Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

    Report Post
    Page 6 of 8 FirstFirst ... 45678 LastLast
    Results 101 to 120 of 160
    1. #1
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,186
      Rep Power : 24275
      Likes Received
      4682
      Likes Given
      2300

      Default CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimedaiwa kutumia mamilioni ya fedha kugharimia mkutano wake wa hadhara unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya mahasimu wao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

      Kinyume na madai ya CCM kwamba lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uhai wa chama na kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yanayojitokeza ndani ya chama hicho, lakini duru za siasa zimedai kuwa, lengo kuu ni kujipima nguvu na CHADEMA ambacho wiki mbili zilizopita kilifanya mkutano wa hadhara katika viwanja hivyo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

      Katika mkutano huo wa CHADEMA ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha ITV, maelfu ya wanachama waliofurika, walifika katika viwanja hivyo kwa njia zao bila kusombwa na magari, wala kupokea posho.

      Ili kuhakikisha mkutano wa leo unafunika ule wa CHADEMA kwa kupata watu wengi, CCM imeamua kuwasafirisha wajumbe wake kwa magari makubwa ya kukodi kama vile malori na mabasi kutoka kila tawi na kuwafikisha katika viwanja hivyo.

      Mbali ya kusombwa kwa magari, CCM pia imeamua kugawa bure fulana na kofia, na kuna madai kuwa chama hicho kitatoa posho kwa wanachama wake watakaohudhuria mkutano huo.

      Mkakati wa kuhakikisha mkutano huo unapata watu wengi, umesukwa kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa kwa zaidi ya wiki moja sasa.

      Kana kwamba hiyo, haitoshi, CCM imeandaa baadhi ya wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) watakaotumbuiza mapema kabla ya kuanza mkutano kwa nia ya kuwavuta wanachama.

      Baadhi ya wasanii hao ni Diamond, Marlaw, Frola Mbasha na wengine wengi ambao walipata kutumika wakati wa mikutano ya kampeni ya Rais Jakaya Kikwete.

      Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, Nape Nnauye alisema baadhi ya mawaziri na makada maarufu ndani ya chama hicho tawala, watahutubia katika mkutano huo.

      Alisema mkutano huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake, ulipangwa siku nyingi kwa lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi wa chama wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa CCM unaoendelea katika ngazi mbalimbali.

      “Kuna vyombo vimesema mkutano huo utahutubiwa na Mzee Mkapa, Mwinyi. Hiyo sio kweli maana hata mwenyekiti wa chama taifa, Rais Jakaya Kikwete hatakuwepo jukwaani,” alisema Nape.

      Aliwataja mawaziri watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano), Steven Wassira, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC), Abdulrahman Kinana na Nape mwenyewe.

      “Mzee Kinana atazungumzia masuala ya katiba na sheria na atatoa kauli kuhusiana na vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar na kueleza msimamo wa chama kuhusu kikundi cha Uamsho cha visiwani humo kinachodaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.

      “Wasira atajikita kwenye uchumi, Dk. Mwakyembe atazungumzia jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya uchukuzi, Magufuli atazungumzia utekelezaji wa ilani katika eneo la ujenzi na mkakati wa kuondoa foleni jijini Dar es Salaam,” alisema Nape.

      Kama ilivyokuwa kwa CHADEMA, CCM nao wameamua kurusha mkutano huo moja kwa moja kupitia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na Televisheni ya ITV na baadhi ya vituo vya redio.

      Aliwataka wananchi, wanachama wa CCM na wakereketwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili kuwasikiliza viongozi wa chama na serikali watakaozungumzia kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015.

      CHADEMA yaipa masharti magumu
      Akizungumzia mkutano huo wa CCM, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, aliponda juhudi za kukusanya watu ili kuonesha kuwa chama hicho tawala bado kinapendwa.

      Akizungumza kutoka Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema CCM inatakiwa kuwaambia Watanzania na wananchi namna gani imetimiza ahadi zake ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, zikiwemo za kuwaletea wananchi maisha bora badala ya kusomba watu kwa magari.

      Dk. Slaa aliongeza kuwa, hali za Watanzania kwa sasa ni mbaya mara mbili hata kabla ya uchaguzi mkuu na kila mtu amepigika vibaya, kinyume kabisa na namna alivyoahidiwa na watawala.

