Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Yaliyojiri Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar) Juni 9,2012

    Report Post
    Page 1 of 46 12311 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 912
    1. #1
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,413
      Rep Power : 10872
      Likes Received
      3796
      Likes Given
      426

      Default Yaliyojiri Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar) Juni 9,2012




















      TEXT UPDATES:

      Ni asubuhi tulivu ya Jumamosi na hali ya hewa ni nzuri kabisa.

      CCM wanatarajiwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani ambavyo wapinzani wao wakuu walivibatiza kwa jina la viwanja vya CDM SQUARE.

      Tayari shamrashamra zimeshaanza hapa uwanjani na shughuli za ujenzi na kupamba majukwaa zinaendelea.Mkutano huu utarushwa live na vituo kadhaa vya Television.

      Tutakuwa hapa uwanjani kuwapa updates kila kitakachoendelea.

      Updates:
      Mpaka muda huu saa 8.30 watu wanaendelea kuja uwanjani ingawa kwa ujumla bado uwanja haujapendeza sana.Tunaendelea kusubiri zaidi huenda ni hizi foleni za Dar zinachelewesha watu.Wanachama kadhaa kutoka matawi mbalimbali wameshafika wakiwa kwenye mabasi na vyombo vingine vya usafiri.Baadhi ya wanachama wanadai wamekodisha kwa gharama zao na wengine wanadai wamekodishiwa na chama.Bado natafuta ukweli wa haya madai yao.

      More updates.
      Viongozi mbalimbali wanaendelea kutoa hotuba zao.Hotuba iliyoshangaza wananchi ni ya Nape Nauye aliyewashambulia kwa maneno makali waislam wa kikundi maarufu cha Uamsho Zanzibar kwamba ni MAJAMBAZI wakubwa.Wengi hawajafurahishwa na maneno yake na wanaona kama ameutukana Uislam.Idadi kubwa ya watu iliguna baada ya kauli hiyo ya Nape.

      More updates....
      Mkutano umemalizika lakini kwa ujumla katika wazungumzaji wote wa CCM na mawaziri walioongea aliyeonekana kuwagusa watu wengi ni Waziri wa uchukuzi Dr Harisson Mwakyembe ambaye alitoa hadi namba yake ya simu 0782242526 kumpigia wakati wowote mwananchi atakapokumbana na adha yoyote kwenye sekta ya usafiri. Mwakyembe kwa kujua anaangaliwa nchi nzima kupitia Television hakumalizia kwa kusifu CCM kama wenzake bali yeye alimalizia kwa kusema Dar Hoyeeee!

      Baadhi ya kadi za CDM na bendera zimerudishwa lakini hakuna hata kiongozi mmoja wa ngazi yoyote aliyejitambulisha hadharani kwamba amejitoa CDM kitu kinachotia shaka malundo ya kadi za CDM zilizorudishwa.Sintofahamu nyingine ni karibia kadi zote za CDM zilizorudishwa hazikuwa na picha ya mwanachama na nyingine hazijapigwa mihuri.

      Mwisho Pamoja na CCM kujitahidi kukusanya watu wengi kwenye mkutano huu wa leo kiuhalisia mkutano huu wa CCM haujaweza kuvunja rekodi ya mkutano wa CDM uliofanyika wiki mbili zilizopita na kuhudhuriwa na maelfu kwa maelfu ya wananchi kiasi kwamba Jiji la Dar lilisimama kwa zaidi ya masaa 6.
      Last edited by Molemo; 9th June 2012 at 22:08.

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      Mzito Kabwela's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th November 2009
      Location : MPUMBULI
      Posts : 6,424
      Rep Power : 0
      Likes Received
      1086
      Likes Given
      7

      Default re: Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar)

      nyinyiem mna tabu mwaka huu!

    4. #3
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,413
      Rep Power : 10872
      Likes Received
      3796
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By Mzito K
      nyinyiem mna tabu mwaka huu!
      Mkuu usidhani kila mtu ni ccm lakini sioni kosa kuhudhuria huu mkutano na kufanya live coverage kwa wadau.

