Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

    Report Post
    Page 1 of 6 123 ... LastLast
    Results 1 to 20 of 103
    1. #1
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana Gani?

      Wanabodi,

      Kufuatia chokochoko ya kuuchokoa Muungano ilioanzishwa na kikundi cha Uamsho huko Zanzibar, zimeanza kutolewa hoja mbalimbali ikiwemo Watanzania tupewe fursa kuujadili Muungano na ikibidi ipigwe kura ya maoni kuwauliza Watanzania na Wanzanzibari kama wanautaka muungano, jee wanataka muungano wa aina gani, na endapo hawautaki, process ya kuuvunja rasmi aianze.

      Wako wengi wanaupenda muungano na wangependa uendelee ila uboreshwe!. Pia wako wanao ona sasa imetosha na muungano uvunjwe!.

      Maudhui ya mada hii ni kuwaeleza wanabodi, jambo muhimu liitwalo "kuridhia" ambapo serikali zote zilipaswa kuuriidhia huo muungano kwa utaratibu unaoitwa "RATIFICATION" ambapo ni serikali ya Tanganyika pekee ndio iliyofanya process rasmi ya "ratification", Zanzibar, haikufanya process bali ilitamka tuu kwa maneno ya mdomo bila tamko lolote rasmi la maandishi, na badala yake, hati ya ratification ya Zanzibar, iliwasilishwa kwenye bunge la Tanganyika na dunia kutangaziwa muungano uliridhiwa pande zote!.

      Kwa vile Zanzibar, haikuuridhia rasmi Muungano, kama ni kweli hizi chokochoko za Uamsho ni uthibitisho kuwa sasa Zanzibar inataka kujitoa katika muungano wetu huu adhimu, kisheria, mlango uko wazi, yaani wide open for Zanzibar to just walk out, with no regret and no strings attached kwa sababu hawakuuridhia ule mkataba wa muungano in then first place!, hivyo mkataba huo hauko binding kwao!.

      Mada yangu hii inakuwa na sehemu zifuatazo.

      1. Kuridhia ni Nini (Ratification).
      2. Rafication Hufanyikaje.
      3. Mikataba ya Kimaifa ni nini? na Jee Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Mkataba wa Kimataifa?.
      4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
      5. Process ya Ratification kwa Upande wa Tanganyika.Process ya Ratification kwa Upande wa Zanzibar.
      6. Hadaa ya Ratification ya Zanzibar, ilipangwa na nani na kwa nini?.
      7. Kukosekana kwa ratification upande wa Zanzibar kunamaanisha nini.
      8. Pamoja na kutokuwepo ratification, Jee Muungano ni halali?
      9. A Way Forward 1:Tudumishe Muungano?, Muungano wa Aina Gani?.
      10. A Way Forward 2:Tuuvunje Muungano?. What are the Consequences?.

      1. Kuridhia ni Nini (Ratification).
      Kuridhia, au ratification, ni process inayofanywa kwa nchi husika kuridhia mikataba ya kimaifa ili kuipa uhalali wa kisheria kutumika katika nchi husika. Mfano mzuri ni mkataba wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika ni nchi, na Zanzibar ni nchi, hivyo ule mkataba wa muungano ni mkataba wa kimataifa.

      Jee kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe?. Jibu ni hapana, sio kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe, ili mkataba wa kimataifa uridhiwe lazima mkutaba husika uwe na kipengele kinacholazimisha mkataba huo kuridhiwa. Tukirudi kwenye mfano wetu wa mkataba wa muungano, kipengele cha VIII cha Articles of Union, kinalazimisha process ya ratification lazima ifanyike ili kuuhalalisha mkataba ule.

      (viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

      Nyerere na Karume wangeweza kuamua wakishasaini makubali yale iishie hapo, ingekuwa hivyo hivyo hitaji la kuridhia lisingekuwepo!.

      2. Rafication Hufanyikaje?.
      Kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwe ni ya maandishi, vivyo hivyo, ratifikation lazima ifanyike kwa maandishi na sio kwa kauli.

      Kwa bunge letu, masharti ya kuridhia hufanywa kwa mujibu wa kifungu cha 63(3)(e) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinachotamka kuwa, Bunge litajadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa na kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni ya 114(11) ya 2007.
      1. Waziri husika huwasilisha mezani kwa spika mkataba husika
      2. Spika ataipa kamati husika kupata maoni yake
      3. Kambi ya upinzani itapewa fursa ya kuandaa maoni yake.
      4. Mkataba huo utatangazwa rasmi kwenye order paper ya siku ya kuwasilishwa
      5. Waziri atawasilisha, kisha maoni ya kamati, maoni ya kambi ya upinzani na majadiliano.
      6. Bunge litakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu
      7. Bunge litarudi kama bunge na kuridhia mkataba husika
      8. Mkataba huo unakuwa sehemu ya sheria za nchi,
      9. Unasainiwa na rais na kutangazwa katika gazeti za serikali GN.
      10.Ndio unakuwa umeridhiwa, yaani ratified!.

      3. Mikataba ya Kimaifa ni nini? na Jee Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ni Mkataba wa Kimataifa?.
      Mkataba wa Kimataifa, ni mkataba kati nchi moja na nchi nyingine, au mikataba yote ya jumuiza za kimataifa ambayo nchi ama hutakiwa kuridhia, au kulazimishwa kuiheshimu hata kama haikuridhia. Mikataba hii au itifaki mbalimbali (protocals), hupaswa kuridhiwa kabla haijawa sheria kwa nchi husika.