      CHADEMA pia kimewataka viongozi watakaohutubia wananchi, waseme waziwazi idadi ya viongozi wa CCM waliokwisha vuliwa magamba hadi sasa, tangu wawatangazie Watanzania kuwa wanapambana na watu hao miaka miwili sasa.

      “CCM isijisumbue wala kujidanganya kusomba watu na kuaminisha umma kuwa bado inapendwa. Watu wameichoka kwa sababu imewadanganya.

      “Tunataka waseme, wamewaleteaje watu maisha bora kama walivyowaambia wakati wa kampeni, na pili waseme ni magamba mangapi yamevuliwa tangu wajitape kufanya hivyo,” alisema Dk. Slaa.

      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    2. Miaka 50

    3. #101
      andrews's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 28th March 2012
      Posts : 1,683
      Rep Power : 0
      Likes Received
      142
      Likes Given
      76

      Default Re: CCM na kubeba watu mpaka lini!?

      ccm kuanzisha al shabab mikoa ya pwani

      KATIKA HALI YA KUWAGAWA WATANZANIA CCM IMEANZA KUWATUMIA BAKWATA KUWAGAWA WANANCHI.WAZIRI WA ELIMU NI MUISLAM MAKAMU WA RAIS MISLAM KATIBU ITIKADI CCM NI MUISLAM,RAIS WA NCHI MUISLAM MKUU USALAMA WA TAIFA NI MISLAM SASA VP LEOBAKWATA WASEME WANA FELISHWA HIZI NI MBINU CHAFU ZA CCM KUWATOA WANANCHI KWENYE WIMBI LA MAGEUZI YA KISIASA NA KUIINGIZA UDINI KWENYE JAMII NI HATARI NA NI LAANA KWA HAWA WANAMTANDAO HUU TUNASEMA ILI TANZANIA IWE NA AMANI 2015 CCM LAZIMA IONDOKE ISITULETEE MAAFA.WAMEANZA UAMSHO NA HAKUNA KARIPIO KALI LILILOTOLEWA KUONESHA CCM INAVYOHUSIKA VILIVYO KABLA YA UCHAGUZI 2015 WASHINDWE WALEGEE NA WASAMBARATIKE.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    4. #102
      Ngarenaro's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th November 2011
      Posts : 282
      Rep Power : 434
      Likes Received
      44
      Likes Given
      1

      Default Re: CCM kupokea wanachama feki leo kutoka CHADEMA

      Chadema leo wameanza kutapatapa tangu asubuhi, mtatunga kila aina ya uongo, CCM inazidi kusonga mbele

    5. #103
      Mwana va Mutwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th June 2009
      Posts : 403
      Rep Power : 587
      Likes Received
      12
      Likes Given
      8

      Default Re: CCM kupokea wanachama feki leo kutoka CHADEMA

      kumbe inawezekana hata zile kadi zinazokusanywa na cdm kwenye mikutano nazo huwa ni feki,na wanachama mamluki

    6. #104
      Skp2ole's Avatar
      Member Array
      Join Date : 13th October 2011
      Posts : 83
      Rep Power : 401
      Likes Received
      4
      Likes Given
      10

      Default Kulala sauzi afrika

      Hivi Wasira huna la kutuambia au? Eti unajisifia kulala nje ya Tanzania

    7. #105
      kwamwewe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2010
      Posts : 856
      Rep Power : 5406
      Likes Received
      99
      Likes Given
      125

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By mungi
      chama cha mapinduzi (ccm), kimedaiwa kutumia mamilioni ya fedha kugharimia mkutano wake wa hadhara unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya jangwani jijini dar es salaam, katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya mahasimu wao, chama cha demokrasia na maendeleo (chadema).

      Kinyume na madai ya ccm kwamba lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uhai wa chama na kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yanayojitokeza ndani ya chama hicho, lakini duru za siasa zimedai kuwa, lengo kuu ni kujipima nguvu na chadema ambacho wiki mbili zilizopita kilifanya mkutano wa hadhara katika viwanja hivyo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

      Katika mkutano huo wa chadema ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha itv, maelfu ya wanachama waliofurika, walifika katika viwanja hivyo kwa njia zao bila kusombwa na magari, wala kupokea posho.

      Ili kuhakikisha mkutano wa leo unafunika ule wa chadema kwa kupata watu wengi, ccm imeamua kuwasafirisha wajumbe wake kwa magari makubwa ya kukodi kama vile malori na mabasi kutoka kila tawi na kuwafikisha katika viwanja hivyo.

