Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano

    Report Post
    Page 4 of 17 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast
    Results 61 to 80 of 334
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,519
      Rep Power : 46714
      Likes Received
      16435
      Likes Given
      8471

      Default Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muungano



      Msitunyonye bana nyie! Msitunyonye mnatudhiri! Tuachaneni angalau tujikung’ute kidogo! Tumekuwa mafukara; mtu mwenye miaka kumi na tatu amepinda mgongo kama mtu wa miaka sabini na tano! … tunachotaka sasa hivi mtuachie tupumue!
      – Mhadhara wa Uamsho Zanzibar Machi 4, 2012.


      Nimekuwa mtetezi wa Muungano kiasi kwamba nimegundua nimebakia peke yangu. Wengine wanautetea Muungano kwa kutumia vitisho na wengine wanautetea kwa kutumia dharau. Binafsi ninaamini muungano unaweza kutetewa kwa hoja maridhiwa zenye kuonesha kuwa Zanzibar na wananchi wa Zanzibar wananufaika na wataendelea kunufaika zaidi katika Muungano kuliko nje ya Muungano. Kwamba hoja za kupinga muungano kwa madai kuwa Wazanzibari wanaonewa na kuwa Zanzibar inakaliwa kama koloni na Tanganyika haina mshiko, ni ya kupuuza na ina uwezo wa kuteka akili za watu wasiotaka kufikiria.


      Baada ya muda mrefu kuwa mtetezi pekee wa Muungano kelele za hivi karibuni zimenibadili kabisa mawazo yangu na sasa nimekuwa na nitaendelea kushakizia muungano uvunjwe ili wale wanaoitaka Zanzibar yao wapewe na ili watu wa bara tuhangaike mambo mengine kuliko kuonekana tunawakandamiza Wazanzibari. Ile hofu ya Mwalimu kiasi cha kuachilia mambo mengi ya Zanzibar kuwa tukiungana kuwa nchi moja kamili kabisa Zanzibar watajiona wamemezwa imetimia kwani pamoja na kuwapa kila kitu Zanzibar bado wapo ambao wanaona wanamezwa!


      Ni kutokana na ukweli huu kwamba hakuna kiongozi au mwanasiasa wa Tanzania awe mzee au kijana mwenye uwezo wa kuutetea Muungano kisomi na kisiasa na kuwapinga wenye hoja dhaifu ndio maana leo naendelea na hoja yangu ya kuwasaidia Wazanzibar watoke kwenye Muungano, wawe na nchi na taifa lao na zaidi ya yote waweze baada ya kutoka kwenye Muungano kuanza mahusiano mapya na bara kama nchi mbili zilizo sawa. Ninaamini tunaweza kuhusiana vizuri zaidi baada ya Zanzibar kutoka na kuwa taifa lao wenyewe kuliko ilivyo hivi sasa ambapo Muungano hauteteleki – zaidi ya kutumia vitisho vya dola.


      Tunawapenda sana ndugu zetu Wazanzibari kiasi kwamba hatutaki kuwang’ang’ania. Wapo kwao wenye kutuchukia sana kiasi kwamba hawataki hata kufikiria sisi ni ndugu zao. Wanatuangalia kwa dharau na kebeki wao wakiamini utukufu wao wa “Zanzibar” isiyokuwepo ndiyo tunu waliyonayo. Ukiwaskiliza sana baadhi ya wapinga muungano kwa kweli kabisa wamejawa chuki isiyo na kifani na chuki hiyo imezaa matunda meusi katika madhihirisho ya chuki dhidi ya watu wa Bara na Wakristu.


      Lakini kitu kimoja ambacho watu wengi hawataki kukifikiria ni kuwa hawa watu wanaopinga Muungano wao wanadai “nchi”. Sasa hakuna aliyewauliza kwamba mbona katiba ya Zanzibar imefanyiwa mabadiliko na kuitangaza kuwa Zanzibar ni nchi? Sasa kama tayari Zanzibar ni nchi wanachodai hawa ni nini? Haiwezekani kuwa wanachodai ni nchi kwani nchi tayari wanayo na Katiba ya Zanzibar inasema hivyo! Wanachotaka siyo nchi! Wanachotaka ni kuwa nje ya Muungano! Hivi ni vitu viwili tofauti.


      Ndio maana basi katika makala ya leo nataka kuwasaidia Wazanzibari hawa na wale ambao wanaamini kuwa muungano haustahili kuteteewa kwa hoja bali kwa vioja. Pendekezo langu ni njia nyepesi za Wazanzibari kujiondoa kwenye Muungano bila kufanya maandamano, mihadhara wala kuwashtumu watu wa Tanganyika. Wazanzibari wakitaka kutoka kweli kwenye Muungano wanaweza kufanya hivyo ndani ya wiki chache tu na wakawa nchi. Nina uhakika serikali ya Muungano haitotumia nguvu kuwalazimisha kubakia! Nyerere mwenyewe alishasema kuwa hawezi kuwalazimisha Wazanzibari kubakia kwenye Muungano.


