Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

    Report Post
    Page 5 of 7 FirstFirst ... 34567 LastLast
    Results 81 to 100 of 127
    1. #1
      salisalum's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th October 2010
      Posts : 312
      Rep Power : 504
      Likes Received
      68
      Likes Given
      4

      Default Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Tuko hapa kwenye kutoa heshima za mwisho kwa Kiongozi aliyetukuka mwanamaendeleo Bob Nyanga Mohammed Makani. MC alitoa nafasi kwa mwakilishi wa CCM kutoa rambirambi. Akainuka Mkama akazoza kama kawaida yake. Anasema Marehemu makani alikuwa mtu safi na mwenye hekima, kama Chadema wangefuata mfano wake ingekuwa vizuri sana. Halafu akasema umakini na umahiri wake unathibitishwa na ukweli kwamba Makani aliweza kufanikiwa kuwa Katibu Mkuu miongoni mwa watu tisa waliotoka kanda moja ya nchi hii. Yaani kwamba pamoja na ukanda bado Makani aliweza kuchaguliwa kuwa katibu mkuu. Mkama alitaka wana msiba tuingie kwenye mambo ya kisiasa na kutuaminisha kuwa Chadema ni chama cha ukanda na ukabila.

      Mwenyekiti Mbowe kwa utulivu na hekima ya hali ya juu, wakati wa zamu yake alitoa ufafanuzi wa kurekebisha kauli hiyo akisema, ''Mdomo huumba, si vema kauli hiyo iachwe hivi hivi bila kurekebishwa''. Mbowe alianza kutaja mtu mmoja mmoja kwa wale waanzilishi wa Chadema waliokuwepo siku ile ya kumpata katibu mkuu. Ilikuwa orodha ndefu kwa kweli, katika orodha hiyo walioonekana kutoka kanda ya kaskazini walikuwa ni Mzee Mtei, Mzee Kimesera na yeye Mbowe wakati huo akiongoza vijana.

      Mkama ametia aibu sana kwanza kugeuza mahali pa msiba pawe pa malumbano ya kisiasa, pili alikuwa amevaa kofia ya kihuni kwenye hafla ya heshima na ibada kama hii, tatu kusema uongo, Nne kamdhalilisha Rais Kikwete ambaye zamu yake ilipofika yeye hakutaka kujiingiza kwenye ujinga wa katibu wake. Yeye amesema, ''Hapa ni mahali pa msiba, tumekuja kuwapa pole wafiwa na kuwaombea subira''.

      Ninashauri CCM katika uchaguzi wao mkuu wafikirie kupata mtu mwenye hekima atakayeweza kubeba dhamana ya chama badala ya kubeba aibu ya chama. Vinginevyo tutaamini kuwa Chama chetu hakiwezi tena kuaminika kupewa dhamana ya kuongoza nchi. IMEKUWA AIBU SANA.
      Jasusi, kiraia, Shwari and 15 others like this.

    2. #81
      MANGUNGO's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 30th August 2011
      Posts : 1,161
      Rep Power : 0
      Likes Received
      254
      Likes Given
      14

      Default

      Quote By Bitabo View Post
      Hawa nape na Mukama ni mtu na kaka yake. Huo chini ni ujumbe wa Nape kwenye FB wall yake
      Nape Nnauye

      Nakulilia Bob Nyanga Makani! Kuna wanasiasa wengi lakini Mzee Makani ni wa aina ya pekee! Kuna wanasheria wengi lakini si wa aina ya Bob Makani! Umepambana kuhakikisha siasa za Tanzania hasa za ndani ya Chama chako zinakuwa za kweli na zisizo na uongo, chuki na ubabaishaji! Bahati mbaya umeondoka wakati siasa hizo zilizokukera zikishika kasi kubwa kwenye Chama chako! Naamini Mungu atainua mwingine wa aina yako au zaidi yako, akiokoe Chama chako, ili kwa pamoja tujenge Demokrasia ya kweli nchini! TANZANIA KWANZA, UZELENDO KWANZA!

