Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

    Report Post
    Page 22 of 27 FirstFirst ... 122021222324 ... LastLast
    Results 421 to 440 of 531
    1. #1
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,892
      Rep Power : 12961
      Likes Received
      4572
      Likes Given
      7577

      Default Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Nimevipima vyama vya upinzani kwenye mizania yangu ya upembuzi yakinifu na kubaini bila ya mashaka yoyote yale bado havipo tayari kimfumo kutupatia Raisi bora na hizi ndizo nondo zangu zilizonifikisha hapo..:-

      a) Vyama vyote vya upinzani vimeiga mfumo mbovu wa kidemokrasia wa ccm na vinaendeshwa kibabe-kibabe mno na huku wenzao wa ccm kuanzia 2010 walianza kujivua gamba la udikteta pale waliporuhusu wabunge wake wachaguliwe na wananchi moja kwa moja...ingawaje bado wana safari ndefu kwenye hili lakini lazima niwapongeze ccm kwa angalau kujaribu....rushwa na kuingiliwa na ngazi za juu katika maoni ya wananchi ni changamoto ambazo ccm itabidi waendelee kuzitafutia muarobaini wake.

      Kwenye hili vyama vya upinzani wapo nyuma na tumeona hata chadema bila ya kupitisha kura ya maoni kwa wapigakura wa Arusha wakitumia kauli za kidikteta kukejeli kura za wanachama wao Arusha pale kamati kuu yao ilipotengua madiwani wakaidi wa Arusha...well, chadema worshippers...that was not democracy at all...it was dictatorship.........face it now before it is too late.....Only the truth will set you free

      b) Vyama vyote vya siasa vyenye wabunge Bungeni vimekumbwa na dhoruba kali la wizi na ubadhirifu wa ruzuku ya hazina na hakuna uthibiti wa aina yoyote ile!!!!!

      Kwa mtazamo wangu kama wapinzani wameshindwa hata kusimamia kidogo ambacho tumewapa ni kwa upuuzi upi utushawishi kuwakabidhi nchi yote?

      Njaa ya viongozi wa upinzani ni kali kulikoni ya viongozi wa ccm ambao pamoja na bandubandu kweli humaliza gogo lakini ccm hawana uchu wa kututafuna kama upinzani walionao.....ccm vibosile wake wamekwisha shiba njaa siyo kali sana kwa kipimo cha malinganisho.................l ol

      c) Mchakato wa katiba mpya umenifungua macho hila na upofu wa wapinzani ambao waliipinga tume kwa vile wao hawajaweka mrija wao ndani yake na kunyonya Hazina baada ya CCM kuwaingiza kingi - au niseme mkenge? - hakuna anayehoji uhalali wa Tume ya kukusanya maoni.

      Wote wanaimba wimbo wa CCM wa ya kuwa tume tajwa haina uwalakini na sasa wamehamia kwenye mabunge mawili ambako wanaona mirija yao ni michache na kwa hiyo wanatafuta namna ya kuiongeza.

      Hii siyo demokrasia hata chembe bali ni ubinafsi tu...period. Mwanamageuzi wa kweli atadai haki hata kama yeye ni mwathirika wa hayo mageuzi siyo yule ambaye hujigeuza mpiga filimbi ya Hamelini pale anapoona masilahi yake yamepigwa na tufani kali sana...anachofanya ni kulinda tonge lake la ugali lisidondokee pabaya tu....lol hao kweli ni wababaishaji tu hawatufai kabisa.........

      USHAURI:

      Hivyo chama chochote kile cha siasa ambacho kitashirikisha wanachama wake katika kuteua viongozi watakaopeperusha bendera za vyama vyao katika ngazi zote ikiwemo ya URAISI, UBUNGE, UDIWANI hadi UENYEKITI WA KITONGOJI kina nafasi njema ya kutupatia viongozi bora...na kutumia utaratibu huohuo katika kuwavua madaraka itakuwa imepiga hatua katika demokrasia shirikishi.

      Have your say too...unaridhika na demokrasia ndani ya vyama vya siasa hasa hivi vya upinzani hata sasa kuviamini kutupatia Raisi na viongozi wengineo bora bila ya kutushirikisha grassroots?
      Last edited by Rutashubanyuma; 6th June 2012 at 12:01. Reason: spelling..................duh
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    2. #421
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,892
      Rep Power : 12961
      Likes Received
      4572
      Likes Given
      7577

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      What do they do with it!.
      If you can monitor that of CDM where you don't belong why not in your party?.
      Kyaiyembe matatizo yanajulikana a muarobaini upo jikoni........
      Waberoya likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    3. #422
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,892
      Rep Power : 12961
      Likes Received
      4572
      Likes Given
      7577

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Duh, sikujua kuwa umeathirika kiasi hicho...I rest my case Rutabushanyuma, nawaachia Watanzania waamue na mpaka sasa naridhika na wanavyoitikia wito wa Chadema. Hawasombwi na malori kuhudhuria mikutano, hawahongwi ili wahudhurie mikutano na badala yake wanachangia hela zao kufanikisha mikutano...kama huwezi kuona kuwa hiyo ni peoples power sina namna ya kukusaidia, you are beyond rehabilitation kama ilivyo CCM.