      Mfano Tanzania iliridhia mkataba wa mahakama ya kimataifa ya Biashara, ICC. Dowans iliposhinda ile kesi, imepaswa kuisajili hukumu hiyo kwenye mahakama zetu (ratification), ili hukumu hiyo igeuke sheria zetu, (domestic law) na kutekelezwa. Watu humu walipiga sana kelele, nilipouangalia mkataba ule humu jf, nikawaambia wana jf wenzangu, hatuna pa kutokea, tozo ile italipwa tuu mara baada ya tozo hiyo kusajiliwa, kinachoendelea sasa ni delaying tactics ambayo nayo tutailipia dearly!.

      Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni mkataba halali wa kimataifa wenye sifa muhimu za mkataba, japo una mapungufu mengi kubwa likiwa ni kitu kinachoitwa "Privity of Contrac" ambapo mkataba ulikuwa kwa lugha ya Kiingereza na signatory mmoja alikuwa msomi anaejua kusoma na kuandika kiingereza, wakati signatory wa pili hakujua kusoma, kuandika wala kiingereza, hivyo alisaini kwa dole gumba!.

      Ufafanuzi zaidi kuhusu Muungano kuwa ni mkataba wa kimataifa, unapatikana pia katika ukurasa wa kwanza wa andiko la
      Prof. Shivji kwenye kitabu cha "The Legal Foundation of the Union in Tanzania and Zanzibar Constitution, DUP, 1990.

      Kwa faida ya wasoma kimombo, tembelea
      http://www.scribd.com/doc/45109599/T...A-AND-ZANZIBAR

      4. Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
      Kila mtu anaelewa Mkataba wa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ulitiwa saini na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Mjini Zanzibar Hapa nitawapa tuu ilivyokuwa kabla na kilichofuata.
      Baada ya Mapinduzi ya Zanzibar, na Nyerere kumsaidia Karume kumshughulikia Johh Okello, Karume alikuwa bado ana wasiwasi wa kudumu kwake kama Mwenyekiti wa BLM, kwa kuzingatia Karume hakushiriki mapinduzi yale, Kiongozi wa mapinduzi alikuwa ni John Okello, Karume alikimbilia bara kujificha! (Japo ilikuja kutangazwa ati alikuwa akiwapeleka wanae Amani na Ali waliokuwa wakisoma kwao Karume (Malawi). Okelo ndie alikuwa Mwenyekiti wa BLM na alimuita Karume kuwa mtangazaji kufuatio kuwa na Kiswahili safi. Karume akamzunguka Okello na kwa kusaidiwa na Nyerere, Okello alishughulikiwa na Karume kuitwaa nafasi ya Mwenyekiti wa BLM!.Kwa vile Karume hakushiriki actively kwenye mapinduzi halisi, alikuwa na wasiwasi wakati wote kuwa wale makamanda wangemrudi!, thanks kwa ulinzi wa askari 300 wa Nyerere, vinginevyo hata hiyo 1971, asingefika!.

      Mwezi Machi, 1964, Nyerere alizungumza na Karume kuhusu Muungano, Karume alikubali hapo hapo na kutaka Press Conference iitishwe siku hiyo hoyo watangaze kuwa wameshaungana na kuwa nchi moja, Nyerere Rais, Karume Makamo. Mwalimu alimgomea Karume na kumwambia afanye siri ili taratibu zifuatwe.

      Mwanzoni mwa Aprili, Mwalimu alimuita AG waTanganyika, Rowland Brown na kumwambia aandae mkataba wa muungano na uwe siri. Kule Zanzibar, Karume akampa likizo AG wa Zanzibar, Wolfgang Dourado ili isitie kauzibe. Akatafutwa Mwanasheria wa Uganda, Daniel Wadada Nabudere (kakaye mwandishi mashuhuri, David Wadada Nabudere) kutoa ushauri kwa Karume kuhusu muungano.

      Tarehe, 22 April, 1964 Nyerere aliyeandamana na Rashidi Kawawa, Oscar Kambona na Job Lusinde walitua ghafla Zanzibar na kwenda moja kwa moja Ikulu ya Zanzibar, wakiwa na hati za muungano na Karume alitakiwa azisaini. Wakati wa utiaji saini huo, ulishuhudiwa pia na Abdallah Kassim Hanga, Abdul-Aziz Ali Twala na Salim Rashidi.

      Karume alitaka kumtumia mwanasheria huyo wa Uganda kusaini kwa niaba ya mwanasheria mkuu wa Zanzibar, ila Nabudere akakataa na kusisitiza lazima zisainiwe na Mwanasheria wa Zanzibar!. Ndipo Rowland Brown akatinga na Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot aliyesimama nafasi ya Dourado!. Hati za muungano zikasainiwa!. Baada ya hapo Nyerere na ujumbe wake wakawaa pipa lao na kurejea Dar!.

      Mkumbuke mpaka Karume anasaini, hajaliambia chochote BLM, siku hiyo jioni Aboud Jumbe aliyekuwa Pemba, ndipo akaelezwa na Karume kilichotokea asubuhi, akashangaa sana!. Jambo kubwa kama hilo limefanyika vipi, BLM, hawajui kitu!.

      Ni baada ya kusainiwa, Bunge la Tanganyika likatunga sheria ya Muungano, ili kuuthibitisha hati zile, 'ratification', na BLM nalo lilipaswa kukaa na kuridhia hati zile!.

