Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

    Report Post
    Page 9 of 17 FirstFirst ... 7891011 ... LastLast
    Results 161 to 180 of 334
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,488
      Rep Power : 46707
      Likes Received
      16317
      Likes Given
      8395

      Default Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano



      Msitunyonye bana nyie! Msitunyonye mnatudhiri! Tuachaneni angalau tujikung’ute kidogo! Tumekuwa mafukara; mtu mwenye miaka kumi na tatu amepinda mgongo kama mtu wa miaka sabini na tano! … tunachotaka sasa hivi mtuachie tupumue!
      – Mhadhara wa Uamsho Zanzibar Machi 4, 2012.


      Nimekuwa mtetezi wa Muungano kiasi kwamba nimegundua nimebakia peke yangu. Wengine wanautetea Muungano kwa kutumia vitisho na wengine wanautetea kwa kutumia dharau. Binafsi ninaamini muungano unaweza kutetewa kwa hoja maridhiwa zenye kuonesha kuwa Zanzibar na wananchi wa Zanzibar wananufaika na wataendelea kunufaika zaidi katika Muungano kuliko nje ya Muungano. Kwamba hoja za kupinga muungano kwa madai kuwa Wazanzibari wanaonewa na kuwa Zanzibar inakaliwa kama koloni na Tanganyika haina mshiko, ni ya kupuuza na ina uwezo wa kuteka akili za watu wasiotaka kufikiria.


      Baada ya muda mrefu kuwa mtetezi pekee wa Muungano kelele za hivi karibuni zimenibadili kabisa mawazo yangu na sasa nimekuwa na nitaendelea kushakizia muungano uvunjwe ili wale wanaoitaka Zanzibar yao wapewe na ili watu wa bara tuhangaike mambo mengine kuliko kuonekana tunawakandamiza Wazanzibari. Ile hofu ya Mwalimu kiasi cha kuachilia mambo mengi ya Zanzibar kuwa tukiungana kuwa nchi moja kamili kabisa Zanzibar watajiona wamemezwa imetimia kwani pamoja na kuwapa kila kitu Zanzibar bado wapo ambao wanaona wanamezwa!


      Ni kutokana na ukweli huu kwamba hakuna kiongozi au mwanasiasa wa Tanzania awe mzee au kijana mwenye uwezo wa kuutetea Muungano kisomi na kisiasa na kuwapinga wenye hoja dhaifu ndio maana leo naendelea na hoja yangu ya kuwasaidia Wazanzibar watoke kwenye Muungano, wawe na nchi na taifa lao na zaidi ya yote waweze baada ya kutoka kwenye Muungano kuanza mahusiano mapya na bara kama nchi mbili zilizo sawa. Ninaamini tunaweza kuhusiana vizuri zaidi baada ya Zanzibar kutoka na kuwa taifa lao wenyewe kuliko ilivyo hivi sasa ambapo Muungano hauteteleki – zaidi ya kutumia vitisho vya dola.


      Tunawapenda sana ndugu zetu Wazanzibari kiasi kwamba hatutaki kuwang’ang’ania. Wapo kwao wenye kutuchukia sana kiasi kwamba hawataki hata kufikiria sisi ni ndugu zao. Wanatuangalia kwa dharau na kebeki wao wakiamini utukufu wao wa “Zanzibar” isiyokuwepo ndiyo tunu waliyonayo. Ukiwaskiliza sana baadhi ya wapinga muungano kwa kweli kabisa wamejawa chuki isiyo na kifani na chuki hiyo imezaa matunda meusi katika madhihirisho ya chuki dhidi ya watu wa Bara na Wakristu.


      Lakini kitu kimoja ambacho watu wengi hawataki kukifikiria ni kuwa hawa watu wanaopinga Muungano wao wanadai “nchi”. Sasa hakuna aliyewauliza kwamba mbona katiba ya Zanzibar imefanyiwa mabadiliko na kuitangaza kuwa Zanzibar ni nchi? Sasa kama tayari Zanzibar ni nchi wanachodai hawa ni nini? Haiwezekani kuwa wanachodai ni nchi kwani nchi tayari wanayo na Katiba ya Zanzibar inasema hivyo! Wanachotaka siyo nchi! Wanachotaka ni kuwa nje ya Muungano! Hivi ni vitu viwili tofauti.


      Ndio maana basi katika makala ya leo nataka kuwasaidia Wazanzibari hawa na wale ambao wanaamini kuwa muungano haustahili kuteteewa kwa hoja bali kwa vioja. Pendekezo langu ni njia nyepesi za Wazanzibari kujiondoa kwenye Muungano bila kufanya maandamano, mihadhara wala kuwashtumu watu wa Tanganyika. Wazanzibari wakitaka kutoka kweli kwenye Muungano wanaweza kufanya hivyo ndani ya wiki chache tu na wakawa nchi. Nina uhakika serikali ya Muungano haitotumia nguvu kuwalazimisha kubakia! Nyerere mwenyewe alishasema kuwa hawezi kuwalazimisha Wazanzibari kubakia kwenye Muungano.


      Njia ya kwanza
      Njia ya kwanza na nyepesi zaidi ya kuweza kujitoa kwenye Muungano ni kwa wananchi wa Zanzibar wakiongozwa na hawa wana- uamsho wawatake watendaji wote wa Muungano wenye asili ya Zanzibar kuachia nafasi zao mara moja na kurudi Zanzibar!


      Hii ni pamoja na majaji, wabunge, mawaziri, maafisa wa polisi na vyombo vingine vya usalama, na wantedaji wengine ambao wako kwenye Muungano. Badala ya kuililia Tanganyika kila kukicha kuwa inawabana mashehe wa Zanzibari wenye kuongoza vuguvugu la kutoka kwenye Muungano waanzishe mihadhara ya kuwataka Wazanzibari wenzao ambao wanatumikia Muungano waachilie nafasi hizo.


      Binafsi ningependekeza kama wataniruhusu waanzishe harakati hizo ili viongozi wote hawa waachilie nafasi zo ifikapo Disemba 10, 2012. Hii ni pamoja na Makamu wa Rais Ghaib Bilal, jaji mkuu na wengine.
      Hawa wote wakishawishiwa kuondoka Wazanzibari wajiandae ama kuwapatia pensheni au kuwatafutia nafasi kwenye serikali ya nchi ya Zanzibar.