      CCM is dying Rutashubanyuma, what signs do you have to see before you can accept this fact? Wengine tulishuhudia ikizaliwa na tunaomba Mungu atupe uzima tushuhudie ikifa na kuzikwa, imechokwa na kwa kuzidi kung'angania madaraka, kinaharakisha tu kuingia kaburini, kalaghabaho! Trust me, some of us have seen it all and for any right thinking individual, this is the right time to jump ship unless you have sworn to sink with it, have you?
      Mag3 Kama chama kina uwezo kwa nini wananchi wake wasisombwe na malori kama ni hoehae kama cdm basi ni kukata mbuga tu.............hivi kwa nini wana cdm hamtaki kabisa kuongelea hiyo people's power ni nini hasa kama siyo kumwuuliza mpigakura wako juu ya maamuzi ambayo alishirikishwa kuyafanya? Kama kuchagua au kuwaondoa viongozi wake wawe madiwani au hata awe mbunge....................what is this people's power ya cc ya cdm tu?

      Mbona kwenye hilo mnaingia mitini na kuishia kuilamu ccm kwa kila kituhata ambavyo vimo ndani ya uwezo wenu?
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    4. #423
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1746
      Likes Received
      1519
      Likes Given
      2835

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By Rutashubanyuma View Post
      Waberoya mashabiki wa cdm wana tatizo moja hawataki wananchi washirikishe katika kutambua viongozi bora lakini huku wakidao cdm ni chama cha people's power ni power ipi ambayo iankataza wapigakura kushirikishwa ?
      chama cha demokrasia...siku niliposikia yaliyompata chacha wangwe, na baadae zitto wakati anagombea uenyekiti nikajua chama kina wenyewe na wenyewe si wananchi!! tuhuma za kafulila, Leticia n.k ni zile zile zinazojulikana

      kesho watamsimaisha mgombea urais lakini si yule aliyepigiwa kura na wanachama, bali aliyeteuliwa na wazee! kwa malengo yao hidden!

      vyama ni vya watu, ila watu hawaonekani wanafanya nini, ila hao watu wapo kwa ajili ya kufacilitate mipango ya wenye vyama...wamefanikiwa kuwaadaa wengi malengo yao ni mazuri kwa mwonekano wa nje...
      Rutashubanyuma likes this.
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    5. #424
      Rutashubanyuma's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 24th September 2010
      Location : Arusha
      Posts : 38,892
      Rep Power : 12961
      Likes Received
      4572
      Likes Given
      7577

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      chama cha demokrasia...siku niliposikia yaliyompata chacha wangwe, na baadae zitto wakati anagombea uenyekiti nikajua chama kina wenyewe na wenyewe si wananchi!! tuhuma za kafulila, Leticia n.k ni zile zile zinazojulikana

      kesho watamsimaisha mgombea urais lakini si yule aliyepigiwa kura na wanachama, bali aliyeteuliwa na wazee! kwa malengo yao hidden!

      vyama ni vya watu, ila watu hawaonekani wanafanya nini, ila hao watu wapo kwa ajili ya kufacilitate mipango ya wenye vyama...wamefanikiwa kuwaadaa wengi malengo yao ni mazuri kwa mwonekano wa nje...
      Waberoya umenikumbusha mengi sana............mengi ya kusikitisha na hawa wapambe wa cdm hawataki kuzungumzia mapungufu yao wanachotaka ni kukamata dola tu at all costs.................
      Waberoya likes this.
      John 14:14 " If you ask anything in My Name, I will do it"

      John 14:15 "If you love Me, keep My commandments."

    6. #425
      Annael's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th September 2011
      Location : Dar es salaam, Tanzania
      Posts : 1,268
      Rep Power : 1514
      Likes Received
      244
      Likes Given
      259

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Jamani mimi nimesomaaaaa hizi post Kusema kweli CCM ndicho chama kinachoweza kutupatia maendeleo. Ila tu kinachoniboa bado wanaenda taratibu sanaaaaa. Ninashukuru maana wameanza kujirekebisha. Tuacheni ushabiki usio na tija
      MTU MPUMBAVU HATA UKIMTWANGA KWENYE KINU PAMOJA NA NGANO UPUMBAVU WAKE HAUMTOKI

    7. #426
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1746
      Likes Received
      1519
      Likes Given
      2835

