Support JamiiForums and Become a 'JF Premium Member' | Click HERE for Details
    Show/Hide This

    Topic: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

    Report Post
    Page 6 of 10 FirstFirst ... 45678 ... LastLast
    Results 101 to 120 of 191
    1. #1
      Mzee Mwanakijiji's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 10th March 2006
      Location : Kijijini
      Posts : 29,512
      Rep Power : 46712
      Likes Received
      16402
      Likes Given
      8461

      Default Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema "Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.

      Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.

      Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

      Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.

      Swali liwe rahisi tu:

      Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

      a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
      b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

      Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

      Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.

      Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

      Ni rahisi sana kumaliza hoja ya Muungano au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.
      [email protected]
      Tunapotaka kubadilisha watawala si kwa sababu tunataka kubadilisha sura; bali kubadilisha utawala! Yaani, tunataka kubadilisha jinsi tunavyotawaliwa siyo tu sura za wanao tutawala M. M. Mwanakijiji

    2. RukaaJuu Final

    3. #101
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Taso
      Nilidhani Kambona aliondoka nchini kuhusiana na migogoro ya siasa mpya ya Azimio La Arusha, na pia kushutumiwa ni bepari au mwizi. Fundikira alifukuzwa baraza la mawaziri na kufungwa jela kwa kesi ya rushwa, sikujua kuwa walifanywa lolote kuhusiana na Muungano. Hebu nielimishe tafadhali. Kambona alifanywa nini? Nilidhani Nyerere alisema hakumfukuza wala kumfanya chochote Kambona, bali aliondoka mwenyewe. Au?
      Na Hanga? na Jumbe? na Kanal Mahfuz?
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    4. #102
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,435
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4795
      Likes Given
      2859

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By zomba
      Ikiwa wewe ni mmoja kati ya ndoa ya watatu na ikavunjika na wewe haumo? fikiri!
      Tufike mwisho, ni wazi huna majibu ya Nyerere kuua EAC, kuhitilafiana na Nkrumah na serikali ya tatu ya muuungano itakuwa na mamlaka gani juu ya nini kwa kipi na gharama za nani.

      Wewe ni moja ya matunda maridhawa ya UAMSHO. ni mfano wa yale tunayosema kila siku kuwa wahudhuriaji wa UAMSHO ni watu wa kumeza tu hata kama utawaamuru wachinje wake zao.

      Wafundishaji wa UAMSHO ni watu wanaopindisha ukweli au wasiojua ukweli au wanafiki tu! Hili la Nyerere kuua EAC tumeliona katika video ya aibu, na kwa bahati mbaya linaonekana kueleweka kama lilivyoletwa.

      Ndiyo maana tunasema ni bora Zanzibar ikajiondokea kabla ya July1 2012 kwasababu madhara ya UAMSHO ni makubwa sana kuliko invyodhaniwa. Udanganyifu wao na uchochezi unaweza kutuzalishia watu kama gaidi wa 9/11 aliye kifungoni Marekani.

      Hakuna serikali 3, mkataba au uhusiano wa EU. Please pack and go ASAP
      JokaKuu and Ngongo like this.

    5. #103
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Nguruvi3

      Hivi umeshajiuliza, hii katiba ni kwa vyama tu? Uamsho wana kila haki ya kuijadili na kujadili wayatakayo.

      Nyerere kama alikuwa na tafauti na Nkrumah basi hizo tofauti, mojawapo ni kuwa Nkrumah was for true unity Nyerere was not.

      Kama EAC ilivunjika na Nyerere alikuwa mmojawapo kati ya hao watatu.

      Biafra Nyerere alipigania na kuchangisha pesa humu mitaani kuunga mkono nchi isambaratike na kuwe na nchi nyingine.

      Usitake kuhalalisha yasiyohalalika.

      Muungano uongolewe kuboreshwa kama sheria zinavyotaka lakini watu wasinyimwe ruksa ya kuongea. Uamsho wameshasema wao hawahusiki na fujo yoyote ile na jana wamefanya mhadhara wao mwingine.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    6. #104
      kwamwewe's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 15th July 2010
      Posts : 856
      Rep Power : 5406
      Likes Received
      99
      Likes Given
      125

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By fairplayer
      naomba nirudie kuuliza:

      Kwani haiwezekani by 1st july 2012 wakawa wamevunja muungano?.

      Mi ningefanya party kabisaa kusherehekea. Hawababeki hawa wamezoea kutawaliwa na waarabu na kufanywa watumwa.
      hamufahamiki nyinyi watu wa kanisa mara muarabu alitufanya watumwa leo unakuja na hoja wazanzibari wamezoea kufanywa watumwa , hizi ni lugha gani???