      Sasa hawa wote wakikubali kuondoka kwenye nafasi zao za Muungano Zanzibar itapata wataalamu wengine wengi ambao wamekuwa wakitumikia Muungano na hivyo kujiongezea hazina ya wataalamu mbalimbali. Lakini pia itafungua ajira za Watanganyika wengi ambao wangeweza kushika nafasi zinazoshikiliwa na Wazanzibari hasa kwa vile Wazanzibari hao wako kimya na hawajitokezi kuutetea Muungano ambao wanautumikia.


      Pamoja na kuwataka viongozi wao na watendaji mbalimbali watoke kwenye Muungano katika harakati za mwanzo za Zanzibar kujitenga wana uamsho hawastahili kulalamikia Watanganyika. Hawahitaji kuendelea kuwaghilibu vijana wa Kizanzibari kuwa inanyonywa na sasa wanahitaji kupumua. Mashehe wa uamsho waende mbali zaidi katik akudai nchi yao. Waanze kuwahamasisha Wazanzibari walioko bara kuamua kuondoka bara na kurudi Zanzibar ili kuendesha shughuli zao huko.


      Watu kama kina Bakheresa wenye biashara kubwa bara itabidi watiwe hamasa waamue kuondoka bara. Siyo hawa tu bali pia wale Wapemba na Wazanzibari waliona maeneo ya ardhi Bara. Hivi ndivyo ilivyotokea Sudan ya Kusini ambapo baada ya nchi hiyo kujitenga Wasudan ya Kusini waliokuwa wanafanya kazi Khartoum waliacha kazi zao na wengi wao wameamua kurudi kwenye nchi yao kuanza kuijenga.


      Wengi tunakumbuka kuwa baada ya Rwanda chini ya Kagame kutulia kwa kiasi Wanyarwanda wengi ambao wengine waliishi kama Watanzania waliacha kazi zao na kurudi kwao Rwanda kuijenga nchi y ao. Nakumbuka baadhi ya wahadhiri kwenye taasisi mbalimbali nchini ambao tuliwadhania ni Wahaya au Waangaza walipoamua kuacha kazi zao kumbe walikuwa ni Wanyarwanda.


      Hili pia litakuwa na faida kubwa sana kwa Zanzibar kwani itapata watu wengi zaidi wenye uwezo na utajiri mkubwa na vile vile itabidi iwaandalie viwanja vipya vya kilimo na makazi maana vile vya bara itabidi waviachilie kuwapisha Watanganyika ambao wanalalamikia kukosa ardhi au kupatiwa ardhi isiy nzuri. Na pia wafanyabiashara hao wa Kizanzibari watakaporudi Zanzibar na kama watataka kuja kufanya biashara Tanganyika itabidi waje kama wawekezaji na hivyo watasaidia katika ukuaji wa uchumi wa Tanganyika kama wageni wengine. Na kama watakuwa wajanja kama wageni wengine wanaweza kutengeneza mamilioni zaidi kuliko wanavyofanya sasa kama raia wa Tanzania!


      Hivyo hilo ni jjambo la kwanza nawashauri wana uamsho; hamasisheni Wazanzibari waondoke Tanzania bara ili warudi Zanzibar ambako watapatiwa nafasi bora zaidi za ajira. Mtakapofanya hivyo, na watu wa Bara nao itabidi waanze kuondoka Zanzibar japo hapo nina uhakika kutakuwa na kazi kidogo. Watu wa Bara ni kina nani Zanzibar?


      Njia ya pili
      Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema,"Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.


      Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano.
      Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa Bara au Serikali ya Muungano.


      Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya Katiba ya Zanzibar.


      Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

      Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la?


      Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.


      Swali liwe rahisi tu:
      Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?


      a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014 na yasipotatuliwa basi kipengele cha “b” kitatimia.

      b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa kwenye Muungano ifikapo Julai 1, 2014.



      Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie", maana yake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014. Baadhi ya watu ambao wamesoma hoja yangu hii ya pili wamedai – na mimi nikakubali – kuwa mwaka 2014 ni mbali sana. Hivyo, Wazanzibari wakitaka kujitenga wanaweza kuja na sheria kwenye kikao kijacho cha baraza la wawakilishi na ninapendekeza Mjumbe Jussa alete muswada wa swali la kura ya maoni ili Wazanzibari wafanye hima ya kujitoa kwenye Muungano.


      Nina uhakika wapo Watanganyika ambao watashukuru sana kwa wao pia kupewa nafasi ya kupumua kuliko kila siku kuimbiwa “Zanzibar, Zanzibar”; kama kweli inavyosemwa Muungano ni kama koti likibana unalivua ni wazi kuwa wanaobanwa na koti hilo sasa siyo Zanzibar tena bali ni watu wa bara na sasa wameamua kuwapa Wazanzibar uwezo kamili (absolute power) kujitoa kwenye Muungano bila kufanya mihadhara mingi wala kushindana na dola.
      Njia hizo hapo juu zitawasaidia Wazanzibari wanaotaka kujitoa watoke salama hasa kwa vile inaonekana hakuna Wazanzibari wanaoutaka Muungano. Watu wa Bara hatutaki kuonekana tunawang’ang’ania Wazanzibari wakati nguvu yote ya kutoka kwenye Muungano wanayo wao.


      Ni matumaini yangu serikali ya Rais Kikwete ambayo imeshindwa kujenga hoja na kuwajibu kwa hoja wana uamsho haitotumia nguvu kuzima harakati za kujitoa kwenye Muungano. Tena ningependa kabisa kutoa pendekezo kwa serikali ya Muungano kukataza kabisa Polisi na JWTZ kuingilia kati mikutano ya wanauamsho na badala yake waache kazi hiyo kwa Valentia, JKU na KMKM.