    5. #4
      peter tumaini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2012
      Location : DSM
      Posts : 575
      Rep Power : 483
      Likes Received
      86
      Likes Given
      54

      Default Kutoka Jangwani 9/6/2012

      Wanabodi,

      kwa sasa nimeshawasili hapa jangwani kuangalia kinachojiri,pilikapilika za upangaji wa viti vya plastic vyeupe unaendelea na uandaaji wa jukwaa umepamba moto huku mabango nayo yakiandikwa.

      Mpaka sasa kuna bango kubwa la kitambaa limewekwa junction ya Morogoro road na kawawa limeandikwa;"KUHUSU VURUGU ZA UAMSHO CCM KUTOA TAMKO LEO SAA SITA''

      Ugawaji wa T-shirt unaendelea hapa Jangwani na mambo mengine mtapata jinsi time inavyojiri.

      Natumia laptop ndogo nimeificha kiaina staweza kutupia picha.

      Watu ni wengi wameletwa na magari toka sehemu mbali mbali za dar hilo halina mjadala,
      Lengo limeelezwa ni kujibu mapigo kwa upinzani.
      Wasira kafika na gari la serikali akiwa amelala na kasema kachoka sana kwani kaja toka J,burg leo.
      Niko jirani na mjumbe wa NEC CCM ana samsung galaxy anachukua picha huku akilinganisha na ule wa CDM,hajasema lengo nikujaza watu au nini?
      Zaidi TV na Radio ziko live kwa sasa jongeeni.
      Last edited by peter tumaini; 9th June 2012 at 15:58. Reason: updates
      mzamifu likes this.

    6. #5
      Bujibuji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2009
      Location : NYUMBANI PANONO
      Posts : 13,813
      Rep Power : 11187
      Likes Received
      6999
      Likes Given
      5173

      Default re: Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar)

      CCM Chanzo cha Mauti
      mzamifu, Kolero and yutong like this.
      KAZI NDIO MSINGI WA MAENDELEO. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE- J. K. NYERERE

    7. Miaka 50

    8. #6
      IGWE's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2011
      Location : Blue Plaza Building-Arusha
      Posts : 5,077
      Rep Power : 3256
      Likes Received
      1244
      Likes Given
      1196

      Default

      Quote By fmpiganaji
      Mkuu usidhani kila mtu ni ccm lakini sioni kosa kuhudhuria huu mkutano na kufanya live coverage kwa wadau.
      Ucjali mkuu,..hilo ni jambo jema..tunasubiri kwa hamu sana hizo update.

    9. #7
      KakaJambazi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 5th June 2009
      Posts : 4,269
      Rep Power : 2732
      Likes Received
      1076
      Likes Given
      935

      Default Re: Kutoka jangwani 9/6/2012

      sa kama huwezi kutuma picha umeanzisha thredi ya nini?
      Mi mwenyewe sitakua na nafasi japo nipo mitaa ya jangwani, nikaona sina sababu ya kuanzisha thredi, au unataka thredi yako ndo iwe ya kwanza kuchangiwa?
      ,,,,,,,,Jisachi

    10. #8
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,413
      Rep Power : 10872
      Likes Received
      3796
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By Bujibuji
      CCM Chanzo cha Mauti
      Tusubiri mkuu kina Wasira wanaweza kutoa sera nzuri leo za maendeleo ya Mtanzania.

    11. #9
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,413
      Rep Power : 10872
      Likes Received
      3796
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By IGWE
      Ucjali mkuu,..hilo ni jambo jema..tunasubiri kwa hamu sana hizo update.
      Msijali wakuu kila kitakachotokea kitawekwa peupe

    12. #10
      peter tumaini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd February 2012
      Location : DSM
      Posts : 575
      Rep Power : 483
      Likes Received
      86
      Likes Given
      54

      Default re: Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar)

      Quote By fmpiganaji
      Mkuu usidhani kila mtu ni ccm lakini sioni kosa kuhudhuria huu mkutano na kufanya live coverage kwa wadau.
      Umenena mkuu nami niko eneo la tukio, ni bora ukajua mbinu na udhaifu wa adui yako ili iwe rahisi kumumaliza.