      Ingalikuwa wakati wa utumwa ulikuwepo ungalikuwa hata huna thamani ya kuuzwa kwani tizama hata unachokiongea hukijui

      Mimi ningalikutoa bure tu maana huna thamani

    7. #105
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,435
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4795
      Likes Given
      2859

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By zomba
      Nyerere kama alikuwa na tafauti na Nkrumah basi hizo tofauti, mojawapo ni kuwa Nkrumah was for true unity Nyerere was not.

      Kama EAC ilivunjika na Nyerere alikuwa mmojawapo kati ya hao watatu.

      Biafra Nyerere alipigania na kuchangisha pesa humu mitaani kuunga mkono nchi isambaratike na kuwe na nchi nyingine.

      Muungano uongolewe kuboreshwa kama sheria zinavyotaka lakini watu wasinyimwe ruksa ya kuongea. Uamsho wameshasema wao hawahusiki na fujo yoyote ile na jana wamefanya mhadhara wao mwingine.
      !!!! !! ?

    8. Miaka 50

    9. #106
      Kiranga's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 29th January 2009
      Posts : 14,164
      Rep Power : 41578
      Likes Received
      6063
      Likes Given
      1057

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Nguruvi3
      !!!! !! ?
      in vacuo.
      Nguruvi3 likes this.
      Allow others to say their say, but always say your piece, it's only right.

    10. #107
      zomba's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 27th November 2007
      Posts : 15,822
      Rep Power : 14621
      Likes Received
      2842
      Likes Given
      1961

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Nguruvi3
      !!!! !! ?
      Simple minds never gets the answers easily. Do your homework.
      System At Work

      "nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe

    11. #108
      JokaKuu's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 31st July 2006
      Posts : 6,837
      Rep Power : 2970
      Likes Received
      2449
      Likes Given
      3518

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Nguruvi3
      Tufike mwisho, ni wazi huna majibu ya Nyerere kuua EAC, kuhitilafiana na Nkrumah na serikali ya tatu ya muuungano itakuwa na mamlaka gani juu ya nini kwa kipi na gharama za nani.

      Wewe ni moja ya matunda maridhawa ya UAMSHO. ni mfano wa yale tunayosema kila siku kuwa wahudhuriaji wa UAMSHO ni watu wa kumeza tu hata kama utawaamuru wachinje wake zao.

      Wafundishaji wa UAMSHO ni watu wanaopindisha ukweli au wasiojua ukweli au wanafiki tu! Hili la Nyerere kuua EAC tumeliona katika video ya aibu, na kwa bahati mbaya linaonekana kueleweka kama lilivyoletwa.

      Ndiyo maana tunasema ni bora Zanzibar ikajiondokea kabla ya July1 2012 kwasababu madhara ya UAMSHO ni makubwa sana kuliko invyodhaniwa. Udanganyifu wao na uchochezi unaweza kutuzalishia watu kama gaidi wa 9/11 aliye kifungoni Marekani.

      Hakuna serikali 3, mkataba au uhusiano wa EU. Please pack and go ASAP
      Nguruvi3,

      ..miaka 40+ ya muungano inatosha.

      ..it is not fair wa-Tanganyika tuendelee kunyonywa na kukaliwa kichwani na kanchi kadogo kama Zanzibar.

      ..mimi naupinga muungano wa serikali 3. pia napinga mapendekezo yanayochomekwa sasa hivi at Tanganyika na Zanzibar ziwe na "muungano wa mkataba."

      ..tuwe makini tusije kutoka kwenye "kero za muungano" na kuingia kwenye "kero za mkataba"
      Nguruvi3 likes this.

    12. #109
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema "Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.

      Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.

      Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

      Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.

      Swali liwe rahisi tu:

      Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

      a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
      b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

      Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

      Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.

      Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

      Ni rahisi sana kumaliza hoja ya Muungano au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.
      Ahsante mkuu wangu. Na ndio maana hushangaa watu wanapojaribu sana kuwajibu Wazanzibar ilihali kazi ya kupata majibu wanayo wenyewe. Nawashangaa sana wanapoiomba serikali ya Jamhuri ifanye referendum au tujadili swala la kuuvunja muungano wakati anayetaka kuvunjika Tanzania ni wao wenyewe. Kuna baraza la Mapinduzi hili ndilo liloingia ubia na serikali ya bara kuanzisha Jamhuri ya Tanzania hawa ndio wenye jukumu na wa kupeleka malalamishi yao huko. Haya maswala ya Nyerere sijui alimfunga Jumbe na lawama kibao zinaletwa na watu ambao hawapo ktk baraza la mapinduzi maana sijasikia mjumbe wa baraza hilo akilalamikia kutaka muungano uvunjwe. Hawa ndio hutoa maamuzi yao na serikali ya Muungano hufuata ama kujadili hoja zinazotokana na baraza hili wala sii mihadhara ya misikitini.
      Last edited by Mkandara; 6th June 2012 at 02:03.
      Mzee Mwanakijiji likes this.
      Exploration of reality