      Alipokuwa hai na hata aliposimama jukwaani ccm mlimponda leo kafariki mnajifanya toa sifa toeni si mtu akiwa hai shame on you.Leo akifa Dr.slaa utasema maneno kama hayo lakini yupo hai leo mnamwona kama MWIBA nchini ukijua anapigania ukombozi wa kweli tatizo lenu mumeweka matumbo yenu mbele kuliko maslai ya wengi,wako wapi twiga wetu,madini yetu,fedha zetu za epa,meremeta,kagoda, nk bro wewe ni kijana lakini tunapoona unatuingiza na kutupeleka mkenge na wazee wako wa magamba tunakudharau sana wewe kijana na una maisha marefu ktk nchi hii wakina lowasa,mkama,msekwa na wazee wengine wa magamba wanao ipapeleka nchi hii wanavyotaka maisha yanahesabika vijana ndio tutakao baki ni wakati wako sasa wa kubadilika na kujivua gamba na kujiunga na siasa safi za kutetea wanyonge na kupigania uhuru wa pili wa nchi hii.

    3. #82
      Candid Scope's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th November 2010
      Posts : 7,708
      Rep Power : 15285
      Likes Received
      3768
      Likes Given
      2906

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Mukama awatibua CHADEMA
      MBOWE AKEREKA, AMJIBU KWA VIELELEZO
      KATIKA kile kilichoonekana kama vijembe vya kisiasa kuutawala msiba wa muasisi wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Bob Makani, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, jana alijikuta katika wakati mgumu kutokana na kauli yake kupingwa vikali na Freeman Mbowe.
      Mukama wakati akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya chama chake katika viwanja vya Karimjee zilikofanyika shughuli za kuuaga mwili wa marehemu, alimsifu Makani akisema alikuwa ni Katibu Mkuu wa Kwanza wa CHADEMA kutoka nje ya kanda ya kaskazini kati ya waasisi wenzake tisa. Mbali na sifa nyingi alizommwagia marehemu, Mukama pia alisema CHADEMA wanatakiwa kuweka kumbukumbu hiyo kwa kuwa alikuwa ni mtu shupavu asiyependa kuongea wala kuhubiri kwa muda mrefu na asiyekumbatia udini, ukabila na ukanda.
      Hata hivyo, wakati Mukama akieleza hayo, viongozi wengi wa CHADEMA walionekana kushangazwa na kauli ile ambapo Mwenyekiti wa chama hicho, Mbowe, katika salamu zake alitumia mwanya huo kumjibu kwa vielelezo.

      Mbowe
      Mbowe alisema kuwa kitendo cha kusema kuwa CHADEMA kiliasisiwa na watu tisa kutoka eneo moja la kanda ya kaskazini ni uchafuzi wa kihistoria ndani ya chama hicho. Katika kuonesha kukerwa na kauli hiyo, Mbowe alilazimika kuwataja waasisi na mikoa yao kuwa ni

      • Edwin Mtei (Arusha),
      • Makani (Shinyanga),
      • Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
      • Edward Barongo (Kagera),
      • Mary Kabigi (Mbeya),
      • Menrad Mtungi (Kagera),
      • Costa Shinganya (Kigoma),
      • Evalist Maembe (Morogoro) na
      • Steven Wassira (Mara).

      “Mimi wakati huo nilikuwa mdogo na shughuli zangu zilikuwa ni kuandaa vikao na mikakati ndani ya chama. Nashangaa sana wakati nakumbuka historia ya chama hiki, hivyo watu wasijaribu kuipotosha,” alisema Mbowe.

      Mbowe pia aligusia suala zima la uanzishwaji wa mchakato wa Katiba mpya akisema ni lazima kufanyike na marekebisho ya mfumo wa kisheria ili kuwapa nafasi wenye uwezo kuingia bungeni na kutoa michango ya maendeleo kwa jamii. Alisema mwaka 1995, 2000 na 2005 Makani aligombea ubunge Shinyanga Mjini akashindwa, hivyo ni vema watu kama hao wenye mchango mkubwa wakaingizwa bungeni kwa ajili ya kuleta changamoto mbalimbali.