      Mbali ya kusombwa kwa magari, ccm pia imeamua kugawa bure fulana na kofia, na kuna madai kuwa chama hicho kitatoa posho kwa wanachama wake watakaohudhuria mkutano huo.

      Mkakati wa kuhakikisha mkutano huo unapata watu wengi, umesukwa kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa kwa zaidi ya wiki moja sasa.

      Kana kwamba hiyo, haitoshi, ccm imeandaa baadhi ya wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (bongo flava) watakaotumbuiza mapema kabla ya kuanza mkutano kwa nia ya kuwavuta wanachama.

      Baadhi ya wasanii hao ni diamond, marlaw, frola mbasha na wengine wengi ambao walipata kutumika wakati wa mikutano ya kampeni ya rais jakaya kikwete.

      Akizungumza na waandishi wa habari jana, katibu wa uenezi na itikadi ccm, nape nnauye alisema baadhi ya mawaziri na makada maarufu ndani ya chama hicho tawala, watahutubia katika mkutano huo.

      Alisema mkutano huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake, ulipangwa siku nyingi kwa lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi wa chama wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa ccm unaoendelea katika ngazi mbalimbali.

      “kuna vyombo vimesema mkutano huo utahutubiwa na mzee mkapa, mwinyi. Hiyo sio kweli maana hata mwenyekiti wa chama taifa, rais jakaya kikwete hatakuwepo jukwaani,” alisema nape.

      Aliwataja mawaziri watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na waziri wa uchukuzi, dk. Harrison mwakyembe, naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia, januari makamba, waziri wa nchi ofisi ya rais (mahusiano), steven wassira, waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki (eac), samuel sitta, waziri wa ujenzi, john magufuli, mjumbe wa halmashauri kuu (nec) na kamati kuu (cc), abdulrahman kinana na nape mwenyewe.

      “mzee kinana atazungumzia masuala ya katiba na sheria na atatoa kauli kuhusiana na vurugu zilizotokea visiwani zanzibar na kueleza msimamo wa chama kuhusu kikundi cha uamsho cha visiwani humo kinachodaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.

      “wasira atajikita kwenye uchumi, dk. Mwakyembe atazungumzia jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya uchukuzi, magufuli atazungumzia utekelezaji wa ilani katika eneo la ujenzi na mkakati wa kuondoa foleni jijini dar es salaam,” alisema nape.

      Kama ilivyokuwa kwa chadema, ccm nao wameamua kurusha mkutano huo moja kwa moja kupitia kituo cha televisheni ya taifa (tbc) na televisheni ya itv na baadhi ya vituo vya redio.

      Aliwataka wananchi, wanachama wa ccm na wakereketwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili kuwasikiliza viongozi wa chama na serikali watakaozungumzia kuhusu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm ya mwaka 2010/2015.

      chadema yaipa masharti magumu
      akizungumzia mkutano huo wa ccm, katibu mkuu wa chadema, dk. Wilbroad slaa, aliponda juhudi za kukusanya watu ili kuonesha kuwa chama hicho tawala bado kinapendwa.

      Akizungumza kutoka jimbo la mtama, mkoani lindi kwa njia ya simu, dk. Slaa alisema ccm inatakiwa kuwaambia watanzania na wananchi namna gani imetimiza ahadi zake ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, zikiwemo za kuwaletea wananchi maisha bora badala ya kusomba watu kwa magari.

      Dk. Slaa aliongeza kuwa, hali za watanzania kwa sasa ni mbaya mara mbili hata kabla ya uchaguzi mkuu na kila mtu amepigika vibaya, kinyume kabisa na namna alivyoahidiwa na watawala.

      Chadema pia kimewataka viongozi watakaohutubia wananchi, waseme waziwazi idadi ya viongozi wa ccm waliokwisha vuliwa magamba hadi sasa, tangu wawatangazie watanzania kuwa wanapambana na watu hao miaka miwili sasa.

      “ccm isijisumbue wala kujidanganya kusomba watu na kuaminisha umma kuwa bado inapendwa. Watu wameichoka kwa sababu imewadanganya.