    13. #110
      Nguruvi3's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 21st June 2010
      Location : Kidabashi-Dongobeshi
      Posts : 3,435
      Rep Power : 2887
      Likes Received
      4795
      Likes Given
      2859

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By JokaKuu
      Nguruvi3,

      ..miaka 40+ ya muungano inatosha.
      ..it is not fair wa-Tanganyika tuendelee kunyonywa na kukaliwa kichwani na kanchi kadogo kama Zanzibar.
      ..mimi naupinga muungano wa serikali 3. pia napinga mapendekezo yanayochomekwa sasa hivi at Tanganyika na Zanzibar ziwe na "muungano wa mkataba."
      .tuwe makini tusije kutoka kwenye "kero za muungano" na kuingia kwenye "kero za mkataba"
      JokaKuu, hawa watu kila wanachopewa bado hawaridhiki kuendela nao ni kuendeleza matatizo.

      Hili la mkataba linachomekwa kiaina ili yale yanayoinufaisha zanzibar ndiyo yawe ya mkataba.
      Hebu jaribu kuuliza mkataba uwe na jambo gani? Hakuna atakayekupa sababu.

      Sasa wamekuja na jingine eti kuwe na mkataba kama wa EU. Maana yake ni ile ile kuondoa vikwazo kwao.
      Kwanini hiyo 'EU' iwe Tanganyika na Zanzibar na siyo EAC!
      Sasa basi tumechoka let them go, tena ASAP. Hakuna Mtanganyika anayeweza kusema kutokuwepo kwa muungano ataathirika, hakuna!
      Mkandara and Mzee Mwanakijiji like this.

    14. #111
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Nguruvi3
      JokaKuu, hawa watu kila wanachopewa bado hawaridhiki kuendela nao ni kuendeleza matatizo.

      Hili la mkataba linachomekwa kiaina ili yale yanayoinufaisha zanzibar ndiyo yawe ya mkataba.
      Hebu jaribu kuuliza mkataba uwe na jambo gani? Hakuna atakayekupa sababu.

      Sasa wamekuja na jingine eti kuwe na mkataba kama wa EU. Maana yake ni ile ile kuondoa vikwazo kwao.
      Kwanini hiyo 'EU' iwe Tanganyika na Zanzibar na siyo EAC!
      Sasa basi tumechoka let them go, tena ASAP. Hakuna Mtanganyika anayeweza kusema kutokuwepo kwa muungano ataathirika, hakuna!
      Nguruvi3, Yule sheikh nadhani hajui kabisa maana ya muungano wa nchi na ndio maana alifikiria ni sawa na jumuiya ya nchi za Ulaya. tena akisisitiza kama Marekani waliamua hivyo sisi tunataka Jumuiya. Ebu atokee kiongozi Marekani aseme anataka kuivunja Marekani au Texas itoke ktk muungano aone cha moto..Yaani sheikh mzima hajui kama Zanzibar iliingia ktk muungano isipokuwa anavyotaka yeye leo tena kwa kusisitiza uhuru wa Sultan kuwa ndio soveign na sii Mapinduzi.

      Kusema kweli kutokana na hali hii nadhani hata mimi naondoa kabisa wazo nafikra za Afrika moja. Sintokubaliana na hata EAC kwa sababu tumetoka huko huko jamani na tutakuja poteza muda na hasara kubwa kwani wapo watu kama hawa siku zote, kazi yao kubwa ni kufikitisha. Afrika ilikuwa na mataifa chini ya 40 tukitegemea kuungana, leo hii tumefika 50 na bado tunagawanyika badala ya kuungana.
      - It's waste of time and money..
      Exploration of reality

    15. #112
      kombo1's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th May 2012
      Posts : 11
      Rep Power : 354
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema "Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.

      Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.

      Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

      Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.

      Swali liwe rahisi tu:

      Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

      a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
      b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

      Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

      Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.

      Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

      Ni rahisi sana kumaliza hoja ya Muungano au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.
      Chukuwa wakati kidogo uangalie hii hapo chini utaelewa kwa nini tunataka kurejesha utaifa wetu haraka awezekanavyo.