      Muungano Ulithibitishwa rasmi na Bunge la Tanganyika kwa kutungiwa sheria na na ikatolewa uthibitisho mwingine uliosainiwa na Fifffoot kuonyesha kuwa BLM liliketi na kuridhia, lakini kiukweli BLM halikukaa, kujadili, wala kupitisha chochote kule Zanzibar!. Kila kitu kilifanywa bara!.

      Aprili 27, 1964 Nyerere na Karume, walitinga katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano zilizosainiwa na Nyerere na Karume, na documents za ratification na tangu hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

      Siku hiyo ya Aprili 27, 1964 ndio siku wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai. Baada ya hapo, Bunge la Muungano likakamata madaraka yote!.

      5. Process ya Ratification kwa Upande wa Tanganyika.Process ya Ratification kwa Upande wa Zanzibar.
      1.
      Msingi mkuu wa ratification mkataba wa muungano ni kifungu hiki kwenye hati za muungano.

      Article VIII of the Articles of Union provides:“ These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples Republic of Zanzibar in conjunction with the cabinet of ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of United Republic and of Zanzibar in accordance therewith2. Lengo la kifungu hicho, ni kwa vile muungano ni mkataba wa kimataifa, ili mkataba huo upate uhalali wa kisheria katika nchi husika, lazima mkataba huo uridhiwe na nchi husika, hivyo kifungu hicho kilimaanisha bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi, walipaswa waridhie mkataba huo kwa kuutungia sheria mahsusi ili kuuhalalisha kisheria ndani ya nchi zao!.

      2. Kuridhia au kutoridhia, hakuondoi uhalali wa mkataba, bali unaondoa uhalali wa kisheria, pale yule ambaye alikosa uhalali wa kisheria pale mwanzo, akiamua hautaki tena ule mkataba, hawajibiki kuuvunja mkataba, but he can just walk away!.

      3. Baada tuu ya hati za Muungano kutiwa saini ile Aprill 22 kule Zanzibar, Mwanasheria Mkuu Tanganyika enzi hizo, Rowland Brown aliandaa ratification na kupelekwa kwenye kikao cha bunge la Tanganyika, likapitisha ratification ile asubuhi ya Aprili 26, 1964 kwa kutunga sheria No. 243 ambayo ilitangazwa kwenye gazeti la serikali ya Tanganyika, GN No. hivyo kutimiza matakwa ya kile kifungu namba viii cha mkataba wa muungano.

      4. Wakati hayo yakiendelea huku Tanganyika, Zanzibar nao kupitia Mwanasheria Wake Mkuu, Wolfgang Dourado, alipaswa kuandaa hiyo sheria ya ratification kule ikiitwa Decree, ili Baraza la Mapinduzi likae na kuipitisha hivyo kuutambua rasmi muungano kisheria. Hili halikufanyika lkwa sababu Dourado alipewa likizo ya siku 7 akapumzike nje ya nchi!. Aliporudi, seven day leter, akakuta game over!. Akaishia kulalamika kichini chini maana angetoa sauti, sijui kama hata unywele ungepatikana!. Ushahidi ni kauli ya Dourado Mwenyewe “I myself have been the Zanzibar Attorney General and Minster responsible for justice between 1984 and 1989. At that time I managed to peruse all the statute books of Zanzibar from 1964 and 1979 when the Revolutionary Council was acting as a legislative Assembly cum the Cabinet. No ratification law or any law to that effect is there. I was not myopic, but even if I was, the first Attorney General of Zanzibar after the Revolution had also testified the same that no law ratifying the Articles of unionexists on the Statute Books of Zanzibar.” Dourado aliyasema hayo katika andiko lake la “The Consolidation of Union” alilowasilisha kwenye semina ya Tanhanyika Law Society, Julai 7, 1983 hapa jijini Dar es Salaam.

      5. Mpaka Mungu amemuita Dourado mbele ya haki, msimamo wake ulikuwa “No law ratifying the Articles of the union of 1964 exists on the statute books of Zanzibar., I as a Principal Legal adviser to the Zanzibar government was not consulted ……… Zanzibar therefore did not have legal or constitutional advice from its Principal Legal adviser.”

      6. Badala yake, Solicitor General wa Tanganyika, PRN Fifoot ndiye alieandaa ratification document ya Zanzíbar ambayo aliisaini yeye na kumpatia Karume ile April, 27, 1964, Karume aiwasilishe kwenye bunge la Tanganyika ile siku Nyerere na Karume walibadilishana hati pale Karimjee. Hati ya aliyoiwasilisha Nyerere was a genuine ratified document iliyokuwa ratified na bunge la Tanganyika!. Hati aliyowasilisha Karume, was a fake one as if ni BLM ndilo nalo limefanya hiyo rafication kama lilivyofanya bunge la Tangayika!, It was just a make belive, kuizuga jumuiya ya kimataifa na hapo ndipo hata hao CIA na iteligensia yao wakaingizwa chaka na kubaki kupiga tarumbeta ya ratification kuwa ilifanyika!.

      7. Hata kama Fifoot aliiandaa hiyo ratification ya Zanzibar, kwa nini hakumpa Douradau naibu wake, ili aisaini na kuipitisha kwenye kikao cha BLM ili angalau ionekane ilipitishwa Zanzibar?!.Kwa vile Zanzibar hawakuwa na bunge, Baraza la Mapinduzi ndilo lililokuwa Bunge, Baraza la Mawaziri na Mahakama, kwanini ile ratification iliyoandaliwa bara, isipelekwe tuu na kupigwa rubber stamp kwenye BLM ili kuipa uhalali kuwa ni kweli BLM waliridhia na kuratify?!.