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By Rutashubanyuma View Post
      Waberoya umenikumbusha mengi sana............mengi ya kusikitisha na hawa wapambe wa cdm hawataki kuzungumzia mapungufu yao wanachotaka ni kukamata dola tu at all costs.................
      inaitwa funika kombe mwanaharamu apite........wamekaa kimya, lakini hatujaona kuwa wametubu au wamebadilika, ila wenye nguvu na maneno mengi wameshinda.....ukweli umefunikwa.Lakini sio kuwa hatakuja kutokea itatokea tu tuombe maamuzi kama yale au udikteta kama ule usitokee wakiwa madarakani!! kwani ndio wako hivyo

      Naunga mkono juhudi zote za kupiga kelele ufisadi zinazofanywa na chama hiki, ila siungi mkono ufisadi wao wenyewe na kuminya demokrasia kwa kisingizio cha kuupinga ufisadi
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    8. #427
      Chesty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2009
      Posts : 1,057
      Rep Power : 710
      Likes Received
      159
      Likes Given
      23

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By Rutashubanyuma View Post
      ccm imeonyesha dira ya kuwa kuna tatizo kubwa la kimfumo wa uendeshaji wa nchi na tuendelee kukafuta ushauri wa kulinusuru taifa kwa kupanua wigo la demokrasia ndani ya chama chetu hususani nani atakayepeperusha bendera ya ccm kwenye uchaguzi wa 2015.............kwa kuhakikisha kura za maoni zinapigwa nchi nzima na chama kinawagharimia wagombea wake wakajielezee huko na kila kura ihesabiwe na kila mpigakura aone kura yake imeheshimiwa na hakuna uchakachuaji.................. ..haya maamuzi cdm hawatakaa kamwe kuyafanya kwani karibu viongozi wote watatupwa nje........
      CCM wanajua nini kinatakiwa kifanyike isipokuwa kinachotakiwa kifanyike ni kwa maslahi ya watanzania wote na hapo ndipo penye conflict na sera yao (Secret Policy) ya kujitajirisha wao na familia zao.

      Ufinyu wa akili unakulead kuamini kuwa CCM wameingia kwenye mfumo wa wizi na ubadhirifu kwa bahati mbaya na kwamba ipo siku watakapo pata uelewa watabadilika.

      Ni nani katika CCM asiyejua kuwa tume iliyopo sio huru, ni nani katika CCM asiyejua kuwa Rais kuwa na madaraka ya kuteua kila position haipelekei kuwa na Good Governance. Yote haya yanatetewa na CCM kwa nguvu zote kwa sababu mwisho wa siku yanawanufaisha hao Mafia wenzako.

      Mfumo bora ndio huo unapigiwa kelele na CDM wa kuwa na tume huru na kupunguza sana nadaraka ya raisi. Sasa tuambie ni kivipi hiyo mitazamo miwili kati ya CDM na CCM inafanana mpaka unaropoka kuwa CDM wanaiga mifumo ya CCM.
      Mag3 likes this.

    9. #428
      Sir R's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd October 2009
      Location : Moshi
      Posts : 1,146
      Rep Power : 720
      Likes Received
      101
      Likes Given
      24

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By Rutashubanyuma View Post
      zomba mie ninatetea mifumo ya utawala bora...........naona upinzani wamekalia kuti kavu tu.atayasema nimenunuliwa nitamwabisha na makala yangu ijayo ambayo nitailima ccm vilivyo........hapo ndipo atajua mie sifungamani na upande wowote ule.........
      CCM usiwape tena nafasi hata kama wapinzani niwadhaifu kiasi gani.
      Wapinzania wanarekebishika lakini CCM ni kama shetani hawezi kutubu akasamehewa.

      Inawezekana vyama vya upinzani vina udhaifu lakini CCM inao udhaifu zaidi.
      Mag3 likes this.
      Umaskini wa Tanzania ni Matokeo ya Akili ndogo kuongoza Nchi

    10. #429
      Chesty's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 30th August 2009
      Posts : 1,057
      Rep Power : 710
      Likes Received
      159
      Likes Given
      23

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By Rutashubanyuma View Post
      Nia ipo, uwezo upo, kazi imeanza.tuache iendelee...................ya kulirekebisha taifa .......wengine waache wakemee kutoka majukwaani......... lemonade
      Sasa nimegundua kuwa Ruta hajui siasa kabisa, anafikiri kuwa CCM na mifumo yake ya wizi ni makosa ya bahati mbaya na sasa wameyagundua. Tambua kuanzia sasa kuwa mifumo hii ya wizi na ujambazi wa mchana inasimamiwa na CCM huku wakijua faida zake kwao na kwa familia zao.