      “tunataka waseme, wamewaleteaje watu maisha bora kama walivyowaambia wakati wa kampeni, na pili waseme ni magamba mangapi yamevuliwa tangu wajitape kufanya hivyo,” alisema dk. Slaa.


      kwani nani aliikataza chadema kumwaga ile pesa ya kanisa wanayopewa ???au hutafunwa na mbowe na slaa

    8. RukaaJuu Final

    9. #106
      DCONSCIOUS's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th October 2010
      Posts : 300
      Rep Power : 498
      Likes Received
      85
      Likes Given
      2

      Default Ccm acheni mipasho na ze comedy

      Ninacho ona ccm wanafanya taarabu na maigizo hapa jangwani hawaelezi wamefanya nn ila wanaeleza kuwanajua kuwa watanzania wanashida. Na wanachama wa ccm wakiambiwa mchele bei juu wana shangilia sasa haya sio maigizo

    10. #107
      lutolucy's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th June 2012
      Posts : 12
      Rep Power : 353
      Likes Received
      2
      Likes Given
      2

      Default Re: Ccm acheni mipasho na ze comedy

      Quote By DCONSCIOUS
      Ninacho ona ccm wanafanya taarabu na maigizo hapa jangwani hawaelezi wamefanya nn ila wanaeleza kuwanajua kuwa watanzania wanashida. Na wanachama wa ccm wakiambiwa mchele bei juu wana shangilia sasa haya sio maigizo
      Ndio maana wapo hapo. wapo hapo kwaajili ya kushangilia kila kitu kisemwacho. Kwani hukumbuki mitusi ya LUSINDE? nawalishangilia vile vile

    11. #108
      Kingilambago's Avatar
      Member Array
      Join Date : 1st May 2012
      Posts : 16
      Rep Power : 359
      Likes Received
      1
      Likes Given
      4

      Default Re: CCM kupokea wanachama feki leo kutoka CHADEMA

      Quote By mandieta
      Hata mm nina card ya chadema nairudisha leo!
      Hii alipaka mnyika.
      Bora umenena

    12. #109
      Ngoiva's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 16th November 2011
      Posts : 234
      Rep Power : 426
      Likes Received
      38
      Likes Given
      0

      Default Mkutano wa ccm jangwani ni faida kwa wamachinga

      Ni dhahiri kuwa mkutano wa ccm, ni faida kwa wafanyabiasha wadogo wadogo/wamachinga. Kwa kweli biashara ya maji, bagia, barafu, pipi, pamoja na juice. Mbali na hapo nape kaporosha matusi kikundi cha uamsho kwa kuwaita majambazi. Tusubiri majibu ya uamsho.

    13. #110
      Expedito Mduda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd September 2009
      Posts : 254
      Rep Power : 542
      Likes Received
      31
      Likes Given
      33

      Default Hivi ccm nani kawaloga?

      Nimeamini kwamba chama cha mapinduzi kimeishiwa, na inaonekana hakuna wa kukirudisha kwenye mstari. Nilifikiri kuiga kwao kufanya mkutano jangwani walitaka kujibu hoja zile zilizotolewa na wenzao wa CDM. Cha kushangaza wanapiga mipasho tu. Tukumbuke wenyewe ndo chama tawala. Eti wanajua maisha magumu ya wananchi. Eti UAMSHO ni mashetani. Malalamiko yote hayo ya nini. Wachukue hatua. Mafisadi wako chamani kwao huko huko. Wachukue hatua! CCM MMEKOSA MSHAURI KABISA KABISA NA SIJUI NANI ATAWAPONYA! CCM KWA HERI. Mtabaki kwenye historia. Hivi na hao mnaowapanga kuongea hamwoni wanawadondosha tu!!

    14. #111
      Profesa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Location : Anywhere in Africa
      Posts : 511
      Rep Power : 751
      Likes Received
      219
      Likes Given
      322

      Default Je CCM inapima mgombea wa uchaguzi ujao? Au wame-panic na upinzani?

      Mkutano huu sioni kama una mantiki kubwa kama nilivyotarajia, zaidi ya kile nilichosema awali, show-off dhidi ya CHADEMA, na kukurupuka pale unaposikia hoja za upinzani kiasi cha kujicontradict wenyewe. Sasa hapa sijajua kampeni za uchaguzi ndio zimeanza au?