      Vikosi vya Muungano vikae pembeni kabisa kwani vitaonekana vinalazimisha watu kuupenda Muungano. Kama Muungano haupo moyoni, muungano hauwezi kuwepo ulimini! Kama watu wanataka mfumo wa Muungano au mambo fulani yabadilike basi tungeona juhudi za haraka za kutatua kero zote za Muungano badala ya hili la “subirini mkatoe maoni kwenye tume”. Watanzania wameshatoa maoni ya kutosha kuhusu Muungano kiasi kwamba kama CCM na serikali yake wangekuwa na uwezo wa kuyatatua basi wangekuwa wamekwishayatatua.


      Nidhahiri kuwa hakuna mwenye uwezo huo na sasa kilichobakia ni sote kwa pamoja kutoka Bara tuseme nasi pasi ya shaka kuwa LET ZANZIBAR GO- Iacheni Zanzibar iende.


      Itaenda wapi zaidi ya kuwa kwenye kivuli cha Tanganyika ndani au nje ya Muungano


      HUU NI MWANZO WA "LET ZANZIBAR GO MOVEMENT 2012"; Kama unaunga mkono kuwaacha Wazanzibar wajitoe kwenye Muungano weka kwenye sahihi yako "I support Let Zanzibar Go Movement 2012"! Tuwasaidie waharikishe wajitoe kwani hakuna kiongozi yeyote ambaye amekuwa na uwezo wa kuutetea Muungano kwa hoja maridhawa badala ya kutumia vitisho na mikwara.
      Last edited by Mzee Mwanakijiji; 6th June 2012 at 17:58.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. Study Abroad

    3. #161
      Nyakageni's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st February 2011
      Posts : 5,229
      Rep Power : 1536
      Likes Received
      764
      Likes Given
      52

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      rudini kwenye topic, acheni udini.

    4. #162
      Chilisosi's Avatar
      Banned Array
      Join Date : 19th October 2008
      Posts : 1,695
      Rep Power : 0
      Likes Received
      371
      Likes Given
      455

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By kwamwewe
      unakuja na mengine, hivi hujioni tu namna unavyoandika , nimekuambia kacheze mdako wacha watu wazima wajadiliane usitupotezee muda
      Kamwewe nikuulize sali jamaa yangu, Hivi wewe binafsi na akili yako kweli unazania wabara wanautaka huu muungano???? kwa sababu gani? wa nini?//?? una wasaidia nini zaidi ya kelele zenu? hivi mnadhani hatuwezi kuifanya mtwara freeport? manake mnapiga kelele utazani mnakitu kinachotusaidia. kama unaamini kuwa tunautaka huu muungano then something is wrong with you , sio rahisi mbara akampenda mzanzibario wakati mzanzibari anamuonyesha wazi kuwa anamchukia vibaya sana. hebu ona leo hiyo bajeti yenu mnazani nani anawalisha???

    5. #163
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7662
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Nonda
      Ukimaliza kunywa chai pitia hii link http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ti-wowote.html

      Wachomaji makanisa hutaki kuwataja, unawajua.
      Unawaogopa au una hisa nao? Una ubia nao?
      @Nondo mkuu wangu jaribu sana kutumia ELIMU na sii ushabiki. Tunafundishwa kwamba kwa kila crime yoyote inayotokea kuna MOTIVE na kama utapenda kulitazama swala hili utagundua ya kwamba CCM wanauhitaji Muafaka wa mseto kuliko CUF. CCM bila muafaka huu haiwezi kushinda uchaguzi Zanzibar na walifanya hivi makusudi kuondoa nguvu ya CUF visiwani. Lakini CUF hawawahitaji CCM hata kidogo na wao wanaweza shinda uchaguzi wowote Zanzibar jambo ambalo CCM hawataki kuliona, Hivyo kama kuna sababu zozote za kuvunja Muafaka huu basi zitatoka CUF na sio CCM kwa sababu CUF haiwahitaji CCM hata kidogo. Kwa hiyo kama kweli kuchomwa makanisa inaweza kusababisha muafaka kuvunjika na ushirikiano kuvunjika basi atakayedhurika na maamuzi haya atakuwa CCM na sidhani kama ndicho wanachokitaka.

      Na watu wengi wanajiuliza imekuwaje makanisa kuchomwa moto wakati miaka yote yalikuwepo, jibu ni rahisi kabisa. Zanzibar haikuwahi kutumia turufu ya Udini ktk siasa zake hadi miaka hii ambayo pekee tunaona kizazi kipya kinaendesha siasa za kupinga Wakristu kuwepo Zanzibar. Haikuwepo wakati wa Sultan wala wakati wa Mapinduzi ila sasa hivi hiki kizazi kipya kimefundwa darasa la chuki kwa Wakristu na hasa kutokana na wageni ambao leo wanajiona wao Wazanzibar kuliko wale walokuwepo kabla...

      Hata Marekani Canada na UK hivi leo unakuta Warusi na wazungu waliotoka nchi za mashariki (USSR na east block) nchi kama Serbia, Czek, Romania wanajiona wao wenyeji wa nchi hizo kuliko wenyeji wenyewe, tena wana roho mbaya kuliko Wazungu wenye asili na historia ya nchi hizo. Wengine wamekuja majuzi tu wametukuta sisi kina Mkandara lakini utawasikia wakisema turudi kwetu Afrika, wakituita Nigger na kadhalika - NDIVYO WALIVYO...Kwa hiyo malezi yenu yamechagia sana kuwepo kwa chuki hii baina ya Waislaam na Wakristu, Wabara na Wazanzibar na yote imetokana na kuitumia dini ya kiislaam kuwa mhuri wa uraia wa Mzanzibar.

      Hatuina sababu ya kurushiana matusi, mnataka kujitenga rahisi sana mmeisha elezwa njia nzuri sana. Fanyeni maandamano kwenda Ikulu, mfuateni Dr.Shein, kina Bilal, Maalim Seif na viongozi wote wa baraza la mawaziri ktk serikali ya mseto na kuwaambia tunataka referendum - Haondoki mtu hadi kieleweke! vuguvugu hili litawapa majawabu badala ya kushinda hapa JF kujishindilia maudhi yasokuwa na tiba. I said it in year 2000 na narudia tena leo, kuwaambia majibu ya hoja zenu zote yako huko huko Zanzibar waulizeni viongozi wenu.
      Black Bat and Nguruvi3 like this.
      Exploration of reality

    6. #164
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,410
      Rep Power : 2881
      Likes Received
      4756
      Likes Given
      2822

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Mkuu Zinedine,
      Manguli wote wa siasa na watu wote wenye mapenzi mema kwa wanadamu wenzao, wasomi na wachambuzi wanakubali bila kificho haya au soni kuhusika kwa JUMIKI katika kuchoma makanisani. Kuhusika kwao si kubeba vibiriti ni uchochezi uliojenga mazingira hayo. Hakuna mhadara wa Jumiki au UAMSHO ambao hautautaja ukristo kama tatizo la Wazanzibar.

