Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

    Report Post
    Page 4 of 8 FirstFirst ... 23456 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 160
    1. #1
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,177
      Rep Power : 24273
      Likes Received
      4679
      Likes Given
      2297

      Default CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      CHAMA cha Mapinduzi (CCM), kimedaiwa kutumia mamilioni ya fedha kugharimia mkutano wake wa hadhara unaotarajiwa kufanyika leo katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, katika kile kinachoonekana kujibu mapigo ya mahasimu wao, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

      Kinyume na madai ya CCM kwamba lengo la mkutano huo ni kuhamasisha uhai wa chama na kutolea ufafanuzi mambo kadhaa yanayojitokeza ndani ya chama hicho, lakini duru za siasa zimedai kuwa, lengo kuu ni kujipima nguvu na CHADEMA ambacho wiki mbili zilizopita kilifanya mkutano wa hadhara katika viwanja hivyo na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi.

      Katika mkutano huo wa CHADEMA ambao ulirushwa moja kwa moja na kituo cha luninga cha ITV, maelfu ya wanachama waliofurika, walifika katika viwanja hivyo kwa njia zao bila kusombwa na magari, wala kupokea posho.

      Ili kuhakikisha mkutano wa leo unafunika ule wa CHADEMA kwa kupata watu wengi, CCM imeamua kuwasafirisha wajumbe wake kwa magari makubwa ya kukodi kama vile malori na mabasi kutoka kila tawi na kuwafikisha katika viwanja hivyo.

      Mbali ya kusombwa kwa magari, CCM pia imeamua kugawa bure fulana na kofia, na kuna madai kuwa chama hicho kitatoa posho kwa wanachama wake watakaohudhuria mkutano huo.

      Mkakati wa kuhakikisha mkutano huo unapata watu wengi, umesukwa kuanzia ngazi ya matawi, wilaya hadi mkoa kwa zaidi ya wiki moja sasa.

      Kana kwamba hiyo, haitoshi, CCM imeandaa baadhi ya wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongo Flava) watakaotumbuiza mapema kabla ya kuanza mkutano kwa nia ya kuwavuta wanachama.

      Baadhi ya wasanii hao ni Diamond, Marlaw, Frola Mbasha na wengine wengi ambao walipata kutumika wakati wa mikutano ya kampeni ya Rais Jakaya Kikwete.

      Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Uenezi na Itikadi CCM, Nape Nnauye alisema baadhi ya mawaziri na makada maarufu ndani ya chama hicho tawala, watahutubia katika mkutano huo.

      Alisema mkutano huo unaotarajiwa kuwa wa aina yake, ulipangwa siku nyingi kwa lengo la kuwakutanisha pamoja viongozi wa chama wa mashina na matawi waliochaguliwa hivi karibuni katika uchaguzi wa CCM unaoendelea katika ngazi mbalimbali.

      “Kuna vyombo vimesema mkutano huo utahutubiwa na Mzee Mkapa, Mwinyi. Hiyo sio kweli maana hata mwenyekiti wa chama taifa, Rais Jakaya Kikwete hatakuwepo jukwaani,” alisema Nape.

      Aliwataja mawaziri watakaohutubia mkutano huo kuwa ni pamoja na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano), Steven Wassira, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), Samuel Sitta, Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) na Kamati Kuu (CC), Abdulrahman Kinana na Nape mwenyewe.

      “Mzee Kinana atazungumzia masuala ya katiba na sheria na atatoa kauli kuhusiana na vurugu zilizotokea visiwani Zanzibar na kueleza msimamo wa chama kuhusu kikundi cha Uamsho cha visiwani humo kinachodaiwa kuwa chanzo cha vurugu hizo.

      “Wasira atajikita kwenye uchumi, Dk. Mwakyembe atazungumzia jinsi serikali inavyoshughulikia masuala ya uchukuzi, Magufuli atazungumzia utekelezaji wa ilani katika eneo la ujenzi na mkakati wa kuondoa foleni jijini Dar es Salaam,” alisema Nape.

      Kama ilivyokuwa kwa CHADEMA, CCM nao wameamua kurusha mkutano huo moja kwa moja kupitia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC) na Televisheni ya ITV na baadhi ya vituo vya redio.

      Aliwataka wananchi, wanachama wa CCM na wakereketwa kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo ili kuwasikiliza viongozi wa chama na serikali watakaozungumzia kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015.

      CHADEMA yaipa masharti magumu
      Akizungumzia mkutano huo wa CCM, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, aliponda juhudi za kukusanya watu ili kuonesha kuwa chama hicho tawala bado kinapendwa.

