Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

    Report Post
    Page 2 of 2 FirstFirst 12
    Results 21 to 33 of 33
    1. #1
      n00b's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th April 2008
      Posts : 768
      Rep Power : 9824
      Likes Received
      1427
      Likes Given
      166

      Default Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

      YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      By Zitto Kabwe

      TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
      06.06.2012
      YAH: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      Ndg. Waandishi wa Habari

      Mwaka 2011/2012 Kambi ya Upinzani Bungeni ilitangaza Vipaumbele vyake katika Bajeti Mbadala ambavyo vilikuwa:

      1. Kupunguza misamaha ya kodi mpaka 1% ya pato la Taifa kutoka 3%

      2. Kupunguza kodi kwenye bidhaa za mafuta ya petrol na dizeli ili kupunguza mfumuko wa bei

      3. Kufuta mfumo wa posho za vikao (Sitting allowances).

      4. Kupeleka sehemu ya tozo ya ujuzi (Skills Development levy-SDL) kwenye bodi ya mikopo ya elimu ya juu.

      Masuala haya pamoja na mengine yalikuwa sehemu ya Bajeti kivuli iliyowasilishwa Bungeni na Kambi ya Upinzani.

      Mapendekezo mawili,

      (1) Kodi za mafuta ya Petrol na Diseli na
      (2) Tozo ya SDL yalikubaliwa na kutekelezwa. Pendekezo la misamaha ya kodi lilikubaliwa lakini Serikali imeshindwa kulitekeleza na pendekezo la kufutilia mbali posho za vikao halikukubaliwa.

      Kambi Rasmi ya Upinzani inataka maelezo ya kina ya kwa nini Serikali imeshindwa kutekeleza ahadi yake iliyoitoa Bungeni kwamba misamaha ya kodi itapungizwa mpaka kufikia 1% ya pato la Taifa. Halikadhalika Kambi ya Upinzani inarejea wito wake wa kufutwa kwa Mfumo wa posho za vikao (sitting allowances).
      Serikali imependekeza Bajeti ya Tshs. 15trillioni kutoka Tshs. 13 trillion. Hata hivyo ni dhahiri kwamba Bajeti ya 2011/12 ilikuwa ina changamoto kubwa za utekelezaji. Serikali ieleze itawezaje kutekeleza Bajeti ya 15trillioni?
      Katika Bajeti Mbadala ya 2012/2013 Kambi ya Upinzani itajikita katika maeneo yafuatayo na kuishinikiza Serikali kuyatekeleza.

      1. Kuendelea kushinikiza kupunguzwa kwa misamaha ya kodi mpaka 1% ya Pato la Taifa. Hivi sasa misamaha ya kodi ni sawa na misaada yote kutoka nchi wahisani, Tshs 1.03 trillioni ni sawa na 3% ya Pato la Taifa.

      2. Kuelekeza raslimali fedha kwenye maendeleo vijijini hasa kujenga miundombinu kama barabara za vijijini na umeme vijijini.

      3. Kuelekeza fedha za kutosha kukarabati Reli ya Kati na kufufua njia za Reli za Tanga, Moshi na Arusha.

      4. Kuongeza wigo wa kutoza tozo la ujuzi (Skills Development Levy) ambapo sasa waajiri wote walipe ikiwemo Serikali na mashirika ya umma. Pia kupunguza tozo hili mpaka 4% ambapo 1/3 itaenda VETA na vyuo vya Ufundi na 2/3 itaenda Bodi ya Mikopo ili kukabili changamoto ya mikopo kwa wanafunzi.

      5. Kushusha kima cha chini cha kodi ya mapato (PAYE) mpaka 9% ili kuwezesha wananchi wa hali ya chini kubaki na fedha za kutumia na kukuza uchumi.

      6. Kuongeza mapato ya ndani na kupunguza mikopo ya kibiashara kwa kuhakikisha mapato ya ndani yanafikia 20% ya pato la taifa, kuongeza nguvu za kisheria na udhibiti ili TRA ikusanye mapato zaidi kwenye kampuni za simu na kwenye shughuli za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi.

      7. Kutayarisha Taifa kuwa na uchumi wa Gesi.

      8. Kupunguza /kufuta kodi kwenye bidhaaa za vyakula kwa muda maalum ili kushusha mfumuko wa bei.

      9. Kuweka mfumo mpya wa elimu kwa kushirikisha sekta binafsi katika kutoa elimu kwa ubora zaidi, ikiwemo kuundwa kwa chombo cha Udhibiti wa Elimu(Regulatory authority)

      10. Kutoa vipaumbele na unafuu vya kikodi kwa viwanda vya ndani vinavyotumia malighafi za nchni hasa za kilimo na zenye kuongeza ajira kama Korosho,Pamba na Mkonge.