      Uwiano wa mafanikio una kasoro kubwa sana utaeleweka kwa mtu ambaye hajaenda shule ila ukintajia idadi ya infrustructures, au idadi ya wanafunzi au vyuo ni lazima ueleze kulingana na idadi ya watu an ukubwa wa nchi, zaidi ya hapo ni kuwa wewe kama kiongozi unaamini unaowahutubia ni mambumbu so nani yuko hapo uwanjani ukiahca viongozi? Je ndio maana hamtaki kuwekeza kwenye elimu na vyuo na utafiti badala yake mnawekeza kwenye yale yatakayowaweka madarakani milele ikiwemo vyombo vya dola na siasa zenu? Huku mkihakikisha no critical mind emerge or prosper, ikiwemo kupuuzia kudumisha ubora wa elimu badala yake mnatudanganya na quantity!!!

      Ninachokiona ni kueleza serikali imefanya nini.... simply a typicle order from JK, sababu ndio stile yake ya hotuba habadiliki... angalau Mwakyembe ingawa nae sehemu kubwa pia alinasa kwenye mtego maana lazima atekeleze maamuzi ya mkutano wa maandalizi.

      Nataka kusikia miaka 50 ijayo Tanzania itafananaje, ili tuwabakize mtekeleze... hizi siku mbili zijazo mnatufanya tuendelee kuganga njaa kisa mnagombania kura wala hamjali nchi hii itafananaje huko mbeleni

      Dah ma-engeneers wa Siasa wako wapi? Vipi sikuizi hampeleki watu kusomea political engeneering Bulgaria na Cuba? Maana wale waliofuzu najua wengi ni wale waliosoma wakati wa vita baridi.

    15. #112
      mooduke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th October 2010
      Posts : 355
      Rep Power : 506
      Likes Received
      39
      Likes Given
      740

      Default Re: CCM na kubeba watu mpaka lini!?

      KINYESI ...... aCHA KUFANYA WATU HAYAWANI


      Quote By andrews
      ccm kuanzisha al shabab mikoa ya pwani

      KATIKA HALI YA KUWAGAWA WATANZANIA CCM IMEANZA KUWATUMIA BAKWATA KUWAGAWA WANANCHI.WAZIRI WA ELIMU NI MUISLAM MAKAMU WA RAIS MISLAM KATIBU ITIKADI CCM NI MUISLAM,RAIS WA NCHI MUISLAM MKUU USALAMA WA TAIFA NI MISLAM SASA VP LEOBAKWATA WASEME WANA FELISHWA HIZI NI MBINU CHAFU ZA CCM KUWATOA WANANCHI KWENYE WIMBI LA MAGEUZI YA KISIASA NA KUIINGIZA UDINI KWENYE JAMII NI HATARI NA NI LAANA KWA HAWA WANAMTANDAO HUU TUNASEMA ILI TANZANIA IWE NA AMANI 2015 CCM LAZIMA IONDOKE ISITULETEE MAAFA.WAMEANZA UAMSHO NA HAKUNA KARIPIO KALI LILILOTOLEWA KUONESHA CCM INAVYOHUSIKA VILIVYO KABLA YA UCHAGUZI 2015 WASHINDWE WALEGEE NA WASAMBARATIKE.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    16. #113
      dosama's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th December 2010
      Posts : 736
      Rep Power : 573
      Likes Received
      296
      Likes Given
      1

      Default CCM wachanachana bendera ya CHADEMA...

      Hiki ni kitendo kinachoruhusiwa kwenye siasa?

      Naomba msaada

      Quote By Gsana
      Ndugu wanajamvi,

      Katika siasa mbaya watawala wetu wanazoleta zitatupeleka pabaya. Ktk mkutano wa ccm leo jangwani mh magufuli kaomba wanaorudi ccm walete kadi,ghafla wakatokea wawili, babu na mtoto mmoja na apo apo kundi la watu kama 30 wakaja mbele na kadi ambazo kwa mbali zote ni mpya pamoja na bendera mbili.

      Ni kinyume na sheria zetu za nchi. Mh Magufuli kasimamia kuchana bendera na kadi zimechanwa vipande vipande mpaka Nape aliposema kadi ziachwe kuchanwa ila zikusanywe, vijana walikuwa wanaendelea na kuchana bendera ya CHDEMA, kwa maelekezo haya ya Nape na Magufuli kuchana bendera ya chama pinzani ni kuwaruhusu waovu wawe wanachana na hata kuchoma moto nembo za mahasimu wao na mwishowe ni kuandaa mapigano ya kichama na kuleta machafuko.

      NIMECHUKIZWA SANA NA MAAMUZI AYA YA NAPE NA MH MAGUFULI... MNAZIPELEKA SIASA SAFI KABURINI, MNAANDAA HATARI.