      Rais Kikwete amlilia

      Rais Jakaya Kikwete naye alielezea kuhuzunishwa kwake na msiba huo na kusema kuwa Bob Makani alikuwa ni mtu muhimu na msaada mkubwa katika michango yake aliyowahi kuitoa katika kukuza uchumi wa nchi. “Nilisikia taarifa za msiba ambao ulinihuzunisha na kushtuka sana nikajaribu kumpigia simu Mwenyekiti wa Chama, Mbowe, lakini hakupatikana kwa kuwa alikuwa katika shughuli kubwa huko Ruangwa, nikamtumia ujumbe mfupi na baada ya kuupokea akanipigia na mimi nilikuwa katika shughuli sikupatikana, hivyo nikampigia tena baadaye ndipo tukazungumza,” alisema Kikwete. Rais Kikwete alisema kuwa ni vema kuhuzunika kwamba tumepoteza mtu muhimu lakini pia iendane sambamba na kusherehekea na kuyaenzi mambo yake mazuri ambayo ameyafanya wakati wa uhai wake.

      Prof. Lipumba akumbusha enzi

      Kwa niaba ya vyama vya upinzani, Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba, alimwelezea Makani kuwa alikuwa mtu mzuri na kwamba CHADEMA inatakiwa kuiga mfano wake wa kuunganisha watu. Alisema alikuwa ni mwana mageuzi aliyeasisi harakati za mabadiliko ya Katiba na kusema alipata suluba pamoja naye katika mapambano hayo. Pia alikumbushia enzi zao za shule akisema Makani alikuwa na akili nyingi darasani. Muasisi wa CHADEMA ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, Erdwin Mtei, alimtaka Makani kuwa alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, na ameeleza masikitiko yake ya kuondokewa na mwenzake.

      Mtei
      Mtei alisema Makani kwa nafasi yake katika BoT alikuwa ni mtu aliyejali maslahi ya nchi na pia mwepesi wa kutoa taarifa za fedha.

      Dr. Slaa
      Akisoma wasifu wa marehemu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alisema walifaidi utawala wa sheria na aina ya uongozi wa Makani kutokana na kuwa mwanasheria. Alisema Makani ni mfano wa kuigwa kwa kuwa alikuwa ni mtu wa watu aliyekuwa na kipaji cha kuelewa wananchi ambapo urefu wake uliweza kuonekana kila mahali alipoenda sambamba na ucheshi wake.

      • Asema kuwa Makani alizaliwa mwaka 1936 katika Hospitali ya Kolandoto, Shinyanga na kusoma shule ya msingi Ibadakuli mkoani humo.
      • Alifauru sekondari na kupelekwa Chuo Kikuu cha Makerere, ambako alifuzu na kupata Shahada ya Kwanza katika Uchumi (BA Economics).
      • Mwaka wa 1961 alikwenda Chuo Kikuu cha Liverpool, nchini Uingereza na 1965 akatunukiwa Shahada ya Sheria (LLB) alirudi nchini ambapo aliajiriwa na serikali kama Mwanasheria wa Serikali kwa muda mfupi kabla hajapandishwa cheo na kuwa Exchange Control Manager wa Benki Kuu.
      • Makani ni mwasisi wa CHADEMA mwenye kadi namba tatu baada ya Edwin Mtei, na marehemu Brown Ngwilulupi. Mwaka wa 1998 akachaguliwa kuwa mwenyekiti chama hadi 2003.
      • Makani pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa bodi za wakurugenzi katika Shirika la Ndege Tanzania, Williamson Diamond, Tanzania Breweries, Benki ya Taifa ya Biashara na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society.

    4. #83
      kookolikoo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2012
      Posts : 1,973
      Rep Power : 761
      Likes Received
      284
      Likes Given
      147

      Default

      Quote By Mungi View Post
      Hivi Katibu mkuu wa CCM
      anachaguliwa au anapachikwa tu? Maana Mkama Dah! huyu siyo kabisa,
      afadhali ya Makamba!
      ni mteuliwa wa mwenyekiti!