      Njia ya kwanza
      Njia ya kwanza na nyepesi zaidi ya kuweza kujitoa kwenye Muungano ni kwa wananchi wa Zanzibar wakiongozwa na hawa wana- uamsho wawatake watendaji wote wa Muungano wenye asili ya Zanzibar kuachia nafasi zao mara moja na kurudi Zanzibar!


      Hii ni pamoja na majaji, wabunge, mawaziri, maafisa wa polisi na vyombo vingine vya usalama, na wantedaji wengine ambao wako kwenye Muungano. Badala ya kuililia Tanganyika kila kukicha kuwa inawabana mashehe wa Zanzibari wenye kuongoza vuguvugu la kutoka kwenye Muungano waanzishe mihadhara ya kuwataka Wazanzibari wenzao ambao wanatumikia Muungano waachilie nafasi hizo.


      Binafsi ningependekeza kama wataniruhusu waanzishe harakati hizo ili viongozi wote hawa waachilie nafasi zo ifikapo Disemba 10, 2012. Hii ni pamoja na Makamu wa Rais Ghaib Bilal, jaji mkuu na wengine.
      Hawa wote wakishawishiwa kuondoka Wazanzibari wajiandae ama kuwapatia pensheni au kuwatafutia nafasi kwenye serikali ya nchi ya Zanzibar.


      Sasa hawa wote wakikubali kuondoka kwenye nafasi zao za Muungano Zanzibar itapata wataalamu wengine wengi ambao wamekuwa wakitumikia Muungano na hivyo kujiongezea hazina ya wataalamu mbalimbali. Lakini pia itafungua ajira za Watanganyika wengi ambao wangeweza kushika nafasi zinazoshikiliwa na Wazanzibari hasa kwa vile Wazanzibari hao wako kimya na hawajitokezi kuutetea Muungano ambao wanautumikia.


      Pamoja na kuwataka viongozi wao na watendaji mbalimbali watoke kwenye Muungano katika harakati za mwanzo za Zanzibar kujitenga wana uamsho hawastahili kulalamikia Watanganyika. Hawahitaji kuendelea kuwaghilibu vijana wa Kizanzibari kuwa inanyonywa na sasa wanahitaji kupumua. Mashehe wa uamsho waende mbali zaidi katik akudai nchi yao. Waanze kuwahamasisha Wazanzibari walioko bara kuamua kuondoka bara na kurudi Zanzibar ili kuendesha shughuli zao huko.


      Watu kama kina Bakheresa wenye biashara kubwa bara itabidi watiwe hamasa waamue kuondoka bara. Siyo hawa tu bali pia wale Wapemba na Wazanzibari waliona maeneo ya ardhi Bara. Hivi ndivyo ilivyotokea Sudan ya Kusini ambapo baada ya nchi hiyo kujitenga Wasudan ya Kusini waliokuwa wanafanya kazi Khartoum waliacha kazi zao na wengi wao wameamua kurudi kwenye nchi yao kuanza kuijenga.


      Wengi tunakumbuka kuwa baada ya Rwanda chini ya Kagame kutulia kwa kiasi Wanyarwanda wengi ambao wengine waliishi kama Watanzania waliacha kazi zao na kurudi kwao Rwanda kuijenga nchi y ao. Nakumbuka baadhi ya wahadhiri kwenye taasisi mbalimbali nchini ambao tuliwadhania ni Wahaya au Waangaza walipoamua kuacha kazi zao kumbe walikuwa ni Wanyarwanda.


      Hili pia litakuwa na faida kubwa sana kwa Zanzibar kwani itapata watu wengi zaidi wenye uwezo na utajiri mkubwa na vile vile itabidi iwaandalie viwanja vipya vya kilimo na makazi maana vile vya bara itabidi waviachilie kuwapisha Watanganyika ambao wanalalamikia kukosa ardhi au kupatiwa ardhi isiy nzuri. Na pia wafanyabiashara hao wa Kizanzibari watakaporudi Zanzibar na kama watataka kuja kufanya biashara Tanganyika itabidi waje kama wawekezaji na hivyo watasaidia katika ukuaji wa uchumi wa Tanganyika kama wageni wengine. Na kama watakuwa wajanja kama wageni wengine wanaweza kutengeneza mamilioni zaidi kuliko wanavyofanya sasa kama raia wa Tanzania!


      Hivyo hilo ni jjambo la kwanza nawashauri wana uamsho; hamasisheni Wazanzibari waondoke Tanzania bara ili warudi Zanzibar ambako watapatiwa nafasi bora zaidi za ajira. Mtakapofanya hivyo, na watu wa Bara nao itabidi waanze kuondoka Zanzibar japo hapo nina uhakika kutakuwa na kazi kidogo. Watu wa Bara ni kina nani Zanzibar?


      Njia ya pili
      Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema,"Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.


      Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano.
      Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa Bara au Serikali ya Muungano.


      Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya Katiba ya Zanzibar.


      Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

      Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la?


      Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.


      Swali liwe rahisi tu:
      Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?


      a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014 na yasipotatuliwa basi kipengele cha “b” kitatimia.

      b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa kwenye Muungano ifikapo Julai 1, 2014.



      Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie", maana yake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014. Baadhi ya watu ambao wamesoma hoja yangu hii ya pili wamedai – na mimi nikakubali – kuwa mwaka 2014 ni mbali sana. Hivyo, Wazanzibari wakitaka kujitenga wanaweza kuja na sheria kwenye kikao kijacho cha baraza la wawakilishi na ninapendekeza Mjumbe Jussa alete muswada wa swali la kura ya maoni ili Wazanzibari wafanye hima ya kujitoa kwenye Muungano.


      Nina uhakika wapo Watanganyika ambao watashukuru sana kwa wao pia kupewa nafasi ya kupumua kuliko kila siku kuimbiwa “Zanzibar, Zanzibar”; kama kweli inavyosemwa Muungano ni kama koti likibana unalivua ni wazi kuwa wanaobanwa na koti hilo sasa siyo Zanzibar tena bali ni watu wa bara na sasa wameamua kuwapa Wazanzibar uwezo kamili (absolute power) kujitoa kwenye Muungano bila kufanya mihadhara mingi wala kushindana na dola.
      Njia hizo hapo juu zitawasaidia Wazanzibari wanaotaka kujitoa watoke salama hasa kwa vile inaonekana hakuna Wazanzibari wanaoutaka Muungano. Watu wa Bara hatutaki kuonekana tunawang’ang’ania Wazanzibari wakati nguvu yote ya kutoka kwenye Muungano wanayo wao.


      Ni matumaini yangu serikali ya Rais Kikwete ambayo imeshindwa kujenga hoja na kuwajibu kwa hoja wana uamsho haitotumia nguvu kuzima harakati za kujitoa kwenye Muungano. Tena ningependa kabisa kutoa pendekezo kwa serikali ya Muungano kukataza kabisa Polisi na JWTZ kuingilia kati mikutano ya wanauamsho na badala yake waache kazi hiyo kwa Valentia, JKU na KMKM.


      Vikosi vya Muungano vikae pembeni kabisa kwani vitaonekana vinalazimisha watu kuupenda Muungano. Kama Muungano haupo moyoni, muungano hauwezi kuwepo ulimini! Kama watu wanataka mfumo wa Muungano au mambo fulani yabadilike basi tungeona juhudi za haraka za kutatua kero zote za Muungano badala ya hili la “subirini mkatoe maoni kwenye tume”. Watanzania wameshatoa maoni ya kutosha kuhusu Muungano kiasi kwamba kama CCM na serikali yake wangekuwa na uwezo wa kuyatatua basi wangekuwa wamekwishayatatua.


      Nidhahiri kuwa hakuna mwenye uwezo huo na sasa kilichobakia ni sote kwa pamoja kutoka Bara tuseme nasi pasi ya shaka kuwa LET ZANZIBAR GO- Iacheni Zanzibar iende.


      Itaenda wapi zaidi ya kuwa kwenye kivuli cha Tanganyika ndani au nje ya Muungano


      HUU NI MWANZO WA "LET ZANZIBAR GO MOVEMENT 2012"; Kama unaunga mkono kuwaacha Wazanzibar wajitoe kwenye Muungano weka kwenye sahihi yako "I support Let Zanzibar Go Movement 2012"! Tuwasaidie waharikishe wajitoe kwani hakuna kiongozi yeyote ambaye amekuwa na uwezo wa kuutetea Muungano kwa hoja maridhawa badala ya kutumia vitisho na mikwara.
      Last edited by Mzee Mwanakijiji; 6th June 2012 at 17:58.
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    2. RukaaJuu Final

    3. #61
      majorbuyoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 1st April 2012
      Posts : 663
      Rep Power : 2613
      Likes Received
      183
      Likes Given
      238

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      "I support Let Zanzibar Go Movement 2012"! Wazanzibar wanataka kufanya majaribio/Utafiti ili waone nini matokeo yake. Wanatak kutenganisha mabehewa mawili katika treni iliyo kwenye mwendo, nia na madhumuni wajue kipi kitaendelea na safari kati ya kichwa cha treni chenye mabehewa(Tanganyika) na mabehewa mawili(Zanzibar) yaliyochomolewa wakati treni inatembea.

    4. #62
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By abdy76
      yaani umeandika upuuzi mtupuuuuu yaani kama ni mtihani bac 0+++=000000000000000000000, unajua watz wengi ni wajinga hawajui haki zao linapo kuja swala la kudai haki zao watawala ni rahisi sana kubadili upepo hoja sio nani ananufaika na muungano nani hanufaiki wananchi wa znz wanataka mabadiliko ya mfumo wa muungano wameona mfumo uliokuwepo hauna faida kwao je ni kosa kisheria? wanataka kura ya maoni iitishwe ili tusipoteze pesa na muda kuwalazimisha watu kuunda katiba wakati muungano wenyewe haupo kisheria kwa ujinga wetu watz maendeleo tutaendelea kuyaona kwenye tv tu aibu tupu
      Wala hujakosea huo mtihani wa 0+++=? nisingeuweza ila weye ulosoma sana.