      Mkuu Mkandara, unajua kuna watu wanjifanya kama hawaelewi ili hali wanaelewa na huo ni unafiki. Matukio ya kuchoma moto si mara ya kwanza, labda nikumbushe kuwa waliochoma vibanda vya Watanganyika hawakuwa na mkono wa usalama wa taifa wala CCM. Walifanya hivyo kwa kuaminishwa kuwa Mtanganyika ni mhalifu, kafir n.k.
      Umetoa narrative nzuri sana ya CCM na CUF, sijui kwa mtu aliyefundiswa chuki anaweza kukuelewa.

      Katika mikutano akitajwa Nyerere utasikia 'laana ya mwenyezi mungu iwe juu yake'! Akitajwa Karume, Jumbe, Wakili, Mwinyi, Amour, Karume jr au Shein ambao wamefanya kazi na kumsaidia 'kafir' Nyerere uwanja unakuwa kimyaa!
      Sababu ni moja, kwamba hadhra imefundishwa kuwa Nyerere ni mbaya si kama binadamu bali Mkristo.
      Vingenevyo tungesikia Karume(laana), Jumbe(laana) hilo hutalisikia.
      Huu ndio unafiki wa Wazanzibar, ambao wanaamini unafiki ni sehemu ya ibada!

      Unafiki huu unakolezwa na fedha za Oman alizokwenda kuchukua Sheikh! masikini wasiojua wanaitikia tu.

      Mkandara/Zinedine akina Nonda wamelishwa chuki na imetua mioyoni mwao, wameaminishwa ili kuiona akhera lazima umchukie mkristo, wala siyo budha au mwingine. Chukia mkristo kwanza ili upate pepo! ukichoma kanisa wewe ni mtu wa pepo!

      Wamefundishwa kuwa kumwita mwislam kafir haifai, kwahiyo mwislam mtanganyika mwite Chogo.
      Ninachotaka kusema hapa ni kuwa JUMIKI inahubiri ukafir.period.

      Hakuna aya hadith au sunna inayofundishwa mwanadamu kumchukia mwanadam mwenzake, jumiki wametoa wapi? Kawaelez jana Ali Hassan Mwinyi

      Jumiki na Uamsho ni CUF wanotumia aya ndani ya siasa tena wakizipindisha ili zikidhi haja zao.

    7. #165
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,692
      Rep Power : 903
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By Saint Ivuga
      kumbe nyie wavisiwani mnataka mfukuzwe na kuchomewa nyumba zenu huku bara ndio mjue kuwa watanganyika hawaupendi muungano? watanganyika sio watu wa aina hiyo..huku watu wanafikiri kabla ya kutenda na wanaangalia mbele hawaangalii chini kama nyie. mwanakijiji keshawafungulia njia kama nyie kweli mmedhamiria fanyeni kweli ila nina uhakika hamuwezi mtaendelea kuikumbatia ccm ambayo ndio imeleta huu muungano msioutaka
      ....well said!u have a point,naunga mkono hoja.let zaznibar go!tumechoka

    8. FemaTV & Radio

    9. #166
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,692
      Rep Power : 903
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By chilisosi
      Kwa mbara yoyote atakayesoma uliyoandika nadhani baada ya kumaliza atakuwa anapiga jaramba kujiandaa na kazi ya kusafisha jiji la dar.
      NIA YA KUWAONDOA KWETU TUNAYO
      UWEZO WA KUWAONDOA TUNAO
      SABABU KUWAODOA TUNAZO
      HAKI YA KUWAONDOA TUNAYO
      CHUKI DHIDI YETU WANAYO
      MITUMBWI YA KUWASAFIRISHIA TUNAYO!
      JESHI LA KUSIMAMIA USAFI TUNALO!
      wao wameisha sema hawatutaki kwao na muungano hawautaki tena wamechoma hadi maduka ya ndugu zetu na makanisa, kila kukicha wanapiga kelele na kuandamana , kila siku zinavyozidi kupita ndio wanavyozidi kutuchukia. kumbukeni dawa ya jipu ni kulikamua litoke.na hawa jamaa wanakoelekea msishangae siku moja wakaanza kujilipua au kutega mabomu bara kama wasomali wanavyofanya huko Kkenya. hawa watu sio wazuri kwetu hata kidogo, inabidi tutengane nao haraka sana na mipaka idhibitiwe, tunataka kuanzia leo ukiona mpemba kariakoo unamuona ni foreigner kama vile tunavyowaona wanigeria, wakenya wazambia nk. visa yake ikiisha arudi kwao, hakuna kuwa na haki yoyote kama vile ardhi, kumiliki nyumba nk.
      HEBU TUANZISHE KULA YA MAONI
      TAKBIIIIIR!
      ...kweli mkuu,inauma sana,then wanaona c km wajinga kwa kukaa kwetu kimya!hivi serikali inaogopa nn?,hawa wapemba waliojaa hum mjini cjui itakuwaje?....Let ZBAR GO!

    10. #167
      Nonda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th November 2010
      Location : Gongo La Mboto
      Posts : 5,797
      Rep Power : 1858
      Likes Received
      933
      Likes Given
      367

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Mkandara
      @Nondo mkuu wangu jaribu sana kutumia ELIMU na sii ushabiki. .....
      Huyu jamaa hapa anafanya haya uliyoshauri hapa. Wala huyu siye Nonda.

      .... vurugu hizo siyo za kidini kama wanavyodhani watu wengi bali ni njia iliyotumika kufikisha ujumbe wa walalamikaji.
      .... Si suala la kidini, ni hoja za kujishikiza tu, kuna masuala ya msingi yanayovishwa hoja za kidini.”