    5. #84
      peter tumaini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2012
      Location : DSM
      Posts : 575
      Rep Power : 487
      Likes Received
      86
      Likes Given
      54

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      ukikosa hekima busara kwako mpaka ufufuo.

    6. #85
      dguyana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th January 2011
      Posts : 426
      Rep Power : 512
      Likes Received
      109
      Likes Given
      66

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Ni laana ya matendo maovu anayoshabikia (Igunga na Arumeru). Kila kitu kiovu unachofanya dunia hulipwa hapahapa. Stay tune.
      Changudoa mwenye wivu a.k.a Jambazi lenye huruma

    7. #86
      Fredrick Sanga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th January 2011
      Location : Kijitonyama
      Posts : 2,988
      Rep Power : 2594
      Likes Received
      641
      Likes Given
      777

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Hapo CCM wamekula chaka.

      • Edwin Mtei (Arusha),
      • Makani (Shinyanga),
      • Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
      • Edward Barongo (Kagera),
      • Mary Kabigi (Mbeya),
      • Menrad Mtungi (Kagera),
      • Costa Shinganya (Kigoma),
      • Evalist Maembe (Morogoro) na
      • Steven Wassira (Mara).

      We shall overcome, righteousness shall always prevail.

    8. #87
      Gwalihenzi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st October 2011
      Posts : 2,490
      Rep Power : 909
      Likes Received
      648
      Likes Given
      413

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Quote By Candid Scope View Post
      Mukama awatibua CHADEMA
      MBOWE AKEREKA, AMJIBU KWA VIELELEZO
      KATIKA kile kilichoonekana kama vijembe vya kisiasa kuutawala msiba wa muasisi wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA), Bob Makani, Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, jana alijikuta katika wakati mgumu kutokana na kauli yake kupingwa vikali na Freeman Mbowe.
      Mukama wakati akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya chama chake katika viwanja vya Karimjee zilikofanyika shughuli za kuuaga mwili wa marehemu, alimsifu Makani akisema alikuwa ni Katibu Mkuu wa Kwanza wa CHADEMA kutoka nje ya kanda ya kaskazini kati ya waasisi wenzake tisa. Mbali na sifa nyingi alizommwagia marehemu, Mukama pia alisema CHADEMA wanatakiwa kuweka kumbukumbu hiyo kwa kuwa alikuwa ni mtu shupavu asiyependa kuongea wala kuhubiri kwa muda mrefu na asiyekumbatia udini, ukabila na ukanda.
      Hata hivyo, wakati Mukama akieleza hayo, viongozi wengi wa CHADEMA walionekana kushangazwa na kauli ile ambapo Mwenyekiti wa chama hicho, Mbowe, katika salamu zake alitumia mwanya huo kumjibu kwa vielelezo.

      Mbowe
      Mbowe alisema kuwa kitendo cha kusema kuwa CHADEMA kiliasisiwa na watu tisa kutoka eneo moja la kanda ya kaskazini ni uchafuzi wa kihistoria ndani ya chama hicho. Katika kuonesha kukerwa na kauli hiyo, Mbowe alilazimika kuwataja waasisi na mikoa yao kuwa ni

      • Edwin Mtei (Arusha),
      • Makani (Shinyanga),
      • Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
      • Edward Barongo (Kagera),
      • Mary Kabigi (Mbeya),
      • Menrad Mtungi (Kagera),
      • Costa Shinganya (Kigoma),
      • Evalist Maembe (Morogoro) na
      • Steven Wassira (Mara).

      “Mimi wakati huo nilikuwa mdogo na shughuli zangu zilikuwa ni kuandaa vikao na mikakati ndani ya chama. Nashangaa sana wakati nakumbuka historia ya chama hiki, hivyo watu wasijaribu kuipotosha,” alisema Mbowe.

