Habari za uhakika muda mchache uliopita nimepata taarifa ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema kabla ya Mbowe... Mzee Bob Makani amefariki.
R.I.P Bob Makani
Kwasababu ya msiba huu, CHADEMA wamesitisha Operesheni Okoa Kusini na wanarejea Dar kwa shughuli ya msiba.
Source: Kutoka kwa ndugu zake.
UPDATES...
Bendera ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ikipepea nusu mlingoti katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaa kufuatia kifo cha Mwasisi wa chama hicho, Mahmoud 'Bob' Makani
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu, Mahmoud 'Bob' Makani
Baadhi ya waombolezaji
DAR ES SALAAM, Tanzania
Aliyekuwa Naibu Gavana wa Tanzania na mwasisi wa Chama cha Demokrasia (Chadema) marehemu, Mahmoud Nyange Makani maarufu Bob Makani, anatarajiwa kuzikwa katika kijiji cha Negezi kilichopo mkoani Shinyanga.
Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Hassan Makani amesema kuwa, marehemu Makani ameacha mke na watoto saba na wajukuu wanane na anatarajiwa kuagwa rasmi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam kesho. kwa hisani ya Kiganyi
Nilimfahamu Bob Makani kwa mara ya kwanza miaka ya nyuma enzi za uenyekiti wake CHADEMA (sikumbuki mwaka) alihutubia viwanja vya bonde nyasi Uyole-Mbeya
Mzee Makani makini, tangulia kwa aman, daima wajukuu zako tutakukumbuka..tunakuahidi kuendeleza vuguvugu la mabadiliko ulilo liasisi enzi za uhai wako
Ndugu wanachadema wenzangu...njia pekee ya kumuuenzi Mzee wetu ni kutoisalit M4C kwa gharama yoyote ile
Huyu Mzee Wangu sijawahi pata Jibu hadi leo Hii Ndugu zake ni Wakristu ila yeye ni Muislam na Watoto wake wote kama sikosei Ismail na Medi wale Wahezaji Mpira Wa Kikapu Misukuma ile Mirefu mirefu sana kama Baba yao...
Mwenyezi Mungu aiweke Roho ya Marehemu Panapo Stahili...
Bageshi...
Follow Us Here