu wa Mhimili mwingine kabisa yaani hayumo serikali wala hayumo Bungeni. Lakini anakuwa mwenyekiti wa Kamati. Sikuwa nafahama hilo na niliposoma nilishani tumedanganyw aikabidi nihakikishe ndani ya katiba.

      Hizi ndizo subject tunazotakiwa tujadili humu JF.
      MpendaTz and KOMBESANA like this.

    6. #5
      Kisanduku's Avatar
      Member Array
      Join Date : 9th July 2009
      Posts : 65
      Rep Power : 516
      Likes Received
      9
      Likes Given
      10

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapat tena leo.

      Katiba ibara ya 89 (1) inasema hivi:
      Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii Bunge laweza kutunga Kanuni za Kudumu kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kutekeleza shughuli zake.
      ********

      Ni kweli bunge linaweza kuweka utaratbu wa kutimiza shughuli zake. Kumbuka kwamba utaratibu inaouweka si lazima uwe wa ndani ya vikao vya Bunge ambazo ndizo shughuli za Bunge.

      Utaratibu kuwekwa na Bunge si lazima uwe shughuli ya Bunge wakati wa kuukamilisha.

      Hata ikiwa vipi, mwiho wa siku huo unaouita utaratibu hauwezi kuishi huko nje. Ni lazima uletwe kama hoja Bungeni ujadiliwe na Bunge zima na huo mjadala ndiy shughuli ya Bunge kwa sababu yupo Spika kavaa joho, quoram ya wabunge imetimia na kikubwa kuliko yote "mace" ipo kuonyesh kwamba kinachofanyika ni shughuli ya Bunge na ina mamlaka ya Bunge.

    7. Miaka 50

    8. Paw
      #6
      Paw's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 1,549
      Rep Power : 2844
      Likes Received
      620
      Likes Given
      2129

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      ...utetezi nje ya vifungu vya katiba.

      Ni wazi kwamba hapa kinachotetewa ni KOSA lililofanyika kwa makusudi mazima ambapo tafsiri yake ni DHARAU dhidi ya Katiba iliyopo.

      Elewa kwamba kuna Kamati za KUDUMU za Bunge ambazo ndizo haswaa tunazoziunganisha kikatiba katika sehemu za shughuli za Bunge.

      Ukweli usipindishwe kwa maneno ya kuokoteza.

      Labda mnifafanulie hapa kisheria kuhusu majukumu (kazi, shughuli na madaraka) ya Bunge kwa undani ili isije ikawa tunaongea vitu tofauti na mada
      TIMING, MpendaTz and Kieleweke like this.
      (BADILIKA, bofya hapa ===> ####)

    9. #7
      Kieleweke's Avatar
      Member Array
      Join Date : 23rd June 2009
      Posts : 79
      Rep Power : 520
      Likes Received
      8
      Likes Given
      12

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Quote By Paw
      ...utetezi nje ya vifungu vya katiba.

      Ni wazi kwamba hapa kinachotetewa ni KOSA lililofanyika kwa makusudi mazima ambapo tafsiri yake ni DHARAU dhidi ya Katiba iliyopo.

      Elewa kwamba kuna Kamati za KUDUMU za Bunge ambazo ndizo haswaa tunazoziunganisha kikatiba katika sehemu za shughuli za Bunge.

      Ukweli usipindishwe kwa maneno ya kuokoteza.

      Labda mnifafanulie hapa kisheria kuhusu majukumu (kazi, shughuli na madaraka) ya Bunge kwa undani ili isije ikawa tunaongea vitu tofauti na mada

      Mkuu,

      Nakuomba uongee kidogo kuhusu Jaji Mkuu na Jaji wa Zanzibar kuongoza kamati ya Bunge.

      Maana yake ni kwamba Bunge linaweza kutengeneza kanuni inayoruhusu hata wewe uwe mwenyekiti wa Kamati ya Bunge.