      Mbowe pia aligusia suala zima la uanzishwaji wa mchakato wa Katiba mpya akisema ni lazima kufanyike na marekebisho ya mfumo wa kisheria ili kuwapa nafasi wenye uwezo kuingia bungeni na kutoa michango ya maendeleo kwa jamii. Alisema mwaka 1995, 2000 na 2005 Makani aligombea ubunge Shinyanga Mjini akashindwa, hivyo ni vema watu kama hao wenye mchango mkubwa wakaingizwa bungeni kwa ajili ya kuleta changamoto mbalimbali.

      Rais Kikwete amlilia

      Rais Jakaya Kikwete naye alielezea kuhuzunishwa kwake na msiba huo na kusema kuwa Bob Makani alikuwa ni mtu muhimu na msaada mkubwa katika michango yake aliyowahi kuitoa katika kukuza uchumi wa nchi. “Nilisikia taarifa za msiba ambao ulinihuzunisha na kushtuka sana nikajaribu kumpigia simu Mwenyekiti wa Chama, Mbowe, lakini hakupatikana kwa kuwa alikuwa katika shughuli kubwa huko Ruangwa, nikamtumia ujumbe mfupi na baada ya kuupokea akanipigia na mimi nilikuwa katika shughuli sikupatikana, hivyo nikampigia tena baadaye ndipo tukazungumza,” alisema Kikwete. Rais Kikwete alisema kuwa ni vema kuhuzunika kwamba tumepoteza mtu muhimu lakini pia iendane sambamba na kusherehekea na kuyaenzi mambo yake mazuri ambayo ameyafanya wakati wa uhai wake.

      Prof. Lipumba akumbusha enzi

      Kwa niaba ya vyama vya upinzani, Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba, alimwelezea Makani kuwa alikuwa mtu mzuri na kwamba CHADEMA inatakiwa kuiga mfano wake wa kuunganisha watu. Alisema alikuwa ni mwana mageuzi aliyeasisi harakati za mabadiliko ya Katiba na kusema alipata suluba pamoja naye katika mapambano hayo. Pia alikumbushia enzi zao za shule akisema Makani alikuwa na akili nyingi darasani. Muasisi wa CHADEMA ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu na Mwenyekiti wa kwanza wa chama hicho, Erdwin Mtei, alimtaka Makani kuwa alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu, na ameeleza masikitiko yake ya kuondokewa na mwenzake.

      Mtei
      Mtei alisema Makani kwa nafasi yake katika BoT alikuwa ni mtu aliyejali maslahi ya nchi na pia mwepesi wa kutoa taarifa za fedha.

      Dr. Slaa
      Akisoma wasifu wa marehemu, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa alisema walifaidi utawala wa sheria na aina ya uongozi wa Makani kutokana na kuwa mwanasheria. Alisema Makani ni mfano wa kuigwa kwa kuwa alikuwa ni mtu wa watu aliyekuwa na kipaji cha kuelewa wananchi ambapo urefu wake uliweza kuonekana kila mahali alipoenda sambamba na ucheshi wake.

      • Asema kuwa Makani alizaliwa mwaka 1936 katika Hospitali ya Kolandoto, Shinyanga na kusoma shule ya msingi Ibadakuli mkoani humo.
      • Alifauru sekondari na kupelekwa Chuo Kikuu cha Makerere, ambako alifuzu na kupata Shahada ya Kwanza katika Uchumi (BA Economics).
      • Mwaka wa 1961 alikwenda Chuo Kikuu cha Liverpool, nchini Uingereza na 1965 akatunukiwa Shahada ya Sheria (LLB) alirudi nchini ambapo aliajiriwa na serikali kama Mwanasheria wa Serikali kwa muda mfupi kabla hajapandishwa cheo na kuwa Exchange Control Manager wa Benki Kuu.
      • Makani ni mwasisi wa CHADEMA mwenye kadi namba tatu baada ya Edwin Mtei, na marehemu Brown Ngwilulupi. Mwaka wa 1998 akachaguliwa kuwa mwenyekiti chama hadi 2003.
      • Makani pia aliwahi kuwa mwenyekiti wa bodi za wakurugenzi katika Shirika la Ndege Tanzania, Williamson Diamond, Tanzania Breweries, Benki ya Taifa ya Biashara na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Law Society.