      Kati yetu sisi na wewe nani asojua haki zake maana unachozungumzia sio madai ya haki ya Wazanzibar pale inapostahili. Kama wewe kweli unaijua haki yako kwa nini usimuulize kiongozi wako Dr.Shein, Bilal Maalim Seif na wengineo ambao wananufaika na Muungano? hayo maandamano kwa nini yasielekee Ikulu kwa Dr,Shein mtake kupata majibu lakini mnaandamana kwa kuitazam Bara ambayo haipo huko. haya wee nambie kitu chochote ambacho bara inanufaika kutoka Zanzibar maanake twende kwa maelezo binafsi kusema kweli sielewi bara tunanufaika nini na muungano zaidi ya kuisoma Historia ya nchi hizi. Kwa fikra zako unafikiri hawa watu wanalipwa na Wazanzibar au unataka nasi tunaze kuuliza hawa watu tunaowalipa mabillionni wakati sii Wabara inakuwaje?.

      Binafsi mkuu wangu napenda sana muungano uvunjike hata kesho maana sababu hasa ya muungano ilitokana na Zanzibar kuwa nchi ya Kikomunist. Ukomunist haupo tena kina Abraham babu wameisha kufa, hao walobakia kina Nassor Moyo na Salim hawana tena nguvu ya kurudisha Ukomunist kwanza hakuna mtu anaupenda hivyo sioni sababu ya kuendelea kuuliza Muungano.

      Kifupi haki yetu haitokani na Muungano wala hakuna jambo lolote ambalo Muungano huu unatuongezea zaidi ya kuwafadhili nyie kama protectorate alipewa Sultan na waingereza. lakini waulize wazanzibar watasema Muingereza alikuwa mbaya sana wakati Sultan mwenyewe alitaka kuwa protected against Portuguese na makoloni mengineyo. Ni akili mbovu kutoelewa maana hasa kwa Wazanzibar wahamiaji ambao wamepoteza uraia huko walikotoka sasa wanatafuta nchi na makazi mapya kwa kudai Uhuru wa Sultan ulopinduliwa.

      Huwezi kumnyofoa Mzanzibar kwa kabila hata kidogo isipokuwa kwa mahamiaji ambao wote wana historia ya kukimbia makwao toka hao WaOman, Washiraz, Wabarush, Wanyamwezi hadi Wangazija wote wampewa hifadhi sasa mnataka kuifanya nchi hiyo kama Wayahudi - Mna akili sana nyie!

      Sisi tunaelewa matatizo yetu wala hayahusiani na kabila, jinsia wala rangi wa tu isipokuwa uongozi wa CCM ambao nyie wasomi mlipiga kura na kuchagua serikali ya mseto ambayo viongozi wake wote ni Wazanzibar bado hamtaki wakati wenzenu wanakula nchi. Na kibaya zaidi kila kiongozi wenu anapoiba huko anakuja jenga bara pengine hili mngelitazama zaidi kuliko kudai nchi wakati hao viongozi wenu wamefungua biashara na account zao bara. Nimekumaliza mkuu kaa pembeni acha wenye kuelewa maana wazungumze.
      Exploration of reality

    5. #63
      muheta's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th May 2012
      Posts : 15
      Rep Power : 356
      Likes Received
      9
      Likes Given
      8

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Let Zanzibar go!! Asante Mzee Mwanakijiji kwa darasa lako, let them decide their destiny kuliko wanavyotuandama wakati uamuzi uko mikononi mwao! Let them go. Waliamua kuvunja katiba ya Jamhuri ya Muungano kwa kujitangazia kuwa wao ni nchi ndani ya nchi na hakuna aliyewauliza, Walivunja katiba ya JMT ya kumpa Rais wa Zanzibar uamiri jeshi mwingine badala ya Rais wa JMT hakuna aliyewauliza!! Sasa kipi kinawashinda kuanzisha mchakato kwenye bunge lao wakaondoka? Ushauri wa Mzee Mwanakijiji ni mzuri sana kwa hatima ya Wazanzibar. Ninaunga mkono ili wachukue hata waondoke! tena ikiwezekana july 1 , 2012

    6. #64
      kara11's Avatar
      Junior Member Array
      Join Date : 11th May 2012
      Posts : 7
      Rep Power : 356
      Likes Received
      1
      Likes Given
      0

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Zamaulid
      na waende wakapewe misaada na ndugu zao wa Oman!lkn for sure watatukumbuka na ukalimu wetu!!
      kupewa misaada na waoman kwani kunatatizo gani? na sifikirii kama kuna mzenji hata mmoja atakae kukumbukeni kwa
      jema isipokua kwa ujambazi na kutuzalilisha.

    7. #65
      Zinedine's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th April 2011
      Posts : 496
      Rep Power : 511
      Likes Received
      179
      Likes Given
      236

      Default

      Quote By Nonda
      Mkuu hapo nilipoweka rangi nyekundu umechanganya madawa/ umefanya madudu.

      Isomeke Bunge la Tanganyika lilifuata sheria na katika kufuata sheria pia ilivunja sheria kwani baada ya sheria ile Bunge la Tanganyika halikukaa tena kama Bunge la Tanganyika. Nani aliwapa uwezo wa kuiua serikali ya Tanganyika na Bunge la Tanganyika?

      Pia isomeke Muungano ni wa Tangayika tu. Hakuna nchi iliyoitwa bara au inayoitwa bara. Usifuate siasa za kisanii/ mazingaombwe.