      Link http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ml#post4006894

      Mengine mengi ambayo umeyagusia katika mchango wako yana wenyewe.Unajaribu kuniingiza kundini. Ni jamaa zako.
      Tafakari hayo maneno aliyosema huyo jamaa yetu.
      Mkandara likes this.

    11. #168
      christine ibrahim's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th February 2012
      Posts : 2,692
      Rep Power : 903
      Likes Received
      430
      Likes Given
      440

      Default

      Quote By Mpiganaji wa watu
      binafsi sioni tunachonufaika nacho sisib wabara kutoka zanzibar zaidi ya wao kutujazia nafac za ajira za vijana wetu huku, alaf kila siku hawaishi kulalamika,waende kama ni jina tanzania tutachukua hata initialsz za MWANZA
      ...duh,hili nalo neno!

    12. #169
      Remote's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th May 2011
      Posts : 4,246
      Rep Power : 1356
      Likes Received
      941
      Likes Given
      182

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      jamani mwanakijiji na nguruvi3, ingieni na kule kwenye mtandao wao wa mzalendo.net mkawape hayo maono yenu.

    13. #170
      Nonda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th November 2010
      Location : Gongo La Mboto
      Posts : 5,797
      Rep Power : 1858
      Likes Received
      933
      Likes Given
      367

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Zinedine
      Nonda, busara mara nyingi iko proportional na umri, sasa wee mbona unataka kuprove-tofauti. Mi ni mfuatiliaji mzuri wa thread zako kwa kuwa sometimes zinanijenga. Sasa vipi siku hizi tena? .... they don't care about fact and they forget even their commonsense!)
      Mkuu Zinedine

      Nashukuru kwa maneno ya ukarimu kuwa unafuatilia michango yangu.

      Kama kweli unafuatilia michango yangu utagundua kuwa mimi nasema kile ninachokiamini baada ya kufatilia taarifa za kulia na kushoto, halafu nachanganya na zangu. Sifuati tu mkumbo.

      Kama imetokea mara hii kuwa tumeelemea upande tofauti wa hoja, au nimekosoa kuwa hoja kuu imejengwa chini ya msingi mbovu uniwie radhi na tukubaliane kutokukubaliana.

      Mijadala ya karibuni imeibuka baada ya Matukio ya Zanzibar. Kuna waliorukia kuwatwisha lawama UAMSHO kuwa wamechoma makanisa...sasa kidogo hili linakuwa-diluted inasemwa kuwa UAMSHO haiwezi kukimbia lawama kuwa haihusiki hata kama wao hawakuchoma lakini wamejenga mazingira ya kufanikisha hilo.

      Hawa jamaa wa UAMHO wanadai kura ya maoni kuhusu Muungano kabla ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya.
      Hili ndio dai lao la msingi baada ya kuangalia hizo video zao.

      Kuna watu wanasema hoja ya UAMSHO ni udini na chuki dhidi ya ukristo na makanisa. Mimi sikubaliani na hoja hii. Hapa pengine ndio unajiuliza mbona Nonda amegeuka siku hizi?

      Watu wameanzisha mada kutaka wazanzibari wajikate, watu hawa wanataka kutuaminisha kuwa UAMSHO ndio mamlaka ya Zanzibar au inawakilisha wazanzibari wote. Mada zina lengo la kuwapinga UAMSHO lakini badala ya UAMSHO, wamewajumlisha/ wamewajumuisha Wazanzibari wote akiwemo Agostino Ramadhani na familia yake na Dr. Shein.

      Kwa hiyo hoja iliyojengwa ilianza vibaya, inataja wazanzibari badala ya UAMSHO. Lakini pia wajenga hoja tayari wameshawahukumu UAMSHO na kuwatia hatiani kuwa wao ndio wamechoma moto makanisa na wanapandikiza chuki baina ya wakristo na waislamu. Kwa hiyo waanzilishi wa mada hizi nao wameanza kujenga hoja na kutoa matamshi ya kusema wanaamsha chuki dhidi ya wazanzibari na pia kuwafundisha njia/ hatua rahisi za kujikata.

      Watu hawa wanasahau haya
      ".... vurugu hizo siyo za kidini kama wanavyodhani watu wengi bali ni njia iliyotumika kufikisha ujumbe wa walalamikaji.
      .... Si suala la kidini, ni hoja za kujishikiza tu, kuna masuala ya msingi yanayovishwa hoja za kidini.” Lisu

      http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la...ml#post4011474

      Muungano una madudu mengi hili kila mtu analikubali. Sasa badala ya kutizama hoja ya msingi ya UAMSHO ambayo nilivyofahamu mimi ni kuwa uwepo mjadala rasmi, wa wazi na mpana kuhusu Muungano na hatima yake. Hoja ambayo nafikiri ikiungwa mkono tutaweza kuifungua pandora box ya Muungano na kuona yaliyofanywa siri kwa miaka 48. vinatokea vikundi vyengine kuzima mjadala wa wazi wa muungano na kupandikiza chuki.

      Jf inaweza kuwa kikundi kama UAMSHO, kwa bahati wengi wanachungulia hapa na kupata tafakuri mpya na kuanzisha movement huko mitaani ya kudai mjadala wa wazi na mpana wa muungano badala yake tunawashawishi wawape salamu jirani zao wafunge vifurushi na vibahasha au wachukue vile tu vinavyoingia katika begi waondoke. Je hao waliopo Kariakoo ni UAMSHO? Je watanganyika wote walioko Zanzibar ni wakristo?

      Hapa sijui kama nimekupa changamoto ya mawazo au nimekutatiza zaidi?

      By the way kuna wengine tayari wamegomea mchakato wa Katiba mpya kwa hiyo sishangai kuwa wanataka kila mtu awe na msimamo kama huo. Bado nafasi ipo ya kutia m-binyo, mkandamizo (pressure)kwa serikali ya Muungano kuwa mjadala rasmi, wa wazi na mpana uwemo katika hadudi rejea ya Tume ya kukusanya maoni ya Katiba. UAMSHO wameonesha njia,ilipasa vikundi vyengine vijenge pale UAMSHO walipoishia na kuepuka kasoro ambazo UAMSHO wamezionesha katika mikakati yao.