      Kazi ya kutunga Kanuni hiyo ni ya Bunge na inafanywa “mace” ikiwepo. Lakini Kamati utakayoongoza haina nguvu au mamlaka ya kibunge.

      Umeuliza kuhusu mamlaka ya Bunge. Mamlaka ya Bunge ni kutunga sheria, kuiuliza serikali. Haya yameainishwa kwenye katiba ambayo najua unaijua.

      Unaweza kusema mbona Kamati zinamuuliza Waziri. Hakuna Kamati inayofanya kazi zake halafu uamuzi wake ukawa wa mwisho. Kamati zote hata kama zimefanya utafiti mzuri kiasi gani, bado inabidi ipeleke findings zake pale Bungeni ili wabunge watoe maamuzi ya mwisho kukiwa kuna “mace”.

      Maana ya “mace” imo kwenye ibara ya 3 ya Kanuni za Bunge kama ifuatavyo:
      Siwa” ni rungu la dhahabu linalotumika kama kielelezo cha mamlaka ya Bunge ambalo hubebwa na Mpambe wa Bunge akimtangulia Spika wakati wa kuingia na kutoka kwenye Ukumbi wa Bunge kabla na baada ya kikao cha Bunge;

      Hivyo, kikao ambacho hakina “siwa/mace” mbele yake hicho si kikao cha Bunge. Unaweza kukiita Kamati au vyovyote. Na ndiyo maana hata uchaguzi wa SPika hufanywa kwenye kikao kama hiki ambacho hakina “mace”.

      Ukiju maana ya “mace” utamaliza ubishi wote. Vinginevyo tutabishana hadi asubuhi.

      Narudia, uku-comment, tueleze kidogo, unaelewaje kuhusu Kamati ya Bunge kuongozwa na Jaji Mkuu.
      MpendaTz likes this.

    10. #8
      PMNBuko's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th December 2010
      Posts : 907
      Rep Power : 607
      Likes Received
      120
      Likes Given
      28

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Mmh, mpita njia tu...
      ".....development is the growth of thoughts....." Yes. We can!!

    11. #9
      Njoka Ereguu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 7th April 2012
      Posts : 503
      Rep Power : 459
      Likes Received
      167
      Likes Given
      30

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Shule nzuri sana hii kwangu, i real liked it and encourange this kind of topics
      KOMBESANA likes this.

    12. #10
      Ditto's Avatar
      Member Array
      Join Date : 30th August 2010
      Location : Johannesburg, South Africa
      Posts : 50
      Rep Power : 453
      Likes Received
      23
      Likes Given
      40

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Ni wakati gani hasa mtu anatambulika kama mbunge? wakati ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi au wakati ameapa mbele ya spika? Tukishajua hilo, hapo ndio tutaweza kukitegua kitendawili cha hao mawaziri maana wanatakiwa wachaguliwe kati ya wabunge(ambao wanatambulika kisheria).
      KOMBESANA likes this.

    13. #11
      Kilasara's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 21st December 2008
      Posts : 538
      Rep Power : 638
      Likes Received
      89
      Likes Given
      137

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Quote By Ditto
      Ni wakati gani hasa mtu anatambulika kama mbunge? wakati ametangazwa na msimamizi wa uchaguzi au wakati ameapa mbele ya spika? Tukishajua hilo, hapo ndio tutaweza kukitegua kitendawili cha hao mawaziri maana wanatakiwa wachaguliwe kati ya wabunge(ambao wanatambulika kisheria).
      Wakati Msimamizi wa Uchaguzi anapotangaza mgombea Ubunge ameshinda, anatamka pia hapo hapo kuwa huyo ni Mbunge wa Jimbo hilo. Pia Rais anaweza kikatiba Kumteua mtu kuwa Mbunge, na anakuwa Mbunge kuanzia hapo. Rais hawezi kumteua mtu kuwa Waziri kabla mtu huyo hajawa Mbunge kwanza: wa kuchaguliwa au wa kuteuliwa.
      MpendaTz, KOMBESANA and Ditto like this.