      Jikumbushe jina la Muungano. Lilikuwa ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na lilipofupishwa likawa Jamhuri ya Muungano wa TanZanIA.
      Mazingaombwe/ kiini macho tu ndio yataleta neno bara.

      Sio nia yangu kuanzisha mjadala katika hili lakini tusiwachanganye wananchi na wasomaji wa JF.

      Let us call spade a spade!
      Nonda, umetoka usingizini au? Uhalali au uharam au 'whatever' juu ya Muungano huu mmeshasema ktk mikutano yenu na JUMIKI, kilichopo hapa ni: LET ZANZIBARI GO!
      Mzee Mwanakijiji and Nonda like this.

    8. Miaka 50

    9. #66
      zumbemkuu's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 11th September 2010
      Location : street dweller
      Posts : 5,345
      Rep Power : 2005
      Likes Received
      2124
      Likes Given
      7829

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      prof. Idrissa Kikula amewajaza wazanzibar pale chuo cha ardhi, amepelekwa UDOM nako admistration wamejaa wazenji, kila sehemu yenye bosi mzenji basi ujue kuna harufu ya uzenji, aaaaagh!! let them go to take our positions, LET THEM GOO!
      Mzee Mwanakijiji likes this.
      "watakaotubeza na kututukana wasameheni wanahitaji ukombozi wa fikra" Mh.G.Lema

    10. #67
      Steve Dii's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th June 2007
      Location : Kihesa - Iringa
      Posts : 6,795
      Rep Power : 3279
      Likes Received
      924
      Likes Given
      2800

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      ...acha wachape lapa, nasi tunasepa zetu. sha'kuwa nongwa ati! wasema kupe kwenye mgongo?..mwenye hila habebeki yakhe!!
      Mkandara and Mzee Mwanakijiji like this.

    11. #68
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,275
      Rep Power : 3570
      Likes Received
      3076
      Likes Given
      464

      Default Re: Zanzibar ni ya Wazanzibar na si chirika na Tanganyika.

      Nani anayeimiliki Oman?
      Mzee Mwanakijiji likes this.

    12. #69
      Bujibuji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 4th February 2009
      Location : NYUMBANI PANONO
      Posts : 13,912
      Rep Power : 11208
      Likes Received
      7069
      Likes Given
      5296

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Laiti kungekuwa na uwezekano wa kuuvunja muungano kwa shoka, mie ningeingia gharama ya kununua msumeno wa umeme ili nirahisishe zoezi la kuuvunja huo muungano
      Mzee Mwanakijiji and JokaKuu like this.
      KAZI NDIO MSINGI WA MAENDELEO. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUENDELEA KWA MSINGI WA FEDHA. NCHI MASIKINI HAIWEZI KUJITAWALA KAMA INATEGEMEA MSAADA KUTOKA NCHI ZA NJE- J. K. NYERERE

    13. #70
      Janjaweed's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 20th January 2010
      Posts : 3,626
      Rep Power : 1130
      Likes Received
      1392
      Likes Given
      1541

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Kwanini bara tusiwe na referendum yetu kuhusu Muungano??
      Kama Vipi nipotezee tu; ntakuboa....

    14. #71
      Atanaye's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 31st October 2007
      Location : Ughaibuni
      Posts : 155
      Rep Power : 622
      Likes Received
      4
      Likes Given
      2

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Inasikitisha kuona kuwa sasa tumefikia hapa, tena mara nyingi tu! Tukumbuke kwamba sasa hivi kuna wale ambao wanachekelea mdahalo huu, wanajua fika kuwa tumefika wanapotaka tufike.

      Nitasisitiza kuwa muungano wowote ule ambao uko nje na matakwa ya mabepari na watwana wa magharibi(kama wapo) basi ni karaha kwao. Ni mtazamo wangu.


      Muungano lazima uudumishwe.
      Mkandara and Mzee Mwanakijiji like this.
      Lepidus

    15. #72
      Taso's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th June 2010
      Posts : 1,175
      Rep Power : 796
      Likes Received
      308
      Likes Given
      121

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      chombo halali cha Zanzibar (siyo Karume tu kama wengi mnavyotaka tuamini ) kiliridhia muungano.
      Chombo gani, kitaje!

    16. #73
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,438
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4802
      Likes Given
      2865

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      [QUOTE]
      Mzee Mwanakijiji;4005445]Ukiwaskiliza sana baadhi ya wapinga muungano kwa kweli kabisa wamejawa chuki isiyo na kifani na chuki hiyo imezaa matunda meusi katika madhihirisho ya chuki dhidi ya watu wa Bara na Wakristu.

      Lakini kitu kimoja ambacho watu wengi hawataki kukifikiria ni kuwa hawa watu wanaopinga Muungano wao wanadai “nchi”. Sasa hakuna aliyewauliza kwamba mbona katiba ya Zanzibar imefanyiwa mabadiliko na kuitangaza kuwa Zanzibar ni nchi? Sasa kama tayari Zanzibar ni nchi wanachodai hawa ni nini? Haiwezekani kuwa wanachodai ni nchi kwani nchi tayari wanayo na Katiba ya Zanzibar inasema hivyo! Wanachotaka siyo nchi! Wanachotaka ni kuwa nje ya Muungano! Hivi ni vitu viwili tofauti.