      Akizungumza kutoka Jimbo la Mtama, mkoani Lindi kwa njia ya simu, Dk. Slaa alisema CCM inatakiwa kuwaambia Watanzania na wananchi namna gani imetimiza ahadi zake ilizotoa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu, zikiwemo za kuwaletea wananchi maisha bora badala ya kusomba watu kwa magari.

      Dk. Slaa aliongeza kuwa, hali za Watanzania kwa sasa ni mbaya mara mbili hata kabla ya uchaguzi mkuu na kila mtu amepigika vibaya, kinyume kabisa na namna alivyoahidiwa na watawala.

      CHADEMA pia kimewataka viongozi watakaohutubia wananchi, waseme waziwazi idadi ya viongozi wa CCM waliokwisha vuliwa magamba hadi sasa, tangu wawatangazie Watanzania kuwa wanapambana na watu hao miaka miwili sasa.

      “CCM isijisumbue wala kujidanganya kusomba watu na kuaminisha umma kuwa bado inapendwa. Watu wameichoka kwa sababu imewadanganya.

      “Tunataka waseme, wamewaleteaje watu maisha bora kama walivyowaambia wakati wa kampeni, na pili waseme ni magamba mangapi yamevuliwa tangu wajitape kufanya hivyo,” alisema Dk. Slaa.

      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    2. Miaka 50

    3. #61
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,177
      Rep Power : 24273
      Likes Received
      4679
      Likes Given
      2297

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By GeniusBrain
      CRAAAAAAAAAAAAAAAAAP hakuna kitu muda huu matumbo yanawauma naona mko busy kuleta uongo wa kila aina, ila ikifika saa 6 mchana na kuhara sasa mtaanza, na mkutano ukiisha saa 12 mnapelekwa na hospitali kuongezewa dripu kwani maji yatakuwa yamewaishia mwilini, na msipo wahiwa ni kifo kabisa.

      GeniusBrain karibu, naona umemaliza kifungo!
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    4. #62
      MNAMBOWA's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th October 2011
      Posts : 714
      Rep Power : 526
      Likes Received
      76
      Likes Given
      31

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      wenye akili wanafahamu ccm ni chama kikubwa huwezi linganisha na chadema.

    5. #63
      kitero's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st February 2012
      Location : Kaskazini
      Posts : 516
      Rep Power : 469
      Likes Received
      98
      Likes Given
      48

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Kwamtindo wa malori, wasanii wa bongo flavor,T-shirt kanga na kofia ni lazima mtu achinjwe.wapo wengi wasiokuwa na khanga kofia na t-shirt so ni lazima waende wakapatiwe hivyo vyote.

    6. #64
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,177
      Rep Power : 24273
      Likes Received
      4679
      Likes Given
      2297

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By MNAMBOWA
      wenye akili wanafahamu ccm ni chama kikubwa huwezi linganisha na chadema.
      Na wenye akili kabisa wanafahamu CCM ni chama cha waizi huwezi linganisha na chama cha wazalendo CHADEMA
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    7. #65
      Elia's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th December 2009
      Location : magogoni
      Posts : 3,205
      Rep Power : 1119
      Likes Received
      490
      Likes Given
      829

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By Nduka
      Waulizeni viongozi wenu ruzuku wanapeleka wapi? Au ndio wanazotumia kujilipa posho na kujengea mahawala zao majumba? Chama kinashindwaje kuwabeba wachaga kutoka kimara hadi jangwani lakini kiweze kumpa mkataba wa kifisadi Josephine yule hawala wa Slaa?
      Nduka, We lazima unakesi na baraza la mitihani .....!!
      "Honesty is very expensive gift. Do not expect it from cheap people".
      -Warren Buffet


    8. RukaaJuu Final

    9. #66
      asigwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st September 2011
      Location : TANDHANIYA
      Posts : 4,389
      Rep Power : 1265
      Likes Received
      1209
      Likes Given
      1253

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      kila la kheri bwana ngoja mkutano umalizike tutaoa tathmini kama nguvu iliyo tumika italingana na matokeo yake

    10. #67
      AcinonyxJubatus's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd November 2010
      Posts : 110
      Rep Power : 456
      Likes Received
      13
      Likes Given
      26

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
      Tasia I likes this.