      8. Siku ile ya April 27, 1964, wakati Nyerere na Karume walipotinga ndani ya bunge la Tanganyika, kubadilishana hati za muungano zilizo kuwa ratified,Nyerere aliwasilisha hati halali ya muungano ilikuwa ratified kihalali na bunge la Tanganyika na kutangazwa rasmi kwenye gazeti la serikali, GN lakini Karume aliwasilisha ile hati iliyosainiwa na Fifoot alijifanya Dourado na kuziwasilisha hati za muungano kwenye bunge la Tanganyika as if ni kweli BLM lilikaa likajadili na kuridhia hizo hati za muungano, na Karume sio tuu amesaini hizo ratification bila kuzipitishia BLM, bali pia amezitungia Decree na kuitangaza katika GN hiyo hiyo ya Tanganyika japo kwenye GN ya Zanzibar sheria hiyo haipo!.

      9. Kisheria, kwenye sheria ya mikataba, place of contact maters much as far as domestic laws are concerned, Ule mkataba wa muungano ni international contract, unaweza kusainiwa popote ndio maana Mwalimu Nyerere na time yake, walifunga safari kwenda Zanzibar. Process ya ratification sio international contact, ni domestic contact kutumia domestic laws (municipal) ambapo ratification hupaswa kufanywa na bunge husika likiwa nchi husika. Bunge la Tanganyika lilitimiza wajibu wake hivyo ratification ya Tanganyika ni legal. Kitendo cha ratification ya Zanzibar kuandaliwa na Fifoot wa Tanganyika na kusainiwa nae, halafu Karume kukabidhiwa sheria hiyo wakati sgeria za Zanzibar kwa wakati huo zilikuwa Decrees na kuiwasilisha bunge la Tanganyika, tangazo la ratification kutolewa kwenye GN ya Tanganyika na sio ya Zanzibar, ni mambo yanaifanya hiyo ratification kuwa voidable na sio void!

      10. Hoja ya “privity’ to contract na “capacity” to contract pia ipo kwa Karume kama Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, alikuwa na capacity to contact kama Karume kwenye zile articles of union, lakini kwenye Ratification, Karume hakuwa na Capacity ya kusaini sheria ambayo haikutungwa na BLM, na kusainiwa na Fifoot badala ya Dourado, na sheria hiyo kutopitishwa na BLM lakini akaiwasilisha as if imeridhiwa na BLM!, na Fifoot hakuwa na capacity to contract kwa niaba ya Dourado!, tena (ninahisi Fifoot alifanya “misrepresentation kujifanya Dourado ndio maana kuna uwezekano mkubwa, Karume hakupewa tena zile original documents!, alikuja mikono mitupu, na kurudi mikono mitupu ndio kule Zanzibar, hizo documents are no where to be seen!!). Emphasis mine!
      11. Hata hivyo, kuna mabishano makubwa kati wanazuoni na wasomi mbalimbali wa sheria kuhusiana na hii issue ya ratification. Mwalimu wangu, Prof. Shivji amesema japo hakuna kumbukumbu zozote kuwa BLM liliridhia, kwa vile BLM limeipitisha sheria ya muungano, huko ndiko kuridhia kwenyewe!, kwa hiyo kwa Shivji, muungano uliridhiwa!.

      12. Aliyekuwa kiongozi wa kambi ya upinzani kwenye BLW, Hon. Abubakar Khamis Bakary ambaye ndie aliyetoa posa ya ndoa na CCM kule BLW na kuunda SUK ambapo kama mshenga, amezawadiwa uwaziri wa sheria anapingana na Prof. Shivji kwa kusema kuwa sheria ambayo haikutungwa na BLM wala haikupitishwa na BLM, sio sheria halali kwa Zanzibar!.

      13. Pamoja na Kutofautiana na Shivji kuhusu uhalali wa ratification, lakini Mhe. Bakari anakubaliana na Shivji kuwa muungano ni halali, kwa sababu, licha yakutokuwepo official ratification kutoka Zanzíbar, hakuna Wanzanzibari wowote waliochukua hatua zozote za kupinga au kulalamika, hivyo hiyo ni dalili kuwa Wanzanzibari wameukubali muungano impliedily not expressly!.

      14. Mwanasheria mwingine wa Zanzibar, al maaruf, Ali Salehe, mwandishi na mtangazaji wa BBC, yeye anashikilia, kwa kwa vile muungano haukuridhiwa, lazima uridhiwe ili kuupa nguvu ya kisheria Zanzibar!. Hivyo anasema ratification ifanyike!. Na hapa ndipo na mimi niliposimamia kuwa Wanzanzibari wafanye ratification kama kweli hawautaki tena muungano, BLW likatae ku ratify ili mlango wa kutokea uwe wazi, wide open!.

      15. Prof. Haroub Othman ametofautiana na Shivji kwa kusema wajumbe wawili wa BLM, Abrahman Mohamed Babu na Khamis Abudulah Ameir, walimweleza kuwa BLM walijadilili hati za muungano na kuridhia! (bila maandishi wala kumbukumbu?). Prof. Haroub anadai siku anaelezwa hayo walikuwa club ya YASU akiwa anacheza na katoto fulani ambacho kalikuwa bado hata hajabalehe, kakiitwa Ali Juma Shamhuna!.