      Pendekezo langu ni njia nyepesi za Wazanzibari kujiondoa kwenye Muungano bila kufanya maandamano, mihadhara wala kuwashtumu watu wa Tanganyika. Wazanzibari wakitaka kutoka kweli kwenye Muungano wanaweza kufanya hivyo ndani ya wiki chache tu na wakawa nchi. Nina uhakika serikali ya Muungano haitotumia nguvu kuwalazimisha kubakia! Nyerere mwenyewe alishasema kuwa hawezi kuwalazimisha Wazanzibari kubakia kwenye Muungano.

      Njia ya kwanza
      Njia ya kwanza na nyepesi zaidi ya kuweza kujitoa kwenye Muungano ni kwa wananchi wa Zanzibar wakiongozwa na hawa wana- uamsho wawatake watendaji wote wa Muungano wenye asili ya Zanzibar kuachia nafasi zao mara moja na kurudi Zanzibar!

      Hii ni pamoja na majaji, wabunge, mawaziri, maafisa wa polisi na vyombo vingine vya usalama, na wantedaji wengine ambao wako kwenye Muungano. Badala ya kuililia Tanganyika kila kukicha kuwa inawabana mashehe wa Zanzibari wenye kuongoza vuguvugu la kutoka kwenye Muungano waanzishe mihadhara ya kuwataka Wazanzibari wenzao ambao wanatumikia Muungano waachilie nafasi hizo.

      Binafsi ningependekeza kama wataniruhusu waanzishe harakati hizo ili viongozi wote hawa waachilie nafasi zo ifikapo Disemba 10, 2012. Hii ni pamoja na Makamu wa Rais Ghaib Bilal, jaji mkuu na wengine.
      Hawa wote wakishawishiwa kuondoka Wazanzibari wajiandae ama kuwapatia pensheni au kuwatafutia nafasi kwenye serikali ya nchi ya Zanzibar.
      Sasa hawa wote wakikubali kuondoka kwenye nafasi zao za Muungano Zanzibar itapata wataalamu wengine wengi.
      Lakini pia itafungua ajira za Watanganyika wengi ambao wangeweza kushika nafasi zinazoshikiliwa na Wazanzibari.
      Mashehe wa uamsho waende mbali zaidi katik akudai nchi yao. Waanze kuwahamasisha Wazanzibari walioko bara kuamua kuondoka bara na kurudi Zanzibar ili kuendesha shughuli zao huko.

      Wale Wapemba na Wazanzibari waliona maeneo ya ardhi Bara. Hivi ndivyo ilivyotokea Sudan ya Kusini ambapo baada ya nchi hiyo kujitenga Wasudan ya Kusini waliokuwa wanafanya kazi Khartoum waliacha kazi zao na wengi wao wameamua kurudi kwenye nchi yao kuanza kuijenga.

      Hili pia litakuwa na faida kubwa sana kwa Zanzibar kwani itapata watu wengi zaidi wenye uwezo na utajiri mkubwa na vile vile itabidi iwaandalie viwanja vipya vya kilimo na makazi maana vile vya bara itabidi waviachilie kuwapisha Watanganyika ambao wanalalamikia kukosa ardhi au kupatiwa ardhi isiy nzuri. Na pia wafanyabiashara hao wa Kizanzibari watakaporudi Zanzibar na kama watataka kuja kufanya biashara Tanganyika itabidi waje kama wawekezaji
      Hivyo hilo ni jjambo la kwanza nawashauri wana uamsho; hamasisheni Wazanzibari waondoke Tanzania bara ili warudi Zanzibar ambako watapatiwa nafasi bora zaidi za ajira. Mtakapofanya hivyo, na watu wa Bara nao itabidi waanze kuondoka Zanzibar japo hapo nina uhakika kutakuwa na kazi kidogo. Watu wa Bara ni kina nani Zanzibar?

      Nina uhakika wapo Watanganyika ambao watashukuru sana kwa wao pia kupewa nafasi ya kupumua kuliko kila siku kuimbiwa “Zanzibar, Zanzibar”; Watu wa Bara hatutaki kuonekana tunawang’ang’ania Wazanzibari wakati nguvu yote ya kutoka kwenye Muungano wanayo wao.

      Nidhahiri kuwa hakuna mwenye uwezo huo na sasa kilichobakia ni sote kwa pamoja kutoka Bara tuseme nasi pasi ya shaka kuwa LET ZANZIBAR GO- Iacheni Zanzibar iende.
      Itaenda wapi zaidi ya kuwa kwenye kivuli cha Tanganyika ndani au nje ya Muungano
      HUU NI MWANZO WA "LET ZANZIBAR GO MOVEMENT 2012"; Kama unaunga mkono kuwaacha Wazanzibar wajitoe kwenye Muungano weka kwenye sahihi yako "I support Let Zanzibar Go Movement 2012"! Tuwasaidie waharikishe wajitoe kwani hakuna
      Mkandara;4004870] Wazanzibar wanataka kujitoa ktk Muungano wajadili na viongozi wao kisha wakilisheni ombi lenu la kujikata halafu ndipo itapangwa ushirika wa kimataifa kama tulivyo na nchi nyingine iwe Kenya au Uganda. uamuzi ni wenu sisi bara hatuna nongwa kabisa isipokuwa mjue tu ya kwamba ni WATU wanaojenga nchi na sii ARDHI kwa watu wake. Maadam wapo Wazanzibar wengi bara ambao kwa matakwa haya watakuja kuwa wageni wakiishi kwa visa na work permit sijui hapa mtakuja sema nini maana huu mungano mnautazama kwa bendera na ramani.