      Baada ya watanzania kupata darasa la uraia na kujua nchi yao inavyoibiwa kupitia kwa wapambanaji akina Dr. Slaa et al nao wanajifanya eti hawakujua kuwa ni mifumo mibaya. Sasa the guilt for CCM ni kuwaibia watanzania kwa miaka yote hii kwa kuwa walikuwa hawajui haki zao.

      Na ndio maana ajenda ya kujirekebisha hatuitaki tunataka waondoke kwanza wakafanye marekebisho wakiwa nje ya government.
      Mag3 likes this.

    11. #430
      Mag3's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 31st May 2008
      Posts : 3,581
      Rep Power : 1817
      Likes Received
      2522
      Likes Given
      2549

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By Chesty View Post
      Sasa nimegundua kuwa Ruta hajui siasa kabisa, anafikiri kuwa CCM na mifumo yake ya wizi ni makosa ya bahati mbaya na sasa wameyagundua. Tambua kuanzia sasa kuwa mifumo hii ya wizi na ujambazi wa mchana inasimamiwa na CCM huku wakijua faida zake kwao na kwa familia zao.

      Baada ya watanzania kupata darasa la uraia na kujua nchi yao inavyoibiwa kupitia kwa wapambanaji akina Dr. Slaa et al nao wanajifanya eti hawakujua kuwa ni mifumo mibaya. Sasa the guilt for CCM ni kuwaibia watanzania kwa miaka yote hii kwa kuwa walikuwa hawajui haki zao.

      Na ndio maana ajenda ya kujirekebisha hatuitaki tunataka waondoke kwanza wakafanye marekebisho wakiwa nje ya government.
      Mkuu Chesty, hapa ni kama unatwanga maji kwenye kinu.. ruta, Waberoya et al...hawako peke yao. Mshuhudie na huyu anayeitwa zomba;
      Quote By zomba View Post
      CCM imedhihirisha tena kuwa ni chama kinachoongoza nchi na kisochofanya madudu ya uongo. Leo nimewaonea sana huruma chadema walipoanza kuchanwa na Nape, wakaja kina Wasira, Maghembe, Magufuli, Tibaijuka. Wakaeleza kwa ufasha kabisa na kujiamini jinsi CCM inayotimiza ahadi zake.

      Wasira akagusia jinsi chadema wanavyoiba hoja na kuwahi kuzitangaza kama ni zao. Magufuli akawakumbusha miradi ya barabara za lami ambayo haijawahi kuonekana barani Afrika kwa kiwango hiki kwa muda mfupi. Nawaonea huruma chadema wanavyopita wakidanganya Watanzania, leo magwanda ya khaki wameumbuka.
      Hawa ni wa kuwaacha tu ...si watu wa kuhangaika nao, Tsunami ya Chadema itawasomba tu. Eti CCM kuwasomba watu kwenye malori na kuwapa posho ili wahudhurie mikutano, ni haki yake kwani inatumia uwezo wake mkubwa wa kifedha. Eti chama cha kidemokrasia hakitakiwi kuchukua hatua dhidi ya wanachama wake kata kama wanasinginya katiba kwa maslahi binafsi.

      Ndio maana CCM imekuwa kimbilio la wahalifu kwani huko kuna kulindana, mhalifu gani atamchukulia hatua mhalifu mwenzake? Matokeo yake wezi wanabembelezwa warudishe walichokwiba, mafisadi wanaokumbatiwa wasije wakaiyumbisha dola na wauaji wa raia wanazawadiwa kwa kupandishwa vyeo. CCM inawahimiza wananchi kuuza utu wao kwa sinia la pilau, kipande cha kanga na kopo la chumvi.

      Sasa CCM imefikia hatua ambayo imetekwa nyara na wahalifu na mtu yeyote mwenye nia ya kuwatetea wananchi ndiye mbaya, hatakiwi humo. Vyombo vya kuwalinda wananchi na mali zao vimegeuka na kuwa vya kidhalilishaji dhidi ya raia wema wanaopinga uonevu. Tazama Chama hiki cha Kifisadi kinavyotetewa humu na baadhi ya wachangiaji hadi mtu anathubutu kuanzisha mada kama hii kukitetea.

      Lakini linalosikitisha kuliko yote ni kuwa kina wanazi ambao pamoja na shida zote hizi na jitihada za Chadema kuwaelimisha wameshindwa kufunguka macho. Ni kama wamelogwa vile, wana imani kuwa kilichooza bado kina ubani, wana imani kuwa ipo siku mlafi atashiba na kuacha tabia yake ya ulafi, wana imani kuwa aliyeonja nyama ya binadamu ataacha...! Lakini siku ya kiama inakuja na hilo wakae wakilijua.
      Mwita Maranya and Chesty like this.
      The true sign of intelligence is not knowledge but imagination.
      Education is what remains after one has forgotten what one has learned in School
      -Albert Einstein.