      Kambi ya Upinzani itaendelea kufuatilia kwa karibu sana suala la kukua kwa deni la Taifa amabalo limefikia hadi Tshs 22 trillioni na kutaka ukaguzi maalum kuhusu akaunti ya Deni la Taifa.

      Kambi ya Upinzani itawekeza kusimamia kwa karibu suala la matumizi yasiyo na tija ya Serikali hasa kwenye magari na posho mbalimbali na Kwamba fedha nyingi zitumike kwa miradi mikubwa ya maendeleo ili kukuza ajira. Halikadhalika namna ya kupta fedha za kutekeleza mpango wa Maendeleo wa Miaka mitano

      Asanteni sana!

      …………………………….
      Zuberi Kabwe Zitto(Mb)

      Waziri Kivuli-Fedha na Uchumi.
      I seriously mean it when I say, 'Get a life'

    2. FemaTV & Radio

    3. #21
      Makupa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 11th April 2011
      Posts : 2,175
      Rep Power : 809
      Likes Received
      249
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Nteko Vano
      Mh. Zitto hongera kwa vipaumbele vinavyolenga kutukomboa kutoka katika hali hii ngumu ya maisha. Hata hivyo nina maswali machache:

      1. Nasikia Mtwara kulikuwa na reli je, kwanini bajeti yenu haikuigusa hiyo reli
      2. Kushinikiza kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma sio kipaumbele chenu? Hamuoni umuhimu wa hili?
      3. (Wadau) naombeni elimu kidogo ya kitu hiki tozo za development skills. Pia ni kwanini wakatwe watumishi wa serikali na mashirika ya umma tu?

      Vinginevyo vimesimama imara kwa maoni yangu
      Mtwara reli itapekeka nini wewe

    4. #22
      jingalao's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 12th October 2011
      Location : kikonga
      Posts : 728
      Rep Power : 529
      Likes Received
      127
      Likes Given
      27

      Default Re: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      huwezi kuongelea bajeti/maendeleo bila kugusa sekta ya afya.huu ni umbumbumbu wa hali ya juu.tumeshuhudia mgomo wa madaktari uliotikisa taifa sasa iweje kambi ya upinzani ikae kimya?watanzania kukosa madawa na huduma bora za afya ni jambo la kupewa kipaumbele.

      KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

    5. #23
      Nteko Vano's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2012
      Location : Dar es salaam
      Posts : 428
      Rep Power : 449
      Likes Received
      90
      Likes Given
      26

      Default Re: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      Quote By Makupa
      Mtwara reli itapekeka nini wewe
      Arusha na Tanga itapeleka nini mkuu?

      Mtwara kuna bandari na ile reli inaenda moja kwa moja bandarin. Je, unafikiri itapeleka nini? Ziada cheki hapo chini

      Mtwara Line (Southern Province Railway) - (defunct)In 1949 a line was built to link the Tanganyika groundnut scheme plantations around Nachingwea with the port of Mtwara. The scheme famously foundered and the railway was abandoned in 1962. Proposals have been made for a new railway to link Mtwara to iron ore deposits in the west, perhaps linking via Songea to Liganga.

      Last edited by Nteko Vano; 6th June 2012 at 18:34.

    6. #24
      Geru's Avatar
      Member Array
      Join Date : 11th August 2009
      Posts : 57
      Rep Power : 508
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default

      Quote By Nteko Vano
      Mh. Zitto hongera kwa vipaumbele vinavyolenga kutukomboa kutoka katika hali hii ngumu ya maisha. Hata hivyo nina maswali machache:

      1. Nasikia Mtwara kulikuwa na reli je, kwanini bajeti yenu haikuigusa hiyo reli
      2. Kushinikiza kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma sio kipaumbele chenu? Hamuoni umuhimu wa hili?
      3. (Wadau) naombeni elimu kidogo ya kitu hiki tozo za development skills. Pia ni kwanini wakatwe watumishi wa serikali na mashirika ya umma tu?

      Vinginevyo vimesimama imara kwa maoni yangu
      NO. 3 hapo juu SDL ni 6% ya gross pay kwa waajiri wote na hii siyo gharama ya mfanyakazi bali mwajiri.

    7. #25
      Pendael laizer's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th January 2012
      Posts : 945
      Rep Power : 560
      Likes Received
      90
      Likes Given
      5

      Default Re: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      Mimi hapo kwenye vipaumbele vya miundo mbinu na umeme vijijini pamoja na misamaa yakodi vitamkomboa mkulima huko kijijini na kuondokana umaskini uliokidhiri huko. HONGERA KAMBI YA UPINZANI.