      Uhuru ni wa WATU sii wa ardhi na mipaka yake hata siku moja, maana hata wewe unaweza kuja bara ukanunua ardhi na ikawa yako au waarabu wanaweza kuja Zanzibar nunua ardhi ukahamishwa wewe kama ilivyotokea Palestine.

      Sasa kama nyie mnaona ardhi ni bora zaidi kuliko wananchi wenyewe jikateni wala hatuna noma kabisa isipokuwa ktk vichwa vyenu wafikirieni WATU wanaoishi mikoani maana kuna waarabu wenye asili ya Zanzibar (kiOman), Washiraz na Wangazija waliohamia bara na wanajulikana kama Wazanzibar. Kama umegundua hakuna Wabara wanaohamia Zanzibar, wamekuja fanya biashara au kufanya kazi huko lakini wao wanajua kuwa ni wageni kama waphilipino kule Dubai kisha ardhi yenyewe iko wapi? lakini kwa Wazanzibar waliohamia bara au wanaotaka kuhamia bara ardhi kubwa na huru kwao kufanya lolote. Muungano huu ni faida kubwa kwa Wazanzibar kuliko bara kumbuka Palestine, Rwanda na Burundi wanachokiomba ni ardhi zaidi wangemshukuru Mungu, nyie ndio kwanza mnataka kujikata kwa ardhi kidogo wakati mko mamillioWazanzibar
      tumewafungulia kila kitabu na kila kurasa. Tunawasaidia, nanyi onyesheni nia ya kujitenga July 1 2012. Hii kampeni ya Let Zanzibar go ndiyo imeanza na mwitikio unatia raha. Pita vijiweni uone jinsi Wabara walivyohamasika na nchi yao.

      Hakuna Mzanzibar atakayedaiwa chochote midhali kipo ndani ya begi lake. Wale wenye dhamana zisizohamishika hakikisheni mnapata wanunuzi kipindi hiki ili kuepuka hasara.
      Huu ni ukarimu kwasababu hakuna mzanzibar aliyewahi kubeba nyumba ardhi au duka kuja nalo. Lakini hatazuiliwa kuondoka na amana zake pale atakapoziuza.

      Ni vema mkaondoka wenyewe kwasababu mtakuwa na wakati wa kujipanga. Mkisubiri kufukuzwa mtajikuta katika wakati mgumu.
      Hakuna mbara atakayenyanyua dongo, kijiwe,unyoya au njiti kumpiga mtu.
      Wabara hatujafikia kiwango hicho cha upuuzi
      Tutatumia njia ifuatayo na ambayo imependekezwa na mwenzetu MM.
      Tutaomba serikali moja bila kuwa na Mwanza au Zanzibar. Zote ziwe JMT.

      Tunajua mlivyo na uchungu wa nchi yenu hili hamtalikubali na hapo mtaondoka bila matayarisho na mtapata hasara.

      Kuna mambo ambayo sasa ni 'off the table''
      1. Hakuna serikali 3 kwasababu hamna cha kuchangia katika serikali ya muungano. Hatudhani kama mumegoma kulipa umeme wa bilioni 50 mtaweza kulipa bill ya bilioni 500!
      Hata kama mtaweza mtabakisha nini chunguni?

      2. Hatuhitaji mkataba. Hatuna kitu ambacho tunadhani tutafaidika kutoka katika mkataba.
      Mkataba ni njia ya ulaghai ya chako ni chetu, changu ni changu. Hatuna tutakachofadika

      3. Hatuhitaji uhusiano special, tutakutana SADC, EAC, COMESA n.k.

      Nashadidia yaliyosemwa,kama mnadhani makamu wa rais na mawaziri ni vibaraka, basi ninyi wafanyakazi wa Zanzibar wazalendo ndani ya muungano onyesheni mfano.
      Pisheni huko mlikoajiriwa ili Wabara wafaidi matunda ya nchi yao kama mtakavyofaidi yenu.
      Vijana wa bara mnaotembea na bahasha za khaki(CV), hili ni kuwakumbusha kuwa dhiki zenu zinalipwa fadhila na matusi, kejeli na moto wa wazanzibar walioziba nafasi zenu.

      Watanganyika, hatuna tunachofaidika na Zanzibar zaidi ya hasara kama Mluguru kulipia bill za umeme kwa UAMSHO [/QUOTE]
      Wazanzibar this is athe point of no return, hamhitaji maandamano wala kelele, nafasi ya kujitoa ipo wazi nasi tutawasaidia

      LET ZANZIBAR GO! ZANZIBAR SHOULD GO ASAP!
      Last edited by Nguruvi3; 7th June 2012 at 06:21.