    12. #431
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 16,053
      Rep Power : 14671
      Likes Received
      2955
      Likes Given
      2099

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Leo magwanda mmeshikwa pabaya kweli. Hivi mnalalamika kuhusu watu kupakiwa kwenye malori, mmeshawahi kuwauliza viongozi wenu wanatumia fedha ngapi kwenye hii mikutano yao na zinakwenda wapi? au ndio yale ma v x 8 sita ya mwenyekiti?
      Rutashubanyuma likes this.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    13. #432
      Ritz's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 1st January 2011
      Location : Republic of Nauru
      Posts : 19,235
      Rep Power : 12776
      Likes Received
      6454
      Likes Given
      999

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Chadema mbona mnalamika sana kuwa watu wameletwa na magari mbona hata nyie fuso za Chadema zilikuwa zinasomba watu kutoka Kimara Bonyokwa, Kimara Temboni, Kimara Suka.
      zomba and Rutashubanyuma like this.

    14. #433
      Bob G's Avatar
      JF Bronze Member Array
      Join Date : 5th October 2011
      Location : UK Manyasi
      Posts : 1,733
      Rep Power : 736
      Likes Received
      301
      Likes Given
      36

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      mawazo yako yamepitwa na wakati, na yanapuuza uwezo mkubwa walionao viongozi wa upinzani Tanzania,

    15. #434
      sheky's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 2nd April 2012
      Posts : 177
      Rep Power : 399
      Likes Received
      39
      Likes Given
      10

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Katika Uongozi kikubwa ni maono na jinsi ya kuweza kufikia maono; ni uwezo wa kuwafanya wasiokuelewa wafanye unaloona na wafurahie mafanikio. Suala la Demokrasia lina wakati ambapo haliwezi kuwa dawa na suluhisho kwa kila tatizo. Wako wanao lalamika na kulaani kuwa Kagame ni dikteta. Unaweza kujiuliza kati ya dikteta Kagame na m-demokrasia Kikwete heri iko wapi? Si mdharau raisi wa Taifa letu hata kama sio chaguo, lakini hoja ni kuwa demokrasia kuna wakati inafaa na kuna wakati ukiwa na visionary dictator inaweza kuwa daraja la kuvuka toka katika ujinga wa kiutawala. Mfumo wetu kwa sasa Tz tunahitaji mtu mwenye msuli wa kuweza kulisukuma trekta hili ambalo limeishiwa mafuta. Bila kuwa na msuli huo bla blah na kudai tunaijua demokrasia kutatutia gizani zaidi. Kwangu ninaona ni wakti mzuri kwa CCM kupisha wengine. Kwa sasa ni heri shetani nisiyemjua kuliko malaika asiyetimiza.
      Rutashubanyuma likes this.

    16. #435
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1746
      Likes Received
      1519
      Likes Given
      2835

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By Mag3 View Post
      Mkuu Chesty, hapa ni kama unatwanga maji kwenye kinu.. ruta, Waberoya et al...hawako peke yao. Mshuhudie na huyu anayeitwa zomba;

      Hawa ni wa kuwaacha tu ...si watu wa kuhangaika nao, Tsunami ya Chadema itawasomba tu. Eti CCM kuwasomba watu kwenye malori na kuwapa posho ili wahudhurie mikutano, ni haki yake kwani inatumia uwezo wake mkubwa wa kifedha. Eti chama cha kidemokrasia hakitakiwi kuchukua hatua dhidi ya wanachama wake kata kama wanasinginya katiba kwa maslahi binafsi.

      Ndio maana CCM imekuwa kimbilio la wahalifu kwani huko kuna kulindana, mhalifu gani atamchukulia hatua mhalifu mwenzake? Matokeo yake wezi wanabembelezwa warudishe walichokwiba, mafisadi wanaokumbatiwa wasije wakaiyumbisha dola na wauaji wa raia wanazawadiwa kwa kupandishwa vyeo. CCM inawahimiza wananchi kuuza utu wao kwa sinia la pilau, kipande cha kanga na kopo la chumvi.

      Sasa CCM imefikia hatua ambayo imetekwa nyara na wahalifu na mtu yeyote mwenye nia ya kuwatetea wananchi ndiye mbaya, hatakiwi humo. Vyombo vya kuwalinda wananchi na mali zao vimegeuka na kuwa vya kidhalilishaji dhidi ya raia wema wanaopinga uonevu. Tazama Chama hiki cha Kifisadi kinavyotetewa humu na baadhi ya wachangiaji hadi mtu anathubutu kuanzisha mada kama hii kukitetea.