      Majibu ya Mbowe yalieleweka na Mukama? au ilikuwa gitaa kwa mbuzi?

    9. #88
      webondo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th April 2012
      Location : Chini ya mwembe
      Posts : 1,167
      Rep Power : 593
      Likes Received
      178
      Likes Given
      381

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Uwezo wake ni mdogo sana, kama angekuwa anapewa nafasi ya kuongea kama NAPE angeharibu zaidi. Kuongea katika halaiki inahitaji hekima na uwezo wa kufikiri haraka na kujua uongee nini kutokana na tukio halisi. Labda utu uzima, msameheni bure.

    10. #89
      sirghanam's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th May 2009
      Posts : 253
      Rep Power : 562
      Likes Received
      65
      Likes Given
      139

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      sasa hivi naona wazi kabisa walitoa marehemu wakaingiza maiti

    11. #90
      Froida's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th May 2009
      Posts : 3,854
      Rep Power : 1343
      Likes Received
      758
      Likes Given
      153

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Quote By Shagihilu View Post
      Kanifurahisha Mh. Mbowe kwa kuweka historia ya Chama vizuri tena kwa lugha nyepesi lakini yenye uzito na msisitizo wa hali ya juu. Aibu kwako Mukama. Maana ulianza kwa mbwembwe kweli (utafikiri hauko msibani!) kuonyesha Chadema imejaa ukanda. Kuna mtu mmoja pale kasema kuna vitu vingi visipoandikwa kwenye vitabu unakuta historia inatoweka. Nadhani hata hili Nape amekuwa akilipigia vuvuzela kweli ila leo amenywea....
      kweli Mwenyekiti wa Chadema Bwana freeman Mbowe aliendelea na kuwataja waasisi wa chadema kama ifuatavyo
      1. Edwini Mtei-Arusha
      2. Bob Makani-Shinyanga
      3. Brown Gwilulupi-Iringa
      4. Mary Kabighi-Mbeya
      5. Menrad mtungi-Kagera
      6. Edward Barongo-Kagera
      7. Costa shinganya-Kigoma
      8. Evalist Maembe-Morogoro
      9. Steven Wassira-Morogoro

      hao ndio historia ya magaeuzi ya kweli nchini haitawaasahau,juhudi zao zinatusogeza kwenye ukombozi wa kweli japo hatuna uhakika tena na Steven Wassira mbwabwajaji

    12. #91
      timbilimu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd September 2010
      Location : DSM
      Posts : 2,718
      Rep Power : 989
      Likes Received
      598
      Likes Given
      10

      Default

      Masahihisho. Siyo Menrad Mtungi,ni Medard Mutungi.
      Quote By Fredrick Sanga View Post
      Hapo CCM wamekula chaka.

      • Edwin Mtei (Arusha),
      • Makani (Shinyanga),
      • Marehemu Brown Ngwilupipi (Iringa),
      • Edward Barongo (Kagera),
      • Mary Kabigi (Mbeya),
      • Menrad Mtungi (Kagera),
      • Costa Shinganya (Kigoma),
      • Evalist Maembe (Morogoro) na
      • Steven Wassira (Mara).

    13. #92
      CAMARADERIE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd March 2011
      Location : 1 Luthuli Street
      Posts : 4,163
      Rep Power : 2723
      Likes Received
      1590
      Likes Given
      1145

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Ubongo wa mzee huyu sijui umedondoka mwilini kwa uzito? Nina wasiwasi na ulipo kwa sasa!

      Safari_ni_Safari likes this.
      A compliment is something like a kiss through a veil

    14. #93
      Johnsecond's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2010
      Posts : 949
      Rep Power : 657
      Likes Received
      156
      Likes Given
      68

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      mukama vs. makamba tofauti ni "u" na "b" hiyo ni 1/6 kufanana ni 5/6 ambayo ni 83% like.