      16. Kufuatia uwepo wa document ya ratification huku bara, na Zanzibar kimataifa ilikufa rasmi siku ile ya April, 26, 1964, hakuna tena anaejali kama hizo ratification documents zili fojiwa huku bara, ndio maana hata tume ya Nyalali, ilizihalalisha na kimataifa everthing is ok na humo humo ndimo hao majasusi wa Marekani, walikolalia na wote wanaoamini muungano uliridhiwa, japo ni kweli kwa bara muungano uliridhiwa kwa kauli na matendo, kwa Zanzibar, uliridhiwa kwa kauli bila matendo!, na sasa tunasikia kauli za kupinga na matendo ya akufukuzaye!.

      17. Kiukweli Karume aliliendesha BLM kibabe sana, yeye kama Rais, Jaji Mkuu na Spika, wale wote waliopingana naye, hakuna ajuaye kilichowakuta ili walishughulikiwa kimya kimya na hata miili yao haikubahatika kuonekena (inasemekana walining’inizwa jiwe shingoni na kutoswa baharini!. Kina Babu kuona hivyo, wakajitimkia zao kabla ya kuwakuta, hayajawakuta. Uvumilivu ulipowashinda waliobaki, nao wakamshughulikia Karume!. (Naamini inteligensia ya Mwalimu alishauona mwelekeo wa Karume kwenye majaaliwa ya muungano, hivyo nae akaacha ya kumkuta yamkute, muungano udumu!.

      18. Baada ya Karume, Aboud Jumbe akaukwaa urais. Dourado akamjulisha Jumbe kuhusu kukosekana kwan proper ratification na iliyopelekwa UN is fake!, wakaandaa document kuujulisha ulimwengu kuhusu hilo!. Seif Sharif akamtonya Nyerere, Jumbe akashughulikiwa ipaswavyo, huku Dourado akaozea jela!. Tukatangaziwa “kuchafuka kwa hali ya hewa Zanzibar” bila kuelezwa kisa ni absence ya proper ratification!.

      19. Wanzanzibar ni watu wazito sana kujifunza, licha ya kujua kilichomkuta Jumbe kilihusu kuutishia muungano, Dr. Salmini nae akataka kucheza karata yake zile siku zake za mwisho mwisho alinukuliwa akisema, wao wanayatambua yale mambo 11 tuu ndio ya halali, hivyo akajenga hoja kubadili katiba aongeze kipindi cha tatu ili ayashughulikie!. Tiss ilimshughulikia yeye na timu yake yote wakatupwa kando!. Hamshaghai kwa nini Salmin baada ya kustaafu hakuitwa popote kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli rasmi?, na yule dada yetu naye akaporwa!.

      20.Kupitia hoja hizo na nyingine ambazo sikuzitaja, Mimi Pasco wa JF, kwa Mamlaka niliopewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Chini ya Kifungu cha "Freedom of Expressions", Sasa Natamka Wazi kuwa Muungano Kati ya Tanganyika na Zanzibar, Haukuwa Ratified Properly in Zanzibar!. Ila pia Nasisitiza, Muungano Huu ni Halali, japo ulikosa uhalali kwa njia ya Expressly in Zanzibar, umepata uhalali huo Impliedly!.

      Angalizo.
      Unaruhusiwa kucoment chochote wakati mada hii ikiteremka, just coments tuu ila naomba sana, maswali juu ya kuhusu hii mada kabla sijafika mwisho, maana sitakujibu mpaka nimalise, ila nikishamaliza sura zote kumi, nitapokea maswali, maoni au mapendekezo. Endepo uliuliza swali kabla sijafika mwisho, na hatimaye ulikuja jibu la swali lako kwenye mada za mbele, sitakujibu upya bali nitakurefer kwenye majibu ya swali lako.

      Hii mada siyo accademic paper, naishusha kwa level ya mwananchi wa kawaida wa Tanzania ambaye ni darasa la saba!. Hata hivyo kwa faida ya wasomi ambao wangependa kuzama deep, mwisho, nitawawekea, references za kusoma zaidi.

      Natanguliza shukrani.

      Pasco.
      Last edited by Pasco; 11th June 2012 at 01:47.

    2. FemaTV & Radio

    3. #2
      Eng. Y. Bihagaze's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 8th September 2011
      Location : Czech(but now in DAR)
      Posts : 766
      Rep Power : 5116
      Likes Received
      583
      Likes Given
      111

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Labda nianze

      Pasco, usijiumize sana babangu, unajikamua bure Kwa nondo unazotaka kujikunja nazo .. Kiini cha suluhu umeshakigusia kwamba serikali haiwezi kufanya maamuzi yake pasipo kuwauliza wananchi wake, Na hii ni Kwa kupitia kura ya Maoni..
      Nadhani kuna dhana kwamba Upande mmoja wa Muungano hawautaki uchumba huu.. Kwa upande wa Bara wananchi wengi hawana uelewa chanya Wala hasi kuhusu muungano .. Wanachojua Zansibar hawatutaki sisi wabara.. Kwa mantiki hiyo kuna Hoja ya baadae ya kujadili mfumo wa upigaji kura..

      Bara yenye wakazi zaidi ya milioni 48 sasa Na Zanzibar yenye wakazi milioni 1.2 ambao ni asilimia 2.4 ya wakazi wa inayoitwa JMT, kura lazima itakuwa Na uwalakini.. Kama watu wote Zanzibar watapiga kura ya kuukataa Muungano, na wakazi milioni 3 tu wa bara wakaukubali, je Hoja ya muungano itabaki MTAMBUZI?

      nadhani labda mjadala makini tuuelekezee kwenye suluhisho la nini kifanyike Na sio uhalali Wa Muungano..