      Video:Kwanini tusiirejeshe jamhuri ya watu wa Zanzibar? | Mzalendo.net

    16. #113

      Quote By Saint Ivuga
      hakuna anayetaka nchi yake hapa lazima kutakuwa na ajenda a siri ama kuna kitu kingine wanataka..ila kama kweli mpo serious mnataka nchi yenu haya mliyoshauriwa hapa chini hamjayaona ?
      Angalia Video hii na ujuwe maumivu ya Wazanzibari

      Video:Kwanini tusiirejeshe jamhuri ya watu wa Zanzibar? | Mzalendo.net

    17. #114
      kombo1's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th May 2012
      Posts : 11
      Rep Power : 354
      Likes Received
      2
      Likes Given
      0

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Kama unatuunga mkono ni vizuri sana, pia jielimishe zaidi kwa kuangalia hii video uone maumivu yetu ya kufutwa utaifa wetu kwa maguvu ya watu wa Tanganyika.

      Video:Kwanini tusiirejeshe jamhuri ya watu wa Zanzibar? | Mzalendo.net

    18. #115
      Mkandara's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 2nd March 2006
      Location : T dot
      Posts : 13,770
      Rep Power : 7663
      Likes Received
      4929
      Likes Given
      4509

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By kombo1
      Chukuwa wakati kidogo uangalie hii hapo chini utaelewa kwa nini tunataka kurejesha utaifa wetu haraka awezekanavyo.

      Video:Kwanini tusiirejeshe jamhuri ya watu wa Zanzibar? | Mzalendo.net
      Mkuu wangu hata hicho kichwa cha video hiyo kinasema Kwanini TUSIIREJESHE JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR...hii inaashiria hjili ni swala lenu na ujumbe ni kwa Wazanzibar (TUSII) hivyo mnataka sisi Bara tuseme nini? tujadili nini? tufanye nini?.. haituhusu. Ndio maana Mwanakijiji anasema mbona rahsi sana kurejesha hiyo Jamhuri. Fuateni maagizo yake mtaipata Zanzibar yenu huru.
      Mzee Mwanakijiji and Nguruvi3 like this.
      Exploration of reality

    19. #116
      Mtu wa Pwani's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 26th December 2006
      Posts : 4,250
      Rep Power : 1491
      Likes Received
      159
      Likes Given
      147

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Mkandara
      Mkuu wangu hata hicho kichwa cha video hiyo kinasema Kwanini TUSIIREJESHE JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR...hii inaashiria hjili ni swala lenu na ujumbe ni kwa Wazanzibar (TUSII) hivyo mnataka sisi Bara tuseme nini? tujadili nini? tufanye nini?.. haituhusu. Ndio maana Mwanakijiji anasema mbona rahsi sana kurejesha hiyo Jamhuri. Fuateni maagizo yake mtaipata Zanzibar yenu huru.
      wangu na ww una spin ? kwa nn tusiirejeshe ... ? kuna question mark umeiondoa na pia umejisahaulisha kuwa ukisema kwa nn nisioe ? maana unaeleza hakuna sababu inayonizuia nisioe, na ndio kilichokusudiwa hapo
      Mkandara likes this.
      Our job is not to make up anybody's mind, but to open minds and to make the agony of the decision-making so intense you can escape only by thinking. ~Author Unknown

    20. #117
      mawazotu's Avatar
      Member Array
      Join Date : 27th April 2010
      Posts : 57
      Rep Power : 472
      Likes Received
      4
      Likes Given
      10

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By chama
      Hongera sana kupata hizo tano mimi natafuta moja mpaka sasa hivi sijaipata!!

      Chama
      Gongo la Mboto DSM.
      haha hahha mkuu basi mimi nitakua kichwa . sasa hivi nataka nitulie nianze kulist upyapole pole faida vs hasara za muungano alafu ndo nitafanya analysis ya huu muungano wetu

    21. #118
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,743
      Rep Power : 1919
      Likes Received
      1179
      Likes Given
      965

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema "Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.

      Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.

      Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

      Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.

      Swali liwe rahisi tu:

      Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

      a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
      b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

      Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

      Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.

      Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

      Ni rahisi sana kumaliza hoja ya Muungano au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.
      Siku zote mgeme akisifiwa sana basi pombe hulitia maji.

      Na hii sasa inakusibu ahali yangu Mwanakijiji. Kwani unasukumwa zaidi na ushabiki na sio facts au maadili ya kiundishi wa habari. Kwani maadili ya kiuandishi wa habari yanakataza sana kwa mwandishi kuandika habari na kuegemea upande mmoja na kuiamulia jamii nini ifanye. Inasema mwandishi ni yule anayeandika kitu chochote kile vile kilivyo bila kupendelea upande wowote na kuiachia jamii ya wasomaji iamue. Kumbuka kuwa kila habari ina sehemu mbili positive na negative.

