Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

    Report Post
    Results 1 to 12 of 12
    1. #1
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,191
      Rep Power : 3553
      Likes Received
      3051
      Likes Given
      461

      Default UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      NA SHARON SAUWA

      5th June 2012

      Wasira naye awashukia

      WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira

      Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imewaonya baadhi ya viongozi waliomo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar ambao walihusika katika vurugu za hivi karibuni zilizofanywa na Jumuiya ya Uamsho kujitoa katika serikali.

      Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, jana mjini Dodoma, wakati wa kikao cha Baraza Kuu ka jumuiya hiyo.

      Shigela aliwataka viongozi wa serikali ambao wanajijua kuwa walijihusisha kwa namna mmoja au nyingine katika machafuko hayo kujiondoa mara moja kabla vijana hao hawajawafuata na kuwataja.

      “Dk. Shein (Rais wa Zanzibar) alisema atakula nao sahani moja, sisi tutakula nao kijiko kwa kijiko,” alisema Shigela huku akishangiliwa na wajumbe wa baraza hilo.

      Hata hivyo, alipoulizwa na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi zaidi, Shigela, alikataa kuwataja.

      Tangu kutokea kwa vurugu hizo zilizoanza Mei 26 hadi Mei 28 mwaka huu na kusababisha athari kubwa kutokana na uchomaji moto wa makanisa, kuvunjwa baa na kuharibiwa kwa mali za watu, zimekuwa zikitolewa kauli zikidai kuwa baadhi ya viongozi wa SUK walihusika kuchochea kutokana na kuwa washirika wa Uamsho.

      Hata hivyo, hadi sasa hakuna majina ya wanasiasa yaliyotajwa moja kwa moja kuhusiana na tukio hilo.

      WASIRA NAYE AWASHUKIA

      WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira, amesema kuwa Kikundi cha Jumuiya ya Uamsho kimevunja sheria kwa kujiingiza katika masuala ya siasa kutokana na kuhoji masuala ya Muungano ambayo ni ya kisiasa kitu ambacho ni kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake.

      Akizungumza jana katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, alisema kikundi cha Uamsho kilianzishwa kutekeleza majukumu ya kidini, lakini katika hali ya kushangaza kimeanza kujihusisha na mambo ya siasa hali iliyopelekea kuzuka kwa vurugu Visiwani Zanzibar.

      Wasira alisema kimsingi, dini ya Kiislamu haina mgogoro na dini nyingine, lakini kitendo cha kikundi cha Uamsho kuzusha vurugu zilizopelekea kuchomwa moto kwa makanisa kadhaa ni uvunjaji wa sheria kwa sababu suala la Muungano halina uhusiano na makanisa.

      “Wakatoliki na Waanglikana walikuwepo visiwa vya Zanzibar tangu miaka 100 iliyopita wakati Muungano una miaka 45 tu, lakini tunashangaa wenzetu wa Uamsho wametoka kwenye masuala ya kidini wamejiingiza kwenye mambo ya kisiasa,” alisema Wasira.

      Wasira alisema wanaosema kwamba Rais Jakaya Kikwete amezuia masuala ya Muungano yasijadiliwe ni waongo kwani Rais alichokisema ni kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiunda haijaundwa kwa lengo la kutaka kuvunja Muungano.

      Alisema tume hiyo iliyoundwa kwa kushirikisha makundi yote yakiwemo ya kidini, kisiasa na jamii imepokelewa na Watanzania kwa furaha kubwa bila malalamiko hivyo kinachotakiwa ni kwa kila mtu kutoa maoni kwa tume ili kuwe na Katiba nzuri yenye ushiriki wa maoni mbalimbali ya wananchi.

      Wasira aliwashukia watu wanaodai kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ina wajumbe wengi wa dini fulani na kusema siyo kweli kwani dini haikuwa sehemu ya sifa za kuteuliwa kwenye bali vigezo na sifa vilizingatiwa.

      MAWAZIRI WALIOTEMWA

      Alisema mawaziri walioachwa kwenye mabadiliko ya baraza jipya la mawaziri haina maana kwamba wote ni wezi kama inavyoelezwa na baadhi ya watu, bali kilichotokea wamewajibika kutokana na makosa pengine yaliyofanywa na wasaidizi wao.