    17. #114
      KANYIMBI's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 6th November 2011
      Location : Tanganyika
      Posts : 178
      Rep Power : 416
      Likes Received
      23
      Likes Given
      63

      Default Re: Hivi ccm nani kawaloga?

      Ni kweli kaka, ni vizuri wangetumia hii nafasi kujibu tuhuma za kutoka chadema na kuelezea wananchi mambo ya maana kama;Kuvua gamba, Katiba mpya, ugumu wa maisha & Muungano. Kwa staili hii wanachokifanya jangwani ni kuendelea kukibomoa chama chao.

    18. #115
      omushaija's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th May 2012
      Posts : 37
      Rep Power : 362
      Likes Received
      6
      Likes Given
      9

      Default re: CCM wachanachana bendera ya CHADEMA...

      Binafsi hata siku ile VIONGOZI wa juu wa chadema walivyokanyaga kanyaga kadi za CCM huku wakichekelea sikufurahia hata kidogo. Hao waliochana kadi hapo ni wanachama walioondoka chadema na wamefanya hivyo kwa hasira za yaliyowafika huko.

      Si umemsikia Nape akiwakataza kabisa kuchanachana?

    19. #116
      kitali's Avatar
      Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Posts : 70
      Rep Power : 374
      Likes Received
      18
      Likes Given
      0

      Default Re: Hivi ccm nani kawaloga?

      yaani wananichefua haswa hao magamba,shit! i hate uuu

    20. #117
      Pastor Achachanda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th May 2012
      Posts : 280
      Rep Power : 412
      Likes Received
      9
      Likes Given
      3

      Default Yah: Jangwani-kwani hatuwezi kujitegemea?

      JF!Namuona Magufuli anaorodhesha barabara zilizojengwa na ccm kwa "misaada".Kwa nini asiseme "kwa hela zetu?"Mnaonaje JF

    21. #118
      Gsana's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th August 2010
      Location : Dar es salaam
      Posts : 2,233
      Rep Power : 889
      Likes Received
      217
      Likes Given
      30

      Default Kuchana Bendera ya CHADEMA

      Ndugu wanajamvi,

      Katika siasa mbaya watawala wetu wanazoleta zitatupeleka pabaya. Ktk mkutano wa ccm leo jangwani mh magufuli kaomba wanaorudi ccm walete kadi,ghafla wakatokea wawili, babu na mtoto mmoja na apo apo kundi la watu kama 30 wakaja mbele na kadi ambazo kwa mbali zote ni mpya pamoja na bendera mbili.

      Ni kinyume na sheria zetu za nchi. Mh Magufuli kasimamia kuchana bendera na kadi zimechanwa vipande vipande mpaka Nape aliposema kadi ziachwe kuchanwa ila zikusanywe, vijana walikuwa wanaendelea na kuchana bendera ya CHDEMA, kwa maelekezo haya ya Nape na Magufuli kuchana bendera ya chama pinzani ni kuwaruhusu waovu wawe wanachana na hata kuchoma moto nembo za mahasimu wao na mwishowe ni kuandaa mapigano ya kichama na kuleta machafuko.

      NIMECHUKIZWA SANA NA MAAMUZI AYA YA NAPE NA MH MAGUFULI... MNAZIPELEKA SIASA SAFI KABURINI, MNAANDAA HATARI.
      Jasusi and JokaKuu like this.

    22. #119
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,267
      Rep Power : 3568
      Likes Received
      3074
      Likes Given
      464

      Default re: CCM wachanachana bendera ya CHADEMA...

      Vyama Vingi Vya Upinzani Nchi za Magharibi Havina Bendera wala Kadi za Wanachama; Unajiandikisha kwenye Computer System basi wanajua wewe ni Chama Gani.

      Kubebe kadi na Bendera Hakuna... Kwahiyo hivyo ni vitu vya kuondolewa kwenye Vyama Vya Kisiasa

      Kinachobani ni Bendera ya Taifa Lenu tu na Bendera ya Rais Wa Nchi

    23. #120
      N-handsome's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd January 2008
      Location : Dar es Salaam
      Posts : 1,859
      Rep Power : 950
      Likes Received
      91
      Likes Given
      478

      Default Re: Kuchana Bendera ya CHADEMA

      Waache wanogeshe ngoma tu

    Page 6 of 8 FirstFirst ... 45678 LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...