      Katika habari yako umeelekeza shutuma zako zaidi kwa WaZnz ima kwa makusudi na kwa nia maaluma au umekuwa huna taaluma ya ziada nje ya uandishi ndio maana umeandika kitu ambacho msomi yoyote anakuweka kando kabisa na kukudharau.

      Ulipaswa kujua yafuatayo kabla kuandika mada yako
      1. Muungano ni nini?
      2. Je Znz na Tanganyika zimeungana kinamna gani (Kimkataba au Kikatiba)?
      3. Mkataba ni nini?
      4. Nani au upande gani wenye haki ya kuulinda au kuuvunja muungano
      ?

      Lakin mimi nitachukua fursa hii kukusaidia mambo kadha
      1. Ni vizuri ujue neno mkataba ni nini. Mkataba ni makubaliano ya hiari baina ya pande zaidi ya moja kushirikiana katika mambo wanayokubaliana. Znz na Tanganyika zimeungana KIMKATABA na SI KISHARIA. Sasa pande zote zina haki sawa ya kukubali kuendelea na muungano au kuukataa muungano huo. Na si Znz peke yao wana haki hiyo.

      Kwa WaZnz wapo wazi kabisa na juhudi nyingi sana zilifanyika na zinaendelea kufanyika kuhakikisha haki inatendeka kwa upande wao pale wanapoona kuna dhulma zinazofanywa mchana kweupeeee na upande wa Tanganyika. Juhudi hizo ni pamoja na kujiandikisha idadi uliosema kupinga muungano, kudai kula ya maoni Znz kabla kufanyika kwa zoezi la kukusanya maoni ya katiba mpya ya Znz na hata kuuchana hadharani muswada wa katiba mpya uliowasilishwa na Bunge la muungano na mengine mengi sana. Mambo ambayo Tanganyika hayajafanyika.

      Haya yote yanafanyika ni kuonyesha hisia zao za kukataa kuburuzwa na Muungano ambao kwa waZnz sasa umekuwa Mvungano. Kwa mujibu wa Katiba ya nchi ya Znz ibara ya 4 kifungu cha 3 na 4 kinabainisha wazi sharia zote zinazotumika Znz zitatungwa na kuridhiwa na Baraza la wawakilishi na kusainiwa na Rais wa Znz na mwenyekiti wa BLM.
      Sasa labda nikuulize Je Sheria ya kuunda muungano iliyopitishwa na Bunge la muungano je ilipita baraza la wawakilishi kuridhiwa? Kwa kuwa haijapitishwa kwanini wa Znz wasiseme kuwa Muungano wenu ni kharamu na hauwezi kukaa kisharia kwa upande wa Znz. Na kwa kutumia nguvu nyingi ndio mnajenga dhana ya kutaka kuwaburuza kikondoo wa Znz jambo ambalo wao hawalitaki.

      Nakushauri tena wenye uwezo wa kuamua kuhusu muungano ni raia wa pande zote mbili za Muungano na sio waZnz pekee yao. Hata Tanganyika kama mnahisi kudhulumika kiuchumi au hata kijamii mna haki kamili kabisa kuupinga muungano kwani kinachotakiwa ni uwazi , ukweli na haki kwa pande zote pasi na kudhulumiana.

      Waznz wameonyesha njia sasa WaTanganyika mpo wapi?

      Last edited by Barubaru; 6th June 2012 at 09:07.
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    22. #119
      Barubaru's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 6th April 2009
      Location : Doha, Qatar
      Posts : 5,743
      Rep Power : 1919
      Likes Received
      1179
      Likes Given
      965