      Tunapowajengea watawala upenyo kama huu tunaoujenga sasa wa kuepuka mjadala wa wazi wa Muungano, wao watagonganisha gilasi na kujisemea kweli "watanzania vichwa vya wendawazimu".

    14. #171
      kwamwewe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2010
      Posts : 856
      Rep Power : 5405
      Likes Received
      99
      Likes Given
      125

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Nguruvi3
      Mkuu Zinedine,
      Manguli wote wa siasa na watu wote wenye mapenzi mema kwa wanadamu wenzao, wasomi na wachambuzi wanakubali bila kificho haya au soni kuhusika kwa JUMIKI katika kuchoma makanisani. Kuhusika kwao si kubeba vibiriti ni uchochezi uliojenga mazingira hayo. Hakuna mhadara wa Jumiki au UAMSHO ambao hautautaja ukristo kama tatizo la Wazanzibar.

      Mkuu Mkandara, unajua kuna watu wanjifanya kama hawaelewi ili hali wanaelewa na huo ni unafiki. Matukio ya kuchoma moto si mara ya kwanza, labda nikumbushe kuwa waliochoma vibanda vya Watanganyika hawakuwa na mkono wa usalama wa taifa wala CCM. Walifanya hivyo kwa kuaminishwa kuwa Mtanganyika ni mhalifu, kafir n.k.
      Umetoa narrative nzuri sana ya CCM na CUF, sijui kwa mtu aliyefundiswa chuki anaweza kukuelewa.

      Katika mikutano akitajwa Nyerere utasikia 'laana ya mwenyezi mungu iwe juu yake'! Akitajwa Karume, Jumbe, Wakili, Mwinyi, Amour, Karume jr au Shein ambao wamefanya kazi na kumsaidia 'kafir' Nyerere uwanja unakuwa kimyaa!
      Sababu ni moja, kwamba hadhra imefundishwa kuwa Nyerere ni mbaya si kama binadamu bali Mkristo.
      Vingenevyo tungesikia Karume(laana), Jumbe(laana) hilo hutalisikia.
      Huu ndio unafiki wa Wazanzibar, ambao wanaamini unafiki ni sehemu ya ibada!

      Unafiki huu unakolezwa na fedha za Oman alizokwenda kuchukua Sheikh! masikini wasiojua wanaitikia tu.

      Mkandara/Zinedine akina Nonda wamelishwa chuki na imetua mioyoni mwao, wameaminishwa ili kuiona akhera lazima umchukie mkristo, wala siyo budha au mwingine. Chukia mkristo kwanza ili upate pepo! ukichoma kanisa wewe ni mtu wa pepo!

      Wamefundishwa kuwa kumwita mwislam kafir haifai, kwahiyo mwislam mtanganyika mwite Chogo.
      Ninachotaka kusema hapa ni kuwa JUMIKI inahubiri ukafir.period.

      Hakuna aya hadith au sunna inayofundishwa mwanadamu kumchukia mwanadam mwenzake, jumiki wametoa wapi? Kawaelez jana Ali Hassan Mwinyi

      Jumiki na Uamsho ni CUF wanotumia aya ndani ya siasa tena wakizipindisha ili zikidhi haja zao.

      wacha kutia sumu

      soma nini mapadri wanasema wala htukusikia watu kulalamika

      Siasa bila dini ni uendawazimu’


      Na Lilian Nyenza


      Kanisa halitaacha kutoa mwongozo kwa watu wake hata kwa mambo ya kisiasa ukiwamo uchaguzi kwa kuwa, siasa bila dini ni sawa na uendawazimu.



      Aidha, imedaiwa kuwa tabia ya kuwalaghai vijana kuwa ni taifa la kesho, ndiyo inayowadumaza kiakili na kuwafanya watumiwe na wanasiasa kufanya fujo, badala ya kujitokeza kuongoza kwa kufuata taratibu za nchi.



      Mkurugenzi wa chama cha kifamilia cha Undugu Association Tanzania, Padri Baptiste Mapunda, alitoa kauli hiyo katika sherehe za kuuaga mwaka 2004 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2005, zilizofanyika katika ukumbi wa Parokia ya Mt. Yosefu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.



      Mkurugenzi huyo wa UNDUGU ASSOCIATION TANZANIA alisema kuwa, Tanzania imeanza kuonesha dalili mbaya za machafuko kutokana na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa kuweka mbele ubinafsi.

      “Tukikaa kimya huku mambo yanaharibika katika jamii; eti tuwaachie wanasiasa wafanye watakavyo, tutakuwa hatutendi wajibu wetu na hivyo, Kanisa halitaacha kusema ukweli kwa maslahi ya umma hata kama unamkera mtu. Hii ni kwa kuwa tunajua wazi kuwa siasa bila dini, ni uendawazimu ambao mtu hajui akifanyacho kwa kuwa akili yake haijatimia kiroho.” alisema.


      Aliitaka jamiii ya Kitanzania ijifunze thamani ya amani na siasa safi kutokana na hali ya amani na usalama katika nchi jirani za Rwanda na Burundi ambayo ni hatari na inasikitisha.


      Alisema vita na mauaji yanayoendelea katika nchi hizo, yanasababishwa na uroho wa madaraka wa watu wachache ambao hawajali utu wa wengine.

      Aliongeza kuwa, “Siku zote tunapaswa kukumbuka kuwa, amani na mapendo ambayo Mungu ametujalia, tunapaswa kuyaenzi sisi sote kwa kuwa siasa bila dini, ni sawa na uendawazimu.”


      Padri Mapunda aliiasa jamii kuendelea kumuomba Mungu ili azidi kuwajalia amani,upendo na utulivu uliopo sasa, kuwa uwepo hata baada ya Uchaguzi Mkuu kupita.

      Amewataka Waamini kuwaombea viongozi wanyanyasaji kama Herode, wabadilike na hivyo, kuongoza nchi kwa haki na akawasihi Watanzania kuyashinda maovu kwa kutenda yaliyo mema.



      Hata hivyo, Padri Mapunda amewatahadharisha vijana kujiepusha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa siasa, kwa nia ya kufanya fujo katika uchaguzi.