      Lakini linalosikitisha kuliko yote ni kuwa kina wanazi ambao pamoja na shida zote hizi na jitihada za Chadema kuwaelimisha wameshindwa kufunguka macho. Ni kama wamelogwa vile, wana imani kuwa kilichooza bado kina ubani, wana imani kuwa ipo siku mlafi atashiba na kuacha tabia yake ya ulafi, wana imani kuwa aliyeonja nyama ya binadamu ataacha...! Lakini siku ya kiama inakuja na hilo wakae wakilijua.
      Mag3 kuna kipindi huwa unachemka to the maximum, na kwangu mimi wewe ni mtu mdogo mno!

      Sikutegemea kuwa kwa akili zako na uzoefu wako uanze ku-mention majina ya watu humu kama akina JF-kata ambao wanajulikana kutoa matusi na bila kujibu hoja

      sasawaberoya hapa anatokea wapi na kwa nini??

      kama waberoya kaandika kitu, jibu right there na sio unakuja kujumuisha

      kama unajiona wewe ndie chadema na ni sifa kuwa chadema please be free to do so!! personally napenda changes lakini sitafikia hatua ya kuvua utu wangu kwa kushindwa kuuliza maswali au kukosoa in the name of change!!

      Yaani ninavyoona mkuu uko radhi kuona slaa anamvua nguo mama yako hadharani (ashakumu si matusi)na utakaa kimya tu simply kwa sababu slaa ni chadema na hakosei!! what a joke!!!

      acha ujinga mkuu, wengine humu tunaweka jf ionekane atleast ina kila watu wa kila caliber, sasa ukitaka kusoma thread za chadema tu hazina 'feel' wala food for thought una gain nini?? na ukitaka waberoya aondoke humu kwa sababu anauliza maswali au kusema ukweli unataka ubaki na akina nani?? hutaki ubongo wako u-gain kitu mkuu au kwa sababu umezeeka? na kuiweka brain yako i-we challenged au kupokea kitu kipya unachoka??

      kwa taarifa yako soma signature yangu iko pale pale na ukome kuandika andika, wazee kama wewe tutatoana nishai humu mpaka uone jukwaa chungu, wageni wageni tutawaacha tu waseme maana hatujuani

      mara ngapi nimeandika thread za kui-support chadema?? nilikuwa nani muda huo?

      Take things easy?? mkuu acheni mapressure na magubu baada ya ku-mess up ujana wenu

      I will always take JF a nice place to enjoy, learn, receive challenge and make friendship as much as I can, mi hasira na stress zenu za maisha bakizeni huko!!

      wote tunataka CCM waondoke madarakani lakini hainifanyi nisiulize mnaotaka kuja mnakujakujaje? mbona hizo tuhuma za Mtei kumweka mbowe kilazima na za chacha wangwe huwa hauzijibu? na kama huwezi kuzijibu nikuweke kwenye category gani? gauche? leave waberoya alone is not of your type!!

      kwa uwezo wangu na akili zangu nakuona kama kinyago tu,. mtu usiyeweza kuuliza wala kukosoa na kutetea kila kitu una akili kweli?? I repeat leave waberoya alone, stop naming me!

      post zako wewe ni kutetea chadema na nyerere tu..what a contradiction!!
      Rutashubanyuma likes this.
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    17. #436
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,915
      Rep Power : 2990
      Likes Received
      2548
      Likes Given
      3634

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By Rutashubanyuma View Post
      Nimevipima vyama vya upinzani kwenye mizania yangu ya upembuzi yakinifu na kubaini bila ya mashaka yoyote yale bado havipo tayari kimfumo kutupatia Raisi bora na hizi ndizo nondo zangu zilizonifikisha hapo..:-

      a) Vyama vyote vya upinzani vimeiga mfumo mbovu wa kidemokrasia wa ccm na vinaendeshwa kibabe-kibabe mno na huku wenzao wa ccm kuanzia 2010 walianza kujivua gamba la udikteta pale waliporuhusu wabunge wake wachaguliwe na wananchi moja kwa moja...ingawaje bado wana safari ndefu kwenye hili lakini lazima niwapongeze ccm kwa angalau kujaribu....rushwa na kuingiliwa na ngazi za juu katika maoni ya wananchi ni changamoto ambazo ccm itabidi waendelee kuzitafutia muarobaini wake.

      Kwenye hili vyama vya upinzani wapo nyuma na tumeona hata chadema bila ya kupitisha kura ya maoni kwa wapigakura wa Arusha wakitumia kauli za kidikteta kukejeli kura za wanachama wao Arusha pale kamati kuu yao ilipotengua madiwani wakaidi wa Arusha...well, chadema worshippers...that was not democracy at all...it was dictatorship.........face it now before it is too late.....Only the truth will set you free

      b) Vyama vyote vya siasa vyenye wabunge Bungeni vimekumbwa na dhoruba kali la wizi na ubadhirifu wa ruzuku ya hazina na hakuna uthibiti wa aina yoyote ile!!!!!