      Kama Muungano una madudu, kwanini madudu hayo yasimwagwe hapa Na tukayadadavua na kupata suluhu linaloweze kuwa msaada Kwa viongozi ambao wanaumiza vichwa Na mzimu huu unaoitwa MUUNGANO?
      Last edited by Eng. Y. Bihagaze; 8th June 2012 at 21:25.
      Pasco likes this.

    4. #3
      Ndjabu Da Dude's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th August 2008
      Posts : 2,440
      Rep Power : 11661
      Likes Received
      305
      Likes Given
      138

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Quote By Pasco
      ambapo ni serikali ya Tanzania pekee ndio iliyofanya process ya "ratification", Zanzibar, haikufanya!.
      Serikali ya Tanzania au serikali ya Tanganyika?
      Pasco and sweke34 like this.

    5. #4
      bumes's Avatar
      Member Array
      Join Date : 26th May 2012
      Posts : 58
      Rep Power : 363
      Likes Received
      12
      Likes Given
      1

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      pasco go and advise the zanzibari all your findings, God knows the end of it all.

      To me all those things are irelevant what people need to say is that we are no longer confortable with this Muungano so we have decided to detach ourselves from it.

      Suppose there is a referendum and 51% zanzibari says we dont want Muungano and 49% says they need it how are you going to treat the minority, are going to ingnore them?.

      Kuubuka Mwalimu Nyerere alisema zambi yakujitenga hayitakufa bali yitaendelea. To me I can say he prophesized, there is every possibility that Muungano shake maybe even break, the milk and honey people hope for will end up a nightmare.

      Best of lucky
      Pasco likes this.

    6. FJM
      #5
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,174
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5323
      Likes Given
      4587

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Pasco, wacha uhuni. Umeanzisha mada hii jana na leo ukasema ungeleta evidence, badala ya kujibu maswali, unakimbiilia kuanza thread nyingine kwa mtindo ule ule wa porojo. That's not how a man should behave. And you had the guts to tell people namna ya kuchangia! Pathetic.
      Yo Yo and Pasco like this.

    7. Miaka 50

    8. #6
      Gwankaja Gwakilingo's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th January 2012
      Location : Masoko Busisya
      Posts : 1,199
      Rep Power : 608
      Likes Received
      326
      Likes Given
      32

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Nayazingatia maamuzi yako nasubiri ukifika ya kumi Comrade
      Pasco and FJM like this.
      kwa pamoja ni lazima twende mbali zaidi ya maneno yetu...........039.mac

    9. FJM
      #7
      FJM's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 7,174
      Rep Power : 2568
      Likes Received
      5323
      Likes Given
      4587

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Pasco, in case una matatizo ya memory, tafadhali angalia tena huu uzi,

      http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...idhania-5.html

      Siku nzima watu wanasubiri ulete "makatarasi" then unakimbilia huku kama kuku anakimbia kufanywa kitoweo cha x'mas. Huku ni kudharau wanaJF. Be a man na ujibu hoja ulizoweka kiporo tangu jana.
      Pasco likes this.

    10. #8
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,657
      Rep Power : 717
      Likes Received
      291
      Likes Given
      36

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Kura ya maoni kuamua uwepo ama usiwepo muungano ni muhimu sasa kuliko wakati mwingine wowote, may be itasaidia makanisa na wakristo kuwa salama.
      Pasco likes this.

    11. #9
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Pasco,
      Hivi Mapinduzi ya Zanzibar yalikubaliwa na wananchi? au niulize hivi yaliongezwa na vyombo gani na hata kutambuliwa na nchi gani. Ukisha hapo tutaendelea maana kwa kila hatua unayotaka kuiweka.
      August and Pasco like this.
      Exploration of reality

    12. #10
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      1. Kuridhia, au ratification, ni process inayofanywa kwa nchi husika kuridhia mikataba ya kimaifa ili kuipa uhalali wa kisheria kutumika katika nchi husika. Mfano mzuri ni mkataba wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika ni nchi, na Zanzibar ni nchi, hivyo ule mkataba wa muungano ni mkataba wa kimataifa.

      Jee kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe?. Jibu ni hapana, sio kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe, ili mkataba wa kimataifa uridhiwe lazima mkutaba husika uwe na kipengele kinacholazimisha mkataba huo kuridhiwa. Tukirudi kwenye mfano wetu wa mkataba wa muungano, kipengele cha VIII cha Articles of Union, kinalazimisha process ya ratification lazima ifanyike ili kuuhalalisha mkataba ule.

      (viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

      Nyerere na Karume wangeweza kuamua wakishasaini makubali yale iishie hapo, ingekuwa hivyo hivyo hitaji la kuridhia lisingekuwepo!.

    13. #11
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,828
      Rep Power : 2968
      Likes Received
      2435
      Likes Given
      3516

      ..let just jump to they way forward.

      ..hayo mengine yanawafaa wewe na wanasheria wenzako.

      ..wa-Zanzibar wameshamwaga damu kuutetea muungano na Tanzania ktk vita vya Kagera na nyinginezo, halafu wewe unaleta habari ya ratification??

      ..tueleze tuuvunje vipi muungano huu kwasababu imethibitika kwamba hauna faida na wananchi hawauhitaji tena.
      Pasco likes this.