    11. #68
      MANI's Avatar
      JF Platinum Member Array
      Join Date : 22nd February 2010
      Location : CHINI YA MBUYU
      Posts : 1,915
      Rep Power : 954
      Likes Received
      569
      Likes Given
      632

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA. Watu wasombwa kwa malori

      Quote By Ezan
      Namimi naweza kupita pale huenda nitapata kitisheti cha kuendea shamba
      Pigia deki mkuu ukienda nacho shamba watu watajua na wewe ni walewale.
      " TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA"

    12. #69
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,297
      Rep Power : 12584
      Likes Received
      5841
      Likes Given
      771

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Mods, unganisha hii thread zimekuwa nyingi

    13. #70
      PauliMasao's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 26th November 2007
      Posts : 229
      Rep Power : 632
      Likes Received
      23
      Likes Given
      20

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Kuna tatizo gani wanachama wa CCM wakipatiwa usafiri kwenda kwenye mikutano ya hadhara? Mbona ni kawaida sana mashabiki kutoka Karatu na Moshi kuletwa na mabasi mjini Arusha kwenye mikutano ya hadhara ya CDM! nendeni Jangwani mkatuwakilishe halafu mtupe habari za maana kwenye toleo la kesho.

    14. #71
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,177
      Rep Power : 24273
      Likes Received
      4679
      Likes Given
      2297

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By ritz
      Mods, unganisha hii thread zimekuwa nyingi
      Kuna thread wenzako wanalalamikia mods hebu pitia huko
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    15. #72
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 18,297
      Rep Power : 12584
      Likes Received
      5841
      Likes Given
      771

      Default

      Quote By Mungi
      Kuna thread wenzako wanalalamikia mods hebu pitia huko
      Kama wewe unavyolalamika na malori...kuna thread zaidi ya 10 zote za Jangwani.

    16. FJM
      #73
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,175
      Rep Power : 2569
      Likes Received
      5327
      Likes Given
      4587

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Nimeona jina la Kinana kwenye list ya watu watakaohutubia leo Jangwani. Kama ni kweli basi nategemea Kinana atatoa tathmini ya biashara ya meno ya tembo pamoja na usafirishaji wa wanyama hai.

    17. #74
      Tasia I's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st April 2010
      Posts : 1,139
      Rep Power : 693
      Likes Received
      150
      Likes Given
      129

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By tindikalikali
      maskini baba/mama/kaka/dada zangu hawa..!
      natamani wangeijua kweli ili kweli iwaweke huru.

    18. #75
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,177
      Rep Power : 24273
      Likes Received
      4679
      Likes Given
      2297

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By ritz
      Kama wewe unavyolalamika na malori...kuna thread zaidi ya 10 zote za Jangwani.
      Wenzako wanalalamika kwamba thread zao zinaunganishwa kwenye thread zingine!
      "Peace is not simply about the absence of violence. It is defined by the presence of fundamental liberties and the prevalence of economic opportunities."

    19. #76
      Tasia I's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st April 2010
      Posts : 1,139
      Rep Power : 693
      Likes Received
      150
      Likes Given
      129

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By AcinonyxJubatus
      Kizuri chajiuza kibaya chajitembeza.
      imepita bila ubishi.

    20. #77
      nundaz's Avatar
      Member Array
      Join Date : 8th June 2012
      Posts : 16
      Rep Power : 353
      Likes Received
      4
      Likes Given
      0

      Default

      tatzo nape na ccm wamelala! m4c inavuruga akili na bado huo ni mwanzo tu!

    21. #78
      Mchwechwele's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 8th January 2011
      Posts : 1,139
      Rep Power : 651
      Likes Received
      327
      Likes Given
      82

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Maskini hana Mpambe

    22. #79
      Crashwise's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2007
      Location : Safarini
      Posts : 13,127
      Rep Power : 14289
      Likes Received
      4015
      Likes Given
      3273

      Default

      Quote By GeniusBrain
      Utamaliza maneno yote leo, ila kuchinjwa kuko pale pale

      mimi nikiwaambia watu kuwa ccm ni chama cha mauji wana kataa, msome masaburi brain halafu kumbuka mwenyekiti wa ccm usa river alie muua kikatili mwenyekiti wa chadema kata ya usa river

    23. FJM
      #80
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,175
      Rep Power : 2569
      Likes Received
      5327
      Likes Given
      4587

      Default Re: CCM yamwaga Mamilioni kuivaa CHADEMA; Watu wasombwa kwa malori

      Quote By MNAMBOWA
      wenye akili wanafahamu ccm ni chama kikubwa huwezi linganisha na chadema.
      Kwa nini wanasomba watu na malori? Kama kweli CCM ni chama kikubwa na kama kweli kama wanajiamini waache kusomba watu na malori halafu tuone Jangwani kukoje.

    Page 4 of 8 FirstFirst ... 23456 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...