      Kwa mtazamo wangu kama wapinzani wameshindwa hata kusimamia kidogo ambacho tumewapa ni kwa upuuzi upi utushawishi kuwakabidhi nchi yote?

      Njaa ya viongozi wa upinzani ni kali kulikoni ya viongozi wa ccm ambao pamoja na bandubandu kweli humaliza gogo lakini ccm hawana uchu wa kututafuna kama upinzani walionao.....ccm vibosile wake wamekwisha shiba njaa siyo kali sana kwa kipimo cha malinganisho.................l ol

      c) Mchakato wa katiba mpya umenifungua macho hila na upofu wa wapinzani ambao waliipinga tume kwa vile wao hawajaweka mrija wao ndani yake na kunyonya Hazina baada ya CCM kuwaingiza kingi - au niseme mkenge? - hakuna anayehoji uhalali wa Tume ya kukusanya maoni.

      Wote wanaimba wimbo wa CCM wa ya kuwa tume tajwa haina uwalakini na sasa wamehamia kwenye mabunge mawili ambako wanaona mirija yao ni michache na kwa hiyo wanatafuta namna ya kuiongeza.

      Hii siyo demokrasia hata chembe bali ni ubinafsi tu...period. Mwanamageuzi wa kweli atadai haki hata kama yeye ni mwathirika wa hayo mageuzi siyo yule ambaye hujigeuza mpiga filimbi ya Hamelini pale anapoona masilahi yake yamepigwa na tufani kali sana...anachofanya ni kulinda tonge lake la ugali lisidondokee pabaya tu....lol hao kweli ni wababaishaji tu hawatufai kabisa.........

      USHAURI:

      Hivyo chama chochote kile cha siasa ambacho kitashirikisha wanachama wake katika kuteua viongozi watakaopeperusha bendera za vyama vyao katika ngazi zote ikiwemo ya URAISI, UBUNGE, UDIWANI hadi UENYEKITI WA KITONGOJI kina nafasi njema ya kutupatia viongozi bora...na kutumia utaratibu huohuo katika kuwavua madaraka itakuwa imepiga hatua katika demokrasia shirikishi.

      Have your say too...unaridhika na demokrasia ndani ya vyama vya siasa hasa hivi vya upinzani hata sasa kuviamini kutupatia Raisi na viongozi wengineo bora bila ya kutushirikisha grassroots?
      Ruta,

      ..kwanza kudai eti tuwachague CCM kwasababu wameisha iba vya kutosha is really an insult to our intelligence. Actually ukiangalia trend za wizi na ufisadi wa CCM utagundua kwamba mambo huenda yakiongezeka toka awamu moja kwenda nyingine.

      ..kwa maoni yangu huu ushauri wako ni sawa na kumshawishi msichana aliyebakwa alale chumba kimoja na njemba iliyombaka kwa mategemeo kwamba njemba hilo limetosheka na haja zake kwa hiyo haliwezi kujaribu kumbaka kwa mara nyingine.

      ..juu ya ufisadi ambao wameshindwa kupambana nao, CCM wanaamini kwamba wana rekodi nzuri ktk kuongoza juhudi za maendeleo ktk nchi. They dont believe that they have let the wananchi down, kwamba wameharibu nchi kimaadili na kuichumi. Sasa chama ambacho kimebweteka kiasi hicho sidhani kama kinastahili imani ya wapiga kura wa Tanzania.

      ..tumefika mahali wa-Tanzania tumekuwa vichekesho ktk eneo hili la Afrika mashariki. Awamu hii ya JK imeshindwa na awamu ya Mwai Kibaki wa Kenya ktk ujenzi wa miundo mbinu wakati wenzetu walikuwa na machafuko baada ya uchaguzi mkuu. Ukiangalia Ethiopia, taifa lililosambaratika vita ya wenyewe kwa wenyewe, na balaa la njaa lilolosababishwa na ukame, leo wanazalisha hydro electric power kutuzidi wa-Tanzania. AMANI yetu na RASILIMALI zetu zimetusaidia nini?

      ..CCM HAIWEZI KUJIREKEBISHA BILA KUSHINDWA UCHAGUZI MKUU KWANZA.