    13. #11
      Nduka's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd December 2008
      Posts : 5,580
      Rep Power : 1633
      Likes Received
      381
      Likes Given
      553

      Default

      Quote By Bujibuji
      CCM Chanzo cha Mauti
      Leo Dar imependeza imepambwa kwa kijani na njano.

    14. #12
      NICE LAMECK's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 209
      Rep Power : 401
      Likes Received
      26
      Likes Given
      37

      Default Re: Kutoka jangwani 9/6/2012

      Tupunguze ukali wa maneno tunachotaka ni habari za mkutano wa magamba na kama atatokea mtu akatuwekea picha itakuwa bora zaidi.
      Memory and peter tumaini like this.

    15. #13
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,413
      Rep Power : 10872
      Likes Received
      3796
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By peter tumaini
      Umenena mkuu nami niko eneo la tukio, ni bora ukajua mbinu na udhaifu wa adui yako ili iwe rahisi kumumaliza.
      Safi sana kamanda.Tusaidiane kumwaga updates kwa wadau kila tukio litakalotokea.Tunaomba na thread zote zitakazoanzishwa ziunganishwe hapa.

    16. #14
      Precise pangolin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 5,670
      Rep Power : 1909
      Likes Received
      1563
      Likes Given
      676

      Default re: Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar)

      Mkuu fmpiganaji hakikisha picha za Mafuso yaliobeba watu unayaweka kwa wingi ili tuweze kufanya analysis ya Gharama za Mkutano
      Kolero and lutolucy like this.

    17. #15
      Wanitakiani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th April 2008
      Posts : 632
      Rep Power : 698
      Likes Received
      129
      Likes Given
      20

      Default Re: Kutoka jangwani 9/6/2012

      Wewe endelea kutujuza hat bila picha......
      peter tumaini likes this.

    18. #16
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,413
      Rep Power : 10872
      Likes Received
      3796
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By Nduka
      Leo Dar imependeza imepambwa kwa kijani na njano.
      Ni kweli mkuu nayaona mafuso mengi yamepambwa bendera kila kona.Kweli Dar imewaka sana.

    19. #17
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,413
      Rep Power : 10872
      Likes Received
      3796
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By Precise pangolin
      Mkuu fmpiganaji hakikisha picha za Mafuso yaliobeba watu unayaweka kwa wingi ili tuweze kufanya analysis ya Gharama za Mkutano
      Usijali mkuu niko na kamanda Peter Tumaini kaeni mkao wa kula.
      peter tumaini likes this.

    20. #18
      Precise pangolin's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 4th January 2012
      Posts : 5,670
      Rep Power : 1909
      Likes Received
      1563
      Likes Given
      676

      Default re: Mkutano wa CCM Viwanja vya Jangwani (Dar)

      Mimi nipo barabara ya Kilwa Road Mafuso yaliyo kodishwa na CCM nayapiga picha. zamani kabla hawaja filisi ile kampuni ya mabasi ya Scandinavia walikuwa wanayatumia sana

    21. #19
      Molemo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Posts : 8,413
      Rep Power : 10872
      Likes Received
      3796
      Likes Given
      426

      Default

      Quote By peter tumaini
      Wanabodi,

      kwa sasa nimeshawasili hapa jangwani kuangalia kinachojiri,pilikapilika za upangaji wa viti vya plastic vyeupe unaendelea na uandaaji wa jukwaa umepamba moto huku mabango nayo yakiandikwa....
      Mkuu tutakuwa pamoja

    22. #20
      Laurence's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2011
      Location : ULIMWENGUNI
      Posts : 2,042
      Rep Power : 1394
      Likes Received
      175
      Likes Given
      41

      Default

      Quote By fmpiganaji
      Tusubiri mkuu kina Wasira wanaweza kutoa sera nzuri leo za maendeleo ya Mtanzania.
      Mfumo uleule watu walewale kwa hyo usitegemee la tofauti kutoka kwa hawa viumbe

    Page 1 of 46 12311 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...