      “Vijana mara nyingi wamekuwa wepesi wa kurubuniwa na vijizawadi vidogo vidogo, ili wafanye kile wanachokitaka wanasiasa wabinafsi. Sasa mimi nasema mkae chini na mlitafakari hilo kwa makini. Mtakao angamia ni ninyi na si wao,” alitahadharisha.



      Alisema vijana ni Taifa la leo na Taifa bila vijana limekufa, hivyo aliwasihi kuwaheshimu wazazi na walezi ili wapate kuishi maisha marefu na yenye heri duniani, kama walivyojaliwa kuuona mwaka huu mpya.



      Naye Mwenyekiti wa Umoja huo, Bw. Benjamini Komba alisema, lengo la Shirika la Undugu, ni kuiunganisha jamii, ikiwa ni pamoja na kuimarisha Ukristo katika kupata hamasa katika kazi ya umisionari, ili ijengeke roho ya umisionari wa kweli nchini Tanzania.



      Bw. Komba alisema kuwa, Shirika limekuwa na mchango mkubwa kwa jamii, kwa kuwa ni chombo cha kuelimisha jamii na kuendeleza mawasiliano na wamisionari wa Afrika ambao wapo ndani na nje ya nchi kwa lengo la kusukuma mbele kurudumu la Injili katika Taifa hili.



      Umoja huo haujishughulishi na mambo ya siasa na hauna ubaguzi wa dini, rangi, imani wala itikadi.


      Katika sherehe hizo, Wanaundugu na watu wengine walialikwa na kuhudhuria pamoja na familia zao.

    15. #172
      Falconer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th October 2008
      Posts : 267
      Rep Power : 593
      Likes Received
      49
      Likes Given
      28

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Mkandara, uanongea pumba tupu. Kwani huu muungano si ulikuwa ni muun gano wa mataifa mawili?. Halafu palikuwa na makubaliano kumi na moja yalioletwa na Mwalimu Julius. Tumeutaka waraka wamuungano, hatukupewa. Tumetaka waraka kuhusu sahihi ya viongozi wetu kuhusiana na muungano, haiko. Tumekwenda umoja wa mataifa kuangalia "legality" ya muungano huu na tumekosa jawabu. Kila njia tuliofuata kuweza kuwaonyesha watu wetu wa zanzibar kuhusu UHALALI wa muungano hatukupatashahda yeyote ile sasa kuuvunja muungano ndio njia peke yake ya kuondosha malalamiko.

    16. #173
      Nonda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th November 2010
      Location : Gongo La Mboto
      Posts : 5,797
      Rep Power : 1858
      Likes Received
      933
      Likes Given
      367

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Nguruvi3
      Mkuu Zinedine,
      Manguli wote wa siasa na watu wote wenye mapenzi mema kwa wanadamu wenzao, wasomi na wachambuzi wanakubali bila kificho haya au soni kuhusika kwa JUMIKI katika kuchoma makanisani. Kuhusika kwao si kubeba vibiriti ni uchochezi uliojenga mazingira hayo. Hakuna mhadara wa Jumiki au UAMSHO ambao hautautaja ukristo kama tatizo la Wazanzibar.

      Mkandara/Zinedine akina Nonda wamelishwa chuki na imetua mioyoni mwao, wameaminishwa ili kuiona akhera lazima umchukie mkristo, wala siyo budha au mwingine. Chukia mkristo kwanza ili upate pepo! ukichoma kanisa wewe ni mtu wa pepo! ........

      ....
      Duh!
      Wacha utani wako, Mkuu Nguruvi3.

      Kwa hiyo wewe ni nguli na ni mtu mwenye mapenzi ambaye unaamini kuhusika kwa UAMSHO katika kuchoma makanisa?

      Upendo ulionao juu ya Nonda umelishwa na nani?

      Acha character assassination trick...rudi kwenye hoja kama unayo, kama huna ni bora kuonesha hekima yako.

      Under belt punch not allowed, sir! Nimefurahi kukusoma, nimeupenda mchango wako.

    17. #174
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,410
      Rep Power : 2881
      Likes Received
      4756
      Likes Given
      2822

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Nonda
      Duh!
      Wacha utani wako, Mkuu Nguruvi3.

      Kwa hiyo wewe ni nguli na ni mtu mwenye mapenzi ambaye unaamini kuhusika kwa UAMSHO katika kuchoma makanisa?

      Upendo ulionao juu ya Nonda umelishwa na nani?

      Acha character assassination trick...rudi kwenye hoja kama unayo, kama huna ni bora kuonesha hekima yako.

      Under belt punch not allowed, sir! Nimefurahi kukusoma, nimeupenda mchango wako.
      Mzee mwinyi na mtu yoyote mwenye akili timamu na miongoni mwa manguli wote waliolaani UAMSHO yumo Sheni.
      Kwani hoja ipi haijajibiwa nikumbushe nikujibu, badala yake zangu hazijibiwi.
      Moja ni hii, Tanganyika ina poteza nini Zba ikiondoka
      Pili, Nini kinawazuia wazanzibar wasiondoke katika muungano

      Kamwewe, hakuna tatizo la siasa na dini, tatizo lililopo ni kuwa UAMSHO hawajitambulishi kama wanasiasa, wamejificha nyuma ya mgongo wa dini. Lakini basi, na hiyo siasa ya UAMSHO si siasa. Hakuna siasa ya kuchochea watu, kuzua uongo, kuleta fitna. Huo ni uzandiki na tofauti ya mwasiasa na mzandiki ni hekima na busara.

    18. #175
      Zinedine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2011
      Posts : 488
      Rep Power : 508
      Likes Received
      175
      Likes Given
      232

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Nonda
      Mkuu Zinedine

      "mimi nasema kile ninachokiamini baada ya kufatilia taarifa za kulia na kushoto, halafu nachanganya na zangu. Sifuati tu mkumbo"

      Mijadala ya karibuni imeibuka baada ya Matukio ya Zanzibar. Kuna waliorukia kuwatwisha lawama UAMSHO kuwa wamechoma makanisa...sasa kidogo hili linakuwa-diluted inasemwa kuwa UAMSHO haiwezi kukimbia lawama kuwa haihusiki hata kama wao hawakuchoma lakini wamejenga mazingira ya kufanikisha hilo



      Kwa hiyo hoja iliyojengwa ilianza vibaya, inataja wazanzibari badala ya UAMSHO. Lakini pia wajenga hoja tayari wameshawahukumu UAMSHO na kuwatia hatiani kuwa wao ndio wamechoma moto makanisa na wanapandikiza chuki baina ya wakristo na waislamu.