      Aliongeza kuwa watu wanapotosha ukweli kwa kueleza kuwa waliongoza mashambulizi yaliyopelekea kuondolewa kwa mawaziri hao ni wabunge kutoka vyama vya upinzani, alisema ni uongo kwani wabunge wa CCM ndiyo waliongoza mapambano hayo.

      MAKUNDI NDANI YA CCM

      Wasira alisema hakuna chama ambacho hakina makundi, lakini makundi yaliyopo ndani ya Chama cha Mapinduzi ni ya kawaida ambayo yanashughulikiwa kichama, lakini kinachooneka yanakuzwa na baadhi ya vyombo vya habari.

      “Matatizo ndani ya chama yapo, lakini siyo ya ajabu maana huwezi kuwa na chama kikubwa kama CCM utegemee kisiwe na na tatizo hata chama cha malaika ni lazima kinaweza kuwa na matatizo, lakini CCM ni chama kikubwa chenye uwezo wa kuhimili mawimbi mengi, “alisema Wasira.

      Alisema mpango wa CCM wa kujivua gamba unatafsiriwa vibaya na baadhi ya vyama ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuja na falsafa ya kusema vua gamba vaa gwanda.

      Wasira alisema CCM ilikuja na kauli mbiu hiyo kwa lengo la kukabiliana na wanachama wake wanaoutaka uongozi kwa kutumia rushwa wasiendelee na rushwa na kwamba kama Chadema wanataka watu wanaotoa rushwa ndio waondoke CCM wakajiunge kwao ni sawa.

      CHANZO: NIPASHE

    2. Miaka 50

    3. #2
      Saint Ivuga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2008
      Posts : 20,648
      Rep Power : 10161
      Likes Received
      5647
      Likes Given
      12664

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      udikteta ...sasa kilichobaki ni kupeleka mswada kwenye baraza la mapinduzi wa kutomtambua makamu wa rais, na kukataza wabunge wetu kwenda dodoma ..tumeweza kuwa na katiba yetu bila kuwashirikisha watanganyika sembuse hili la Muungano
      JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.

    4. #3
      nngu007's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 2nd August 2010
      Posts : 11,191
      Rep Power : 3553
      Likes Received
      3051
      Likes Given
      461

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      Kama CCM wangekuwa wakweli tusingekuwa hapa, sasa kama wanajua hao watu walio kwenye serikali ya Zanzibar wawataje basi? kila siku CCM ndio tabia yao kuongea kwa Mafumbo kuwa wanajua kinachoendelea wanawajua hao wanajua nani kafanya makosa yale, lakini hali itatulia bila kutajwa kwa wakosaji na kusahaulika na wananchi, hawajui kuwa pia heshima ya chama CHA CCM inadondoka.

      Midomo Mingi Ndani ya CCM, kutunga Jazba za kujibu Maneno ya kiswahili lakini hawajui kujitoa Mhanga na kutajana ni nani kafanya kosa gani kwa Majina ili wawe wasafi. Wanatufanya sisi Wananchi Wajinga tunahitaji hizo Khanga, Kofia, Skafu, T-Shirt na Burudani za Wanamuziki kama sisi hatuna pa kwenda.

      Angalia Wassira Analala Bungeni Picha zinampiga, Anazomewa Jimboni kwake sasa hapa anaongea kama Parapanda na ni kitu kinachohitaji replacement ya hali ya Juu, amekuwa kwenye Siasa Tangu 1960 kwanini anawazibia watoto wake Ulaji?

    5. #4
      Tume ya Katiba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2012
      Location : Chumbuni-Zanzibar
      Posts : 2,675
      Rep Power : 0
      Likes Received
      538
      Likes Given
      273

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      Kiongozi wa UVCCM tanganyika anatoa amri kwa kiongozi wa serikalizanzibar? kweli wamelewa na madaraka hawa vijana!

    6. #5
      Saint Ivuga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st August 2008
      Posts : 20,648
      Rep Power : 10161
      Likes Received
      5647
      Likes Given
      12664

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      Quote By Tume ya katiba
      Kiongozi wa UVCCM tanganyika anatoa amri kwa kiongozi wa serikalizanzibar? kweli wamelewa na madaraka hawa vijana!
      na sijui kwa nini mnaendelea kuwachekea
      Tume ya Katiba likes this.
      JF the best place to be. and the POWER of God be with us all the time.