    18. #437
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1746
      Likes Received
      1519
      Likes Given
      2835

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By sheky View Post
      Katika Uongozi kikubwa ni maono na jinsi ya kuweza kufikia maono; ni uwezo wa kuwafanya wasiokuelewa wafanye unaloona na wafurahie mafanikio. Suala la Demokrasia lina wakati ambapo haliwezi kuwa dawa na suluhisho kwa kila tatizo. Wako wanao lalamika na kulaani kuwa Kagame ni dikteta. Unaweza kujiuliza kati ya dikteta Kagame na m-demokrasia Kikwete heri iko wapi? Si mdharau raisi wa Taifa letu hata kama sio chaguo, lakini hoja ni kuwa demokrasia kuna wakati inafaa na kuna wakati ukiwa na visionary dictator inaweza kuwa daraja la kuvuka toka katika ujinga wa kiutawala. Mfumo wetu kwa sasa Tz tunahitaji mtu mwenye msuli wa kuweza kulisukuma trekta hili ambalo limeishiwa mafuta. Bila kuwa na msuli huo bla blah na kudai tunaijua demokrasia kutatutia gizani zaidi. Kwangu ninaona ni wakti mzuri kwa CCM kupisha wengine. Kwa sasa ni heri shetani nisiyemjua kuliko malaika asiyetimiza.
      your post is contradicting!! unatetea kuwa sio mara zote demokrasia inafanya kazi!! lakini unasema ccm ni wakati wao kuondoka?? wanaondokaje? kidemokrasia au? na kama sio ki-demokrasio huoni ccm wanaweza kuchukua ushauri wako kuwa muda wote demokrasia haifanyi kazi kwa hiyo wakaa madarakani kibabe?? elaborate please!!
      Rutashubanyuma likes this.
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    19. #438
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1746
      Likes Received
      1519
      Likes Given
      2835

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By JokaKuu View Post
      Ruta,

      ..CCM HAIWEZI KUJIREKEBISHA BILA KUSHINDWA UCHAGUZI MKUU KWANZA.

      CCM haiwezi kujirekebisha ikishindwa uchaguzi mkuu, itakufa!! simply kwa sababu haikujengwa kuweza kujirekebisha!!

      na ugonjwa huu ndio mnaoupeleka chadema kuwa hakitakuwa chama cha kujirekebisha kwa sababu hamuwezi kukosoa uozo uliomo humo na makosa yao!!

      kujirekebisha ni tabia
      JokaKuu and Rutashubanyuma like this.
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    20. #439
      Waberoya's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 3rd August 2008
      Location : Busia-Uganda
      Posts : 5,948
      Rep Power : 1746
      Likes Received
      1519
      Likes Given
      2835

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      Quote By JokaKuu View Post
      Ruta,

      ..kwanza kudai eti tuwachague CCM kwasababu wameisha iba vya kutosha is really an insult to our intelligence. Actually ukiangalia trend za wizi na ufisadi wa CCM utagundua kwamba mambo huenda yakiongezeka toka awamu moja kwenda nyingine.

      ..kwa maoni yangu huu ushauri wako ni sawa na kumshawishi msichana aliyebakwa alale chumba kimoja na njemba iliyombaka kwa mategemeo kwamba njemba hilo limetosheka na haja zake kwa hiyo haliwezi kujaribu kumbaka kwa mara nyingine.

      ..juu ya ufisadi ambao wameshindwa kupambana nao, CCM wanaamini kwamba wana rekodi nzuri ktk kuongoza juhudi za maendeleo ktk nchi. They dont believe that they have let the wananchi down, kwamba wameharibu nchi kimaadili na kuichumi. Sasa chama ambacho kimebweteka kiasi hicho sidhani kama kinastahili imani ya wapiga kura wa Tanzania.

      ..tumefika mahali wa-Tanzania tumekuwa vichekesho ktk eneo hili la Afrika mashariki. Awamu hii ya JK imeshindwa na awamu ya Mwai Kibaki wa Kenya ktk ujenzi wa miundo mbinu wakati wenzetu walikuwa na machafuko baada ya uchaguzi mkuu. Ukiangalia Ethiopia, taifa lililosambaratika vita ya wenyewe kwa wenyewe, na balaa la njaa lilolosababishwa na ukame, leo wanazalisha hydro electric power kutuzidi wa-Tanzania. AMANI yetu na RASILIMALI zetu zimetusaidia nini?

      ..CCM HAIWEZI KUJIREKEBISHA BILA KUSHINDWA UCHAGUZI MKUU KWANZA.
      agreed, Ruta alikosea hapa!
      Mwita Maranya likes this.
      You are not supposed to be so blind with patrotism that you cant face reality. Wrong is wrong no matter who says it. Malcom X

    21. #440
      Tangawizi's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 25th June 2009
      Posts : 943
      Rep Power : 696
      Likes Received
      188
      Likes Given
      184

      Default Re: Amini usiamini, CCM ina jukumu la kutupatia Rais bora mwaka 2015...

      CCM baada ya mkutano wa leo, kweli kuna dalili ya kutupatia Rais?
      "Carpe Diem...Seize the Day"

    Page 22 of 27 FirstFirst ... 122021222324 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...