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Mjadala wa Muungano sasa wageuka kama kaa la moto
      Salim Said na Salma Said, Zanzibar
      WAKATI Watanzania leo wanaungana nchini kote kuadhimisha miaka 45 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar, kero mbalimbali zinazoukabili sasa ni wazi zinatishia kuusambaratisha.
      Hali hii inatokana na watu wengi katika pande mbili za Muungano kushindwa kukubaliana na muundo wake pamoja na kuwapo kero nyingi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi.
      Baadhi ya watu nchini wamedai kuwa kero za Muungano zimekuwa zikiusukasuka kwa muda mrefu sasa kutokana na serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupata kigugumizi cha kufanya mjadala wa kitaifa kutafuta suluhu ya kero hizo.
      Wakizungumza katika kipindi cha Kipimajoto kinachorushwa na ITV juzi usiku, Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) Zanzibar, Juma Duni Haji, alisema bila ya kuwa na serikali tatu kero za Muungano zitaendelea kudumu.
      “Serikali ya Zanzibar ni ya watu na kila penye watu pana ardhi na pia ukisikia kuwa kuna harusi unategemea kumkuta mwanamke na mwanamume ukiwakuta wanaume watupu utashtuka,” alisema Duni.
      “Shughuli za serikali ni tatu (jurisdiction) kuna Muungano, Zanzibar na Tanzania Bara, hivyo kila shughuli hapa inahitaji serikali na hapo tutamaliza kero za Muungano kama walivyo wenzetu wa Uingereza.”
      Alisema, Mkataba wa Muungano ni wa kimataifa na kama hivyo ndivyo, hauwezi kuingiliwa na upande mmoja tu na kufanyiwa mabadiliko bila ya makubaliano ya walioungana.
      Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi Samuel Ruhuza alisema, serikali zinajaribu kupotosha historia kwa kuwa wanaitangaza tarehe tisa ya Uhuru wa Tanganyika kuwa ni ya Uhuru wa Tanzania na wanafunzi wanafundishwa hivyo shuleni, jambo ambalo si kweli.
      Aidha, alifafanua kuwa wanaiacha Desemba 12 ya Uhuru wa Zanzibar na kusherehekea siku ya Mapinduzi ya Zanzibar na watu hawajui siku ya Uhuru wa Zanzibar.
      “Tunapotosha na kufuta historia yetu, hali hii ni mbaya sana,” alisema Ruhuza na kuongeza:
      “Zanzibar ina rais ambaye hana dola na hawezi kupinduliwa kwa sababu huwezi kumkamata mtu na kumshtaki kuwa ni haini anataka kupindua Zanzibar, ni kichekesho”.
      Ruhuza alikiri kuwepo kwa kero za Muungano na kuthibitisha kuwa serikali tatu ndio suluhu ya kudumu ya kero hizo.
      Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Victor Kimesera alisisitiza kuwa makubaliano ya msingi ya Muungano yamekorogwa na kuingiliwa bila ya makubaliano ya pande mbili husika.
      Alisema hiyo ndio sababu moja ya kutofikiwa kwa malengo ya Muungano kwa kuwa upande mmoja uliingia na kuongeza mambo ya Muungano bila ya makubaliano.
      “Mambo ya msingi ya Muungano yalikuwa 11 tu, lakini sasa yameongezwa na kufikia 24 haya ndiyo yanayoleta mijadala na migogoro isiyokwisha,” alisema Kimesera.
      Kwa upande wake, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Azaveli Lwaitama alisema, Muungano ulisababishwa na sababu za kiusalama na amani.
      “Mzee Abeid Karume alikubali kuungana kwa sababu alikuwa anahitaji amani na usalama kutokana na hofu aliyokuwa nayo ya kuvamiwa na mataifa ya Magharibi; na huku Mwalimu Nyerere alikuwa na hofu ya kuathirika iwapo Zanzibar ingevamiwa. Si unajua machafuko yakiwa Zanzibar na Bara pia yana gharama zake,” alisema Lwaitama na kuongeza:
      “Tatizo la Muungano sio jina, jina si chochote. Tatizo linakuzwa kwa utashi wa wanasiasa tu, na ardhi ya Zanzibar kwa sababu ni ndogo ndio maana kukawa na vikwazo kwa watu wa Bara kumiliki, lakini kwetu sisi ardhi ni kubwa hata wakija Wazanzibari wote hawawezi kuimaliza.”
      “Mwalimu alikubali hayo ili Wazanzibari wasijione kama vile wamemezwa na ndio maana hata serikali, bendera na wimbo wa taifa wanavyo. Ukimwona mtu wa bara anapigia kelele hilo huyo ni mangi wa Tanganyika.”
      Lwaitama alipingana na kauli ya wanasiasa kuwa serikali tatu ndio suluhu ya kudumu ya matatizo ya Muungano, na kupendekeza kuwa serikali moja ndio suluhu na kwamba nchi haiwezi kutoka katika serikali mbili ikaenda kwenye serikali tatu ni kichekesho.
      “Hata Mwalimu alisema, tukitoka serikali mbili ni kwenda serikali moja na sio tatu. Tukitoka mbili na kwenda tatu badala ya moja ni kioja na kichekesho kikubwa,” alisema Lwaitama.
      Naye Kiongozi Mwandamizi kutoka Ofisi ya Waziri Kiongozi Zanzibar, Enzi Talib Aboud alisema wakati umefika serikali ya Tanganyika ikarejeshwa.
      Aboud alisema hayo jana wakati akijadili mada yake iliyowasilishwa katika kongamano la kitaifa kwa niaba yake na Mwanasheria, Ali Omar ambalo liliwashirikisha wanafunzi kutoka vyuo vikuu vya Zanzibar, viongozi mashuhuri, wasomi na viongozi wa vyama vya siasa.
      Aboud alisema serikali ya Tanganyika irejeshwe ili iweze kusimamia mambo ambayo hayamo katika orodha ya Muungano kwa upande wa Tanzania Bara ili mfumo unaotumika Zanzibar utumike na Bara.
      Alisema tangu kuundwa kwa Muungano SMZ, imekuwa na katiba na serikali yake ambayo inasimamia mambo ya ndani ya Zanzibar ambayo hayamo katika orodha ya mambo ya Muungano.
      Alisema kwamba, uchumi wa Zanzibar umekuwa ukififia kutokana na vikwazo mbalimbali vilivyomo katika mfumo wa Muungano na kushauri Zanzibar ipate haki zake zote za misaada, utambulisho wake wa kidola na uwakilishi wake katika jumuiya za kimataifa ili iweze kukuza uchumi na kuinua kipato cha wananchi wake.
      Aboud ambaye ni mwadhishi wa habari mkongwe aliyewahi kufanya kazi katika vyombo vya habari kadhaa ya Tanzania Bara na kukamata nafasi za juu za serikali ya Zanzibar, alisema kwamba wakati umefika mkataba wa awali wa Muungano ukapelekwa katika Baraza la Wawakilishi ili wajumbe wapate nafasi ya kuridhia mkataba huo.
      Alisema mkataba huo wa Muungano baada ya kufikiwa mwaka 1964 uliridhiwa na upande mmoja wa Muungano, lakini baraza la kutunga sheria wakati huo Zanzibar (Baraza la Mapinduzi) halikupewa nafasi ya kuridhia mkataba uliosainiwa na Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Sheikh Abeid Amani Karume.
      Kongamano hilo limefuatia kuzuiwa kwa maandamano ya kuunga mkono suala la mafuta na gesi asilia kuondolewa katika orodha ya mambo ya Muungano kama ilivyopendekezwa na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
      Juzi Mkuu wa Polisi wilaya ya Mjini, Mkadam Khamis Mkadam, alisema suala la mafuta na gesi asilia ni suala la kikatiba na linapaswa kujadiliwa na mabaraza ya kutunga sheria na sio jumuiya au taasisi nyingine, hivyo jeshi la polisi haliwezi kuruhusu kufanyika kwa maandamano hayo.
      Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Chama cha UPDP, Haji Othman Haji, alisema kwamba Muungano ulifikiwa kwa maamuzi ya Nyerere na Karume, lakini wananchi hawakupewa muda wa kutosha wa kufikiria na kuamua katika suala hilo.
      Naye Profesa Abdul Sharif ambaye ni mtafiti wa mambo ya historia alisema wananchi katika taifa wamegawanyika kutokana na mitazamo tofauti kuhusu Muungano wakiwapo wanaofikiria uvunjwe na uundwe upya ili kwa kuzingatia masilahi ya kiuchumi badala ya kisiasa pekee.
      Kwa upande wake Ali Mohammed Said alisema wananchi wajadili uhalali wa Muungano wenyewe badala ya kujadili kero zake kwa kuwa ufumbuzi wa matatizo hayo ni kurudi kuangalia mfumo wake.
      Awali, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, Ustadh Farid Hadi aliwataka wananchi wa Zanzibar kuondoa woga na kujadili kwa uwazi matatizo yanayoukabili Muungano kwa masilahi ya wananchi wake na vizazi vijavyo.
      Chanzo: mwananchi.co.tz
      Published in:

      on April 26, 2009 at 5:25 pm Comments Off
      [IMG]file:///C:\DOCUME~1\ENGMAT~1\LOCALS~1\ Temp\msohtmlclip1\01\clip_imag e001.gif[/IMG]
      Ukiwa mchoyo, usiwe mroho.

      Man Sharaf naf'sahu, fahuwa rasul

    23. #120
      Ntemi Kazwile's Avatar
      JF Senior Expert Member Array
      Join Date : 14th May 2010
      Location : Bongo salidalam
      Posts : 1,873
      Rep Power : 832
      Likes Received
      135
      Likes Given
      449

      Default Re: Kama kweli Wazanzibari "wengi" wanataka watoke kwenye Muungano mbona ni rahisi sana...

      Quote By Mzee Mwanakijiji
      Kuna maneno na kauli za baadhi ya watu wachache wakizungumza kana kwamba wanawakilisha "wengi". Utasikia mtu anayepinga Muungano anasema "Wazanzibari hatuutaki Muungano" na wakati mwingine kudai "Wazanzibari wengi hawautaki muungano". Sasa mara nyingi wanaposema "wengi" mtu wa kawaida (asiyetaka kufikiri sana) anaweza kuamini kabisa kuwa ni kweli "wengi" hawautaki Muungano.