    17. #74
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,519
      Rep Power : 46714
      Likes Received
      16435
      Likes Given
      8471

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Taso
      Chombo gani, kitaje!

      soma kule kwingine
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    18. #75
      Sir Leem's Avatar
      JF Tanzanite Member Array
      Join Date : 14th March 2008
      Posts : 435
      Rep Power : 659
      Likes Received
      41
      Likes Given
      0

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By kwamwewe
      haya mbona unayaandika hapa tu huwezi weka muhadhara ukawaambia watu haya ??? unakimbilia JF na Magazetini tu !!!

      Mbona waliokuwemo katika system tokea kuundwa Huo Muungano , wengine wahai wanasema vyengine???
      Unafikri ana ubavu huo?
      Mzee Mwanakijiji likes this.

    19. #76
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,519
      Rep Power : 46714
      Likes Received
      16435
      Likes Given
      8471

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Sir Leem
      Unafikri ana ubavu huo?
      kweli unafikiri kuna yeyote anayeweza kujadiliana na mimi kwa hao jamaa? zaidi itakuwa ni yale yale tu "ooh wewe Mkristu huelewi!". Hakuna size yangu kule. Siyo kwenye hili aisee.
      [email protected]
      The Best of Tanzanian Socio-Political Blogging - http://www.mwanakijiji.com

    20. #77
      punainen-red's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 18th November 2010
      Posts : 1,737
      Rep Power : 854
      Likes Received
      390
      Likes Given
      19

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Wazanzibar mmepewa njia rahisi ya kusepa, mda wa makelele umekwisha...KWAHERINI!!
      Mzee Mwanakijiji likes this.

    21. #78
      muheta's Avatar
      Member Array
      Join Date : 24th May 2012
      Posts : 15
      Rep Power : 356
      Likes Received
      9
      Likes Given
      8

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Tuliwapenda sana kwa miaka 46 lakini naona hawapendeki! potelea mbali, hakuna anayekataa kuwapatia talaka wanayoitaka!!! Wanachotakiwa kufanya ni kuomba talaka yao, waende! Let them go. Tumechoka na kelele zao kila siku.

    22. #79
      Nonda's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th November 2010
      Location : Gongo La Mboto
      Posts : 5,834
      Rep Power : 1866
      Likes Received
      939
      Likes Given
      367

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Quote By Zinedine
      Nonda, umetoka usingizini au? Uhalali au uharam au 'whatever' juu ya Muungano huu mmeshasema ktk mikutano yenu na JUMIKI, kilichopo hapa ni: LET ZANZIBARI GO!
      Zinedine
      Bado nimelala..niko kwenye ndoto kuwa niko katika mikutano yetu na JUMIKI.


      Mkuu kama umesoma mchango wangu na kuelewa nimefanya masahihisho kidogo juu ya matumizi ya majina Tanzania na bara katika mchango wa Pasco.

      Unasema:Kilichopo hapa ni :Let ZANZIBARI GO!

      Why don't we let Zanzibar go?

      Haiwezekani baada ya gazabu, hasira tulizonazo kuwaambia "pack and go!"

      I would rather have the courage to say "GO!"

      Kwa sababu gani hatu"opt" hii option? Hakuna mwenye uwezo/ujasiri katika viongozi,wabunge ,watendaji wa Tanganyika wa kusema" Zanzibar go!"

      Nani ametoka usingizini? Zinadine au Nonda?

      Kwa bahati mbaya Mijadala ya sasa imeanza/imeanzishwa juu ya dhana kuwa UAMSHO(waislamu wa Zanzibar) wamechoma makanisa. This was a false start kwa mijadala hii. Tumeingia mtego wa Magamba.
      Zinedine likes this.

    23. #80
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Let Zanzibar Go! - Kwanini Zanzibar hawahitaji kuwashawishi Watanganyika ili watoke kwenye Muung

      Nonda, mkuu ebu tazama picha hiyo hapo juu kisha utuambie kama kweli hao ni Magamba?.. Hawa ni wananchi wenye hasira na wenye kuitaka haki yao kwa nini nasi tusiwasikilize ikiwa tunawasikia watu wa Palestine au Burma..

      Maadam tunawapa muda tosha ifikapo July mosi 2014 wawe tayari wameisha fanya maamuzi ya kura za maoni basi hatuna sababu ya kuendelea kulonga. Kazi kwao, badala ya kuandamana walivamie bunge lao kesho na kuomba kupiga kura za maoni kama walivyofanya mwaka 2010.

      Viongozi wa serikali ya mseto kutoka CUF na CCM Zanzibar (baraza la Mapinduzi) wapeni wananchi wenu haki yao ya msingi, tena kama ikiwezekana nasi bara tuandamane kuwaunga mkono Wazanzibar ili wapewe ruksa ya haki yao kudai kuondoka ktk Muungano ifikapo July 1 2014.
      Chief and Nguruvi3 like this.
      Exploration of reality

    Page 4 of 17 FirstFirst ... 2345614 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...