    7. FemaTV & Radio

    8. #6
      IsayaMwita's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 9th March 2008
      Location : Tarime
      Posts : 1,044
      Rep Power : 870
      Likes Received
      82
      Likes Given
      6

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      tumekusikia mzee wasira, ccm jinasueni kwa hili, haya...., sasa tunaona miluzi mingi ni lazima...., wakati mnahangaika kusolve kule znz wenzenu tunajijenga, kazi mnayo ccm.

    9. #7
      Simba Mangu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 24th November 2010
      Location : matiti hills ndutu
      Posts : 146
      Rep Power : 459
      Likes Received
      21
      Likes Given
      21

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      Quote By nngu007

      NA SHARON SAUWA

      5th June 2012

      Wasira naye awashukia

      WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira

      Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imewaonya baadhi ya viongozi waliomo ndani ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) Zanzibar ambao walihusika katika vurugu za hivi karibuni zilizofanywa na Jumuiya ya Uamsho kujitoa katika serikali.

      Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, jana mjini Dodoma, wakati wa kikao cha Baraza Kuu ka jumuiya hiyo.

      Shigela aliwataka viongozi wa serikali ambao wanajijua kuwa walijihusisha kwa namna mmoja au nyingine katika machafuko hayo kujiondoa mara moja kabla vijana hao hawajawafuata na kuwataja.

      “Dk. Shein (Rais wa Zanzibar) alisema atakula nao sahani moja, sisi tutakula nao kijiko kwa kijiko,” alisema Shigela huku akishangiliwa na wajumbe wa baraza hilo.

      Hata hivyo, alipoulizwa na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi zaidi, Shigela, alikataa kuwataja.

      Tangu kutokea kwa vurugu hizo zilizoanza Mei 26 hadi Mei 28 mwaka huu na kusababisha athari kubwa kutokana na uchomaji moto wa makanisa, kuvunjwa baa na kuharibiwa kwa mali za watu, zimekuwa zikitolewa kauli zikidai kuwa baadhi ya viongozi wa SUK walihusika kuchochea kutokana na kuwa washirika wa Uamsho.

      Hata hivyo, hadi sasa hakuna majina ya wanasiasa yaliyotajwa moja kwa moja kuhusiana na tukio hilo.

      WASIRA NAYE AWASHUKIA

      WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Steven Wasira, amesema kuwa Kikundi cha Jumuiya ya Uamsho kimevunja sheria kwa kujiingiza katika masuala ya siasa kutokana na kuhoji masuala ya Muungano ambayo ni ya kisiasa kitu ambacho ni kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake.

      Akizungumza jana katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, alisema kikundi cha Uamsho kilianzishwa kutekeleza majukumu ya kidini, lakini katika hali ya kushangaza kimeanza kujihusisha na mambo ya siasa hali iliyopelekea kuzuka kwa vurugu Visiwani Zanzibar.

      Wasira alisema kimsingi, dini ya Kiislamu haina mgogoro na dini nyingine, lakini kitendo cha kikundi cha Uamsho kuzusha vurugu zilizopelekea kuchomwa moto kwa makanisa kadhaa ni uvunjaji wa sheria kwa sababu suala la Muungano halina uhusiano na makanisa.

      “Wakatoliki na Waanglikana walikuwepo visiwa vya Zanzibar tangu miaka 100 iliyopita wakati Muungano una miaka 45 tu, lakini tunashangaa wenzetu wa Uamsho wametoka kwenye masuala ya kidini wamejiingiza kwenye mambo ya kisiasa,” alisema Wasira.

      Wasira alisema wanaosema kwamba Rais Jakaya Kikwete amezuia masuala ya Muungano yasijadiliwe ni waongo kwani Rais alichokisema ni kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiunda haijaundwa kwa lengo la kutaka kuvunja Muungano.

      Alisema tume hiyo iliyoundwa kwa kushirikisha makundi yote yakiwemo ya kidini, kisiasa na jamii imepokelewa na Watanzania kwa furaha kubwa bila malalamiko hivyo kinachotakiwa ni kwa kila mtu kutoa maoni kwa tume ili kuwe na Katiba nzuri yenye ushiriki wa maoni mbalimbali ya wananchi.

      Wasira aliwashukia watu wanaodai kuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ina wajumbe wengi wa dini fulani na kusema siyo kweli kwani dini haikuwa sehemu ya sifa za kuteuliwa kwenye bali vigezo na sifa vilizingatiwa.