      Mfano unaotolewa siku za hivi karibuni ni "sahihi 500,000" za wanaodaiwa "Wazanzibari" wasiotaka Muungano. Sasa kwenye mahali ambapo pana watu milioni 1.5 hivi idadi hiyo ni kubwa sana; ni theluthi moja ya watu wote wa Zanzibar. Sasa kama kweli wapo watu wengi hivi njia rahisi ya kutaka kujitoa kutoka kwenye Muungano siyo mihadhara wala hawahitaji kabisa kuwalalamikia watu wa bara au serikali ya Muungano.

      Kwa wanaokumbuka wananchi wa Zanzibar walishinikiza vyama vyao viwili vya CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na waliweza kufanya hivyo baada ya kupitisha sheria ya kura ya maoni ambayo hatimaye iliandika upya katiba ya Zanzibar. Wananchi wakaweza kujitokeza na kupiga kura ya maoni. Walifanya hivi bila kuomba kibali Muungano na kiasi cha kuweza kuandika kwenye Katiba Yao vitu ambavyo ni kinyume na Katiba ya Muungano.

      Sasa kama waliweza kufanya hili ni kitu gani kinawashinda kutaka viongozi wao wa kisiasa kuandia sheria ya kupiga kura ya maoni kama wanautaka Muungano au la? Kwa vile hoja ya kupinga MUungano inadaiwa inakubaliwa na watu wa vyama vyote ni wazi kuwa ni rahisi sana kwa watu wa Uamsho na Wazanzibari wengine kuhakikisha kuwa BLW linapokaa linaazimia kupitisha kura ya maoni kuhusu Muungano na kutaka sheria iletwe ya kuuliza swali la Muungano.

      Swali liwe rahisi tu:

      Je unataka Zanzibar ibakie kwenye Muungano wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania?

      a. Ndio ibakie - Ikibakia kero na matatizo ya Muungano kutatuliwa ifikapo Julai 1, 2014
      b. Hapana isibakie - isipobakia Zanzibar itajitoa ifikapo Julai 1, 2014

      Ijulikane mapema kuwa ikisemwa kuwa "ndio ibakie" manake ni kuwa masuala ya muundo na mfumo wa Muungano yatajadiiliwa na kushughulikiwa kwenye Katiba Mpya na yatakuwa tayari kumalizwa yote ifikapo 2014

      Na ikisemwa Hapana isibakie manae ni kuwa mazungumzo ya kuvunja Muungano yataanza na ifikapo Julai 1, 2014 Zanzibar itajitoa kwenye Muungano.

      Wazanzibar waandae kura hiyo ya maoni wao wenyewe kama walivyofanya kwenye ile ya mabadiliko ya Katiba na lolote watakaloamua Tanzania Bara WATAHESHIMU uamuzi huo.

      Ni rahisi sana kumaliza hoja ya Muungano au kutokuwepo Muungano. Yote YAMO MIKONONI MWA WAZANZIBARI. Hawahitaji kutuambia hawautaki Muungano, hatuhitaji watuambie tunawakandamiza kama wanataka kutoka kweli na siyo mikwara mbuzi njia nyeupeeeee!!! Andikeni sheria, itisheni kura ya maoni, pigeni kuchagua 'b' and then mambo yatakua yameiva ifikapo 2014 tutawasaidia kufunga mizigo.

      Ahsante - you are such a useful commentator! Keep it up broda
      “If people are not laughing at your dreams at least once a week, you are aiming too low.” Robin Sharma.

    Page 6 of 10 FirstFirst ... 45678 ... LastLast

    User Tag List

    Posting Permissions

    • You may not post new threads
    • You may not post replies
    • You may not post attachments
    • You may not edit your posts
    •  

    Who are WE?

    JamiiForums is a 'User Generated Content' site; anyone can register (MUST) and comment or start a new topic.

    You are always welcome! Read more...

    Where are we?

    We have our offices in Dar es Salaam but we still work virtually.

    For anything related to this site please Contact us.

    Contact us now...

    DISCLAIMER

    JamiiForums, its partners, affiliates and advertisers are not responsible for the content of threads/topics that are submitted by users..

    Read more...

    Forum Rules

    JamiiForums is moderated under the rules set by users and moderators to safeguard you.

    You MUST read them and comply accordingly. Read more...

    Privacy Policy

    We are committed to respecting your privacy rights when visiting any JamiiForums.com page, such as this one.

    Read our Privacy Policy. Proceed here...