    14. #12
      KOMBESANA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2009
      Posts : 525
      Rep Power : 611
      Likes Received
      114
      Likes Given
      1485

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      kweli hii ni shule!shukrani kwa kutufungua mawazo hata kama maswali bado ni mengi.katika ulimwengu wa firka mmetuelekeza kiasi kwamba anayetaka kutambua zaidi aendelee kusoma,kuuliza,kutafiti,kuchun guza na kuhoji ili akili zetu zikue

    15. #13
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,659
      Rep Power : 717
      Likes Received
      291
      Likes Given
      36

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Na hata kama angekosea ungemfanyanini Rais yupo juu ya sheria?
      Paw likes this.

    16. Paw
      #14
      Paw's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 1,549
      Rep Power : 2844
      Likes Received
      620
      Likes Given
      2129

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Quote By Kieleweke
      Mkuu,

      Nakuomba uongee kidogo kuhusu Jaji Mkuu na Jaji wa Zanzibar kuongoza kamati ya Bunge.

      Maana yake ni kwamba Bunge linaweza kutengeneza kanuni inayoruhusu hata wewe uwe mwenyekiti wa Kamati ya Bunge.....
      Mkuu labda nikueleweshe kwa mifano inayoishi..

      Katika mfumo wa Asasi nyingi kuna kipengele muhimu cha Mikutano ya ASASI ambapo mengi yameainishwa mule.

      Tuangalie kwenye hii mikutano, utakuta mfumo wa ASASI (Katiba) umeweka mkutano mkuu wa wadau wa asasi husika na utaratibu na washiriki wake ni obvious. Ila kuna kipengele cha mkutano wa dharura ambapo hutambulika kama kikao/ mkutano halali lakini huwa haupo kwenye ratiba za kalenda za asasi.

      Hivyo suala la Jaji Mkuu, au hata mimi kuingia na kuongoza kamati za Bunge ni suala la extraordinary na siyo kwa ratiba iliyowekwa rasmi.

      Tunashuhudia kwamba suala la uwajibikaji limeachwa kwa kada ya chini ambapo zimetungwa sheria na kanuni mbalimbali endapo kutakuwepo na ukiukwaji wa taratibu zilizopo. Ila WAKUBWA wanapoamua kupindisha ama kukiuka taratibu huwa kunatumika utaratibu wa kutetea makosa hayo na KUYAPOTEZEA...
      MpendaTz likes this.
      (BADILIKA, bofya hapa ===> ####)

    17. #15
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 769
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default

      Quote By Paw
      Mkuu labda nikueleweshe kwa mifano inayoishi..

      Katika mfumo wa Asasi nyingi kuna kipengele muhimu cha Mikutano ya ASASI ambapo mengi yameainishwa mule.

      Tuangalie kwenye hii mikutano, utakuta mfumo wa ASASI (Katiba) umeweka mkutano mkuu wa wadau wa asasi husika na utaratibu na washiriki wake ni obvious. Ila kuna kipengele cha mkutano wa dharura ambapo hutambulika kama kikao/ mkutano halali lakini huwa haupo kwenye ratiba za kalenda za asasi.

      Hivyo suala la Jaji Mkuu, au hata mimi kuingia na kuongoza kamati za Bunge ni suala la extraordinary na siyo kwa ratiba iliyowekwa rasmi.

      Tunashuhudia kwamba suala la uwajibikaji limeachwa kwa kada ya chini ambapo zimetungwa sheria na kanuni mbalimbali endapo kutakuwepo na ukiukwaji wa taratibu zilizopo. Ila WAKUBWA wanapoamua kupindisha ama kukiuka taratibu huwa kunatumika utaratibu wa kutetea makosa hayo na KUYAPOTEZEA...
      Bunge siyo assasi (institution). Bunge ni mkusanyiko (Assembly).