    8. Miaka 50

    9. #26
      Nteko Vano's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2012
      Location : Dar es salaam
      Posts : 428
      Rep Power : 449
      Likes Received
      90
      Likes Given
      26

      Default Re: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      Quote By Geru
      NO. 3 hapo juu SDL ni 6% ya gross pay kwa waajiri wote na hii siyo gharama ya mfanyakazi bali mwajiri.
      Ahsante mkuu hiki kitu nimekisikia hapa Pape amenipa darasa hapo juu na wewe umeniongezea.

    10. #27
      Nsuri's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd October 2011
      Posts : 563
      Rep Power : 497
      Likes Received
      170
      Likes Given
      130

      Default

      Mh. Zitto tunashukuru sana. Mimi nadhani serikali iangalie upya namna inavyokusanya ushuru. Tuna vyanzo vingi sana vya mapato esp. Customs. TRA hawafanyiqi vizuri' fedha nyingi zinabaki mikononi mwa watumishi wa TRA. Pia hivi mapato yanayokusanywa na mashirika ya umma kama TCRA' TPA' Tanapa yanaenda wapi?wanatumia fedha za umma vibaya.

    11. #28
      mwana wa africa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 17th April 2011
      Posts : 429
      Rep Power : 495
      Likes Received
      56
      Likes Given
      4

      Default Re: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      Quote By Nteko Vano
      Mh. Zitto hongera kwa vipaumbele vinavyolenga kutukomboa kutoka katika hali hii ngumu ya maisha. Hata hivyo nina maswali machache:

      1. Nasikia Mtwara kulikuwa na reli je, kwanini bajeti yenu haikuigusa hiyo reli
      2. Kushinikiza kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma sio kipaumbele chenu? Hamuoni umuhimu wa hili?
      3. (Wadau) naombeni elimu kidogo ya kitu hiki tozo za development skills. Pia ni kwanini wakatwe watumishi wa serikali na mashirika ya umma tu?

      Vinginevyo vimesimama imara kwa maoni yangu
      NTEKO VANO

      Hakuna mantiki yoyote kuongeza mshahara wakati hatuwezi kukabiliana na mfumuko wa bei. jambo la muhimu ni kudhibiti mfumuko wa bei ili mwananchi aweze kupanga bajeti kwa kipato anachokizalisha na kwa wafanyakazi wa umma kupunguzwa kodi ya PAYE hadi 9% ni zaidi ya ongezeko la mshahara. kubadilika kwa tarakimu katika mshahara hakuna mashiko kama kunasbabisha gharama za maisha kupanda.

    12. #29
      Ruttashobolwa's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 22nd February 2012
      Posts : 13,448
      Rep Power : 19777
      Likes Received
      4284
      Likes Given
      1187

      Default Re: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      Vipaumbele ni mevikubali sana.
      Kama serikali itazingatia,basi itakuwa budget ya ukombozi kwa mtanzania,lakin kwa mtindo wa kutokubaliana na mambo ya wapinzani hasa kwenye kodi ya mafuta.

      Ni wakati sasa ccm wajue na kusoma alama za nyakati , watu wamechoka na maisha na wanataka utendaji sio maneno.

      Big up zitto

    13. #30
      Nteko Vano's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 28th February 2012
      Location : Dar es salaam
      Posts : 428
      Rep Power : 449
      Likes Received
      90
      Likes Given
      26

      Default Re: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

      Quote By mwana wa africa
      NTEKO VANO

      Hakuna mantiki yoyote kuongeza mshahara wakati hatuwezi kukabiliana na mfumuko wa bei. jambo la muhimu ni kudhibiti mfumuko wa bei ili mwananchi aweze kupanga bajeti kwa kipato anachokizalisha na kwa wafanyakazi wa umma kupunguzwa kodi ya PAYE hadi 9% ni zaidi ya ongezeko la mshahara. kubadilika kwa tarakimu katika mshahara hakuna mashiko kama kunasbabisha gharama za maisha kupanda.
      Mkuu, PAYE kwa sasa ni 13% kama sikosei, hivyo itashuka kwa asilimia 4%. Ni wazo zuri lakini nilikuwa nafikiria ni vema tungepambana kote kote kupunguza mfumuko wa bei, kushusha kodi ya PAYE na kupigania kuongeza mshahara wa kima chini. Kumbuka haya ni mapendekezo ya kambi ya upinzani yanaweza kutekelezwa au la. Hata hivyo inflation haitashuka kwa mara moja hivyo bado kupigania ongezeko la mshahara kuna umuhimu wake.