      MAWAZIRI WALIOTEMWA

      Alisema mawaziri walioachwa kwenye mabadiliko ya baraza jipya la mawaziri haina maana kwamba wote ni wezi kama inavyoelezwa na baadhi ya watu, bali kilichotokea wamewajibika kutokana na makosa pengine yaliyofanywa na wasaidizi wao.

      Aliongeza kuwa watu wanapotosha ukweli kwa kueleza kuwa waliongoza mashambulizi yaliyopelekea kuondolewa kwa mawaziri hao ni wabunge kutoka vyama vya upinzani, alisema ni uongo kwani wabunge wa CCM ndiyo waliongoza mapambano hayo.

      MAKUNDI NDANI YA CCM

      Wasira alisema hakuna chama ambacho hakina makundi, lakini makundi yaliyopo ndani ya Chama cha Mapinduzi ni ya kawaida ambayo yanashughulikiwa kichama, lakini kinachooneka yanakuzwa na baadhi ya vyombo vya habari.

      “Matatizo ndani ya chama yapo, lakini siyo ya ajabu maana huwezi kuwa na chama kikubwa kama CCM utegemee kisiwe na na tatizo hata chama cha malaika ni lazima kinaweza kuwa na matatizo, lakini CCM ni chama kikubwa chenye uwezo wa kuhimili mawimbi mengi, “alisema Wasira.

      Alisema mpango wa CCM wa kujivua gamba unatafsiriwa vibaya na baadhi ya vyama ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimekuja na falsafa ya kusema vua gamba vaa gwanda.

      Wasira alisema CCM ilikuja na kauli mbiu hiyo kwa lengo la kukabiliana na wanachama wake wanaoutaka uongozi kwa kutumia rushwa wasiendelee na rushwa na kwamba kama Chadema wanataka watu wanaotoa rushwa ndio waondoke CCM wakajiunge kwao ni sawa.

      CHANZO: NIPASHE

      Huyu APE hana lolote akumbuke mwaka 1995 alivyo hamia nccr alisema akirudi chchm atakuwa maiti je anavyozungumza yeye ni msukule? au kwa kuwa alimpiga mzee ndolanga na kupata jina la taiyson ndio anabweka? tumdharau hana jipya alisha jitabiria umauti

    10. #8
      Power G's Avatar
      JF Gold Member Array
      Join Date : 20th April 2011
      Location : Msoga Kijijini
      Posts : 2,407
      Rep Power : 991
      Likes Received
      773
      Likes Given
      259

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      Quote By Tume ya katiba
      Kiongozi wa UVCCM tanganyika anatoa amri kwa kiongozi wa serikalizanzibar? kweli wamelewa na madaraka hawa vijana!
      Labda kwa kuwa Zanzibar ni koloni la Tanganyika ndiyo maana hata kifaranga tu kina uwezo wa kutoa amri.
      TANZANIA ITAJENGWA NA WENYE MOYO NA KULIWA NA WENYE MENO KAMA AKINA EL, JK, EC na RA

    11. #9
      mtotowamjini's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 23rd April 2012
      Location : None of Your Business
      Posts : 4,531
      Rep Power : 1263
      Likes Received
      1109
      Likes Given
      28

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      ni hao cuf ndio wenye fujo...chama cha waarabu kile
      Every saint has a past, every sinner has a future' ...Oscar Wilde

      One man's good fortune is another man's misfortune

    12. #10
      wade kibadu's Avatar
      Senior Member Array
      Join Date : 3rd April 2012
      Posts : 102
      Rep Power : 379
      Likes Received
      5
      Likes Given
      11

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      Its very sad to reach the point that we have in union of Tanganyika na Zanzibari.
      Bt therea some who know each and every thing that going on bt we shall see the end of uniön.

    13. #11
      Head teacher's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2012
      Posts : 610
      Rep Power : 485
      Likes Received
      124
      Likes Given
      6

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      Cuf ya jussa imehusika na ubaguzi

    14. #12
      tusichoke's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd April 2011
      Posts : 657
      Rep Power : 543
      Likes Received
      77
      Likes Given
      8

      Default Re: UVCCM: Uamsho wamo serikalini: Wasira naye awashukia

      Wameanza kutapatapa anayelazimisha muungano usijadiliwe ni CUFau CCM?Ccm wajue wakati wa kucheza na akiri za watu umepita,wakumbuke wanaccm nao ni wazanzibar na wanahaki ya kuhoji muungano.Ngoja tusubiri time will tell

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...