      Jaji kuwa m/kiti wa kamati si dharura. Ni deliberate plan imo ndani ya katiba
      MpendaTz likes this.

    18. Paw
      #16
      Paw's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 1,549
      Rep Power : 2844
      Likes Received
      620
      Likes Given
      2129

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Quote By SubiriJibu
      ....Jaji kuwa m/kiti wa kamati si dharura. Ni deliberate plan imo ndani ya katiba
      Hayo ni matakwa ya KATIBA. Je katiba hiyo hiyo inaruhusu waziri kuapishwa kabla ya kiapo cha ubunge?

      A plain truth hapa ni kwamba Serikali kwa ukuu wake imekiuka vipengele vya katiba hasa kwa kumshauri vibaya rais kuhusu kuwaapisha mawaziri ambao si wabunge.

      Kuapa kwao jana hakuondoi kosa lililofanyika awali. Ni mfano mbaya usiopaswa kuigwa
      MpendaTz likes this.
      (BADILIKA, bofya hapa ===> ####)

    19. #17
      kijonjolow's Avatar
      Member Array
      Join Date : 14th April 2012
      Posts : 23
      Rep Power : 362
      Likes Received
      4
      Likes Given
      20

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Haya ndio mawozo uzamifu katika hoja kwa na wengine ni shule tosha na iwapo mtu anabisha basi ajenge hoja kama ulivyoweza kuchambua kwa hili raisi hakukosea kabisa kabisa!!!!
      SubiriJibu and Paw like this.

    20. #18
      SubiriJibu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th June 2009
      Posts : 270
      Rep Power : 769
      Likes Received
      192
      Likes Given
      163

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Quote By Paw
      Hayo ni matakwa ya KATIBA. Je katiba hiyo hiyo inaruhusu waziri kuapishwa kabla ya kiapo cha ubunge?

      A plain truth hapa ni kwamba Serikali kwa ukuu wake imekiuka vipengele vya katiba hasa kwa kumshauri vibaya rais kuhusu kuwaapisha mawaziri ambao si wabunge.

      Kuapa kwao jana hakuondoi
      kosa lililofanyika awali. Ni mfano mbaya usiopaswa kuigwa
      Moderators,
      Naomba mnipige life ban iwapo huyu Paw akinitajia kifungu cha katiba kinachomkataza Rais kuwaapisha kama alivyofanya.
      Paw likes this.
      ...Kanisa halijawahi kumtuhumu Dr. Slaa kwa wizi wa hela za ujio wa Papa...{Jude Thaddaues O.F.M. Cap, Archbishop of Mwanza and President of Tanzania Episcopal Conference (TEC), March 20, 2012}

    21. #19
      Mamndenyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 12,136
      Rep Power : 31825
      Likes Received
      6021
      Likes Given
      19619

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Hapa panahitaji umakini kwenye kusoma hii.

    22. Paw
      #20
      Paw's Avatar
      Super Moderator Array
      Join Date : 14th November 2010
      Posts : 1,549
      Rep Power : 2844
      Likes Received
      620
      Likes Given
      2129

      Default Re: Rais hakukosea kuwateua wabunge na hapohapo kuwapa Uwaziri. Wameapa tena leo.

      Quote By SubiriJibu
      Moderators,
      Naomba mnipige life ban iwapo huyu Paw akinitajia kifungu cha katiba kinachomkataza Rais kuwaapisha kama alivyofanya.
      Mkuu wala usijiapize kwa suala hili.
      Kwanza weka majibu ya swali langu hilo hapo chini kabla sijajibu la kwako
      Quote By Paw
      Hayo ni matakwa ya KATIBA. Je katiba hiyo hiyo inaruhusu waziri kuapishwa kabla ya kiapo cha ubunge?
      (BADILIKA, bofya hapa ===> ####)

    Page 1 of 2 12 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...