    14. #12
      Mungi's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 23rd September 2010
      Location : Hapa!!!
      Posts : 10,170
      Rep Power : 24271
      Likes Received
      4677
      Likes Given
      2296

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Ukiwa Tanganyika unasema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Ukiwa Zanzibar unasema Muungano wa Zanzibar na Tanganyika.
      JokaKuu and Pasco like this.

    15. #13
      August's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th June 2007
      Posts : 2,744
      Rep Power : 1162
      Likes Received
      251
      Likes Given
      2511

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Quote By Pasco
      1. Kuridhia, au ratification, ni process inayofanywa kwa nchi husika kuridhia mikataba ya kimaifa ili kuipa uhalali wa kisheria kutumika katika nchi husika. Mfano mzuri ni mkataba wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar, Tanganyika ni nchi, na Zanzibar ni nchi, hivyo ule mkataba wa muungano ni mkataba wa kimataifa.

      Jee kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe?. Jibu ni hapana, sio kila mkataba wa kimataifa ni lazima uridhiwe, ili mkataba wa kimataifa uridhiwe lazima mkutaba husika uwe na kipengele kinacholazimisha mkataba huo kuridhiwa. Tukirudi kwenye mfano wetu wa mkataba wa muungano, kipengele cha VIII cha Articles of Union, kinalazimisha process ya ratification lazima ifanyike ili kuuhalalisha mkataba ule.

      (viii) These Articles shall be subject to the enactment of laws by the Parliament of Tanganyika and by the Revolutionary Council of the Peoples' Republic of Zanzibar in conjunction with the Cabinet of Ministers thereof, ratifying the same and providing for the Government of the united Republic and of Zanzibar in accordance therewith.

      Nyerere na Karume wangeweza kuamua wakishasaini makubali yale iishie hapo, ingekuwa hivyo hivyo hitaji la kuridhia lisingekuwepo!.
      kulikuwa hakuna muda wa kuridhia huo muungano by enactment of laws by the revolutionary goverment? kama hawakuridhia kwa kufanya hivyo lakini wakaendelea kuishi kama wamefanya hivyo, then mkataba ni halali by implication.
      mimi nike jifanya ni agent wako na wewe ukaniacha niishi hivyo, then mimi ni agent wako by implication.
      Pasco likes this.

    16. #14
      Manyi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th December 2011
      Posts : 1,720
      Rep Power : 721
      Likes Received
      290
      Likes Given
      260

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Inabididi wanasheria watufafanulie vizuri tafsiri ya hii Article of Unioni. Bwama Pasco, ukisoma vizuri hii makitu, ina technical language ambayo kwa haraka haraka unaweza tafsiri unavyojua wewe. Unaamini kwamba hata kukaa kimya bila kuridhia/kujibu ni ishara tosha ya kukubali? Tafsiri ndo inayogomba! Cha muhimu ni kuangalia muundo wa muungano, kuuvunja kwa sasa ni ngumu sana!
      Pasco likes this.

    17. #15
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      2. Ratification hufanyikaje?.
      Kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwe ni ya maandishi, vivyo hivyo, ratifikation lazima ifanyike kwa maandishi na sio kwa kauli.

      Kwa bunge letu, masharti ya kuridhia hufanywa kwa mujibu wa kifungu cha 63(3)(e) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinachotamka kuwa, Bunge litajadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa na kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni ya 114(11) ya 2007.
      1. Waziri husika huwasilisha mezani kwa spika mkataba husika
      2. Spika ataipa kamati husika kupata maoni yake
      3. Kambi ya upinzani itapewa fursa ya kuandaa maoni yake.
      4. Mkataba huo utatangazwa rasmi kwenye order paper ya siku ya kuwasilishwa
      5. Waziri atawasilisha, kisha maoni ya kamati, maoni ya kambi ya upinzani na majadiliano.
      6. Bunge litakaa kama kamati kupitia kifungu kwa kifungu
      7. Bunge litarudi kama bunge na kuridhia mkataba husika
      8. Mkataba huo unakuwa sehemu ya sheria za nchi,
      9. Unasainiwa na rais na kutangazwa katika gazeti za serikali GN.
      10.Ndio unakuwa umeridhiwa, yaani ratified
      Mzee Mwanakijiji likes this.

    18. #16
      sweke34's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th September 2010
      Posts : 2,493
      Rep Power : 1255
      Likes Received
      734
      Likes Given
      1240

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Nduhu shikolo...

    19. #17
      platozoom's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th January 2012
      Posts : 3,979
      Rep Power : 8269
      Likes Received
      2681
      Likes Given
      3661

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Pasco haachi vitimbi..............anafaa sana kwenye comedy....Ameanzisha mada ya "puppet" ambayo mjadala wake ni kama huu na bila shaka wachangiaji ni walewale halafu karuka na kuanzisha uzi mpya! HEBU KUA
      Pasco likes this.
      "Education is something that remain in your head after forgeting what you learn at school"

    20. #18
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,506
      Rep Power : 46711
      Likes Received
      16374
      Likes Given
      8453

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Quote By Pasco
      2. Ratification hufanyikaje?.
      Kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwe ni ya maandishi, vivyo hivyo, ratifikation lazima ifanyike kwa maandishi na sio kwa kauli.

      Pasco.
      Where did you get the assertion that "ni lazima ifanyike kwa maandishi na siyo kwa kauli"? Sheria gani ya Kimataifa inayosema hivyo or this is your construction based on a false premise - kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni ya kimaandishi vivyo hivyo...