    14. #31
      kamau ngilisho's Avatar
      Member Array
      Join Date : 14th April 2012
      Posts : 39
      Rep Power : 365
      Likes Received
      3
      Likes Given
      0

      Default"display:none" id="progress_4006099" style="display:none;visibility:hidden;" data-cfsrc="template/JamiV1/default/misc/quote_icon.png" alt="Quote" /> By Nteko Vano

      Mh. Zitto hongera kwa vipaumbele vinavyolenga kutukomboa kutoka katika hali hii ngumu ya maisha. Hata hivyo nina maswali machache:

      1. Nasikia Mtwara kulikuwa na reli je, kwanini bajeti yenu haikuigusa hiyo reli
      2. Kushinikiza kuongeza mishahara kwa watumishi wa umma sio kipaumbele chenu? Hamuoni umuhimu wa hili?
      3. (Wadau) naombeni elimu kidogo ya kitu hiki tozo za development skills. Pia ni kwanini wakatwe watumishi wa serikali na mashirika ya umma tu?

      Vinginevyo vimesimama imara kwa maoni yangu
    nadhani kuna neno hujalisoma hapo juu badala ya ongezeko la mishaara anataka kodi ipunguzwe kwenye mishahara.
    Reply With Quote

  • #32
    Kimbunga's Avatar
    JF Platinum Member Array
    Join Date : 4th October 2007
    Location : Kisiwani Juma
    Posts : 7,472
    Rep Power : 6167
    Likes Received
    3040
    Likes Given
    1015

    Default

    Quote By msolopa ganzi
    yeah ni kweli kuna haja ya kufufua njia ya reli ya tanga,moshi mpaka arusha pamoja na kukarabati reli ya kati itasaidia sana barabara zetu ziweze kudumu,na kuboresha uchumi wetu kwa kasi.
    MKuu msolopa ganzi hili ni tatizo la taifa. Serikali ikifanikiwa kuimarisha hizo reli na mizigo iwe inapitia kwenye reli basi itakuwa ukombozi mkubwa kwenye kuimarisha barabara zetu. Lakini mkuu nani akubali kuimarisha hizi reli wakati wadau wenyewe ndio hao wanaomiliki malori yanayobeba mizigo na kuharibu barabara! Tusubiri tumuone Dr. Mwakyembe atafanya nini.

  • #33
    Mkira's Avatar
    JF Senior Expert Member Array
    Join Date : 10th May 2006
    Posts : 417
    Rep Power : 1140
    Likes Received
    36
    Likes Given
    7

    Default Re: Taarifa kwa Umma: VIPAUMBELE VYA KAMBI YA UPINZANI KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013

    Quote By Nteko Vano
    Mkuu, PAYE kwa sasa ni 13% kama sikosei, hivyo itashuka kwa asilimia 4%. Ni wazo zuri lakini nilikuwa nafikiria ni vema tungepambana kote kote kupunguza mfumuko wa bei, kushusha kodi ya PAYE na kupigania kuongeza mshahara wa kima chini. Kumbuka haya ni mapendekezo ya kambi ya upinzani yanaweza kutekelezwa au la. Hata hivyo inflation haitashuka kwa mara moja hivyo bado kupigania ongezeko la mshahara kuna umuhimu wake.

    YAANI CHADEMA MKITUMIA HII KETE YA KUSHUSHA PAYE LITAKUWA RUNGU LA MWISHO LAKUPIGILIA KWENYE KICHWA CHA JOKA CCM,

    MTU UNAPATA MSHAHARA MILION TATU UNALIPA PAYE LAKI NANE HUKU UKIENDA HOSPITAL HUPATI HUDUMA BADO ILI MTOTO WAKO APATE ELIMU BORA INABIDI ULIPE ZAIDI YA MILION MOJA KWA CHECHEKEA! yaani kama kuna manyanyaso makubwa ambayo JOKA CCM LINAWAFANYIA WAAJIRIWA WOTE NCHINI NI HUYU MDUDU PAYE. hatukatia tena tunaweza lipa zaidi kama basi utaona zinafanya nini katika kukufanya uishi kwa raha! pia na Kama serilaki haina vyanzo vingine cha ajabu wa 3 africa kuzalisha dhahabu lakini kodi haikusanywi huko kwa sasabu tu kuna vijoka ndani ya JOKA KUU CCM VINAMILIKI VISHARE VICHACHE AU VIMEHONGWA!

    Zitto na chadema tumieni hii kete vizuri MFANYAKAZI ATAKAE WANYIMA KURA ATAKUWA NI SEHEMU YA JOKA KUU CCM HAS 2015 ZIDISHENI MOTO KUHUSU PAYE. muda wa kulipa PAYE KUBWA BADO KWA SASABU TUNA VYANZO VINGI VYA KODI!

  • Study Abroad
    Page 2 of 2 FirstFirst 12

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...