      ".
      Nonda, sasa unazidi kunitatiza na kunifanya nisielewe stand yako. Sisi tunatofautiana na uamsho, lakini na wee unatofatiana zaidi na uamsho. Wanajf wameshaeleza humu kuwa kufanya vurugu kwa uamsho au kuhusiwa kwao katika kuchoma makanisa au kupendikiza chuki haina maana kwamba Sheikh Farid alibeba Dumu lake la petrol na kibiriti mkononi, la hasha, walitengeneza mazingira ya kufanya hivyo; hii hawatoki, ndo maana Vuai alisema hivi:
      "Chukua CD za mihadhara ya Uamsho; chukua CD za hiyo mikutano mitano ya CCM; halafu ziweke hadharani watu waone na kusikiliza. Waache waamue ni nani aliyechochea vurugu,” ameeleza Vuai kwa sauti ya upole.

      Sasa haya aliyosema Vuai na hapo nilipoeka bluu juu, nakushauri angalia video hii then urudi utuambie umeona nini, : WAZANZIBARI WAKIONESHA HISIA ZAO -KONGAMANO KIDUTANI 4 - YouTube

      Kam haina direct link, just copy it and paste on a new opened tab!

    19. #176
      kwamwewe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2010
      Posts : 856
      Rep Power : 5405
      Likes Received
      99
      Likes Given
      125

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Nguruvi3
      Mzee mwinyi na mtu yoyote mwenye akili timamu na miongoni mwa manguli wote waliolaani UAMSHO yumo Sheni.
      Kwani hoja ipi haijajibiwa nikumbushe nikujibu, badala yake zangu hazijibiwi.
      Moja ni hii, Tanganyika ina poteza nini Zba ikiondoka
      Pili, Nini kinawazuia wazanzibar wasiondoke katika muungano

      Kamwewe, hakuna tatizo la siasa na dini, tatizo lililopo ni kuwa UAMSHO hawajitambulishi kama wanasiasa, wamejificha nyuma ya mgongo wa dini. Lakini basi, na hiyo siasa ya UAMSHO si siasa. Hakuna siasa ya kuchochea watu, kuzua uongo, kuleta fitna. Huo ni uzandiki na tofauti ya mwasiasa na mzandiki ni hekima na busara.

    20. #177
      Black Bat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Abbottabad
      Posts : 2,479
      Rep Power : 9580
      Likes Received
      682
      Likes Given
      575

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Remote
      jamani mwanakijiji na nguruvi3, ingieni na kule kwenye mtandao wao wa mzalendo.net mkawape hayo maono yenu.
      wakiingie kule ile laziam wapigwe ban. kule watu wametanguliza jazba mbele
      ukipenda niite double biiiiiii!! tchao

    21. #178
      mangikule's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th June 2012
      Posts : 907
      Rep Power : 530
      Likes Received
      174
      Likes Given
      235

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Pasco
      Kwa wasiojua ukweli wa mambo, msingi mkuu wa muungano ni dhima ya Nyerere na Karume in good faith!.

      Baada ya dhima ikafuatia kitendo cha kuungana rasmi kwa kuchanganya udogo na kusaini zile hati za muungano.

      Baada ya hapo muunngano huo uliridhiwa bara tuu (ratified) kwa bunge la Tanganyika kuupitisha mkataba huo uliokuwa na mambo 11 hivyo kupata nguvu za kisheria!.

      Zanzibar nao walitakiwa kuuridhia mkataba huo wa muungano kwa kuuratify lakini jambo hili halikufanyika!. Hivyo wanasheria wangeweza kabisa kuishitaki Tanzania kwa kuipora mamlaka Zanzibar na kuikalia kimabavu miaka yote hiyo!.

      Kufuatia kukosekana kwa uhalali wa kisheria wa muungano kule Zanzibar, hivyo Wanzanzibar wako huru kujitoa kwenye muungano kwa amani kabisa kwa kung'ang'ana kuwa sheria, taratibu na kanuni, hazikufuatwa!.

      Maadam Wanzanzibari wanacholilia ni haki na uhuru wao, nawaombeni tuwateende haki kwa kuwapatia wanachotaka.

      Naiunga kauli ya Mzee Mwanakijiji kwa asilimia 100%, "Let them go!."
      Ndiyo let them GOOOO!! wape UHURU wanaoutaka. Nimeishi muda wote sijaona faida za huu muungano. Waachieni hao.

    22. #179
      Black Bat's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th October 2007
      Location : Abbottabad
      Posts : 2,479
      Rep Power : 9580
      Likes Received
      682
      Likes Given
      575

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By kwamwewe
      nani anajua elimu ya huyu sheihe
      ukipenda niite double biiiiiii!! tchao

    23. #180
      amagoma's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 14th March 2008
      Location : Dsm
      Posts : 7
      Rep Power : 572
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Jamani, hakika nimechoka. Nimechoka kusikia maelezo ya namna moja na kila siku ya Zanzibar kuonewa na Bara utadhani ni kweli. Kitu kikirudiwa mara nyingi na watu wasipokuwa makini wanaweza kudhani kinachosemwa ni kweli.

      Hapana, sasa umefika wakati tuwaruhusu hawa wenzetu wajitenge - waende zao. Kipi hasa tunachobembeleza toka kwao, matusi? Let them go NOW! December 2012 ni mbali. Wapeleke BLW mswada na waupitishe na wabunge wao walioko katika Bunge la muungano wafanye hivyo, nasi tuwaunge mkono.

      Jamani imetosha nasi tusikubali matusi haya kuendelea, yafike mwisho na mwisho wake ni sasa

    24. Miaka 50
    Page 9 of 17 FirstFirst ... 7891011 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...