      How did you get this conclusion kuwa ni 'lazima' iwe?
      Pasco likes this.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    21. #19
      Pasco's Avatar
      JF Premium Member Array
      Join Date : 22nd September 2008
      Posts : 9,839
      Rep Power : 7368
      Likes Received
      6153
      Likes Given
      22273

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      3. Mkataba wa Kimataifa ni nini, una sifa gani na Jee Muungano watu ni mkataba wa kimataifa?.
      Mkataba wa Kimataifa, ni mkataba kati nchi moja na nchi nyingine, au mikataba yote ya jumuiza za kimataifa ambayo nchi ama hutakiwa kuridhia, au kulazimishwa kuiheshimu hata kama haikuridhia. Mikataba hii au itifaki mbalimbali (protocals), hupaswa kuridhiwa kabla haijawa sheria kwa nchi husika.

      Mfano Tanzania iliridhia mkataba wa mahakama ya kimataifa ya Biashara, ICC. Dowans iliposhinda ile kesi, imepaswa kuisajili hukumu hiyo kwenye mahakama zetu (ratification), ili hukumu hiyo igeuke sheria zetu, (domestic law) na kutekelezwa. Watu humu walipiga sana kelele, nilipouangalia mkataba ule humu jf, nikawaambia wana jf wenzangu, hatuna pa kutokea, tozo ile italipwa tuu mara baada ya tozo hiyo kusajiliwa, kinachoendelea sasa ni delaying tactics ambayo nayo tutailipia dearly!.

      Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, ni mkataba halali wa kimataifa wenye sifa muhimu za mkataba, japo una mapungufu mengi kubwa likiwa ni kitu kinachoitwa "Privity of Contrac" ambapo mkataba ulikuwa kwa lugha ya Kiingereza na signatory mmoja alikuwa msomi anaejua kusoma na kuandika kiingereza, wakati signatory wa pili hakujua kusoma, kuandika wala kiingereza, hivyo alisaini kwa dole gumba!.

      Ufafanuzi zaidi kuhusu Muungano kuwa ni mkataba wa kimataifa, unapatikana pia katika ukurasa wa kwanza wa andiko la
      Prof. Shivji kwenye kitabu cha "The Legal Foundation of the Union in Tanzania and Zanzibar Constitution, DUP, 1990.

      Kwa faida ya wasoma kimombo, tembelea
      THE UNION BETWEEN TANGANYIKA AND ZANZIBAR
      Mzee Mwanakijiji likes this.

    22. #20
      Mag3's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 31st May 2008
      Posts : 3,540
      Rep Power : 1805
      Likes Received
      2463
      Likes Given
      2502

      Default Re: Jee Wajua Kuwa Zanzibar Haikuridhia Muungano?!. Ina Maana Gani?.

      Quote By Pasco
      2. Ratification hufanyikaje?.
      Kwa vile mikataba yote ya kimataifa ni lazima iwe ni ya maandishi, vivyo hivyo, ratifikation lazima ifanyike kwa maandishi na sio kwa kauli.

      Kwa bunge letu, masharti ya kuridhia hufanywa kwa mujibu wa kifungu cha 63(3)(e) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinachotamka kuwa, Bunge litajadili na kuridhia Mikataba yote inayohusu Jamhuri ya Muungano na ambayo kwa masharti yake inahitaji kuridhiwa na kwa mujibu wa Kanuni za Bunge, Kanuni ya 114(11) ya 2007...
      Pasco...point of information please, zingatia hii;
      The first moves of the revolutionary government were to suspend the Lancaster House 1963 independence constitution, ban all political parties except the ASP and proclaim a constitutional decree that established a constitutional government (Serikali ya Mapinduzi) and the rule of law. The constitution was set aside and the revolutionary council (Baraza la Mapinduzi) became the legislative body. Although it was stipulated that the constituent assembly was to be convened in one year's time to endorse a new constitution, this only occurred in 1979 and the first election was held in 1980.
      Ni katiba ya mwaka 1980 iliyounda Baraza la Wawakilishi na kuwezesha uchaguzi wa kwanza tokea mapinduzi ya mwaka 1964. Lazima tusisahau kuwa mara tu baada ya mapinduzi, Jamhuri ya Unguja na Pemba iliyoanzishwa haikuwa na katiba, haikuwa na bunge na haikuwa na baraza la Mawaziri, mihimili hii yote ilipigwa marufuku na majukumu yake yote kukasimiwa kwa Baraza la Mapinduzi kwa njia ya "decree".

      Nafikiri kosa kubwa linalofanywa na wengi ni kushindwa kuzingatia tofauti katika majukumu na taratibu kiutendaji kati ya iliyokuwa Baraza la Mapinduzi la 1964 na Baraza la Wawakilishi la 1980 tunapojadili kuridhiwa kwa Muungano na vyombo hivi viwili. Tanganyika tulikuwa na vyombo vilivyoendeshwa kwa kwa misingi ya katiba rasmi ya nchi tofauti na Zanzibar iliyokuwa chini ya constitutional decree.
      A decree is a rule of law issued by a head of state (such as the president of a republic), according to certain procedures (usually established in a constitution). It has the force of law. The particular term used for this concept may vary from country to country.
      The true sign of intelligence is not knowledge but imagination.
      Education is what remains after one has forgotten what one has learned in School
      -Albert Einstein.

    Page 1 of 6 123 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...