    15. #94
      Kite Munganga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 19th November 2006
      Posts : 857
      Rep Power : 815
      Likes Received
      72
      Likes Given
      83

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Quote By Precise pangolin View Post
      Mimi sijawahi kumuona Mukama aki kamua mimi huwa namuona na vikofia vyake utafikiri sokomoko wa kwenye gazeti la udaku la Sani
      Mimi kwa mambo yake humfananisha baba huyu na Karikenye !...CCM wafikirie mbinu mbadala kabla ya 2015
      Tanzania ni Nchi ya amani iliyozeeka!

    16. #95
      tubadilike-sasa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st January 2012
      Posts : 493
      Rep Power : 471
      Likes Received
      99
      Likes Given
      281

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Jamani msishangae sana maana hayo ya Mukama yametoka moyoni.Kwa sababu swala la ukanda na udini imekuwa ni mikakati ya CCM tangu uchaguzi wa 2010. Kama kitu umekiwekea mkakati,halafu kila kukicha unakirudiarudia hata kama si cha kweli kinakuwa "internalized". Hii ni dhambi ambayo CCM wameianzisha na huko mbele itawatafuna tu. Wanatia kibiriti msitu ambao nao wamo ndani

    17. #96
      Safari_ni_Safari's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th October 2007
      Location : Kibaruani
      Posts : 12,462
      Rep Power : 24251
      Likes Received
      5099
      Likes Given
      2738

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Quote By CAMARADERIE View Post
      Ubongo wa mzee huyu sijui umedondoka mwilini kwa uzito? Nina wasiwasi na ulipo kwa sasa!

      Ha ha haa! There is a point here

      Zogolo Dangu Dawika Miye!

    18. #97
      KISAKA MORIS's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Posts : 367
      Rep Power : 434
      Likes Received
      30
      Likes Given
      47

      Default

      Quote By ritz View Post
      Siasa za Tanzania ndivyo zilivyo kupigana madogo tu.
      Wewe tushakuzoea hakuna anayekushangaa maana ukweli kwako ni sumu, kama siasa za Tanzania ni (madogo) nadhani ulimaanisha madongo, ndiyo aliyoyaongea katibu wako mkuu wa chama ila mwenyekiti wako wa chama akakataa kujiingiza kwenye mtego huo.

    19. #98
      WildCard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2008
      Posts : 6,481
      Rep Power : 1989
      Likes Received
      1810
      Likes Given
      59

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Msihangaike na Mzee Mukama. Yeye sio na hajawahi kuwa MWANASIASA. Cheo hiki cha Ukatibu Mkuu wa CCM kilimdondokea tu na kimemzidi sana. Sidhani kama atabaki nacho baada ya uchaguzi mkuu wa CCM baadae mwaka huu. Yeye, Makamba na Mzee Gama ni kati ya Makatibu Wakuu wa CCM wabovu kabisa CCM imepata kuwa nao.

    20. #99
      Bobuk's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th October 2010
      Posts : 2,181
      Rep Power : 949
      Likes Received
      889
      Likes Given
      1

      Default

      Quote By IkizuJF View Post
      neno MKAMA maana yake ni UPEPO, yaani VAPOUR kwa kiingereza. so ni bora tuendelee kumwita vapour.
      Usipotoshe watu maana na neno MKAMA ni Mtemi/Mfalme

      Lakini pia anaweza kuwa MKAMA wa UONGO

    21. #100
      WildCard's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd April 2008
      Posts : 6,481
      Rep Power : 1989
      Likes Received
      1810
      Likes Given
      59

      Default re: Mukama: Katibu Mkuu wa CCM atia aibu kwenye Msiba wa Bob pale Karimjee

      Quote By Bobuk View Post
      Usipotoshe watu maana na neno MKAMA ni Mtemi/Mfalme

      Lakini pia anaweza kuwa MKAMA wa UONGO
      Bobuk,
      Makabila ya Mara hayakuwa na Watemi/Wafalme wa asili. IkizuJF yuko sahihi zaidi.

    Page 5 of 7 FirstFirst ... 34567 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...